Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1687 | 1688 | (Page 1689) | 1690 | 1691 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega amewatembelea wananchi wa Kijiji Tambani ambao hawana mawasiliano ya kuvuka kwenda kutokana na daraja kuchukuliwa na maji.

  Akizungumza na wananchi cha Tambani, Ulega amesema kuwa mvua hizo zimeleta athari hivyo unahitajika ufumbuzi wa haraka.

  Amesema usafiri wa mitumbwi si salama katika kutoa huduma ya usafiri kwa wananchi wa kijiji cha tambani na maeneo mengine. Kutokana na wananchi hao kukosa mawasiliano Mbunge huyo ametoa sh.milioni moja pamoja na mifuko ya saruji 100 ili kuweza kutengeneza daraja hilo.

  Wananchi wa kijiji hicho kwa kila kaya wamekubalina kutoa sh.10,000 ambazo zitafanya kazi katika ujenzi wa daraja hilo pamoja na nguvu zao zitatumika. Diwani wa Tambani, Ally Mtamilwa amsema kuwa ujio wa Mbunge wa jimbo la Mkuranga ameeta matumaini kwa wananchi na kuahidi nae kutoa mifuko 20 ya saruji.
  Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega akiwa katika kivuko ambacho si salama kuelekea upande wa pili alipotembelea kijiji cha tambani ambao wamekosa mawasiliano leo.

  Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega akikabidhi msaada wa sh.milioni moja kwa ajili ya ujenzi wa daraja lilichukuwa na maji katika kijiji cha Tambani.
  Wananchi wakisubiri kivuko ambacho si salama na kuwagharimu kulipa sh.500 kwa kila safari wanayoifanya kwenda katika vijiji vingine kupata mahitaji .(picha na Emmanuel Massaka Globu ya Jamii )
  Diwani wa Tambani , Ally Mtamilwa akizungumza na wananchi wake wakati wa ziara ya mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega.
  Wananchi wa wa kijiji cha Tambani ambao wamekosa mawasiliano kutokana na daraja kuchukuliwa na maji,wakimsikiliza Mbunge wao Mh. Abdallah Ulega aliekwenda kuwatembelea na kujionea hali halisi na leo.


  0 0

  MKUTANO maalum wa Kijiji cha Ikungi wilayani Ikungi mkoani Singida umemuondoa Mwenyekiti wa kijiji hicho Hussein Ikusi kutokana na matumizi mabaya ya madaraka kwa kufanya ubadhirifu wa mali za kijiji zenye thamani ya shilingi milioni 9.

  Ubadhirifu huo aliufanya toka alipoingia madarakani mwaka 2014 akishirikiana na aliyekuwa mtendaji wa kijiji hicho Hamis Isango aliyehamishiwa kijiji cha Irisya.

  Hayo yalibainika baada ya halmashauri ya kijiji kuitisha kikao maalum tarehe 24 aprili mwaka 2017 wakimtuhumu mwenyekiti kwa hoja zipatazo 5.

  Hoja hizo ni kushindwa kusimamia mali za kijiji,kushindwa kusimamia mipaka ya kijiji,kushindwa kuonyesha ushirikiano na uongozi wa halmashauri ya wilaya,Ofisi ya mkuu wa wilaya na taasisi za serikali zilizopo wilayani,kuwa chanzo cha migogoro badala ya kuwa mtatuzi na kushindwa kusimamia usomaji wa mapato na matumizi ya kijiji kwa mujibu wa sheria kwa kipindi cha miaka miwili na nusu.

  Ubadhirifu huo umebainishwa na mkaguzi wa mahesabu ya ndani Kitundu Mkumbo aliyeagizwa na mkuu wa wilaya hiyo Miraji Mtaturu kufanya ukaguzi wa mapato na matumizi ya kijiji baada ya kupokea tuhuma kuhusiana na mwenyekiti huyo.


  Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Ikungi waliohudhuria mkutano maalum wa kijijji hicho wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu hayupo pichani.Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu katikati akiwa na kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo Haika Massawe na kaimu mwenyekiti wa kijiji hicho Athuman Seleman wakiwa kwenye mkutano maalum wa kijiji.
  Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akizungumza na wananchi hawapo pichani kwenye mkutano maalum wa kijiji cha ikungi,kulia kwake ni kaimu mwenyekiti wa kijiji hicho Athuman Seleman na kushoto kwake ni kaimu mkurugenzi wa halmashauri Haika Massawe.
  Mkaguzi wa ndani wa halmashauri ya Ikungi Kitundu Mkumbo akisoma taarifa ya ukaguzi mbele ya mkutano maalum wa kijiji cha Ikungi.  0 0


  NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

  WANANCHI visiwani vya Zanzibar wameshauriwa kuendeleza kwa vitendo Utamaduni wa uzalendo wa kusaidiana wakati wa maafa mbali mbali yanayotokea nchini bila kujadili tofauti za kisiasa na kidini.

  Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Saadala “ Mabodi” mara baada ya ujenzi wa nyumba ya Balozi wa Nyumba kumi Bi. Asha Abdalla Baruti iliyobomoka kutokana na maafa ya mvua zinazonyesha nchini, huko Fuoni Migombani.

  Dkt. Mabodi alisema maafa yanapotokea hayachagui sehemu ya kuathiri bali yanawakumba wananchi wote hivyo ni muhimu wanajamii kushirikiana kwa mambo ya kijamii na kimaendeleo na kuacha siasa za utengano na chuki.

  Ujenzi huo umefanyika kutokana na agizo la Naibu Katibu Mkuu huyo alipowataka uongozi wa CCM na UVCCM Wilaya ya Dimani Unguja, kumjengea makaazi ya muda mwananchi huyo ambaye hakuwa na sehemu ya kuishi kutokana na nyumba yake kuharibiwa na mvua zilizonyesha hivi karibuni.

  Alisema hatua ya Chama hicho kutoa msaada na kushiriki katika masuala ya shughuli za kijamii kwa wananchi itakuwa ni utamaduni endelevu kwa Unguja na Pemba.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdalla Juma Saadala “ Mabodi” na kushoto ni Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Nd. Abdulghafar Idrissa akifanya kazi ya kukandika udongo katika nyumba ya mwananchi Bi. Asha Abdalla wa Shehia ya Fuoni Migombani aliyebomokewa nyumba yake kutokana na maafa ya mvua zilizonyesha juzi Unguja.
  Baadhi ya wananchi wakiwa katika harakati za ujenzi wa nyumba hiyo uko Fuoni Migombani Unguja.
  Baadhi ya wananchi wakiwa katika harakati za ujenzi wa nyumba hiyo uko Fuoni Migombani Unguja.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdalla Juma Saadala “ Mabodi” akitoa shukrani zake kwa wananchi mbali mbali walioshiriki katika ujenzi huo na kuhakikisha Bi.Asha Abdalla anapata makaazi ya kuishi. Picha na Afisi Kuu CCM Zanzibar.


  0 0

  Mkurugenzi wa Michezo Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Yusufu Singo (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa mashindano ya mbio ya Km 21 ya Dasani Marathon 2017 baada ya kuwakabidhi zawadi zao eneo la Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay Dar es Salaam leo. 
  Mshindi wa kwanza, Augustine Sule (aliyesimama juu), Mshindi wa pili Stephano Huche (wa pili kushoto) na mshindi wa tatu Said Makula. Kushoto ni Nalaka Hettierachchi Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Coca Cola Kwanza iliyodhamini mashindano hayo kupitia kinywaji cha maji ya Dasani.
  Kwa upande wa walemavu aliyeshinda ni Shukuru Khalfan, wa pili alikuwa Mathias John na Jonis Stephano alishika nafasi ya tatu.Mshindi wa kwanza wa mbio za Km 21 kwa upande wa wanaume na wanawake kila mmoja alikabidhiwa sh. mil 1, wa pili sh. 750,000 na wa tatu sh. 600,000.
  Baadhi ya washiriki wakimalizia mbio zao katika Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay
  Washiriki wakivishwa medali baada ya kumaliza kukimbia katika mashindano hayo
  Elizabeth Ikengo wa NMB Bank akivishwa medali baada ya kumaliza mbio hizo

  Timu ya NMB Bank iliyoshiriki katika mashindano hayo.

  0 0


  0 0
  0 0

   Mkurugenzi wa kampuni ya Yara Mr. Alexandre Macedo (kati) akikata utepe kuashiria  uzinduzi wa ghala la kuhifadhi mbolea nchini Rwanda. Mr. Macedo ni msimamizi pia wa Yara Rwanda na Burundi ambapo hupata huduma zake za mbolea kupitia Tanzania
   Afisa kilimo mwandamizi  wa kampuni ya kuzalisha na kusambaza mbolea Yara Tanzania Ltd, Bw.Maulidi  Mkima (katikati) akiwa shambani kwa mkulima wa viazi katika kijiji cha Simambwe Wilaya ya Mbeya Furaha Ngala (kushoto) kwa ajili kukagua maendeleo ya zao hilo baada ya kutumia mbolea ya YaraMila WINNER, YaraLiva NITRABOR na YaraVita TRACEL BZ mpangilio wa lisha linganifu kwenye viazi. Kulia ni bwana shamba msaidizi wa kampuni hiyo kutoka Mbeya Medson Joseph
   Afisa kilimo wa kampuni ya uzalishai na usambazaji wa pembejeo za kilimo Yara Tanzania Ltd, Bw. Maulid Mkina kushoto akitoa elimu juu ya matumizi bora ya mbolea ya YaraMila WINNER, YaraLiva NITRABOR na YaraVita TRACEL BZ kwa ajili ya viazi kwa wakulima wa viazi katika kijiji cha Simambwe Wilaya ya Mbeya wa tatu ni mmiliki wa shamba hilo Bw.Furaha Ngala
  Afisa kilimo kutoka kampuni ya Yara Tanzania Ltd wazalishaji na wasambazaji wa mbolea mbalimbali  Bw. Maulid Mkima akiwa na mkulima wa viazi katika kijiji cha Simambwe Wilaya ya Mbeya Bw. Furaha alipotembelea shambani kwake na kuona matokea ya zao hilo baada ya kutumia mbolea aina ya YaraMila WINNER, YaraLiva NITRABOR na YaraVita TRACEL BZ.

  0 0  0 0

  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Iddi Mgwatu, ametembelea na kukagua kivuko cha MV. Nyerere kinachotoa huduma kati ya Bugorola na Ukara katika kisiwa cha Ukerewe mkoa wa Mwanza na kujionea utendaji kazi wa kivuko hicho pamoja na changamoto zake.

  Akiongea na watumishi wa kivuko hicho baada ya kujionea changamoto ya uendeshaji wa kivuko hicho, Dkt. Mgwatu alisema “tutanunua injini mbili mpya na kukifanyia matengezo ya kinga kivuko hiki ili kuongeza zaidi ufanisi wake na hatimae kiweze kusafirisha abiria na mali zao kwa haraka zaidi na katika hali ya usalama mkubwa kwani injini zilizoko sasa zimechoka hivyo kushindwa kuendesha kivuko ipasavyo.”

  Aidha Dkt. Mgwatu aliwataka watumishi wa kivuko cha MV. Nyerere kufanya kazi kwa bidii sambamba na kuziba mianya ya uvujaji wa mapato ya serikali, pamoja na kuzingatia weledi na uadilifu katika utendaji wa kazi.

  Katika hatua nyingine, Dkt. Mgwatu alitembelea kivuko cha MV. Mara katika Mkoa wa Mara pamoja na kivuko cha MV. Ruvuvu katika mkoa wa Kagera na kujionea utendaji kazi wa vivuko hivyo pamoja na changamoto zake.
  Kivuko cha MV. Nyerere kinachotoa huduma kati ya Bugorola na Ukara katika kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza.
  Fundi wa kivuko cha MV. Nyerere akionyesha utendaji wa injini mojawapo ya kivuko cha MV. Nyerere kinachotoa huduma kati ya Bugorola na Ukara katika kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza. Nyuma yake ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Iddi Mgwatu.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Iddi Mgwatu (wa pili kushoto) akiangalia utendaji kazi wa moja ya injini ya kivuko cha MV. Nyerere katika chumba cha mifumo ya kuendeshea kivuko hicho. Kivuko cha MV. Nyerere kinatoa huduma kati ya Bugorola na Ukara katika kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza.
  Kivuko cha MV. Mara kinachotoa huduma kati ya Iramba na Majita mkoani Mara.
  Kivuko cha MV. Ruvuvu kinachotoa huduma katika eneo la Rusumo Mkoani Kagera. Picha na Theresia Mwami.

  0 0
  0 0


   Michezo ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari-UMISSETA Copa Coca- Cola kwa Mkoa wa Mbeya imezinduliwa rasmi mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Sokoine na uzinduzi huo ulionogeshwa na wachezaji wa timu ya soka ya Mbeya City ambao walishiriki kufanya mazoezi na timu za wanafunzi na kutoa ushuhuda wa michezo hiyo ilivyoibua vipaji vyao.

  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Amos Makalla,ambaye alikuwa mgeni rasmi anataka kuwaona vijana wengi wakishiriki mazoezi na michezo mbalimbali kwa kuwa michezo kama ilivyo hii ya UMISSETA Inaibua na kukuza vipaji pia sekta ya michezo bado inazo fursa nyingi za kujiajiri. 

  Alisema kampuni ya Coca- Cola imeonyesha njia kwa kudhamini michezo hii na kutoa wito kwa makampuni mengine kujitokeza kudhamini michezo ya vijana kwa kuwa ndio tanuru la kuwaandaa wachezaji na kuibua vipaji. ‘’Leo hii tunaona hawa vijana wa Mbeya City wapo hapa kutoa ushuhuda wao, wanapokea mpunga (mshahara) wa maana lakini chimbuko lao wametokea kwenye michezo hii ya Copa Coca- Cola. 

  Naamini kupitia michezo hii Mbeya tutapata wachezaji wengi zaidi’.Alisema. Ofisa Msaidizi Masoko wa Coca- Cola Pamela Lugenge, alisema lengo la kampuni ya Coca Cola kuuungana na Serikali kupitia UMISSETA ni kuona wanaibua vipaji vingi vya vijana walioko shule za sekondari ambako wanaamini ndiko chimbuko la kupata timu ya taifa na klabu mbalimbali nchini.
  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa michezo ya Umisseta Copa Coca Cola katika uwanja wa Sokoine mjini Mbeya mwishoni mwa wiki.
  Meneja Masoko Msaidizi wa Coca-Cola,Pamela Lugenge,akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa michezo ya Umisseta Copa Coca Cola katika uwanja wa Sokoine mjini Mbeya mwishoni mwa wiki.
  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, akikabidhi vifaa vya michezo kwa timu za shule zitakazoshiriki mashindano ya UMISSETA Copa Coca-Cola wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo mwishoni mwa wiki.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Teddy na Talkia Tumbi ambao ni mtu na dada yake wamefanya uzinduzi wa studio ya nywele na kuuza shanga na vito (jewelry) iliyopo kwenye mji wa Clemmons, North Carolina nchini Marekani. Studio hiyo ambayo ilizinduliwa siku ya Jumamosi May 13, 2017 ilihudhuriwa na Watanzania mbalimbali waliofika kuwaunga mkono.
  Teddy Tumbi akimwandalia mteja (hayupo pichani)shanga alizonunua kwenye studio yao iliyofunguliwa siku ya Jumamosi May 13, 2017 Clemmons, North Carolina nchini Marekani. Studio hii ya kutengeneza nywele na kuuza shanga na vito (Jewelry) na anuani kamili ni 2575 Old Glory Road, Clemmons, NC 27012 simu 336 343 8170.

  Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Watanzania North Carolina, Bi. Glory Alex akipata matunda ya ufunguzi wa studio hiyo kwa kutengeneza nywele zake alipokwenda kuwaunga mkono Teddy na Talkia Tumbi mtu na dada yake walipofungua studio ya nywele na kuuza shanga na vito.

  Mmoja ya wateja akitengeneza urembo wa nywele studioni hapo.
   
  Muonekano wa studio.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeahidi kuajiri watumishi wa idara ya afya ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi na watumishi ambao wameondolewa katika utumishi wa umma kwa kukosa sifa ya kuwa na vyeti halisi baada ya zoezi la uhakiki wa vyeti nchini.

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameyasema hayo jana wakati wa maadhimsho ya Siku ya Wauguzi Duniani ambapo kitaifa imefanyika katika hospitali ya St. Gasper, Itigi Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.

  Waziri Ummy amesema serikali inatambua mzigo mkubwa wa majukumu kutokana na uhaba wa wauguzi ambao umesababishwa na baadhi yao kuondolewa katika utumishi kwa kukosa vyeti halisi na hivyo imetenga bajeti ya kuajiri wauguzi wa kutosha nchini huku akiahidi kutoa kipaumbele kwa mkoa wa Singida.

  “Kuna baadhi ya Zahanati na vituo vya afya vimefungwa kwa kutokana na sakata la vyeti feki, lakini pia tunatambua kuwa wauguzi hamtoshi na hivyo kupelekea muuguzi mmoja kutoa huduma kwa wagonjwa wengi, hali hii inapunguza ufanisi wenu na kuwanyima haki ya kupumzika”, ameongeza Waziri Ummy.

  Aidha ameagiza waajiri wa utumishi wa umma na hasa halmashauri zote nchini kupeleka maombi ya watumishi wa kada za afya ili wizara iweze kutangaza nafasi hizo zijazwe na watanzania wenye sifa huku akisisitiza kuwa nia ya serikali ya awamu ya tano ni kuboresha huduma za afya kwa wananchi.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisisitiza jambo katika maadhimisho ya siku ya wauguzi iliyofanyika kitaifa katika hospitali ya St. Gasper Itigi, Mkoani Singida.
  Wauguzi kutoka mikoa mbalimbali nchini wakila kiapo cha uuguzi katika maadhimisho ya siku ya wauguzi iliyofanyika kitaifa katika hospitali ya St. Gasper Itigi, Mkoani Singida.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiwakaribisha wauguzi kutoka mikoa mbalimbali nchini pamoja na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu katika maadhimisho ya siku ya wauguzi iliyofanyika kitaifa katika hospitali ya St. Gasper Itigi, Mkoani Singida.
  Wauguzi kutoka mikoa mbalimbali nchini wakiandamana na kuonyesha ujumbe mbalimbali mbele ya Mgeni rasmi Waziri wa Afya Ummy Mwakimu katika maadhimisho ya siku ya wauguzi iliyofanyika kitaifa katika hospitali ya St. Gasper Itigi, Mkoani Singida.
  Waziri wa Afya Ummy Mwakimu akisaini zawadi ya mafuta ya alizeti aliyopewa na wenyeji wake halmashauri ya Itigi katika maadhimisho ya siku ya wauguzi iliyofanyika kitaifa katika hospitali ya St. Gasper Itigi, Mkoani Singida.  0 0

  Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora Dk. Laurian Ndumbaro (kushoto) akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya za Mamlaka za Serikali za Mitaa (ALAT) Steven Mhapa (katikati) wakati wakiingia ukumbi wa Mikutano wa chuo cha Ufundi Morogoro kufunga mafunzo ya Mameya, Wenyeviti wa Halmashauri, Madiwani na Waandishi wa Mihutasari wa Vikao vya Halmashauri mbalimbali nchini. Kulia ni Mkuu wa Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Dk Henry Mambo. TPSC ndio wanaendesha mafunzo hayo. 
  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Utumishi na Utawala Bora Dk. Laurian Ndumbaro kwa Mameya, Wenyeviti wa Halmashauri, Madiwani na Waandishi wa Mihutasari wa Vikao vya Halmashauri , wa kwanza kushoto ni Gulahamfeez Mkadam Mwenyekiti wa Jumuiya za Mamlaka za Serikali za Mitaa (ALAT) ,wa tatu kushoto ni Meya wa Manispaa ya Morogoro Paschal Kihanga na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania Dk.Henry Mambo. TPSC iliendesha mafunzo hayo kwa kushirikiana na ALAT. 
  Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Dk. Henry Mambo akizungumza wakati wa mafunzo kwa Mameya, Wenyeviti wa Halmashauri, Madiwani na Waandishi wa Mihutasari wa Vikao vya Halmashauri mbalimbali nchini, mafunzo hayo ambayo yaliendeshwa na TPSC kwa kushirikiana na ALAT.
  Baadhi ya wajumbe wa mafunzo ya Mameya, Wenyeviti wa Halmashauri, Madiwani na Waandishi wa Mihutasari wa Vikao vya Halmashauri mbalimbali nchini wakifuatilia mafunzo hayo ambayo yaliendeshwa na TPSC kwa kushirikiana na ALAT.

  0 0

  Mwanamitindo, muigizaji  na Miss Tanzania namba mbili 2006, Jokate Mwegelo ametoa wito kwa watu maarufu nchini kusaidia kuondoa changamoto katika sekta mbalimbali ili kupunguza mzigo kwa serikali. Jokate alisema hayo wakati wa mahafali ya wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya Sekondari ya Jangwani ambapo jumla ya wanafunzi 118 walihitimu katika shule hiyo.

  Mrembo huyo ambaye ni Kaimu Katibu Hamasa wa Chipukizi wa  Umoja wa Vijana  wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) amesema kuwa Tanzania ina watu wengi maarufu na wenye uwezo, lakini wachache tu ndiyo wamekuwa wakijitolea kusaidia sekta mbalimbali husasani elimu na afya.

  Alisema kuwa kwa hali ilivyosasa, ni vigumu kwa serikali kutatua matatizo yote na kuwaomba  wanamuziki, wasanii, wafanyabiashara na viongozi mbalimbali wa vyama na serikali kujitolea kusaidia kutatua matatizo katika jamii.

  Alifafanua kuwa shule ya wasichana ya Jangwani ni kongwe  kutokana na kuanzishwa Mei 28, 1928, lakini mpaka sasa inakabiliwa na matatizo mbalimbali wakati kuna wahitimu wengi ambao kwa sasa wana nyandhifa na wanashindwa kuchangia.

  “Mimi sijasoma Jangwani, lakini niliguswa na matatizo ya viwanja vya michezo na kuamua kujenga uwanja wa mpira wa kikapu na mpira wa pete (netiboli), nashukuru viwanja kwa sasa vinatumiwa na shule zinazozunguka maeneo haya,naomba wengine wasaidie, kuondoa changamoto zilizopo,” alisema Jokate.

  Mrembo huyo pia amewaomba viongozi wa serikali na wafanyabiashara  waliosoma katika shule ya Sekondari ya wasichana ya Jangwani, kusaidia kuondoa changamoto za shule hiyo.

  Awali, Makamu Mkuu wa Shule hiyo, Amos Mgongolwa alisema mbali ya uchakavu wa majengo, shule yao haina madarasa na mabweni ya kutosha, haina  ukumbi wa kufanyia shughuli mbalimbali kama sherehe na kulazimika kufanyia eneo la wazi, shule haina hata gari moja kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwa pamoja na matibabu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.

  Mgongolwa amesema wanafunzi wenye mahitaji maalum, ulazimika kutumia baiskeli za miguu mitatu ili kwenda  kwenye shughuli mbalimbali za kimamoso nje ya shule.
  Miss Tanzania namba mbili 2006 na Kaimu Katibu Hamasa wa Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Jokate Mwegelo akikabidhi zawadi mbalimbali kwa wanafunzi wa Kidato cha Sita wa shule ya Sekondari ya Jangwani mara baada ya kumaliza mtihani wao.
  Miss Tanzania namba mbili 2006 na Kaimu Katibu Hamasa wa Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Jokate Mwegelo akikabidhi cheti kwa wanafunzi wa Kidato cha Sita wa shule ya Sekondari ya Jangwani mara baada ya kumaliza mtihani wao.
  Kaimu Mkuu wa shule ya Jangwani, Amos Mgongolwa akizungumza katika mahafali hayo.
  Jokate Mwegelo akizungumza katika mahafali hayo.

  0 0

  Karibu Cultural Promotions Organization in collaboration with Legendary Music Entertainment and Promotions Company Limited are organizing the 4th edition of the “Karibu Music Festival”, an annual Three (03) Days International cultural event aiming at African Culture Promotion to the world, as well as introducing other countries’ culture to Africa, and building up friendship/collaboration opportunities among all participants. In the aspects of music, dance, paintings, theater, crafts, and many others, all artists who can share our passion and goal together, you are welcomed to participate in this event to present your great talents and promote yourself!

  The festival involves International artists from Africa, Europe, America, and Asia who will perform at the main stage and conduct their unique Workshop classes. This will be 100% LIVE performance among 3 days!! It will also feature Musicians selling and showcasing their CDs (Albums), craftsmen and artisans selling unique products, cultural food and drink vendors, Also a Cinema and graffiti venues for more art adventures. The big Live performance stage with the high quality sound system from Legendary Music will be set nearby the College of Arts and Culture Bagamoyo-TASUBA, from 3rd (Fri) – 5th (Sun) NOVEMBER 2017. Let us share the wonderful moment on the stage!!!

  All application must be submitted through the link below.


  0 0


  0 0

  Mabalozi wa Kundi la Mtandao wa Kijamii wa Whatsaap la Saratani Info wakiwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC tayari kutembelea kitengo cha Saratani katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC.
  Mabalozi wa Kundi la Mtandao wa Kijamii wa Whatsaap la Saratani Info wakiwa wamebeba zawadi mbalimbali kwa ajili ya kutoa kwa wagonjwa wa Saratani katika Hosptali ya Rufaa ya KCMC.
  Mkuu wa Kitengo cha Saratani katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC,Dkt Furaha Silventi akizungumza na mabalozi wa kundi la Saratani Info lilipotmbelea kitengo hicho.


  0 0

  SERIKALI yaja na mpango mkakati wa kudumisha matibabu ya uzazi pingamizi ili kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano nchini Tanzania. 

  Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati waa ufunguzi wa mkutano wa nne wa`masuala ya Ganzi uliofanyika jijini Dar es salaam. 

  “Huwezi kutoa huduma bora na salama ya uzazi pingamizi bila kuwa na wataalamu wa ganzi ili kufanywa upasuaji usio na maumivu hivyo katika mkutano huu tunapanga kuwa na wataalamu wengi wa huduma hiyo ili kutoa huduma bora nchini. 

  Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa licha ya kudumisha matbabu ya uzazi pingamizi pia Serikali imejidhatiti kujenga vituo vya afya vinavyotoa huduma hiyo kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla. 

  Mbali na hayo Dkt. Ulisubisya amesema kuwa mkutano huo unalenga kutoka na malengo ya kutoa huduma bora kwa wagonjwa mahututi pamoja na kutoa huduma ya ganzi kwa wanaohitaji kupasuliwa. Mkutano huo ulioandaliwa na Chama cha Wataalam Wa Ganzi nchini (SATA) umeudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka Sweden,Cameroon, Marekani , Tanzania ili kuweza kujua mchango wa kupunguza vifo vya wajawazito kutokana na huduma ya ganzi.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa ufunguzi wa mkutano wa nne wa`masuala ya Ganzi uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
  Waandishi wa habari wakimsikilliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.


  0 0

  Uandikishaji ulifanyika Tegeta Complex jijini Dar es Salaam huku timu zaidi ya 20 zikijitokeza kujiandikisha. Michuani ya Sprite Bball Kings inaendeshwa na kituo cha Televisheni na Radio cha East Africa (EATV/Radio) kwa udhamini wakampuni ya Coca-Cola. 

  Ikiwa ni siku ya kwanza kwa timu mbali mbali za michuani ya kikapu ya Bball Kings, zaidi ya timu 20 zimejitokeza kujiandikisha mwishoni mwa wiki hii wakati wa zoezi la uandikishaji linaloendelea jijini Dar es Salaam. 

   Michuani ya mchezo wa kikapu ya Bball Kings inayoendeshwa na kituo cha Televisheni na Radio cha East Africa (EATV/Radio) kwa kushirikiana na Kampuni ya Coca-Cola kupitia kinywaji chake cha Sprite siku ya jumamosi imeshuhudia wawakilishi wa timu mbalimbali wakijitokeza na kujaza fomu za ushiriki, huku wawakilishi wa timu hizo wakijigamba kujidhatiti kikamilifu kuchukua ubingwa wa mwaka huu. 

  Kati ya timu zilizojitokeza ni pamoja na Cavarious, Lycans, Tegeta Camp, Lord Baden, K-Warriors, DMI, St Joseph na MJ Junior. Nyingine ni Oilers, TMT, Mchenga, Bahari Beach, Street Boys, Street Warriors, Chanika Legends, God With Us, Weusi Basketball Club, Junior Basketball Club na Celestial Basketball Team. 

   Akizungumza wakati wa uandikishaji wa timu shiriki, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na Masoko wa wa EATV, Roy Mbowe alisema mwitikio wa timu mbalimbali umejaa hamasa kubwa na wa kuridhisha, huku kila timu iliyojitokeza ikiwa na wachezaji wasiozidi 10.

   “Mashindano hayo yanahusu vijana wenye umri wa kuanzia miaka 16 na watapaswa kuunda timu ya wachezaji 10 ambao watachuana na timu nyingine zitakazokuwa zimejiandikisha, huku tukitoa fursa katika wachezaji hao 10, timu inaweza kuwa na wachezaji wasiozidi watatu kutoka katika timu kubwa za Ligi Darasa la Kwanza za za kikapu za hapa nchini,’’alisema Mbowe. 

  Michuano ya Sprite Bball Kings itaendeshwa kwa njia ya mtoano katika hatua ya kwanza ili kupata timu 16 zitakazoingia hatua ya pili na kutaja zawadi kwa timu itakayotwaa ubingwa itakuwa ni Sh.milioni 10 wakati mshindi wa pili atapata Sh.milioni tatu huku pia kukiwa na zawadi ya Sh milioni mbili kwa mchezaji bora (MVP). Mashindano hayo yatakayoshirikisha wachezaji kutoka mikoa yote nchini, yanatarajiwa kuanza mwezi huu na kumalizika Julai mwanzoni.
  Kiongozi wa timu ya mpira wa kikapu ya Weusi Basketball Club ya jijini Dar es Salaam, Mntambo Mngeja (kulia) akipata maelekezo ya juu ya kujiandikisha kutoka kwa mratibu ya michuano ya Sprite Bball Kings, Basilisa Biseko wakati wa zoezi la uandikishaji wa timu mbalimbali kwa ajili ya ushiriki wa michuano hiyo. 

older | 1 | .... | 1687 | 1688 | (Page 1689) | 1690 | 1691 | .... | 3286 | newer