Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live

Waziri wa Fedha na Mipango akutana na viongozi waandamizi wa IMF na balozi wa Hungary

$
0
0
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba ( kulia)  wakipeana mkono baada ya kumalizika kwa Mkutano kati yao uliohusu suala la Uchumi katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang (kushoto) wakiagana baada ya kumaliza mkutano kati yao, katika Mkutano huo Zhang aliipongeza Serikali kwa hatua nzuri za ukuaji wa Uchumi.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu (kulia) akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba (kushoto) baada ya kumalizika kwa Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es salaam
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto) akipongezana na Balozi wa Hungary hapa nchini mwenye makazi yake Nairobi Kenya, Laszlo Mathe (kulia), baada ya kumalizika kwa Mkutano kati yao kuhusu uwekezaji wenye tija kwa pande zote mbili. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA



Yara Tanzania Ltd yajikita kuwapiga msasa wataalamu wake ili kusaidia wakulima kwa haraka

$
0
0
 Afisa mwandamizi wa kilimo wa Burka Coffee Estates mkoani Arusha Bw. James Odhiambo (wa pili kushoto) akielezea jambo kwa mkurungezi wa kampuni ya Yara Tanzania Bw. Alexandre Macedo (kulia) walipotembelea shamba hilo pamoja na wataalamu wengine kutoka kwenye kampuni. 
Bw. Alexandre alisema moja ya vitu vikuu Yara Tanzania Ltd inajikita ni pamoja kuwapiga msasa wataalamu wa kampuni hiyo mara kwa mara ili waongeze ujuzi kwenye sekta hiyo na kuwasaidia wakulima kwa haraka wanapokutana na changamoto za kilimo upande wa mbolea.                    
"Wataalamu wetu wanao uwezo mkubwa wa kutambua ukosefu wa virutubisho kwenye mmea ila kama kampuni huandaa mafunzo kama haya ili kuwaongezea ujuzi wa kutambua na kutatua changamoto za mbolea wanazopata wakulima. Yara inatengeneza mipangilio maalumu ya lishe linganifu ya mimea baada ya tafiti  ya miaka mitatu. 
"Mfano mpangilio wa lishe ya zao la kahawa upo tayari na wakulima wanapewa semina mbalimbali kuhusu lishe hiyo kwani tafiti za udongo na virutubisho vinavyohitajika kwenye zao hilo ili liwe bora na mavuno yaongezeke ulishafanyika. 
"Ila kuna changamoto zingine hujitoteza ambazo wataalamu wetu hukumbushwa jinsi ya kuzitatua kupitia mafunzo kama haya ya mara kwa mara" Asema Bw. Alexandre
Picha ya zao freshi la kahawa iliyotapa virutubisho muhimu kupitia mbolea maalumu za zao hilo kutoka Yara Tanzania Ltd.

NHIF Vacancy Opportunities

MKURUGENZI MTENDAJI WA IMF ASISITIZA UMUHIMU WA KILIMO NA NISHATI KATIKA KUKUZA UCHUMI WA TANZANIA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba (wa pili kulia) akieleza kuwa Tanzania inakua kwa kasi kiuchumi jambo ambalo linawavutia viongozi wengi kufuatilia kwa karibu maendeleo yake, alipokutana na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto), katika Ukumbi wa Wizara Jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiongoza Mkutano kati yake na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba (mbele kulia) ambapo alisema mahitaji makubwa wa nchi ni maendeleo ya kilimo na upatikanaji wa nishati ya umeme ili viweze kuchochea uchumi wa viwanda. Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (watatu kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba (wa tatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na Maafisa waandamizi wa Wizara hiyo baada ya kumalizika kwa mkutano kuhusu hali ya uchumi katika Ukumbi wa Wizara Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba (hayupo pichani) wakimuaga baada ya kumalizika kwa Mkutano katika ukumbi wa Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

SHIRIKA LA FEDHA DUNIANI-IMF LAAHIDI KUIKOPESHA ZAIDI TANZANIA ILI KUKUZA UCHUMI

$
0
0

Na Benny Mwaipaja, WFM

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang (kushoto) ameahidi kufungua madirisha ya mikopo kwa nchi ya Tanzania kutokana na jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali za kukuza uchumi.

Bw. Zhang aliyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), katika ofisi za Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam.

“Shirika la Fedha la Kimataifa limeziona jitihada za kukuza uchumi wa nchi ambapo mpaka sasa Tanzania inaongoza katika nchi za Afrika Mashariki na ipo juu ya wastani wa ukuaji wa uchumi Barani Afrika” Alisema Bw. Zhang.

Ameishauri Serikali kuendelea kushirikiana na Sekta binafsi  katika ukuaji wa Uchumi ili uchumi huo uwe endelevu. Aidha ameitaka Serikali kuwa na mfumo shirikishi wa kifedha utakao wanufaisha wananchi wengi.

Naye Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), amesema kuwa juhudi za Tanzania  kwa sasa ni  kuchochea ukuaji wa Kilimo na kuongeza uzalishaji wenye tija

“Umasikini haujatatuliwa kwa kiwango ambacho Serikali ingependa kukiona, kwa kuwa mpaka sasa watu walio katika  umasikini na ukosefu wa huduma za lazima ni takribani asilimia 34.4 “, aliongeza Dkt. Mpango

Kama nchi imeamua kwenda kwenye uchumi wa kati na jambo ambalo linatiliwa mkazo ni upatikanaji wa umeme wa kutosha na wenye bei nafuu .

Amesema kuwa Serikali imefanya juhudi za kupeleka umeme mpaka vijijini lakini bado kazi hiyo haijakamilika. Pia suala la miundombinu ya ya usafirishaji ni changamoto, ukiwemo usafiri wa reli kutoka Mashariki hadi Magharibi mwa nchi ambao ni wazamani na umeharibika.

“Serikali imeamua kujenga Reli yenye kiwango cha Kimataifa (Standard gauge)  ambayo ni ya gharama, na kwa makadirio ya awali zinahitajika Dola Bilioni 7.6, lakini umechukuliwa uamuzi huo ili kuharakisha Maendeleo”aliongeza Dkt. Mpango 

“Tayari tumeanza ujenzi wa reli hiyo kwa fedha za ndani kwa takribani Kilometa 200 kutoka Dar es salaam mpaka Morogoro na tutaendelea na ujenzi kadri fedha zinavyo patikana” alifafanua Waziri Mpango .

Amesema kuwa, kumekuwa na tatizo la ahadi za Wahisani kutotekelezwa kwa wakati jambo linalofanya baadhi ya shughuli za maendeleo kutotekelezwa kwa wakati.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba, alisema ni  vema Serikali ikaendelea kuangalia vipaumbele  katika ujenzi wa miundombinu ili iweze kuchochea uchumi.
“Suala la ajira hasa kwa vijana linatakiwa kufanyiwa kazi na pia kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na ufanyaji biashara kwa Sekta Binafsi kwa kuwa Sekta Binafsi imekuwa na mchango mkubwa katika Maendeleo kwa nchi nyingi Duniani” Alishauri Bw. Mkwezalamba.
Ameishauri Tanzania kuendelea kuwekeza kikamilifu katika Sekta ya Elimu kwa kuwa ni moja ya eneo ambalo kama likifanyiwa kazi kikamilifu litaleta Matokeo chanya na ya haraka katika ukuaji wa Uchumi.
Akitoa ufafanuzi wa hoja hizo, Waziri Mpango, amesema Serikali imeendelea kuhakikisha kunakuwa na viwanda vingi ili vijana wengi waweze kupata ajira. Aidha tayari Tanzania imeanza kutekeleza Elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne ili kutoa fursa kwa watu wengi zaidi kupata elimu.

Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Bwana Amour Hamad Amour akagua miradi ya maendeleo namtumbo

$
0
0
Inline image 1
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Bwana Amour Hamad Amour aliyepiga magoti akiangalia Tanki la maji na uwepo wa maji katika Tanki hilo ambapo alilidhishwa na uwepo wa maji katika kijiji cha Njalamatata wilayani Namtumbo na kuridhishwa na mradi huo uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 713.

WAZIRI MHAGAMA KUFUNGUA MKUTANO WA BODI ZA MIFUKO YA HIFADHI

$
0
0
Mh. Jenister Mhagama
NA BALTAZAR MASHAKA.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Walemavu Jenister Mhagama, anatarajiwa kufungua mkutano wa Bodi za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania (TSSA).

Mkutano huo unaoratibiwa na Jumuiya ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania (TSSA) utafanyika jijini Arusha kuanzia Mei 19 na 20, mwaka huu na utahusu ushiriki wa mifuko hiyo kwenye uwekezaji wa uchumi wa viwanda.

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa TSSA Meshack Bandawe alisema mkutano huo utakaofunguliwa na Waziri Mhagama, utashirikisha mifuko saba ya Tanzania bara na mmoja wa Zanzibar.

 Alisema Bodi pamoja na Wakuu wa mifuko hiyo watapata fursa ya  kujadili mafanikio, hatua na maendeleo yaliyofikiwa kwenye uwekezaji wa uchumi wa viwanda wenye tija na fursa nchini.

“ Kwenye mkutano huo ambao tumewaalika wadau mbalimbali tutaangalia mafanikio nachngamoto tulizozipata katika uwekezaji wa viwanda kama fursa muhimu hapa nchini,

“Pia tutangalia maendeleo ya ukuaji wa mifuko kiuchumi ili kutuwezesha kutekeleza kwa ufanisi uwekezaji wetu uwe na tija ambao utasaidia kukuza uchumi wan chi,”alisema Bandawe.

Katibu Mkuu huyo wa TSSA alisema kuwa mifuko hiyo imeanza utekelezaji kwwa kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ya viwanda  na baadhi ya miradi hiyo iko kwenye upembuzi yakinifu.
Meshack Bandawe

Alidai kuwa miradi hiyo ikikamilika itatengeneza ajira kwa vijana wa Tanzania ambao watakuwa wananchama wa mifuko yenyewe  na hivyo kuwa tija katika taifa kwa ujumla.

Kwa mujibu wa Bandawe  nia ya mkutano huo ni kufikia lengo la uwekezaji wa viwanda na ndiyo maana wamewaalika Msimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA), Benki Kuu (BOT),Wizara ya Viwanda na Biashara, Tume ya Mipango na Msajili wa Hazina.

Bandawe alieleza kuwa TSSA inaundwa na mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo ni NSSF, PPF,LAPF,GEPF,NHIF,WCF na ZSSF.

Halmashauri kunufaika na Tsh 250 bilioni za mradi wa maji vijijini

$
0
0

Halmashauri za wilaya zimetakiwa kuongeza ufanisi katika kusimamia miradi ya maji kwa kuchangamkia fursa ya fedha za kitanzania bilioni 250 zilizotolewa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Uingereza (DFID) kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa usambazaji maji safi na salama vijijini (2016-2020).

Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Injinia Jackson Mutazamba aliwaambia wakurugenzi wa wilaya katika semina inayofanyika mjini Morogoro jana kuwa ni halmashauri chache tu ndio zimeanza kupata fedha hizi mara baada ya kukidhi vigezo vinavyotakiwa na wafadhili.

"Kuna fedha za kutosha katika mradi huu ukilinganisha na mwamko wa halmashauri katika kuchangamkia fursa hii ya kuongeza mtandao wa maji katika maeneo yao," alisema na kuongeza kuwa fedha hizi zinaweza kuzisaidia halmashauri kuanzisha miradi mipya na kukarabati ile ya zamani ili iweze kutoa maji kwa wakati wote wa mwaka.

Alisema moja ya sharti la upatikanaji wa fedha hizi ni ufanisi katika utekelezaji wa miradi iliyopita na ubora wa ripoti za kila mwezi kama ambavyo programu hii inavyozitaka halmashauri. Kigezo hiki ni muhimu sana katika kuvuka hatua moja hadi nyingine na kupata fungu kubwa zaidi la fedha ambalo litawezesha kutekeleza miradi mikubwa zaidi katik halmashauri husika.

Kwa mfano halmashauri zinaweza kupokea aina mbili za malipo kama vile paundi za kiingereza 50 kwa ajili ya kuendeleza kituo cha maji na fungu hili linaweza kuongezeka hadi paundi 1,500 kulingana na ufanisi wa utekelezaji katika hatua ya mwanzo.

"Ukipata paundi zaidi ya 1,500 kwa mara moja kwa miradi ya vijijini ni nyingi sana katika kuiboresha na kuifanyia matengenezo ya mara kwa mara ili kuhakikisha upatikanaji wa maji wakati wote. Na pia fedha hizi zinaweza kutumika kuanzisha vituo vipya vya kusambazia maji hivyo kufanya mtandao wa maji kuwa mkubwa zaidi katika eneo husika," alisema.


Mratibu wa mradi wa usafi wa mazingira uitwao Nipo Tayari Juliana Kitira akimuonyesha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kakonko, Kigoma, Elinatha Elisha takwimu za hali ya usafi wa mazingira katika halmashauri yake kwenye simina inayofanyika Morogoro. Mradi huo pia unahamasisha uwepo wa vyoo bora na kunawa mikono na maji safi baada ya kutoka chooni.
Mkurugenzi wa wilaya ya Bagamoyo Fatuma Latu akiangalia msimamo wa wilaya yake katika usafi wa mazingira kupitia mradi wa Nipo Tayari chini ya Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii Jinsia, Watoto, Walemavu na Wazee kwenye semina inayofanyika mjini Morogoro.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Simanjiro mkoani Manyara Yefred Myenzi akiapa kuwa yupo tayari kutekeleza kwa vitendo kampeni ya nchi nzima ya usafi wa mazingira iitwayo Nipo Tayari kwenye semina inayofanyika mjini Morogoro. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Sabas Damian Chambasi akiapa kuwa yupo tayari kutekeleza kwa vitendo kampeni ya nchi nzima ya usafi wa mazingira iitwayo Nipo Tayari kwenye semina inayofanyika mjini Morogoro. 


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Zanzibar haibaguliwi katika EAC

$
0
0
Serikali ya Zanzibar inashiriki moja kwa moja bila ukomo katika masuala yote ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), hivyo Wazanzibari wamehimizwa kuchangamkia fursa zilizopo kwenye Jumuiya hiyo na kuondokana na dhana kuwa eti, Serikali yao inabaguliwa.

Akiwasilisha mada leo kuhusu ushiriki wa Zanzibar katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye semina ya masuala ya mtangamano wa EAC inayofanyika Pemba, Afisa wa Ushirikiano wa Kimataifa kutoka Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Bw. Suleima Haji alitoa ufafanuzi wa kina kuonesha namna Zanzibar inavyoshiriki katika EAC.

Bw. Haji alieleza kuwa licha ya Zanzibar kuwa sehemu ya muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ushiriki wake umedhihirika katika mgawanyo wa miradi ya maendeleo ya EAC, hususan miradi ya Miundombinu. Alisema Zanzibar iliwasilisha mapendekezo ya miradi 10 kwenye Sekretarieti ya EAC na kutokana na vipaumbe vilivyowekwa miradi 3 imekubaliwa na mchakato wa kuitekeleza unaendelea.

 Miradi hiyo ni ujenzi wa Bandari ya Marhubi kisiwani Pemba, upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba na ununuzi wa meli kubwa zitakazosafirisha abiria na mizigo kwenye nchi wanachama wa EAC.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akimkaribisha Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii, Bw. Eliabi Chodota kutoa mada kwenye semina ya mtangamano inayoendelea Kisiwani Pemba. Ushiriki na mwitikio katika semina hiyo umekuwa mkubwa kwa washiriki ambapo wameonekana kuvutiwa sana na semina hii pia wamekuwa wadadisi wazuri wa kutaka kujua zaidi fursa zinazo patikana kwenye mtangamano huo. 
Bw. Chodota akitoa mada kwenye semina ya mtangamano inayoendelea Pemba.  
Bw. Salehe akijibu maswali hayo na kutolea ufafanuzi kwa baadhi ya mambo. 




KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

NAIBU KATIBU MKUU CCM BARA, RODRICK MPOGOLO ZIARANI JIMBO LA ILALA, TEMEKE.

$
0
0

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza na Wanachama, Viongozi wa CCM wa Jimbo la Ilala wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, jana.
Baadhi ya Wanachama wa CCM Jimbo la Ilala wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu CCM Bara.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akiwasili kwenye Ukumbi wa CCM Ilala kwa ajili ya kuzungumza na Wanachama, Viongozi wa CCM wa Jimbo la Ilala wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, jana.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza na Wanachama, Viongozi wa CCM wa Jimbo la Ilala wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, jana.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, wakati akiondoka kwenye Ukumbi wa CCM Ilala baada ya kuzungumza na Wanachama, Viongozi wa CCM. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)

Huduma ya Zahati ya mimea sasa yatolewa BURE na Yara Tanzania Ltd

$
0
0
Mamia ya wakulima wanamiminika kwenye duka dogo la pembejeo lilipo Mafinga mkoani Iringa kupeleka mazao yao kwa ajili ya kupata utatuzi. Bwana shamba wa kampuni ya Yara Tanzania Ltd Bw. Andrew Mwangomile bila kuchoka amekuwa akiwaelezea wakulima walioleta mahindi yao kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi wa changamoto zao.
Bwana shamba huyo alipohojiwa aliesema, Yara Tanzania tumeandaa huduma maalumu inayoitwa "crop clinic day" (siku ya zahanati ya mimea) huduma hii inafanana na ile binadamu au kiumbe hai yeyote anapohitaji huduma ya kwanza akijisikia kuumwa ili kupata huduma ya kwanza. Kwenye siku hii maalumu wakulima huleta mizizi, majani au zao lenyewe kwa ajali ya bwana shamba kuweza kumsaidia kutatua kwa haraka tatizo linalokabili mmea huo."  
'Moja ya kauli mbiu zetu ni mkulima afanikiwe na kuweza kulisha dunia kwa kutoa huduma muhimu zinazoweza kumsaidia mkulima kuzalisha mazao bora na sio bora mazao. Yara Tanzania inahakikisha ili mpango huo utekelezeke ni kusaida wakulima kutatua changamoto mbali mbali ya mazao. 
"Siku ya zahanati kwetu ni muhimu na tunatoa huduma hii Bure kwenye mikoa yote nchini kushikiana na mawakala wadogo na wakubwa", aliongeza bwana shamba huyo  alipohojiwa kwa njia ya simu afisa masoko na mawasiliano wa kampuni hiyo Bi. Linda Byaba 
Wakulima wakipata maelezo yaliopo kwenye kipeperushi cha mahindi cha Yara Tanzania kutoka kwa Bw. Andrew Mwangomile  baada ya zao lake kugundulika na changamoto kadhaa hanani ya mimea ilitolewa
 Bwana Shamba Andrew Mwangomile akielezea aina ya virutubisho vinavuohitajika kwenye zao la mahindi na vinavyopatikana kwenye mbolea aina ya YaraMila CEREAL
 Afisa Ugani wa Yara Tanzania Andrew Mwangomile akiwaelezea wakulima waliotembelea kwenye duka la pembejeo lengo la Zahanati ya mimea iliyoanzishwa na Yara Tanzania kwa kutumia mfano wa zao la mahindi
 Picha ya zao la mahindi lililoletwa na mkulima kwa ajili ya uchunguzi siku ya zahanati ya mimea.

MAKUMBUSHO NA NYUMBA YA UTAMADUNI KUADHIMISHA SIKU YA MAKUMBUSHO DUNIANI.

$
0
0
Bw Achiles Bufure, Mkurugenzi Makumbusho 
na Nyumba ya Utamaduni Dar es salaam 

Tarehe 18 May ni siku ya Makumbusho Duniani kwa apata Tanzania, Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni itaungana na Makumbusho zote katika kuadhimisha siku hii muhimu hivyo watanzania wameshauriwa kuudhuria katika maadhimisho hayo ili waweze kupanua uwelewa zaidi wa mambo mbali mbali yanayo huyu maisha yao na nchi kwa ujumla. 
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar Es Salaam Bwana Achiles Bufure ofisini kwake, Bwana Bufure ameongeza kuwa katika Maadhimisho hayo, kutakuwa na Onesho maalum litakalo onesha vifaa mbali mbali vya ofisi alivyotumia Muhasisi wa Taifa hili Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere, Mafunzo shirikishi kwa watoto juu ya shughuli za kimakumbusho na Onesho la jukwaani.  
Wananchi mbali mbali wameisifu Mkumbusho na Nyumba ya Utamaduni kwa kuadhimisha siku hiyo kwa kufungua milango hata kwa watu wasio na uwezo wakulipia pindi wanapo tembelea Makumbusho hiyo kwakuwa na wao watapata nafasi adhimu ya kujifunza mambo yanayo husu nchi yao kwa kupitia vioneshwa vilivyopo ndani ya Makumbusho. 
 Maadhimisho hayo ya Siku ya Makumbusho Duniani yatadumu kwa muda wa wiki moja kuanzia leo ili kutoa nafasi kwa watanzania warika mbali mbali kutembelea Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni na kwa tarehe 18 May hakutakuwa na kiingilie cha kuingia na kutembelea maonesho mbalimbali yaliyopo Makumbusho hiyo iliyopo mkabala na chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dar es Salaam, Posta.


introducing New Song, New Group from P-Funk Majani's Bongo Records Bongolos ft Asteria - WAPE

$
0
0
Bongolos ni kundi la wanamuziki wawili, Drew (Kiume) na Tamu (Kike), lenye makazi yake jijini Dar es Salaam, Tanzania. Bongolos ni kundi lililoundwa na mtayarishaji mkongwe wa muziki Afrika Mashariki P-Funk Majani ndani ya Bongo Records mwaka 2016. Jina Bongolos lilipatikana kutoka kwa mwanamuziki wa hip hop wa Marekani, Mims baada ya kuja kufanya kolabo nchini Tanzania chini ya Bongo Records.
Drew wa Bongolos alikutana na mtayarishaji P-Funk Majani baada ya kuona ujumbe mfupi wa maneno kwenye mitandao ya kijamii kwamba mtayarishaji huyo alikuwa anatafuta wanamuziki chipukizi. Tamu wa Bongolos alikutana na mtayarishaji huyo baada ya kuunganishwa na rafiki yake.
Bongolos wanafanya muziki ambao ni mchanganyiko wa muziki wa kufoka na kuimba ambao pia unawezwa kuitwa Bongo Flava. Muziki wao umejawa na vionjo vya Kiafrika kwenye mirindimo yake. Bongolos wameachia ngoma yao ya kwanza iitwayo Wape.

Song : WAPE

Artists : Bongolos ft Asteria Mvungi

Music Producer : P-Funk Majani

Copyright Holder : Bongo Records Ltd

MAREKANI KUENDELEA KUSAIDIA WATU WA TANZANIA KUKABILIANA NA VVU/UKIMWI

$
0
0
Serikali ya Marekani kupitia Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR), umeidhinisha mpango wa kutoa Dola za Kimarekani Milioni 526 katika kipindi cha mwaka mmoja ujao kwa ajili ya kukabiliana na VVU/UKIMWI nchini Tanzania. Msaada huu utaongeza idadi ya Watanzania wanaopatiwa matibabu ya kufubaza VVU kufikia milioni 1.2 na utaimarisha mapambano dhidi ya VVU kupitia huduma za upimaji, matibabu, kufubaza (viral suppression) na kuzuia maambukizi ili hatimaye kufikia lengo la kuutokomeza kabisa UKIMWI ifikapo mwaka 2030. 
Fedha hizo zitafadhili miradi mbalimbali inayotekelezwa chini Mpango wa Utekelezaji wa  PEPFAR Nchini utakaoanza kutekelezwa Mwezi Oktoba 2017 hadi Septemba 2018, na ni ongezeko la asilimia 12.3 ya bajeti ya mwaka jana.  Chini ya mpango huu mpya, PEPFAR itafanya kazi na Serikali ya Tanzania na wabia wake kadhaa kutoa huduma ya upimaji wa VVU kwa Watanzania milioni 8.6 na kutoa matibabu ya kufubaza VVU kwa watu 360,000 watakaobainika kuwa wameambukizwa virusi hivyo kufanya idadi ya Watanzania watakaokuwa wakipata matibabu hayo kufikia milioni 1.2.  Bajeti iliyotengwa inajumuisha pia utoaji wa huduma na matibabu kwa watoto yatima na wale walio katika mazingira hatarishi pamoja na kukabiliana na ukatili wa kijinsia.  Hali kadhalika, katika kuimarisha jitihada za kuzuia maambukizi mapya ya VVU, PEPFAR itasaidia mpango wa tohara ya hiari kwa wanaume (VMMC) ambapo wanaume 890,000 watapatiwa huduma hiyo. 
Mpango huu unaendeleza ubia wa muda mrefu kati ya Marekani na Tanzania katika sekta ya afya ikiwa ni pamoja na muongo mmoja wa ushirikiano uliowezesha kudhibiti kwa mafanikio makubwa maambukizi ya VVU na kufanyakazi tukilenga katika kuwa na Kizazi kisicho na UKIMWI. Akitoa maoni yake kuhusu mpango huu ulioidhinishwa, Kaimu Balozi wa Marekani nchini Virginia Blaser alisema “Kwa niaba ya Watu wa Marekani tuna furaha kubwa kuendelea kuwasaidia watu wa Tanzania na kuendeleza ubia uliopo baina yetu. Kwa pamoja tunafanya kazi ili hatimaye kuwa na Kizazi Kisicho na UKIMWI Tanzania – ambacho hakuna hata mtu mmoja anayeachwa nyuma.”  
Wadau na wabia wa PEPFAR walioshiriki katika uandaaji wa mpango huu na watakaoshiriki katika utekelezaji wake ni pamoja na Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS), Programu ya Pamoja ya Umoja wa Mataifa ya Kudhibiti VVU/UKIMWI (UNAIDS), Mfuko wa Kimataifa wa Kupambana na Kifua Kikuu, UKIMWI na Malaria (GFTAM), Shirika la Afya Duniani (WHO), Taasisi ya Bill na Melinda Gates, Taasisi ya Benjamin Mkapa ya kukabiliana na VVU/UKIMWI (BMAF) na Mtandao wa Kitaifa wa Wanawake wanaoishi na VVU/UKIMWI (NETWO+). 

Kwa taarifa zaidi kuhusu PEPFAR nchini Tanzania tafadhali tembelea tovuti ya Ubalozi wa Marekani https://tz.usembassy.gov/our-relationship/pepfar/.


MAGAZETI YA LEO ALHAMIS MAY 18,2017

KINANA AONGOZA KIKAO CHA MAKATIBU WAKUU WA VYAMA VYA UKOMBOZI WA KUSINI MWA AFRIKA NCHINI ANGOLA

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Ndugu Abdrahamani Kinana yuko nchini Angola akiongoza ujumbe wa CCM katika kikao cha Makatibu Wakuu wa Vyama vya ukombozi wa kusini mwa Afrika( Front Line State parties). Pia Ndugu Katibu Mkuu ameongoza Majadiliano na vyama Rafiki vilivyoshiriki Mkutano huo kikiwemo Chama Cha Kikomunisti Cha watu wa China .
Ujumbe wa CCM ambao umejumuisha katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi( Ndg.Humphrey Polepole) Katibu wa Siasa na Uhusiano wa kimataifa Ndg. Ngemela Lubinga na watendaji wa Jumuiya za Chama hicho katika mazungumzo na ujumbe wa  Chama Cha Kikomunisti Cha watu wa China nchini Angola. Vyama rafiki vimepongeza CCM mpya na mwenendo wake.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  (kushoto) akizungumza jambo na baadhi ya viongozi wa vyama Rafiki vilivyoshiriki Mkutano huo kikiwemo Chama Cha Kikomunisti Cha watu wa China nchini Angola.

Maelfu ya akina mama waendelea kunufaika na huduma ya wazazi nipendeni

$
0
0
Maelfu ya akina mama wanaendelea kunufaika na huduma ya ujumbe mfupi wa maandishi unaotolewa bure na Vodacom Tanzania Foundation wa ‘Wazazi Nipendeni’, unazidi kuendelea kuwanufaisha maelfu ya akina mama wajawazito kupitia dondoo mbali mbali za kiafya.

Akiongea na mtandao huu Faidha Abdallah pichani ambaye ni mkazi wa Buguruni jijini Dar es Salaam anasema amekuwa akitumia huduma hiyo ambayo imekuwa msaada mkubwa kwake.

“Kupitia huduma hii ninaweza kujifunza namna ya uzazi salama kupitia simu yangu ya kiganjani bila malipo yoyote. Nimekuwa nikipokea ujumbe kila wiki na ninaishukuru  Vodacom Tanzania Foundation pamoja na wadau wengine waliofanikisha huduma hii nzuri,” anasema.

 “Pamoja na kuwa nimezaa na kukuza watoto wawili, sikufahamu kuwa kumbe ni muhimu sana kumnyonyesha mtoto kwa miezi sita bila kumkatisha kabla ya kuanza kumlisha aina nyingine ya chakula,” anaelezea

Naye Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald alisema jijini Dar es Salaam kuwa, zaidi ya wateja milioni moja wamejiunga na huduma hiyo tangu izinduliwe mwaka 2012.

“Wateja waliojiunga na huduma hii wamepokea jumla ya ujumbe mfupi unaofikia milioni 55 wenye maelekezo mbali mbali  juu ya afya bila malipo. Ujumbe wanaopokea ni pamoja na kubaini dalili hatari kwa uja uzito mapema, maendeleo ya mtoto, namna ya kuepuka maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa  mtoto, vyakula muhimu kwa mama mja mzito, uhuhimu wa  mama kuhudhuria kliniki mapema,” anaeleza
Oswald  anasema, kupitia ujumbe mfupi akina mama wajawazito wanaelimishwa namna ya kuishi wakiwa na afya ili waweze kujifungua watoto wenye afya bora pia watu wengine kama vijana, akina mama na wazee wanaweza kujifunza namna ya kujikinga na magonjwa mbali mbali kama Malaria na mengineyo.
Wateja wetu  wanaweza kupata   huduma hii ya bure kwa kutuma ujumbe kwenye namba 15001 au 15012 na wataweza kupokea ujumbe mfupi kupitia simu zao za viganjani.

MHE. SYLVESTER MABUMBA BALOZI WA TANZANIA NDANI YA MUUNGANO WA VISIWA VYA KOMORO AWASILISHA HATI ZAKE ZA UWAKILISHI

$
0
0
Balozi wa Tanzania ndani ya Muungano wa Visiwa vya Komoro, Mhe. Sylvester M. Mabumba tarehe 15 Mei alikabidhi hati zake za uwakilishi kwenda kwa Mhe. Azali Assoumani, Rais wa Muungano wa Visiwa vya Komoro. Hafla ya kukabidhi hati hizo ilifanyika kwenye Ukumbi wa Ikulu ya Komoro ijulikanayo kama  Beit. Wakati akisoma risala yake, Mhe. Balozi alijitambulisha kwa Mhe. Rais na kueleza furaha yake ya kuteuliwa kwake kuwa Balozi wa pili kutoka Tanzania kuja kutumikia nchini Komoro. Aidha, Mhe. Balozi alieleza furaha yake kwa mapokezi mazuri aliyopatiwa tangu kuwasili kwake Visiwani  Komoro ambapo aliongezea kwa kueleza kuwa anajisikia yupo nyumbani. 
Alieleza kuwa anatambua kazi kubwa iliyopo mbele yake na kuahidi kuwa katika kipindi chake wakati akiwa Balozi nchini hapa atajitahidi kukuza mahusiano yaliyopo baina ya Tanzania na Komoro. Sambamba na hilo, Mhe. Balozi alieleza dhamira yake ya kutaka kuona mahusiano baina ya nchi hizi mbili yanakuwa na manufaa kwa pande zote halikadhalika kukua kwa uhusiano wa kindugu kwani mahusiano baina ya Tanzania na Komoro ni ya kihistoria. 
 Akijibu risala hiyo, Mhe. Azali Assoumani, Rais wa Muungano wa Visiwa vya Komoro naye alianza kwa kuonyesha furaha yake ya kuwasili kwa Balozi pamoja na kukiri kupokea barua ya kurejea Balozi aliyepita na kuwasili kwa Balozi wa sasa. Alieleza kuwa kila Mkomoro hujisikia nyumbani pindi anapo tembelea Tanzania kutokana na ukarimu wanao onyeshwa wanapokuwa huko. Aidha Mhe. Rais alimuhakikishia Mhe. Balozi kuwa atarajie kupata ushirikiano wake pamoja na wa Serikali yake katika kipindi chote atakapo kuwa hapa. 
Mhe. Balozi Mabumba alichukua fursa hiyo pia ya kumuomba Mhe. Rais Azali afanye ziara ya kikazi nchini Tanzania ili kuweza kudumisha mahusiano yaliyopo baina ya nchi hizo mbili. 

 Balozi wa Tanzania ndani ya Muungano wa Visiwa vya Komoro, Mhe. Sylvester M. Mabumba akiwasili kwenye Ikulu ya Komoro ijulikanayo kama  Beit tayari kwa kukabidhi hati zake za uwakilishi  kwa Mhe. Azali Assoumani, Rais wa Muungano wa Visiwa vya Komoro.
 Balozi wa Tanzania ndani ya Muungano wa Visiwa vya Komoro, Mhe. Sylvester M. Mabumba akisoma risala yake kwenye Ikulu ya Komoro ijulikanayo kama  Beit kabla ya kukabidhi hati zake za uwakilishi  kwa Mhe. Azali Assoumani, Rais wa Muungano wa Visiwa vya Komoro.
 Balozi wa Tanzania ndani ya Muungano wa Visiwa vya Komoro, Mhe. Sylvester M. Mabumba akikabidhi hati zake za uwakilishi  kwa Mhe. Azali Assoumani, Rais wa Muungano wa Visiwa vya Komoro kwenye Ikulu ya nchi hiyo. 

MWALIMU COMMERCIAL BANK PLC (MCB), YAZINDUA KAMPENI YA WEKA AKIBA NA USHINDE, WATEJA KUONDOKA NA IPADS

$
0
0
MWALIMU Commercial Bank PLC imezindua kampeni ya “Weka Akiba na Ushinde” kwa Wateja wake na wananchi kwa ujumla.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mei 18, 2017 wakati akizindua kampeni hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank PLC, Bw. Ronald Manongi alisema, “Draw hiyo ipo wazi kwa wateja wote waliopo na watakaojiunga na sifa kubwa ya kuingia kwenye draw hiyo ni kwa mteja aliyepo au anayejiunga, kuweka akiba ya Shilingi 50, 000 au zaidi.” Alisema Bw. Manongi.

Akifafanua zaidi Afisa huyo Mtendaji Mkuu wa benki hiyo alisema, kampeni hiyo ambayo itawawezesha wateja kupata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali kila mwezi kwa kipindi cha miezi miwili.“Mteja anapoweka akiba (fedha), kiasi cha Shilingi 50,000 au zaidi, atapata alama, (Point) moja itakayomuwezesha kushiriki kwenye draw.” Alisema.

Alisema, kadiri Mteja anapoweka akiba zaidi ndivyo Anavyojiwekea nafasi nzuri ya kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo IPADS na vocha za manunuzi zenye thamani ya Shilingi 100,000 na kwamba kila itakapochezeshwa draw hiyo, washindi wanane (4) na kujishindia zawadi mbalimbali.

Akielezea hudma za benki hiyo, Bw.Manongi alifafanua kuwa Mwalimu Commercial Bank inatoa gharama nafuu na rafiki za kibenki na ni suluhisho la kifedha kwa walimu, watumishi wa serikali na wananchi kwa ujumla na kutoa wito kwa Wateja wapya kuja kufungua Akaunti na kuweka akiba ili wapate nafasi ya kuingia kwenye draw hiyo.

Naye Mkuu wa kitengo cha Biashara na Masoko wa Benki hiyo, Bw. Valence Luteganya alisema, “Huduma za kibenki za MCB ni bora na nafuu, tunawahakikishia wateja wetu waje kufanya maamuzi ya kifedha yaliyo sahihi kwani tunatoa huduma mbalimbali za kibenki zilizo nafuu.” Alisema na kuongeza kuwa MCB pia inatoa huduma za ATM zilizounganishwa na mtandao wa Umoja switch ambao una ATM zaidi ya 200 nchi nzima.

“Lakini si hivyo tu pia huduma bora za kibenki kupitia simu za mkononi (Mobile Banking), huduma ya bure ya ujumbe wa SMS ukiwa na usalama na kuwawezesha wateja kupata taarifa za mara kwa mara kuhusiana na Akaunti zao. Hivyo natoa wito kwa wananchi kwa ujumla kuja na kujiunga na Benki yetu kwa huduma bora na za uhakika.” Alisema. 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank PLC, Bw. Ronald Manongi, (katikati), akiwa na Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko, Bw. Valence Luteganya, (kulia) na Meneja Masoko, Bi. Rahma Ngassa, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mei 18, 2017.
Mkuu wa kitengo cha Biashara na Masoko wa Benki hiyo, Bw. Valence Luteganya, akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari,mapema leo jijini Dar kuhusiana na kampeni yao wanayotarajia kuianza hivi karibuni.

Waandishi wa habari wakisikiliza maeleoza mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank PLC, Bw. Ronald Manongi kuhusiana na namna kampeni hivyo itakavyofanyika.

Meneja Masoko wa benki hiyo, Bi. Rahma Ngassa,(kushoto), akizungumzia ubora wa huduma za kibenki kwenye benki hiyo na namna wanavyoweza kutoa huduma ya ushauri mbalimbali kwa wateja wao,Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa MCB, Bw. Manongi.
 
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live




Latest Images