Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1668 | 1669 | (Page 1670) | 1671 | 1672 | .... | 3272 | newer

  0 0
  0 0

   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akipata maelezo Kutoka  kwa,  Afisa Utawala wa TPC aliyeshika kofia  Bwana Jafari Ally  kuhusiana  na Shughuli zinazo endelea katika kiwanda cha Kutengeneza  Sukari  cha TPC  , Kushoto kwa Waziri Mkuu  aliyevaa shasti jeupe ni Meneja wa kiwanda  Bwana  Pascal Petiot, Waziri Mkuu alitembelea Kiwanda  hicho hivi karibuni.
   Waziri Mkuu  Kassim  Majaliwa, akipata maelezo  Kutuko  kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Sukari cha (TPC) Bwana Robert  Baissac,  kuhusu mbegu za kisasa za Miwa zinazozalishwa  kitika  Shamba Darasa  la Kiwanda cha Sukari cha TPC Kilichopo  Mkoani Kilimanjaro Waziri Mkuu alitembelea Kiwanda  hicho hivi karibuni
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akipata maelezo  kutoka kwa  Meneja wa Kiwanda cha Sukari (TPC) Bwana  Pascal Petiot  kuhusiana na Mitambo Mipya ya Kompyuta ambazo zimefungwa  ili kuongeza Ufanisi Katika Kiwanda  cha TPC Kilichopo Mkoani Kilimanjaro, Waziri Mkuu alitembelea Kiwanda  hicho hivi karibuni
   Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa,  akiangalia Mitambo  mipya   inayofungwa  katika Kiwanda cha   kutengeneza  Sukari  cha  TPC, Kilichopo Mkoani Kilimanjaro, Waziri Mkuu alitembelea Kiwanda  hicho hivi karibuni
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akisalimiana na kiongozi wa Chama  cha Wafanyakzi  wa kiwanda cha Sukari  TPC (TASIWU)  Bwana Bilali Omari, waliopo katikati aliyeva  Tisheti ni Mkurugenzi Mtendaji wa TPC  Bwana  Robert  Baissac na Meneja wa Kiwanda hicho Bwana  Pascal  Petiot, Waziri Mkuu alitembelea Kiwanda  hicho hivi karibuni. PICHA NA PMO

  0 0


  Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

  Raia wa Kenya, Samson Mbaria Pirias maarufu kama Babaa, 38, na raia wa Tanzania, Lohelo Boniphace Mwabulanga anayejulikana zaidi kama Diblo, 43, wamepandishwa kizimbani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,  wakikabiliwa na tuhuma za kusafirisha binadamu kutoka nchini Kenya kwenda Afrika Kusini kuwafanyisha kazi kwa lazima.

  Mwendesha Mashtaka Wakili wa Serikali, Elia Athanas amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 4(1) (a) na (1) (2) (c) na 4 cha sheria ya kusafisha binadamu sura ya sita ya mwaka 2008.

  Wakili Athanas amedai kuwa, Februari 28,mwaka huu, huko Chanika wilaya ya Ilala washtakiwa hao walikutwa wakiwasafirisha watu 11 kutoka Kenya kwenda Afrika Kusini kwa lengo la kuwafanyisha kazi kinguvu.

  Aliwataja watu hao kuwa ni Dhaha Maliya All, Hassen Gales Omar, Ahmed Lobiso Abdi,Dhawil Ayantu Duri, Omar Yahye Mohammed, Hikma Ibrahim Omar, Istahil Ali Shukri, Rashid Omar Yusuf,Abdul Khalid Asiis, Abbdulah Sartu na Hassen Guled Omar.

  Hata hivyo, washtakiwa hao wote wawili wamekana tuhuma hizo na wamerudishwa rumande kwa sababu shtaka linalowakabili la kusafirisha binadamu ni moja kati ya mashtaka yasiyo na dhamana.

  Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa shauri hilo bado haujamalika. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 17,mwaka huu kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya kutajwa tena.

  0 0

  Na Nuru Juma & Husna Saidi- MAELEZO

  Waandishi wa Habari nchini wametakiwa kuzingatia kanuni,sheria na taratibu za uandishi katika kuandika habari zitakazoleta umoja,mshikamano na maendeleo na siyo uchochezi ili kujenga jamii bora.

  Hayo yamesemwa leo Jijini Mwanza na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Harrison George Mwakyembe kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani.

  Dkt. Mwakyembe aliongeza kwa kusema kuwa Serikali inatambua umuhimu wa siku ya uhuru wa vyombo vya habari ambapo siku hiyo huwa maalum kwa wadau wa tasnia hiyo kukutana na kujadiliana mambo mbalimbali ikiwa ni njia ya kujenga jukwaa la ushirikiano.

  “Uhuru wa habari una ukomo wake hivyo ni muhimu kwa vyombo vya habari hapa nchini kuajiri watu wenye taaluma hiyo kwa kuachana na makanjanja ili viheshimike kwa kutoa taarifa zenye kuzingatia maadili ya uandishi”, alisema Dkt. Mwakyembe.

  Alizidi kufafanua kuwa katika kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, kalamu ya mwandishi wa habari itetee ukweli na si mambo ya haramu kwa sababu ya siasa au rushwa ambayo huwa kichocheo cha uvunjifu wa amani.

  Aidha aliitaka Idara ya Habari (MAELEZO) kuwa na utaratibu wa kukutana na wahariri kila mwezi ili kuweza kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili tasnia nzima ya habari nchini.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi alisema uandishi wa habari si biashara ya kawaida bali ni kazi yenye kuhitaji uweledi mkubwa hivyo waandishi wanatakiwa kufuata taratibu na sheria za uandishi.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella amehitimisha kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, yaliyofanyika kitaifa Jijini Mwanza.

  RC Mongella amewasisitizia wanahabari kujikita zaidi katika weledi kwenye utendaji wao wa kazi ili kuondokana na migogoro inayoweza kujitokeza wakati wakitimiza majukumu yao.Amewahimiza zaidi waandishi wa habari kujikita kwenye habari za uchunguzi na utafiti wa kina katika habazi zao huku akihimiza zaidi ushirikiano.
  Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi (kushoto) akifuatilia maadhimisho hayo. Kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Salome Kitomari.
  Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC, Deogratius Sonkolo (kulia) na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini TEF, Theophil Makunga (kushoto), wakifuatilia maadhimisho hayo.
  Mkurugenzi wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC, Abubakar Karsan, akichangia mada kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, kitaifa Jijini Mwanza.


  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  UCHAGUZI wa viongozi wa Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu (TAFCA) Mkoa wa Kinondoni uliokuwa ufanyike Mei 7 mwaka huu jijini Dar es Salaam sasa umesogezwa mbele hadi Juni 4.


  Uamuzi wa kusogeza mbele uchaguzi huo umetokana na mwitikio mdogo wa uchukuaji fomu kwa wagombea. Muda wa uchukuaji fomu sasa umeongezwa hadi Mei 7 mwaka huu.

  Fomu kwa ajili ya wagombea zinatolewa kwenye ofisi za Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kinondoni (KIFA) kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 10 jioni.

  Ada ya fomu kwa wagombea wa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TAFCA ni sh. 50,000 wakati Mhazini, Mhazini Msaidizi na wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni sh. 30,000.

  Ajenda ya uchaguzi itatanguliwa na Mkutano Mkuu wa Kawaida ambao mbali ya taarifa ya utendaji, Kamati ya Utendaji inayomaliza muda wake pia itawasilisha ripoti ya mapato na matumizi.

  Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA Kinondoni inaongozwa na Mwenyekiti wa zamani wa TAFCA, Ramadhan Mambosasa.

  Kamati ya Utendaji ya TAFCA Kinondoni inayomaliza muda wake inaongozwa na Mwenyekiti Eliutery Mholery (0715 621 667) na Katibu Mkuu wake Mbwana Makata (0655 520 129).


  0 0

   Mdhamini wa Taasisi ya Kilimanjaro Dialogue, Habib Miradji (katikati) akiongoza mjadala jijini Dar es Salaam leo, kuhusu umuhimu wa wanahabari kuandika habari za kudumisha amani nchini ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani. Mjadala huo uliandaliwa na taasisi hiyo. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
    Mdhamini wa Taasisi ya Kilimanjaro Dialogue, Habib Miradji (katikati) akiongoza mjadala jijini Dar es Salaam leo, kuhusu umuhimu wa wanahabari kuandika habari za kudumisha amani nchini ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani. Mjadala huo uliandaliwa na taasisi hiyo. Kutoka kulia ni Rais wa taasisi hiyo, Ali Akkiz na Mshauri wa masuala ya Habari, Felix Kaiza.
   Mshauri wa Masula ya Habari, Felix Kaiza akielezea umuhimu wa wamiliki wa vyombo vya habari kuweka utaratibu wa mafunzo ya ndani (In House Training) kwa waandishi wa habari ili kuinua weledi pia alishauri kuwepo na Exchange Program kati ya vyombo vya habari nchini na nje ya nchini jambo ambalo huwaongezea uwezo wanahabari.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Uongozi wa Klabu ya Simba, umeweka bayana uamuzi wao wa kwenda Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kudai haki yao baada ya kupokwa pointi tatu na Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji huku wakiwa wanasubiri barua kutoka Bodi ya Ligi ili wawasilishe malalamiko yao.

  Simba imefikia hatua hiyo baada ya Kamati ya utendaji kukaa na kuamua kwa kauli moja kulipeleka mbele zaidi suala hilo kutokana na kuona kasoro za kikanuni katika maamuzi yaliyotolewa na Kamati ya Uendeshaji wa Usimamizi wa Ligi kwa sababu ambazo wanaziona si za msingi kutokana na kanuni kuwa wazi.

  Akizugumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam, Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva, amesema wanachokisubiria kwa sasa ni ku njia zipo nyingi za wao kupata haki yao, hivyo wanasubiri kupewa barua kutoka Bodi ya Ligi ambayo wataiambatanisha kwenda Fifa kudai haki yao.

  Aveva amesema wamefuatilia njia za kudai haki yaona wameambiwa gharama inaweza kuanzia dola 15,000 na wapo tayari kulipa ili tupate haki yao ambayo mpaka sasa wanasikia tu kama wamepokwa pointi 3 walizopatiwa na kamati ya saa 72 baada ya kushinda rufaa yao dhidi ya Kagera Sugar ambayo inadaiwa ilimchezesha beki wake, Mohammed Fakhi akiwa na kadi tatu za njano dhidi yao.

  Maazimio hayo yaliyofikiwa kwa pamoja na kamati ya utendaji yameainisha kuwa pamoja na hilo, pia wanapeleka malalamiko yao kuhusiana na mchezaji wao Mbaraka Yusuph aliyeidhinishwa kucheza katika klabu ya Kagera wakati tayari akiwa na leseni ya kuchezea ya klabu ya Simkba.

  Raisi wa Klabu ya Simba Evance Aveva akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uamuzi wa kamati ya Utendaji wa klabu hiyo kuazimia kwa pamoja kupeleka malalamiko yao Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA kutokana na kutokufa nyiwa haki na Shirikisho la Mpiera wa Miguu Nchini TFF.
   Raisi wa Klabu ya Simba Evance Aveva akionesha leseni ya mchezaji Mbaraka Yusuph waliyopatiwa na  Shirikisho la Mpiera wa Miguu Nchini TFF.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa JHPIEGO nchini Tanzania Ndg. Jeremie Zoungana, aliyekuja kuzungumza nae na kubadilishana uzoefu wa kazi, kabla ya kuanza kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma
  Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (kulia) akizungumza na ugeni uliomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma, ukiongozwa na Mkurugenzi Mkazi wa JHPIEGO nchini Tanzania Ndg. Jeremie Zoungana (wa pili kulia).
  Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Mradi wa USAID wa Boresha Afya, Ndg. Dustan Bishanga (wa pili kushoto) akizungumza leo katika kikao kilichofanyika Ofisini kwake Mjini Dodoma. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

  0 0


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  HISTORIA inaendelea tena kuandikwa baada ya bendi kongwe mbili za muziki wa Dansi nchini DDC Mlimani Park "Sikinde Ngoma Ukae" na OTTU Jazz "Msondo Ngoma" zitakutanishwa tena katika jukwaa moja kumtafuta nani mkali wa kulisakata rumba Mei 20 mwaka huu.

  Bendi hizo kongwe zitakutana tena katika jukwaa  moja  na kumtafuta nani mkali huku kila upande ukitamba kumgaragaza mwenzake na kuibuka kidedea katika mpambano huo.

  Pambano hilo linatarajiwa  kufanyika Mei 20 Mwaka huu katika ukumbi wa Traventine Magomeni huku mashabiki wa kila upande wakiombwa kuja kuhudhuria kwa wingi kuwaona wakali hao huku burudani za  nyimbo za zamani zikiratajiwa kutawala kwenye usiku huo.

  Akizungumza kuelekea pambano hilo, mratibu Abdulfareed Hussein alisema mpambano huo wa nani zaidi utamuliwa na mashabiki wa dansi watakaojitokeza siku hiyo na zaidi kutakuw ana zawadi ambayo ni siri itakayotolewa siku hiyo.

  Alisema kiingilio cha pambano hilo kitakuwa ni Sh. 10,000 ili kuwapa nafasi wadau wa dansi kushuhudia na kutoa maamuzi ya nani zaidi kati ya bendi hizo mbili.
  Mratibu Abdulfareed Hussein akiwa katika picha ya pamoja na waimbaji wa bendi za  DDC Mlimani Park "Sikinde Ngoma Ukae" na OTTU Jazz "Msondo Ngoma" wakijiandaa na mpambano wa kumsaka Mkali nani Mei 20 mwaka huu.
   Mratibu Abdulfareed Hussein akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mpambano wa kumsaka mkali wa muziki wa dansi baina ya  DDC Mlimani Park "Sikinde Ngoma Ukae" na OTTU Jazz "Msondo Ngoma" utakaofanyika Mei 20 mwaka huu. Pembeni ni viongozi na waimbaji wa bendi hizo kulia ni Abdallah Hemba  kutoka Sikinde na kulia ni Meneja wa Bendi ya Msondo Said Kibiriti. 
   Muimbaji wa bendi ya Sikinde Abdallah Hemba akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mpambano huo baina yao na Msondo utakaofanyika Mei 20 mwaka huu. Kushoto ni  Mratibu Abdulfareed Hussein.
    Meneja wa Bendi ya Msondo Said Kibiriti akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mpambano huo baina yao na Msondo utakaofanyika Mei 20 mwaka huu akiwa sambamba na waimbaji wa timu hiyo Romario na Juma Katundu.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  · Mnufaika wa Airtel FURSA bidhaa zake ziko sokoni mikoa zaidi ya mitano

  Mradi wa Airtel Fursa umeendelea kufanikiwa kwa kuendelea kuwezesha vijana nchini ambapo mmoja kati ya waliowezeshwa mwaka jana Bi Threria Maliatabu mkazi wa Mbagala jijini Dar es Saalam ameelezea jinsi mradi huo ulivyomuwezesha kukuza kipato na kupata mafanikio ya kuanza kujenga nyumba yake binafsi, kujinunulia shamba la eka 2 huku akiwaasa vijana wenzake nchni na wale wote waliowezeshwa na Airtel FURSA kuchangamkia fursa hizi pindi zinapotokea.

  Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es saalam , Bi Maliatabu ambaye anajishughulisha na biashara ya uchoraji wa picha za sanaa alisema “ najivunia sana kuwa mmoja kati ya vijana walioshikwa mkono na Airtel Fursa kwa sababu program hii imeweza kunitoa kutoka niliopokuwa hadi kufika kwenye haya mafanikio niliyo nayo leo. 

   Kwakweli nimekuwa na mafanikio makubwa sana ikiwemo kuboresha kiwango cha bidhaa zangu , nimefanikiwa kuanza ujenzi wa nyumba yangu ya vyumba vinne na pia nimeweza kukunua shamba la eka 2 Mkuranga mkoa wa pwani. lengo langu ni kuanzisha shughuli za kilimo ili kutanua wigo wa biashara yangu lakini pia kuendelea na shughuli yangu ya uchoraji nayoifanya kwa sasa”

  Aidha Maliatabu alifafanua kuhusu changamoto mbalimbali katika biashara ikiwemo masoko ya nje , usafiri wa kusambaza bidhaa zake huku akieleza kuwa baadhi ya changamoto hizi ameshaanza kuzishughulikia na kuomba wadau mbalimbali kuweza kumsaidia.
  Theresia Maliatabu, mnufaika wa mradi wa Airtel Fursa akimsikiliza mteja wakati alipohudhuria maonyesho ya bidhaa na kuonyesha kazi ya uchoraji wa picha za Sanaa anazozifanya hivi karibuni.


  0 0

  Wakazi wa Kinondoni  Mahakamani wamelalakia maji yaliyozingira nyumba zao kutokana na baadhi ya wakazi hao kujenga katika mkondo wa maji.

  Akizungumza leo mkazi wa eneo hilo Bi. Khadija Hamis amesema kutokana na mvua za  masika zinazoendelea kunyesha wanapata adha kubwa ya maji hayo yanayotuama kwenye eneo hilo.

  Amesema kuwa baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamezingirwa na maji kwa wiki mbili sasa na hakuna chochote kinachofanyika.

  Aidha amesema kutokana na hali hii kuendelea ,wanaiomba serikali kutatua tatizo hili mara baada ya kuisha masika.
   Mvua zinazoendelea  kunyesha  maeneo mbalimbali katika jiji la Dar es Salaam iliyoanza kunyesha wiki iliyopita, zimesababisha maafa, uharibifu wa miundombinu ya baarabara pamoja na baadhi nyumba katika eneo la Kinondoni Mahakamani kuzungukwa na maji ya mvua  jijini Dar es Salaam.
   Mwanafunzi akikwepa   dimbwi la maji machafu ya mvua kama yanavyoonekana pichani leo jijini Dar es Salaam.picha zote na Emmauel Massaka,Globu ya jamii.


  0 0

  Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi akizungumza na Wataalam wa kujitolea kutoka Japani waliokuja kutoa huduma nchini wakati wa hafla fupi ya kuwakaribisha Wataalam hao iliyofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi leo.
  Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi akiwa katika picha ya pamoja na Wataalam wa kujitolea kutoka Japani waliokuja kutoa huduma nchini.
  Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi akizungumza na Mwakilishi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo Japani (JICA) nchini, Bw. Toshio Nagase mara baada ya hafla fupi ya kuwakaribisha Wataalam wa kujitolea kutoka Japani waliokuja kutoa huduma nchini.

  0 0

  Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar.

  Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo amesema tatizo la kuharibika kwa mashine ya kusagia taka katika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja siku za karibuni kulipelekea kurundikana kwa taka na kusababisha usumbufu kwa wananchi.

  Amesema baadhi ya wafanyakazi wakorofi wa Hospitali hiyo walitumia kasoro hiyo kuzitupa taka kwenye ufukwe wa bahari, nyuma ya Hospitali, ambapo ni kosa kwa mujibu wa sheria na kanuni za afya na uhifadhi wa mazingira.

  Waziri Mahmoud ametoa kauli hiyo alipofanya ziara ya kutembelea mashine ya kusagia taka zinazozalishwa katika Hospitali hiyo ambayo hivi sasa imefanyiwa matengenezo na ipo tayari kufanyakazi na kuondosha kero hilo.

  Amesema wafanyakazi saba waliobainika kufanya kosa la kutupa taka sehemu ya ufukwe wamechukuliwa hatua za nidhamu na kuuagiza uongozi wa Hospitali ya Mnazimmoja kutomvumilia mfanyakazi atakaekiuka kanuni za afya.

  Hata hivyo Waziri wa Afya amekiri kuwa uzalishaji wa taka katika Hospitali ya Mnazimmoja umekuwa mkubwa kutokana na ongezeko kubwa la wagonjwa baada ya kutanuliwa na kufikia daraja la kuwa Hospitali ya rufaa.
  Waziri wa Afya Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo akipata maelezo ya mashine mpya ya kusagia taka za hospitali kwa Mtaalamu wa mashine hizo kutoka Kenya Benard Abere. Picha na Makame Mshenga. 


  0 0

  Na. Hassan Mabuye & Muhammad Salim.

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ameamuru kusimamishwa kazi Afisa Mipango Miji wa Lindi Ndugu Castory Manase Nkuli baada ya kunyang`anya ardhi ya vijiji vya Ruvu na Mchinga hekari 4000 na kumilikisha kampuni ya Azimio Housing Estate kinyume cha sheria ya Ardhi.

  Mhe. Lukuvi aligundua hayo baada ya kuona utaratibu wa umilikishaji wa ardhi haukufuatwa  na badala yake kuonekana kuwa na mianya ya rushwa kwa kuwa ardhi hiyo imehamishwa kutoka ardhi ya kijiji hadi kumilikishwa kwa kampuni ya Azimio ambapo kisheria ilitakiwa hati ya eneo hilo itoke kwa idhini ya Rais.

  Aidha, Afisa Mipango Miji huyo aligundulika kuwa na kosa la kughushi kwa kujifanya ni Afisa ardhi baada ya kuandika barua na kuisaini kwa niaba ya Afisa ardhi wakati yeye ni Afisa Mipango Miji ili kuimilikisha kampuni ya Azimio Housing Estate ambalo pia ni kosa kisheria.

  Akithibitisha makosa hayo Kaimu Mkurugenzi Mipango Miji na Vijiji kutoka Wizara ya Ardhi Bi Immaculate Senje amesema kwamba utaratibu wa umilikishaji wa ardhi hiyo haukufuatwa ambapo kisheria ilitakiwa hati ya eneo hilo itoke kwa idhini ya Rais na baada ya Tangazo la Serikali na kuridhiwa na wana kijiji. 

   “Kama nyie hamna uwezo wa kumfukuza kazi basi mie namsimamisha kazi kuanzia leo hafai kuwa mtumishi wa serkali” alisema Mhe. Lukuvi na kuagiza eneo hilo lirudi na kuwa mali ya serikali “ Sasa hiyo ardhi lazima irudi itakua mali ya serikali kuanzia leo” .

  katika ziara hiyo, Mhe. Lukuvi ametembelea ofisi za ardhi Lindi na kufanya ukaguzi katika Masijala za ardhi na kuangalia mfumo wa ukusanyaji kodi ya pango la ardhi, kisha kuwaagiza watendaji wa ardhi mkoani hapo kuhakikisha wanatoa hati kwa wakati na kukusanya kodi ya pango la ardhi kwa kila mmiliki wa ardhi ili kuongeza pato la serikali.

  Pia alitembelea ofisi za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mkoani hapo na kupokea taarifa kutoka kwa Meneja wa shirika hilo mkoani Lindi Ndugu Gibson Mwaigomole. Katika taarifa hiyo Mhe. Lukuvi amelishauri Shirika la Nyumba la Taifa kufanya uwekezaji mkoani Lindi kwa kujenga ofisi za kisasa pamoja na Nyumba zenye gharama nafuu.

  Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi akiwa pamoja na waziri Lukuvi na watendaji wa mkoa ameeleza kuwa sekta ya ardhi mkoani hapo inachangamoto nyingi lakini ofisi yake inaendelea kufanya jitihada za makusudi kuhakikisha changamoto hizo zinapungua au kuzimaliza kabisa kwa maslahi ya watu wa Lindi na Tanzania kwa ujumla. 

   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimsimamisha kazi Ndugu Castory Manase Nkuli Afisa Mipango Miji wa Lindi kuhusu tuhuma za kumilikisha ardhi kinyume cha sheria.
    Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (kushoto) wakihakiki nyaraka na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi (kulia) katika ziara ya Mhe. Lukuvi mkoani Lindi.
   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi, watendaji na viongozi wa Mkoa wa Lindi wakiwa katika mkutano wakati wa ziara ya Mhe. Lukuvi mkoani Lindi.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  0 0


  SIMU.TV: Ripoti ya Tanzania ya hali ya haki ya mwaka 2016 inaonsha kuwa haki ya kuishi kwa watanzania imeendelea kuwa mashakani kutokana na uwepo wa adhabu ya kifo na mauji ya kishirikina. https://youtu.be/B9gjumjVeWQ
  SIMU.TV: Wanahabari nchini wametakiwa kuwa wajasiri na kutekeleza majukumu yao bila woga kwa maana woga unazorotesha uhuru wa utoaji wa habari. https://youtu.be/g8v6JImFd2Y
  SIMU.TV: Wakulima na wafugaji kutoka vijiji 32 vilivyopo wilayani Mbarali mkoani Mbeya wameiomba serikali kubatilisha mpango wake wa kuvifanya vijiji hivyo kuwa sehemu ya hifadhi ya Ruaha. https://youtu.be/XrSbVuIklyo

  SIMU.TV: Kampuni ya Tanzanite One imeamua kujenga kituo cha afya cha kisasa katika mji mdogo wa Mererani ili kusogeza huduma za afya karibu na jamii inayozunguka mgodi huo. https://youtu.be/6vWMz5ViYCc

  SIMU.TV: Madereva wa bodaboda jijini Dar es Salaam wametajwa kuwa waathirika wakubwa wa rushwa ya barabarani wanapokuwa katika majukumu yao. https://youtu.be/xcA54fdtO94

  SIMU.TV: Wafanyabiashara wadogo na wakubwa wa madini nchini wametakiwa kuchangamkia fursa ya maonesho ya madini jijini Arusha ili kuitangaza Tanzania. https://youtu.be/JSBC9P7nYSM

  SIMU.TV: Uongozi wa klabu ya Simba umesema kuwa utakata rufaa FIFA kutokana na kupokwa pointi tatu za walizopewa na kamati ya saa 72 ya TFF. https://youtu.be/6Le08phW5mI

  SIMU.TV: Rais wa klabu ya Simba Evance Aveva amesema mchezo wao wa fainali za FA dhidi ya Mbao Fc utakua mchezo mgumu kutokana na ukubwa wa mashindano yenyewe. https://youtu.be/5Atb7wgSNCE

  SIMU.TV: Klabu ya Atletico Madrid jana ilishindwa kutamba mbele ya Real Madrid baada ya kukubali kichapo cha mabao matatu kwa bila kwenye mchezo wao wa nusu fainali za klabu bingwa Ulaya. https://youtu.be/dR4FlS9CUK8

  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akihutubiwa wakati wa Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Vyombo vya Habari Duniani huadhimishwa kila mwaka mwezi wa mei 3, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Chuo cha Habari Kilimani Zanzibar. Kushoto kwake ni  Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharini Unguja Mhe. Ayoub Mohamed  (kati) na Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Bw. Kajubi Mukajanga. na kuume kwake ni Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar Ndg Chande Omar na  Mhe. Hassan Abdulla Mitawi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo.
  Wanahabari  toka vyombo vya habari Zanzibar wakifuatilia hafla hiyo. 
  Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Habari Tanzania ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo Mhe.  Hassan Abdallah Mitawi akitoa maelezo ya hafla hiyo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja kutowa machache na kumkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kuhutubia Kongamano hilo la kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari.
  Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Bw. Kajubi Mukajanga akitowa maelezo wakati wa Kongamano hilo la Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, yaliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Kilimani Zanzibar. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA
  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack. Kushoto ni Kamanda  wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro.Kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga, Bw. Kadama Malunde.
  Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wa habari mkoa wa Shinyanga kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani Mei 3,2017
  Katibu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Stephen Wang'anyi akisisitiza jambo ukumbini.
  akizungumza ukumbini
  Picha ya pamoja Mkuu wa mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Zainab Telack,wadau wa habari na waandishi wa habari
  Picha ya pamoja Mkuu wa mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Zainab Telack,wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga na waandishi wa habari. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA


  0 0


older | 1 | .... | 1668 | 1669 | (Page 1670) | 1671 | 1672 | .... | 3272 | newer