Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1678 | 1679 | (Page 1680) | 1681 | 1682 | .... | 3284 | newer

  0 0
 • 05/09/17--04:39: ANATAFUTWA NA WAZAZI WAKE

 • MTOTO HUYU PICHANI ANAITWA LINDA RAYMOND KOMBE AMEPOTEA NYUMBANI KWAO KINONDONI MKWAJUNI TAR 6/05/2017 KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA,YEYOTE ATAKAYEMUONA AWASILIANE NA WAZAZI WAKE KWA NAMBA 0714 282527, 0654 700777. ZAWADI NONO ITATOLEWA KWA ATAKAYEFANIKISHA KUPATIKANA KWAKE

  0 0

   Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Waziri wa mabo ya Ndani Mhe.Mwigulu Nchemba katika  kikao cha Ishirini cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 9, 2017.
   Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akizungumza jambo Mbunge wa Arusha Mjini Mhe.Godbless Lema katika  kikao cha Ishirini cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 9, 2017.
   Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Najma Giga akiongoza  kikao cha Ishirini cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 9, 2017.
   Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Mwigulu Nchemba akijibu hoja Mbalimbali za Wabunge  katika  kikao cha Ishirini cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 9, 2017.
   Mbunge wa Segerea Mhe.Bonnah Kaluwa  akiuliza swali katika  kikao cha Ishirini cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 9, 2017.

  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI Mhe.Selemani  Jafo akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha Ishirini cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 9, 2017.


  0 0

  Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.

  MCHUNGAJI wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, George Milulu ameieleza Mahakama ya  kuwa alisikia uvumi kwamba Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Josephat Gwajima amefariki dunia.

  Mchungaji Milulu amedai hivyo leo, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati akitoa utetezi wake dhidi ya shtaka linalomkabili yeye na wenzake la kukutwa na silaha.

  Akiongozwa na Wakili wake Peter Kibatala, amedai kuwa, alipata taarifa ya uvumi kwamba Askofu Josephat Gwajima amefariki katika Hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam.

  Akielezea ilivyokuwa amedai yeye ni Mchungaji wa Kanisa la ufufuo na uzima tangu mwaka 2008.

  Amedai kuwa, Machi 29, 2015 alikuwa hospitali ya TMJ ambapo alikuta watu ni wengi, lakini muda mfupi baadaye waliamuliwa na Polisi wakae eneo moja wakiwemo waliokuwa waumini waliokuwa juu ya ghorofa washuke chini.

  Shahidi huyo ambaye ni mshtakiwa wa nne katika kesi hiyo ameongeza kuwa kabla hawajajua sababu ya kukusanyika upande mmoja walipewa amri nyingine ya kuingia ndani ya gari la Polisi aina ya Land cruiser na kupelekwa kituo cha Oysterbay.

   Wakili Kibatala alimuuliza kama alipokuwa TMJ aliwahi kuliona begi lenye silaha ambalo lilitolewa mahakamani kama kielelezo, alijibu kuwa hakuwahi kuliona.

  Naye shahidi George Mzava alieleza kuwa hajawahi kukutwa na begi lolote katika hospitali ya TMJ kama ilivyoelezwa kwenye hati ya mashtaka. Alidai kuwa baada ya kukamatwa na Polisi walifikishwa Oysterbay ambapo waliamriwa wavue mikanda na kuanza kuhojiwa mmoja mmoja.

  Aidha shahidi huyo ameieleza mahakama yeye na wenzake hawakuiona hiyo silaha wanayodaiwa kukutwa nayo wala begi la Askofu Gwajima. Amedai kuwa kwa mara ya kwanza kuiona silaha hiyo ni pale ilipopelekwa mahakamani hapo kama kielelezo pamoja na risasi zake.

  Hata hivyo, wakili wa serikali Shadrack Kumar alipomuuliza shahidi huyo kuwa yeye ni mlinzi wa Askofu Gwajima ama ni Askofu, alijibu kuwa ni Askofu.

  Kesi hiyo itaendelea kesho.

  Washtakiwa katika kesi hiyo ni  Askofu Gwajima, George Mzava, Yekonia Bihagaze (39) na  Georgey Milulu ambao wote wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa wakimiliki Bastola aina ya Berretta pamoja na risasi 20 kinyume cha sheria.

  Wanadaiwa kuwa Machi 29, 2015 katika Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni A walikutwa wakimiliki Bastola aina ya Berretta yenye namba ya siri CAT 5802 bila ya kuwa na kibali toka kwa mamlaka inayohusika na silaha na milipuko.

  0 0

  Balozi Mteule wa Tanzania nchini India, Baraka Luvanda akiongea akipokea Kitabu cha maswala ya Uwekezaji kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Clifford Tandari wakati Balozi huyo alipotembelea kituo hicho, Balozi Luvanda ameiomba TIC iweze kushirikiana naye ili kuweza kuongeza idadi ya Wawekezaji wa India nchini Tanzania kwenye sekta mbalimbali kama Afya, viwanda na Utalii. Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji amesema India ni mshirika mkubwa wa Tanzania katika Uwekezaji na moja kati ya nchi tano bora zenye uwekezaji mkubwa hapa nchini na kumuomba Balozi Luvanda kuhakikisha anajitahidi kutangaza fursa zaidi za Uwekezaji zilizopo hapa nchini ili uwekezaji uwe na manufaa kwa maeneo mengi zaidi ya nchi.
  Balozi Mteule wa Tanzania nchini India, Baraka Luvanda (wa pili kushoto) akipata maelezo mafupu kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Clifford Tandari (kulia) wakati Balozi huyo alipotembelea kituo hicho jana.

  0 0

  SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limetoa semina juu ya umuhimu wa hifadhi ya jamii kwa wanacama wa kikundi cha Umoja wa Miradi ya Viziwi Tanzania UMIVITA.

  Semina hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na shirika hilo ambapo ilihusisha wanachama wapatao mia mbili.

  Akizungumza katika semina hiyo Ofisa Matekelezo Mkuu wa NSSF Mkoa wa Temeke, Nuhu Ramadhani alisema wanachama hao walipata fursa ya kuifahamuvizuri NSSF na kujua mafao yanayotolewa na shirika hilo yakiwemo pensheni ya uzeeni,pensheni ya ulemavu,pensheni ya urithi, msaada wa mazishi, mafao ya kuumia kazini, mafao ya uzazi na matibabu bure kwa mwananchama na wategemezi wake.

  Aisha NSSF ilitoa fursa kwa Wanachama wa UMIVITA waliohudhuria semia hiyo kujiandikisha kuwa wanachama.
  Ofisa Uhusiano na Masoko wa NSSF, Anna Nguzo, akizungumza wakati wa semina iliyoandaliwa na NSSF wa ajili ya wanachama wa Kikundi cha Umoja wa Miradi kwa Viziwi Tanzania.

  Ofisa Matekelezo Mwandamizi wa NSSF Mkoa wa Temeke, Naphisa Jahazi, akizungumza wakati wa semina hiyo.

  Mwenyekiti wa Umoja wa Miradi kwa Viziwi (UMIVITA), Jamal Amiri akizungumza wakati wa semina iliyoandaliwa na NSSF kwa ajili ya wanachama wa Kikundi cha Umoja wa Miradi kwa Viziwi Tanzania.
  Wanasemina.


  0 0

   Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi  Ukaguzi Nd.Mohamoud Houssein (katikati) mara baada ya mapokezi alipotembelea  katika Bandari ya   Doraleh  Container Terminal  jana ambayo ni maalum kwa upokeaji wa Makontena kutoka kwenye meli mbali mbali zinazowasili katika Bandari hiyo, alipotembelea  akiwa katika ziara maalum ya kiserikali nchini Djibouti akiwa na ujumbe aliofuanata nao terehe 08/05/2017.
   Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) pamoja na Viongozi wengine wakipata maelezo kutoka kwa Mtaalam wa Mashine  karika Bandari  ya   Doraleh  Container Terminal  jana  ambayo ni maalum kwa upokeaji wa Makontena kutoka kwenye meli mbali mbali zinazowasili katika Bandari hiyo, Dk.Shein yupo nchini Djibouti katika  ziara maalum ya kiserikali   akiwa na ujumbe aliofuanata nao
   Makontena yenye mizogo mbali mbali yakiwa katika eneo maalum lililotengwa na kuwekwa katika Bandari  ya   Doraleh  Container Terminal nchini Djibouti ambapo  Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na ujumbe wake jana walitembelea eneo hilo akiwa katika ziara maalum ya kiserikali.
   Mashine za kuchukulia Makontena katika meli zinazofunga gati katika  Bandari  ya   Doraleh  Container Terminal nchini Djibouti ambapo  Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na ujumbe wake  jana walitembelea eneo hilo akiwa katika ziara maalum ya kiserikali.
   Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akitambulishwa na Mkuu wa Bandari ya Djibouti Bw,Saad Omar  Guelleh (katikati) kwa viongozi wakati aliposalimiana nao jana  wakati  alipotembelea katika Bandari  ya   Doraleh  Multipurpose  nchini Djibouti  akiwa katika ziara maalum ya kiserikali  na ujumbe wake,(kushoto) Waziri wa Vifaa na Usafirishaji Mhe.Mohamed Abdoulkader Moussa.(Picha na Ikulu)

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Hussein Makame, NEC 

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa wito kwa wananchi walioko kwenye halmashauri mbalimbali nchini, kuitumia vyema fursa ya utoaji wa elimu ya mpiga kura kupitia redio za kijamii kwenye halmashauri zao ili kuondoa manung’uniko kwenye chaguzi.

  Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Bw. Kailima Ramadhani wakati akizungumzia mpango wa kutoa elimu ya mpiga kura nchi nzima ulioanza kutekelezwa Mei 8 mwaka huu hii katika mikoa kumi nchini.
  Alisema kupitia mpango huo wananchi wanaosikiliza redio za kijamii kwenye halmashauri nchini, watapata fursa ya kujifunza elimu ya mpiga kura na kuelewa masuala yote muhimu yanayohusu mfumo mzima wa kupiga kura. 

  “Tumepanga mpango, Tume itasambaa nchi nzima kuzungumzia elimu ya mpiga kura kwenye redio za kijamii zilizoko kwenye halmashauri zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.” alisema Bw. Kailima.

  Alisisitiza kwa kutoa wito kwa wananchi walioko maeneo ambayo Tume itakwenda kutoa elimu ya mpiga kura, wasikilize na kuuliza maswali ili waweze kuelewa.

  “Hii ni fursa kwa wananchi ambayo muda mrefu hawajawahi kuipata, hivyo nawaomba wafuatilie ili waweze kuelimika zaidi ili yale manung’uniko ya kura yatakuwa yamekwisha na tutakuwa na uchaguzi mzuri zaidi ya ile ambayo tumeifanya.” Alifafanua Bw. Kailima.

  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani akitoa elimu ya mpiga kura kupitia redio A FM ya mkoani Dodoma leo Mei 9 mwaka huu huku akifuatiliwa kwa makini na watangazaji wa redio hiyo.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

  Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.

  Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi,na Mawasiliano imetenga Shilingi bilioni thelathini(30) katika mwaka wa fedha 2017/2018 ili kukamilisha malipo ya fidia kwa wananchi wa Kipunguni wanaopisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege.
   
  Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Ujenzi,uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Edwin Ngonyani Bungeni Mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Segerea Mhe.Bonnah Kaluwa.

  “Ni kweli Serikali ilifanya uthamini wa mali za wananchi ili kupisha upanuzi wa kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Dar es Salaam mwishoni wa miaka ya 90 ambapo maeneo yaliyoainishwa kwa ajili ya upanuzi huo ni Kipawa,Kigilagila na Kipunguni”,Alisema Mhe.Ngonyani

  Ameongeza kuwa kutokana na gharama za fidia na uhaba wa fedha,Serikali imekuwa ikilipa fidia kwa wakazi hao kwa awamu.Ambapo Mwaka 2009/10 wakazi wapatao 1500 wa eneo la Kipawa walilipwa fidia zinazofikia shilingi bilioni 18 ambapo zoezi hilo lilikamilika Januari 2010.

  Katika mwaka wa Fedha 2010/2011 Serikali ililipa Shilingi Bilioni 12 za fidia kwa wakazi 864 wa Kigilagila na Malipo yalikamilika Januari 2011.Katika mwaka 2013/14 Serikali ililipa Shilingi Bilioni 1.2 ikiwa ni fidia kwa wakazi 59 kati ya wakazi 801 kwa eneo la Kipunguni.

  Aidha katika malipo hayo ni wakazi 742 wa Kipunguni ndio ambao hawajalipwa fidia zao zenye thamani ya takribani 19.“Mwaka wa Fedha 2016/17 Serikali imetenga Shilingi Bilioni tano kwa ajili ya kulipa fidia kwa wakazi hao wa Kipunguni”Alisisitiza Mhe.Ngonyani.

  0 0

  Na Karama Kenyunko,blogu ya jamii.

  Baada ya mahakama kutoa hati ya kukamatwa Video Queen Agnes Gerald maarufu kama Masogange (28) kwa kushindwa kutoka mahakamani mara kadhaa, hatimae leo amejisalimisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

  Mapema mwezi uliopita, mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ilitoa amri ya kukamatwq kwa mshtakiwa Masogange kwa kushindwa kuhudhuria mahakamani mara mbili katika kesi ya dawa za kulevya inayomkabili.

  Hatua hiyo ya kutaka kukamatwa kwa Masogange ilikuja baada ya upande wa mashitaka katika shauri lililopita, kuomba mahakama hiyo kutoa hati ya kumkamata kutokana na mshitakiwa huyo pamoja na wadhamini wake kutofika mahakamani, licha ya kupewa onyo.

  Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri alikubali maombi hayo na kutoa hati ya kumkamata mshtakiwa ambaye ni Masogange.

  Hata hivyo, Masogange amefika mahakamani hapo leo mapema na alipoulizwa na Hakimu Mashauri sababu za kumfanya yeye kutofika mahakamani, amedai kuwa alifika lakini alichelewa.

  Wakilli wa serikali Shadrack Kimaro, ameieleza mahakama kuwa upelelezi katika kesi hiyo umekamilika na ameiomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kumsomea mshitakiwa maelezo ya awali(PH).

  Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 13 mwaka huu kwa ajili ya PH.
  Awali ilidaiwa kuwa,Masogange anakabiliwa na tuhuma za kutumia dawa za kulevya aina ya heroin diacety na Oxazepam.

  Awali ilidaiwa kuwa, kati ya Februari 7 na 14 mwaka huu, maeneo yasiyofahamika jijini Dar es Salaam, Masogange alitumia dawa za kulevya aina ya heroin (diacety/morpline) kinyume na sheria.
  Aidha anadaiwa, kutumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam

  0 0


  Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kagera.


  WAKAZI wa Mkoa wa Kagera wamejitokeza kwa wingi katika viwanja vya soko kuu la Manispaa ya Bukoba kwenye zoezi la upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza bure.

  Zoezi hilo linakoratibiwa na ofisi za mfuko wa bima ya afya(NHIF)Mkoa wa Kagera kwa kushirikiana na ofisi za makao makuu ya mfuko huo linatafanyika kwa muda wa wiki nzima.

  Meneja wa mfuko wa Bima ya afya Mkoa wa Kagera Elias Odhiambo alisema kuwa zoezi hilo la upimaji afya litahusisha magonjwa yasiyoambukiza kama shinikizo la damu(BP),Sukari,macho,uzito na urefu pia watakaokutwa na matatizo watapewa ushauri wa kitaalam.

  Odhiambo alisema kuwa zoezi hilo ni sehemu ya majukumu ya mfuko wa NHIF ya kuhudumia wananchi lakini wanaendelea kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko huo wa matibabu ili wawe na uhakika wa matibabu pale wanapougua wao na familia zao.

  Alisema lengo lao ni kuwafikia wananchi zaidi ya elf moja katika maeneo ya Manispaa ya bukoba hivyo aliwataka wananchi wa Bukoba kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo la kupima afya zao.

  Mgeni rasmi katika ufunguzi wa zoezi hilo Mkuu wa Wilaya ya Muleba Injinia Richard Ruyangu aliwataka wananchi wote kujiunga na mfuko wa bima ya afya ili kuwa na uhakika wa matibabu pale wanapougua wao na familia zao.

  Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Muleba akipima afya katika uzinduzi wa zoezi la upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza linaloratibuwa na mfuko wa bima ya afya NHIF Kagera.
  Mgeni rasmi katika uzinduzi wa zoezi la upimaji afya bure wa magonjwa yasiyoambukiza Mkuu wa Wilaya ya Muleba Injinia Richard Ruyango akiongea na wananchi waliojitokeza katika zoezi hilo(hawapo pichani).
  Meneja wa mfuko wa bima ya afya(NHIF)Mkoa wa Kagera Elias Odhiambo akiongea jambo wakati wa zoezi la ufunguzi wa upimaji afya bure kwa magonjwa yasiyoambukiza kwa wakazi wa manispaa ya bukoba.


  Baadhi ya wakazi wa manispaa ya bukoba waliojitokeza kupima afya zao wakimsikiliza mgeni rasmi(hayupo pichani)katika uzinduzi wa zoezi hilo.


  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0  0 0  0 0

  NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

  WANAWAKE wa Dini ya Kiislamu wa Msikiti wa Khoja Shia Ithna Asheri jijini Mwanza wametoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 2 kwa Hospitali ya Butimba ya Wilaya ya Nyamagana ili kusaidia kupunguza changamoto zinazoikabili.

  Mwenyekiti wa kina mama hao Radhida Ahmed akimkabidhi msaada huo Kaimu Mganga Mkuu wa Jiji la Mwanza, Dk. Kajiru Mhando alisema utasaidia kupunguza kero kwa wagonjwa na kuzitaka taasisi zingine zijitokeze kutatua changamoto za hospitali hiyo hasa ujenzi wa wodi ya wazazi.

  Alisema msaada huo umelenga kuonyesha mshikamano wao kwenye jamii katika kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa mjukuu wa Mtume, Imam Mahdi (A.T.F.S) ambayo hudhimishwa Mei 7, kila mwaka.

  “ Tuliguswa na changamoto zinazoikabili hospitali yetu hii ya wilaya lakini pia kuonyesha mshikamano wetu na jamii tukaona tuje kutoa msaada huu kwa ajili ya kuwapunguzia wagonjwa kero na changamoto,Wapo wenye utajiri waone na kuguswa na matatizo ya wenzao na kuwasaidia hasa wagonjwa” alisema Rashida.

  Aliutaja msaada huo walioukabidhi kuwa ni magodoro 10, mashuka pea 25 na foronya zake, mablanketi 50 na vyandarua 50, vifaa vya usafi (mifagio 10, brashi 10 na Squizers 10) pamoja na sabuni ya maji (Detol) lita 10 na ya unga kg 15.
  Msaada iliyotolewa katika hospiali ya Butimba jijini Mwanza kutoka kwa wanawake wa Dini ya Kiislamu wa Msikiti wa Khoja Shia Ithna Asheri Mwanza.
  Wanawake wa Dini ya Kiislamu wa Msikiti wa Khoja Shia Ithna Asheri Mwanza wakabidhi Blanketi
  Dk Kajiru akipokea moja ya godoro kati ya 10 yalitolewa msaada wa akinamama wa Msikiti wa Khoja Shia Ithna Asheri Mwanza
  Mwenyekiti wa Wanawake wa msikiti wa Khoja Shia Ithan Ashaeri Rashida Ahmed pamoja na Mrs karimu wakimfurahia mtoto Hajida walipotelea wodi ya wazazi kwenye hospitali ya Butimba.


  0 0


  Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Mawasiliano na huduma za Mitandao Bw.Abdi Youssoef wakati alipotembelea katika Ofisi ya kampuni Telecom Nchini Djibouti akiwa katika ziara ya kiserikali kwa mualiko wa Rais wa nchi hiyo Mhe,Ismail Omar Guelleh[Picha na Ikulu.] 

  Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiuliza suala wakati alipotembelea kampuni ya Simu ya Telecom Nchini Djibouti akiwa katika ziara ya kiserikali kwa mualiko wa Rais wa nchi hiyo Mhe,Ismail Omar Guelleh[Picha na Ikulu.] 

  Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa ofisa wa kampuni ya Simu ya Telecom Nchini Djibouti wakati alipotembelea katika Ofisi ya kampuni hiyo akiwa katika ziara ya kiserikali kwa mualiko wa Rais wa nchi hiyo Mhe,Ismail Omar Guelleh[Picha na Ikulu.] 

  0 0

  Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

  Baada ya mahakama kutoa  hati ya kukamatwa Video  Queen Agnes Gerald maarufu kama Masogange (28) kwa kushindwa kutoka mahakamani mara kadhaa, hatimae leo  amejisalimisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

  Mapema mwezi uliopita, mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ilitoa amri ya kukamatwa kwa mshtakiwa Masogange kwa kushindwa kuhudhuria mahakamani mara mbili katika kesi ya dawa za kulevya inayomkabili.

  Hatua hiyo ya kutaka kukamatwa kwa Masogange  ilikuja baada ya upande wa mashitaka katika shauri lililopita, kuomba mahakama hiyo kutoa hati ya kumkamata kutokana na mshitakiwa huyo pamoja na wadhamini wake kutofika mahakamani, licha ya kupewa onyo.

  Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri alikubali maombi hayo na kutoa hati ya kumkamata mshtakiwa ambaye ni Masogange.

  Hata hivyo, Masogange amefika mahakamani hapo leo mapema na alipoulizwa na Hakimu Mashauri sababu za kumfanya yeye kutofika mahakamani, amedai kuwa alifika lakini alichelewa.

  Wakilli wa serikali Shadrack  Kimaro, ameieleza mahakama kuwa upelelezi katika kesi hiyo umekamilika na ameiomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kumsomea mshitakiwa maelezo ya awali(PH).

  Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 13 mwaka huu kwa ajili ya PH.
  Awali ilidaiwa kuwa,

  Masogange anakabiliwa na tuhuma za kutumia dawa za kulevya aina ya heroin diacety na Oxazepam.

  Awali ilidaiwa kuwa, kati ya Februari 7 na 14 mwaka huu, maeneo yasiyofahamika jijini Dar es Salaam,  Masogange alitumia dawa za kulevya aina ya heroin (diacety/morpline) kinyume na sheria.
  Aidha anadaiwa, kutumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam

  0 0

  Na Vero Ignatus, Arusha
  Kutokana na mvua inayonyesha mfululizo Mkoani Arusha imeleta maafa makubwa katika familia ya mzee Jonathani Kalambiya{55} mkazi wa sokoni II katika kijiji cha kinyeresi wilayani Arumeru Mkoani Arusha baada ya mti mkubwa uliong’olewa na maji kuangukia nyumba yake na kuua watoto wake wote watano.
  Mkasa huo wa kusikitisha ulitokea jana majira ya saa 7 usiku baada ya mti huo kung’olewa na maji uliangukia nyumba hiyo iliyokuwa jira na mti huo.Kamanda wa polisi Mkoani Arusha,Charles Mkumbo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja watoto waliokufa katika tukio hilo ni pamoja na watoto wawili wanafunzi wa mzee huyo ambaye ni mlinzi wa hospital ya ya Dr Mohamed ya Jijini Arusha.
  Mkumbo aliwataka wanafunzi ambao ni watoto wa mzee Kalambwia ambaye siku ya tukio alikuwa kazini ni pamoja na Miliamu Jonathani(16) mwanafunzi wa kidatu cha pili wa shule ya sekondari ya Inaboishu.

  Kamanda alimtaja mwanafunzi mwingine ni ambaye ni mtoto wa mzee huyo ni Grolia Jonathani(11) mwanafunzi wa shule ya msingi Kinyeresi iliyoko wilayani Arumeru Mkoani Arusha.Amesema watoto wengine wa mzee huyo ni pamoja na mtoto wa kwanza wa mzee huyo aliyetambuliwa kwa jina la Giliad Jonathani(31),Lazaro Lomnyaki (26) na Best Jonathani(20).

  Kamanda Mkumbo alisema kuwa mti huo uliokuwa katika mlima wa Lake mana uliangukia nyumba hiyo baada ya kung’olewa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika Jiji la Arusha na Mkoa kwa ujumla.Alisema na kuitakia pole sana familia yam zee huyo kwani tukio hilo ni majonzi makubwa sana kwake kwani familia nzima imeondoka na kumtaka kuwa na uvumilivu katika wakati huu mgumu kwake.

  Kamanda Mkumbo ametoa wito na ushauri kwa wakazi wa Arusha kuchukuwa tahadhari katika kipindi hiki cha mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kwa kukarabati nyumba zao na kuacha kujenga chini ya mti ama kwenye vyanzo vya maji.

  Amesema kujenga katika vyanzo vya maji ama chini ya mti ni kujitafutia majanga mengine hivyo ni vema kila mkazi wa Mkoa wa Arusha kuchukuwa tahadhali hiyo.Aidha kamanda ametoa tahadhari kutokana na habari za uzushizinazoendele kuwa jana kwenye kuaga miili ya wanafunzi kuna mtu alidondoka juu ya mti na kufariki pamoja na mama mmoja mtoto wake mdogo alifariki,amesema habari hizo siyo za kweli wananchi wazipuuze kabisa .

  Kamanda wa polisi Mkoani Arusha,Charles Mkumbo 

  nyumba ikiwa imeangukiwa na mti kama inavyoonekana katika picha
  Mti ulioanguka ukang'ookana shina lake na kuangukia nyumba na kusababisha maafa hayo ya watu watano wa familia moja.


  Jitihada za uokozi zikiendelea .
  Miili ikiwa imeshapakiwa ndani ya gari la polisi.

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa zamani, Lawrence Masha kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Kiembesamaki, Ibrahim Raza kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 9, 2017.
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 9, 2017. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge, Job Ndugai kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 9, 2017. Katikati ni Mbunge wa zamani, Hezekia Wenje.


  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Habari Ndugu, 
   Naomba tuungane mkono kwa pamoja baada ya maneno mengi kuongeleka kuwa mimi ni msanii wa kiki. Ila sio kweli kuhusu hili na kuthibitisha nimeamua niachie wimbo mpya unaoenda kwa jina la "NUNDU" kama zawadi kwa watanziania na mashabiki wangu wote kiujumla. 
  NUNDU ni wimbo wangu wa tatu officially kuachiwa, na nimemshirikisha mkongwe wa muziki nchini CPWAA pamoja na RONEI ambaye ni upcoming hatari kutoka SGS SABUKA MUSIC, Record Label inayomilikiwa na IRENE SABUKA. Tutashukuru kwa support yako ya muziki mzuri. Wako Mtiifu, 
   Harmorapa.

  0 0

  Tembo wakiwa wamejificha kwenye vichaka ndani ya eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) leo. Kwa mujibu wa taarifa za Wahifadhi wa Wanyamapori inaelezwa kuwa sehemu ya eneo hilo litakuwa ni njia ya tembo (maeneo ya mapito ya wanyamapori) ambayo ilipitika kwa miaka mingi iliyopita na kwamba tembo wana kumbukumbu hata kama walipita njia hiyo kwa zaidi ya miaka 50 iliyopita. Imeelezwa kuwa njia hiyo ya mapito ya wanyamapori itakua ilitumiwa na wanyamapori kuhama eneo moja hadi jengine ikiwemo maeneo ya hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Ruaha, Serengeti, Pori Tengefu la Rugwa na maeneo mengine ya hifadhi na kwamba maeneo hayo mengi kwa miaka ya hivi karibuni yameshaingiliwa na shughuli za kibinadamu ambazo hazisababishi tembo hao kusahau njia hizo au kutokuzitumia tena.
  Tembo hao wakiwa ndani ya eneo chuo kikuu hicho cha Dodoma leo. Hakuna madhara yeyote yaliyoripotiwa kusababishwa na tembo hao na taratibu za kuwarudisha kwenye maeneo yao ya hifadhi zimeshaanza kuchukuliwa na uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambapo Askari wa Wanyamapori wamefanya zoezi la kuwafukuza kuwarudisha kwenye maeneo yao ya hifadhi.
  Prof. Julius Nyahongo wa Chuo Kikuu cha Dodoma akitoa somo kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma namna ya kuchukua tahadhari juu ya ugeni wa tembo hao chuoni hapo. Aliwaeleza wanafunzi hao kuwa mazingira ya chuoni hapo yataendelea kuwa salama kwakuwa tembo hao wapo katika njia yao ya mapito na pengine kumewahi kukucha kabla ya wao kufika mwisho wa safari yao, hivyo kwa msaada wa askari wa wanyamapori ambao wamewasili chuoni hapo itasaidia  kuwaondoa tembo hao waweze kuendelea na safari yao hadi kwenye maeneo ya hifadhi.
  Wanafunzi mbalimbali wa Chuo Kikuu cha Dodoma walikusanyika wakiwa na shauku ya kuwaona tembo hao.
  Msafara wa viongozi mbali mbali wa Serikali ukiambatana na Askari Polisi na Askari wa Wanyamapori ukisogelea eneo walilokuwepo tembo hao kwa ajili ya kuanza kuwafukuza kutoka katika maeneo hayo ya chuo kwenda kwenye maeneo yao ya hifadhi.
  Prof. Julius Nyahongo wa Chuo Kikuu cha Dodoma (wa pili kulia), Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania, Paschal Shelutete (wa tatu kulia) na maafisa wengine wa Serikali na vyombo vya ulinzi na usalama wakiangalia eneo walilokuwa wamejificha tembo hao chuoni hapo.
  Askari wa wanyamapori wakiingia ndani ya eneo walilokuwa wamejificha tembo hao kwa ajili ya kuanza kuwafukuza eneo hilo kuelekea kwenye maeneo yao ya hifadhi. Imeelezwa kuwa pindi tembo hao watakapofukuzwa kwa milio maalum ya risasi hutafuta njia wanazozijua wenyewe za kurudi kwenye maeneo yao ya hifadhi.
  Tembo hao wakianza kuondoka katika eneo hilo baada ya askari wa wanyamapori kuanza kuwaondoa eneo hilo kwa kutumia milio maalum ya risasi. (PICHA NA HAMZA TEMBA-WIZARA YA MALIASILI NA UTALII)

older | 1 | .... | 1678 | 1679 | (Page 1680) | 1681 | 1682 | .... | 3284 | newer