Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1692 | 1693 | (Page 1694) | 1695 | 1696 | .... | 3278 | newer

  0 0


  0 0
  0 0  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  KAMPUNI ya michezo ya kubahatisha ya Nchini Kenya SportPesa imeimgia mkataba na klabu ya Yanga wa udhamini wa miaka mitano ukiwa na thamani ya takribani bilioni 5.

  Uwekaji huo wa saini umefanyika leo katika makao makuu ya Klabu ya Yanga ukishuhudiwa na wanachama mbalimbali wakiongozwa na viongozi wa Kamati ya Utendaji akiwemo Makamu Mwenyekiti Clement Sanga.

  Akizungumza baada ya kutia saini hati ya makubaliano ya mkataba huo, Makamu Mwenyekiti wa Yanga Sanga amesema kuwa mkataba huu utakuwa na faida kubwa sana kwa klabu kwani wameweza kuongelea mambo mbalimbali ya kimaendeleo yakiwemo soka la Vijana.

  Sanga amesema ni mara ya kwanza katika mikataba waliyowahi kuingia akiwa kama kiongozi umekuwa na viyi vingi sana vya kimaendeleo ukiachilia fedha wanazozipata za udhamini.

  "katika mikataba tuliyowahi kuingia nikiwa kiongozi wa Yanga huu ni moja ya mkataba tuliozungumzia maendeleo ya klabu mbali na fedha tunazozipata ila tumeangalia katika Uwanja wetu wa Kaunda na hata soka la Vijana na mambo mengine mengi,"amesema Sanga.

  Mkurugenzi wa mawasiliano wa SportPesa nchini Tanzania Tarimba Abbas amesema Yanga watapata zaidi ya bilion 5 kwa miaka mitano na kwa mwaka wa kwanza wataanza kwa kupata milion 950 na itaongezeka kwa asilimia 5 kila mwaka na hii inakuwa klabu ya pili kuweza kuingia nao mkataba baada ya Simba kusaini wiki iliyopita.

  Tarimba amesema makubaliano yao na Yanga yapo ambayo hayajawekwa wazi ni ya ndani ya klabu na si vizuri kuyasema ila kuhusu bonus zitakuwa sawa ambapo timu ikichukua ubingwa wa ligi au kagame au michuano yoyote ya kimataifa kutakuwa na fedha watakazopatiwa nje ya fedha ya udhamini.

  Klabu Yanga inatarajiwa kufaidika na udhamini hasa kwa makubaliano waliyoingia ya kukarabatiwa uwanja wa mazoezi, kukuza vipaji vya soka la vijana pamoja na kupatiwa gari la wachezaji.
  Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya SportPesa Pavel Slavkov akikabidhiana hati ya makubaliano ya mkataba na Mkamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement Sanga ukiwa ni mkataba wa miaka kitano wenye thamani ya zaidi bilioni 5, uwekaji huo wa saini na makabidhiano yamefanyika leo Makao Makuu ya klabu hiyo Jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa mawasiliano wa SportPesa nchini Tanzania Tarimba Abbas na kushoto ni Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga Charles Mkwasa.
  Makamu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uwekaji saini wa hati ya makubaliano ya mkataba wa udhamini baina ya Klabu ya Yanga na Kampuni ya Michezo ya kubahatisha ya SportPesa ya nchini Kenya, uwekaji huo umefanyika leo Makao Makuu ya klabu hiyo Jijini Dar es salaam.


  0 0


  0 0

  NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

  WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Walemavu Jenister Mhagama, anatarajiwa kufungua mkutano wa Bodi za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania.

  Mkutano huo unaoratibiwa na Jumuiya ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania (TSSA) utafanyika Arusha Mei 19 na 20 mwaka huu,utahusu hatua iliyofikiwa mwaka huu na mada kuu, itakuwa uchumi wa viwana kama fursa ya uwekezaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii nchini.

  Pia utaangalia hatua iliyofikiwa ya ushiriki wa mifuko hiyo kwenye uwekezaji wa viwanda na uchumi wa viwanda wenye tija.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza jana, Katibu Mkuu wa TSSA Meshack Bandawe alisema mkutano huo utakaofunguliwa na Waziri Mhagama, utashirikisha bodi nane za mifuko pamoja na wakuu wa mifuko hiyo ya hifadhi.

  Alisema kwenye mkutano huo Bodi, Wakuu wa mifuko hiyo pamoja na wadau watapata fursa ya kujadili mafanikio , hatua na maendeleo yaliyofikiwa kwenye uwekezaji wa uchumi wa viwanda nchini.

  “ Kwenye mkutano huo tutaangalia mafanikio na hatua iliyofikiwa katika uwekezaji wa viwanda kama fursa muhimu hapa nchini ili uwekezaji wetu uwe na tija ambao utasaidia kukuza uchumi wa nchi na mifuko yenyewe ,”alisema Bandawe.

  Katibu Mkuu huyo wa TSSA alisema kuwa mifuko hiyo imeanza utekelezaji kwwa kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ya viwanda na baadhi iko kwenye upembuzi yakinifu.Alidai kuwa miradi hiyo ikikamilika itatengeneza ajira kwa vijana wa Tanzania ambao watakuwa wananchama wa mifuko yenyewe na hivyo kuwa na tija katika taifa kwa ujumla.

  Kwa mujibu wa Bandawe nia ya mkutano huo ni kufikia lengo la uwekezaji wa viwanda na utahudhuriwa na Msimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA), Benki Kuu (BOT),Wizara ya Viwanda na Biashara, Tume ya Mipango, Msajili wa Hazina na wadau wengine.

  Bandawe alieleza kuwa TSSA inaundwa na mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo ni NSSF, PPF,LAPF,PSPF, GEPF,NHIF,WCF na ZSSF.

  0 0

  Mwenyekiti wa bodi ya Utalii nchini, Jaji Thomas Mihayo akiwakaribisha Wasnaii hao katika Hotel ya Ramada Incore jijini Dar es Salaam
   Mwenyekiti wa bodi ya Utalii nchini, Jaji Thomas Mihayo  akikabidhi zwadi ya Tisheti kwa wageni hao ambao wamekuja kutalii nchini
  Mwenyekiti wa bodi ya Utalii nchini, Jaji Thomas Mihayo akiwa katika picha ya pamoja na wasnii kutoka nchini china

   Wasanii Maharu saba kutoka nchini China ,Lu Yi, Du Haitao,Yao Di,Tian Liang,Yin Zheng,Mai Dina na Hao Shaowen wakicheza ngoma kwa pamoja na kikundi cha Sanaa za utamaduni hapa nchini cha Wanne Star
  --
   Wasanii Maharu saba kutoka nchini China ,Lu Yi, Du Haitao,Yao Di,Tian Liang,Yin Zheng,Mai Dina na Hao Shaowen, wakishuka kwenye gari ndani ya uwanja wa ndege wa kimataifa Jijini Dar es Salaam wakitokea nchini  China  kwa ajili ya kutembelea mbuga za Wanyama hapa nchini na Vivutio vya kitalii.  0 0

  Na Nuru Juma-MAELEZO

  Serikali inamkakati wa kuhakikisha inajenga Magereza katika maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa kilimo ambayo pia yana ukubwa wa kutosha ili kazi ya kuwarekebisha wafungwa iwe rahisi kufanyika huku shughuli za uzalishaji zikiwa zinaendelea.

  Hayo yamesemwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. Mwigulu Nchemba alipokuwa akijibu swali la Mhe Devotha Minja Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro. 

  “Magereza hayo yatajengwa katika maeneo yenye Kilimo na yatakuwa ni kwa ajili ya watu waliokwisha hukumiwa huku yale Magereza ya mijini yawe kwa ajili ya mahabusu tu ili wawe karibu na Mahakama,”alisema Mwigulu. 

  Aliongeza kuwa mkakati huo wa Serikali ni wa muda mrefu na wanahitaji kufanya hivyo ili kurahisisha shughuli za maendeleo zinazofanywa na wafungwa na pia kupunguza msongamano wa wafungwa katika Magereza.

  Hili pia linatokana na tamko la Mh.Rais Dkt John Pombe Magufuli alilowahi kulitoa hivi karibuni kuwa wafungwa wako katika kutumikia adhabu hivyo wanatakiwa kufanya kazi hasa za kilimo ili kwanza kujipatia chakula na sio kukaa tu bure na kusubiri kila kitu wafanyiwe na serikali.


  0 0


  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  Uchangiaji wa damu salama unahitajika kutokana na kuwa na wahitaji wengi ambao wanatakiwa kuwekewa katika kuokoa maisha yao.
  Hayo ameyasema Afisa Uhamasishaji wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama Kanda ya Mashariki , Fatuma Mjungu wakati uchangiaji wa damu katika kiwanda cha Lake Cement kilichopo Kimbiji Manispaa Kigamboni jijini Dar es Salaam , amesema kuwa kwa mwaka jana walikusanya damu chupa 160,000 lakini malengo yake ni ukusanyaji wa chupa 300,000.
  Fatuma amesema kutokana na mikakati waliojiwekea kwa mwaka huu watafikia lengo la kukusanya damu chupa 300,000 kwa kuhamasisha wananchi kuchangia damu.

  Amesema Lake Cement wamekuwa wakijitoa katika katika suala la uchangiaji damu na kutaka viwanda vingine kujitokeza katika kufanya uchangiaji damu popote pale watawafikia.

  Afisa Rasilimali wa Watu wa Lake Cement, Ahmed Nyang’anyi amesema kuwa wanatambua umuhimu wa damu katika kuokoa maisha kwa watu wanaohitaji kwa akina mama wakati wa uzazi na makundi mbalimbali .
  Nyang’anyi amesema kuwa wataendelea kuchangia damu kila mwaka kutokana na mahitaji yake kwa wahitaji ni wengi ikilinganishwa na damu iinayokusanywa.

  Meneja wa Afya, Mazingira Mahala Pakazi, Happy Mboma amesema hakuna kiwanda kinachozalisha damu hivyo kila mtu anawajibu wa kuchangia damu katika kuokoa maisha wahitaji wa damu.Amesema kuwa wanaochangia damu nao ni wahitaji damu hiyo kwa sababu hakuna mtu ambaye anajua atapata uhitaji damu wakati gani.
  Makamu wa Rais wa Kiwanda Lake Cement, Afroz Ansari akizungumza na waandishi wa habari wakati uchangiaji damu katika kiwanda hicho leo jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Kiwanda Lake Cement, Afroz Ansari akiwa katika uchangiaji damu.
  Afisa Uhamasishaji wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama Kanda ya Mashariki , Fatuma Mjungu akizungumza wakati uchangiaji damu wa kiwanda cha Lake Cement juu ya uhitaji damu katika kuokoa maisha.
  Afisa Rasilimali wa Watu wa Lake Cement, Ahmed Nyang’anyi akizungumza wakati wa uchangiaji damu wa kiwanda hicho leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Na: Frank Shija – MAELEZO 

  WADAU mbalimbali wameipongeza Serikali kwa uamuzi wa kuivunja Mamlaka ya Ustawishaji wa Makao Makuu Dodoma (CDA) iliyofikiwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli. 

  Wakitoa maoni yao juu ya umauzi huo wa Serikali, wameeleza kuwa kuvunjwa kwa Mamlaka hiyo kumekuja wakati muafaka kwani kutapunguza kero na migogoro ya ardhi iliyokuwa ikiendelea katika Manispaa ya Dodoma. 

  Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maalum iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana,iliyokuwa inashughulikia changamoto za wananchi dhidi ya CDA, Bw. Aron Kinunda alisema kuwa uamuzi huo huko sahihi kwani umekuja wakati muafaka kwa kuzingatia malengo halisi ya uanzishaji wa mamlaka hiyo kuwa yamekamilika kwa asilimia kubwa ukizingatia na mahitaji halisi ya wakati huu. 

  “Ni hatua nzuri katika mustakabari wa maendeleo ya Dodoma, kwani sasa migogoro mingi ya ardhi iliyokuwa inatokana na mgongano wa kisheria haitarajiw kujitokeza tena na badala yake Manispaa itajikita katika kuweka mazingira rafiki ya umiliki wa ardhi ikiwemo kuongeza muda wa hati ya umiliki kutoka miaka 33 hadi 99 kama ambavyo maeneo mengine ya nchi yanavyofanya.” Alisema Kinunda. 

  Aliongeza kuwa wananchi watakuwa wamefarijika sana kwani walikuwa wanaiona CDA kama adui yao mkubwa ambapo imesababisha malalamiko mengi ya kuchukuliwa ardhi zao bila ya kulipwa fidia na urasimu katika upimaji na utoaji wa hati za viwanja. 


  0 0


  Na Nuru Juma,MAELEZO,DAR ES SALAAM

  SERIKALI kupitia mradi wa awamu ya 3 ya usambazaji wa umeme vijijini (REA) imekusudia kusambaza umeme katika vijiji, vitongoji vyote, taasisi za umma na maeneo ya pembezoni mwa nchi ikiwemo visiwa.

  Hayo yamesemwa leo bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani alipokua akijibu swali la Mbunge wa Bukoba Mjini (CHADEMA) Wilfred Rwakatale.

  Dkt. Kalemani amesema kupitia mradi wa REA, Serikali inatarajia kukamilisha usambazaji umeme vijijini mwaka 2020 hadi 2021, na Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) inaendelea kusambaza umeme maeneo yote ya mjini ambayo hayajapata nishati ya umeme.

  “Baadhi ya vijiji ambavyo vipo ndani ya mamlaka za miji vinapelekewa umeme na shirika la Tanesco na bei ya Tanesco na REA ni tofauti kwani kwa mteja wa awali wa Tanesco hulipia 177,000 na REA hulipia 27,000””, alisema Mhe.kalemani.

  Kwa mujibu wa Kalemani amesema Serikali bado inaendelea kujiridhisha na kuangalia ni vijiji gani vinastahili kupelekewa umeme kwa mradi wa REA ili kuhakikisha kuwa malengo ya mradi yanaweza kufikiwa katika muda uliopngwa.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) imekusanya shilingi bilioni 63,015,450,230 kwa kipindi cha Octoba 2013 mpaka Februari 2017 tangu kuanzishwa kwa mtambo wa kuhakiki na kusimamia Huduma za Mawasiliano(TTMS) nchini.
  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Edwin Ngonyani wakati akijibu swali la Mbunge wa Kigamboni.
  “Mtambo huu umesaidia Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) kuongeza ufanisi katika kusimamia Sekta ya Mawasiliano pamoja na kwenda sambamba na kasi ya mabadiliko yanayotokea katika Sekta ya Mawasiliano Duniani kote,”aliongeza Ngonyani
  “Kuanzia Oktoba 2013 hadi Februari 2017, kiasi cha shilingi 63,015,450,230 zilipatika na katika hizo bilioni 56,987,368,631 zimewasilishwa hazina na shilingi bilioni 6,028,081,599 zimewasilishwa Tume ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH) kwa ajili ya kugharamia tafiti mbalimbali zenye manufaa kwa nchi yetu ambapo kabla ya mfumo huu mapato hayo hayakuwepo.”
  “Aidha pamoja na mafanikio hayo jitihada za kuboresha zaidi mfumo huu ili kuweza kubaini na kujiridhisha juu ya mapato yote yatokanayo na huduma za mawasiliano na yanayokidhi mahitaji ya Mamlaka ya Mapato Tanzania,Benki kuu ya Tanzania na TCRA zinaendelea,” aliongeza Naibu waziri Ngonyani.

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Aziz P. Mlima akizungumza kwenye kikao cha Wataalamu ngazi ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.  Mkutano huu ni maandalizi ya Mkutano wa 34 wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki unaotarajiwa kufanyika tarehe 18 Mei, 2017 Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam. 
  Mkurugenzi wa Siasa, Ulinzi na Usalama Bw. Stephene Mbundi akisisitiza wakati wa Mkutano wa ngazi ya Wataalam kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam
  Sehemu ya wajumbe wakifuatilia mkutano
  Katibu Mkuu Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Liberat Mfumukeko akifuatilia Mkutano.

  0 0

  Mtayarishaji wa muziki nchini,  Sheddy Clever ameitaka serikali iweke sheria na viwango vya kudhibiti watayarishaji wa muziki feki ambao ni chanzo cha kusababisha nyimbo kutodumu mda mrefu katika tasnia hali inayopelekea kushuka kwa muziki bongo.

  Sheddy amedai serikali inapaswa pia kusimama na kuangalia maslahi ya watayarishaji wa muziki kwani wamekuwa wakiwatajirisha wasanii huku wao wakibaki kwenye maisha yale yale.
  “Maprodyuza feki ni wengi sana wale waliopo real ni wachache sana. Zamani kina P -Funk walikuwa wanatengeneza nyimbo zinadumu muda mrefu na ni kali lakini za sasa hivi imebidi ma director wa video wawe wabunifu kutengeneza video kali ili wimbo uonekane ni mzuri,” amesema Sheddy 
  Ameongeza kuwa  kwa upande wa maslahi inabidi serikali ijipange ituwekee maslahi mazuri kwani mtayarishaji wa muziki kama anahitaji maisha mazuri itambidi awe ana kazi nyingine na siyo kutegemea production tu. Unaweza ukawa na hit kibao redioni lakini maisha yako yakawa ya tabu sana,”
  Mtayarishaji huyo mwenye uwezo wa hali ya juu  ameshatengeneza hit nyingi  za msani maharufu nchini Naseeb Abdul "DIAMOND "ikiwemo ‘Marry You’ ya Diamond na Ne-Yo.

     0 0

   Ubalozi wa Marekani imeingia rasmi katika ubia na Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar kwa kusaini Hati ya Makubaliano  (MOU) ya kuwa na programu ya mabadilishano ya kitamaduni ya wiki moja itakayohusisha kuwaleta nchini Tanzania Mwongozaji wa Filamu wa Kimarekani Judd Ehrlich na mtaalamu wa filamu Debra Zimmerman kutoka tarehe 9 hadi16 Julai, 2017.  Hati hiyo ya Makubaliano ilisainiwa na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Virginia Blaser na Mkurugenzi wa  ZIFF Fabrizio Colombo.  
  Judd Ehrlich ni muongozaji wa filamu ya maisha na matukio halisia (documentary) iitwayo  Keepers of the Game, ambayo inaangazia jitihada za timu ya wasichana kutoka makabila ya asili ya Marekani ikitafuta kushinda ubingwa wa mkoa wa mchezo uitwao  lacrosse, ambao kitamaduni ulikuwa ni mchezo wa wanaume na wavulana tu.  Debra Zimmerman ni mtaalamu wa filamu na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi iitwayo Women Make Movies (Wanawake Watengeneza Filamu) ambayo imedhamiria kuongeza uwezo na fursa kwa wanawake wanaohusika katika utengenezaji wa filamu.


  Kupitia ubia na ZIFF, Ehrlich na  Zimmerman watafanya kazi moja kwa moja na watengeneza filamu wa Kizanzibari wanaochipukia wakati wa tamasha la 20 la filamu la Zanzibar. Wataendesha warsha kadhaa kuhusu utengenezaji wa filamu za maisha na matukio halisia na utafutaji masoko na usambazaji wa filamu pamoja na kuendesha warsha mahsusi kuhusu ushiriki wa wanawake katika tasnia ya filamu.  
  Akizungumza katika hafla fupi ya kusaini Hati ya Makubaliano, Kaimu Balozi Blaser alisema “tunafuraha kuimarisha msaada wetu kwa watu wa Zanzibar kupitia programu hii ya mabadilishano ya kitamaduni.  Kwa pamoja tutatoa fursa kwa watengeneza filamu wa Kimarekani na Kizanzibari kutumia sanaa hii kama nyezo ya kushughulikia masuala mbalimbali yanayogusa jamii zao.”

   Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Virginia Blaser na Mkurugenzi wa  ZIFF Fabrizio wakitia sahihi hati hiyo ya Makubaliano  (MOU) ya kuwa na programu ya mabadilishano ya kitamaduni ya wiki moja itakayohusisha kuwaleta nchini Tanzania Mwongozaji wa Filamu wa Kimarekani Judd Ehrlich na mtaalamu wa filamu Debra Zimmerman kutoka tarehe 9 hadi16 Julai, 2017.
   Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Virginia Blaser na Mkurugenzi wa  ZIFF Fabrizio wakibadilishana hati baada ya kutia hati hiyo ya Makubaliano  (MOU)
  Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Virginia Blaser na Mkurugenzi wa  ZIFF Fabrizio wakiongea na wanahabari baada ya kutia sahihi hati hiyo ya Makubaliano  (MOU).


  0 0


  Msanii Dogo Mfaume amefariki dunia katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa anapata matibabu kwa kusumbuliwa na uvimbe kichwani. Kibao hiki cha "KAZI YANGU YA DUKANI" kilimpatia tuzo ya mwaka 2008. Globu ya Jamii inatoa rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kwa kumpoteza msanii huyo hodari. Mola aiweke roho yake mahali pema peponi - Amin

  0 0

  Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (wa pili kushoto) akimsikiliza Afisa kutoka Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) akizungumza jambowakati wa Maonyesho ya baadhi ya Mitambo yao, katika tukio lililofanyika leo katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma. wa pili kulia, ni Waziri wa Viwanda, Biashara  na Uwekezaji, Mheshimiwa Charles Mwijage. PICHA NA OFISI YA BUNGE.    

  0 0

  Mchezaji nyota wa Mchezo wa Tenisi wa nchini Urusi, Maria Sharapova, amenyimwa kadi maalumu ya kuingia kwenye mashindano ya wazi ya Ufaransa maarufu kama ‘French Open’ yanayotarajiwa kuanza katikati ya Mwezi huu.
  Mkuu wa shirikisho wa mchezo wa Tensis nchini Ufaransa, Bernard Giudicelli Ferrandini, alikanusha zaidi ya mara mbili kuwa mchezaji huyo hatoweza kushiriki mashindano hayo na kusema.
  “Mwaliko huo ungeliweza kutolewa kwa mchezaji ambaye ametoka kuwa majeruhi lakini sio kwa aliyefungiwa kwa kashfa ya matumizi ya dawa za kusisimua misuli”
  “Samahani sana Maria, samahani na kwa mashabiki zake”.
  “Pengine nitakuwa nimewaangusha, pengine pia nitakuwa nimemkwaza , lakini ni jukumu langu, wajibu wangu,kuhakikisha ninalinda viwango vya wachezaji katika michezo pasipo shaka yoyote kwamba pengine ametumia madawa ama la kutokana na matokeo.”
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, na mshindi mara tano wa Grand Slam , aligundulika kutumua madawa yaliyopigwa marufuku michezoni mwaka 2016 katika mashindano ya wazi ya Australia.

  0 0

  RC Shigela alipotembelea Kampuni inayojenga mradi mkubwa wa kiwanda cha Saruji Tanga. Kiwanda hicho muhimu kwa uchumi wa Tanzania kitazalisha zaidi ya Tani milioni 7 za Saruji kwa Mwaka.
  Alionana na Mwenyekiti wa Kampuni hiyo pamoja na Viongozi wa Mji wa Yangzhou ambao kwa upande wao walikubaliana kuanzisha ushirikiano wa Maendeleo baina ya Miji hiyo miwili (Sister Cities).
  Tanga tujiandae kwa uwekezaji huu mkubwa na wa mfano!
   Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigela (kati) akiwa nchini China akikagua mitambo na mashine zilizofungwa tayari kwa kusafirishwa kupelekwa mkoa Tanga kwa ajili ya uwekezaji wa kiwanda cha Cement kitakachogharimu Dola za  Kimarekani 1.4 bilion kitakachozalisha tani milioni saba na kuajiri watanzania 4000.  Ujenzi wa kianda hicho unatarajiwa kuanza mwezi ujao. Kushoto ni Ndg. Suleiman Serela, Mtanzania aliye masomoni nchini China akichukua PhD ya Sheria
   Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigela (kati) akiwa na wenyeji wake nchini China akikagua mitambo na mashine zilizofungwa tayari kwa kusafirishwa kupelekwa mkoa Tanga kwa ajili ya uwekezaji wa kiwanda cha Cement 
   Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigela na  Ndg. Suleiman Serela wakiwa nchini China wakioneshwa mfano wa kiwanda cha cement kitachojengwa mkoani Tanga 
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigela (kati) akiwa na mwenyeji wake nchini China akiendelea kukagua mitambo na mashine zilizofungwa tayari kwa kusafirishwa kupelekwa mkoa Tanga kwa ajili ya uwekezaji wa kiwanda cha Cement 

  0 0


  0 0

  Umoja wa watanzania Ujerumani UTU e.V watingisha jiji la Essen nchini Ujerumani baada ya kufanya mkutano mkuu kwa mujibu wa katiba  ulioandamana na sherehe za ushindi wa viongozi wapya. 
  Hapo jijini Essen katika ukumbi wa Bob's Cafe, watanzania zaidi ya 75 ambao wanaishi nchini humo walihudhuria mkutano huo ili kutimiza haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wao, katika safu ya uongozi mpya Mhe Mfundo Peter Mfundo alichaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa umoja huo baada ya kukosa mpinzani. 
  Makamo mwenyekiti mpya ni Mhe Salim Malumbo Jr. Katibu mkuu ni Julieth Myn, muweka Hazina ni Bi Nashe Mvungi, Mkaguzi wa mahesabu  namba 1 ni Mhe Bi Jovither Mushashu, Mkaguzi wa mahesabu namba 2 ni mhe Bi. Lilian Sorogo. Mjumbe namba Moja ni  Mhe Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja na Mjumbe namba 2 ni Mhe Vanessa Lymo. pamoja na mengi yalioongelewa kwenye mkutano huo azma ya  umoja wa watanzania Ujerumani UTU e.V ni kuwaendeleza watanzaniawanaoishi hapa ujerumani na hata kuwaletea maendeleo watanzania wanaoisho Tanzania, umoja ni Nguvu na utengano ni Udhaifu
     akishukuru baada ya kuchaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa umoja huo baada ya kukosa mpinzani
   Wajumbe wa Umoja wa Watanzania Ujerumani UTU e.V wakikata keki na mwenyekiti Mhe Mfundo Peter Mfundo
   Wajumbe wa Umoja wa Watanzania Ujerumani UTU e.V wakikata keki
   Wajumbe wa Umoja wa Watanzania Ujerumani UTU e.V wakikata keki
   Wajumbe wa Umoja wa Watanzania Ujerumani UTU e.V wakifurahi na mwenyekiti Mhe Mfundo Peter Mfundo

older | 1 | .... | 1692 | 1693 | (Page 1694) | 1695 | 1696 | .... | 3278 | newer