Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 166 | 167 | (Page 168) | 169 | 170 | .... | 3272 | newer

  0 0
 • 06/18/13--03:15: Tantrade announcement.


 • 0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa picha ya X-Ray, ya mmoja kati ya majeruhi waliolazwa kwenye Hospitali ya Mount Meru, Joseph Anthony, mkazi wa Karoleni, baada ya kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu lililotokea wiki iliyopita katika mkutano wa Chadema eneo la Soweto jijini Arusha. Imeelezwa kuwa hadi jana Juni 17, 2013, wakati makamu alipowatembelea majeruhi hao watu watatu waliliripotiwa kufariki dunia.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wananchi wa jijini Arusha waliokusanyika nje ya Hospitali ya Mount Meru jana, wakati Makamu alipokuwa na ziara ya kuwatembelea kuwajulia hali majeruhi wa mlipuko wa Bomu uliotokea wiki iliyopita katika mkutano wa Chadema jijini Arusha, ambapo jumla ya watu 70 walijeruhiwa na watatu walifariki dunia. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mwilongo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari, aliyelazwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Selian, mkoani Arusha baada ya kudaiwa kushambuliwa mwishoni mwa wiki iliyopita wakati akiwa katika uchaguzi mdogo wa Udiwani wa Kata ya Makuyuni, Monduli. Awali Nasari alikaririwa akieleza kuwa anamaumivu ya mgongo baada ya kushambuliwa na vitu vigumu na vijana wa Kimasai. Kwa mujibu wa maelezo ya Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt. Paul Kweka, anayemtibu Mbunge huyo, alimueleza Makamu wa Rais kuwa mbunge huyo, baada ya kupimwa na kupigwa picha za X-Ray, ameonekana kuwa hana tatizo lolote la kiafya.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Dkt. Geofrey, kuhusu jinsi mtoto, Aboubakar Adam, mkazi wa Sakina jijini Arusha, aliyelazwa katika Hospitali ya ARumeru baada ya kujeruhiwa na bomu wakati akiwa miongoni mwa watu waliokuwa katika Uwanja wa Soweto kwenye Mkutano wa Chadema wiki iliyopita. Makamu wa Rais, alifanya ziara ya kuwatembelea kuwajulia hali majeruhi wa mlipuko huo, waliolazwa katika Hospitali za Arumeru, Selian na Mtakatifu Elizabeth, jana Juni 17, 2013.


  0 0

  Waziri wa Fedha Dkt .William Mgimwa (kushoto) na Balozi wa Japan nchini Masaki Okada(kulia)wakibadilishana hati ya makubaliano ya mkopo wa riba nafuu ambapo Japan itaikopesha Tanzania shilingi bilioni 77.7 kwa ajili ujenzi wa barabara ya juu kwa juu katika makutano ya TAZARA jijini Dar es salaam na fedha nyingine zitasaidia katika kupunguza umaskini. Sherehe zilifanyika jana (leo) mjini Dodoma na kuhudhuriwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli(katikati).
  Waziri wa Fedha Dkt .William Mgimwa (katikati ) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari jana (leo) mjini Daodoma juu ya mkopo wa riba nafuu wa shilingi bilioni 77.7 ambao utatumika katika ujenzi wa barabara ya juu kwa juu katika makutano ya TAZARA jijini Dar es salaam na fedha nyingine kwa ajili ya kupunguza umaskini zilizotolewa na Japan. Sherehe zilifanyika jana (leo) mjini Dodoma na kuhudhuriwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli(kushoto). Mwingine katika picha ni Balozi wa Japan nchini Masaki Okada(kulia).
  Balozi wa Japan nchini Masaki Okada(kulia) akizungumza na waandishi wa habari jana (leo) mjini Dodoma mara baada yake kusaini na Tanzania hati ya makubaliano ya mkopo wa riba nafuu ambapo Japan itaikopesha Tanzania shilingi bilioni 77.7 kwa ajili ujenzi wa barabara ya juu kwa juu katika makutano ya TAZARA jijini Dar es salaam na fedha nyingine zitasaidia katika kupunguza umaskini. Wengine ni Waziri wa Fedha Dkt .William Mgimwa (katikati) na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli(kushoto).
  Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Japan hapa nchini(JICA) Yasunori Onishi(kulia) akielezea mkakati watakaoutumia katika ujenzi wa daraja la juu katika makutano ya TAZARAjana(leo) mjini Dodoma wakati wa sherehe za kusaini hati ya makubaliano ya mkopo wa riba nafuu ambapo Japan itaikopesha Tanzania shilingi bilioni 77.7 kwa ajili ujenzi wa barabara ya juu kwa juu katika makutano ya TAZARA jijini Dar es salaam na fedha nyingine zitasaidia katika kupunguza umaskini. Wengine ni Balozi wa Japan nchini Masaki Okada ( wa pili kutoka kulia) , Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa (wa pili kushoto) na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli(kushoto).
  Waziri wa Fedha Dkt .William Mgimwa (katikati ) na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Japan hapa nchini(JICA) Yasunori Onishi(kulia)wakisaini hati ya makubaliano ya mkopo wa riba nafuu ambapo Japan itaikopesha Tanzania shilingi bilioni 77.7 kwa ajili ujenzi wa barabara ya juu kwa juu katika makutano ya TAZARA jijini Dar es salaam na fedha nyingine zitasaidia katika kupunguza umaskini. Sherehe zilifanyika jana (leo) mjini Dodoma na kuhudhuriwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli(kushoto).
  Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Japan hapa nchini(JICA) Yasunori Onishi(kulia) na Waziri wa Fedha wakibadilishana hati ya ujenzi wa daraja la juu katika makutano ya TAZARAjana(leo) mjini Dodoma wakati wa sherehe za kusaini hati ya makubaliano ya mkopo wa riba nafuu ambapo Japan itaikopesha Tanzania shilingi bilioni 77.7 kwa ajili ujenzi wa barabara ya juu kwa juu katika makutano ya TAZARA jijini Dar es salaam na fedha nyingine zitasaidia katika kupunguza umaskini. Wengine ni Balozi wa Japan nchini Masaki Okada ( kulia) , na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli(katikati)
  Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli(kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari jana(leo) mjini Dodoma juuu ya juhudi za Serikali ya Rais Jakaya Kikwete ya kupunguza msongamano katika Jiji la Dar es salaam ambapo jana (leo) Tanzania imepata mkopo wa shilingi bilioni 52.5 kutoka Japan kwa ajili ya Ujenzi wa Barabara za Juu katika makutano ya TAZARA. Wengine ni Waziri wa Fedha Dkt . William Mgimwa(katikati) na Balozi wa Japan nchini Masaki Okada(kullia). Picha na GCU-HAZINA_Dodoma.

  0 0
 • 06/18/13--03:40: IN LOVING MEMORY


 • 0 0

  Mkuu wa Idara ya Mauzo na Maduka wa Vodacom Tanzania, Bi.Upendo Richard(kulia)akimkabidhi funguo Meneja wa duka jipya la Vodacom lililopo Millennium Tower ghorofa ya kwanza Bi.Miriam Minja,ikiwa ni inshara ya uzinduzi rasmi wa duka hilo.Anaeshuhudia ni Mkuu wa kitengo cha Mahusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo Bi.Joseline Kamuhanda.
  Meneja wa duka jipya la Vodacom lililopo Millennium Tower ghorofa ya kwanza Bi.Miriam Minja,akifungua duka hilo kwa mara ya kwanza tayari kwa kutoa huduma kwa wateja wa kampuni hiyo,akishuhudiwa na Mkuu wa Idara ya Mauzo na Maduka wa Vodacom Tanzania, Bi.Upendo Richard(kulia)na Mkuu wa kitengo cha Mahusiano ya jamii na Mawasiliano wa kampuni hiyo Bi.Joseline Kamuhanda.
  Mkuu wa kitengo cha Mahusiano ya jamii na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bi.Joseline Kamuhanda,akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa duka jipya la kampuni hiyo lililopo Millennium Tower ghorofa ya kwanza.Tayari kabisa kwa kutoa huduma kwa wateja wake.
  Huku jiji la Dar es Salaam likiendelea kukua kwa kasi na kushuhudia ongezeko kubwa la watu kutoka sehemu mbalimbali, upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii umekuwa ukikabiliwa na changamoto kadhaa kutokana na kasi ya utoaji huduma kutoendana na kasi ya ongezeko la watu.

  Katika kukidhi haja hiyo ya utoaji wa huduma kwa wateja na elimu kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam, Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imeendelea kupanua wigo wa ajira na huduma kwa kufungua duka la huduma kwa wateja katika jengo la Milenium Tower lililoko Makumbusho jijini Dar es Salaam.

  Akizungumzia wakati wa uzinduzi wa duka hilo, Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Joseline Kamuhanda, amesema Vodacom ni kampuni pekee ambayo imeendelea kuongoza kwa kuwa na maduka mengi ya mauzo na huduma kwa wateja kwa kufikisha maduka 66 ikiwa ni kampuni pekee kuwa na maduka mengi ya huduma na kufanikisha adhma ya kukidhi mahitaji ya huduma kwa wateja wa kampuni hiyo, huku Dar es Salaam ikiwa na idadi ya maduka 21.

  “Ukuaji wa huduma kwa kampuni ya Vodacom umekuwa kwa kasi, huduma kama ya M – Pesa sasa imepanuka kwa kasi na kutoa huduma kwa watanzania zaidi ya milioni 10. Kufuatia mafaanikio haya tunalazimika kuhakikisha upatikanaji wa huduma kwa wateja ni wa uhakika” alisema Kamuhanda na kuongeza kuwa, “Kuongoza katika sekta ya mawasilaino kuna changamoto zake, lazima tuhakikishe tunaendana na kasi ya ukuaji na ongezeko la watu na uhitaji wa huduma zetu kwa watu wa aina mbalimbali.

  Aidha Kamuhanda alisema kuwa Kufunguliwa kwa duka hilo sasa sio tu kunaboresha upatikanaji wa huduma pia ni fursa pekee ya kuendelea kupanua wigo wa ajira kwa watanzania.

  “Ufunguzi wa duka hili unatoa fursa ya ajira kwa watanzania, ambapo wafanyakazi wapatao 3 watatoa huduma kwa wateja wetu hivyo ni hatua kubwa kwa kutengeneza ajira kwa wafanyakazi wapya. Hadi kufikia sasa, Vodacom imetoa ajira za moja kwa moja kwa wafanyakazi 500 na wengine zaidi ya 450,000 wenye ajira zisizo rasmi,” alisema Kamuhanda.

  0 0

  Mhe. Eng. Christopher Chiza, Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, leo asubuhi tarehe 18 Juni 2013 ametoa hotuba yake, akijadili hali ya chakula na kilimo duniani katika Kikao cha 38 cha Mkutano wa FAO kinacho endelea tangu tarehe 15 Juni 2013 hadi 22 Juni 2013. Mkutano huu, ambao ndiyo ngazi ya juu ya maamuzi katika shirika hili la Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO), hapo tarehe 21 July 2013 utafanya uchaguzi wa Mwenyekiti mpya wa Baraza la FAO (Independent Chair of the FAO Council - ICC), na Mteule (Nominee) wa Tanzania, Balozi Wilfred Joseph Ngirwa, ndiye mgombea pekee wa nafasi hiyo akiungwa mkono na kundi la Afrika na lile la G77 & China. Uchaguzi huo unafuatia Mhe. Luck Guyau, raia wa Ufaransa, kumaliza muhula wake wa pili, na wa mwisho, wa miaka miwili (biennial) kama taratibu za FAO zinavyotaka. Bolozi Ngirwa alikuwa mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) ya hapa Roma kwa miaka 6 hadi Machi, 2012 ambapo Balozi wetu nchini Italia, Eng. Dr. James Alex Msekela, alichukua nafasi hiyo.

  0 0

  Baadhi ya makocha wakiwemo wachezaji wa zamani wakifuatilia mafunzo ya ukocha ngazi ya pili.
  Kocha mkuu wa Twiga Stars, Rogasian Kaijage akitoa somo kwa makocha wanaoshiriki kozi ya ukocha ngazi ya pili ndani ya darasa kwenye Ukumbi wa Harbours Club, Kurasini.
  Kocha mkuu wa Twiga Stars akitoa somo kwa makocha wa kozi ya ngazi ya pili kwa vitendo.

  KOZI ya makocha wa ngazi ya pili (Intermediate) inayosimamiwa na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), inatarajiwa kufungwa Jumanne ijayo baada ya kudumu kwa wiki nne.

  Kozi hiyo ilianza Juni 3 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Harbours Club, uliopo Kurasini chini ya Mkufunzi Rogasin Kaijage, ambaye ni Kocha wa timu ya Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’ ambapo makocha mbalimbali pamoja na wachezaji wa zamani wamejitokeza kushiriki. 

  Ofisa Habari wa DRFA, Mohamed Mharizo alisema kozi hiyo imekuwa na mafanikio na wanatarajia makocha walioshiriki katika kozi hiyo watakuwa na mchango mkubwa katika kuendeleza mpira wa miguu katika mkoa wa Dar es Salaan na Taifa kwa ujumla.

  “Hadi sasa tunashukuru kuona tunafanikisha kozi hii ambayo wengi wameitikia wito, mwisho wa kozi hii ndio mwanzo wa kozi nyingine.

  “Lakini haya ya kozi ya makocha ni moja ya majukumu ya Kamati ya Ufundi ya DRFA yaliyoainishwa katika Katiba, hivyo hili ni moja ya shabaha yetu na mengine mengi mazuri yanafuata,” alisema Mharizo.

  Kozi hiyo ni ya kwanza kuendeshwa na DRFA tangu kuingia madarakani kwa uongozi mpya wa chama hicho Desemba 12, chini ya Mwenyekiti wake Almas Kassongo.

  0 0

  Mgeni rasmi katika mashindano ya ngoma za asili kwa Mkoa wa Tabora Mstahiki Meya wa manispaa ya Tabora Gulamhussein Remtullah akizungumza na wakazi wa Mkoa huo katika mashindano hayo chini ya udhamini wa kampuni ya Bia Tanzania kupitia bia yake ya Balimi Extra , mashindano hayo yamefanyika katika shule ya sekondari Iyungi.tolle
  Kushoto meneja wa matukio wa kampuni ya Bia Tanzania - tbl kanda ya ziwa Bwana Erick Mwayela akimkabidhi Meya wa Manispaa ya Tabora Mstahiki Meya Gulamhussein Remtullah kitita cha shilingi laki sita ikiwa ni zawadi ya mshindi wa kwanza wa mashindano ya Ngoma za asili kwa mkoa wa Tabora mashindano hayo yamedhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania kupitia Bia yake ya Balimi Extra kulia aliyevaa fulani ya balimi ni kiongozi wa kundi la Mwenge la manispaa hiyo ambao ndio wameibuka washindi wa shindano hilo.
  Meya wa Manispaa ya Tabora katikati Akimkabidhi kiongozi wa kundi la Mwenge fedha tasilimu shilingi laki sita mara baada ya kundi hilo kutangazwa Washindi wa shindano la ngoma za asili kwa mkoa wa Tabora ambalo limefadhiriwa na kampuni ya Bia Tanzania Tbl kupitia Bia yake ya Balimi Extra kulia kwake ni Meneja matukio wa kampuni hiyo kanda ya Ziwa Bw Eric Mwayela.

  0 0

  Afisa Uhakiki wa Miradi ya Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania(Tanzania Media Fund) TMF.Sanne Vanden Barg akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari wa magazeti ya Changamoto na The Football wakati ujumbe wa TMF ulipotembelea katika ofisi za Ladyband zilizopo mtaa wa Daima Mikocheni jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Miradi wa TMF Alex Kanyambo na Kushoto ni Naibu Mhariri Mtendaji wa Gazeti hilo Samson Kamalamo.

  0 0
 • 06/18/13--04:20: mapitio ya magazeti leo

 • 0 0

  Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini kwa kushirikiana na Chuo cha Sokoine cha Kilimo (SUA) chini ya ufadhili wa shirika la ‘Climate Change Agriculture and Food Security CCAFS’ linalotekeleza mradi wa elimu ya asili katika utoaji wa utabiri wa hali ya hewa katika wilaya ya Lushoto.

  Akizungumza katika uzinduzi huo,Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania , Dkt Agnes Kijazi alisema utekelezaji wa mradi huu ulianza Agost 2012 na unatarajiwa kuisha mwezi Desemba 2013 ambapo watabiri wa asili wapatao 27 wamehusishwa.

  Dkt Kijazi alisema kwa vile wilaya ya Lushoto hupata misimu miwili ya mvua kwa mwaka yaani Vuli na Masika, watabiri hao waasili walihusihwa katika kutoa utabiri wa Vuli 2012 na Masika 2013, na kubaini kushabihiana kwa kiasi kikubwa kwa utabiri wa kisayansi uliotolewa na TMA pamoja na ule wa asili, viashiria vya asili vinavyotumika ni pamoja na wadudu,mimea,wanyama na upepo.

  Aliendelea lusema katika kuhakikisha kwamba utabiri wa hali ya hewa unawafikia wakulima kwa wakati ndipo TMA na SUA wameanzisha mfumo wa FarmSMS ambapo uendeshwaji wake utakuwa TMA.

  Akizundua rasmi mfumo huo, Kwa niaba ya MKuu wa Wilaya ya Lushoto Bwana Charles Moshi aliwashukuru TMA pamoja na SUA kwa kuwakumbuka wakulima wa Wilaya yake, kwa vile Wilaya ya Lushoto ni moja ya eneo lililoathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi kwa kupata upungufu wa mvua katika maeneo mengi, hivyo natarajia kwa mfumo huu wakulima wataweza kupata taarifa sahihi na kwa wakati, Bw. Moshi alisema wazee wa lushoto wamekuwa wakitoa utabiri wa hali ya hewa kwa njia ya asili tangu zamani, ni faraja yetu kuona sasa watabiri wa asili wataweza kuungana na watabiri wa kisayansi katika kutoa utabiri wa eneo husika katika wilaya yetu, hali hii isaidia kuweka kumbukumbu za viashiria vya asili vya utabiri wa hali ya hewa kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

  Aliendelea kuwashukuru wa TMA kwa kuweka kituo cha hali ya hewa kinachojiendesha chenyewe (Automatic Weather Station) katika Wilaya yake na kuahidi kuwa uongozi wa wilaya ya Lushoto utahakikisha matokeo ya utafiti yanakuwa endelevu Akizungumza kwa niaba wa wazee wa asili na wakulima wa Wilayani Lushoto,Bw. Benard alisema kutokana na mabadiliko ya tabia nchi baadhi ya viashiria vinapotea hivyo kwa kushirikiana na utabiri wa kisayansi hii itasaidia wakulima kujua hali ya hewa sahihi na pia kuwepo kwa kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.

  Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini kwa kushirikiana na SUA kupitia msimamizi wa mradi Profesa Henry Mahoo wamezindua rasmi huduma ya FarmSMS ambapo mkulima ataweza kupata utabiri wa hali ya hewa, ushauri na tahadhari za hali ya hewa kupitia simu ya mkononi.
  Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt.Agnes Kijazi akifafanua jambo kwa wakulima na watabiri wa asili.
  Baadhi ya wakulima na watabiri wa asili wakifuatilia uzinduzi wa FarmSMS.
  Bw.Edwin Ligenge, mtaalam kutoka TMA akieleza jinsi ya kujiunga na huduma ya FarmSMS.
  Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Bw. Charles Moshi(wa tano kutoka kulia mstari wa mbele), Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi( wan ne kutoka kulia mstari wa mbele), Msimamizi wa mradi na mwakilishi kutoka SUA Prot. Mahoo (wa pili kutoka kushto mstari wa mbele) katika picha ya pamoja na wataalam kutoka TMA, SUA na watabri wa asili na wakulima.

  0 0


  0 0
 • 06/18/13--07:00: taarifa ya msiba
 • FAMILIA YA MAREHEMU MWALIMU. PHILIP NHIGULA WA MALYA MWANZA WANASIKITIKA KUONDOKEWA KWA BABA YAO MPENZI MWALIMU PHILIP NHIGULA (86) ALIYEFARIKI TAREHE 17/06/2013 SAA SABA MCHANA HOSIPITALI YA TAIFA MUHIMBILI AMBAKO MWILI UMEHIFADHIWA.


  SHUGHULI ZOTE ZA MIPANGO YA MAZISHI ZINAFANYIKA KIJITONYAMA, DAR ES SALAAM NYUMBANI KWA MTOTO WA MAREHEMU MRS. SAYAYI. MAZISHI YATAFANYIKA JUMAMOSI TAREHE 22/06/2013 MAKABURI YA KINONDONI.

  TAARIFA ZIWAFIKIE NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI POPOTE PALE WALIPO.

  0 0

  Mahmoud Ahmad,Arusha

  Jeshi la polisi limekipiga marufuku chama cha demokrasia na maendelo (CHADEMA) kufanya shughuli zozote za kuaga miili ya marehemu kwenye viwanja vya Soweto kwani zoezi la uchunguzi bado linaendelea kwenye viwanja hivyo huku mabomu yakirindima uwanjani hapo.

  Akizungumza ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani hapa Liberatus Sabas alisema kutokana na uchunguzi unaoendelea wa tukio la bomu kwenye viwanja hivyo imeonelea kuwa si busara kuweka mkusanyiko wa watu kwani kutaharibu upelelezi. Kamanda Sabas alisema kuwa kwa hiyo jeshi hilo limewataka viongozi wa chama hicho kuwaeleza wafuasi wao mahali sahihi watakapoweza kufanyia shughuli hiyo lakini si kwenye viwanja hivyo.

  Hali kwenye viwanja hivyo imekuwa ya pilika pilika tangia juzi kwa wafuasi wa chama hicho kujikusanya tokea asubuhi hadi jioni kwa madai ya kuomboleza tukio la bomu la kurushwa kwa mkono lililotokea uwanjani hapo juzi.

  Hata hivyo viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo walikuwa wamukusanyana kwenye uwanja huo hali iliyoendelea kuleta mvutano kati ya viongozi wa jeshi la polisi na wafuasi hao baada ya kukaidi amri ya jeshi hilo mabomu yalirindima uwanjani hapo.

  Baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho walikuwepo uwanjani hapo akiwemo mbunge wa jimbo la ubungo John Mnyika,Ezekia Wenje na wabunge mbali mbali wa chama hicho walikuwa kwenye kikao cha bunge kinachoendelea hali hiyo imeliweka jiji hili kusimama shughuli zake kutokana na mabomu hayo.

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Ngosi Mwihava akifungua mafunzo kwa wakufunzi wa Vyuo vya ufundi na Taasisi za Teknolojia kutoka Zanzibar na Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Kigoma na Morogoro. Mafunzo hayo ya siku nne yamefunguliwa leo katika Hotel ya Blue Pearly jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mazingira - Ofisi ya Makamu wa Rais, Dk. Julius Ningu.
  Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia hotuba ya ufunguzi kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Ngosi Mwihava (Hayupo pichani)mafunzo hayo ni maalum kwa wakufunzi wa Vyuo vya ufundi na Taasisi za Teknolojia kutoka Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Kigoma, Morogoro na Zanzibar. Mafunzo hayo ya siku nne yamefunguliwa leo katika Hotel ya Blue Pearly jijini Dar es Salaam yanalenga kukuza uelewa wa kutambua gesi haribifu kwa mazingira.
  Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Ngosi Mwihava (waliokaa wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo.

  0 0

  KUMRADHI WADAU: LUGHA ILIYOTUMIKA KWENYE HABARI HII NI YA KIARABU NA KINA SIE LUGHA HIYO NI NOT RICABO,LAKINI MAHOJIANO NA MSICHANA HUYO AMBAYE NI MTANZANIA YAPO KWA LUGHA YA KIMOMBO,HIVYO MSIACHE KUANGALIA VIDEO HII MPAKA MWISHO.


  0 0

  IMG_7191
  Mwanasheria –Mshauri Mwelekezi katika Masuala ya Haki za Ardhi - Emmanuel Massawe akifafanua jambo kwa wageni waalikwa wakati wa hafla ya kuwatangaza rasmi mabalozi wa OXFAM katika Kampeni ya GROW nchini itakayowezesha mfumo wa chakula kuwa wa haki na salama.

  Taasisi isiyo ya kiserikali ya OXFAM kwa kupitia Kampeni yake ya GROW imewakutanisha pamoja masupa staa saba wa Tanzania wakiwemo Mbunge wa Kawe Mh. Halima Mdee pamoja na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mh. Shy-Rose Bhanji kufanyakazi pamoja na vikundi vya wanawake wajasiriamali na wazalishaji, kwa lengo la kuhakikisha hakuna mtanzania atakayeteseka kwa njaa wakati mbinu za kilimo zinaweza kufanikiwa.

  Akizungumza wakati wa kuwatambulisha rasmi mabalozi wa OXFAM kupitia kampeni hiyo, mmoja wa mabalozi hao Bi. Khadija Mwanamboka amesema kilimo sio tu ni sekta endelevu nchini Tanzania bali pia ni Nyanja inayowezesha kupatikana kwa chakula kwa familia na akiba ya chakula kwa taifa kwa kuwa asilimia 80 ya wajasiriamali nchini ni wakulima.

  Nchini Tanzania takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 60 ya wajasiriamali wanawake wanajihusisha na kilimo kikiwepo cha mbogamboga na matunda.

  Aidha kampeni hiyo inakusudia kuendeleza na kukuza uzalishaji utakaoyafanya mazao hayo ya kilimo kuwa na bei muafaka kwa faida ya wakulima hao wa chini na wa kati.
  IMG_7195
  Naibu Mkurugenzi Mkazi OXFAM-Justin Morgan akziungumza na wageni waalikwa namna kampeni hiyo itakavyofanya kazi zake za uhamasishaji hapa nchini.


  0 0
 • 06/18/13--14:30: Article 22


 • 0 0

  Watanzania waishio kwenye mji wa Nurnberg na sehemu za jirani na mji huo nchini Ujerumani,wameshiriki vyema Maonyesho ya Afrika Festival Nurnberg iliyofanyika kuanzia tarehe 13.-16. Juni 2013 mjini huo.Wageni mbali mbali walifanikiwa kutembelea Banda la Tanzania kujionea mambo mbali mbali yaliopo nchini kwetu.
  Bwana Ramadhani Barungi akitoa maelezo kwa mgeni.
  pilikapilika katika Banda la Tanzania.
  Wageni wakionja maandazi na chapati.
  Bwana Mukada Kidawa kushoto na Bwana Erick Morro, mwenyekiti wa Watanzania Nurnberg wakipokea msaada wa vifaa vya michezo na muziki kwa ajili ya Taasisi ya Talent Search and Empowerment.

  0 0
 • 06/18/13--20:00: ngoma azipendazo ankal

older | 1 | .... | 166 | 167 | (Page 168) | 169 | 170 | .... | 3272 | newer