Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109921 articles
Browse latest View live

BENKI YA NMB YAFANIKISHA SIKU YA WAUGUZI MKOANI GEITA

$
0
0
Mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali mstaafu Ezikiel Elias Kyunga akiwa kwenye picha ya pamoja na kamati ya ulinzi na usalama pamoja na mwakilishi wa makampuni ambayo yamefadhili shughuli ya siku ya wauguzi ambapo Benki ya NMB iliwakilishwa na Meneja Mahusiano Biashara za Serikali Kanda ya Ziwa, Suma Mwainunu.
Meneja Mahusiano Biashara za Serikali Kanda ya Ziwa wa Benki ya NMB, Suma Mwainunu akitoa shukrani kwa wao kama Benki kushirikishwa kwenye shughuli hiyo ya siku ya wauguzi Duniani huku akihaidi kuwa Benki yao itaendelea kushirikiana na serikali katika juhudi zake mbalimbali.
Sehemu ya Washiriki siku ya wauguzi iliyofanyika Mkoani Geita hivi karibuni.

RambiRambi kutoka Korea ya Kusini

NEWS ALERT: TRENI YA ABIRIA ILIYOKUWA IKIELEKEA BARA YAACHA NJIA, MAZIMBU MOROGORO

$
0
0
 Treni ya abiria iliyokuwa ikitokea jijini Dar es salaam kwenda Mikoa ya Tabora, Mwanza na Kigoma, imepata ajali usiku wa kuamkia leo katika eneo la stesheni ya Mazimbu Mkoani Morogoro.

Kwa mujimu wa Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Reli Tanzani, Midladjy Maez amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa tano usiku baada ya Mabehewa matatu kuacha njia na mengine manne kuegama na kusababisha abiria mmoja alietambulika kwa jina la Ashura Mrisho aliyekuwa akitokea Ngerengere kwenda Tabora kujeruhiwa na baada ya kuangukiwa na mizigo. 
Mabehewa 13 yamerejeshwa Morogoro ili kufanyika utaratibu wa kuwapangia usafiri mbadala abiria wa treni hiyo. Taarifa zaidi zitafuata wakati Uongozi wa TRL, Wahandisi na Mafundi wa reli wakishughulikia ajali hiyo.

KCB BANK YAPELEKA DIASPORA BANJKING NCHINI MAREKANI

SI KWELI KWAMBA TUMEMKADIRIA SHILINGI MILIONI 400 MSANII DIAMMOND-KAYOMBO

$
0
0

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said .

MKURUGENZI wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Richard Kayombo, ameendelea kukanusha kwamba, Mamlaka hiyo haijamkadiria msanii wa muziki wa kizazi kipya,Nassib Abdul ( Diamond Platnamuz) kulipa kodi ya shilingi Milioni 400. 

Hayo ameyasema leo Mei 13, 2017 wakati akifafanua hoja mbalimbali kwa waandishi wa habari wanaoshiriki semina ya siku moja iliyoandaliwa na TRA ili kutoa elimu ya ulipaji kodi kwa waaandishi na kufanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam. 

“Tuko kwenye hatua za awali za mazungumzo bado hatujakadiria kodi amnayopaswa kulipa Diamond, na kwa bahatio nzuri tumekaa naye na bado tuko kwenye mazungumzo na sio kweli kwamba tumemkadiria shilingi Milioni 400,” Alisema na kuongeza .

“Tunajaribu kujua vyanzo vyake vya mapato, lakini hata kama imetokea mtu umekadiriwa kulipa kodi kwa kiasi Fulani na hujaridhika unayo nafasi ya kukata rufaa kwa Kamishna Mkuu wa TRA, na ndapo hujaridhika na rufaa hiyo ipo Mamlaka nhyingine ambayo iko nje ya TRA, Tax Tribunal, na bodi ya Rufaa za kodi.” Alifafanua Bw.Kayombo. 

“Hivyo mtu asiwe mnyonge anayo nafasi ya kukata rufaa, tatu ndani ya TRA, na mbili nje ya TRA ikiwa ni pamoja na Mahakamani, kwa hivyo watu wasiogope. Alisema. Awali akifungua semina hiyo. Bw. Kayombo aliwaasa waandishi wa habari kujenga uzalendo kwa kuunga mkono juhudi za Mamlaka ya Mapato Tanania TRA, katika kuelimisha umma umuhimu wa kulipa kodi ili kuiwezesha serikali kutoa huduma stahiki kwa wananchi. 

“Najua kihistoria linapokuja swala la kulipa kodi huwa kuna changamoto nyingi watu kuelewa swala hili, lakini napenda niwaeleze ndugu zangu, ili kuiwezesha serikali kutoa huduma stahiki kwa wananchi ni lazima watu walipe kodi, hivyo waandishi wa habari mnao wajibu mkubwa kutumia taaluma yenu kuelimisha umma umuhimu wa kulipa kodi, Alisema Bw. Kayombo. 

Kayombo amesema, TRA kwa niaba ya serikali ya ndiyo chombo chenye mamlaka ya kukusanya kodi za serikali kutoka kwa watu binafsi, makampuni na taasisi za umma. 

“Huduma za usafiri, elimu, afya na miundombinu itakuwa bora tu endapo wananchi watatimiza wajibu wao wa kulipa kodi.” Alisema na kuongeza katika semina hii waandishi wa habari watapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo kodi ikiwemo kodi ya majengo kutoka kwa watalamu wa kodi wa TRA.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA), Bw. Richard Kayombo (katikati), akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina ya siku moja ya ujasiriamali na elimu ya kulipa kodi kwa waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam leo Mei 13, 2017. Kulia ni Mwenyekiti wa semina hiyo, Bi. Angella Msangi na kushoto ni Afisa Kodi Mkuu wa TRA, Bw.Mwangosi 
Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TRA, Bi. Rachael Mkundai, (kulia), akiwakaribisha waandishi wa habari kwenye semina. Kushoto ni Mwenyekiti wa semina, Bi. Angella Msangi .
Mkutano huo ukiendelea
Waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya ufunguzi .

HOSPITALI YA MKURANGA YAPOKEA MSAADA WA VIFAA VYA WODI YA WAZAZI KUTOKA TAASISI YA DHI-NUREYN

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii .

HOSPITALI ya Wilaya ya Mkuranga imepata msaada wa wodi ya wazazi vyenye thamani ya sh. Milioni 65 kutoka kwaTaasisi ya Dhi Nureyn .

Akizungumza baada ya makabidhiano ya vifaa wodi ya wazazi , Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega amesema kuwa wodi ya wazazi katika hospitali hiyo ilikuwa na hali mbaya kwa kukosa vitu muhimu ambavyo vinasababisha kupoteza maisha kwa mama au mtoto .

Amesema kuwa kutokana na wanawake wa Wilaya walikuwa hawana uhakika katika masuala ya uzazi lakini sasa suluhisho limepatikana kwa taasisi hiyo kutoa vitu hivyo katika kuokoa maisha ya mama na mtoto katika hospitali hiyo .

Ulega amesema kuwa kutokana tatizo hilo aliamua kwenda kuomba katika taasisi ya Dhi-Nureyn ambao waliangalia mahitaji katika wodi ya wazazi na kuamua kutoa msaada huo licha kuwa na changamoto zingine katika hospitali ya Mkuranga .

Nae Mwenyekiti wa taasisi ya Dhi-Nureyn , Sheikh Said Abri amesema kuwa baada ya kupata maombi kutoka kwa Mbunge wa Mkuranga ,Abdallah Ulega juu ya hospitali ya Wilaya ya Mkuranga hasa katika kuokoa maisha mama na mtoto tuliona jambo la msingi kutekeleza.

Amesema kuwa wataendelea kuwa kusaidia kadri ya uwezo unapopatikana ili hospitali hiyo kuendelea kutoa huduma bora kwa kuwa na vifaa vinavyostahili katika kuhudumia wananchi.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkuranga, Steven Mwandambo amesema kuwa msaada huo umekuja kwa wakati mwafaka kutokana na vifaa hivyo kukosekana kwa muda mrefu huku mipango ilikuwa ikifanyika.
 Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega akiwa na viongozi wa Wilaya ya Mkuranga wakikabidhiwa vifaa vya Wodi ya wazazi kutoka kwa watendaji wa Taasisi ya Dhi-Nureyn katika Hafla ilyofanyika Mkuranga.
 Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega akiwa na viongozi wa Wilaya ya Mkuranga wakikabidhiwa vifaa vya Wodi ya wazazi kutoka kwa watendaji wa Taasisi ya Dhi-Nureyn katika Hafla ilyofanyika Mkuranga.
.

 Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega Akizungumza na wananchi wakati wa makabidhibiano ya vifaa katika wodi ya wazazi katika hospitali ya Mkuranga leo jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Taasisi ya Dhi-Nureyn,Shekh Said Abri akizungumza juu msaada huo waliotoa katika hospitali ya Wilaya ya Mkuranga.Picha na Chalila Kibuda-Globu ya Jamii Mkuranga.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MAKUSANYO YA KODI YA PANGO LA ARDHI YAONGEZEKA MARADUFU.

$
0
0

Na. Hassan Mabuye, Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Ardhi.

Serikali imefanikiwa kukusanya jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 76 cha makusanyo ya kodi ya pango la ardhi hadi kufikia tarehe 13 Mei 2017 kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa.

Akiongea katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Yamungu Kayandabila amesema kiwango cha makusanyo ya kodi ya ardhi hakijawahi kufukiwa ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo kwa sasa Wizara ya Ardhi imeisha kusanya kiasi cha shilingi bilioni 76 cha kodi ya pango la ardhi.

Juhudi za kukusanya kodi ya pango la ardhi kwa viwanja vilivyopimwa zinaendelea vizuri licha ya changamoto iliyopo hususan muamko wa wananchi katika kulipa kodi, amesema Dkt. Kayandabila.

“Ni matumaini yangu kuwa katika kipindi kilichobaki Wizara itafikia lengo la kukusanya kiasi cha makusanyo ya kodi ya pango la ardhi kilichowekwa kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ambacho ni kiasi cha shilingi bilioni 111.7”. Amesema Dkt. Kayandabila.

Amesema, Serikali kuanzia mwezi julai, 2017 kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi itaanza kukusanya kodi ya pango la ardhi kwenye viwanja na mashamba yasiyopimwa. Lengo la utaratibu huu ni kuongeza wigo wa mapato yatokanayo na kodi ya pango la ardhi.

Utaratibu huu utawafanya wananchi wote wanaomiliki ardhi waweze kulipa kodi. Hata hivyo, ni vema ieleweke kuwa uamuzi huu hauna lengo ya kupunguza juhudi za Wizara katika kupanga, kupima na kumilikisha ardhi kwa wananchi, isipokuwa utaratibu huu unajenga dhana ya uwajibikaji kwa wananchi wote katika kulipa pango la ardhi kwenye maeneo yao.

Aidha, serikali imeanza Ujenzi wa mfumo wa kielektronic wa kumbukumbu za Ardhi (Integrated Land Management System) ambao umeanza kutekelezwa. Mfumo huo ukikamilika utasaidia sana kuwa na kumbukumbu sahihi za wamiliki wa ardhi na hivyo kurahisisha ukusanyaji wa kodi za Ardhi.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila akiongea na watumishi wa wizara hiyo katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi na kuwataka waongeze jitihada za makusanyo ya kodi ya pango la ardhi.
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Yamungu Kayandabila wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi.
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Yamungu Kayandabila wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi.
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Yamungu Kayandabila wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi.

Serikali ya JPM Itafanikiwa katika Vita Dhidi ya Dawa za Kulevya - Mrema

$
0
0


 Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole nchini Tanzania Agustine Lyatonga Mrema akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa program ya uanzishaji wa Klabu za Kupambana na dawa za Kulevya mashuleni jana Jijini Dar es Salam.Hafla hiyo ilienda sambamba na utoaji wa tuzo za heshima kwa baadhi ya wadau wa masuala ya kijamii wakiwemo Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi, Mohamed Dewji, Mustafa Sabodo, Mchungaji Dkt. Getrude Rwakatale na Mrema aliyepokea tuzo zote kwa niaba ya wengine.Tuzo hizo zimetolewa na Taasisi ya Mama’s and Papa’s For Community Reform Rehabilitation Center (MPFCR). Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Bi. Emmi Ally Ghahae na Mrakibu wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Scholastica Luhamba.
 Mrakibu wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Scholastica Luhamba akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa program ya uanzishaji wa Klabu za Kupambana na dawa za Kulevya mashuleni jana Jijini Dar es Salam.Uzinduzi huo ulienda sambamba na utoaji wa tuzo za heshima kwa baadhi ya wadau wa masuala ya kijamii wakiwemo Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi, Mohamed Dewji, Mustafa Sabodo, Mchungaji Dkt. Getrude Rwakatale na Agustine Lyatonga Mrema( kulia) aliyepokea tuzo zote kwa niaba ya wenzake
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mama’s and Papa’s For Community Reform Rehabilitation Center (MPFCR) Bi. Emmi Ally Ghahae akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa program ya uanzishaji wa Klabu za Kupambana na dawa za Kulevya mashuleni jana Jijini Dar es Salam.Hafla hiyo ilienda sambamba na utoaji wa tuzo za heshima kwa baadhi ya wadau wa masuala ya kijamii akiwemo Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi, Mohamed Dewji, Mustafa Sabodo, Mchungaji Dkt. Getrude Rwakatale na Mrema aliyepokea tuzo zote kwa niaba ya wengine.Tuzo hizo zimetolewa na taasisi hiyo. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole nchini Tanzania Agustine Lyatonga Mrema na Mrakibu wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Scholastica Luhamba.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mama’s and Papa’s For Community Reform Rehabilitation Center (MPFCR) Bi. Emmi Ally Ghahae akionyesha tuzo maalum kwa kutambua mchango wa Mhe. Agustine Lyatonga Mrema (mwenye kofia) katika kuthamini jamii  wakati wa hafla ya uzinduzi wa program ya uanzishaji wa Klabu za Kupambana na dawa za Kulevya mashuleni jana Jijini Dar es Salam. Hafla hiyo ilienda sambamba na utoaji wa tuzo za heshima kwa baadhi ya wadau wa masuala ya kijamii wakiwemo Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi, Mohamed Dewji, Mustafa Sabodo, Mchungaji Dkt. Getrude Rwakatale ambapo Mrema alipokea tuzo zote kwa niaba ya wengine.

Introducing Lorenzo's brand new Video ft Mesen Selekta

Introducing SiSi Sio Kundi (SSK) New Tanzanian Rap Group, Debut single/video

WMA REKEBISHENI MIZANI KWENYE MAGHALA YA KOROSHO-MAJALIWA

$
0
0
*Serikali kugawa salpha bure kwa wakulima wa korosho

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi wa Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) kuhakikisha wanafanya marekebisho ya mizani katika maghala ya kuhifadhia korosho ili kuepuka changamoto ya kutofautiana kwa uzito wa bidhaa hiyo kila inapofikishwa kutoka katika vyama vya msingi.

Amesema kitendo cha mizani za kwenye maghala hayo kupunguza uzito wa korosho zinazopelekwa kutoka kwenye Chama cha Ushirika cha Msingi (AMCOS) hakivumiliki, hivyo Wakala wa Vipimo ipendekeze aina ya mizani zitakazotumika katika upimaji wa korosho.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Mei 13, 2017) wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Tasnia ya Korosho uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma.

“Kuna jambo baya sana linaendelea kila korosho inayofikishwa katika ghala kuu lazima kilo ziwe zimepungua kwa zaidi ya kilo mia moja mpaka elfu, kwa nini korosho tani kumi zikiletwa kwenye mizani yenu zinasoma tani nane kwa nini?

“Na huwa haitokei ikasoma tani kumi na mbili, wakati wote huwa inasoma chini tu, watu wa WMA mpo fanyesni marekebisho, haiwezekani tukavumilia wizi huu. Huna mkorosho hata mmoja lakini mwaka huu utasikia umeuza tani zaidi ya elfu tano.Jambo hili lisijitokeze tena,” amesisitiza.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wawa Dau wa Tansnia ya Korosho Nchini ambao umefunguliwa na Waziri Mkuu May 13, 2017 katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango Mkoani Dododma .(PICHA NA OWM)
Wadau wa Tasnia ya Korosho wakimsikilza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wawa Dau wa Tansnia ya Korosho Nchini ambao umefunguliwa na Waziri Mkuu May 13, 2017 katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango Mkoani Dododma
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho , Mama Anna Abdala baada ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wawa Dau wa Tansnia ya Korosho Nchini katikati ni Waziri wa Kilimo ,Mifugo na Uvuvi Dr Chales Chizeba , Waziri Kuu amefungua Mkutano huo May 13, 2017 katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango Mkoani Dododma.
(PICHA NA OWM).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BENKI YA NMB YAIKABIDHI SERIKALI GAWIWO LA SHILINGI BILIONI 1.7

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM-Dodoma 
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa mara ya kwanza imetoa gawiwo la shilingi bilioni 1.7 kwa Serikali ambayo inamiliki asilimia 30 ya hisa za Benki hiyo. 
Hundi kifani ya kiasi hicho cha fedha alikabidhiwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), kwaniaba ya Waziri Mkuu, katika tukio la Benki hiyo kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake, tukio lililofanyika katika Hoteli ya Morena Mjini Dodoma. 
Hii ni Mara ya kwanza kwa Benki hiyo kutoa gawiwo kwa wanahisa wake katika kipindi cha miaka 9 baada ya kuanza kupata faida ya uwekezaji wake hapa nchini. 
Dkt. Mpango aliishukuru Benki hiyo kwa kuanza kutoa gawiwo kwa wanahisa wake baada ya ukame wa muda mrefu na kuelezea matumaini yake kwamba kiasi cha gawiwo kitaongezeka zaidi miaka ijayo. 
Hata hivyo alizitaka Benki zote hapa nchini kupunguza riba za mikopo inazotoza kwa wateja wao hasa baada ya Benki Kuu ya Tanzania-BOT kupunguza riba za mikopo kwa mabenki kutoka asilimia 16 hadi asilimia 12. 
Alizitaka pia taasisi za fedha nchini, kuwekeza fedha katika kutekeleza Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo kwa njia ya mikopo kwa wateja wao kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vitakavyosisimua uchumi na kukuza ajira nchini. 
Alipongeza pia juhudi zilizofanywa na Benki hiyo kufanya uwekezaji mkubwa kwenye mtandao wa malipo ya kielektroniki ikiwa ni maagizo ya Serikali kwamba malipo yote ya Serikaloi yafanyike benki au kupitia miamala ya kielektroniki. 
“Nimefurahi kuthibitishiwa kwamba, kutoka tarehe 1 Julai 2016 hadi kufikia tarehe 30 Aprili 2017, NBC imekusanya fedha za Serikali na kuzituma kielektroniki katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) jumla ya Shillingi Billioni 991” aliongeza Dkt. Mpango. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Nehemiah Mchechu, alieleza Mkakati wa Benki hiyo ya tatu kwa ukubwa hapa nchini ikitanguliwa na Benki za NMB na CRDB, huku ikiwa imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi trilioni 1, kwamba imejipanga kusogeza huduma zake kwa wananchi na wafanyabiashara wa kati na wa chini kabisa.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania Bw.  Edward Marks, akizungumza jambo wakati wa maadhimisho ya Benki yake kutimiza miaka 50, tukio lililofanyika Mjini Dodoma Jana usiku.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya NBC, Bw. Nehemiah Mchechu, akitaja mafanikio makubwa yaliyofikiwa na Benki hiyo, wakati wa uzinduzi rasmi wa maadhimisho ya Benki hiyo kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Morena, Mjini Dodoma.
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Josephat Kandege, akipokea tuzo kwaniaba ya wabunge, tuzo iliyotolewa na NBC kutambua mchango wa Bunge katika kuanzishwa kwa Benki hiyo miaka 50 iliyopita.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akionyesha alama ya dole! akifurahia gawiwo la shilingi bilioni 1.7 zilizotolewa na NBC kwa Serikali, ambayo inamiliki asilimia 30 za hisa katika Benki hiyo
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akishukuru baada ya kupokea gawiwo la shilingi bilioni 1.7 zilizotolewa na NBC kwa Serikali, ambayo inamiliki asilimia 30 za hisa katika Benki hiyo
Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee Samwel Malecela, akitoa neon la shukurani kwenye hafla ya Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake, sherehe zilizofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Morena mjini Dodoma. (Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)

WADAU GODWIN D. MSIGWA NA DKT. FARAJA H. MPANGIKE WAMEREMETA LEO DAR ES SALAAM

$
0
0
Wadau Godwin D. Msigwa na Dkt. Faraja H. Mpangike wakitangazwa kama mume na mke katika kanisa la Dar es salaam Pentecostal Church (DPC) jijini Dar es salaam jioni hii
 Wadau Godwin D. Msigwa na Dkt. Faraja H. Mpangike wakionesha pete zao baada ya kutangazwa kuwa mume na mke katika kanisa la Dar es salaam Pentecostal Church (DPC) jijini Dar es salaam jioni hii
  Wadau Godwin D. Msigwa na Dkt. Faraja H. Mpangike wakifurahia baada ya kutangazwa kuwa mume na mke katika kanisa la Dar es salaam Pentecostal Church (DPC) jijini Dar es salaam jioni hii
 Wadau Godwin D. Msigwa na Dkt. Faraja H. Mpangike wakeielekea kwenye ukumbi wa Impala Mbezi Beach jijini Dar es salaam walikoandaa bonge la mnuso. Globu ya Jamii imawapa hongera na kuwatakia maisha mema ya ndoa.

BREAKING NEWZZZ!! CRITICAL ALERT TO COMPUTER USERS - COMPUTER INFECTION REPORTED

Mrema: Serikali ya JPM Itafanikiwa Vita Dhidi ya Dawa za Kulevya

$
0
0
Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole nchini Tanzania Agustine Lyatonga Mrema akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa program ya uanzishaji wa Klabu za Kupambana na dawa za Kulevya mashuleni jana Jijini Dar es Salam.Hafla hiyo ilienda sambamba na utoaji wa tuzo za heshima kwa baadhi ya wadau wa masuala ya kijamii wakiwemo Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi, Mohamed Dewji, Mustafa Sabodo, Mchungaji Dkt. Getrude Rwakatale na Mrema aliyepokea tuzo zote kwa niaba ya wengine.Tuzo hizo zimetolewa na Taasisi ya Mama’s and Papa’s For Community Reform Rehabilitation Center (MPFCR). Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Bi. Emmi Ally Ghahae na Mrakibu wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Scholastica Luhamba.
Mrakibu wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Scholastica Luhamba akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa program ya uanzishaji wa Klabu za Kupambana na dawa za Kulevya mashuleni jana Jijini Dar es Salam.Uzinduzi huo ulienda sambamba na utoaji wa tuzo za heshima kwa baadhi ya wadau wa masuala ya kijamii wakiwemo Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi, Mohamed Dewji, Mustafa Sabodo, Mchungaji Dkt. Getrude Rwakatale na Agustine Lyatonga Mrema( kulia) aliyepokea tuzo zote kwa niaba ya wenzake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mama’s and Papa’s For Community Reform Rehabilitation Center (MPFCR) Bi. Emmi Ally Ghahae akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa program ya uanzishaji wa Klabu za Kupambana na dawa za Kulevya mashuleni jana Jijini Dar es Salam.Hafla hiyo ilienda sambamba na utoaji wa tuzo za heshima kwa baadhi ya wadau wa masuala ya kijamii akiwemo Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi, Mohamed Dewji, Mustafa Sabodo, Mchungaji Dkt. Getrude Rwakatale na Mrema aliyepokea tuzo zote kwa niaba ya wengine.Tuzo hizo zimetolewa na taasisi hiyo. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole nchini Tanzania Agustine Lyatonga Mrema na Mrakibu wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Scholastica Luhamba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mama’s and Papa’s For Community Reform Rehabilitation Center (MPFCR) Bi. Emmi Ally Ghahae akionyesha tuzo maalum kwa kutambua mchango wa Mhe. Agustine Lyatonga Mrema (mwenye kofia) katika kuthamini jamii wakati wa hafla ya uzinduzi wa program ya uanzishaji wa Klabu za Kupambana na dawa za Kulevya mashuleni jana Jijini Dar es Salam. Hafla hiyo ilienda sambamba na utoaji wa tuzo za heshima kwa baadhi ya wadau wa masuala ya kijamii wakiwemo Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi, Mohamed Dewji, Mustafa Sabodo, Mchungaji Dkt. Getrude Rwakatale ambapo Mrema alipokea tuzo zote kwa niaba ya wengine.
Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole nchini Tanzania Agustine Lyatonga Mrema akipokea risala kutoka kwa mmoja wa wanufaika wa Taasis ya Mama’ and Papa’s For Community Reform Rehabilitation Center (MPFCR) Sempeho Samweli Mtangi wakati wa hafla ya uzinduzi wa program ya uanzishaji wa Klabu za Kupambana na dawa za Kulevya mashuleni jana Jijini Dar es Salam. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Bi. Emmi Ally Ghahae. Hafla hiyo ilienda sambamba na utoaji wa tuzo za heshima kwa baadhi ya wadau wa masuala ya kijamii wakiwemo Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi, Mohamed Dewji, Mustafa Sabodo, Mchungaji Dkt. Getrude Rwakatale ambapo Mrema alipokea tuzo zote kwa niaba ya wengine.


KWA SIMU TOKA LONDON – Mahojiano na Janet Chapman – Nini Faida ya Ujenzi wa Ramani za Vijijini Afrika?

$
0
0
Na Freddy Macha
Janet Chapman ni kati ya Waingereza wanaojitolea (bila malipo ), miaka mingi kujaribu kusaidia Afrika, hususan Tanzania. Akiwa mwanachama wa Shirika la Misaada ya Maendeleo Tanzania (TDT) na Jumuiya ya Waingereza na Watanzania (BTS) karibuni amejihusisha na suala la kutokomeza Ukeketaji. Katika mahojiano na Kwa Simu Toka London - Mei 11, 2017 anafafanua mradi mpya wa kujenga ramani vijijini Tanzania, yaani "Mapping". Je maana na faida yake nini? Kufaidi zaidi mahojiano bofya CC dirisha la You Tube upate maelezo yaliyoandikwa kitaaluma kuelewa kinachosemwa.

KWA SIMU TOKA LONDON- Utambulisho- Freddy Macha

AZAM SPORTS: Mtangazaji maarufu wa RTD Ahmed Jongo Ahitaji Msaada Wa Matibabu

MBUNGE WA CCM AMWAGA VIFAA TIBA VYENYE THAMANI YA SH. MILIONI 33 VITUO VYA AFYA NA ZAHANATI SHINYANGA

$
0
0
 
 Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ametoa msaada wa vifaa tiba ikiwemo vitanda vya kisasa vya kujifungulia,vitanda vya wagonjwa na viti vya wagonjwa katika vituo vya afya na zahanati katika halmashauri ya Shinyanga vijijini na Kishapu vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 33.

 Mbunge huyo amekabidhi vifaa tiba hivyo katika Kituo cha afya Tinde,zahanati ya Solwa,zahanati ya Nyashimbi,kituo cha afya Samuye katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini na kwa upande wa Kishapu ni Kituo cha afya Nhobola,Mwang’haranga,Dulusi na Songwa.
  
Vifaa hivyo vinatokana na jitihada zilizofanywa na mbunge huyo Azza Hilal Hamad kufika katika ubalozi wa China nchini Tanzania kuomba asaidiwe vifaa tiba hivyo ili kukabiliana na vifo vya mama na mtoto mkoani Shinyanga.

Akizungumza leo Jumamosi May 13,2017 wakati wa kukabidhi vitanda vitatu vya kisasa vya kujifungulia,vitanda 9 vya wagonjwa na viti vitatu (wheel chairs) vyenye thamani ya shilingi milioni 9.7 katika kituo cha afya Tinde kilichopo Shinyanga vijijini,mheshimiwa Hamad alisema vitasaidia kupunguza adha ya upungufu wa vitanda katika kituo hicho kilichojengwa mwaka 1920.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)  akimkabidhi Mganga Mkuu wa kituo cha afya Tinde,Dkt. Dama s Mnyaga Nyansira,shuka kwa ajili ya vitanda vya kulalia wagonjwa
 Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwahutubia wakazi wa kata ya Tinde wakati akikabidhi vifaa tiba hivyo 
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) akipokelewa kwa shangwe katika kituo cha afya Tinde kilichopo Shinyanga vijijini alipofika kukabidhi vitanda vya kisasa na viti vya wagonjwa vyenye thamani ya shilingi milioni 9.7

WAALIMU NA WANAFUNZI WILAYANI KONDOA WATAKIWA KUHAKIKISHA WANAFANYA VIZURI KWENYE MITIHANI YA TAIFA MWAKA HUU

$
0
0
Na Mahmoud Ahmad, Globu ya Jamii - Kondoa

Mkuu wa wilaya ya Kondoa Sezaria Makota amewataka waalimu,watendaji na wadau wa elimu wilayani humo kuhakikisha ufaulu wa wanafunzi unavuka lengo walilojiwekea sanjari na kuhakikisha maabara zinakamilika kwa wakati kwenye shule mbalimbali ili vifaa vya maabara walivyoahidiwa na wizara ya elimu wapewe kwa wakati.

Kauli hiyo ameitoa kwenye sherehe za tathmini ya sekta ya elimu wilayani humo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Kondoa Irangi.

Amesisitiza kuwa suala la kuwapatia elimu watoto wilayani humo ni jukumu ambalo linahitaji ushirikiano wa wadau wote wa elimu na si suala la walimu pekee hivyo kwa umoja wao wanatakiwa kutoa ushirikiano ili kuweza kufanikiwa kufikia malengo katika sekta hiyo.

“Tumekuwa nyuma katika sekta ya elimu hivyo nawasihi wadau wote kuhakikisha wanafunzi wilayani hapa wanapata huduma muhimu ilikuweza kufikia malengo tarajiwa ya ufaulu wao na kuweza kuwa kwenye kumi bora za shule bora hapa nchini naahidi kulivalia njuga suala hilo ilikuweza kufikia malengo”alisisitiza Dc Makota.

Kwa Upande wake mkurugenzi wa wilaya Kondoa Vijijini Falessy Kibassa alisema kuwa atahakikisha suala hilo linafanikiwa, lengo likiwa kuwawezesha waalimu na wadau kufikia malengo tarajiwa ya ufaulu na atalivalia njuga katika kuhakikisha masuala ya elimu wilayani humo yanakuwa ya mafanikio na mfano wa kuigwa mkoani hapa.

Nae Afisa elimu msingi Alphonce Mwamwile alisema kuwa sekta ya elimu wilayani humo japokuwa inakabiliwa na changamoto kubwa za uhaba wa waalimu katika shule nyingi pamoja na utoro, ukosefu wa chakula mashuleni wakati wa mchana watajitahidi kuhakikisha elimu inakuwa sanjari na ufaulu wa wanafunzi.

Afisa elimu Sekondari Hildacard Saganda alisema kuwa kumekuwepo na changamoto kubwa ya umaliziaji wa maabara katika shule za sekondari hivyo kuwakosesha wanafunzi wanaojifunza masomo ya sayansi kukosa kujifunza kwa vitendo ila watahakikisha wanashirikiana na wadau wengine katika kutatua changamoto hiyo.

Kwa upande mwingine Mbunge wa Kondoa vijijini Ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Ashatul Kijaji ameahidi kutoa Photocopy mashine kwa ajili ya mitihani ya kila mwezi kwa wanafunzi wa shule za wilaya hiyo.
Viewing all 109921 articles
Browse latest View live




Latest Images