Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 165 | 166 | (Page 167) | 168 | 169 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Adhabu za viboko kwa watoto imeelezwa kuwa inachangia kwa kiasi kikubwa woga na kuwafanya washindwe kuwa wadadisi hali ambayo ina athari kubwa kwao kitaaluma.

  Rais wa Rottary Club Mzizima, Ambroce Nshala alisema hayo juzi, wakati wa hafla ya chakula cha mchana na watoto waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) iliyoandaliwa na Kituo cha Afrika Sana na Umoja wa makanisa hospitalini hapo.

  Alisema Nshala kuwa ingawa serikali imerudisha adhabu hiyo lakini yeye binafsi anaona haipo sahihi kwani si lazima mtoto achapwe ndio aweze kujifunza kwani uzoefu unaonyesha kuwa viboko mara nyingi huwakanganya wanafunzi.

  Alisema elimu bila viboko inawezekana kikubwa ni ushirikiano baina ya wazazi, walimu na walezi katika makuzi ya watoto na wale ambao inatokea wakakosea basi ni vema wakapewa adhabu mbadala kama vile kufanya usafi na hata kufagia.

  “Watoto wapewe adhabu mbadala na sio viboko kwani aadhabu hizo zinaweza kuwajenga zaidi na kuwafanya watoto hao wakosefu kweli kujutia makosa yao badala ya kuwa kama ilivyo sasa” alisema na kuongeza kuwa adhabu ya viboko pia ina athari kisaikolojia kwa watoto.

  Awali akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Kituo cha Sanaa cha Afrika Sana Ailinda Sawe alisema watoto wa kike ambao ndio wengi kulingana na sensa ya hivi karibuni ndio wahanga wakubwa wa mambo yote yasiyofaa.

  Alisema uamuzi wa kujumuika na watoto hao umetokana na taasisi yake na umoja wa makanisa hospitalini hapo kuguswa na kundi hilo la watoto ambao wengi wao wamelazwa hapo kwa muda mrefu kutokana na maradhi yanayowasumbua na amewataka wanajumuia wengine kulikumbuka kundi hilo.

  “Kuna watoto hapa wamelazwa kwa miezi sita hadi mwaka na mbaya zaidi wengine wametoka mikoani na hawana ndugu wala jamaa hivyo wanahitaji msaada wa wanajamii” alisema na kuongeza kuwa watoto hao wanasumbuliwa na matatizo tofauti ikiwa ni pamoja na saratani ya damu, uvimbe wa vichwa na magonjwa mengine.
  Rais wa Rottary Club Mzizima, Ambroce Nshala akizungumza wakati wa hafla hiyo chakula cha mchana.
  Mkurugenzi wa Kituo cha Sanaa cha Afrika Sana Ailinda Sawe pia alitoa neno wakati wa hafla hiyo.
  Watoto wakitoa Burudani.


  0 0

  Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye tai ya rangi ya taifa) akiwa na Wajumbe wa Bodi ya Dinka Foundation ya Uholanzi. Asiye na tai ni Mhe. Leo Bellekom Mwenyekiti wa Bodi ya Dinka Foundation na mwenye tai nyekundu ni Mstahiki Drs J.Th. Jan Hoekema Mayor wa Wassenaar Uholanzi. Bodi ya Dinka na jiji la Wassenaar kwa pamoja Wanajenga shule ya msingi ya kimataifa ya Dinka Arusha. Hadi sasa wameishatumia Euro 224,000 na wanaendelea kutafuta fedha za kuendelea na ujenzi. Balozi Kamala amekutana na Bodi ya Dinka leo hii Uholanzi na kuishukuru kwa kazi nzuri inayofanya ya kutafuta fedha, kujenga shule ya Dinka na kutoa elimu bora kwa Watanzania. Mchoro ulioshikwa na Balozi Kamala unaonyesha shule itakavyokuwa ujenzi ukikamilika.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Dinka Mhe. Leo Bellekom (mwenye kompyuta) akimueleza Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala mipango mbalimbali ya kuendeleza ujenzi wa Shule ya Kimataifa ya Dinka inayojengwa Arusha Tanzania. Kikao kimefanyika leo ofisini kwa Mstahiki Meya wa Wassenaar, Uholanzi.

  0 0
 • 06/17/13--02:54: mapitio ya magazeti leo

 • 0 0

  Mahmoud Ahmad, Arusha
  Serikali imewapeleka nchini Kenya Vijana wawili waathirika wa mlipuko wa mabomu juzi Arusha kwenda kupatiwa matibabu zaidi kwenye hospital ya Agakhan ya jijini Nairobi.

  Mkuu wa mkoa waArusha Mhe Magessa Mulongo amesema leo kuwa kutokana na maombi ya mama wa watoto hao na kujali wananchi wake serikali imeamua kuwapeleka watoto Sharifa na Fatuma Jumanne nchini Kenya kwa matibabu zaidi.

  Mhe Mulongo alisema kuwa kutokana na ripoti ya madaktari wa hospitali ya Selian na hali za vijana hao kuwa mbaya,  serikali imeamua kugharamia matibabu ya majeraha  kwenye viungo vyao vya mwili na Kichwa.

  Alisema kuwa timu ya madaktari wa mifupa kutoka Hospitali ya Muhimbili kitengo cha mifupa cha MOI tayari wapo jijini hapa kuungana na madaktari wa hospitali za Selian na hospital ya mkoa Mount Meru kuendelea na matibabu ya waathirika hao.

  “iimeamua kwa dhati kuendelea kutoa msaada kwa waathirika ili kuweza kuwatibu wote waliopata majeraha kwenye kadhia hii ya bomu na kuwa wapo pamoja katika kila hali kuhakikisha wanapona kwa gharama yeyote”alisema Mulongo.

  Wakati huo huo Viongozi wa kitaifa akiwemo Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wapo njiani kuja jijini hapa kuendelea kuwapa na kuwafariji wafiwa na waathirika wa bomu lililotupwa kwenye mkutano wa kampeni wa chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) wakati wakifunga kampeni ya uchaguzi mdogo wa udiwani kwenye kata ya Kaloleni jijini hapa juzi.

  0 0

  Waziri waNchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohd Aboud Mohd kulia akibadilishana mawazo na Waziri wa Afya Juma Duni Haji nje ya Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi mbweni nje ya mji wa Zanzibar.
  Muakilishi wa Jimbo La Mji Mkongwe Ismail Jussa Ladhu wakwanza kushoto wakibadilishana mawazo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala bora Haji Omar Kheir katikati na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Zanzibar Othman Masoud Othman katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi mbweni nje ya mji wa Zanzibar.
  Muakilishi wa Jimbo la Uzini Mohd Raza akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Thuwaiba Edington Kisasi wamwanzo kushoto na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haji Omar Kheir wa mwanzo kulia katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni nje ya mji wa Zanzibar.

  0 0

  NA RAYA HAMAD - MAELEZO ZANZIBAR

  Imeelezwa kuwa moja kati ya neema alizopewa mwanaadamu ni umri mrefu hivyo ni wajibu wa kila mmoja wetu kuutumia vyema uhai wake kwa kutenda mema na kushukuru kila siku kwani hapaswi mwanaadamu kuwa aasi bali anachotakiwa ni kumuabudu Mola wake aliyemuumba .

  Kadhi mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis ameyasema hayo katika dua ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kutimiza miaka 93 ya kuzaliwa kwa Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Alhajj Aboud Jumbe Mwinyi iliyofanyika Kiembe Samaki .

  Sheikh Khamis Haji ametowa ukumbusho kwa kusema kuwa “ Ifanye dunia kama kwamba utaishi milele kwa maana ya kutenda mazuri na kumuabudu Allah kama tulivyoamrishwa katika dini pia ifanye akhera yako kama utakufa sasa kwa maana ya kujiandaa kwa kutenda amali njema na kuomba msamaha kila siku .

  Katika khutba yake iliyosomwa na Ustadh Moh’d Yoyota kwa niaba yake Rais Mstaafu Awamu ya Pili Alhajj Aboud Jumbe amesema kuwa anamshukuru Mola wake kwa umri aliyomjaalia kwani ameshuhudia neema nyingi ambazo hazina kiima kisicho kifani,kina wala mizani katika maisha yake na kupitia nyanja tofauti za maisha hadi M/Mungu atakapomjaalia mwisho wa maisha yake.

  Alhajj Aboud Jumbe ameongeza kusema kuwa anamshukuru Mola wake kwa kumpa rehema zake huruma na hisani pale alipokabidhiwa dhamana ya kuongoza baadae kumnusuru na kumfariji na hatimae kumuongoza pale alipoteleza mnamo asiyoyaridhia kwani majibu sahihi ya mithani yetu wanaadamu yanasubiri siku ya malipo ambayo yatupasa tutambue kuwa kila mmoja wetu atakutana nayo.

  “Namuomba Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu azidi kuitakasa amali yangu na kunipa khusni l khatima mimi pamoja na waislamu wenzangu “

  Akitowa shukurani kwa waalikwa waliohudhuria katika dua hiyo kwa niaba ya familia ndugu Mustafa Aboud Jumbe ambae ni mtoto wake amesema kuwa lengo la kusoma dua hii ni kukumbushana namna gani tunatumia neema na kila mmoja vipi atautumia uhai wake na kusisitiza kuwa dua hio ni mwenyewe baba yao aliyetowa utaratibu juu ya namna gani isomwe dua hio “Tumekuwa tukipata masuala mengi kuhusu hali ya mzee wetu jibu ni kwamba hajambo ila uzee tu ndio unaomsumbua, nuru ya macho imepotea ,kusikia kumekuwa shida kidogo lakini anasikia na anazungumza na hii shughuli yake ya leo amepanga mwenyewe”alisisitiza Mustafa Jumbe.

  Nae Sheikh Moh’d Iddi ametowa wito kwa jamii kufanya matendo mema kwani kuwepo kwetu ipo historia ambayo M/ Mungu amewashushia waja wake na aliyebahatika kuishi kwa kumuabudu huyo atakuwa amefaulu.

  Miongoni mwa waliohudhuria katika dua hio ni pamoja na Kadhi Mkuu Mstaafu Sheikh Habib Ali Kombo baadhi ya Masheikh, Familia yake, baadhi ya wanafunzi aliwahi kuwasomesha na kuwafundisha kazi .

  0 0

  Mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia, Kundi C, Kanda ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Ivory Coast (The Elephants) iliyochezwa jana (Juni 16 mwaka huu) imeingiza sh. 502,131,000 kutokana na watazamaji 57,203.

  Tiketi za kushuhudia mechi hiyo ziliuzwa kwa sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.

  Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 76,596,254.24 wakati wa gharama za uchapaji tiketi ni sh. 7,809,104.

  Asilimia 15 ya uwanja sh. 62,658,846.26, asilimia 20 ya gharama za mechi sh. 83,545,128.35 na asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 20,886,282.09.

  Asilimia 60 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 250,635,385.06 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 12,531,769.25 ambayo ni asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa TFF.

  Mechi iliyopita ya Stars dhidi ya Morocco (Lions of the Atlas) kwenye uwanja huo iliingiza sh. 226,546,000.

  Boniface Wambura
  Ofisa Habari
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

  0 0

  Mkazi wa Mbagala Bi.Halima Ibrahim(kushoto)akimweleza ofisa wa Vodacom Tanzania, Pasco Magesa (katikati) jinsi anavyonufaika na Promosheni ya Cheka Nao. Vifurushi vya Cheka Nao vinawawezesha wateja kuongea na mitandao yote bila mipaka kwa bei nafuu. Ili kujiunga, mteja anatakiwa kupiga *149*01#. Anayeshuhudia kulia ni Meneja Uhusiano wa Jamii wa Vodacom Tanzania.Bw.Matina Nkurlu.
  Ofisa wa Vodacom Tanzania, Rehema Meleki (wa pili kutoka kulia) akimwelezea Bw.John Mhiza (kushoto) ambaye ni mkazi wa Mbagala, jinsi ya kujiunga na ofa ya Cheka Nao,nakumwezesha mteja wa mtandao huo kuongea bila mipaka na mitandao yote nchini. Kujiunga na Ofa hiyo mteja anatakiwa kupiga *149*01#.
  KAMPUNI ya Simu za Mikononi ya Vodacom Tanzania, jana ulifanya zoezi la kuwatembelea wakazi na wananchi wa Mbagala, jijini Dar es Salaam, sambamba na kuwafikishia huduma za usajili wa namba zao za simu pamoja na kuelimishwa juu ya huduma ya Cheka Nao na zinginezo kwa kwa ujumla.

  Shughuli hiyo ilianza asubuhi kwa wahudumu wa mtandao huo kuzungumza pia na wateja wao, ambao walijumuika pamoja kupewa huduma hizo, huku ikienda sambamba na urudishwaji wa namba zilizopotea nyumba kwa nyumba na kufanyiwa pia usajili.

  Akizungumza katika shughuli hiyo kutembelea wateja wao, Meneja Mauzo wa Vodacom, Kanda ya Mbagala, Idd Mawe, alisema kuwa lengo la kuwatembelea wateja wao ni kuwapa elimu inayohusu mtandao wa simu wa Vodacom Tanzania, unaotumiwa na watu wengi huku ukiwa na huduma mbalimbali.

  Alisema wateja wengi walijumuika pamoja na kupewa elimu inayohusu mtandao wao, huku wale wasiosajiliwa wakipewa fursa hiyo, jambo ambalo limepokelewa kwa furaha, baada ya kuwagogezea karibu huduma zao, huku wakikutana na changamoto nyingi, zikiwapo za wateja kutokuwa na uelewa juu ya usajili wa simu zao.

  “Vodacom ni mtandao ulioenea Tanzania nzima, hivyo tumeamua kuja Mbagala na kusambambaza wahudumu wetu sehemu nyingi za Mbagala kwa ajili ya kupata huduma zinazohusu matumizi bora ya simu za mkononi, hususan za Vodacom.

  “Naamini wananchi walitumia vyema nafasi hiyo, huku tukiamini kuwa utendaji kazi huu itaendelea, kwa ajili ya kufanya kazi kwa ushirikiano na wateja wetu kwa namna moja ama nyingine, hasa katika kipindi hiki ambacho ni lazima kila mteja awe amesajili namba yake,” alisema.

  Kwa mujibu wa Mawe, wataendelea kufanya zoezi hilo kwa kipindi cha mwezi mmoja ili kuwapatia elimu hiyo wateja wao, huku kitu pekee kinachohitajika ni kufika na kitambulisho halisi chenye picha kwa ajili ya kusajiliwa.

  Huduma nyingine zinazotolewa na Vodacom ni pamoja na kuweka na kutuma pesa M-PESA, Cheka Nao, ambapo wateja anaweza kujishindia fedha taslimu mpaka kiasi cha Tsh Milioni 100 na kuboresha maisha yao kwa kupitia Mtandao huo ulionea nchi nzima.

  0 0

   Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Bw. Mwanga Ekzaudi ambaye ndio alikuwa mgeni rasmi katika Semina hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

   Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi Bw. Constantine Mashoko akitoa hotuba ya kumkaribisha mgeni rasmi.

   Wadau wa Semina hii wakisikiliza kwa makini hoja zilizokuwa zinatolewa. 
  Watoa mada katika semina hiyo, kutoka kushoto ni Mkaguzi wa Ndani Chuo Kikuu cha Mzumbe Bw. Barikiel Nkinda, Mkaguzi Mkuu wa Ndani Tume ya Pamoja ya Fedha Bw. Cassim Mambo na Mkaguzi Mkuu wa Ndani Mradi wa Mabasi yaendayo kasi (DART) Bw. Alphonce Muro.
   Baadhi ya Sekretarieti ya maandalizi ya mkutano huo wakifanya mapitio ya mada ambazo ziliwasilishwa katika semina hiyo kutoka kushoto ni Bw. Elikira Mathew, Bi. Lightness Mality pamoja na Bi. Wapheba Setembo. 
   Baadhi ya wajumbe walioshiriki kwenye semina hiyo katika picha ya pamoja. Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Fedha.

  0 0

  Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam,Edward Otieno(kulia) akimkabidhi mjasilamali,Pinie Mwasha mashine ya maabara (Outclave sterilizer) wakati wa zoezi la kukabidhi vifaa vya ruzuku kwa wajasiliamali waliofuzu kwenye program ya Safari Lager Wezeshwa kwa kanda ya Pwani iliyofanyika katika Viwanja vya Leaders Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Katikati ni Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo.
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam,Edward Otieno(kulia) akimkabidhi mjasilamali,Jamhuri Oiso mashine ya kutengeneza soli za viatu wakati wa zoezi la kukabidhi vifaa vya ruzuku kwa wajasiliamali waliofuzu kwenye program ya Safari Lager Wezeshwa kwa kanda ya Pwani iliyofanyika katika Viwanja vya Leaders Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

  0 0


  0 0

  Benki ya NMB imeendelea kuwa kinara katika kubuni na kuboresha huduma mbali mbali za kibenki, ili kuwawezesha wateja wake kupata unafuu na urahisi wa upatikanaji wa huduma za kibenki nchini Tanzania. Katika kulizingatia hili mwishoni mwa wiki Benki ya NMB ilizindua akaunti ya Chap Chap ambayo kusudi kubwa ni kuwafikia wananchi wote kule waliko na kuwafungulia akaunti zao.Kikubwa zaidi ni kwamba mteja ataweza kufungua akaunti papo hapo na kupata kadi yake ya kutolea fedha ndani ya dakika kumi

  • Mambo muhimu zaidi ambayo mteja wa Chap Chap anaweza kufaidika nayo ni pamoja na:
  • Kuona salio la akaunti yako popote ulipo
  • Kuweka fedha na kutoa fedha kwa mawakala wa M- pesa
  • Kutuma fedha kwa wasio na akaunti mahali popote nchini kwa kutumia huduma ya Pesa Fasta
  • Kununua vocha za muda wa maongezi kutoka kwenye mtandao wowote wa simu
  • Kuchukua fedha hadi shillingi 1.000,000/= kutoka kwenye ATM

  Mheshimiwa waziri wa fedha Dk William Mgimwa akichukuliwa alama za vidole na Ofisa mauzo ya Nje NMB Abdul Kandoro mara baada ya uzinduzi rasmi wa NMB chap chap akaunti mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma

  Ofisa mtendaji mkuu wa benki ya NMB Mark Wiessing akimshukuru mheshimiwa waziri wa fedha Dk William Mgimwa mara baada ya kuzindua akaunti ya NMB Chap chap .

  Sehemu ya maofisa na wageni waalikwa kwenye uzinduzi huo

  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mkutano wa Mawaziri wa Utumishi wa Umma Barani Afrika Mh. Celina O. Kombani (MB), akihutubia katika sherehe za ufunguzi wa Siku ya Utumishi wa Umma barani Afrika, Accra Ghana.
  Baadhi ya waalikwa kutoka nchi mbalimbali wakimsikiliza Mh. Kombani (MB) akihutubia katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Accra.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani, kushoto, pamoja na Katibu Mkuu-Utumishi Bw. George D. Yambesi wakiwa katika Banda la Tanzania pamoja na baadhi ya watumishi wa ofisi yake.
  Mh. Kombani (MB) akitoa maelekezo kwa baadhi ya washiriki wa Tanzania, wa pili kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi.

  0 0

  Kwa mara ya kwanza Tanzania imeshiriki kwenye usiku wa San Diego Zoo, Jimboni California kwa kutangaza utalii wa wanyama Tanzania na vitutio vyake tarehe 15 Juni 2013.

  Tanzania iliwakilishwa na Balozi wake wa Hiari kutoka jiji la San Francisco, CA Bw. Ahmed Issa na Afisa Ubalozi Mindi Kasiga ambapo walipata fursa ya kuzungumzia utalii wa Tanzania kwa wageni waliohudhuria na pia kuendeleza mahusiano baina ya San Diego Zoo na Tanzania hususan kwenye upande wa uhifadhi.

  Tamasha hili ambalo hufanyika kila mwaka huvutia maelfu ya wadau na washirika wa sekta ya wanyama na utalii wa Marekani na wengi wao hutokea Jimbo la California na vitongoji vyake.

  Mwaka huu 2013, ubalozi ulipata mwaliko kutoka kwa mmoja wapo wa waandaji wa tamasha hilo Bw. Richard Rovsek kwa kupitia taasisi yake ya Spirit of Liberty, ambaye alishirikisha (kwa mialiko) baadhi ya nchi ambazo zinatangaza utalii wa wanyama Tanzania, South Africa, Botswana na Kenya.

  San Diego Zoo ni mojawapo ya bustani za wanyama kubwa nchini Marekani ambapo ina ukubwa wa hekari za eneo (acres) mia moja (40ha) na inahifadhi aina (species) mia nane za wanyama wapatao elfu nne.

  Bustani hii ambayo inashika nafasi ya sita duniani kwa ukubwa wake huandaa tamasha hili maalum kila mwaka ikizawadia washirika wake na kuchangisha pesa kwa ajili ya kuendeshea shughuli zake hususan zile za uhifadhi na elimu kwa umma.

  Kwa mwaka 2012 bustani hii ya wanyama iliingiza kiasi cha dola za kimarekani milioni mia saba kwenye uchumi wa Jiji la San Diego ambapo nusu ya gharama hizo ni kutokana na viingilio vya wageni wanaomiminika kila siku.  Mbali na mualiko wa tamasha la San Diego Zoo, Bw. Rovsek aliandaa hafla ya chakula cha mchana kwa heshima ya Mabalozi wa Hiari wa Tanzania, Botswana na Afrika ya Kusini iliyofanyika San Diego Yatch Club nje kidogo ya jiji hilo.
  Balozi wa Hiari wa Tanzania Bw. Ahmed Issa akijitambulisha kwenye hafla fupi iliyoandaliwa kwa heshima yake na mabalozi wengine wa hiari watatu na Bw. Richard Rovsek wa taasisi ya Spirit of Liberty mjini San Diego CA tarehe 15 Juni 2013
  Bw. Ahmed Issa kwenye picha ya pamoja na Afisa Ubalozi Mindi Kasiga na Bwana na Bibi Richard and Jerry Rovsek baada ya chakula cha mchana na kumtambulisha Bw. Ahmed kwa washiriki wa biashara na wadau wa utalii jijini San Diego, CA.


  0 0

  Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Idd Azan ambaye ni Mbunge wa Kinondoni, wameanza kujichua kwa ajili ya mapambano yao ya ndondi katika Tamasha la Matumaini 2013 litakalofanyika Julai 7 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Halima Mdee atazipiga na Jacqueline Wolper wakati Idd Azan akionyeshana ubabe na Jacob Steven 'JB'
  (Picha na Luqman Maloto /GPL, DODOMA)

  0 0

  Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye tai yenye rangi ya taifa) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Uholanzi (NUFFIC) Bwana Freddy Weima aliye kushoto kwa Balozi Kamala. Mwanzo kulia ni Bi Ute Jansen Mkuu wa Kitengo cha Mpango wa Uholanzi wa Kujenga Uwezo wa Vyuo Vikuu(NICHE) na wa pili kulia ni Bi Johanna Van Nieuwenhuizen Mkuu wa Idara ya Utawala ya NUFFIC. Balozi Kamala ameishukuru Uholanzi kwa kubuni na kutekeleza mpango wa kusomesha Watanzania Uholanzi kupitia taasisi ya NUFFIC na ameomba Uholanzi kuendelea kutekeleza mpango huo. Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya NUFFIC amebainisha kwamba Serikali ya Uholanzi imeongeza miaka minne kuanzia tarehe moja mwezi ujao kuendelea kusomesha Watanzania Uholanzi katika vyuo mbalimbali. Balozi Kamala ameishukuru serikali ya Uholanzi kwa uamuzi huo. Balozi Kamala amekutana na viongozi wa taasisi ya NUFFIC leo hii ofisini kwao, The Hague, Uholanzi.

  0 0
 • 06/18/13--01:42: KIJIWE CHA UGHAIBUNI
 • 0 0

  Mradi wa Uendelezaji Miji Tanzania (TSCP), ambao upo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) ambao ulizinduliwa rasmi 2010, umedhihirisha jinsi ulivyoshamiri kwa kiwango kikubwa. Mabadiliko makubwa yameshaanza kuonekana katika Miji 7 ambamo Mradi huu unaendelea na shughuli zake. Mikoa hii ni; Arusha, Dodoma, Mwanza, Mtwara, Mbeya, Tanga na Kigoma Haya yalibainishwa hivi karibuni wakati wa Kikao cha kutathimini utekelezaji wa Tscp kilichofanyika Dodoma Hoteli – Dodoma. Kikao hicho kilikusanya wajumbe wa Benki ya Dunia, DANIDA, OWM-TAMISEMI na wawakilishi wa Halmashauri kwa kusudi la kutathimini kama Mradi huo unaendelea vyema kufanya ipaswavyo au la. Pia kubaini kama matakwa ya mipango ya Mradi yanafanikiwa na kutoa ushauri ambao utasaidia kufanikisha mafanikio ya kutimiza makusudi ya Mradi kama inavyotarajiwa.
  wajumbe wa Benki ya Dunia, DANIDA, OWM-TAMISEMI na wawakilishi wa Halmashauri wakiwa katika mazungumzo juu ya mradi huo.
  UJENZI WA STANDI YA MABASI MAKUBWA DODOMAUKIENDELEA, UJENZI HUU UNAOFANYWA NA MRADI WA UENDELEZAJI MIJI WA TSCP, ULIO CHINI YA OFISI YA WAZIRI MKUU - TAMISEMI.

  0 0

  Waziri wa Kazi na Ajira,Mhe. Gaudentia Mugosi Kabaka,  akihutubia Kikao cha 102 cha Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) kinachoendelea kufanyika, Geneva Uswisi. Kikao hiki kinakutanisha Wawakilishi wa Serikali, Vyama vya Waajiri na Wafanyakazi toka nchi wanachama 189 wa Shirika hilo. Kikao kilianza tarehe 5/6/2013 na kinatarajia kuisha tarehe 20/6/2013.

  0 0older | 1 | .... | 165 | 166 | (Page 167) | 168 | 169 | .... | 3270 | newer