Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

Kliniki ya Afya ya Akili kutolewa kupitia Hospitali zote za Rufaa nchini- Dk.Kigwangalla

0
0
Kliniki ya Afya ya Akili kutolewa kupitia Hospitali zote za Rufaa nchini- Dk.Kigwangalla Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Khamisi Kigwangalla amekutana na viongozi wa Chama Cha Walemavu wa Afya ya Akili (TUSPO), waliomtembelea Bungeni jana Mei 22.2017, Bungeni Dodoma.Viongozi hao walikaribishwa na Wabunge wawakilishi wa Watu wenye changamoto mbali mbali za ulemavu nchini, Mhe. Amina Mollel (Mb.) na Mhe. Stella Ikupa (Mb.). 

Katika kikao hicho Dkt. Kigwangalla ameweza kujadiliana nao mambo mbalimbali viongozi hao wa TUSPO ikiwemo uanzishwaji wa Kliniki ya Afya ya Akili kupitia Hospitali zote za Rufaa za Mkoa hapa nchini.“Nimekutana na Viongozi wa TUSPO ambao wanashughulika na masuala ya Afya ya Akili. Tulijadili mambo mengi na niliwaelezea mikakati mbalimbali inayotekelezwa na Serikali kwenye eneo hili, ikiwemo Uanzishwaji wa Kliniki za Afya ya Akili kwenye Hospitali zote za Rufaa za Mkoa nchini nzima. 

Lakini pia Uanzishwaji wa Rehabilitation Centers kwenye kila kanda na usambazaji wa Madaktari bingwa wa Afya ya Akili na wataalamu wote wanaohitajika kutoa huduma hizi kwenye Hospitali na vituo hivi” Ameeleza Dkt. Kigwangalla.Aidha, ameongeza kuwa, amewaahidi uongozi huo wa TUSPO, kuwa atafuatilia juu ya hatua ambayo mchakato wa kukamilisha muundo wa kisheria (legal framework) ulipofikia na sababu za kukwama kwake toka sheria ya afya ya akili ilipotungwa mwaka 2008.

“Serikali ya awamu ya tano ni sikivu kwa wananchi wake bila kubagua. Nina aahidi kulifuatilia sualala uanzishwaji wa Baraza la Afya ya Akili, kwani tayari sheria ilishatungwa muda mrefu. Na kwamba ni kwa nini Baraza la Afya ya akili halijaanzishwa toka sheria itungwe mpaka leo na kwa nini mpaka leo hakujawa na kanuni za Afya ya akili kuelekeza juu ya mambo mbalimbali” alieleza Dkt. Kigwangalla ambapo amewaahidi kuwapa taarifa ya utekelezaji wa masuala hayo kwenye Bunge la Mwezi November 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Khamisi Kigwangalla akizungumza na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Walemavu wa Afya ya Akili (TUSPO), waliomtembelea Bungeni jana Mei 22.2017, Bungeni mjini Dodoma.

Kuhusu Magonjwa ya Akili:Magonjwa ya akili ni magonjwa ambayo yanaathiri uwezo wa mtu kufikiri, kuhisi, kutambua na kutenda, na hivyo kuwa na tabia au mwenendo uliotofauti au usioendana na jamii husika kiimani, kimila, desturi, na nyanja nyingine za kijamii. Tabia hizo zinatokana na ugonjwa wa akili kuathiri ufanisi na shughuli za mtu husika (mgonjwa) au huathiri jamii nzima inayomzunguka endapo mgonjwa huyo hatopatiwa matibabu stahiki na kwa wakati muafaka. 

  Kwa Tanzania imeeelezwa kuwa baadhi ya wagonjwa wengi wa akili hawafiki katika vituo vya kutolea huduma za afya na badala yake kuishia kwenye tiba za jadi au kutelekezwa na kunyanyapaliwa huku takwimu za zinaonyesha kuwa Tanzania ina idadi ya watu takriban milioni 45 na kutokana na taarifa ya afya ya akili kwa mwaka 2014/15 inaonyesha kuwa idadi ya watu 817,532 wanaugua magonjwa mbalimbali ya akili nchini, hii ni karibu asilimia 2 ya watanzania wote. 

  Pia idadi hii ni ongezeko la wagonjwa 367,532 ukilinganisha na takwimu za mwaka 2013/14 walikuwa ni 450,000. Kati ya wagonjwa wote wa akili kwa mwaka 2014/15 wanawake ni ni 332,000 na wanaume ni 485,532.Mkoa wa Dar-Es-Salaam unaongoza kwa kuwa n awagonjwa wengi nchini ukifuatiwa na mkoa wa Dodoma na mkoa wa mwisho ni Lindi. Idadi hiyo ya wagonjwa ni wale walioweza kuhudhuria katika vituo vya kutolea huduma ya afya hapa nchini.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Khamisi Kigwangalla (mwenye koti nyeusi kulia) akifanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Walemavu wa Afya ya Akili (TUSPO), waliomtembelea Bungeni jana Mei 22.2017, Bungeni mjini Dodoma.

Wachimbaji wadogo wa madini nchini watakiwa kuepuka ajali zisizo za lazima

0
0
Wachimbaji wadogo wa madini nchini wametakiwa kuepuka ajali zisizo za
lazima kwani tangu mwaka 2008 hadi Mei 2017 zimetokea ajali 125 kwenye
migodi yenye leseni na vifo ni 213.

Ajali zilizotokea kwenye maeneo ya wachimbaji wadogo wasio na leseni
nchini (maeneo ya mifumuko ya uchimbaji madini) katika kipindi hicho
ni 56 na kusababisha vifo vya wachimbaji 140.

Kamishna wa madini nchini, mhandisi Benjamin Mchwampaka aliyasema hayo wakati akizungumza na mameneja na wamiliki wa migodi mji mdogo wa Mirerani, wilayani Simanjiro mkoani Manyara.

Mhandisi Mchwampaka alisema ajali nyingi kwenye migodi ya wachimbaji
wadogo zinasababishwa na uzembe, kwani kwa mwaka huu pekee hadi Mei 15 ajali zilizotokea ni 11 na kusababisha vifo 26.

Alisema kwenye machimbo ya madini ya Tanzanite mji mdogo wa Mirerani,
ajali zilizotokea kwa wachimbaji wadogo kwa kipindi cha 2008/2017 ni
31 na wachimbaji wadogo waliopoteza maisha ni 40.
Viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini, Chama cha wachimbaji wadogo wa Madini Mkoani Manyara, (Marema) na wachimbaji wa madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro, wakiwa kwenyemafunzo ya usalama migodini.
Kamishna wa madini Tanzania, mhandisi Benjamin Mchwampaka akizungumza na wachimbaji wa madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, kuhusiana na usalama kwenye migodi yao.
Viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini, Chama cha wachimbaji wadogo wa Madini Mkoani Manyara, (Marema) na wachimbaji wa madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro, wakiwa kwenye
mafunzo ya usalama migodini.

GAG AITUNUKU HATI SAFI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI

0
0

Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serilkali nchini CAG ameitunuku hati safi ya hesabu na matumizi sahihi ya Fedha za Umma Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, baada ya kufanya ukaguzi na kujiridhisha na matumizi yaliyozingatia taratibu, Sheria na kanuni za fedha za Umma kwa mwaka wa Fedha wa 2015 – 2016.

Taarifa ya Afisa habari na Mawasiliano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kwa vyombo vya habari Bw. Ndimmyake Mwakapiso, imefafanua kuwa CAG ametunuku hati hiyo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, baada ya kufanya ukaguzi wa kawaida wa kila mwaka kwa mujibu wa sheria za fedha zinazompa mamlaka ya kukagua hesabu za mamlaka za serikali za Mitaa.

Mwakapiso, ametanabaisha baadhi ya vigezo vilivyozingatiwa kwenye ukaguzi huo, kuwa ni pamoja na ujenzi wa miradi inayoendana na thamani ya fedha zilizotumika, uzingatiaji wa sharia na taratibu za Manunuzi ya tenda, matumizi mazuri ya fedha za miradi ya maendeleo na zile za zatumizi ya kawaida sanjari na uandaaji wa taarifa za fedha unaozingatia viwango vya kimataifa( IPSAS)

"Huu ni mwaka wa 05 mfululizo Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi inapata hati safi ya CAG. Aidha kwa mujibu wa kanuni za ukaguzi, Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali mara baada ya kukamilisha ukaguzi wake kwa mwaka wa fedha husika, anaweza kutoa moja kati ya hati zifuatazo Hati safi, Hati yenye mashaka au Hati chafu",alisema .
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Profesa Riziki Shemdoe kutoka makitaba ya Kitengo cha habari.

BALOZI WA UINGEREZA NCHINI TANZANIA AMTEMBELEA RC MAKONDA.

0
0
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke, amemtembelea Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na kufanya nae mazungumzo yenye lengo la kuongeza na kuimarisha Ushirikiano uliopo baina ya jiji la Dar es salaam na London, nchini Uingereza.

Katika mazungumzo yao, Mhe Makonda na Bi. Cooke wamekubaliana kuongeza kasi ya Ushirikiano baina ya majiji makubwa mawili Dar es salaam Tanzania na London nchini Uingereza, makubaliano ambayo yatasaidia kupatikana kwa vifaa vya kisasa vya kuzuia na kupambana na majanga kama vile moto na mafuriko, ambapo Mhe MAKONDA ameomba kupatiwa magari ya kisasa ya shughuli za kuzima moto na uokoaji.

Mhe MAKONDA pia ameomba kusaidiwa vifaa maalum vya UTAMBUZ*I wa mifumo ya teknolojia ya kamera za kisasa zitakazofungwa *barabarani kwa ajili ya kusaidia USALAMA wa magari, raia na mali zao mifumo ambayo inafanya kazi katika jiji la London nchini Uingereza, hatua itakayokwenda sambamba na ujengewaji UWEZO kwa maofisa wa polisi wa Mkoa wa Dar es salaam katika matumizi ya mifumo hii.

Katika kukabiliana na changamoto ya MIGOGORO ya ARDHI mkoani Dar es salaam, Mhe MAKONDA ameomba kusaidiwa kuwajengea uwezo maafisa ARDHI na Mipango miji wa Mkoa wa Dar es salaam katika matumizi ya kisasa ya upimaji na upangaji ardhi, mafunzo ambayo yatakwenda sambamba na upatikanaji wa vifaa vya kisasa vya kupima ardhi, jambo litakalosaidia kuondoa KERO ya upatikanaji wa HATI pamoja na vibali vya UJENZI Mkoa wa Dar es salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda akimkaribisha mgeni wake Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke,alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar  na kufanya nae mazungumzo yenye lengo la kuongeza na kuimarisha Ushirikiano uliopo baina ya jiji la Dar es salaam na London, nchini Uingereza.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda akizungumza na mgeni wake Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke,alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar.


Maziko ya Marehemu Mzee Taimur Saleh Juma unguja

0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kushoto) alipojumuika na Waislamu mbali mbali katika kumswalia Marehemu Mzee Taimur Saleh Juma katika Msikiti wa Ijumaa Mchangani Mjini leo,marehemu aliwahi kushika nyazifa mbali mbali katika Serikalia ya Mapinduzi Zanzibar
 Baadhi ya Waislamu wakiitikia dua iliyoombwa baada ya Swala ya Maiti ya Marehemu Mzee Taimur Saleh Juma  katika msikiti wa Mchangani Mjini,ambapo Viongozi mbali mbali wa Serikali na Vyama vya Siasa walihudhuria na kwenda kuzikwa katika makaburi ya Kianga alipozikwa Marehemu huyo 
 Viongozi na Waislamu wakilibeba jeneeza la mwili wa Marehemu Mzee Taimur Saleh Juma baada ya kuswaliwa katika Msikiti wa Ijumaa Mchangani Mjini na kuelekea katika mazishi yake yaliyofanyika leo katika makaburi ya Kianga wilaya ya Magharibi "A"Unguja
 Baadhi ya waislamu na Wananchi mbali mbali wakilibeba jeneeza lenye mwili wa Marehemu Mzee Taimur Saleh Juma baada ya kuswaliwa katika Msikiti wa Ijumaa Mchangani Mjini na kuelekea katika mazishi yake yaliyofanyika leo makaburi ya Kianga wilaya ya Magharibi "A"Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kulia) alipojumuika na Viongozi mbali mbali na Waislamu  katika kumzika Marehemu Mzee Taimur Saleh Juma katika makaburi ya Kianga Wilaya ya Magharibi "A" Unguja yaliyofanyika. 
Picha na IKULU

WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA KUUNGA MATREKTA YA URSUS

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Maisha ya jamii ya Wahadzabe wanaoishi upande wa Ziwa Eyasi

0
0
 Wanaume wa jamii ya Kihadzabe wanaoishi kwenye pori la Myembe lililopo ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngogorongoro upande wa Ziwa Eyasi wakipanda mti wa mbuyu kurina asali. Kabila la Wahazabe ni moja ya jamii za wawindaji na wakusanyaji wanaopatikana Tanzania ambao chakula chao kikuu ni nyama, matunda, mizizi na asali. 

HONGERA KIONGOZI: Bwana Julius Indaya (katikakati) kiongozi wa jamii ya Wahadzabe wanaoishi upande wa Ziwa Eyasi akivishwa ngozi ya nyani na wenzake mara baada ya kufanikiwa kumkamata mnyama huyo kwa ajili ya kitoweo cha siku. Kwa utamaduni wa kabila la Wahadzabe kuvishwa ngozi ya mnyama ni ishara ya pongezi kwa mtu aliyefanikisha kukamatwa mnyama wakati wa uwindaji. Picha na Abuu Kimario - Bodi ya Filamu Tanzania


SERIKALI IMEKAMATA VYOMBO 2795 KATIKA KUZUIA UVUVI HARAMU.

0
0
Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.
Serikali kupitia Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi katika kipindi cha mwaka 2010-2015 imekamata   vyombo 2795,injini za Mitumbwi 118,magari 297 na pikipiki 33 kwa sababu ya uvuvi haramu na utoroshwaji haramu kupitia  maziwa makubwa,mwambao wa Bahari ya Hindi na Mipaka ya Nchi.

Hayo yamesemwa leo Bungeni na Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe.William Ole Nasha wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Fakharia Khamis.

“Katika kukabiliana na wavuvi haramu,Wizara imeanzisha na kuimarisha vituo 25 vya Doria kwenye Maziwa makuu,Mwambao wa Bahari ya Hindi na mipaka ya nchi”Alisema Mhe.Ole Nasha.

Aidha amesema kuwa kuwepo kwa vituo hivyo kumeongeza uwezo wa kukabiliana na uvuvi na biashara haramu kupitia operesheni mbalimbali  ambapo pamoja na jitihada za Serikali tatizo hili bado linaitaji mkazo mkubwa sana katika maneo ya mialo na masoko.

Aidha Serikali imeanzisha kikosi kazi cha Kitaifa Mult Agency Task Team (MATT) ambacho kinafanya kazi ya kudhibiti uhalifu wa mazingira ikiwemo kudhibiti uvuvi haramu hususan matumizi ya mabomu katika shughuli za uvuvi uku pia Maboresho ya Sera,Sheria,na Kanuni za Uvuvi zikifanyiwa kazi ili kuimarisha usimamizi na matumizi endelevu ya rasilimali za uvuvi nchini.

Kwa upande mwingine katika kipindi hicho cha 2010-2015 watuhumiwa 3792 walikamatwa na kesi 243 zilifunguliwa mahakamani ambapo pia jumla ya  shilingi 158,559,323 zilikusanywa ikiwa ni faini kutokana na makosa mbalimbali uku watuhumiwa 11 wakifungwa.

Mhe.Ole Nasha pia alitoa wito kwa wabunge ambao ni wajumbe katika halmashauri waendelee kutoa elimu kwa wavuvi kuhusu madhara ya uvuvi haramu, na kuhimiza Halmshauri zao katika kudhibiti uvuvi haramu kwenye maeneo yao.


“Naziomba Jamii za Wavuvi na wadau wote washirikishwe katika kusimamia rasilimali za uvuvi na matumizi endelevu kwa ajili ya kuwapatia wananchi ajira,chakula na uchumi wao na Taifa kwa ujumla ili kudhibiti uvuvi haramu”Alisisitiza Mhe.Ole Nasha.

ZURIEL'S ANNUAL DUSUSU AWARDS - 2017

0
0
It is possible you have heard or read about Zuriels annual DUSUSU Awards, which she presents to an African First Lady, whose work in the area of Girls Education in their countries exemplifies Zuriels belief in the need for not just political office holders, but non office holders to fight for, on the African continent.
She began this initiative in 2014, after her maiden First Lady's colloquy she convened in Lagos in April 2014. That year, the DUSUSU First Lady Award went to Salma Kikwete of Tanzania, in 2015 to Margaret Kenyatta of Kenya, and in 2016 to Monica Geingos of Namibia.
What makes this award very personal to the First Ladies who receive it is that there is nothing 'political. or 'economically driven' about it, rather, it is being presented by a Girl, who is not just passionate about Girls Education and globally recognized for it, but she herself recognizes the singular efforts of those on the African continent - First Ladies, who are quietly but measurably making a difference in this fight. So as it were, more than any other Award these First Ladies receive, this one is very dear to them as well.

It is also unique, because they cannot campaign for it, and are not privy in any way to the selection criteria, otherwise, they could position themselves for it.
Announcement Next Week
Zuriels committee would be announcing the recipient for the Awards next week, and she would be making the travel to the recipients country to personally present the Award, as she has done in the past, in the State House, Presidential Palace, or Prime Ministers Residence - as applicable.



JAMES BOND AFARIKI DUNIA

0
0
 Roger Moore, muigizaji marufu wa sinema aba za ujasusi za James Bond kati ya mwaka 1973 na 1985, amefaruiki dunia kwa ugonjwa wa saratani, kwa mujibu wa familia yake. Amefariki akiwa na umri wa miaka 89.
"Tunajua kwamba mapenzi yetu kwako na kuhusudiwa vitakuzwa mara nyingi ulimwenguni kote na watu waliomfahamu kutokana na filamu zake, maonesho katika TV na ukereketwa wake kwa kuifanyia kazi  UNICEF ambayo aliamini ni fanaka kubwa katika maisha yake", watoto wake Deborah, Geoffrey na  Christian, wamesema katika taarifa iliyowekwa kwenye akaunti yake rasmi ya Twitter siku ya Jumanne.
Familia hiyo itafanya mazishi yake ya kifamilia huko Monaco, kama alivyohusia yeye mwenyewe, taarifa hiyo inaeleza.

Marehemu Moore alijulikana zaidi kama mtu aliyemrithi muigizaji Sean Connery katika mlolongo wa sinema za James Bond.


Timu ya Azania yawasili nchini baada ya kushiriki kwenye mashindano ya Standard Chartered Uingereza

0
0
Mashindano ya kombe la Standard Chartered yaliyokuwa yanafanyika nchini Uingereza yamemalizika na kombe hilo kutwaliwa na timu ya nchini Singapore. 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kuwasili timu ya Azania iliyowakilsiha nchi za Afrika ya Mashariki, Meneja Uhusiano wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Mariam Sezinga amesema timu ya Azania ilikwenda Uingereza kushindana kwenye mashindano ya “Standard Chartered-Road to Anfield” iliyokuwa inahusisha wateja wa benki hiyo. Timu zilizoshiriki kwenye mashindano hayo zilikuwa ni timu nane kutoka Singapore, Uingereza, India, Nigeria, Botswana, Honk Kong, Korea na Tanzania.
Meneja Uhusiano wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Mariam Sezinga (nguo nyeusi) akiwasili na Wachezaji wa Timu ya Azania katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wakitokea nchini Uingereza kwenye mashindano ya kombe la Standard Chartered-Road to Anfield 2017.

Katika michuano hiyo timu ya Azania iliweza kutinga nusu fainali ambapo ilicheza na Uingereza na kutolewa kwa mikwaju ya penati. Timu ya Singapore iliibuka mabingwa wa kombe Standard Chartered –Road to Anfield kwa mwaka 2017. Mariam alisema timu hiyo imefanya vizuri kwenye mashindano hayo japo hawakufanikiwa kutwaa kombe hilo mara baada ya kutolewa kwenye michuano hiyo. Alisisitiza wao kama Benki ya Standard Chartered Tanzania hawajakata tamaa na hii ilikuwa ni fursa nzuri kwa vijana kuonesha vipaji vyao ili kufikia malengo waliyojiwekea. 
 Na pia ameipongeza timu ya Azania kuiwakilisha vyema Tanzania kwa kuwa ni mara ya kwanza kuingia kwenye mashindano hayo na pia wamejitahidi kupigana mpaka kufikia kuingia nusu fainali ya mashindano hayo. Nahodha wa timu ya Azania, Khalid Sultan Said ameishukuru benki ya Standard Chartered Tanzania kwa kuona umuhimu wa michezo hapa nchini na wameweza kujifunza mengi kwenye michuano hiyo iliyokuwa ikiendeshwa nchini Uingereza ambapo timu yao ilitolewa kwenye nusu fainali. Lakini wao wanaamini hapa ni mwanzo na watapigana mpaka siku kombe liweze kutua hapa nchini. 
 Wachezaji wa timu ya Azania wakiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakitokea nchini Uingereza. 
 Meneja Uhusiano wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Mariam Sezinga (wa tatu kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wachezaji wa Timu ya Azania mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wakitokea nchini Uingereza kwenye mashindano ya kombe la Standard Chartered-Road to Anfield 2017.

 Wachezaji wa Timu ya Azania wakiwasiliana na ndugu jamaa na marafiki mara baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakitokea nchini Uingereza.

Rais Magufuli amteua Bw. Tixon Nzunda kuwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI - Elimu

CHATO WATAKIWA KUCHANGAMKIA KILIMO CHA MIHOGO CHENYE TIJA ILI KUINGIA KATIKA SOKO LA KIMATAIFA

0
0
Na Dotto Mwaibale, Chato

MAOFISA Ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita wameombwa kuwa weredi zaidi katika masuala ya kilimo ili elimu waliyonayo waweze kuitoa kwa wakulima ili nao waweze kulima kilimo chenye tija cha zao la mihogo ili zao hilo liweze kukubalika katika soko la kimataifa.

Mwito huo umetolewa na Mtaalamu wa masuala ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru jijini Mwanza, Dk. Jeremiah Simon wakati akitoa mafunzo kwa maofisa Ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita leo ambayo yameandaliwa na Tume ya Sayansi ya Teknolojia (Costech) kupitia Jukwaa la Wazi la Bioteknolojia kwa manufaa ya kilimo (OFAB). 

Alisema hivi sasa nchi ya China na Tanzania zimesaini mkataba wa ununuzi wa zao la muhogo jambo ambalo ni fursa kwa wakulima wetu wa hapa nchini wakiwemo wa kutoka wilaya ya Chato.

"Hii ni fursa kubwa kiuchumi lakini ni vema sasa tukaingia katika kilimo chenye tija ili mihogo yetu iweze kuingia katika soko la kimataifa badala ya kuendelea na kilimo kisicho na tija" alisema Simon.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita (RAS), Selestine Gesimba akiwaonesha shamba la mfano la mahindi ambalo lipo nje ya ofisi yake wataalamu hao wa kilimo pamoja na wanahabari (hawapo pichani). Kulia ni Mshauri wa Jukwaa la Kilimo na Bioteknojia (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange na kushoto ni Mratibu wa Jukwaa hilo Tanzania, Philbert Nyinondi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita (RAS), Selestine Gesimba akionesha shamba la mfano la alizeti ambalo lipo nje ya ofisi yake. Kushoto ni Mratibu wa Jukwaa hilo Tanzania, Philbert Nyinondi.
Zao la alizeti likioneshwa.
Ofisa Program wa OFAB kutoka Shirika la AATF, Suleiman Okoth (wa nne kutoka kulia), akiwa na wataalamu hao wakilimo wakati wakiangalia bwawa la samaki la mfano lililopo nje ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Geita.

WASICHANA 8000 KUNUFAIKA NA MRADI WA UNESCO WA ELIMU

0
0
Wasichana 8,000 waliopo shuleni na 600 ambao hawako shuleni watanufaika na mradi mkubwa wa kuwawezesha wasichana na wanawake vijana kupata elimu. Mradi huo wa miaka minne wenye gharama ya dola za Marekani milioni 5 utafanyika katika wilaya tano nchini. 

 Wilaya hizo ni Ngorongoro, Kasulu, Sengerema, Micheweni na Mkoani. Mradi huo ambao upo hatua ya pili umeanza kwa kongamano lililofunguliwa jana na Katibu Mkuu wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Dk Leonard Akwilapo. Mgeni rasmi kwenye kongamano hilo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt Leonard Akwilapo akifungua rasmi kongamano la viongozi mbalimbali wa wizara na wilaya tano nchini kujadili na kupanga mikakati ya namna bora ya kuwawezesha wasichana na wanawake vijana katika wilaya husika kupata elimu katika kipindi cha miaka minne ijayo.

Mradi huo mkubwa kwa mujibu wa Katibu mkuu huyo umelenga kuwaokoa wanafunzi kabla hawajakumbwa na matatizo yanayokatisha masomo yao. Aidha utawapa fursa za kuboresha zaidi mafunzo mbalimbali waliyonayo ambao utawafanya kuwa watu wazuri zaidi katika jamii na hivyo kuchangia maendeleo ya taifa na jamii walizopo. 

 Katibu mkuu huyo ambaye alifungua kongamano na kuzindua mradi huoi awamu ya pili alisema kwamba ni matumaini yake kwamba jamii itaukumbatia mradi huo ili kuwa na taifa lenye mafanikio makubwa katika malengo ya maendeleo endelevu ya dunia kwa kuzingatia lengo namba tano. Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akitoa neno la ufunguzi katika kongamano la viongozi mbalimbali wa wizara na wilaya tano nchini kujadili na kupanga mikakati ya namna bora ya kuwawezesha wasichana na wanawake vijana katika wilaya husika kupata elimu katika kipindi cha miaka minne ijayo.

 Amewataka wazazi na vijana kutimiza wajibu wao kwa kubadilika kitabia na kutambua umuhimu wa elimu katika kufanikisha wanachotaka ambacho ni maendeleo binafsi , familia na taifa kwa ujumla. Katika hotuba yake alisema ni matumaini kwamba wadau katika mradi huo watafaikisha katika kipindi cha miaka minne mipango yote iliyolenga kuboresha huduma kwa wasichana na wanawake vijana, kushawishi jamii kubadilika na kuachana na tamaduni mbaya kama ndoa za utotoni na ukeketaji. 

 Naye Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na utamaduni UNESCO, Zulmira Rodrigues alisema mradi huo ulioanza mwaka jana na kufanyiwa tathmini umeonesha changamoto kubwa ya watoto wa kike ikiwamo mimba za utotoni,ukeketaji na kushindwa masomo. Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la misaada Korea International Cooperation Agency (KOICA) nchini, Joonsung Park akitoa neon kuhusu ufadhili wa KOICA ambao imeutoa katika mradi huo na mipango yao ya kusaidia Tanzania



MAGAZETI YA LEO JUMATANO MAY 24,2017

PROF. MBARAWA AITAKA BODI YA DMI KUBORESHA MIUNDOMBINU

0
0

Serikali imeitaka Bodi ya Chuo Cha Bahari Dar es Salaam (DMI), kuhakikisha inaboresha miundombinu ya chuo na kuzingatia miiko na kanuni za ufundishaji ili wanafunzi wanaohitimu chuoni hapo waweze kukidhi mahitaji ya soko.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amesema hayo leo jijini Dar es salaam, wakati akizindua bodi hiyo na kusisitiza kuweka mikakati madhubuti ya kuboresha majengo kwa kutangaza zabuni kwa uwazi ili kuepuka mianya ya rushwa.

“Hakikisheni mnakuwa na mpango madubuti wa kuboresha majengo ya chuo ili chuo kibaki na hadhi yake, lakini pia hakikisheni mntoa elimu bora kwa wanafunzi wanaokuja kusoma hapa ili waweze kupata misingi imara itakayowawezesha kuajiriwa ndani na nje ya nchi mara baada ya kuhitimu masomo yao”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Ameongeza kuwa Serikali ina uhitaji wa wataalam wengi kwenye masuala ya bahari hivyo ni wajibu wa bodi kusimamia chuo na kuhakikisha wataalam hao wanazalishwa kwa wingi chuoni hapo ili kukidhi mahitaji ya soko kitaifa na kimataifa.

Amewataka wakufunzi wa chuo hicho kuhakikisha wanatumia lugha nzuri kwenye ufundishaji ili kuwaweka wanafunzi karibu na kuhakikisha wanapata taaluma inayotakiwa kwani kuwepo kwa waalimu hao kunategemea kuwepo kwa wanafunzi.

“Ni lazima tufungue milango kwa wanafunzi sababu wapo wanaoelewa haraka na wanaoelewa taratibu, hivyo tukae nao muda mrefu ili kubaini changamoto zao lakini pia tuwe waangalifu juu ya matumizi ya lugha tunazotumia kwa wanafunzi wakati tunapofundisha”, amefafanua Prof. Mbarawa.

BancABC wins best emerging Bank in Tanzania

0
0

BancABC has been announced as the Best Emerging Bank in Tanzania for the year 2017. The bank won the award during The Banker Africa – East Africa Awards 2017 which were held in Nairobi last week.

Speaking during the event which was held at Kenya’s capital crown plaza, Robin Amlot who is the CEO of CPI Financial, the organizers of the Awards, said that the annual Banker Africa Awards are continent – wide programmes open to all banks and financial institutions in Africa. ‘The aim of this award is to recognize outstanding performance and excellence in the financial services industry’, said Amlot.

To his part, BancABC Managing Director Dana Botha said that winning the award has proven the bank’s commitment which is fully aligned to our vision to be the premier financial service institution in sub – Saharan Africa and to obtain top 5 market position in countries of operation.



‘We have always been working hard to achieve better results and would like to thank our customers who voted for us. BancABC which is part of Atlas Mara has been named in the 2017 Banker Africa, East Africa Awards as the Best Emerging Bank in Tanzania. The results are based on nominations and votes from the Bankers’ subscribers. It has been our objective for the bank to have awards whilst we fix our value propositions for excellence’, said Botha.
BancABC wins Best Emerging Bank in Tanzania Award during The Banker Africa – East Africa Awards 2017 at the ceremony held last week in Nairobi at the crown plaza. From left to right: Mr. Robin Amlot CEO of CPI Financial, Ms Upendo Nkini , Head of Marketing - BancABC, Ms Joyce, Malai Head of Retail & Business Banking, Mr. Dana Botha Managing Director, Mr. Imani John – Head of Finance and Mr. Matthew Amlot Editor of Banker Africa.

OFISI YA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI QATAR YAZINDULIWA RASMI

0
0


Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar yazinduliwa rasmi.

Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar zilizinduliwa rams tarehe 19 Mei 2017. Shughuli za ufunguzi ziliongozwa na Mhe. Fatma Mohammed Rajab, Balozi wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Qatar ambaye alisaini kitabu cha wageni kuashiria kuanza rasmi kwa shughuli za Ubalozi.

Wawakilishi wa makundi mbalimbali ya Watanzaia wanaoishi nchi Qatar walishiriki katika hafla hiyo.

Mhe. Balozi alitumia fursa hiyo kuzungumza machache na Watanzania walioshiriki. Aliwaeleza kwamba kufunguliwa kwa Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar ni sehemu ya kutekeleza malengo ya Serikali ya Tanzania ya kusogeza huduma zake kwenda kuwekeza Tanzania hususan katika sekta ya viwanda. Aliwahakikishia kwamba Ubalozi utawapatia ushirikiano watakaouhitaji katika kufanikisha azma hiyo.

Balozi aliwapongeza Watanzania hao kwa kuendelea kuwa na sifa nzuri nchini Qatar na kudumisha mshikamano miongoni mwao. Aliwahimiza waendelee kuwa raia wema na kulinda haiba na jina la Tanzania kwa kufuata sheria za nchi wanapoishi. Alisema milango ya Ubalozi itakuwa wazi kupokea ushauri wao katika mambo ambayo yatalenga kuleta tija na mafanikio kwa taifa. 

Naye Bw. Said Ahmed, Mwenyekiti wa Watanzania wanaoishi Qatar aliishukuru Serikali kwa kusikia kilio chao na hatimaye kufungua Ubalozi na kuwa na Balozi Mkazi nchini Qatar. Alimueleza Balozi kwamba jamii ya Watanzania wanaoishi Qatar itashirikiana na Ofisi za Ubalozi na kufanya kazi bega kwa bega katika kuitafutia maslahi Tanzania. Wawakilishi hao waliomba Ubalozi uandae mkutano mkubwa utakaowawezesha Watanzania wengi zaidi kushiriki ili kusikia maoni yao na changamoto zinazowakabili. Balozi aliahidi kufanya mkutano huo mapema iwezekanavyo. 

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, 
Doha, Qatar 24 Mei, 2017 .
Mhe. Fatma Mohammed Rajab, Balozi wa Tanzania nchini Qatar akiongea na Watanzania waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar 
Mhe. Balozi Fatma Mohammed Rajab akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar 

Waziri Mahiga Aongoza Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa SADC nchini Lesotho

0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, amezihimiza taasisi za Serikali na za dini nchini Lesotho kudumisha amani na usalama kwenye kipindi cha uchaguzi na baada ya uchaguzi mkuu nchini hapa ili kuwezesha Serikali itakayoingia madarakani kufanya kazi kwa ufanisi zaidi kwa ajili ya wananchi wa Lesotho. 

Uchaguzi huo mkuu wa wabunge ambao ni wa tatu kufanyika ndani ya kipindi cha miaka mitano, unatarajiwa kufanyika tarehe 3 Juni 2017 ambapo vyama 26 kati ya 30 vilivyojiandikisha, vitashiriki kwenye kinyang’anyiro hicho cha kuchagua wawakilishi Bungeni. 

Kwa mujibu wa Katiba ya Falme ya Lesotho, kiongozi wa chama kitakachoshinda viti vingi zaidi vya ubunge kwenye uchaguzi huo ndiye atakayeapishwa kuwa Waziri Mkuu na Kiongozi wa Serikali, ambapo mkuu wa nchi na mtawala mkuu anaendelea kuwa Mfalme Letsie III. 

“Wakati umefika sasa kwa Jumuiya yetu ya SADC kushiriki kwenye uangalizi wa uchaguzi huu tukiwa na habari njema ya kurejesha matumaini kwa wananchi kuhusu mustakabali wa uongozi. Lakini pia tuwe na ujumbe mzito kwa Serikali ijayo ili iweze kufanya mageuzi ya kweli kwenye nyanja mbalimbali kwa manufaa ya wananchi” Mhe. Mahiga amehimiza kwa wajumbe wa timu ya waangalizi wa uchaguzi.

Tangu alipowasili nchini hapa tarehe 22 Mei 2017, Dkt. Mahiga na ujumbe wake wamekutana na wadau mbalimbali wakiwemo Tume Huru ya Uchaguzi ya Lesotho na Umoja ya Makanisa wa Lesotho kwa lengo la kupata maoni ya kina kabla ya kuzindua Timu ya Uangalizi ya SADC (SADC Elections Observersion Mission - SEOM) tarehe 25 Mei 2017. 
Dr. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrioka Mashariki na Mkuu wa Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa SADC akizungumza na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Lesotho, Mhe. Jaji Mstaafu Lesao Lehohla (wa pili kutoka kulia) alipotembelea tume hiyo mjini Maseru Lesotho kabla ya kuzindua rasmi Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi ya SADC. 
Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Mkuu wa Umoja wa Makanisa wa Lesotho Archbishopp Gerald Tlali Lerotholi na ujumbe wake alipotembelea ujumbe huo kusikiliza maoni yao kuhusu uchaguzi mkuu nchini humo unaotarajiwa kufanyika tarehe 3 Juni 2017. 
Dkt. Mahiga na ujumbe wake wakikamilisha majumuisho ya mikutano mbalimbali waliyoifanyana na wadau . 
 Dkt Mahiga akiagana na wenyeji wake nje ya Tume Huru ya Uchaguzi. 


Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images