Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1690 | 1691 | (Page 1692) | 1693 | 1694 | .... | 3272 | newer

  0 0

   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akizungumza na Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hazem M. Shabat, ofisini kwake jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Bunge).
   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akimsikiliza  Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hazem M. Shabat,  wakati alipozungumza naye ofisini kwake jijini Dar es Salaam. 
   Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hazem M. Shabat akimueleza jambo Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai wakati akimkabidhi barua Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
   Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hazem M. Shabat akimkabidhi Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai kitabu mara baada ya kuzungumza naye Ofisini kwake jijini Dar es Salaam. 

  0 0


   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (katikati) akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Kunduchi Beach, Jijini Dar es salaam leo, juu ya kuwepo kwa Mkutano Mkuu wa wanahisa wa Benki hiyo, unaotaraji kufanyika Mei  20, 2017 Jijini Arusha. Kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Saugata Bandyopadhyay na kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mkuu anaeshughulikia Huduma Shirikisho katika Benki hiyo, Esther Kitoka.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akionyesha kitabu cha ripoti ya Mwaka kwa waandishi wa habari katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Kunduchi Beach, Jijini Dar es salaam leo. Kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Saugata Bandyopadhyay na kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mkuu anaeshughulikia Huduma Shirikisho katika Benki hiyo, Esther Kitoka.

  0 0


  George Binagi-GB Pazzo @BMG.

  Wakazi wa Jiji la Mwanza wameingia katika taharuki baada ya kutokea uvumi wa taarifa za mti kugoma kung’olewa katika eneo la Pasiansi ambapo kuna shughuli ya upanuzi wa barabara inayoelekea uwanja wa ndege wa Mwanza.

  Taharuki hiyo ilianza tangu jana majira ya jioni ambapo mamia ya wananchi walijazana katika eneo hilo ili kushuhudia mgomo wa mti huo ambao inasadikika ulikuwa ukitoa sauti za kulalama mithiri ya binadamu.

  Zoezi la kuung’oa mti huo aina ya mwembe limefanikiwa hii leo majira ya saa tatu asubuhi baada ya shughuli pevu ya kuung’oa kwa kutumia mashine aina ya burudoza huku baadhi wakihusisha tukio hilo na imani za kishirikina na wengine wakisema ni upotoshaji tu ulifanyika juu ya tukio hilo.

  Kasim Mlisu ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya ujenzi ya Nyanza Road Works inayojenga barabara ya Pasiansi, amesema taarifa za mti huo kuzungumza ni za upotoshaji na kwamba zoezi la kuung’oa lilichukua muda mrefu tangu juzi ili kupisha hatua za upimaji wa ukubwa wake na kusubiri mashine aina ya“skaveta” iliyofanikiwa kuung’oa.

  Katibu wa Chama cha Tiba asilia mkoani Mwanza CHAWATIATA, Kawawa Athuman, amesema tukio la mti kuzungumza ama kugoma kung’olewa halina ukweli wowote kwa karne hii ya 21 japo matukio ya aina hiyo yalikuwepo enzi za kale kabla ya ujio wa dini barani Afrika ambapo amewatahadharisha watumiaji wa mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kujiepusha na usambazaji wa taarifa za upotoshaji.
  Hapa msumeno ulikata ila mti ukagoma kuanguka licha ya kuvutwa
  Zoezi la kuung'oa mti huo likiwa limefanikiwa
  Zoezi la kuung'oa mti huo likiwa limefanikiwa.


  0 0


  0 0

  Makamu wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akimshukuru Kaimu Afisa Mkuu wa wateja wadogo na wakati wa Benki ya NMB, Abdulmagid Nsekela kwa niba ya NMB kwa udhamini walioutoa ili kufanikisha mashindano hayo.
  Makamu wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akimshukuru Kaimu Afisa Mkuu wa wateja wadogo na wakati wa Benki ya NMB, Abdulmagid Nsekela kwa niba ya NMB kwa udhamini walioutoa ili kufanikisha mashindano hayo. Kaimu Afisa Mkuu wa wateja wadogo na wakati NMB Abdulmajid Nsekela akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa mashindano ya michezo ya taasisi za Elimu ya juu na Vyuo vikuu mjini Zanzibar.Uzinduzi huu ulifanyika mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Amani na kuhudhuliwa na wageni mbali mbali akiwemo Makamu wa Rais Mhe. Balozi Idd. NMB na Sanlam kampuni ya Bima nchini wakiwa ndio wadhamini wakuu wa Mashindano hayo. Mkuu wa Mkoa mjini Zanzibar Mhe. Ayoub Mohamed (Pili Kushoto) akiwa kwenye kikao cha kuwashukuru wadhami wakuu wa mashindano hayo ya Michezo ya taasisi za elimu ya juu pamoja na vyuo vikuu mjini Zanzibar. Kikao hiki kilifanyika mara baada ya uzinduzi rasmi.


      MAKAMU wa Rais wa Pili wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd, ameipongeza Benki ya NMB kwa kudhamimi Mashindano ya Michezo kwa Taasisi za Elimu na Vyuo Vikuu Zanzibar (ZAHILFE 2017), iliyozinduliwa juzi Jumapili, huku akiwataka washiriki kuitumia vema fursa hiyo.

   NMB imedhamini mashindano hayo kwa kiasi cha Sh. Mil. 20, ambako timu kutoka taasisi za elimu na vyuo vikuu Zanzibar, vitachuana hadi Mei 26, bingwa wa mashindano hayo yanayofanyika kwenye Uwanja wa Amaan, atakapopatikana. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa michuano hiyo,

  Balozi Idd, aliishukuru NMB kwa kuipa umuhimu mkubwa na kudhamini mashindano hayo, huku akichagiza washiriki kuonyesha vipaji, ili kujijengea wigo wa mafanikio michezoni. “Tunawashukuru na kuwapongeza wafadhili wa mashindano haya, Benki ya NMB pamoja pamoja Sunlam, kwa kuona umuhimu wa kushirikiana na vijana wetu hapa Zanzibar. Ombi langu kwa vijana, ni kuitumia fursa hii kujinufaisha kimichezo, kwani michezo ni ajira kwa sasa,” alisema Balozi Idd.

   Kwa upande wake, Kaimu Ofisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati wa NMB, Abdulmajid Nsekela, aliushukuru uongozi wa ZAHILFE kwa kuona umuhimu wa kuifuata NMB kuomba udhamini, akisema beki hiyo ni mahala sahihi pa kukimbilia katika michezo. “Tulipopata maombi ya kushiriki mashindano haya, tulifurahi sana kwani hii ilionyesha ni jinsi gani mmetambua umuhimu wa NMB katika michezo.

   “Tunajivunia kuwa nanyi katika wiki hii nzima na pia tunaomba wanafunzi pamoja na wazazi watembelea banda la NMB, lilipo viwanjani hapa ili wapate Elimu ya Huduma za Kibenki.” alisema Nsekela. Zaidi ya wanafunzi 2,000 kutoka Taasisi za Elimu na Vyuo Vikuu Zanzibar, wanatarajia kuchuana katika michezo mbalimbali ikiwemo soka, netiboli, kikapu, mpira wa meza (table tennis) na mingineyo, kusaka mabingwa wa ZAHILFE 2017.

  0 0

  Na Veronica Simba – Dodoma.

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amekataa kusaini ombi la uhamishaji wa leseni ya uchimbaji wa kati wa madini ya Shaba Namba ML 571/2017 kutoka kwa mtanzania David Stanley Kayongoya kwenda Kampuni ya Mechanized Minerals Supreme Mining Company Limited inayomilikiwa na raia kutoka China.  Profesa Muhongo alikataa kusaini leseni hiyo yenye ukubwa wa kilomita za mraba 0.43 katika eneo la Fufu wilayani Chwamwino mkoani Dodoma, baada ya kubaini kuwa mtanzania anayetaka kuhamishia leseni hiyo kwa Raia wa China, hatanufaika kwa kiwango kinachoridhisha.  Akizungumza na wawekezaji mbalimbali wa sekta husika, waliofika Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma, kwa ajili ya kusainiwa leseni zao za uwekezaji, jana (Mei 15), Profesa Muhongo alisisitiza kuwa ni lazima wawekezaji katika sekta husika wazingatie suala la maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla, wakati wanapotekeleza kazi zao za uwekezaji.  Waziri Muhongo alimwagiza mwekezaji huyo raia wa China kujadiliana kwa mara nyingine na mtanzania mwenye eneo husika (David), ili kuhakikisha ananufaika ipasavyo na uwekezaji huo.  “Ili niweze kusaini leseni hii, rudini mezani, mzungumze na kukubaliana ili David aweze kunufaika. Hatuwezi kukubali kuona watanzania wakidhulumiwa namna hii,” alisisitiza Waziri.


   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), akizungumza na wawekezaji mbalimbali katika sekta ya madini, waliowasilisha maombi ya kupatiwa leseni kwa ajili ya kuwekeza katika sekta husika.
   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akisaini leseni mbalimbali za wawekezaji katika sekta ya madini.

   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akikabidhi leseni ya uchimbaji wa kati wa madini ya ‘Marble’ iliyohamishwa kutoka kwa Salim Mohamed Salum (wa pili kutoka kushoto) kwenda kwa wawekezaji wa kampuni ya S & T Marble and Mining Limited (kulia). Wa kwanza kushoto ni Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka.

  0 0
 • 05/16/17--08:08: Article 11


 • 0 0

  Bank ya biashara Africa CBA imeanzisha huduma ya kuwahudumia wateja kibinafsi (private banking) kwa kuwafuata wateja wake walipo tofauti na mfumo uliozoeleka wa wateja kufuata bank.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo hivi karibuni jijini Arusha mkurugenzi wa Bank hiyo Gift Shoko alisema lengo la kianzisha huduma hiyo ni kutoa fursa kwa watu wote kuchangia pato la taifa.

  "Hivi sasa kuna watu wanakosa muda wa kwenda Bank kupanga foleni kutokana na majukumu mbalimbali, hivyo kuwepo kwa huduma hii kutawarahisishia kupata huduma bila kwenda Bank" alisema Shoko na kuongeza

  "Ni fursa kwa taasisi na mashirika mbali mbali kuchangamkia huduma hii kwani itaambatana na kuduma kama kupewa vyumba vya kufanyia mikutano, kupewa msaada wa kisheria, kupata matibabu ya nje ya nchi na mteja kupewa mtu maalimu wa kumhudumia"

  Kwa upande wake Solomon Kawiche mkuu wa kitengo cha masoko CBA alisema huduma hiyo itakuwa kwenye mikoa ya Arusha, Mwanza na Dar es salaam licha ya kuwa na matawi Mbeya, Kigoma, Mtwara, Moshi na Tunduma.

  Bank hiyo iliyoanza miaka ya 60 ambayo ipo Tanzania, Kenya na Uganda, yenye makao makuu mjini Nairobi hivi karibuni inatarajia kuanzaisha tawi Ivory cost kwa lengo la kujitanua zaidi kibiashara.
  Mkurugenzi wa Bank ya biashara Africa CBA Gift Shoko akizungumza hivi karibuni jijini Arusha katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya kuwahudumia wateja kibinafsi (private banking) kwa kuwafuata wateja wake walipo tofauti na mfumo uliozoeleka wa wateja kufuata bank(Habari Picha na Pamela Mollel blog)
  Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi CBA N.Kitomari akizungumza katika uzinduzi huo hivi karibuni jijini Arusha katika hafla ya uzinduzi wa huduma mpya kwa wateja binafsi (private banking) kwa kuwafuata wateja wake walipo tofauti na mfumo uliozoeleka wa wateja kufuata bank 
  Julius Konyani Mkuu wa kitengo cha wateja binafsi katika benki ya CBA akizungumza jambo katika hafla ya uzinduzi wa hudum mpya kwa wateja binafsi (private banking) kwa kuwafuata wateja wake walipo tofauti na mfumo uliozoeleka wa wateja kufuata bank .
  Julius Konyani Mkuu wa kitengo cha wateja binafsi akimkabidhi zawadi moja ya wateja wa benki hiyo katika uzinduzi wa huduma mpya ya kuwahudumia wateja kibinafsi (private banking) kwa kuwafuata wateja wake walipo tofauti na mfumo uliozoeleka wa wateja kufuata bank .


  0 0


  0 0  0 0


  0 0

  Na.Vero Igantus.Arusha

  Mamlaka ya usimamizi wa Bima nchini(TIRA)imezindua mfumo wa uhakiki wa Bima kwa njia ya simu za mkononi kanda ya Kaskazini ambapo zoezi hilo limeambatana na ukaguzi wa bima kwenye vyombo vya moto na kubaini bima feki katika baadhi ya magari na pikipiki.

  Akizindua mfumo huo kwa kanda ya kaskazini uliofanyika jijini Arusha Kamishna wa Bima Nchini Dkt.Boghayo Saqware amesema kuwa kampeni yao ina laengo la kuondoa bima feki sokoni ambazo zinazouzwa ama kutengenezwa na wahalifu ,ambalo kwa mujibu wa sheria wanafanya kosa la jinai.

  “Tumeanzia Pwani na sasa tupo Arusha na zoezi hili litakuwa endelevu,kwahiyo tunawaasa wananchi wanunue bima halali,tumezindua mfumo ambao ni rahisi kwa mtu anaenunua bima kujihakikishia kuwa bima hiyo ni feki au halali .”alisema Dkt.Boghayo.

  Kamishna huyo amesema kuwa kwa miaka( 3) kesi (10) za Bima feki ziliamuliwa ,watu(5) walihukumiwa kifungo jela,(2) wamelipa bilioni 20,000,000, hadi 40,000,000,mashauri ya jinai yaliyopo mahakamani yalifunguliwa mwaka 2016 Mbeya(1) Mafinga(2) Mara(1) na Dar es salaam (3) na kufikia jumla ya kesi mpya 7,ambapo mashauri yaliyopo kwenye uchunguzi wa polisi ni (10).

  Kwa upande upande wake Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Kanda ya kaskazini Eliezer Rwekiza amesema kuwa zoezi hilo katika Jiji la Arusha litaendelea kwa wiki nzima ambapo wataelekea Kilimanjaro ,Tanga ambapo amesema kuwa 10% ya magari hapa nchini Tanzania hayana Bima halali,amesema hadi sasa hapa nchini kuna makampuni 31 ya Bima,mawakala 500 madalaliwa Bima ni zaidi ya 100.

  Kaishna wa Bima nchini Dkt.Boghayo Saqware akiwa anazungumza na wauza bima,madalali wa bima,mawakala wabima,wauza bima,jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani, viongozi wa vyama vya wamiliki wa mabasi pamoja na umoja wa waendesha pikipiki.Picha na Vero Ignatus Blog.
  Meneja wa Mamlaka ya usimamizi wa Bima (TIRA)Kanda ya kaskazini Eliezer Rwekiza akizugumza katika uzinduzi huo wa uhakiki wa Bima kwa njia ya simu ya mkononi,uliofanyika Jijini Arusha leo,wa kwanza kulia ni Kamisha wa Bima Taifa Dkt.Boghayo Saqware,akifuatiwa na aliyepo kulia kwake ni Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Nuru Suleiman

  Meneja waTEHEMA kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA)Aron Mlaki akiwa anawonyesha namna ya kutambua Bima kama ni halali au ni feki kwa kutumia simu ya mkononi .Picha na Vero Ignatus Blog.
  Mkurugenzi wa masoko kutoka Mamlaka ya usimamizi wa Bima (TIRA) Bi.Adelaida Muganyizi akiwa anazungumza na wauza bima,madalali wa bima,mawakala wabima,wauza bima,jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani, viongozi wa vyama vya wamiliki wa mabasi pamoja na umoja wa waendesha pikipiki.


  0 0
 • 05/16/17--09:26: Article 5


 • 0 0

  Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.

  MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Viettel Tanzania ‘Halotel’, Do Manh Hong na wenzake nane wamehukumiwa kulipa faini ya zaidi ya milioni 700 baada ya kupatikana na hatia katika mashtaka saba likiwemo la uhujumu uchumi. 

  Hukumu hiyo, imetolewa baada upande wa mashtaka kuomba kufanyia marekebisho hati ya mashtaka kwa kuondoa mashtaka matatu Kati ya kumi yaliyokuwa yakiwakabili.


  Mashtaka mapya ni pamoja na kusimika mitambo ya mawasiliano bila kibali cha TCRA, kutumia mitambo ambayo haijathibitishwa na kuitia hasara Serikali na TCRA ya milioni 459.


  Akisoma Hukumu hiyo, Hakimu Wilbard Mashauri amesema amewatia hatiani washtakiwa mwenyewe baada ya kukiri kutenda makosa yao.
  Kabla ya kuwasomea hukumu, Hakimu aliwauliza upande wa mashtaka kama walikuwa na lolote ambapo wakili, Johavenes Zacharias ameiomba mahakama kutoka adhabu stahiki kwa washtakiwa.


  Naye Wakili wa utetezi, aliiomba mahakama kuwapa adhabu ndogo washtakiwa kwa kuwa hilo ni kosa lao la kwanza na wanafamilia zinazowategemea.Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mashauri amewahukumu washtakiwa kulipa faini ya jumla ya faini ya milioni 700. Akifafanua adhabu hiyo, hakimu Mashauri amesema kila mshtakiwa anatakiwa kulipa faini ya milioni tano kwa kila shtaka linalomkabili na pia walipe milioni 459 kwa TCRA kwa hasara waliyoisababisha. 

  Ameongeza kuwa, ametoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwao na kwa wafanyabiashara wengine wanaohujumu uchumi.Ameongeza kuwa, watuhumiwa wamekuja nchini kuwekeza kwenye biashara na siyo kuhujumu mitambo ya nchini.

  "Washtakiwa hawa ni wafanyabiashara na wamekuja kwa ajili ya kuwekeza, hivyo ili kuonyesha Tanzania ipo makini kwenye masuala ya uwekezaji lazima wafuate sheria" amesema Mashauri.
   Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya simu ya Halotel, Do Manh Hong, mwenye tisheti ya kijani na wenzake ambao ni raia wa Pakistan na Sri Lanka wakirudishwa mahabusu baada ya kuhukumiwa kulipa faini zaidi ya milioni 700 baada ya kupatikana na hatia ya mashtaka saba likiwemo la uhujumu uchumi


  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Tao Zhang aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Tao Zhang aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Tao Zhang aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Tao Zhang mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Tao Zhang wanne kutoka (kushoto) Gavana wa Benki Kuu (BOT) Profesa Beno Ndulu, wapili kutoka kulia, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango watatu kutoka kushoto pamoja na ujumbe wa Mkurugenzi huyo wa IMF. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Tao Zhang mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

  0 0

   
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akioneshwa na kupatiwa maelezo ya kazi za sehemu mbalimbali za studio za Redio na Televisheni za  Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) alipotembelea leo kuangalia uendeshaji wake na kuongea na watumishi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiuliza jambo wakati akioneshwa sehemu mbalimbali za studio za Redio na Televisheni za  Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) alipotembelea leo kuangalia uendeshaji wake na kuongea na watumishi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika moja ya studio za Televisheni za Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) na mtangazaji Bi. Asha Haji alipotembelea leo kuangalia uendeshaji wake na kuongea na watumishi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikaribishwa na Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dkt Ayoub Rioba kuzungumza na watumishi Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) alipotembelea leo kuangalia uendeshaji wake na kuongea na watumishi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na watumishi Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) alipotembelea leo kuangalia uendeshaji wake na kuongea na watumishi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na watumishi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) alipotembelea leo kuangalia uendeshaji wake na kuongea na watumishi.

  0 0  0 0

  LG Event Photo 1.jpg

  Mr. Rama Esteem from Dar es Salaam, who was just a guest guest at the LG 2017 System Air Conditioning Tech Seminar and the Launch of the new eco-friendly & energy efficient air conditioning solutions products for Tanzania, receives the 43in, LG Flat Screen Smart TV from LG Technical Director Hebert Wamalwa. Looking on is Mr. Janghoon Chung, Managing Director of LG Electronics Africa Logistics FZE. The event took place in Dar es Salaam over the weekend.

  LG Event Photo 5.JPG
  A Dar es Salaam lady, Diyu Patrick, from Tontan Project Tech. Co. Ltd, who was just a guest guest at the LG 2017 System Air Conditioning Tech Seminar and the Launch of the new eco-friendly & energy efficient air conditioning solutions products for Tanzania, found her self a winner of LG Ultra Modern Microwave, as she receives it from LG Technical Director Hebert Wamalwa. Looking on is Mr. Janghoon Chung, Managing Director of LG Electronics Africa Logistics FZE. The event took place in Dar es Salaam over the weekend.

  LG Event Photo 9.jpg
  Some of the LG, AC’s displayed during the LG 2017 System Air Conditioning Tech Seminar and the Launch of the new eco-friendly & energy efficient air conditioning solutions products for Tanzania. The LG showcased the prowess of its inverter technology platform with green refrigerants, which is designed to facilitate continuous optimum cooling.  0 0

  Mr Puaz is a Tanzanian Photographer, Music Influencer and a songwriter goes by his real name Joel Vicent Joseph. Born 31st March 1985 in Arusha, Mr Puaz is popularly known for being a top  Music Influencer and Social Media Analyst in East Africa. Over the past four years he has been working with many artists to help them grow in the Music Industry. Among The artists he has worked with is Diamond Platnumz, Shetta, Darassa and many more.

  In  early 2004 he started his music career  as well as  entertainment talent in Arusha where he recorded his first song called SWEET BABY, that enjoyed immense airplay in different radio stations in Arusha. 
  A year later he decided to join a music Group called Space Unit as a Dancer and at the same time forming a Music Group called Top Unit.  
  His journey to the Music Industry was hard during that time but he then decided to work with Telcom companies like Vodacom Tanzania and then TIGO Tanzania.
  In 2015 he started working closely with the biggestst artist in Africa called Diamond Platnumz and was among the WCB WaSafi Ambassadors who support Diamond Platnumz on Digital promotions. Then he became Music Manager for the  artist named Shetta in 2016 and they worked together on his new song called NAMJUA.
  Mr Puaz has a lot of knowledge in the entertainment industry and now he has joined one of the biggest companies in Africa called Spice Vas Africa to help local Musicians on content distributions worldwide. 
  More information about Mr Puaz go to www.mrpuaz.com

  0 0

   Katibu Tawala wa Wilaya ya Lindi, Thomas Safari akizindua rasmi Kampeni ya Hedhi Salama kwa Wasichana iliyoandaliwa na Chama cha Tanzania Girl Guids (TGGA), ikiwa ni sehemu ya shamrashamra ya maadhimisho ya Siku ya Hedhi Duniani itakayofikia kilele Mei 28. Uzinduzi huo ulifanyika kwenye Uwanja wa Ilulu mjini Lindi leo. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa TGGA, Mkoa wa Lindi, Zuhura Mohamed na Katibu Mkuu wa TGGA, Grace Shaba. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA-KAMANDA WA MATUKIO BLOG
   Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari Mkoa wa Lindi wakiingia kwa maandamano kwenye Uwanja wa Ilulu, wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo.

   Wanafunzi wakiimba wimbo wa hamasa ya kampeni hiyo.older | 1 | .... | 1690 | 1691 | (Page 1692) | 1693 | 1694 | .... | 3272 | newer