Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

Halotel yatoa ufafanuzi juu ya kesi iliyokuwa inawakabili

$
0
0
Kampuni ya mawasiliano ya simu ya mkononi Halotel wamekiri makosa yalitokea na wameahidi kufuata sheria za nchi katika utoaji wa Huduma kwa wananchi.

Kampuni hiyo imesema, itahakikisha inashirikiana na serikali katika kuboresha huduma za mawasiliano kwa watanzania wote, vijijini hadi mjini.

Mkurugenzi mtendaji wa Halotel Le Van Dai, amesema hayo leo ofisini kwake wakati akitoa ufafanuzi juu ya kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa inaikabili kampuni hiyo na aliyekuwa mkurugenzi wao Do Manh Hong.

Amesema, katika kesi hiyo kulikuwa na mashtaka saba, lakini wao walihusishwa katika vipengele viwili tu ambavyo ni kushindwa kutoa taarifa za usajiri wa kampuni ya Unex ambayo ilisajili laini 1000 walizouza na kushindwa kutimiza majukumu yao kwa kuiuzia kampuni hiyo laini za simu wakati ikiwa haijasajiliwa na kutokuwa na kibali cha TCRA.Kwa kutumia mwanya huo Unex walisimika mitambo ambayo ilisababisha hasara ya milioni 459 kwa serikali.

Amesema, Halotel pamoja na kwamba walikuwa wakishtakiwa pamoja na raia saba wa Pakistani walilipa faini iliyokuwa ikiwahusu wao na hasara hiyo kwa kuwa hawan uhusiano wowote na hao waliobaki.

"Mitambo iliyotumika kuiba mawasiliano ya simu haikuwa yetu, hatukufahamu kama Wateja wetu Unex, walitumia mitambo hiyo kuiba mawasiliano lakini hatuna uhusiano wowote na washtakiwa wengine ambao tumehusishwa nao na hata mitambo iliyotumika siyo ya kwetu" amesema Leo Van Dai.

Ameongeza kuwa Halotel haihusiki kwa vyovyote vile na mashtaka yanayowakabili raia hao wa Pakistani kama vile kusimika mitambo ya mawasiliano kwani wao wanafanya kazi zao kwa kufuata taratibu na sheria za nchini.

Aidha mkurugenzi huyo ametanabaisha kuwa, Halotel imeazimia kufanikisha jitihada za serikali katika kutoa huduma bora za mawasiliano na kuwa wanatarajia kuunganisha vijiji zaidi ya 1500 katika mwaka huu wa fedha kuongeza ufanisi wa huduma za mawasiliano.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel ,Le Van Dai akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa ufafanuzi wa kesi iliyokuwa inawakabili katika mahakama ya Kisutu iliyofanyika leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Wakili wa Halotel, Fatuma Seif na Kulia ni Wakili Christopher Masai

TADB YABISHA HODI VISIWANI ZANZIBAR

$
0
0



Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) imeanza kuchangamkia fursa za uwekezaji katika sekta ya kilimo na mifugo visiwani Zanzibar kwa kuanza mchakato wa kutoa mikopo kwa wakulima na wakazi wa visiwa hivyo wanaojishughulisha katika uchakataji wa mazao ya kilimo visiwani humo. 

Akizungumza wakati wa walipotembelea Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, visiwani humo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Francis Assenga alisema kuwa TADB ikiwa chombo cha Muungano ina wajibu kusaidia juhudi za Serikali katika kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini Tanzania hasa katika kuchagiza mapinduzi na maendeleo katika Sekta ya Kilimo, ambayo inaajiri zaidi ya asilimia 75 ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi nchini na pia kutoa kiasi cha zaidi ya asilimia 65 cha mali ghafi kwa ajili ya viwanda vya nchi.

“Uanzishwaji wa TADB unatokana na Serikali kutambua umuhimu wa uwekezaji wenye tija kwenye maeneo yote ya sekta ya Kilimo na kuleta mapinduzi ya dhati ya Kilimo ili kuwezesha upatikanaji wa mikopo na mitaji ya riba nafuu ikiwa ni pamoja na kuhamasisha mabenki na taasisi zingine za fedha nchini kutoa mikopo zaidi kwenye sekta ya Kilimo,” amesema.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anaeshughulikia Kilimo na Maliasili Bibi  Maryam Juma Abdullah (aliyesimama) akiwakaribisha ugeni kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB). 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anaeshughulikia Kilimo na Maliasili Bibi  Maryam Juma Abdullah (aliyesimama kulia) akizungumza wakati wa ugeni kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) ulipotembelea Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi. Ugeni huo upo visiwani Zanzibar kuangalia maeneo ya uwekezaji visiwani humo. 

Wanaomsikiliza ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Francis Assenga (kushoto) na wajumbe wa Bodi ya TADB, Bw. Hussein Mbululo (wapili kushoto) na Bibi Rehema Twalib ambaye ni Mkuu wa Msafara huo (wapili kulia). 
Mjumbe wa Bodi ya TADB, Bibi Rehema Twalib ambaye ni Mkuu wa Msafara huo (aliyesimama) akizungumza wakati walipotembelea Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar. 


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Maelfu ya akina mama waendelea kunufaika na huduma ya wazazi nipendeni

$
0
0
Maelfu ya akina mama wanaendelea kunufaika na huduma ya ujumbe mfupi wa maandishi unaotolewa bure na Vodacom Tanzania Foundation wa ‘Wazazi Nipendeni’, unazidi kuendelea kuwanufaisha maelfu ya akina mama wajawazito kupitia dondoo mbali mbali za kiafya.

Akiongea na mtandao huu Faidha Abdallah pichani ambaye ni mkazi wa Buguruni jijini Dar es Salaam anasema amekuwa akitumia huduma hiyo ambayo imekuwa msaada mkubwa kwake.

“Kupitia huduma hii ninaweza kujifunza namna ya uzazi salama kupitia simu yangu ya kiganjani bila malipo yoyote. Nimekuwa nikipokea ujumbe kila wiki na ninaishukuru Vodacom Tanzania Foundation pamoja na wadau wengine waliofanikisha huduma hii nzuri,” anasema.

“Pamoja na kuwa nimezaa na kukuza watoto wawili, sikufahamu kuwa kumbe ni muhimu sana kumnyonyesha mtoto kwa miezi sita bila kumkatisha kabla ya kuanza kumlisha aina nyingine ya chakula,” anaelezea

Naye Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald alisema jijini Dar es Salaam kuwa, zaidi ya wateja milioni moja wamejiunga na huduma hiyo tangu izinduliwe mwaka 2012.

“Wateja waliojiunga na huduma hii wamepokea jumla ya ujumbe mfupi unaofikia milioni 55 wenye maelekezo mbali mbali juu ya afya bila malipo. Ujumbe wanaopokea ni pamoja na kubaini dalili hatari kwa uja uzito mapema, maendeleo ya mtoto, namna ya kuepuka maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, vyakula muhimu kwa mama mja mzito, uhuhimu wa mama kuhudhuria kliniki mapema,” anaeleza

Oswald anasema, kupitia ujumbe mfupi akina mama wajawazito wanaelimishwa namna ya kuishi wakiwa na afya ili waweze kujifungua watoto wenye afya bora pia watu wengine kama vijana, akina mama na wazee wanaweza kujifunza namna ya kujikinga na magonjwa mbali mbali kama Malaria na mengineyo.

Wateja wetu wanaweza kupata huduma hii ya bure kwa kutuma ujumbe kwenye namba 15001 au 15012 na wataweza kupokea ujumbe mfupi kupitia simu zao za viganjani.

Ben Paul Ndani Ya Miss Ustawi Ijumaa

$
0
0
Mwanamuziki nyota wa kizazi kipya nchini, Ben Paul atatumbuiza katika mashindano ya kumsaka mrembo wa Chuo cha Ustawi wa Jamii (Miss Ustawi) yaliyopangwa kufanyika Ijumaa (Mei 19) kwenye ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga jijini.

Mratibu wa mashindano hayo, Catherine Boniface alisema kuwa Paul ambaye anatamba na wimbo wa Moyo Machine, Phone na nyinginezo nyingi, pia atatambulisha wimbo wake mpya aliomshirikisha mwanamuziki nyota nchini, Darasa.

Mashindano hayo yamedhaminiwa na kinywaji cha Windhoek, yatashirikisha jumla ya warembo 12 ambao walikaa kambini kwa muda wa wiki mbili wakijifua chini ya mwalimu wao, Clara Michael na matron, Catherine Boniface.

Warembo ambao wamepitishwa na kamati ya mashindano hayo ni Fatma Kivea, Elice Mwakajila, Melody Thomas, Diana Mwaibula, Hapifania Shedoekulu, Careen Kileo. Wengine ni Angelina Michael, Ruth Deogratius, Consolator Samwel, Loyce Jeck na Elizabeth Julius.

Rais wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Yohana Mabena akizungumza wakati wa  kuwatambulisha warembo wao kwa wadhamini wakuu, kampuni ya Mabibo Beer. Kulia ni msemaji wa kampuni ya Mabibo Beer, Andrea Missama na kushoto kwa Mabena ni Waziri wa Michezo wa Ustawi, Ashura Jingu. Nyuma ni warembo wa miss Ustawi 2017. 
Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ben Paul akizungumza akizungumza wakati wa kutambulishwa kuwa msanii wa kutumbuiza katika mashindano Miss Ustawi 2017 yaliyopangwa kufanyika Ijumaa (Mei 19) kwenye ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga, jijini.

Miss Ustawi anayemaliza muda wake Evelyn Andrew akizungumza wakati wa utambulisho wa warembo hao kwa wadhamini wakuu. Evelyn anavua taji hilo, Ijumaa (Mei 19) wakati wa mashindano ya kumsaka mrembo wa chuo hicho kwenye ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga. 

IKUNGI WAANZISHA MFUKO WA ELIMU ILI KUONDOA CHANGAMOTO KATIKA SEKTA HIYO.

$
0
0


MKUU wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida Miraji Mtaturu amekutana na kamati ya mfuko wa elimu wilaya na kuwaomba kuwa wazalendo katika kutafuta njia za kutatua changamoto za elimu wilayani humo. 

Mfuko huo umeundwa baada ya uanzishwaji wake kuridhiwa na kikao cha baraza la madiwani kilichoketi hivi karibuni. 

Akizungumza katika kikao cha kuwapatia majukumu yao Mtaturu amesema mfuko huo utakuwa na jukumu la kuratibu masuala yote yatakayosaidia kuboresha utoaji wa elimu katika shule za msingi na sekondari. 

“nawapongezeni kwa heshima mliyopewa ya kuteuliwa kuwa wajumbe wa kamati hii,naimani kuwa mtafanya kazi kwa uzalendo mkubwa ili matunda ya uwepo wenu yaonekane kwa kuitoa elimu yetu hapa ilipo na kuipeleka mbali zaidi,”alisema Mtaturu. 

Alisema wakifanikiwa kuondoa changamoto zilizopo watakuwa wameboresha mazingira ya utoaji elimu na kuongeza ufaulu wa watoto jambo ambalo waliazimia walipokutana wadau wa elimu. 
Mkuu wa Wilaya Ikungi Miraji Mtaturu katikati akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya mfuko wa elimu wilaya ns viongozi wa halmashauri baada ya kumaliza kikao nao. 
Mjumbe mwakilishi wa madhehebu ya dini sheikh Salum Ngaa akichangia hoja wakati wa kikao kilichoongozwa na mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu pichani wakiwa na wajumbe wa kamati ya mfuko wa elimu wilaya. 
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi Haika Massawe akichangia hoja wakati wa kikao cha wajumbe wa kamati ya mfuko wa elimu wilaya. 

MABASI YANAYOBEBA WANAFUNZI MKOANI SINGIDA YAKAGULIWA.

$
0
0
Jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani Mkoa wa Singida limeanzisha zoezi kambambe la kukagua mabasi yanayotumika kusafirisha wanafunzi huku likisisitiza kuwa zoezi hilo kuwa endelevu.

Akizungumza kwa niaba ya kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Singida, RTO Mrakibu wa Polisi Peter Raphael Majira, amesema zoezi hilo lililoanza jana litaendelea kwenye wilaya zote za mkoa wa Singida.

Amesema lengo ni kuhakikisha mabasi hayo yanakidhi mahitaji yote ya sheria za usalama barabani, wakati wote yanapokuwa barabarani.

Amesema pia wanatoa elimu na wanawakumbusha madereva na wamiliki wa mabasi hayo, juu ya wajibu wao na umuhimu wa kuzingatia kwa umakini mkubwa sheria za usalama barabarani. 


Aidha RTO Peter amesema wanawakumbusha madereva kujenga utamaduni wa kuwa na tahadhari zaidi na kitendo hicho kitapunguza kwa kiwango kikubwa ajali za barabarani.

Pia ametumia fursa hiyo kuwataka wenye watoto wanaotumia mabasi hayo wahakikishe mtoto anakaa kwenye kiti chake na si kuchangia kiti.

“Mzazi/mlezi usikubali kabisa mwanao achangie kiti, umelipitia kiti kwa nini achangie na wanafunzi mwingine. Na ninyi wamiliki wa mabasi haya kama kuna hafla wanafunzi wanakwenda kuhudhuria iwapo wamejaa (yaani kila mwanafunzi ana kiti chake), peleka hao waliopata viti halafu urudie wengine” amesisitiza mrakibu Peter.

Askari wa usalama barabarani mkoani Singida, E.8763. Sgt. Benes Lucas akikagua mabasi yanayotumika kusafirisha wanafunzi mjini hapa jana. 
Baadhi ya mabasi kati ya 20 yanayotumika kusafirisha wanafunzi Mkoani Singida yakifanyiwa ugazi na askari usalama barabarani kwa lengo la kujiridhisha ubora wake. 
RTO Mkoa wa Singida Mrakibu wa polisi Peter Raphael Majira akitoa taarifa ya zoezi la ukaguzi wa mabasi yanayotumika kusafirisha wanafunzi kwa lengo la kukagua ubora na pia kuwakumbusha madereva na wamiliki wa mabasi hayo juu ya sheria za usalama barabarani. 


WAKUU WA POLISI KUTOKA NCHI ZA SADC KUKUTANA ARUSHA.

$
0
0

Mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la wakuu wa Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO) unatarajia kufanyika Mei 24, 2017 mkoani Arusha chini ya mwenyekiti wa Shirikisho hilo kipindi hiki ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu.

Mkutano huo utatanguliwa na mikutano ya kamati tendaji za SARPCCO kabla ya kufunguliwa rasmi Mei 24, 2017 na Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba ambapo mambo mbalimbali yatajadiliwa ikiwemo jinsi ya kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka kwa kufanya Operesheni za pamoja katika kubaini na kukabiliana na makosa mbalimbali yakiwemo dawa za kulevya, wizi wa magari, usafirishaji haramu wa binadamu na ugaidi.

Vilevile, mkutano huo utajadili utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa na Wakuu wa Upelelezi wa SARPCCO pamoja na kamati tendaji za sheria, Mafunzo na kamati tendaji ya Jinsia na watoto katika mkutano wao uliofanyika mwezi Machi mjini Bagamoyo.

Aidha suala la michezo baina ya Majeshi ya Polisi kwa nchi wanachama nalo linatarajiwa kujadiliwa katika mkutano huo.

SARPCCO iliundwa mwaka 1995 kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa Majeshi ya Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu. Shirikisho hilo linaundwa na Nchi kumi na tano ambazo ni Tanzania, Angola, Botswana, Malawi, Lesoto, Mauritius, DRC, Msumbiji, Namibia, Afrika Kusini, Zambia, Zimbabwe, Swaziland, Madagascar na Syshelis.

Imetolewa na:-
Advera Bulimba-ACP

Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.

MATUKIO KATIKA PICHA: YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 28, MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO MAY 18, 2017.

$
0
0



 Naibu Spika  wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk.Tulia Ackson  akiongoza    kikao cha Ishirini na nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 18, 2017.
8950-Mhagama na Makamba
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akizungumza jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe.January Makamba   katika kikao cha Ishirini na nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 18, 2017.
8987-Mhe.Kijaji
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dk.Ashatu Kijaji akifafanua jambo katika  kikao cha Ishirini na nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 18, 2017.
8994-Mhe.Makamba
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe.January Makamba akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha Ishirini na nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 18, 2017.


TANZIA:DKT SUBILAGA KASISELA KAGANDA AFARIKI DUNIA

$
0
0
 It is with deep sorrow that the family of Dr Honesmo Balilonda Kaganda of The Kairuki Hospital in Dar Es Salaam, announce the death of their beloved wife, mother, sister, friend and colleague, DR SUBILAGA KASISELA KAGANDA. Dr Subi passed away in India while on treatment on the 17th May 2017. Her funeral will be held in Dar-es-Salaam on Saturday, May 20th 2017 at Msasani Lutheran Church at 12 midday followed by her burial at Kinondoni Cemetery. May her Soul Rest In Peace. Hebrews 13:14-16

ROTARY AND CCBRT IN PARTNERSHIP FOR A NEW CLINIC

$
0
0
Rotary Tanzania has today signed a Memorandum of Understanding with Comprehensive Community Based Rehabilitation (CCBRT) where by Rotary is pledging funds to support the construction of CCBRT’s new clinic to provide appointment based, private eye, orthopaedic and ear, nose and throat (ENT), physiotherapy as well as imaging services.

Rotary Dar Marathon in Partnership with Bank M will support CCBRT by contributing funds amounting to USD 1.5M over a period of 2017-2019. The grant is in in support of CCBRT’s social enterprise project, which aims to expand revenues to be able to support subsidised care in the Disability Hospital. Funds will be used to complete construction of the Clinic, which will open in February 2018, and support the equipping and outfitting of the facility.

Speaking on this new initiative of Rotarians providing communities with quality heath care facilities, Rotary Dar Marathon Board Chair Sharmila Bhatt said “We are very pleased to support an institution like CCBRT providing high quality care to patients and especially in the area of disability. Part of this investment will be raised locally through Rotary Dar Marathon in partnership with Bank M while other funds will be obtained through our Rotary Foundation.”

Erwin Telemans, CCBRT’s CEO, commented on the new partnership with enthusiasm. “We’re lucky to have Rotary as a partner in this exciting endeavour,” he said. “We hope more partners will see the opportunity in supporting CCBRT’s growth as a social enterprise.”

Rotary always aspires to serve the community by investing in areas where the most good can be achieved and through this project CCBRT will be able to continue offering affordable disability care to more people who cannot afford to pay for services from profits attained through the new private clinic.

The Rotary Dar Marathon Chairperson 2017 Catherinerose Barretto said “On behalf of the presidents of the seven clubs of Rotary in Dar es Salaam which are the organizers of the Rotary Dar Marathon each year, I would like to take this opportunity to share our excitement on this project and we hope all our other supporters individuals and companies alike will continue to support the marathon so that we can achieve this very ambitious and significant goal.”
CCBRT CEO Mr. Erwin Telemans and Rotary Dar Marathon (RDM) board chair Ms. Sharmila Bhatt signing the Memorandum of Understanding whereby RDM in partnership with Bank M will support the construction of CCBRT new clinic by 1.5mio USD. The signing ceremony took place at the hospital premises in Dsm yesterday. Witnessing (seated) are Rotary Oysterbay club president Mr. Alfred Woiso, University of Dsm Rotary Club incoming president Dr. Eugenia Kafanabo. Others are CCBRT Deputy CEO Ms. Haika Mawalla (standing left) and Rotary Clubs presidents.
CCBRT CEO Mr. Erwin Telemans and Rotary Dar Marathon Board chair Ms. Sharmila Bhatt exchanging documents after signing the agreement whereby Rotary in partnership with Bank M will contribute 1.5mio USD between 2017-2019 to fund the construction of a new clinic at CCBRT. The signing ceremony took place in Dsm yesterday.

Huduma ya Zahati ya mimea yaanza kutolewa BURE na Yara Tanzania

$
0
0
Mkulima Christopher Nduva (kushoto) kwa furaha akipokea maelezo yaliyopo kwenye kipeperushi cha mahindi cha Yara Tanzania kutoka kwa Afisa Ugani (bwana shamba) wa Yara Tanzania, Andrew Mwangomile (pili kulia) baada ya zao lake kugundulika changamoto inayolikabilia. Kulia ni muhusika mkuu wa duka la pembejeo Bw. Antony Kalenga ambapo huduma ya zahanani ya mimea ilitolewa. 

Wakulima wamiminika kwenye duka dogo la pembejeo lilipo Mafinga kwa ajili ya kupeleka mazao yao kwa ajili ya kupata utatuzi. Bwana shamba wa kampuni ya Yara Tanzania Ltd, Andrew Mwangomile aliwaelezea wakulima walioleta mahindi yao kwa ajili ya kupatia ufumbuzi wa changamoto zinazowakumba.

Bwana shamba huyo alipohojiwa aliesema, Yara Tanzania imeandaa huduma maalumu inayoitwa "crop clinic day" (siku ya zahanati ya mimea) huduma hii inafanana na ile ya binadamu au kiumbe hai yeyote anapohitaji huduma ya kwanza akijisikia kuumwa ili kupata huduma ya kwanza. Kwenye siku hii maalumu wakulima huleta mizizi, majani au zao lenyewe kwa ajali ya bwana shamba kuweza kumsaidia kutatua kwa haraka tatizo linalokabili mmea huo."

Moja ya kauli mbiu zetu ni mkulima afanikiwe na kuweza kulisha dunia kwa kutoa huduma muhimu zinazoweza kumsaidia mkulima kuzalisha mazao bora na sio bora mazao. Yara Tanzania inahakikisha ili mpango huo utekelezeke ni kusaida wakulima kutatua changamoto mbali mbali ya mazao. Siku ya zahanati kwetu ni muhimu na tunatoa huduma hii Bure kwenye mikoa yote nchini kushikiana na mawakala wadogo na wakubwa. Aliongeza alipohojiwa kwa njia ya simu afisa masoko na mawasiliano wa kampuni hiyo Bi. Linda Byaba.
Afisa Ugani (bwana shamba) wa Yara Tanzania, Andrew Mwangomile akiwaelezea wakulima waliotembelea kwenye duka la pembejeo lengo la Zahanati ya mimea iliyoanzishwa na Yara Tanzania kwa kutumia mfano wa zao la mahind.
Afisa Ugani (bwana shamba) wa Yara Tanzania, Andrew Mwangomile  akielezea aina ya virutubisho vinavuohitajika kwenye zao la mahindi na vinavyopatikana kwenye mbolea aina ya YaraMila CEREAL.

Article 8

Article 7

RC MAKONDA: KAULI ZA WATENDAJI SERIKALINI ZINAPASWA KUAKISI UWAJIBIKAJI KATIKA JAMII

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul C. Makonda Leo Mei 18, 2017 amefanya mazungumzo na Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi kutoka Manispaa za Ubungo, Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala Na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam
Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi kutoka Manispaa za Ubungo, Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala Na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam wakifatilia  kwa makini maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul C. Makonda Leo Mei 18, 2017
Mkurugenzi wa Manispaa ya ubungo Ndg john Lipesi Kayombo akifatilia kwa makini maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul C. Makonda Leo Mei 18, 2017 wakati wa kika na Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi kutoka Manispaa za Ubungo, Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala Na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul C. Makonda akisisitiza jambo.Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

TTCL yadhamini semina ya vijana

$
0
0
SHIRIKA la Trust Care Tanzania Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wameandaa semina ya kuwajengea uwezo wa kifikra wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali vya jijini Dar es Salaam ikiwa na lengo la kuwabadili wanafunzi kwa ujumla kuwa na mawazo chanya yatakayowawezesha kutumia fursa anuai zinazowazunguka katika jamii mara baada ya masomo yao.

Akizungumzia semina hiyo inayotarajiwa kufanyika Jumamosi ya tarehe 20/05/2017 katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE) kuanzia majira ya saa tatu asubuhi, Mkurugenzi Mtendaji wa Trust Care Tanzania Foundation, Zambert Mbwafu alisema semina hiyo ni maalum kwa wanafunzi waliopo vyuoni kwa ajili ya kuwajengea uwezo.
Alizitaja mada ambazo wanafunzi wanatarajia kufundishwa ni pamoja na Umuhimu wa Kujiamini na Kujijengea Uwezo, Uwezo wa Uthubutu, Vipaji na Jinsi ya Kuviendeleza, Maadili na Nidhamu katika Kazi na Ubunifu katika Kufikia Malengo. “Semina inawaandaa vijana waliopo na ambao wanatarajia kumaliza elimu yao ya juu hivi karibuni kupata elimu na ujuzi utakaowasaidia wakiwa shule na baada ya kumaliza masomo yao ili waweze kwenda sambamba na mahitaji ya ulimwengu wa sasa…” alisema Bw. Mbwafu.Akifafanua zaidi Mkurugenzi, Zambert Mbwafu, alivitaja vyuo vitakavyoshiriki katika semina hiyo; ni pamoja IFM, CBE, DIT, DUCE, TIA, UDSM, MUHAS, CHUO CHA DIPLOMASIA, KIU, CHUO CHA USTAWI WA JAMII NA CHUO KIKUU CHA TUMAINI.
 Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Injinia Enocent Msasi akizungumza katika mkutano na wanahabari leo kuzungumzia semina ya wanavyuo inayotarajia kufanyika Jumamosi ya tarehe 20/05/2017 katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE) kuanzia majira ya saa tatu asubuhi. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Trust Care Tanzania Foundation, Zambert Mbwafu na Ofisa Masoko wa Kampuni ya TTCL, Lulu Kamalamo (kulia) wakiwa katika mkutano huo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Trust Care Tanzania Foundation, Zambert Mbwafu akizungumza katika mkutano na wanahabari leo kuzungumzia semina ya wanafunzi wa vyuo vikuu inayotarajia kufanyika Jumamosi ya tarehe 20/05/2017 katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE) kuanzia majira ya saa tatu asubuhi. Kulia ni Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Injinia Enocent Msasi akiwa katika mkutano huo
Mkurugenzi wa Elimu na Utafiti wa Trust Care Tanzania Foundation, Fadhila Nyoni akifafanua jambo juu ya semina ya wanafunzi wa vyuo vikuu katika mkutano na wanahabari leo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Trust Care Tanzania Foundation, Zambert Mbwafu akifuatilia mazungumzo hayo.

Rais Dkt.Magufuli kukabidhi uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni

$
0
0
Na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kukabidhi uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni baada ya kumaliza muda wake.
Tanzania imemaliza uenyekiti wake baada ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt Augustine Mahiga kukabidhi uenyekiti wa Mawaziri wa Afrika Mashariki kwa Uganda mwezi Aprili mwaka huu. 
Dkt Mahiga amesema, Tanzania imekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa miaka miwili mfululizo kwani baada ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kumaliza muda wake, Wakuu wanchi wanachama wa jumuiya hiyo walimchagua Rais Magufuli kuendelea kuwa Mwenyekiti. 
“Kwa hiyo pamoja na hilo lakini pia kuna mambo mengi ambayo tumejadiliana na mengine yatatolewa uamuzi na Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,” amesema Dkt. Mahiga. 
 Amesema karibu marais wa nchi zote wanachama wanatarajiwa watakuwepo isipokuwa Sudani Kusini ambayo imetoa udhuru.
 Marais ambao wamethibitisha kuhudhuria ni pamoja na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Rais wa Rwanda, Paul Kagame, Rais wa Uganda, Yoweri Museveni na Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza.
 Waziri wa  mambo ya Nje ,Uhusiano wa Afrika Mashariki,Balozi Dk Augustine Mahiga akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki ,Dkt. A.M Kirunda Kivejinja katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.
Mawaziri  mbalimbali wa Jumuia ya Afrika Mashariki waliohudhuria Mkutano huo
 Mawaziri  mbalimbali wa Jumuia ya Afrika Mashariki waliohudhuria Mkutano huo
Mawaziri  mbalimbali wa Jumuia ya Afrika Mashariki waliohudhuria Mkutano huo
Mawaziri  mbalimbali wa Jumuia ya Afrika Mashariki waliohudhuria Mkutano huo. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI AWAFUNDA VIONGOZI WAANDAMIZI WA UHAMIAJI, MKOANI KILIMANJARO

$
0
0

  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi Mhe. Meja Jenerali Projest Rwegasira (Katikati) akiongoza Kikao kazi cha Viongozi Waandamizi wa Idara ya Uhamiaji (hawapo pichani). Wa pili kutoka kushoto ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala(wa pili toka kulia) ni Kamishna wa Uhamiaji – Zanzibar, Johari M. Sururu(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda-TRITA, Kamishna Maurice David Kitinusa(wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Utawala na Fedha, Edward P. Chogero.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala akitoa hotuba fupi kwenye Kikao kazi cha Maafisa Waandamizi wa Idara ya Uhamiaji kilichofanyika hivi karibuni Mjini Moshi.
Maafisa Waandamizi wa Uhamiaji wakifuatilia kwa makini hotuba ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala(hayupo pichani)kwenye Kikao kazi hicho kama inavyooneka katika picha.
Kamishna wa Pasipoti na Uraia, Gerald Kihinga akitoa ufafanuzi katika Kikao kazi cha Viongozi Waandamizi wa Idara ya Uhamiaji mbele ya Katibu Mkuu Mhe. Meja Jenerali Projest Rwegasira (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa kikao hicho kilichofanyika hivi karibuni mjini Moshi.
Kamishna wa Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka, Samuel R. Magweiga akifafanua jambo kwa mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi Mhe. Meja Jenerali Projest Rwegasira(hayupo pichani) katika kikao hicho.



Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala(kulia) akimuongoza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira kukagua moja ya majengo mbalimbali ya Chuo Cha Uhamiaji cha Kikanda-TRITA kilichopo Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi Mhe. Meja Jenerali Projest Rwegasira akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Makamishna wa Idara ya Uhamiaji(waliosimama). Wa pili toka kushoto ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala(wa pili toka kulia ni Kamishna wa Uhamiaji – Zanzibar, Johari M. Sururu(wa kwanza kulia)ni Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda-TRITA, Kamishna Maurice Kitinusa(Picha zote na:- Kitengo cha Uhusiano Chuo Cha Uhamiaji cha Kikanda-TRITA Moshi, Kilimanjaro)

Bitdefender Antivirus blocks world’s most aggressive piece of ransomware with next-generation detection technologies

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 18.05.2017

MAMIA YA WANANCHI WAJITOKEZA KUJISAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA WILAYA YA MUFINDI

$
0
0

Wananchi wa Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa wamejitokeza kwa wingi kusajili Vitambulisho vya Taifa kufuatia maelekezo ya Mkuu wa mkoa huo Mhe. Amina Masenza ambaye amejizatiti kuweka historia ya kuwa mkoa wa kwanza kwa wananchi wake kuwa na Vitambulisho vya Taifa; baada ya kufanikisha kwa asilimia kubwa zoezi la kuwasajili Watumishi wa Umma lililofanyika nchi nzima.

Kwa kuanza; zoezi la Usajili kwa mkoa wa Iringa limeanza katika Wilaya ya Mufindi ambapo zaidi ya wananchi 70,000 wameshajiliwa katika Kata 20 kati ya Kata 36 zilizopo Wilaya humo, huku wananchi 50,000 wakiwa tayari na Vitambulisho vya Taifa.

Akizungumza wakati wa kukagua utekelezaji wa zoezi hilo; Mkuu wa Wilaya ya Mufindi ambako zoezi hilo linaendelea kwa sasa Mhe. Mhe. Jamhuri William amesema “kama Wilaya wamejipanga kuhakikisha zoezi la kuwasajili wananchi linafanyika katika muda mfupi iwezekanavyo na kwamba uhamasishaji umefanyika kwa njia mbali mbali kuhakikisha wananchi wanatumia vema fursa Iliyopo”

Amesisitiza mbali na kuwasajili wananchi; Wilaya ya Mufundi pia inaendelea na zoezi la kuwasajili Wageni na Wakimbizi wanaoishi kihalali Wilayani humo, lengo likiwa ni kupata taarifa sahihi za watu na kuimarisha upatikanaji wa huduma kiurahisi kwa wananchi.

Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Amina Masenza alizindua kuanza kwa zoezi la usajili mkoa wa Iringa na kuelekeza kwa kushirikiana na NIDA kila Wilaya kuhakikisha ndani ya siku 60 kuwa wamekamilisha zoezi la kuwasajili wananchi Vitambulisho vya Taifa; na kuwahakikishia wananchi Ofisi yake itahakikisha wananchi wote wakaosajiliwa wanapata Vitambulisho vyao kwa wakati ili matumizi kuanza mara moja.

Wananchi wakipokea maelekezo ya namna ya kushiriki zoezi la Usajili linaloendelea Wilayani Mufindi. 
Baadhi ya wananchi katika Kata ya Ifwagi wakiwa kwenye foleni kusajiliwa zoezi la Vitambulisho vya Taifa linaloendelea Wilayani Mufindi. 
Maafisa wa NIDA wakiendelea na zoezi la uchukuaji alama za Vidole, picha na saini ya Kielektroniki wakati wa zeozi la Usajili likiendelea kwa wananchi wa Wilaya ya Mufindi. 
Afisa Usajili mkoa wa Iringa bwana George Mushi akizungumza jambo na wananchi wa Kata ya Ikongosi wakati wakisubiri kupata huduma ya usajili vitambulisho vya Taifa (NIDA) .

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images