Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110104 articles
Browse latest View live

CCM ZANZIBAR YAAHIDI KUENZI USHIRIKIANO NA CHAMA CHA CPC CHA CHINA

$
0
0
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Saadala akizungumza na Balozi mdogo wa China Zanzibar Bw. Xie Xiaowu juu ya masuala mbali mbali ya kimaendeleo huko  Afisi Kuu Zanzibar.

 Balozi mdogo wa China Zanzibar Bw. Xie Xiaowu akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Saadala  juu ya mahusiano ya CPC na CCM huko Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Saadala akitoa ufafanuzi kwa Balozi mdogo wa China Zanzibar Bw. Xie Xiaowu juu ya  michoro na picha za waasisi mbali mbali wa vyama vya ukombozi duniani zilizopo katika chumba cha historia alichofariki Mwasisi Mzee Abeid Amani Karume Kisiwandui Zanzibar. 

Introducing "UTANIUMIZA" by Amor

MATUKIO KATIKA PICHA: YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 26, MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO MAY 16, 2017.

$
0
0
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Dkt Hussein Mwinyi akisoma hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake katika  kikao cha Ishirini na Sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 16, 2017. Bajeti ya wizara hiyo imepitishwa jioni hii.

 Viongozi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa na wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt.Florens Turuka na Naibu Katibu Mkuu Imaculate Ngwalle,Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo,Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali James Mwakibolwa na Meja Jenerali Michael Isamuhyo wa JKT wakiwa katika kikao cha Ishirini na Sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei.
 Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali James Mwakibolwa akizungumza jambo na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Michael Isamuhyo katika viwanja vya Bunge leo Mjini Dodoma.
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali James Mwakibolwa wakizungumza jambo na Viongozi mbalimbali wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama leo katika viwanja vya Bunge leo Mjini Dodoma.

TRADEMARK EAST AFRICA YAIWEZESHA ZANZIBAR KUTUMIA MBINU ZA KISASA

TIB CORPORATE BANK LIMITED YAINGIA UBIA NA MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA (TRA)

$
0
0
Benki ya TIB Corporate imeingia ubia na TRA kwa kuunganisha mifumo yao ya malipo ili kuwezesha kulipa kodi kwa urahisi.
TAXBANK Ni mfumo wa kisasa wa ukusanyaji wa kodi ambao umerahisisha ulipaji  wa kodi kwa wateja wetu. Kwa kupitia utaratibu huu Bank imeunganisha mfumo wake wa malipo moja kwa moja na mfumo wa TRA, hivyo mlipa kodi akilipia katika tawi lolote la bank, taarifa zake zinaonekana mara moja katika mtandao wa TRA hivyo kumuwezesha mlipa kodi kuendelea na taratibu zingine kwa haraka na  kiurahisi zaidi. 
TIB Corporate Bank Ltd (TIB CBL) ni benki ya  biashara inayomilikiwa na Serikali kwa 100%. Benki inatoa huduma zote za kibenki za kibishara kwa  mashirika na taasisi za aina mbalimbali za serikali na  binafsi , pia benki inatoa huduma kwa watu binafsi.

Benki ina matawi  6 kwa sasa,  Dar es salaam (3), Mwanza , Arusha na Mbeya. 
Benki inatoa huduma mbalimbali  kutokana na mahitaji ya mteja. Baadhi ya  huduma hizo ni pamoja na; akaunti za aina mbalimbali kwa makampuni na watu binafsi, mikopo ya aina mbali mbali ya muda mfupi na wa kati, Dhamana za Kibenki(Guarantees),Uuzaji na ununuaji wa fedha za kigeni, ushauri wa uwezekaji katika hati fungani,ukusanyaji wa fedha na kuwezesha malipo ya jumla kwa makampuni pamoja na ulipaji wa mishahara kwa njia rahisi na ya haraka

Huduma zote hizi hutolewa kwa umahiri na ufanisi mkubwa ili kuhakikisha mteja anafurahia mahusiano yake na benki. 
Benki imejiunga na mfumo  huu wa ulipaji kodi, ili kusaidia kufanikisha malengo ya serikali katika kuongeza ufanisi katika kukusanya kodi. Kwa kupitia mfumo huu mlipa kodi anapata huduma bora zaidi pamoja na faida zifuatazo:

·         - Kumrahisishia mlipa kodi  kufanya muamala wa kulipa kodi kwa haraka na ufanisi.

·         - Kupunguza uwezano wa makosa katika ulipaji wa kodi

·         - Kupunguza ghrama za uendeshaji na miamala.
TIB Corporate ndio yenye dhamana ya kusimamia sehemu kubwa ya  akaunti za mamlaka ya Bandari-TPA. Tayari tunalo tawi dogo ndani ya bandari ili kuhakikisha kuwa tunawezesha ulipaji wa kodi zote na tozo za bandari kwa ukaribu. Kutoa huduma za kibenki kwa masaa 24 sambamba na agizo la raisi wetu Mhe. John Pombe Magufuli kuzitaka taasisi husika katika bandari kutoa huduma kwa masaa 24.
 Mkurugenzi Mkuu wa  TIB Corporate Bank Bw. Frank Nyabundege akizungumza jinsi bank ilivyojipanga kutoa huduma hiyo
Kamishna Jenerali  wa TRA Bw.Charles Kichere akikabidhiana mkataba na mkurugenzi mkuu wa TIB Corporate Bank Bw. Frank Nyabundege. Wakishuhudiwa na mkurugenzi wa huduma na elimu kwa wateja wa TRA Bw. Richard Kayombo na Mkuu wa Kitengo na Masoko na mahusiano ya Kampuni wa TIB Corporate Bi. Theresia Soka
 Wafanyakazi wa TIB Corporate wakifurahia baada ya kusaini mkataba Frank Nyabundege- Mkurugenzi mkuu,  Bi.Theresia Soka – Mkuu wa masoko na mahusiano ya Kampuni, Bi. Bahati Minja- Mkurugenzi wa matawi na huduma kwa wateja, Bw. Mwallu Mwachang’a –Mkurugenzi wa biashara
 Kamishna Jenerali wa TRA Bw. General Charles Kichere akizungumza juu ya mpango huo
Mkurugenzi Mkuu wa  TIB Corporate Bank Bw. Frank Nyabundege akizungumza jinsi bank ilivyojipanga kutoa huduma hiyo

BENKI YA CBA YAZINDUA HUDUMA MPYA YA KUWAFATA WATEJA WAKE WALIPO

$
0
0
Mkurugenzi wa Bank ya biashara Africa CBA Gift Shoko akizungumza hivi karibuni jijini Arusha katika hafla ya uzinduzi wa  huduma ya kuwahudumia wateja kibinafsi (private banking) kwa kuwafuata wateja wake walipo tofauti na mfumo uliozoeleka wa wateja kufuata bank(Habari Picha na Pamela Mollel blog)
 Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi CBA N.Kitomari akizungumza katika uzinduzi huo hivi karibuni jijini Arusha katika hafla ya uzinduzi wa huduma mpya kwa wateja binafsi (private banking) kwa kuwafuata wateja wake walipo tofauti na mfumo uliozoeleka wa wateja kufuata benki.
Julius Konyani Mkuu wa kitengo cha wateja binafsi akimkabidhi zawadi moja ya wateja wa benki hiyo katika uzinduzi wa huduma mpya  ya kuwahudumia wateja kibinafsi (private banking) kwa kuwafuata wateja wake walipo tofauti na mfumo uliozoeleka wa wateja kufuata bank.


BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 16.05.2017

Article 1


MAGAZETI YA LEO JUMATANO MAY 17, 2017

DAI RISITI

Wakurugenzi wajadili upatikanaji wa maji Morogoro

$
0
0
Usimamizi usiofaa wa miradi mbalimbali ya maji nchini umeelezwa kuwa ni kikwazo kwa juhudi za kuwezesha upatikanaji wa maji kwa kila familia.

Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Maji na Umwagiliaji Injinia Jackson Mutazamba katika semina ya inayofanyika mjini Morogoro ikijuimuisha wakurugenzi kutoka halmashauri zote nchini.

Alisema lengo la semina hiyo ni kuweza kuwahimiza na kuwajengea uelewa zaidi wakurugenzi hawa namna ya kufanya miradi ya maji iweze kuwa na tija na kufanya upatikanaji wa maji kwa wananchi isiwe kikwazo.

"Utawala bora katika usimamizi wa miradi ya maji ni kitu cha msingi sana katika kufanya miradi ya maji iwe endelevu mara baada ya kuanzishwa na kuweza kuwapatia wananchi maji wakati wote wa mwaka," alisema.

Alisema hadi mwezi wa tatu mwaka huu mtandao wa maji ulikuwa umefikia asilimia 72 nchini pote lakini miradi mingine haifanyi kazi kutokana na utawala mbovu hivyo kufanya kuwe na upungufu mkubwa wa maji.

Alisema wakurugenzi wa wilaya ni viungo muhimu sana katika kufanya miradi hii ya maji iwe endelevu ukizingatia kuwa serikali na wadau wa maendeleo wamekuwa karibu sana katika kuhakikisha miradi mingi ya maji inaanzishwa.

Pia wakurugenzi wanaweza kusimamia uanzishwaji wa kamati maalumu za maji ambazo zinasimamiwa moja kwa moja na wananchi wenyewe hivyo kufanya miradi hii iwe endelevu.

Akiwasilisha makadirio ya bajeti kwa mwaka 2017/18 bungeni Dodoma wiki iliyopita, Waziri wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Injinia Gerson Lwenge alisema serikali imejipanga kuanzisha miradi mipya mingi ili kuweza kuongeza mtandao wa maji kufikia asilimia 95.


Mkurugenzi wa halmashauri ya mpanda  Rojas John Lomuli akiahidi kuitikia wito wa kuendeleza usafi wa mazingira ili kuhakikisha halamashauri yake inafikia kiwango cha juu katika utekelezaji wa kampeni ya Nipo Tayari iliyowashirikisha wakurugenzi wa halmashauri nchini kuhusu skimu ya malipo kwa matokeo  inayofanyika mjini morogoro
Mkurugenzi wa halmashauri ya kondoa Khalifa Kondo akionyesha ishara ya kampeni ya Nipo Tayari ya kutekeleza usafi wa mazingira katika mji wake wakati wa semina ya kwa wakurungenzi wa halamashauri nchini kuhusu skimu ya malipo kwa matokeo inayofanyika mjini morogoro.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Ikungi mkoani Singida Rustika Turuka akielezea matarajio yake wakati wa semina ya utekerezaji wa kampeni ya Nipo Tayari iliyowashirikisha wakurugenzi wa halmashauri nchini kuhusu skimu ya malipo kwa matokeo, inayofanyika mjini Morogoro


   

NAIBU KATIBU MKUU CCM BARA ZIARANI JIMBO LA TEMEKE, ASEMA HANUNULIWI KWA 'JERO'

$
0
0

Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rodrick Mpogolo,amesema hakuna mtu anayeweza kukinunua Chama Cha Mapinduzi, kwa kuwa ni Chama kikubwa kilichoanzishwa na waasisi makini.

Amesema waasisi walizingatia misingi ya haki umoja na mshikamano ,wakaondoa dhulma, chuki na ubaguzi wa kila aina hivyo si rahisi mtu kufanya biashara na CCM.

Mpogolo alisema hayo jana alipozungumza na viongozi na wanachama wa CCM katika majimbo ya Temeke na Mbagala jijini Dar es Salaam,ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kuimarisha Chama.

Alisema CCM inaendesha shughuli zake kwa uhuru na itahakikisha uchaguzi wake unafanyika kwa haki pasipo kuingilia na wanachama wenye tabia ya kununua madaraka.

Mpogolo aliwaagiza watendaji wa Chama na jumuiya kusimamia uchaguzi unaendelea kufanyika kwa haki bila kuwashinikiza wanachama kwa kuwa wanawafahamu viongozi wanaowataka.

"Hatutaki vurugu CCM, tunapenda amani,umoja na mshikamano. Wenye ni ya kutumia uchaguzi huu kupanga mitandao yao, wataambulia patupu,watatumia fedha na uongozi hawatapata,"alisema.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Rodrick Mpogolo, akizungumza na wanachama na Viongozi wa CCM Kata ya Mtoni, wakati akiwa katika mfululizo wa ziara zake za kuimarisha Chama, kwa Mkoa wa Dar es Salaam,jana
Baadhi ya Wanachama wa CCM Kata ya Mtoni wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Rodrick Mpogolo.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza kutoa shukrani zake kwa wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala (hawapo pichani) kwa mapokezi, wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama kwa Jimbo la Temeke jana.
Naibu akiagana na baadhi ya Viongozi ofisini kwa Mkuu wa Wilaya.

Watumishi wa umma kuweni karibu na wananchi, Balozi Mwinyi

$
0
0
Taasisi za Serikali zimehimizwa ziwe karibu na wananchi ili ziweze kuwahudumia na kuwaelimisha juu ya huduma inazozitoa. Wananchi wengi wamekuwa wakilalamika mara kwa mara kuhusu watumishi wa umma kutotumia weledi na ubunifu katika kuwahudumia wananchi jambo ambalo likiachwa liendelee, Tanzania itaachwa nyuma ndani ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na ulimwengu mzima kwa ujumla.

Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Mwinyi katika semina kuhusu elimu ya mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na fursa zake inayotolewa na wataalamu wa Wizara yake kisiwani Pemba. Semina hiyo iliyoanza jana inafanyika kwenye uwanja wa Gombani, Pemba na itamalizika tarehe 18 Mei 2017.

"Kuna fursa nyingi za kiuchumi katika Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki lakini kama wananchi wetu hatutawasaidia na kuwaelimisha kuhusu nyaraka na masharti yanayokidhi vigezo wataachwa nyuma na kubaki kuwa watazamaji na walalamikaji" Balozi Mwinyi alisema.

Wajasiriamali walielezea masikitiko yao juu ya ugumu wa kupata hati za kusafiria kutokana na mlolongo wa masharti hususan, inapotokea kuwa safari ni ya ghafla. Aidha, wajasiriamali wamekuwa wakilalamika kuwa wanapata tabu kusajili bidhaa zao katika mamlaka zinazosimamia ubora wa viwango wa bidhaa, chakula na madawa kwa kuelezwa kwamba bidhaa zao ni duni, hivyo wameiomba Serikali iwawezeshe kupata teknolojia ya kisasa ikiwa ni pamoja na vifungashio.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhani Mwinyi akitoa mwongozo kwa wajumbe wa semina ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki inayoendelea kufanyika kisiwani Pemba. Pamoja na mambo mengine amewahimiza wananchi kuchangamkia fursa zinazopatikana kwenye mtangamano. 
Mbunge wa jimbo la Konga, Mhe. Mbarouk Ali akichangia jambo kwenye semina. 
Sehemu ya wajumbe wakiendelea kusikiliza mada mbalimbali zilizokuwa zikiendelea kutolewa kwenye semina. 
Afisa kutoka Ofisi za Uhamiaji Pemba Bw. Haji Kassim Haji akijibu hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na wajumbe kwenye semina juu ya upatikanaji wa Hati ya Kusafiria ya Afrika Mashariki. 

PUBLIC NOTICE FROM MUHIMBILI UNIVERSITY OF HEALTH AND ALLIED SCIENCES

TIBA MTANDAO KUANZIA OLOLOSOKWAN OKTOBA MWAKA HUU

$
0
0
WATU waliopembezoni ambao wamekuwa na shida kubwa ya kupata madaktari bingwa, wataanza kupata nafuu baada ya kuanza kwa mradi wa tiba mtandao unaoendeshwa kwa pamoja kati ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi-Muhimbili, UNESCO pamoja na wadau wengine. 

Hayo yalisemwa katika warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza. Kwa mujibu wa Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Zulmira Rodrigues utoaji huo wa tiba mtandao kwa majaribio utaanza mapema zaidi kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu. Mratibu wa E-Medicine kutoka Idara ya Tiba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Liggy Vumilia akisoma hotuba kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza inayoendelea katika ukumbi wa MUHAS jijini Dar Es Salaam.

Alikuwa anatarajia mifumo yote kuwa tayari ifikapo Julai na hivyo kuwa na nafasi ya kuwa katika matibabu ifikapo Oktoba. Katika warsha hiyo aliwahimiza wataalamu kujadiliana kiundani changamoto mbalimbali na namna ya kuweka ripoti ili kuja kusaidia wakati mradi utakapoenda kitaifa. 

Katika warsha hiyo iliyokutanisha wataalamu mbalimbali wa tehama na madaktari kutoka Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Dar es Salaam Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya katika hotuba yake ya ufunguzi iliyosomwa na Dk Liggyle Vumilia alielezea matumaini yake kuhusiana na mradi huo wa majaribio. Aliwataka washiriki wa warsha hiyo kuona uwezekano wa kuanza mradio huo mapema zaidi baada ya kuhakikisha kwamba dhana imekubalika na namna ya kuitekeleza inaeleweka miongoni mwa wadau. Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi-Muhimbili (MUHAS), Prof Eligius Lyamuya alipokuwa akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza inayoendelea chuoni hapo jijini Dar es Salaam.

Mradio huo unaoanza kwa majaribio kufuatia juhudi za UNESCO zilizoanzishwa kwa msaada wa Samsung unahusisha zaidi wagonjwa wanaoweza kufika kupata matibabu katika kijiji cha kidigitali cha Ololosokwan na kwa kuanzia huduma hiyo itatolewa kwa mama na mtoto na afya ya kinywa, masikio, pua na koo (ENT), ambapo mabingwa kutoka KCMC na MUHAS wanaweza kufanya tiba kwa kutumia mtandao. 

Kliniki ya Digitali ilizinduliwa katika kijiji cha Ololosokwan Ngorororo, Arusha mnamo mwezi Novemba mwaka 2016. Wataalamu hao kutoka Shirika la Afya Duniani, Mwakilishi wa Tamisemi, Wizara ya Afya, DMO wa Ngorongoro, wataalamu kutoka KCMC na MUHAS wamekutana jana katika Kampasi ya Muhimbili (MUHAS), ili kuangalia dhana mpya kwa ajili ya utoaji huduma za afya kwa njia ya mtandao katika kijiji cha Wamasai, Mkoani Arusha cha Ololosokwan. Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akizungumza katika warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza inayoendelea jijini Dar Es Salaam.

 Kijiji hicho tayari kina uwezo wa kupata huduma hizo. 

Mradi huo ukifanikiwa unatarajiwa kupanuliwa kwenda sehemu mbalimbali zinazohitaji matibabu ya mabingwa lakini uwezo wa kufika huko haupo. “Dhana hii itawezesha kuendelea na utoaji wa huduma bora za afya, zenye ufanisi wa kitaalamu zaidi katika maeneo ya vijijini, ambayo mara nyingi huachwa nyuma katika utoaji wa huduma hizo,” alisema Zulmira na kuongeza kuwa dhana ya utabibu mtandao inalenga hasa kuinua utumiaji wa teknolojia ya kidigitali ya kisasa, ambapo utekelezaji wake utakuwa mfano elekezi wa kuboresha matumizi ya teknologia katika karne ya ishirini na moja katika utoaji wa huduma za afya nchini na barani Afrika. 

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

SERIKALI YASISITIZA KUKAMATWA KWA ALIYEMJERUHI MTOTO KWA KOSA LA KUDOKOA CHAKULA

$
0
0
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imelaani vikali kitendo cha mtoto wa miaka mitatu (jina limehifadhiwa), mkazi wa kata ya Rudete mkoani Geita, aliyeelezwa kwamba amejeruhiwa na mama wa kambo kwa kuchomwa moto mwilini akituhumiwa kuiba chakula alichobakiziwa baba yake.

Wizara imesikitishwa na tukio hili maana linakinzana na kaulimbiu ya Madhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Familia kwa mwaka 2017, ambayo pamoja na mambo mengine,  inasisitiza wazazi na walezi, kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao wa kuimarisha malezi kwa ajili ya ustawi wa watoto katika familia na jamii kwa ujmla.

Katika kutekeleza utoaji wa haki za Mtoto na ustawi wake, wadau wote wanaotoa huduma kwa mtoto wanasisitizwa kusimamia upatikanaji wa haki zote za msingi katika familia na jamii, ikiwemo haki ya kuishi, kulindwa, kuendelezwa, kushirikishwa na kutobaguliwa. 

Wizara inawaomba wananchi kote nchini kutoa ushirikiano katika kuwafichua wanaotenda vitendo vya unyanyasaji dhidi ya watoto kwa kutoa taarifa kwenye mamlaka husika, ili kuhakikisha wahusika wa vitendo vya ukatili wanachukuliwa hatua.

Napenda kutoa maelekezo kwa Maafisa Maendeleo, Ustawi wa Jamii wa kuhakikisha kuwa mtoto huyo anapatiwa huduma ya matibabu haraka ili kumrejesha katika afya njema. 

Kwa vile, jukumu la ulinzi na usalama wa mtoto linatekelezwa kwa ushirikiano mkubwa wa Polisi, tunaamini kuwa suala hili litafuatiliwa kuhakikisha kuwa watuhumiwa wa vitendo hivi vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya huyo mtoto mdogo wanapatikana.  

Azma ya Wizara yenye dhamana ya Watoto, ni kuhakikisha kuwa familia zinaendelea kuwa kitovu cha upatikanji wa haki, ustawi na maendeleo kwa maslahi ya watoto wetu.

NEWZ ALERT:Rais Magufuli ateua Mkurugenzi Mtendaji TIC na RAS Morogoro

TAKUKURU KUBANA WEZI TASNIA YA KOROSHO

MAKAMU WA RAIS,SAMIA SULUHU HASSAN AFUNGUA MAFUNZO YA SIKU TATU YA POLISI WANAWAKE KUTOKA JUMUIYA YA MAENDELEO YA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA JIJINI DAR LEO

$
0
0
Polisi wanawake kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SARPCO,wakimsikiliza Makamu wa Rais,Samia Suluhu Hassan alipokuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ya siku tatu
Makamu wa Rais Mh.Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya polisi wanawake kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SARPCO,leo katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jijini ,Dar es Salaam.Mh Samia ndiye mgeni rasmi wa mafunzo hayo.Picha na Adam Mzee/VPO.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akishiriki ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya polisi wanawake kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SARPCO,leo katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jijini ,Dar es Salaam.Mh Samia ndiye mgeni rasmi wa mafunzo hayo.Picha na Adam Mzee/VPO.
 Makamu wa Rais Mh.Samia Suluhu Hassan akifuatilia moja ya taarifa wakati wa ufunguzi wa  mafunzo ya siku tatu ya polisi wanawake kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SARPCO.Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere ,Dar es Salaam.Kushoto kwake ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,IGP Ernest Mangu.
Polisi wanawake kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SARPCO wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mafunzo hayo ya siku tatu. 

Makamu wa Rais (wa nne kulia) Mh.Samia Suluhu Hassan akishiriki ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya polisi wanawake kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SARPCO,leo katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jijini ,Dar es Salaam.Mh Samia ndiye mgeni rasmi wa mafunzo hayo.Picha na Adam Mzee/VPO

 Mafunzo ya siku tatu ya polisi wanawake kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SARPCO,yakiendele leo katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jijini ,Dar es Salaam.Mh Samia ndiye mgeni rasmi wa mafunzo hayo.Picha na Adam Mzee/VPO.  
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni wakati wa Mafunzo ya siku tatu ya polisi wanawake kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SARPCO,yakiendele leo katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jijini ,Dar es Salaam.
Baadhi ya Askari wanaoshiriki ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya polisi wanawake kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SARPCO,wakiwasili kwa Gwaride katika.Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere ,Dar es Salaam.

Atupwa jela miaka ishirini kwa kukutwa na mafuta ya Simba.

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu Said Rajabu Said (36), kifungo cha miaka 20 jela baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na mafuta ya Simba.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Wilbard Mashauri, baada ya kumaliza ushahidi kutoka kwa mashahidi wa upande wa mashtaka na washtakiwa kujitetea.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kufanya kosa hilo kinyume na kifungu 86(1)(2)(c)(ii) ya sheria ya wanyama pori namba 5 ya 2009.

Akisoma hukumu Hiyo Hakimu Mashauri amesema kuwa upande wa mashtaka wamethibitisha bila kuacha shaka kuwa mshtakiwa Said ametenda kosa hilo.

Kabla hajamsomea mshtakiwa adhabu yake, Mashauri aliuliza upande wa mashtaka kama walikuwa na lolote la kusema ambapo wakili wa Serikali, Adolf Mkini aliomba mahakama itoe adhabu kwa mujibu wa sheria ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia na nia ya kutenda makosa kama hayo.

"Mheshimiwa hakimu, sina kumbukumbu za makosa ya nyuma kwa mshtakiwa, ila naomba mahakama yako tukufu itoe adhabu Kali kwa mshtakiwa na kwa wengine kwenye nia ya kuharibu maliasili za nchi", amesema Mkini.

Kwa upande wa mshtakiwa Said katika utetezi wake ameiomba mahakama imuachie huru kwa sababu ana watoto watano na familia inayomtegemea na yeye ndio kila kitu kwenye familia hiyo.

" Nimezingatia yote yaliyosemwa na upande wa mashtaka na utetezi wa shahidi, nchi hii ina sheria zake za kulinda maliasili hivyo, Mahakama inakuhukumu kwenda jela miaka ishirini ile iwe fundisho kwako na kwa wengine wenye tabia kama yako".

Mshtakiwa anadaiwa kuwa, Februari 8,2016 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, alikamatwa akiwa na mafuta ya Simba yenye thamani ya Sh 10,711,400 bila ya kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa wanyama pori.
Viewing all 110104 articles
Browse latest View live




Latest Images