Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109606 articles
Browse latest View live

SERIKALI YATOLEA UFAFANUZI KAZI YA OFISI YA MDHIBITI NA MKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI

0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM-Dodoma

Serikali imeeleza kuwa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haijawahi kumuhusisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika ukaguzi wa Balozi au ukaguzi wowote ule kama Umoja wa Mataifa kwa sababu hakuna ulazima wa kufanya hivyo Kikatiba na Kisheria.

Hayo yameelezwa Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango (MB), Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Kiwengwa Khamisi Mtwana Ally (CCM), aliyetaka kujua ni mara ngapi Ofisi hiyo ya Bara imeishirikisha Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Zanzibar.

Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alisema kuwa, Ofisi hizo kila moja ina mipaka yake ya kufanya ukaguzi na kwamba jukumu la ukaguzi wa Taasisi za Muungano lipo kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali imeanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na kwamba majukumu ya Ofisi hiyo yameainishwa katika ibara ya 143(2) ya katiba hiyo”. Alisema Dkt. Kijaji 
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango (MB), Dkt. Ashatu Kijaji.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MASHIRIKA YA KIMATIAFA YAOMBWA KUISAIDIA TANZANIA KUWAUNGANISHA RAIA WAPYA NA WATANZANIA WENGINE

0
0
Na Tiganya Vincent-Kaliua
18.5.2017

Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiako wa Kimataifa, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashiriki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Celestine Mushi ametoa wito kwa 
Mashirika Kimataifa na Umoja wa Ulaya kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuwasaidia atanzania wapya (waliokuwa wakimbizi wa Burundi) kuhakikishwa anaunganishwa na jamii ya Watanzania mara baada ya kupata uraia.

Balozi Mushi ametoa kauli hiyo jana katika eneo la Ulyankulu wilayani Kaliua wakati alipokuwa na Ujumbe wa Mabalozi kutoka Nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya ikiwemo Uingereza.

Alisema kuwa baada ya Serikali kuwapatia waliokuwa baadhi ya wakimbizi wa Burundi Uraia ni vema nchi hizo na Mashirika ya Kimataifa yakasaidia kuongeza raslimali mbalimbali ambazo zitaisaidia Serikali iweze kuwaunganisha vizuri raia hao wapya na raia wengine hapa nchini.

Balozi Mushi aliongeza fedha za Serikali pekee hazitoshi kukamilisha zoezi la kuwaunganisha raia hao kwasababu yapo mahitaji ya wananchi mengine hapo nchini yanayotegemeza hizo fedha kidogo inazokusanya kutokana na vyanzo vyake mbalimbali vya mapato na hivyo ni vema nao wakasaidia kwa upande wao.

Alisema kuwa kimsingi raia hao wapya wanakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo ukosefu wa maji safi na salama, uhaba wa vifaa tiba, zahanati , kutokuwa na miundombinu ya kutosha ya elimu na kukosa elimu ya kutosha kuhusu uzazi wa mpango.

Alisema kuwa kukosekana kwa elimu ya kutosha kumewafanya wakazi hao wawe na familia kubwa ambazo hawawezi wakati mwingine kuziwezesha katika huduma za jamii.

NBC YATOA GAWIWO LA BIL 1. 7 SERIKALINI

Mkutano wa 34 wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki wamalizika emma.masaka@gmail.com

0
0

Mkutano wa 34 wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam umefikia tamati. Mkutano huu uliofanyika katika Hoteli ya Serena umehudhuriwa na Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka nchi wanachama, watendaji mbalimbali kutoka Wizara, mashirika ya umma, Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, na taasisi mbalimbali za Serikali ndani ya Jumuiya. 

Pamoja na mambo mengine Mkutano huu ulikuwa ni maalum kwa ajili ya kuandaa agenda zinazo hitaji maamuzi ya Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Agenda hizo zinatokana na taarifa ya utekelezaji wa maagizo na maelekezo mbalimbali ya Mkutano uliopita wa Wakuu wa nchi wa Jumuiya wa mwaka 2015/2016, iliyo andaliwa na Mkutano wa ngazi ya wataalamu. 

Baadhi ya mambo yaliyopo kwenye taarifa hiyo ya utekelezaji wa maagizo na maelekezo mbalimbali ya Mkutano uliopita wa Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka 2015/2016 ambayo imekabidhiwa kwa Baraza la Mawaziri yanajumuisha mambo yafuatayo; 

Waheshimiwa Mawaziri wa Tanzania waliohudhuria Mkutano wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Afrika Mashariki unapigwa kabla ya kuanza kwa Mkutano 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wamasuala ya Afrika Mashariki wa Uganda Mhe.Dkt.A.M Kirunda Kivejinja kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Baraza la Mawaziri uliofanyika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam. 

SERIKALI YATOA WITO KWA WALIMU WA MICHEZO MIPYA KUJITOKEZA

MRADI WA REA KUFIKA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI

Wizara ya Mambo ya Nje yatoa elimu ya Mtangamano Pemba

0
0

Serikali ya Zanzibar imeahidi kuwa itaendelea na jitihada za kuimarisha huduma za kiuchumi kwa madhumuni ya kuweka mazingira mazuri ya kibiashara ili wananchi waweze kunufaika na fursa zinazopatikana kwenye Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Issa Gavu alipokuwa anafunga semina ya siku nne kuhusu mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na fursa zake iliyofanyika Pemba kuanzia tarehe 15 hadi 18 Mei 2017.

Mhe. Gavu alitoa wito kwa wanasemina hao ambao wengi wao walikuwa ni wajasiriamali kutengeneza bidhaa zenye ubora kwa kuzingatia mabadiliko ya teknolojia ya ulimwengu wa sasa ili ziwe na uwezo wa kushindana na bidhaa nyingine katika soko la EAC.

Aidha, Mhe. Gavu aliahidi kuwa Serikali itasaidia wajasiriamali washiriki makongamano, semina, maonesho na warsha mbalimbaili zinazofanyika nchini na nje ya nchi ili iwe fursa kwao kujifunza mambo mapya yanayoendana na ulimwengu wa sasa kwa lengo la kuboresha biashara zao.

Mhe. Gavu aliwasihi wote waliopata na watakaopata fursa za mafunzo kuwa mabalozi wazuri kwa wenzao ili kwa pamoja watumie mbinu, ujuzi na uzoefu wanaoupata kukabili changamoto za ushindani wa soko kulingana na mahitaji ya sasa.

Alisisitiza umuhimu wa nchi zote wanachama wa EAC kuwahudumia raia wa nchi zote kwa usawa bila ubaguzi. Alisema endapo nchi moja ikiwa na tabia ya kunyanyasa raia wa nchi nyingine inaweza kusababisha dhana ya kulipiza kisasi hatimaye vurugu na kuleta mkanganyiko katika Jumuiya. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Issa Gavu akisoma hotuba ya kufunga semina kuhusu elimu ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na fursa zake. Semina hiyo iliandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ilifanyika Pemba kuanzia tarehe 15 - 18 Mei 2017. Wengine katika picha, kushoto ni katibu wa Wizara hiyo, Bw. Salum Salum na Mkurugenzi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Eliabi Chodota. 
Kulia ni Mbunge wa Wete, Mhe. Ali Mbarouk akifuatilia kwa makini semina ya mtangamano. 
Washiriki wa semina hiyo ambao wengi wao walikuwa wajasiriamali wakisikiliza hotuba ya kufunga semina. 
Washiriki wengine wakifuatilia hotuba ya Mhe. waziri wa Nchi. 
Mhe. Waziri wa Nchi akiendelea kuwahutubia wana semina na watu wengine waliohudhuria sherehe za ufungaji. 

ZANTEL YAZINDUA VIFURUSHI VYA BURE KWA MITANDAO YOTE YA KIJAMII ILI KUWANUFAISHA VIJANA

0
0

Kampuni ya simu inayoongoza kwa huduma za vifurushi vya intaneti, Zantel imeanzisha huduma mpya ya vifurushi vya bure kwa wateja wake ikiwalenga zaidi vijana, ambapo tafiti zinaonyesha ndio watumiaji wakubwa wa mitandao ya kijamii.

Akizindua rasmi huduma hiyo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Bw. Benoit Janin amesema wateja wa Zantel wanaojiunga na vifurushi vyetu vya kila siku, wiki na mwezi watapata nafasi ya kutumia mitandao ya Facebook, Twitter pamoja na huduma ya kusikiliza muziki bure kwenye application ya ‘Mdundo.com’.

Aliongeza kwa kusema “Tunajisikia fahari kubwa sana kuweza kuzindua huduma hii mpya ikiwa ni mwendelezo wa jitihada zetu za kupanua na kutoa huduma za kibunifu na kuhakikisha wateja wetu wanaendelea kufurahia mtandao wetu wa Zantel wenye huduma ya intaneti ya kasi zaidi ya 4G Tanzania nzima.

Akifafanua zaidi kuhusu huduma hiyo, Mkuu wa kitengo cha huduma ya Vifaa na intaneti Zantel, Hamza Zuberi alisema, “Kwa wateja wa Zantel watakaonunua vifurushi vya siku, wiki na mwezi ambavyo ni ;-Sh.500/= kwa 500MB, Sh.1000/= kwa 1.2GB, na Tsh.1500/= kwa 2.5G watapata nafasi ya kufurahia huduma hizo za bure. Huduma hizi ni kwa wateja wenye simu au vifaa vyenye uwezo wa kupokea huduma ya intaneti. Kwa wateja wetu wanaotumia simu au vifaa visivyo na uwezo huo wanaweza kujipatia simu au vifaa hivyo kwa gharama nafuu kabisa katika maduka ya Zantel jijini Dar es Salaam na visiwani Zanzibar ili na wao waweze kufurahia ofa hii”.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Benoit Janin akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa vifurushi vya bure kwa mitandao yote ya kijamii uliofanywa na kampuni hiyo jana jijini Dar es salaam kwa lengo la kuwanufaisha hasa vijana ambapo pia wateja wa Zantel watapata huduma ya kusikiliza muziki kwenye Application ya Mdundo.com bure. Kulia ni Meneja Chapa na Mawasiliano wa Zantel Rukia Mtingwa. 
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Benoit Janin akigawa Modem kwa wanafunzi wa Chuo cha usimamizi wa fedha cha IFM katika hafla ya uzinduzi wa vifurushi vya bure kwa mitandao yote ya kijamii uliofanywa na kampuni hiyo jana jijini Dar es salaam kwa lengo la kuwanufaisha hasa vijana, ambapo pia wateja wa Zantel watapata huduma ya kusikiliza muziki kwenye Application ya Mdundo.com bure. Anayeshuhudia katikati ni Meneja wa Data na Vifaa vya intaneti Zantel, Hamza Zuheri. 
Meneja wa Data na Vifaa vya intaneti Zantel, Hamza Zuheri (kulia) na Meneja wa Muziki na uendeshaji Mdundo.com, Prisna Nicholaus wakimuonyesha Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Benoit Janin (wa pili kulia) Application ya Mdundo.com ambayo wateja wa Zantel wataipata bure baada ya kujiunga na huduma mpya ya vifurushi vya bure kwenye mitandao yote ya kijamii iliyozinduliwa na Kampuni ya Zantel jana jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia kushoto ni Meneja Chapa na Mawasiliano wa Zantel Rukia Mtingwa. 



NAIBU KATIBU MKUU CCM BARA MPOGOLO AWAFUNDA VIONGOZI, WANACHAMA JIMBO LA SEGEREA NA UKONGA

0
0

Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar

UBABE na unafiki wa baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) inaelezwa kuwa ndio chanzo cha kupoteza jimbo la Ukonga na mengine ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rodrick Mpogolo, alisema hayo jana wakati alipozungumza na wanachama na viongozi wa Chama katika majimbo ya Ukonga na Segerea.

Alisema viongozi hao waliendekeza mizengwe na umimi, ambapo matokeo yake waliwavuruga wanachama na jimbo likachukuliwa na upinzani,sasa wanajuta.

"Tumewasababishia wanachama kubaki kama wakiwa, hawana mbunge,na sehemu zingine hawana madiwani. Yote ni kutokana na ubinafsi na makundi yaliyokiumiza Chama,"alisema.

Mpogolo alisema CCM haiwezi kukubali viongozi wachache wenye roho za chuki waendelee kuwanyanyasa wanachama wenzao kwa sababu ya maslahi ya makundi yao."Naomba kila mwanachana afanye mabadiliko ndani ya nafsi yake. 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza na Wanachama, Viongozi wa CCM Kata ya Tabata, Jimbo la Segerea, wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, jana. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO).
Wanachana wa CCM Jimbo la Segerea wakiinua mikono kufurahia hotuba ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo,jana.
Wanachama wa CCM Jimbo la Ukonga wamsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Rodrick Mpogolo,wakati akiwahutubia kwenye Ukumbi wa Check Point jana.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TANZANIA NA KOMORO ZAAHIDI KUENDELEA KUIMARISHA USHIRIKIANO.

0
0
Balozi wa Tanzania katika Muungano wa Visiwa vya Komoro, Mhe. Sylvester M. Mabumba mapema wiki hii alikabidhi hati za utambulisho kwa Rais wa Muungano wa Visiwa vya Komoro Mhe. Azali Assoumani. Hafla ya kukabidhi hati hizo ilifanyika kwenye Ukumbi wa Ikulu ya Komoro ijulikanayo kama Beit.

Wakati akihutubia, Mhe. Mabumba alijitambulisha kwa Mhe. Rais na kueleza furaha yake ya kuteuliwa kuwa Balozi wa pili kutoka Tanzania kuja kutumikia nchini Komoro. Aidha, alieleza furaha yake kwa mapokezi mazuri aliyoyapata tangu kuwasili kwake Visiwani humo na kwamba yamemfanya ajisikie yupo nyumbani. 


Alieleza kuwa anatambua kazi kubwa iliyopo mbele yake na kuahidi kuwa katika kipindi chake wakati akiwa Balozi nchini humo atajitahidi kukuza mahusiano yaliyopo baina ya Tanzania na Komoro. Sambamba na hilo, Mhe. Balozi alieleza dhamira yake ya kutaka kuona mahusiano baina ya nchi hizi mbili yanakuwa na manufaa kwa pande zote halikadhalika kukua kwa uhusiano wa kindugu kwani mahusiano baina ya Tanzania na Komoro ni ya kihistoria.

Pia Mhe. Rais Assoumani katika hotuba yake naye alianza kwa kuonyesha furaha yake ya kuwasili kwa Balozi pamoja na kukiri kupokea barua ya kurejea Balozi aliyepita na ya kuwasili kwa Balozi wa sasa. Vilevile alieleza kuwa kila Mkomoro hujisikia nyumbani pindi anapo tembelea Tanzania kutokana na ukarimu wanao onyeshwa wanapokuwa huko. 

Aidha Mhe. Rais alimuhakikishia Mhe. Balozi kuwa atarajie kupata ushirikiano wake pamoja na wa Serikali yake katika kipindi chote atakapo kuwa nchini humo.
Mhe. Balozi Mabumba alitumia fursa hiyo pia kumuomba Mhe. Rais Assoumani kufanye ziara ya kikazi nchini Tanzania ili kuweza kudumisha mahusiano yaliyopo baina ya nchi hizo mbili.



Balozi wa Tanzania katika Muungano wa Visiwa vya Komoro Mhe. Sylvester M. Mabumba (kulia) akiwasili katika Ikulu ya Komoro kwaajili ya hafla ya kuwasilisha Hati za Utambulisho, kushoto ni Mnikulu wa Ikulu ya Komoro Bw.Hashim Mohamed. Hafla ya kukabidhi Hati hizo ilifanyika mapema wiki hii katika Ikulu hiyo.

Mhe. Balozi Mabumba akijitambulisha sambamba na kutoa salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya kukabidhi Hati za Utambulisho. 

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YAKUTANA NA WATAALAM WA MFUMO WA TAARIFA ZA KIJIOGRAFIA (GIS) UTAKAOTUMIKA KUPUNGUZA GHARAMA ZA UKUSANYAJI TAKWIMU MBALIMBALI NCHINI

0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa kikao cha pamoja baina ya wataalam kutoka Kampuni ya esri- inayojishughulisha na kutoa huduma za Mfumo wa Taarifa za Kijiografia (GIS), walipokutana leo Jijini Dar es Salaam ili kujadili namna mfumo huo unavyoweza kutumika wakati wa zoezi la ukusanyaji wa takwimu mbalimbali nchini. Kulia ni Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Shirila la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA Tanzania) Dkt. Hashina Begum.
Mtalaam kutoka kampuni ya esri – inayojishughulisha na kutoa huduma za Mfumo wa Taarifa za Kijiografia (GIS), Bi. Linda Peters akielezea jambo wakati wa kikao baina ya wataalam kutoka Kampuni hiyo na Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni wataalam kutoka Kampuni hiyo Bw. Patrick Kipchumba na Mhandisi Anthony Gakobo.
Baadhi ya wataalam kutoka Kampuni ya esri – inayojishughulisha na kutoa huduma za Mfumo wa Taarifa za Kijiografia (GIS), wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) walipokutana leo Jijini Dar es Salaam ili kujadili namna mfumo huo unavyoweza kutumika wakati wa zoezi la ukusanyaji wa takwimu mbalimbali nchini.
Mtalaam wa Mfumo wa Taarifa za Kijiografia (GIS) Anthony Gakobo akionyesha moja ya kifaa kinachotumika katika kuhakiki uhalisia wa taarifa za kijiografia mbele ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni watalaam wa mfumo huo Bw. Patrick Kipchumba na Bi. Linda Peters.
Mshauri wa Masuala ya Kitakwimu kutoka Benki ya Dunia – Tanzania, Bi. Elizabeth Talbert akifafanua jambo wakati wa kikao cha pamoja baina ya wataalam kutoka Kampuni ya esri- inayojishughulisha na kutoa huduma za Mfumo wa Taarifa za Kijiografia (GIS) na menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ili kujadili namna mfumo huo unavyoweza kutumika wakati wa zoezi la ukusanyaji wa takwimu mbalimbali nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi kutoka UNFPA, Benki ya Dunia – Tanzani , watalaam kutoka Kampuni ya esri inayojishugulisha na kutoa huduma za Mfumo ya Taarifa za Kijiografia (GIS) pamoja na Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mara baada ya kumaliza kikao kujadili namna mfumo wa GIS unavyoweza kutumika wakati wa zoezi la ukusanyaji wa takwimu mbalimbali nchini.

(Picha zote na Frank Shija – MAELEZO) 

Wakurugenzi waahidi kutekeleza kampeni ya maji 'Nipo Tayari'

0
0





Mratibu wa kampeni ya mazingira ijulikanayo kama Nipo Tayari Juliana Kitila akimuonyesha kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Ulanga mkoani Morogoro Peter Nkaya ( wakanaza upande wa kushoto) hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mambo sita ya ya usafi wa mazingira kwenye halmashauri yake ikiwa ni kampeni ya kuendeleza muitikio wa usafi mkoani Morogoro.
Kaimu Mkurugenzi halmashauri ya Ulanga mkoani Morogoro ‘akiapa’ kuwa yuko tayari kuungana na serikali katika kutekeleza swala la usafi sambamba na halmashauri yake.
Mratibu wa kampeni ya ya mazingira ijulikanayo kama Nipo Tayari Juliana Kitila akitoa maelezo kwa mkurugenzi wa halmashauri ya Kisarawe Mussa Gama juu ya kampeni ya hiyo mjini Morogoro jana.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Kisarawe Mussa Gama akishilia bango la Nipo Tayari kama ishara ya kuwa yuko tayari kushiriki kikamilifu katika kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira ijulikanayo kama Nipo Tayari wakati wa semina mjini Morogoro jana.

Kapondo: Mshiko wa Biko umekuja wakati nina uhitaji mkubwa wa pesa

0
0
MSHINDI wa Droo ya Bahati Nasibu ya Biko Ijue Nguvu ya Buku iliyochezeshwa juzi Jumatano, Stanley Kapondo, amekabidhiwa fedha zake jumla ya Sh Milioni 10, huku akisema kuwa pesa hizo zimekuja wakati muafaka ili kuondoa changamoto zinazomkabili katika maisha yake.

akabidhiano hayo yamefanyika jana katika benki ya NMB jijini Dar es Salaam kwa kusimamiwa na Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, ikiwa ni siku moja baada ya kumpata mshindi wao wa droo ya Jumatano.
Mfanyakazi wa Shirika na Umeme TANESCO Stanley Kapondo, katikati akipokea fedha zake jumla ya Sh Milioni 10 alizoshinda katika bahati nasibu ya Biko katika droo ya Jumatano. Kulia ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven na kushoto ni afisa wa NMB aliyesimamia uingizaji wa fedha hizo katika akaunti ya Kapondo.
Mfanyakazi wa Shirika na Umeme TANESCO Stanley Kapondo kushoto akifurahia fedha zake za ushindi wa droo ya Biko alizoshinda katika droo ya Jumatano. Kulia ni Meneja Masoko wa Biko Goodhope Heaven.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Kapondo alisema alikuwa na uhitaji mkubwa wa pesa, hivyo aliamua kucheza Biko kama sehemu ya kutafuta suluhu ya matatizo yake.

Alisema pamoja na kuamua kucheza Biko, hakuamini kwamba angeshinda Sh Milioni 10, badala yake alikuwa anawazia ushindi wa Sh Milioni moja aliyoona ni rahisi.

“Niliamua kuchezaa biko kwa kufanya miamala kwenye simu yangu kwa kuweka namba ya kampuni ambayo ni 505050 na kwenye namba ya kumbukumbu niliweka 2456 kama wanavyohitaji ambapo kucheza mara nyingi zaidi ndio sababu ya kutangazwa mshindi.

Pesa nilizopokea kutoka Biko si za kwanza maana nimekuwa nikishinda zawadi za papo kwa hapo hadi Sh 50,000, hivyo binafsi nikajikuta nawaamini zaidi Biko ukizingatia kuwa licha ya kuwahi kucheza bahati nasibu nyingi, lakini kwa umri wangu wa miaka 52 sijawahi kubahatika,” Alisema Kapondo ambaye pia ni mtumishi wa Shirika na Umeme Tanzania TANESCO, Ubungo.

Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, aliwataka Watanzania kucheza kwa wingi huku akisema zawadi za Sh Milioni 10 zitawaniwa katika droo ya Jumatano na Jumapili huku zile za papo kwa hapo zikiendelea kulipwa kwa kupitia simu za wachezaji wao.

“Biko imezidi kukolea, hivyo ni wakati wa kucheza mara nyingi ili mjiwekee mazingira mazuri ya ushindi maana zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja zinatolewa kila siku saa na kila siku, hivyo unachotakiwa ni kufanya miamala kwnye simu zenu za Tigo, Vodacom na Airtel, huku tiketi ikipatikana kwa Sh 1000 au zaidi,” Alisema Heaven.

Kwa mujibu wa Heaven, tiketi moja ya Sh 1000 itakuwa na nafasi mbili ikiwa ni ushindi wa papo kwa hapo pamoja na nafasi ya kuingia kwenye droo kubwa ya kuwania Sh Milioni 10, watu wakishauriwa kucheza mara nyingi zaidi ili wajiwekee mazingira mazuri ya ushindi wa Biko.

WASANII NYOTA SABA KUTOKA CHINA NA WAPIGA PICHA 100 WATAMBELEA TRENI YA TAZARA LEO

0
0
--
 Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii nchini Jaji Thomas Mihayo akizungumza katika mkutano mfupi uliofanyika katika Stesheni ya Tazara jijini Dar es Salaam,kuhusu ujio wa Wasanii nyota saba kutoka nchini China na wapiga picha 100,ambao pia walitembelea Treni ya TAZARA na kujionea mambo mbalimbali yaliyokuwa yakinyika hapo.
 Baadhi ya Wasanii hao Nyota wakiwasili katika  Stesheni ya TAZARA Jijini Dar es Salaam
 aziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe Rashid Ali Juma akizungumza  wakati wa kuwakaribisha wasanii hao nyota kutoka nchini China
 Muongoazaji wa filamu ya siri za familia akitoa Salamu za Wasanii hapa nchini
 Wasanii hao Nyota wakiwa wameketi kwa pamoja  wakati wa mkutano
 Wasanii hao  ikawakiwa katika kurekodi sehemu ya vipindi vitakavyorushwa katika cheneli za nchini China

Serikali yaipongeza Timu ya Taifa ya Vijana “Serengeti Boys” walimu na viongozi wao kwa ushindi wa magoli 2 –1 dhidi ya Angola


MAGAZETI YA LEO IJUMAA MAY 19,2017

TAMASHA LA MUZIKI WA INJILI LA KIMATAIFA KUFANYIKA JUMAPILI UPANGA JIJINI DAR

0
0

Tamasha la muziki wa injili lenye ubora wa kimataifa linatarajia kufanyika Jumapili,Mei 21 katika ukumbi wa Kanisa la City Christian Center (CCC Upanga mkabala na Mzumbe University

Tamasha hili linalojulikana Ni Salama moyoni, ambapo mwanamuziki Mchungaji PAUL SAFARI ndiye atakayekuwa muhusika mkuu ambapo atarekodi nyimbo zake kwa njia ya moja kwa moja (yaani live).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini DSM, Mchungaji SAFARI amesema tamasha hilo limeandiliwa kwa katika viwango vya ubora wa hali ya juu ili kuendana na viwango vya Kimataifa.

“Ki ukweli tumejiandaa vizuri katika maombi, mazoezi na maandalizi yote ya tamasha. Hili siyo tukio la kukosa maana kila mmoja atae hudhuria ataondoka na furaha na baraka za Mungu”. amesema mchungaji Safari.

Wanamuziki mbali mbali kama a John Lisu, Moses Zamangwa na Movement for Christ nao watatumbuiza katika tamasha hilo linalotarajiwa kuvuta watu wengi.

Mchungaji Safari Paul ni mmoja wa wachungaji katika kanisa la DPC na pia mwimbaji mkongwe wa nyimbo za injili. Amekuwa sehemu ya watu waliokuza muziki wa injili Tanzania na amelea na kukuza waimbaji wengi, na ameshiriki kurekodi nyimbo akishirikiana na vikundi mbali mbali ndani na nje ya nchi.

Albamu yake ya kwanza inayoitwa Furaha ya Bwana mwaka 2006. Na sasa baada ya miaka kumi na moja, Pastor Safari ameandaa Ni Salama Mubashara au Live DVD recording ya Ni Salama.

Tamasha hili la aina yake, limeandaliwa kwa ubora wa hali ya juu ili kuendana na viwango vya Kimataifa. “Ki ukweli tumejiandaa vizuri katika maombi, mazoezi na maandalizi yote ya tamasha. Hili siyo tukio la kukosa maana kila mmoja atae hudhuria ataondoka na furaha na baraka za Mungu”. asema Pastor Safari. Tamasha hili la Ni Salama yaani Ni Salama Live DVD recording, litafanyika tarehe 21/05/2017 katika Kanisa la City Christian Center (CCC Upanga mkabala na Mzumbe University). Pia Pastor Safari atasindikizwa na John Lisu, Moses Zamangwa na Movement for Christ.

Lengo ni kupeleka ujumbe wa neno la Mungu duniani kote kwa njia ya muziki na uimbaji na kuleta madariko katika maisha ya watu. “Watanzania tunasifika sana kwa uimbaji na tumejaliwa na Mungu katika eneo hili, lakini miziki yetu haifiki mbali kwa sababu tunakosa ufanisi na ubora katika kazi zetu. Naami Tamasha la Ni Salama litakuwa ni chachu kwa wanamuziki na waimbaji wote. Narudia tamasha hili litaweka historia. Hivyo usikose” asema Pastor Safari Paul.

KUMEKUCHA SHINDANO LA MR & MISS TEKU-MBEYA 2017

STAR TIMES YAINGIA UBIA NA TPB KUUZA LUNINGA ZA KIDIJITALI KWA MKOPO

0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Kampuni ya startimes imeingia ubia na benki ya TPB kwa lengo la kuwakopesha wateja televisheni za kidigitali kwa awamu kupitia mkopo ambao utamwezesha mteja kulipa mpaka miezi kumi na miwili kutoka benki ya TPB.

akizungumza na Waandishi wa habari jijini dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa mpnago huo Makamu wa Rais wa Star Media Tanzania Zuhra Hanif Fazal, amesema kuwa ubia huo unamwezesha mteja wa startimes kulipia kwa njia rahisi zaidi televisheni ya kidigitali sio tu kwa mara moja bali kwa awamu kupitia Benki ya TPB.

"wateja wataweza kuipata huduma hii katika mikoa mitano ambayo ni Dar es salaam, Dodoma, Mwanza Arusha na Mbeya ambapo kuna matawi ya Benki hiyo" amesema Zuhra.

Akiongea katika uzinduzi, Meneja Mahusiano wa StarTimes, Antony Katunzi amesema ushirikiano huu unaashiria wazi mapinduzi ambayo Benki na Kampuni ya Televisheni zinaweza kuleta, kwa kurahisisha ulipiaji kwa wateja wao na jamii kwa ujumla ili kuwezesha kila familia kumiliki luninga ya kidigitali ya StarTimes.

Naye Amos Kasanga, Meneja Masoko wa Benki ya TPB amesema benki hiyo imekubaliana na StarTimes kutoa mikopo hiyo midogo kwenye mikoa mitano ambapo huduma hiyo itapatikana. Njia hii ni rahisi zaidi kwa wateja kutumia.

“Najisikia furaha kubwa leo tunapozindua njia nyingine ambayo inazileta pamoja kampuni hizi kubwa mbili Tanzania, na hii itatoa fursa kwa wateja na kila familia ya kitanzania kumiliki luninga ya kidigitali na kufurahia maisha ya kidigitali kwa kupata vipindi mbali mbali kutoka kila kona ya dunia”

Kwa hatua hii, wateja na wasio wateja wa StarTimes, wote wanaweza kulipia luninga za kidigitali za StarTimes kwa awamu kupitia matawi ya Benki ya TPB. 

Watanzania waishio mijini na vijijini sasa wataweza kumiliki luninga za kidigitali kwa urahisi, kulingana na mahitaji na uwezo wao kifedha.

Tunayo matoleo mbalimbali ya luninga za kidigitali kwa ajili ya wateja wetu kulingana na mahitaji na uwezo wao. Tuna luninga ya inchi 24 kwa Tsh. 45,000/=,kwa kila mwezi kwa miezi kumi na miwili (12),inchi 32 Tsh 64,000/= na inchi 40 kwa Tsh. 99,000/= .
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Star Media Tanzania Zuhra Hanif Fazal akikata utepe kwa pamoja na Meneja wa Teknolojia wa Benki ya Posta Tanzania(TPB), James Msuya wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya Mikopo ya Luninga za kisasa kwa kushirikiana na Star Times.
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Star Media Tanzania Zuhra Hanif Fazal wakifungua kitambaa kwa pamoja na Meneja wa Teknolojia wa Benki ya Posta Tanzania(TPB), James Msuya kuashiria uzinduzi wa huduma za mikopo ya Luninga za Star Times Kupitia benki ya Posta.
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Star Media Tanzania Zuhra Hanif Fazal na Meneja wa Teknolojia wa Benki ya Posta Tanzania(TPB), James Msuya wakionyesha moja ya Luninga zitakazokuwa zinakopeshwa kupitia benki ya Posta.
Baadhi ya watumishi wa kampuni ya StarTimes Tanzania ambao wamehudhuria sherehe hiyo.

KUMBUKUMBU YA MIAKA MIWILI LA KIFO CHA MAREHEMU SOLOMON MAPUNDA (BABA SAMANTHA)

Viewing all 109606 articles
Browse latest View live




Latest Images