Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1696 | 1697 | (Page 1698) | 1699 | 1700 | .... | 3284 | newer

  0 0

   Mhusika mkuu katika Mchezo wa Jukwaani wa 'UNTOLD SORY ' Amani Kipimo akiwa jukwaani katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini dar es Salaam.
   Sehemu ya Waigizaji  wa mchezo wa kuigiza wa Untoldy Story wakiwa jukwaani  wakati wa utambulishwaji wa mchezo huo
   Msanii mkongwe wa Luninga na Jukwaani Susan Lewis akiwa na Mhusika mkuu wa mchezo wa Untold Story Amani Kipimo 'Ngasu'
   sehemu ya watu waliofika kushuhudia mchezo huo wa Untold Story ambao ulibua hisia na kuwa gumzo kwa watu wengi sana.


  0 0

  Katibu Mkuu wizara ya Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Salum Maulid Salum, akizungumza kwenye ufungaji wa semina kwa wajasiriamali, juu ya mtangamano wa Afrika Mashariki, iliofanyika uwanja wa Gombani Chakechake Pemba,  na kutayarishwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
  Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe: Issa Haji Ussi “Gavu’ akizungumza kwenye ufungaji wa semina ya siku nne, kwa wajasiriamali kisiwani Pemba, juu ya mtangamano wa Afrika Mashariki, iliofanyika uwanja wa Gombani Chakechake.
  Wajasiriamali, wafanyabiashara na baadhi ya wakuu wa taasisi za serikali kisiwani Pemba, wakisikiliza hutuba ya Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe: Issa Haji Ussi “Gavu’ wakati akifunga semina juu ya mtangamano wa Afrika Mashariki, iliofanyika uwanja wa Gombani Chakechake.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Fatma Salum- MAELEZO.

  Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imeanza rasmi utekelezaji wa mradi wa kukarabati Shule ya Sekondari Pugu iliyopo Jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi mkataba wa ujenzi kwa Mkandarasi wa mradi ambaye ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bibi. Graceana Shirima alieleza kuwa zaidi ya shilingi milioni 984 zitatumika katika awamu ya kwanza ya ukarabati wa shule hiyo.

  “Awamu ya kwanza ya ukarabati wa shule hii itaanza tarehe 1 Juni, 2017 na itafanyika kwa muda wa miezi minne. Ukarabati katika awamu hii utahusisha madarasa, vyoo kwa ajili ya wanafunzi walemavu, mabweni, jengo la utawala, mifumo ya TEHAMA, mifumo ya maji safi na maji taka pamoja na mifumo ya umeme”alifafanua Bibi. Shirima.

  Alieleza kuwa zoezi hilo la ukarabati lilitanguliwa na upembuzi yakinifu wa kubaini hali halisi ya mahitaji ya ukarabati na kazi hiyo ilifanywa na Mtaalamu Elekezi (Consultant).

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bw. Msongela Palela alipongeza jitihada za TEA za kukarabati miundombinu ya elimu hasa kwa shule kongwe za Sekondari nchini kote mradi ambao utasaidia kuboresha elimu na kuwezesha wanafunzi kusoma katika mazingira bora.
  Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bibi. Graceana Shirima akiongea wakati wa hafla ya makabidhiano ya mkataba wa ukarabati wa shule ya Sekondari Pugu ya Jijini Dar es Salaam unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa ufadhili wa TEA.
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bw. Msongela Palela akizungumzia faida zinazotokana na mradi wa ukarabati wa shule ya Sekondari Pugu ya Jijini Dar es Salaam unaofanywa na shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa ufadhili wa Mamlaka ya Elimu.
  Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bibi. Graceana Shirima akimkabidhi mkataba wa ukarabati wa shule ya Sekondari Pugu Jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi Uendelezaji Miliki NHC Bw. Hassan Mohamed, ukarabati huo unafanywa na Shirika la Nyumba la Taifa.

  Baadhi ya Majengo ya Shule ya Sekondari Pugu yatakayofanyiwa ukarabati na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa ufadhili wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) na yatagharimu zaidi ya milioni mia tisa. (Picha zote na Frank Mvungi-Maelezo).

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kimetakiwa kuhakikisha kwamba wanatumia vyema kijiji cha kidigitali cha Ololosokwan katika kuhakikisha kwamba taifa linakuwa na uwezo mkubwa katika tiba mtandao.

  Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya wakati akifunga warsha ya siku 2 ya tiba mtandao iliyofanyika chuoni hapo. 

  Warsha hiyo ilikuwa inakokotoa tiba mtandao ili kuwezesha mradi wa majaribio wa Tiba mtandao unaohusisha wadau mbalimbali kutekelezwa. Kitovu cha mradi huo ni kijiji cha Ololosokwan kilichopo Waso wilayani Ngorongoro. 
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya akizungumza na wataalamu kutoka KCMC, MUHAS wadau kutoka The Africa Foundation, Aga Khan Foundation, Ubalozi wa Uswisi, Bill & Melinda Gates Foundation, XPRIZE pamoja na Maafisa wa afya wa mikoa na wilaya za Arusha na Ngorongoro walioshiriki kwenye warsha ya siku mbili ya tiba mtandao iliyofanyika MUHAS jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Thebeauty.co.tz)

  Katibu huyo alisema kutumia kikamilifu kwa kijiji hicho hakumaanishi kuwa na majengo bali kutumia kufunza wataalamu mbalimbali kutokana na ukweli kuwa kijiji hicho sasa kitakuwa mfano wa utendaji katika kusaidia wananchi wa Tanzania. 

  “Uwapo wa kijiji hiki ni tukio kubwa kwetu kwani ni kijiji cha kujifunzia, namna ya kutibu, namna ya kukusanya takwimu namna ya kubaini mahitaji na … ni mfano wa namna gani teknolojia inaweza kufanya mambo makubwa” alisema Ulisubisya . 

  Alisema yeye anaamini kwamba si lazima wataalamu watiba wafundishwe eneo moja, kama ilivyo sasa, lakini wanaweza kufundishwa katika eneo kama Ololosokwan na hivyo kuwajenga pia kisaikolojia kwamba wanaweza kufanyakazi pembezoni bila ya tatizo. 
  Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (kushoto) akichangia jambo wakati wa kuhitimisha warsha ya siku 2 ya tiba mtandao iliyofanyika chuoni hapo. Wa pili kushoto ni mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof Ephata Kaaya (wa pili kulia) na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Prof Eligius Lyamuya (kulia).

  Alisema mafanikio ya dhana ya tiba mtandao yatasaidia sana kuboresha hali ya watanzania kwa kuwa mahitaji yao yatajulikana mapema na kutokana na ukweli kuwa mradi wenyewe unahusisha pia ukusanyaji wa data wa uhakika kwa kuzingatia mahudhurio ya watu na magonjwa yao. 

  Pia alisema kwa utekelezaji thabiti utaonesha namna ambavyo Watanzania tuko mbele na kusema kwamba mradi huo wa tiba mtandao anauelewa na ameupigania sana nje ya nchi ambako amekwenda kuzungumza. 

  “Mwaka jana mwezi Desemba nilienda kwenye mkutano Washington unaohusu Tiba mtandao na tumeuza sana hili wazo la tiba mtandao kwa wenzetu, kwa hiyo watakuja kujifunza tunafanyaje” alisema Dk. Ulisubisya na kuongeza kwamba Wizara yake itatoa ushirikiano wa kutosha kuona dhana hiyo inatekelezeka tena kwa ufanisi. 
  Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi - Muhimbili (MUHAS), Prof Eligius Lyamuya (kulia) akitoa maoni wakati wa kufunga warsha ya siku 2 ya tiba mtandao iliyofanyika chuoni hapo.


  0 0

  Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar imesema itakuwa ya mwanzo kuanza kutumia fursa za mikopo nafuu inayotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) ili kuchagiza uwekezaji katika sekta ya uchakataji wa mazao na masoko ili kuongeza tija kwa maendeleo visiwani Zanzibar.

  Mkakati huo umewekwa bayana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Bakari H. Bakari wakati akizungumza na ugeni kutoka TADB uliomtembelea Ofisini kwake.

  Bw. Bakari amesema kuwa ujio wa Benki hiyo unatoa fursa kubwa sana kwa sekta zilizo chini ya wizara yake ikiwamo biashara, viwanda na masoko.

  “Tuna imani kubwa ujio wa TADB utatusaidia kutatua changamoto zinazozikabili sekta hizi ambazo zinakabili na changamoto ikiwemo ukosefu wa masoko ya mazao; ufinyu wa bei za mazao; miundo mbinu mibovu ya usafirishaji; maghala ya kuhifadhi mazao; nishati ya umeme na miundombinu hafifu vijijini; ufinyu au kutokuwepo kwa ongezeko la thamani kwa mazao ya kilimo; mabadiliko ya hali ya hewa; na mmomonyoko wa udongo,” alisema.

  Akizungumza wakati wa mazungumzo hayo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Francis Assenga alisema uanzishwaji wa TADB unatokana na Serikali kutambua umuhimu wa uwekezaji wenye tija kwenye maeneo yote ya sekta ya kilimo na kuleta mapinduzi ya dhati ya Kilimo ili kuwezesha upatikanaji wa mikopo na mitaji ya riba nafuu  ikiwa ni pamoja na kuhamasisha mabenki na taasisi zingine za fedha nchini kutoa mikopo zaidi kwenye sekta ya Kilimo.

  Bw. Assenga alisema visiwa vya Zanzibar vitaingizwa rasmi katika mpango wa biashara wa Benki na ametoa wito kwa wakulima na wafanyabiashara wa mazao ya kilimo visiwani humo kuchangamkia fursa zinazotolewa na TADB.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar, Bw. Bakari H. Bakari (katikati) akiongoza kikao cha pamoja na Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB), kilichofanyika katika Makao Makuu ya Wizara hiyo.
   Mjumbe wa Bodi ya TADB, Bibi Rehema Twalib ambaye ni Mkuu wa Msafara huo (wapili kulia) akizungumza wakati walipotembelea Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar, Bw. Bakari H. Bakari.
   Wajumbe wa kutokana TADB wakifuatilia kwa makini mazungumzo na uongozi wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar. Mazungumzo hayo yalifanyika katika Makao Makuu ya Wizara hiyo.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na: Nuru Juma-MAELEZO.

  Daktari Mshauri kutoka Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA) Dkt. Ali Mzige amewataka watanzania kuepuka uzito mkubwa na kitambi ili kufanya miili yao kukaa mbali na magonjwa yanayosababishwa na vitu hivyo.

  Dkt. Mzige amezungumza hayo leo katika ukumbi wa maelezo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari.

  Aliongeza kuwa watu wengi wanachukulia kawaida na wengine wanapenda kuwa na kitambi na uzito mkubwa lakini ni vitu vyenye madhara makubwa na husababisha magonjwa ambayo ni magumu kutibika.

  “Unene uliokithiri huleta shida kwenye moyo, shinikizo kubwa la damu,kisukari, saratani za aina mbalimbali, kushindwa kupumua vizuri na magonjwa mengine mengi hivyo watu wanatakiwa kuepuka ili kujinusuru na magonjwa hayo,” alisema Dr Mzige.

  Aliongeza kuwa tafiti zinaonyesha asilimia kubwa wanawake wanavitambi na uzito uliokithiri kuliko wanaume hali inayotokana na wanawake wengi kupendelea kula vyakula vyenye mafuta mengi.

  Aidha aliwataka watanzania kuwa na utamaduni wa kula vyakula vya asili,kufanya mazoezi na kupima afya zao mara kwa mara ili kujua mapema kama ana tatizo lolote la kiafya na kujiepusha na maradhi yanayoweza kuepukika.

  Aliongeza kuwa uzito wa mtu unatakiwa kulingana na umri na urefu kwani mtoto wa mika 5 anapaswa kuwa na kilo 18, kijana mwenye miaka 14 mvulana kilo 48 na msichana kilo 49 huku mtu mzima mwanaume mwenye urefu wa futi 5 na inchi 8 anapaswa kuwa na kilo 68.

  Tiba nzuri na iliyosahihi ya kuepuka maradhi mengi ni kutokaa masaa 4 bila kufanya kazi,kuzuia kitambi kisijitokeze kwa kula kiasi cha chakula kinacholingana na mahitaji yako, kupunguza ulaji wa sukari na mafuta na kuepuka unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara.
  Mshauri wa Afya ya Jamii kutoka Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), Dkt. Ali Mzige akionyesha Jarida linaloandaliwa na Shirika la Afya Duniani wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa kujua magonjwa katika ngazi ya familia alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), Dkt. Mashombo Mkamba. 
  Picha na: Frank Shija - MAELEZO 


  Mwenyekiti wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), Dkt. Mashombo Mkamba akielezea jambo kuhusu umuhimu wa kujua magonjwa katika ngazi ya familia alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mshauri wa Afya ya Jamii kutoka Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), Dkt. Ali Mzige 
  Mshauri wa Afya ya Jamii kutoka Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), Dkt. Ali Mzige akifafanua jambo kuhusu umuhimu wa kujua magonjwa katika ngazi ya familia alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA). 

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB PLC, Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya Wanahisa wa Benki hiyo, iliyofanyika leo kwenye katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.Semina hiyo, itafuatiwa na Mkutano Mkuu wa 22 wa Wanahisa wa Benki hiyo, utakaofanyika kesho Mei 20, 2017.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB PLC, Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya Wanahisa wa Benki hiyo, iliyofanyika leo kwenye katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha. Semina hiyo, itafuatiwa na Mkutano Mkuu wa 22 wa Wanahisa wa Benki hiyo, utakaofanyika kesho Mei 20, 2017.
  Mwenyekiti wa semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB, Mwasajuni akiongoza semina hiyo
  Katibu wa Benki ya CRDB, John Rugambwa akipitia moja ya vitabu vya mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye semina ya Wanahisa wa Benki hiyo, iliyofanyika leo kwenye katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.
  Mkurugenzi wa Masoko, Utafitii na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB PLC, Tully Mwambapa akifatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye semina ya Wanahisa wa Benki hiyo, iliyofanyika leo kwenye katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.
  Naibu Wakurugenzi  Watendaji wa Benki ya CRDB PLC,  Saugata Bandyopadhyay (kulia) na Esther Kitoka wakiteta jambo, wakati wa ufunguzi wa semina ya Wanahisa wa Benki hiyo, iliyofanyika leo kwenye katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.


  0 0


  Na Karama Kenyuko, Globu ya Jamii

  Wafanyabiashara wa kemikali Bashirifu wameaswa kufuata sheria za nchi Katika kudhibiti matumizi yasiyokuwa salama ya kemikali hizo.

  Hayo yamesemwa Leo na Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya kampuni ya Tecno Net Scientific kukutwa na Kemikali Bashirifu bila ya kuwa na kibali wala usajili.

  Profesa Manyele amesema, mwaka 2014 waliipatia kampuni hiyo usajili wa miaka miwili, lakini baada ya kibali chao kuisha wamekiuka sheria na kuendelea kuagiza Kemikali bashirifu kwa kutumia vibali bandia.

  Ameongeza kuwa, kufuatia kugundua hayo, vyombo vya dola vinafanya uchunguzi wa shughuli za kampuni hiyo na pindi taratibu za uchunguzi utakapokamilika kampuni hiyo itafikishwa mahakamani.

  Aidha ameongeza kuwa, ili kuhakikisha kemikali hizo zinatumika katika hali iliyosalama, wafanyabiashara wote wanaojihusisha na Kemikali, kudhibiti matumizi matumizi yasiyofaa na kuzuia kutumia kwa kutengeneza mabomu, milipiko dawa za kulevya au kutumia kama silaha kama ilivyokuwa kwenye suala la watu kumwagiwa tindikali.

  Aidha Prof. Manyele amesema, wafanyabiashara wote wanaojihusisha na biashara ya Kemikali bashirifu kuhakikisha wanaenda Kutoa taarifa mwenyewe pindi vibali vyao vikiisha ili wapatiwe usajili mpya.Amesema, Serikali haitasita kuwachukulia hatua wafanyabiashara wa kemikali wasiokuwa waaminifu na wanaovunja matakwa ya sheria katika uingizaji na usafirishaji wa Kemikali bashirifu.

  Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa Samwel Manyere akizungumza na waandishi habari juu uingizaji Kemikali bashirifu ambazo zinafuata sheria iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam

  0 0
  Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), umesema utaendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi wa hospitali hiyo na kushughulikia tatizo la upungufu wa wauguzi.
   
  Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru ameyasema hayo leo katika maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani, Tawi la Muhimbili ambayo huadhimishwa Mei 12 kila mwaka. Kauli mbiu ya mwaka huu “ Wauguzi Mbiu ya Kufikia Malengo Endelevu ya Milenia.”
   
  Profesa Museru amesema Serikali ipo bega kwa bega na hospitali hiyo katika kupata ufumbuzi wa tatizo hilo. “Serikali imeahidi kutatua tatizo la upungufu wa wauguzi katika siku chache zijazo,” amesema Profesa Museru.
   
  Amesema uongozi wa hospitali unashughulikia posho za wauguzi na pia 
  kuboresha mazingira ya kazi ili wauguzi watoe huduma bora kwa wagonjwa.
  “Pia uongozi wa muhimbili utaendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi ili wafanye kazi wa ufanisi,” amesema Profesa Museru.
   
  Awali mwakilishi wa wauguzi, Debora Bukuku alisoma risala ikielezea changamoto mbalimbali zikiwamo mazingira magumu na hatarishi ya kazi na pia kupitia risala hiyo waliomba wapatiwe posho za sare pamoja na kuboreshewa maslahi mengine.
   
  Katika hatua nyingine, Mkurugenzi amewataka madaktari na wauguzi kuendelea kuandika machapisho ambayo yanaeleza mafanikio na changamoto za utoaji huduma zilizopo katika hospitali hiyo.
   
  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza na wauguzi leo katika maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani ambayo hufanyika Mei 12,kila mwaka.
  A
   Baadhi ya Wauguzi wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Museru katika maadhimisho hayo.
  A 1
   Baadhi ya Wauguzi wakirudia kiapo kwamba wataendelea kutoa huduma kwa wagonjwa kwa kuzingatia uadilifu.
  A 2
  Muuguzi wa Muhimbili, Furaha Tada akitoa mada kwenye maadhimisho hayo leo.
  A 3
  Wauguzi wakifuatilia mada iliyowasilishwa na mmoja wa wauguzi wa hospitali hiyo.


  0 0


  Mkurugenzi wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF), Fabrizio Colombo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa Tamasha la Filamu za nchi za Majahazi leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mtaalam wa Habari na Masoko wa ZIFF, Bi. Lara Presdon na Meneja wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF), Daniel Nyalusi.
  Mtaalam wa Habari na Masoko wa ZIFF, Bi. Lara Presdon akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa Tamasha la Filamu za nchi za Majahazi leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF), Fabrizio Colombo.
  Mwenyekiti wa Taasisi ya Emerson’s Zanzibar Foundation, Said ELG akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Tuzo ya Filamu itakayotolewa na taasisi yake katika Tamasha la Filamu za nchi za Majahazi leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF), Fabrizio Colombo.
  Baadhi ya waamdishi wa habari wakifuatilia mkutano wa waandaaji wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) leo jijini Dar es Salaam. Picha na: Frank Shija – MAELEZO 

  0 0
 • 05/19/17--06:55: TAARIFA KWA UMMA


 • 0 0

  Mkurugenzi wa Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Leah Kihimbi akimkabidhi bendera ya Taifa mshiriki wa mashindano ya Miss Word Super Model 2017, Miss. Asha Ally Mabula (kushoto) wakati wa hafla ya kumkabidhi bendera hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari – MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam. Miss huyo anatarajia kuondoka nchini leo kuelekea Macau nchini China ambapo atashiriki mashindano hayo. Katikati ni Afisa Utumishi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
  Baadhi ya waandishi wa habari wakishuhudia tukio la kumkabidhi bendera ya Taifa mshiriki wa Miss Word Super Model, Asha Ally Mabula anayetarajia kushiriki mashindano hayo Macau nchini China.
  Mkurugenzi wa Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Leah Kihimbi akizungumza wakati wa tukio la kumkabidhi bendera ya Taifa mshiriki wa mashindano ya Miss Word Super Model 2017, Miss. Asha Ally Mabula (kushoto) leo Jijini Dar es Salaam. Miss huyo anatarjia kuondoka leo kuelekea Macau nchini China ambapo atashiriki mashindano hayo.
  Miss Super Model 2017 Asha Ally Mabula akizungumza wakati wa tukio la kukabidhiwa bendera ya Taifa kwa ajili ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Miss Word Super Model 2017 leo Jijini Dar es Salaam. Miss huyo anatarajia kuondoka leo kuelekea Macau nchini China ambapo atashiriki mashindano hayo. Kutoka kulia ni Afisa Utumishi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Mkurugenzi wa Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Leah Kihimbi na Meneja Mkuu wa Tanzania Miss Super Model Ibrahim Thabit.
  Picha na: Frank Shija – MAELEZO.

  0 0  Mratibu wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa kwa Vijana Tanzania, Tajiel Urioh akizungumza na waandishi wa habari leo (hawapo pichani) kuzungumzia Mkutano Mkuu Kivuli wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa unaokutanisha vijana utakaofanyika kuanzia tarehe 22 hadi 26 mwezi Mei, 2017 mjini Arusha katika Ukumbi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela. Mratibu wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa kwa Vijana Tanzania, Tajiel Urioh akizungumza na waandishi wa habari leo (hawapo pichani) kuzungumzia Mkutano Mkuu Kivuli wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa unaokutanisha vijana utakaofanyika kuanzia tarehe 22 hadi 26 mwezi Mei, 2017 mjini Arusha katika Ukumbi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa Tanzania, Arafat B. Lesheoe.

  AKIZUNGUMZA na waandishi wa habari Mratibu wa Mkutano Mkuu Kivuli wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa, Tajiel Urioh alisema mkutano huo ni maigizo ya vitendo ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa ambapo vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 30 kutoka sehemu mbalimbali wanapata fursa ya kujifunza Diplomasia, Uongozi na namna Umoja Wa Mataifa unavyofanya kazi.

  Bw. Tajiel Urioh alisema kuwa, Mkutano huo unaojulikana kama kongamano kubwa kabisa la vijana nchini linalowaleta pamoja vijana wadogo kutoka nchi mbalimbali tangu mwaka 1997. Aidha aliongeza kuwa Mkutano huo Mkuu Kivuli wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa utafanyika mjini Arusha katika Ukumbi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela kuanzia tarehe 22 hadi 26 mwezi wa Mei mwaka 2017, ambapo vijana takribani 200 kutoka katika nchi mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria kujadili masuala yanayohusiana na Afya ya Uzazi na Uzazi wa Mpango, Demokrasia na Amani katika nchi zinazoendelea, Kuhama kuelekea kwenye Nishati safi na ya teknolojia mbadala na Elimu kwa Maendeleo Endelevu.

  Aliongeza kuwa majadiliano ya mwaka huu yatajikita katika mada kuu: “Kuwawezesha Vijana katika Diplomasia na Uongozi”. Mada hii inalenga kuwezesha ushiriki wa vijana na kuwajengea uwezo kwenye masuala ya Diplomasia na Uongozi kwa kuwapa mafunzo ya vitendo katika mada ngumu ambazo zitawaongezea ujuzi wa majadiliano na kufikia muafaka wa masuala mtambuka yanayogusa maslahi ya mataifa.

  “Tunaishi katika ulimwengu ambao diplomasia yenye ujasiri na uongozi vinahitajika sana hivyo basi kuwakuza vijana katika uwanja huu itachangia kukua kwa mataifa yenye watu wenye uwezo wa kuamua mambo yao. Katika mkutano wa mwaka huu wajumbe watakuja na maazimio mbalimbali ambayo kwa namna moja hama nyingine yatakuwa na manufaa katika maisha yao ya kila siku na watu wanaowazunguka katika jamii zao,” alisema Bw. Urioh.
  Mratibu wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa kwa Vijana Tanzania, Tajiel Urioh akizungumza na waandishi wa habari leo (hawapo pichani) kuzungumzia Mkutano Mkuu Kivuli wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa unaokutanisha vijana utakaofanyika kuanzia tarehe 22 hadi 26 mwezi Mei, 2017 mjini Arusha katika Ukumbi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela. Kushoto ni Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo akiwa katika mkutano huo pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa Tanzania, Arafat B. Lesheoe.

  “Ni matarajio yangu makubwa kwamba mtakuwa tayari kujifunza kuendana na mada kuu ya ‛ Kuwawezesha Vijana katika Diplomasia na Uongozi′ lakini pia kubadilishana mawazo na wajumbe wengine na kutengeneza mtandao wa vijana wenye fikra mnazoendana nazo,” aliongeza Tajiel Urioh, Mratibu wa Kitaifa wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2017.

  Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo alisema kongamano kama hilo la vijana lina umuhimu mkubwa kwa vijana kwani huwajenga vijana kupitia Club za UN. Aliwataja miongoni mwa vijana ambao ni matunda ya Club za UN ni pamoja na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka, Balozi wa Tanzania nchini Japan, Benedict Kikove, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Salum Hapi, Mbunge wa Kibamba (Chadema), John John Mnyika na wengine wengi.

  0 0

   Rais wa Uchezaji wa Mpira wa Miguu Tanzania ‘Free Style Football’ , Morison Jumanne (wakwanza kulia) akizungumza na waandishi wa habari  (hawapo pichani) juu ya maonesho ya kimataifa ya uchezaji wa mpira wa miguu  unaonza leo  katika maeneo mbalimbali ya wazi na mitaa jijini Dar es Salaam, katikati ni Makamu wa Rais wa Uchezaji wa Mpira wa Miguu Tanzania, Pascal Changa na kushoto ni Bingwa wa Dunia  wa Uchezaji wa Mpira wa Miguu 2012 kutoka nchi ya Japan ,Kotaro Tokuda
   Bingwa wa Dunia  wa Uchezaji wa Mpira wa Miguu 2012 kutoka nchi ya Japan ,Kotaro Tokuda akizungumza na waandishi wa habari juu ya ziara yake nchini Tanzania  ni kwa ajili ya maonesho ya wazi ya mchezo huo  Mkoa wa Dar es Salaam.
  Bingwa wa Dunia  wa Uchezaji wa Mpira wa Miguu 2012 kutoka nchi ya Japan, Kotaro Tokuda akionyesha umahiri wa mchezo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.


  0 0

  Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO 
  Kampuni ya Techno Net Scientific inayojishughulisha na uingizaji pamoja na uuzaji wa kemikali imekutwa na kemikali zilizoingizwa nchini kwa njia za udanganyifu kwa kutumia vibali vya bandia. 
  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkemia Mkuu wa Serikali(GCLA), Prof. Samwel Manyele alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kampuni hiyo kukutwa na kemikali bashirifu bila kuwa na usajili wala kibali cha kufanya shughuli za kuuza na kusambaza bidhaa hiyo.
  Prof. Manyele amesema kampuni hiyo ilikuwa na usajili wa miaka miwili kuanzia April 30 mwaka 2014 hadi Aprili 30, 2016 ambapo kwa mujibu wa Sheria ya Kemikali kampuni hiyo ilipaswa kusitisha shughuli zake hadi pale cheti cha usajili kitakapopatikana.
  “Ingawa shughuli zake zilisitishwa lakini kampuni hiyo iliendelea kufanya kazi bila kuwa na cheti cha usajili hivyo ofisi yangu iliungana na Mamlaka ya Kudhibiti dawa za kulevya na Mamlaka ya Chakula na Dawa kufanya ukaguzi wa pamoja ambapo kwa sasa tumewaachia vyombo vya dola kufanya uchunguzi wao” amesema Prof Manyele.
  Amefafanua kuwa Sheria ya Kemikali za Viwandani na Majumbani Sura ya 182 na kanuni zake inatoa masharti kuwa kila mtu anayetaka kujihusisha na shughuli za kemikali kwa namna yoyote ni sharti awe amesajiliwa na kufanyiwa ukaguzi.
  Aidha, ametoa rai kwa wafanyabiashara wote wa kemikali na umma kwa ujumla kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua za kisheria kwa makampuni na wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu na wanaovunja matakwa ya Sheria katika uingizaji, usafirishaji, uhifadhi na utumiaji wa kemikali ikiwemo kemikali bashirifu nchini.
  Prof. Manyele amewaomba wananchi kutoa taarifa na kuwafichua wafanyabiashara wa kemikali wanaokiuka matakwa ya Sheria kwa ajili ya kuchukuliwa hatua stahiki za kisheria ambazo zitapelekea wengine kuwa na matumizi salama ya kemikali na kuzuia madhara kwa watu na mazingira.
   Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Profesa Samwel Manyele (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam kuhusu kampuni ya TECHNO NET SCIENTIFIC kukutwa na kemikali bashirifu bila kuwa na usajili wala kibali cha kufanya shughuli za kuuza na kusambaza kemikali. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Huduma za Ubora wa Bidhaa, Bw. Daniel Ndiyo, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Biashara Bw. George Kasinga na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sayansi Jinai na Huduma za Vinasaba.  Bi. Hadija Mwema, 

  Sehemu ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wa Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Profesa Samwel Manyele (hayupo pichani) leo Jijini Dar es Salaam uliohusu kampuni ya TECHNO NET SCIENTIFIC kukutwa na kemikali bashirifu bila kuwa na usajili wala kibali cha kufanya shughuli za kuuza na kusambaza kemikali.


  0 0
 • 05/19/17--10:46: TAIFA STARS MPYA HII HAPA
 • Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania, Salum Mayanga (pichani) leo Ijumaa  Machi 19, 2017 ametangaza majina ya wachezaji 24 watakaounda kikosi hicho cha Timu ya Taifa Stars ambacho sasa kinachodhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti.


  Katika mkutano na wanahabari uliofanyika Makao Makuu ya TFF, yaliyoko Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam, Mayanga alisema kikosi hicho kinaundwa na makipa Aishi Manula  (Azam FC), Benno Kakolanya  (Yanga SC) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar). 

  Walinzi wa pembeni upande wa kulia aliwataja Shomari Kapombe    (Azam FC) na Hassan Kessy (Yanga SC) wakati upande wa kushoto wapo Mohammed Hussein (Simba) na Haji Mwinyi  (Yanga SC). 
  Mayanga aliwataja walinzi wa kati Erasto Nyoni  (Azam FC), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Aggrey Morris  (Azam FC) ilihali aliwataja viungo wa kuzuia kuwa ni Himid Mao (Azam FC) na Jonas Mkude (Simba SC). 
  Kadhalika wako viungo wa kushambulia Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla  (Simba SC) na Muzamiru Yassin (Simba) wakati viungo wa kulia waliotajwa ni Simon Msuva (Yanga SC) na Shizza Kichuya (Simba SC). 
  Viungo wa kushoto ni Farid Mussa (Teneriffe, Hispania)  wakati washambuliaji ni Mbwana Samatta (KRC Genk- Ubelgiji), Thomas Ulimwengu (AFC Eskilstuna – Sweden), Ibrahim Ajib (Simba SC), Mbaraka Yusufu (Kagera Sugar) na Abdurahman Mussa (Ruvu Shooting).

  Pia Mayanga aliwataja wasaidizi wake kuwa ni Kocha Msaidizi kuwa ni Novatus Fulgence  wakati Kocha wa Makipa, Patrick Mwangata wakati Meneja wa atakuwa Danny Msangi; Mtunza Vifaa, Ally Ruvu wakati Daktari wa timu atakuwa Richard Yomba huku Daktari wa viungo   akiwa ni Gilbert Kigadya. 

  Timu hiyo itaingia kambini Machi 23, 2017 kwenye Hoteli ya Urban Rose, Dar es Salaam mpaka tarehe 29 baada ya hapo itasafiri kwenda Misri kwa kambi ya wiki moja kabla ya kurejea kuja kucheza mchezo wa kufuzu Mataifa huru ya Afrika mchezo  na Lesotho, mchezo utachezwa Tarehe 10  mwezi wa 6 mwaka huu jijini Dar es Salaam.


  0 0


  Kampuni ya bia ya Serengeti Brewaries Ltd (SBL), imezindua bia mpya aina ya Lite, ikiwa ni muendelezo wa bia mama ya Serengeti Premium Lager.
   
  Akizungumza na waandishi wa Habari, wakati wa uzinduzi wa bia hiyo, mkurugenzi wa fedha na bodi ya SBL, Kalpesh Mehta, amesema bia hiyo itakayokwenda kwa jina la Serengeti Premium Lite inazalishwa kwa kutumia utaalamu wa kisasa.

  Aidha bia hiyo ina ladha kamili ambayo burudani yake ni zaidi ya bia zote za aina ya Lite ambazo kwa sasa zipo sokoni.Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, bia hiyo inauzwa sh.1500 kwa chupa na kwamba inatarajiwa kuteka soko na jumuiya ya wanywaji wake ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakitafuta bia halisi ya kitanzania.

  Ameongeza kuwa, Bia hiyo mpya haina sukari kwa hiyo itakuwa ni chaguo zuri kwa wale wote wasiotumia sukari."Huu ni mwitikio wa wateja wetu ambao wamekuwa wakiitafuta bia ya aina hii kwa muda mrefu"

  "Tunaamini kuwa bia hii Ya Serengeti Premium Lite, ambayo imebuniwa na kutengenezwa na wazalishaji bia (bremaster), wa kitanzania kwa watanzania, itawaleta wateja wetu pamoja zaidi kadri watakapokuwa wakifurahia urithi wetu wa amina hii ya bia", amesema Mehta.

  Ameongeza kuwa, bia hiyo ya Premium Lite ina ubora wa kimataifa sawa na bia mam ya Serengeti Premium Lager ambayo nimepokea zaidi ya medalist 10 za ubora wa kitaifa na kimataifa.

   Mkurugenzi wa Fedha na Bodi ya SBL ,Kalpesh Mehta akizungumza na waandishi wa Habari juu ya uzinduzi wa bia mpya ya Serengeti ya sh.1500 katika ukumbi wa Serena Leo jijini Dar es salaam,kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko, Ceaser Mloka kulia ni Anitha Lwehumbiza
  Mkurugenzi wa Masoko, Ceaser Mloka akizungumza na waandishi wa Habari juu ubora wa bia iliyozinduliwa ya Serengeti ya sh.1500 Leo jijini Dar es Salaam.

  0 0


  0 0

  Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi Awadhi Haji ameendelea kutembeklea vituo mbalimbali vya Bajaji na Bodaboda jijijni katika juhudi za Jeshi la Polisi kupunguza kama si kuondoa kabisa ajali za barabarani. ACP Awadhi leo ametembelea kituo cha Africa sana eneo la Sinza na kutoa elimu ya usalama barabarani kwa madereva wa vyombo hivyo vy abiria, akiwataka kuzingatia na kufuata sheria za usalama barabarani pamoja kuhakikisha wanatengeneza pikipiki zao ili ziwe katika ubora wa kubeba abiria. Madereva hao wamefurahia hatua ya kamanda huyo kupita kila pembe ya jiji kutoa elimu, wakisema hatua hiyo ni ya kutia moyo kwani inaimarisha uhusiano mwema kati yao na wana usalama barabarani.
   Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi Awadhi Haji akielezea umuhimu wa kuwa na Bajaji na Bodaboda zisizo na hitilafu ili kuhakikisha usalama wa abiria
   Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi Awadhi Haji akisisitiza umuhimu wa kuvaa helmet kwa dereva pamoja na abiria
  Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi Awadhi Haji akikagua uimara wa Bodaboda

  0 0

    Na MatukiodaimaBlog 
  WACHIMBAJI wawili  wadogo wa madini ya dhahabu katika kijiji cha Masuluti kata ya Magulilwa tarafa ya Mlowa wilaya ya Iringa mkoani Iringa wamefariki dunia baada ya kukosa hewa wakiwa kazini ndani ya mgodi.
  Afisa mtendaji wa kijiji cha Masuluti Venjaslaus Kiunosile amesema kuwa tukio hilo  limetokea leo Majira ya saa  5 asubuhi, na kwamba taarifa ya tukio hilo alipewa na mchimbaji mwenzao aliyewatembelea marehemu hao kwa ajili ya kuwasalimia. 
  Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Julius Mjengi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa miili ya marehemu hao imetolewa katika mgodi huo. Aliwataja waliofariki dunia kwa kukosa hewa kuwa ni Haus Kaijage (32) mkazi wa Bukoba na James Mlawa(22) mkazi wa Magulilwa.
  Alisema chanzo cha watu hao kupoteza maisha ni kukosa hewa baada ya kuingiza jenereta la kuvuta maji mgodini kwa lengo la kuvuta maji, na baada ya kuliwasha walikosa hewa.
  Alisema alisema wachimbaji hao walichukua mashine hiyo na kuiingiza ndani na mgodi baada ya awali kuharibika na kuwa jeshi la polisi linamshikilia kwa mahojiano mmiliki wa mgodi huo Samweli Msigwa.
  Kamanda Mjengi alitoa wito kwa wachimbaji wadogo katika mkoa wa Iringa kuzingatia usalama katika uchimbaji wa madini.
  Kwa upande wake Mganga mfawidhi wa kituo cha afya Mgama Dkt Baraka Mwifune alisema uchunguzi alioufanya unaonyesha  watu hao walipoteza maisha kwa kukosa hewa.
  Mmiliki wa mgodi huo Samweli Msigwa alisema kuwa akiwa njiani kuelekea eneo la mgodi kwa ajili ya kusaidia kutengeneza mashine ya kuingiza hewa katika mgodi huo ndipo alipopata taarifa ya wachimbaji hao wawili kati ya Sita kupoteza maisha kwa kukosa hewa. 
  Alisema mgodi huo ulikuwa na wachimbaji sita kabla ya wanne kwenda mgodi mpya wa Ismani na hivyo walibaki hao wawili na kuwa anamiliki mgodi huo kihalali na ana kibali kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.
   Kamanda  wa  polisi  mkoa  wa Iringa  Julius Mjengi kushoto akitazama shimo la mgodi  katika  kijiji  cha Msuluti  kata ya Magulilwa wilaya ya Iringa ambalo wachimbaji  wawili  wadogo wawili  walipoteza maisha kwa  kukosa  hewa wakati  wakichimba madini jana asubuhi
   Mmiliki wa mgodi huo Samweli Msigwa (kulia) akihojiwa na polisi. Katikati ni kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Julius Mjengi 
   Kamanda  wa  polisi  mkoa  wa Iringa  Julius Mjengi kushoto akikagua mazingira wa  mgodi huo  katika  kijiji  cha Msuluti  kata ya Magulilwa wilaya ya Iringa ambalo wachimbaji  wawili  wadogo wawili  walipoteza maisha kwa  kukosa  hewa wakati  wakichimba madini jana asubuhi
  Wananchi wa Msuluti kata ya Magulilwa   wilaya ya  Iringa  wakiwa wamebeba mmoja kati ya  miili ya  wachimbaji  wadogo  wawili  waliokufa mgodini kwa  kukosa hewa  leo.

older | 1 | .... | 1696 | 1697 | (Page 1698) | 1699 | 1700 | .... | 3284 | newer