Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA


EFM REDIO YAMTUNZA MAMA

0
0
Katika kuazimisha siku ya mama duniani Efm redio kupitia kipindi chake cha uhondo wametoa zawadi kwa  wakina mama wa wasikilizaji wao katika tafrija fupi iliopewa jina la “Begi la mama”

Tafrija hiyo ilifanyika katika ofisi za efm redio siku ya jana kuanzia saa 6:00 mchana hadi saa 9:00 Alasiri.  Begi la mama lilitolewa kwa wakina mama 15 ambao stori zao ziliandikwa na watoto wao na kuonekana kugusa mioyo ya wasikilizaji wengi kwa yale magumu waliopitia.
  Mtayarishaji wa kipindi cha uhondo Asha manga akipeleka begi la mama likiwa limejaa zawadi kem kem
 Timu nzima ya kipindi cha Uhondo ikiongozwa na Dina Marios wakimtunza mama nguo kutoka katika begi.
 Muda wa chakula ukafika.
 Mtangazaji wa kipindi cha uhondo akimuhoji mshindi ambae alikuja na mama yake kwaajili ya kuzawadiwa begi hilo.
 Mama akiwa kashikilia zawadi alizotunzwa na Efm redio.
 Timu nzima ya kipindi cha uhondo ikiongozwa na Dina Marios mstari wa pili (wakwanza kushoto) akifatiwa na Sofia Amani, Leah Chambo, Rdj Con wengine ni Bi, Hindu, Swebe Santana, Asha manga, na wengineo.

WANANCHI WA UHAMBILA WAASWA KUACHA KUHARIBU VYANZO VYA MAJI NA MALIASILI ZAO

0
0
Na Fredy Mgunda, Iringa.

Wananchi wa kijiji cha uhambila wilayani Mufindi Mkoani Iringa wametakiwa kutunza na kuvilinda vyanzo vya maji na maliasili zilizopo katika kijiji hicho.

Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara wa kijiji hicho Afisa mradi kutoka shirika la LEAT upande wa wilaya ya mufindi Jamali Juma alisema kuwa wananchi wanatakiwa kujiepusha na ukataji miti hovyo na kulima vinyungu kwenye vyanzo vya maji kwa kuwa kufanya hivyo kunasababisha ukame.

“Mkiangalia zamani maeneo haya yalikuwa ya kijani na tulikuwa na mito midogo midogo mingi iliyokuwa inatililisha maji msimu mzima lakini hali ya sasa haipo hivyo kutokana na kutaka miti na kuaharibu vyanzo maji nawaomba wananchi acheni hiyo tabia ili tuwe na Mazingira mazuri kama zamani”alisema juma

Ukataji miti na uharibifu wa vyanzo unasababisha madhara mengi makubwa na ndio maana tunaona sasa kumekuwa na magonjwa mengi ambayo yanaathari ya moja kwa moja kwa mwanadamu lakini pia uharibifu huo husababisha mabadiliko ya vipindi vya mvua na kukosekana kwa mvua za kutosha.

Juma alisema kuwa dunia kwa sasa inakabiliana na swala la mabadiliko ya tabia nchi hata hivyo wananchi mnatakiwa kuwa umakini ili msije mkaishi kwenye jangwa kutokana na uharibifu wetu.

“Ni kosa la jinai kwa mtu yoyote yule kukata miti bila kibali au kuharibu vyanzo vya maji kutokana na sheria zetu za mwaka 1982 hivyo kukata miti au kuaribu vyanzo vya maji sio haki ya msingi ya mwananchi” alisema Juma

viongozi wa shirika la LEAT pamoja na viongozi wa kijiji cha Uhambila wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wakati wa kujadili maswala ya utunzaji wa Maliasili na vyanzo vya maji vilivyopo eneo hill.
Baadhi ya wananchi wakisikiliza kinachoendelea kwenye mkutano wa kijiji wa kujadili maswala ya utunzaji wa vyanzo vya maji pamoja Maliasili za kijiji hicho.


NEWZ ALERT:RAIS DKT MAGUFULI ARIDHIA MAOMBI YA KUACHA KAZI KWA VIONGOZI HAWA

MAGAZETI YA LEO JUMANNE MAY 16,2017

Wananchi wa Pemba wahimizwa kuchangamkia fursa za kiuchumi katika Soko la EAC

0
0


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga amewataka wakazi wa Pemba na Tanzania kwa ujumla kuchangamkia ipasavyo fursa za Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kujiongezea kipato. 

Mhe. Waziri alieleza kuwa katika ulimwengu wa leo hakuna nchi duniani itakayoweza kujiimarisha kiuchumi peke yake bila kushirikiana na nchi nyingine. Ndio maana hata zile nchi zilizoendekea kama Marekani na nchi za Ulaya wana umoja wao kwa madhumuni ya kuongeza nguvu na kasi ya maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa. 

Waziri Mahiga aliyasema hayo alipokuwa anafungua semina kuhusu elimu ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na fursa zake kwa wananchi wa Pemba ambayo itatolewa na wataalamu wa Wizara yake kwa siku nne kuanzia leo kwenye Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Gombani.

Mhe. Waziri alieleza kuwa kabla, wakati na baada ya ukoloni nchi za Afrika Mashariki zilikuwa na aina moja au nyingine ya Ushirikiano kwa madhumuni ya kuimarisha uchumi wa nchi zao, waliotutawala. Aina moja ya Ushirikiano ni ule Umoja wa Huduma ambao ulianzishwa mwaka 1961. Umoja huo ulianzisha mashirika mbalimbali kama vile bandari, ndege, hali ya hewa, posta na reli ambayo yalikuwa yanaendeshwa kwa pamoja.

Alisema Tanzania ipo katika eneo la kimkakati ndani ya Jumuiya ikiwa ni pamoja na kuwa na eneo kubwa kuliko nchi zote, idadi kubwa ya watu, ukanda mkubwa wa bahari na ardhi nzuri yenye rutuba na kihistoria Pemba ni eneo lenye rutuba nzuri kuliko maeneo yote ya Afrika Mashariki. Hivyo, kutokana na sifa hizo hakuna budi wananchi wa Pemba na Tanzania kwa ujumla kujipanga vizuri ili kuchangamkia fursa hizo badala ya kubaki kuwa watazamaji na walalamikaji.
Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), akizungumza kwenye ufunguzi wa semina ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kisiwani Pemba. Semina hiyo inatolewa kwa wajasiriamali wa Pemba ili waweze kuchangamkia fursa za mtangamano. Semina hiyo inafanyika katika Ukumbi wa Mikutano uliopo katika Uwanja wa mpira wa Gombani. 
Naibu Waziri wa Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora wa Serikali ya Zanzibar Mhe. Khamis Juma Maalim akisoma hotuba ya ukaribisho. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Mwinyi naye akielezea jambo kwenye ufunguzi wa semina hiyo ya Mtangamano wa Afrika Mashariki. 
Ufunguzi wa Semina ukiendelea 
Wakiwa katika picha ya pamoja. 




YAJUE MATUMIS SAWIA YA MBOLEA AINA YA YARAMILA WINNER

0
0
Mbolea ya YaraMila Winner Ni mbolea ya NPK ya kupandia inayowekwa kwenye udongo wa mazao ya mboga mboga na matunda Matumizi 1. Kupandia – Weka kisoda kimoja hadi viwili kimoja kwa mmea kuzunguka shina wiki moja baada ya kuota 2. Kukuzia- Tumia vifuniko viiwili baada ya siku 14 kulingana na hitaji Zingatia · Udongo wako uwe na unyevunyevu wakati wa kuweka mbolea · Weka umbali wa sentimita 5 kutoka kwenye shina · Tafadhali wasiliana na bwana shamba wa kampuni ya Yara kwa maelekezo na mahitaji maalumu

INTRODUCING: Beka Flavour - Libebe

0
0
wimbo wa kwanza kutoka kwa Beka Flavor ambaye ni member wa Yamoto Band, ambaye amekuwa akisikika mara nyingi katika nyimbo za kundi lakini kwa sasa amefanya wimbo akiwa mwenyewe baada ya uongozi kuwaruhusu kufanya kazi za binafsi huku kundi likiendelea kama kawaida.

THREE CHILD SURVIVORS FROM TANZANIA BUS CRASH ARRIVE IN U.S.

0
0
SAMARITAN'S PURSE HAS RESPONDED TO THE EAST AFRICAN NATION'S TRAGEDY BY TRANSPORTING THE HURTING CHILDREN TO THE U.S. FOR URGENTLY NEEDED MEDICAL CARE.

Samaritan’s Purse has brought three severely injured Tanzanian children, the only survivors of a bus accident that killed 35 people and recently made world news, to the United States. They will be receiving specialized trauma care at a hospital in Sioux City, Iowa.

On Friday, May 12, Samaritan’s Purse sent our DC-8 airplane to Tanzania to pick up the children—Wilson, a 12-year-old boy; Sadhia, a 12-year-old girl; and Doreen, a 13-year-old girl. Their mothers have accompanied them on the journey, along with a Tanzanian doctor and nurse, as well as Ed Morrow, director of World Medical Mission, the medical arm of Samaritan’s Purse. They all arrived in Charlotte late Sunday night, May 14.

Update: The children are resting well at Carolinas Medical Center and are expected to be transported to Mercy Medical Center in Sioux City today. “I appreciate the Carolinas Medical Center responding quickly overnight to accommodate these children,” Franklin Graham said. (as of May 15)]
“When I heard about the tragic bus accident in Tanzania and the three children who survived, I knew Samaritan’s Purse had to do everything we could to help,” President Franklin Graham said.

Thirty-two of the children’s primary school classmates and three adults—two teachers and the driver—were killed in the May 6 crash when their bus plunged off a gravel road into a steep ravine in remote northern Tanzania. They were on the way to another school to take an exam when the accident occurred. Tanzania President John Magufuli called the accident a national tragedy.

How the plight of the surviving children came to the attention of Franklin Graham is providential at every step and begins with three missionaries who acted as Good Samaritans at the scene of the horrifying crash. The missionaries, serving with Siouxland Tanzania Education Medical Ministries (STEMM), happened upon the accident moments after it occurred.

Jumping out of their vehicle and rushing to join others already scurrying to help were Jennifer Milby, a licensed nurse practitioner; Manda Volkers, a nurse with 25 years of experience; and Kevin Negaard, the executive director of Sunnybrook Church in Sioux City.
As they pulled bodies from the wreckage, the missionaries found three children who, despite massive injuries, still had heartbeats. After stabilizing them, the missionaries helped put them into arriving ambulances, which rushed them to a local hospital.

“Kevin, Jennifer, and Manda were by the sovereignty of God late by an hour and a half that morning to where they were going,” explained Dr. Steven Meyer, a Sioux City orthopedic surgeon and STEMM’s co-founder and board president.

“If they had been two minutes earlier, they never would have seen it, and they never would have known about it. “There’s no question that God put them there at that point in time,” Dr. Meyer added.

The three visited Wilson, Sadhia, and Doreen at the hospital the next day and thanked God they were alive and stabilized. But the team knew the children needed much more extensive medical care beyond what local hospitals could provide. That’s when they sensed that God wanted them to do everything they could to bring them to America. They approached Dr. Meyer and other board members who were also in Tanzania for that trip and told them of their conviction.
They discussed it, prayed about it, and contacted medical personnel at the Mercy Medical Center in Sioux City as to its feasibility. They received the green light.

Now they had to receive approval from the Tanzanian government. At the same time, how would the children be transported to Iowa? Major pieces of the puzzle still had to be solved. The STEMM team prayed for God’s direction. Over the next 72 hours, His provision became clear.

God Answers Many Prayers

READ MORE HERE

HALMASHAURI NCHINI ZAKUMBUSHWA WITO WA KUNUNUA DAWA ZA KUUA VILUWILUWI VYA MBU WAENEZAO MALARIA

0
0

Na Benedict Liwenga-WHUSM.

Halmashauri nchini zimetakiwa kuitikia wito wa kununua dawa za kuua viluwiluwi vya mbu wa malaria zilizoanza kuzalishwa hapa nchini ili kukabiliana na ugonjwa wa malaria.

Kauli hiyo imetolewa jana na Kaimu Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Kuzalisha Viuadudu vya Kuua Viluwiluwi vya Mbu wa Malaria cha Tanzania Biotech Products Limited kilichopo Kibaha Mkoani Pwani, Bw. Samwel Mziray wakati alipokutana na Waandishi wa habari na kufanya nao mazungumzo juu ya shughuli zinazofanywa katika kiwanda hicho.

Bw. Mziray amesema kuwa, dawa za kuua viluwiluwi vya mbu wa malaria zinapaswa kununuliwa na kila Halmashauri nchini kwa maagizo yaliyotolewa na Serikali kupitia waraka wake kwa kuwa kiwanda hicho kinachomilikiwa na serikali kwa asilimia 100 kilijengwa ikiwa ni sehemu ya mkakati wa serikali katika kupambana na malaria nchini. 

Hata hivyo amebainisha kwamba mpaka sasa mwitikio wa halmashauri umekua mdogo kwani ni halmashauri mbili tu za Geita pamoja na Mbogwe ndizo zimeshanunua dawa hizo.

“Lengo la Serikali kuja na mpango huu ni kupunguza vifo vitokanavyo na malaria nchini na kupunguza gharama kubwa ya kununua dawa na vifaa tiba vya kupambana na malaria”, alisema Mziray.

Amesema kwamba iwapo kama halmashauri zitanunua dawa hizo na kuzitumia, ugonjwa huo utapungua kwa kiasi kikubwa nchini na hivyo serikali kuelekeza fedha zake katika shughuli za maendeleo.

Amesema kwamba, kwa Afrika kiwanda hicho ni moja ya kiwanda kilichobahatika kujengwa Tanzania ambapo nia ya Serikali ni kutokomeza ugonjwa wa malaria kwa kuharibu mazalia ya mbu.
Jengo la Kiwanda cha Kuzalisha Viuadudu vya Kuua Viluwiluwi vya Mbu wa Malaria lililozinduliwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ethiopia, Mhe. Hailemariam Desalegn tarehe 2 Julai, 2015 Kibaha, Pwani.
Mtaalam wa Maabara ya Uandaaji Bakteria katika Kiwanda cha Kuzalisha Viuadudu vya Kuua Viluwiluwi vya Mbu wa Malaria kilichopo Kibaha Mkoani Pwani Bw. Fumbuka Pauline akiwaeleza Waandishi wa habari baadhi ya kazi wazifanyazo wakati wa kuwaandaa bakteria 15 Mei, 2017. Kushoto ni Kaimu Meneja Mkuu wa Kiwanda hicho, Bw. Samwel Mziray.
Mmoja wa Waandishi wa Habari (kulia) akipiga picha ya bakteria wanaoonekana kwa kifaa maalum cha kuangalia bakteria (Microscope) katika Maabara ya kuaandaa bakteria 15 Mei, 2017 Kibaha, Mkoani Pwani.
Mtaalam wa Maabara ya Uandaaji bakteria katika Kiwanda cha Kuzalisha Viuadudu vya Kuua Viluwiluwi vya Mbu wa Malaria kilichopo Kibaha Mkoani akiangalia bakteria kwa kutumia kifaa maalum (Microscope) kabla ya kuwapeleka sehemu inayohusika kwa ajili ya hatua nyingine, 15 Mei, 2017.

Serikali yatoa fedha 100% kwa ajili ya manunuzi ya dawa nchini

0
0
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

Serikali imetoa asilimia miamoja ya fedha za bajeti ya dawa kwa mwaka 2016/2017 kwa ajili ya manunuzi ya dawa ikiwa ni moja ya mikakati ya kuboresha sekta ya afya nchini.

Akizungumza katika mahojiano ya kipindi cha TUNATEKELEZA kinachoratibiwa na Idara ya Habari – MAELEZO na kurushwa na kituo cha televisheni cha TBC, Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Dawa Laurean Bwanakunu alisema kuwa serikali inawahakikishia wananchi kuwa katika mwaka wa fedha 2016/2017 imetenga fedha za kutosha ili kuhakikisha kuwa dawa zinapatikana katika vituo vya kutolea huduma za afya.

“Ikiwa ni asilimia 81 ya upatikanaji wa dawa pamoja na vifaa tiba katika maeneo ya mjini na vijijini, ambapo Bohari Kuu ya Dawa inahudumia vituo 5642 nchi kote” alisema Bwanakunu.

Pia, Bwanakunu alibainisha kuwa hivi sasa kumekuwepo na upatikanaji wa dawa muhimu 110 kati ya 135 katika vituo mbalimbali vinavyotoa huduma za huduma za afya.

Katika kuboresha huduma za usambazaji wa dawa nchini , Bohari Kuu ya Dawa imefanikiwa kufungua maduka ya dawa 7 katika mikoa ya Dar es salaam, Arusha, Geita, Mbeya na Lindi, ambapo imeanza kusafirisha dawa kwa kutumia ndege na treni ili kufikisha dawa kwa wakati katika vituo mbalimbali vya afya nchini.

Aidha, Mikoa na Halmashauri zimetakiwa kuwasilisha maombi yao ya dawa kwa wakati ili kutatua changamoto ya upungufu wa dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Benki ya CRDB tawi la USA RIVER laibuka kinara wa jumla kampeni ya tumia simbanking Ulipwe.

0
0
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la USA RIVER, Bi Jennifer Tondi akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bi. Esther  Kitoka baada ya tawi lake kuibuka mshindi wa jumla wa kampeni ya Tumia Simbanking Ulipwe.

KWA SHERIA ZETU ZILIVYO HAITAWEZEKANA TUNDU LISSU KUMSHITAKI MAKONDA.

0
0
 
Na   Bashir    Yakub.

SHERIA  ZILIZOPITIWA :
1. Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Jinai, Sura ya 20.
2. Sheria  ya Huduma za Mashtaka  kwa Taifa, Na. 27/2008.
3. Kanuni  za  Adhabu, Sura  ya  16.
_______________

Tundu Lissu anasema  anaamua kumshitaki Makonda kwa kosa la kughushi nk. kwa kuwa Serikali imekataa na haioneshi nia ya  kumfikisha mahakamani Makonda.

Kama sababu ni kuwa serikali imekataa kumpeleka Makonda mahakamani  ndio maana  Tundu Lissu na wenzake wanaamua sasa kuchukua hatua basi nao hawatafanikiwa.

Kwa sheria ilivyo hawatafanikiwa mpaka serikali  wanayosema haitaki itake.  Kwa mujibu wa kifungu cha  97 cha Sheria ya Mwenendo wa Kesi  za Jinai kazi ya kufungua na kuendesha mashtaka  yote ya jinai ni kazi ya serikali kupitia  ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai (DPP).

Hata hivyo  kwa mujibu wa kifungu cha 99(1)  cha sheria hiyohiyo ni kweli bila ubishi kuwa mtu binafsi  au Wakili yeyote binafsi kama alivyo Tundu Lissu naye  anaweza  kufungua na kuendesha mashtaka ya jinai dhidi ya mtu yeyote mkosaji kama ilivyo kwa DPP wa serikali.

Pamoja na hayo kifungu cha  97 cha sheria hiyo ya Mwenendo wa Kesi za Jinai kinasema kuwa ikiwa mashtaka yamefunguliwa na mtu binafsi au Wakili binafsi kama alivyo Tundu Lissu basi  mwendesha mashtaka wa serikali  akiamua anaweza kuchukua kesi hiyo.

Pia kifungu kinasema zaidi kuwa Wakili huyo binafsi katika kesi hiyo aliyofungua atalazimika  kufuata maelekezo   ya  mwendesha mashtaka  huyo wa serikali wakati wote  wa kesi.

Maana yake ni kuwa ikiwa mwendesha mashtaka wa serikali atamwamuru Tundu Lissu kubadili jambo lolote katika kesi aliyofungua basi atalazimika kulibadilisha. Lakini kubwa kuliko yote ikiwa mwendesha mashtaka wa serikali atamwamuru Tundu Lissu kufuta kabisa kesi ya Makonda  basi atalazimika kuifuta. Hii ndio maana ya kifungu hicho.




KUSOMA  ZAIDI  sheriayakub.blogspot.com

Kura zinazoharibika zinatokana na ukosefu wa elimu ya mpiga kura

0
0
Hussein Makame, NEC-aliyekuwa Dodoma 

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa kura zilizoharibika zinazopatikana kwenye chaguzi zinasababishwa na wapiga kura wengi kukosa elimu ya mpiga kura.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Bw. Kailima Ramadhani wakati akijibu swali la mmoja wa watangazaji wa kituo cha Redio AFM cha mkoani Dodoma katika mfululizo wa kutoa elimu ya mpiga kura kupitia vituo vya redio.

Mtangazaji huyo alihoji kwa nini inajitokeza unapotokea uchaguzi kunakuwa na kura zisizo halili au kura zilizoharibika wakati Tume imekuwa ikitoa elimu ya mpiga kura katika chaguzi zilizopita.

Bw. Kailima alijibu kuwa kinachosababisha hali hiyo ni ukosefu wa elimu ya mpiga kura kwa wananchi, na ndio maana Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria ya Taifa ya Uchaguzi iliona umuhimu wa kutoa elimu hiyo katika kipindi chote cha mwaka.

“Mkurugenzi tusalie hapo kwenye kura halali na zilizoharibika, elimu hii umekuwa ukiitoa maeneo mbalimbali na leo tuko hapa AFM, kwa nini hadi leo tunakuwa na kura zilizoharibika na kura zisizo halali” alihoji.

Akijibu swali hilo, Bw. Kailima alisema ukosefu wa elimu ya mpiga kura ndio unaosababisha hali hiyo na ndio maana Katiba iliona kuna umuhimu wa Tume kutoa elimu hiyo kwa muda wote bada ya kutoa wakati wa kipindi cha uchaguzi.

“Ukiendea kifungu cha 4C cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kimesema Tume itatoa elimu ya mpiga kura.Lakini tumekuwa na tatizo la kutotoa elimu ya mpiga kura baada ya uchaguzi na imekuwa ikitolewa wakati wa uchaguzi baada ya uteuzi na wagombea wakiteuliwa leo kesho kampeni inaanza” alisema Bw. Kailima na kuongeza:

“Kama Tume na wadau wanaanza kutoa elimu ya mpiga kura katika kipindi hicho, sasa mpiga kura atazingatia kusikiliza kampeni za chama badala ya kusikiliza utaratibu mzima wa namna ya kupiga kura kama”

Alisema kwa kuwa Tume imeanza kutoa elimu ya mpiga kura katika kipindi chote cha mwaka itasaidia sana ifikapo uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kura zilizoharibika zitakuwa chache sana.

Kuhusu kura kuharibika, Bw. Kailima alisema kura yoyote iliyowekwa alama ya vema kwenye eneo la mgombea itahesabika kuwa kura halali.

“Kwa mujibu wa muongozo na maelekezo yaliyotolewa na Tume kwa wasiamamizi wa uchaguzi, alama yoyote ikiwemo ya X itakayowekwa kwenye chumba cha picha ya mgombea au jina la chama cha mgombea au kwenye chumba cha wazi itakubalika kwamba ni alama halali” alisema.

Alifafanua kuwa karatasi ya kura itakataliwa iwapo haina muhuri wa kituo au itakuwa na kitu au alama inayomtambulisha mpiga kura na iwapo, haijawekwa alama inayotambuliwa kuwa ni halali.

Aliongeza kuwa karatasi ya kura itakayopigwa kwa mgombea aliyejitoa kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi au ikawekwa alama kwa mgombea zaidi ya mmoja na iwapo haina alama yoyote, itakataliwa.

Hata hivyo, Bw. Kailima aliongeza kuwa uamuzi wa uhalali wa kura kituoni utaamuliwa na msimamizi wa kituo iwapo atarijiridhisha kuwa kura imeharibika na haiwezi kuhesabiwa na ataikataa na haitahesabiwa.

Tume imeanza kutekeleza mpango wa kutoa elimu ya mpiga kura kupitia vituo vya redio za kijamii katika mikoa yote ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ikiwa ni sehemu ya kutekeleza matakwa ya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi ya kutoa elimu ya mpiga kura muda wote.
 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani (kulia) akisalimiana na Meneja Mkuu wa Redio AFM ya Dodoma Bw. Tatenda J. Nyawo baada ya kutoa elimu ya mpiga kura kupitia redio hiyo hivi karibuni.

TANZANIA NA CHINA ZATILIANA SAINI MKATABA WA KUUZA BIDHAA ZA MUHOGO

0
0
Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano,Mhe.Prof Makame Mbarawa (Wa tatu kushoto waliosimama) akishuhudia Utiaji saini mkataba wa kuuza China bidhaa za muhogo kutoka Tanzania Mkataba huo umesainiwa leo mjini Beijing Jamhuri ya watu wa China kati ya Balozi wa Tanzania nchini China Mhe.Balozi Mbelwa Kairuki kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Li Yuanping Naibu Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya udhibiti na ukaguzi wa mazao kwa niaba ya Serikali ya jamhuri ya China Mhe.Mbarawa yupo mjini Beijing ambapo aliwakilisha serikali ya Tanzania kwenye mkutano wa One belt one Roads Forum.

Balozi wa Tanzania nchini China Mhe.Balozi Mbelwa Kairuki kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Li Yuanping Naibu mkurugenzi mkuu wa taasisi ya udhibiti na ukaguzi wa mazao kwa niaba ya Serikali ya jamhuri ya China wakitia saini mkataba wa kuuza China bidhaa za muhogo kutoka Tanzania .
Balozi wa Tanzania nchini China Mhe.Balozi Mbelwa Kairuki kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipeana mkono na Naibu Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya udhibiti na ukaguzi wa mazao, Li Yuanping kwa niaba ya Serikali ya jamhuri ya China mara baada ya kutiasaini mkataba wa kuuza China bidhaa za muhogo kutoka Tanzania .

NEWZ ALERT:MALIMA NA DEREVA WAKE WAFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU KWA TUHUMA ZA KUMSHAMBULIA ASKARI POLISI

0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Aliyekuwa Naibu Waziri wa fedha na mbunge wa Mkuranga, Adam Kigoma Malima amefikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kumshambulia askari polisi.

Malima anashtakiwa pamoja na dereva wake Ramadhani Mohamed Kigwande anayekabiliwa na tuhuma za kujeruhi.

Washtakiwa wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Wakili wa serikali, Mwanaamina Kombakono amedai, Mei 15 mwaka huu huko Masaki katika wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam mshtakiwa Malima alitenda kosa.

Imedaiwa, siku hiyo mshtakiwa Malima alimzuia afisa wa polisi mwenye namba H.7818 PC Abdul kufanya kazi yake ya kumkamata dereva wake Kigwande aliyekuwa amefanya kosa la kumjeruhi Joseph Mwita ambaye ni afisa operation wa Priscane Business Enterprises.

Kombakono ameongeza kuwa, siku na mahali hapo, mshtakiwa Kigwande kwa nia ya kukataa kukamatwa, alimjeruhi afisa operation hiyo(Joseph Mwita) ambaye alikuwa anakamatwa kwa kosa la kupaki gari vibaya na kumsababishia Mwita Majeraha Mwilini.

Watuhumiwa wote wamekana kutenda makosa hayo na wako nje kwa dhamana.mahakama imemtaka kila mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja atakaye saini dhamana ya milioni 5. Aidha Mahakama imemtaka kila mdhamini awe na barua ya utambulisho kutoka ofisi yoyote inayotambulika.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 15, mwaka huu ambapo kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi bado haujakamilika.Wakili Kibatala ameieleza mahakama kuwa, tarehe ya kutajwa kwa kesi hiyo atawasilisha pingamizi la awali juu ya mapungufu ya kisheria yaliyopo kwenye shtaka la shambulio linalomkabili Malima Peke yake.

Amedai kuwa, katika shtaka hilo maelezo ya kosa na tuhuma hazifanani.

RAIS WA ZANZIBAR DK,ALI MOHAMMED SHEIN AFANYA ZIARA YA KUWAFARIJI WAATHIRIKA WA UPEPO WILAYA YA MAGHARIBI B UNGUJA

0
0
 Baadhi ya nyumba zilizoathirika kutokana na Upepo mkubwa uliotokezea hapo jana katika shehia ya Kinuni,Mwanakwerekwe na Pangawe zikionekana kuezekwa na wenyewe. Jumla ya nyumba 123 ziliathirika kutokana na Upepo huo Wilaya ya Magharibi B unguja.
 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud katikati akiwatembelea pamoja na kuwafariji waathirika wa Upepo uliotokezea katika shehia ya Kinuni, Mwanakwerekwe na Pangawe ambapo jumla ya nyumba 123 ziliathirika kutokana na Upepo huo Wilaya ya Magharibi B unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohammed Shein akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Pangawe na Kijitoupele Shamsi Vuai Nahotha wakati alipofanya ziara ya kuwatembelea na kuwafariji waathirika wa Upepo uliotokezea katika shehia ya Kinuni,Mwanakwerekwe na Pangawe ambapo jumla ya nyumba 123 ziliathirika kutokana na Upepo huo Wilaya ya Magharibi B unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohammed Shein akipata maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud alipofanya ziara ya kuwatembelea na kuwafariji waathirika wa Upepo uliotokezea katika shehia ya Kinuni,Mwanakwerekwe na Pangawe ambapo jumla ya nyumba 123 ziliathirika kutokana na Upepo huo Wilaya ya Magharibi B unguja.PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

NAIBU SPIKA WA BUNGE ATEMBELEWA NA UGENI KUTOKA JHPIEGO

0
0
Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (kulia) akizungumza jambo pale alipotembelewa na ugeni kutoka Shirika la kimataifa lisilo la kiserikali linalotekeleza Miradi Mbali mbali ya Afya hapa nchini lijulikanalo kama Jhpiego, wakiongozwa na Rais na Mtendaji Mkuu wa Jhpiego wa Dunia Dkt. Leslie Mancuso (kushoto), Makamu wa Rais Mwandamizi, Dkt. Alain Damiba (katikati) katika kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.

Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson (kulia) akimsikiliza Rais na Mtendaji Mkuu wa Jhpiego wa Dunia Dkt. Leslie Mancuso (kushoto) akizungumza jambo wakati ugeni kutoka Shirika la kimataifa lisilo la kiserikali linalotekeleza Miradi Mbali mbali ya Afya hapa nchini lijulikanalo kama Jhpiego, lilipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. katikati ni Makamu wa Rais Mwandamizi, Dkt. Alain Damiba
Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson (kulia) akimsikiliza Rais na Mtendaji Mkuu wa Jhpiego wa Dunia Dkt. Leslie Mancuso (wa tatu kulia) akizungumza jambo pale ugeni kutoka  Shirika la kimataifa lisilo la kiserikali linalotekeleza Miradi Mbali mbali ya Afya hapa nchini lijulikanalo kama Jhpiego, ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

SERIKALI IMEKUSANYA BILIONI 63 KUPITIA MTAMBO WA KUHAKIKI NA KUSIMAMIA HUDUMA ZA MAWASILIANO YA SIMU NCHINI.

0
0
Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.

Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) imekusanya shilingi bilioni 63,015,450,230 kwa kipindi cha Octoba 2013 mpaka Februari 2017 tangu kuanzishwa kwa mtambo wa kuhakiki na kusimamia Huduma za Mawasiliano(TTMS) nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Edwin Ngonyani wakati akijibu swali la Mbunge wa Kigamboni Mhe.Dkt Faustine Engelbert leo Bungeni.

“Mtambo huu umesaidia Mamlaka ya Mawasiliano nchini kuongeza ufanisi katika kusimamia Sekta ya Mawasiliano pamoja na kwenda sambamba na kasi ya mabadiliko yanayotokea katika Sekta ya Mawasiliano Duniani kote”,Aliongeza Mhe.Ngonyani.

Aidha kati ya pesa izo bilioni 56,987,368,631 zimewasilishwa hazina na shilingi bilioni 6,028,081,599 zimewasilishwa Tume ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH) kwa ajili ya kugharamia tafiti mbalimbali zenye manufaa kwa nchi yetu ambapo kabla ya hapo kahukuwa na mapato hayo.

Amesema mtambo huu umeiwezesha TCRA kuwa na uwezo wa kusimamia mawasiliano ya simu za Kimataifa na zile za mwingiliano,pia mtambo huo umesaidia kudhibiti mawasiliano ya Simu za ulaghai za kimataifa na kusimamia ubora wa mitandao katika kutoa huduma bora kwa wananchi,kudhibiti namba tambulishi za vifaa vya mawasiliano nchini pamoja na usimamiaji wa miamala ya fedha  inayopita katika mitandao ya simu hapa nchini.

“Aidha pamoja na mafanikio hayo jitihada za kuboresha zaidi mfumo huu ili kuweza kubaini na kujiridhisha juu ya mapato yote yatokanayo na huduma za  mawasiliano na yanayokidhi mahitaji ya Mamlaka ya Mapato Tanzania,Benki kuu ya Tanzania na TCRA zinaendelea”Aliongeza Mhe.Ngonyani.

Aidha Serikali itaendelea kuwajengea uwezo wataalamu wa TCRA ili waweze kuendana na kasi ya ukuaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano hususani katika eneo hili la kuchakata taarifa mbalimbali za huduma za mawasiliano zinazopatikana kutoka kwa watoa huduma ili kuweza na kujiridhisha juu ya mapato yote.

APANDISHWA KIZIMBANI KWA KUTISHIA KUUA

0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Mkazi mmoja wa jijini Dar es Salaam anayefahamika kwa jina la Ahmad Khalifa amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu kwa kosa la kumtishia kumua Hawa Mshama.

Akisomewa mashtaka hayo katika Mahakama ya mwanzo Kinondoni mbele ya Hakimu Marko Mochiwa chini ya kifungu cha 89 -16 (2) mnamo tarehe 9/5/2017 eneo la Kinondoni Msisiri mshatikiwa alitoa lugha ya matusi kwa Bi Hawa Mshama .

Hata hivyo mshatikiwa alikana shitaka hilo na kuambiwa kuwa dhamana iko wazi na akishindwa ataenda mahabusu mpaka kesi hiyo itakapotajwa tena Mei 24.
Ahmad Khalifa akingizwa katika mahakama ya mwanzo Kinondoni
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images