Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110129 articles
Browse latest View live

Maadhimisho Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Yaanza Mwanza

$
0
0
Mtaalamu wa Mawasiliano nchini, Innocent Mungy akiwasilisha mada kwenye kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza. Kongamano hilo lililoanza leo Mai 2, 2017 linamalizika kesho Mei 3. Mkurugenzi wa Wakfu wa Vyombo vya Habari nchini 'TMF', Ernest Sungura akiwasilisha mada kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza. Baadhi ya wanataaluma ya habari na wadau anuai wa vyombo vya habari wakiwa kwenye kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza.
Baadhi ya wanataaluma ya habari na wadau anuai wa vyombo vya habari wakiwa kwenye kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza.

TAHADHARI YA UTAPELI

Madaktari Hospitali ya BLK India Watembelea Muhimbili leo

$
0
0
Madaktari kutoka Hospitali ya BLK ya nchini India leo wametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa lengo la kuangalia mazingira ya kospitali kama yanaruhusu kuanzishwa huduma za upandikizaji Figo (Renal Transplant).

Pia, madaktari hao wametembelea vyumba vya upasuaji, vyumba vya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU), Maabara Kuu pamoja na Radiolojia.

Daktari Bingwa wa Mfumo wa Mkojo ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Urolojia MNH Dk. Ryuba Nyamsogoro amesema mbali na hilo pia wataalam hao kwa kushirikana na watalaam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wataendesha kambi ya siku mbili kwa ajili ya kutoa huduma ya upasuaji wa kuunganisha mishipa ya damu kwa wagonjwa wanaosafishwa damu (AV Fistula).

‘‘Leo tutawapitia na kuwandaa wagonjwa wote ambao wanatakiwa kufanyiwa upasuaji ili kesho tufanye shughuli hii,’’ amesema Dk. Nyamsogoro. Kambi hiyo itaanza Mei 03 hadi 04, mwaka huu na wagonjwa kati 20 hadi 30 wantarajiwa kufanyiwa upasuaji huo.
Mkurugenzi wa Utumishi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Makwaia Makani ambaye anamwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Museru - kizungumza na madaktari kutoka Hospitali ya BLK ya India wanaohusika na upandikizaji wa figo na wataalamu wengine.
Kutoka kulia ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa mfumo wa Mkojo, Dk Hardev Bhatyal wa Hospitali ya BLK ya nchini India, Mkuu wa Maabara wa BLK, Dk. Anil Handoo na Ofisa uhusiano wa hospitali hiyo, Vigyat Singh wakimsikiliza mkurugenzi wa Utumishi, Makwaia Makani leo.
Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji, Dk Julieth Magandi wa Muhimbili, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi wa MNH, Dk Praxeda Ogweyo, Mkurugenzi wa Uuguzi, Agnes Mtawa wa MNH na Mkuu wa Idara ya Urolojia wa hospitali hiyo, Dk Ryuba Nyamsogoro wakifuatilia mkutano huo leo.
Madaktari na wataalamu wengine wa Hospitali ya BLK kutoka India wakitembelea vyumba vya upasuaji Muhimbili leo.
Madaktari na wataalamu wengine wa Hospitali ya BLK kutoka India na wenzao wa Muhimbili wakimsikiliza Mkuu wa Idara ya Mionzi, Dk Flora Lwakatare (kushoto) wakati walipotembelea idara hiyo leo.
Wageni hao wakiwa katika chumba cha ultrasound hospitali ya Taifa Muhimbili leo.

STAR MEDIA TANZANIA YACHANGIA MILIONI ISHIRINI KWA SERENGETI BOYS

$
0
0
Kampuni ya Star Media Tanzania imekabidhi hundi ya shilingi milioni ishirini (20) kwa Waziri Wa Habari Utamaduni na Michezo Dk. Harisson Mwakyembe katika harambee ya kuchangia timu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka kumi na saba Serengeti Boys iliyofanyika April 30, 2017 katika ukumbi wa J.K Nyerere Convetion Center.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mkurugenzi wa StarTimes Tanzania Mr.Wang Xiaobo amesema kuwa “Tunafuraha kubwa sana kuichangia Serengeti boys pamoja na serikali katika jitihada za kukuza michezo nchini

“Tunaitakia timu kila la kheri iweze kuwakilisha vema nchi katika medani za kimichezo kuwa mafanikio ya baadae yanategemea msingi mzuri na uwekezaji mzuri kwa vijana kwani ni hazina nzuri na tegemeo la kesho kwa kuliletea mafanikio taifa.Mbali na uchangiaji huu tutaendelea kuchangia michezo mingine pamoja na shughuli za kiuchumi na kijamii ili kuisaidia nchi katika jitihada zake za kuleta maendeleo kwa wananchi” amesema Xiaobo .

Akizungumza wakati wa kupokea hundi hiyo Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na michezo Dk.Harrison Mwakyembe amewashukuru Star Media Tanzania na ameahidi kuwa serikali itaendelea kushirikiana na wadau katika kufanikisha malengo yao na pia michezo kwa ujumla .

Pia,Ameongeza kuwa bado sekta ya michezo inakabiliwa na changamoto mbalimbali lakini wizara yake itaendelea kurekebisha ikishirikiana na wadau wengine ili kuleta mabadiliko katika sekta hii.
Waziri wa Habari , Sanaa,Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa harambee iliyoandaliwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa ajili ya kuchangia timu ya taifa ya Vijana chini ya Miaka 17 Serengeti Boys.
Mkurugenzi wa Shirika la utangazaji Tanzania (TBC), Dk. Ayoub Rioba akizungumza wakati wa Harambee ya kuchangia Timu ya Taifa ya Serenegeti Boys.

Lake Cement inalinda mazingira ya wananchi wa Kimbiji –Katemba

$
0
0
 
Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii 

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni , Stephen Katemba amesema kiwanda cha Lake Cement kinafuata sheria za utunzaji wa mazingira kwa wananchi wa Kimbiji. 

Katemba amesema hayo wakati alipokwenda kusherekea siku ya wafanyakazi na kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii zinazofanywa na Lake Cement, amesema kuwa kiwanda kwa kufuata sheria ya mazingira na sheria za wafanyakazi kamwe migogoro haiwezi kutokea. 

Amesema kuwa wafanyakazi lazima wafanye kazi kwa kujituma ili kiwanda kiweze kujiendesha katika kuweza kufikia malengo ya kutimiza kwa wafanyakazi wake. 
Katemba amesema wakati kitendo cha Kiwanda kudhamini mashindano mbalimbali katika eneo la kimbiji ni kuonyesha kiwanda kinajua wajibu wake. 

Makamu wa Rais wa Lake Cement , Afroz Ansary amesema wanawajibu wa kuwa karibu na jamii ya Kimbiji katika shughuli za kijamii . Mafanikio ya kiwanda yanatokana na jamii inayozunguka kushirikiana katika masuala mbalimbali ya kijamii. 

Nae Afisa Utumishi wa Kiwanda hicho, Ahmed Mstapha amesema kuwa kiwanda cha Nyati Cement kinatekeleza majukumu yake kwa jamii inayozunguka kiwanda hicho. 

Amesema kuwa wataendelea kuwa karibu na wananchi katika shughuli mbalimbali ambazo zinajitokeza katika eneo la Kimbiji.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni, Stephen Katemba akizungumza na wafanyakazi mara baada kutembelea kiwanda hicho katika siku ya wafanyakazi na kushiriki shughuli mbalimbali ikwemo ya upandaji jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Lake Cement, Afroz Ansary akizungumza juu ya udhamini wa shughuli mbalimbali zinazofanywa na kiwanda hicho.
Meneja Rasilimali Watu wa Lake Cement, Julieth Domel akizungumza juu jinsi wanavyoshugulika na wafanyakazi wa kiwanda kwa kufuata sheria za Kazi. 

SERENGETI BOYS YABADILISHWA KITUO, YAPANGIWA LIBREVILLE

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Timu ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 Serengeti Boys wameendelea limbwi la ushindi baada ya jana kutoka kifua mbele kwa kuifunga Cameroon katika mchezo wa kirafiki uliofanyika nchini Cameroon.

Timu hizo zitarudiana tena  katika mchezo mwingine wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika kesho Jumatano, Mei 3, mwaka huu.

Mbali na hilo, Afisa habari wa Shirikisho Alfred Lucas amesema kuwa timu ya Serengeti Boys imebadilishiwa kituo kutoka Port Gentil na sasa imepangiwa Libreville.

Serengeti Boys imepangwa kundi B pamoja na timu za Niger, Angola na Mali ambako watafungua nayo mchezo Mei 15, mwaka huu. Kwa mabadiliko hayo, Kundi A lenye timu za Cameroon, Ghana, Guinea pamoja na wenyeji Gabon, litakuwa Port Gentil.

Kwa sasa Serengeti Boys wako Cameroon kwa kambi ya wiki moja iliyoanza Aprili 29, mwaka huu ambako tayari imecheza na wenyeji Cameroon mchezo mmoja na kushinda bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika jijini Yauonde. 

Timu ya Serengeti inahitaji kushinda mechi mbili za mwanzo ili kujihakikishia nafasi ya kwenda kombe dunia  la vijana chini ya miaka 17 litakalofanyika nchini India.

MICHUZI TV: NEC YATANGAZA NAFASI WAZI YA KITI CHA MBUNGE WA VITI MAALUM CHADEMA

$
0
0

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza kuwepo kwa nafasi wazi ya Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, kufuatia kifo cha Mbunge wa Viti Maalum wa chama hicho Mhe. Dr. Elly Marko Macha aliyefariki tarehe 31 Machi 2017.

Akitoa taarifa ya nafasi hiyo kuwa wazi Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage amesema kuwa kwa mujibu wa Kifungu cha 37 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Mhe. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameijulisha Tume juu ya kuwepo kwa nafasi wazi ya Mbunge huyo.

Amesema taratibu za kujaza nafasi hiyo zinaendelea kwa kuzingatia Ibara ya 78 (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ikisomwa pamoja na kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.

Upelelezi kesi ya Wema wakamilika.

$
0
0
Na Karama Kinyunko.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa kesi ya kukutwa na bhangi inayomkabili Msanii maarufu nchini wa filamu, Wema Isaack Sepetu (28) na wenzake wawili umekamilika.

 Wakili wa Serikali, Onolina Moshi aliyaeleza hayo leo  mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa. 

Mheshimiwa, kesi hii leo imekuja kwa ajili ya kutajwa lakini upelelezi umekamilika naomba ahirisho kwa ajili ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali (PH). Amesema Moshi.Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo   hadi Juni Mosi,2017 kwa PH.

Wema amewakilishwa mahakamani hapo na Wakili Tundu Lissu.

Mbali na Wema washtakiwa  wengine ni mfanyakazi wake wa ndani, Angelina Msigwa (21) na Matrida Seleman Abbas (16) aliyetambuliwa kuwa ni mkulima.Watuhumiwa hao wawili wanatetewa na wakili Peter Kibatala na Hekima Mwesigwa.

 Wema ambaye ni mshindi wa taji ya Urembo wa Tanzania (Miss Tanzania) mwaka 2006 alifikishwa mahakamani hapo na kupandishwa kizimbani baada ya kusota mahabusu katika kituo kikuu cha Polisi (Police Central ) Dar es Salaam kwa muda wa siku Sita.

Awali ilidaiwa kuwa, Februari 4 mwaka huu, huko Kunduchi Ununio, wilaya ya Kinondoni, washtakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja wa bangi na vipande viwili.

Hata hivyo washtakiwa hao wote walikana mashtaka hayo na wapo nje kwa dhamana.

VPL KUENDELEA TENA WIKIENDI HII

$
0
0


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

BAADA ya kusimama kwa kipindi cha takribani wiki tatu Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea tena Jumamosi Mei 6 na Jumapili Mei 7, mwaka huu kwa jumla ya michezo sita.

Kwa mujibu wa ratiba, michezo ya Jumamosi kutakuwa na michezo mitano ilihali Jumapili kutakuwa na mechi moja.

Afisa habari wa Shiriukisho la Mpira wa Miguu Alfred Luacs amesema kuwa michezo ya Jumamosi itakuwa ni kati ya Toto African na JKT Ruvu katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati Majimaji ya Songea itakuwa mwenyeji wa Mwadui kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.

Kagera Sugar itaalikwa na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani wakati Young Africans ya Dar es Salaam itaialika Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Siku hiyo ya Jumamosi Mei 6, mwaka huu Azam FC itaialika Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Azam Complex ulioko Mbagala, Dar es Salaam ilihali Jumapili kutakuwa na mchezo kati ya Simba SC na African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Wakati mechi zote zitaanza saa 10.00 jioni, mchezo kati ya Azam na Mbao utaanza saa 1.00 usiku.

KESI YA MABOSI JAMII FORUM YAANZA KUSIKILIZWA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetaarifiwa kuwa, amri ya kukamatwa kwa Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya jamii Forums, ilitolewa na afisa Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SSP Ramadhan Kindai.
Kauli hiyo imetolewa na yeye mwenyewe SSP Kindai wakati akitoa ushahidi wake mbele ya hakimu Thomas Simba dhidi ya mkurugenzi mtendaji wa Jamii Forum, Maxence Melo na Mwanahisa wa Kampuni hiyo, Mike William.

Shahidi huyo wa kwanza wa upande wa mashtaka amedai, alitoa amri hiyo baada ya washtakiwa kushindwa kutoa taarifa sahihi iliyochapishwa kwenye mtandao wa Jamii Forums..

Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Mohamed Salum, Kindai amedai kuwa waliomba taarifa kutoka kwenye kampuni ya jamii Forums kutokana na kesi iliyofunguliwa na Afisa Msimamizi wa mauzo ya rejareja wa Oil Com, Usama Mohammed.

Ameongeza kuwa Usama alifika kwenye ofisi yao na kulalamika kuwa Februari 13,2016 kuna habari ilichapishwa kwenye mtandao wa Jamii Forums kwamba kampuni ya Oil Com wanakwepa kodi bandari ya Dar es Salaam na kwamba wanaiibia serikali.

Amedai kuwa katika kufuatilia kupata ukweli, ASP Fatuma Kigondo aliingia kwenye mtandao huo kutafuta aliyechapisha taarifa hizo ambapo waligundua kuwa ni Fahara JF Expert member ndiye aliyechapisha taarifa hiyo.
Kufuatia hayo, Februari 23, mwaka Jana Kigondo aliandika barua kwenda kwa Mkurugenzi wa Jamii forums ili awapatie taaarifa za mtu huyo ambapo walipokea barua toka Jamii Forums ikidai kuwa wanahaki ya kulinda faragha za wateja wao.
Pia barua hiyo ilikuwa ikitaka kujua tunaomba taarifa hizo kwa kifungu kipi cha sheria na kwamba Majibu hayo hayakuwa chanya kwa kile walichokiomba.
Aliongeza kuwa, waliandika tena barua Aprili Mosi, 2016 kuwakumbusha Jamii Forums kutoa taarifa walizoziomba sababu kwa mujibu wa kifungu cha 10 (2) Cha Sheria ya Mashauri ya Jinai (CPA) kinawapa mamlaka ya kuomba nyaraka kutoka katika ofisi yoyote na lakini hawakujibu.

Amedai kuwa kutokana na hayo waliona wanakosa haki ya kuendelea na upelelezi, na kuwa wanawadhoofisha katika upelelezi wo ndipo wakaona wawakamate.
Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa kesho. Maxence Melo na Mike William  wanadaiwa kuwa kati ya Aprili Mosi na Desemba 13, mwaka jana, huko Mikocheni wakiwa wakurugenzi wa Mtandao wa Jamii Media Co Ltd ambao unaendesha tovuti ya jamii forums wakijua jeshi la Polisi Tanzania linafanya uchunguzi kuhusiana na mawasiliano ya kimtandao yaliyochapishwa katika tovuti yake kwa njia ya kuuzuia uchunguzi huo walishindwa kutekeleza amri ya kutoa taarifa alizonazo.
Maxence Melo na Mike William wakiwa mahakamani.
BOFYA HAPA

YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA KUMI NA TANO MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO MAY 2, 2017.

$
0
0
  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai  akiongoza kikao cha kumi na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 2, 2017.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamadi Masauni akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  katika kikao cha kumi na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 2, 2017.
 Mbunge wa Viti Maalum(CHADEMA) Mhe.Upendo Peneza akiuliza swali katika kikao cha kumi na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 2, 2017.
Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Haki,Maadili na madaraka ya Bunge  Mhe.Almas Maige akisoma hoja za kamati hiyo kuhusu Shauri la kudharau Mamlaka ya Spika linalowahusu Mhe.Freeman Mbowe,Mhe Halima Mdee  na Mhe.Ester Bulaya na Shauri la kuingilia Uhuru  na Haki za Bunge linalowahusu Bw.Paul Makonda na Pastory Mnyeti katika kikao cha kumi na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 2, 2017.
Picha Zote na Daudi Manongi- Dodoma MAELEZO,DODOMA.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

DKT NCHIMBI: MWAJIRI NA MWAJIRIWA SI MTU NA ADUI YAKE

$
0
0
Waajiri wote Mkoani Singida hususani wakurugenzi wa halmashauri ambao ndio wenye watumishi wengi wameelekezwa kujenga mahusiano mazuri baina yao ili kuboresha utumishi wao.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ametoa maelekezo hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi mkoani hapa yaliyofanyika katika uwanja wa Peolpe’s mjini Singida.

Dkt. Nchimbi amesema mwajiri na mtumishi sio maadui bali wanapaswa kujenga mahusiani mazuri hasa kwa mwajiri kujenga mazoea ya kufahamu sifa za watumishi wake, shida na matatizo yao.

Ameongeza kuwa waajiri wamekuwa wakisubiria watumishi wakosee ndio wawape adhabu lakini haipaswi kuwa hivyo kwani mwajiri anatakiwa ahakikishe anaweka mazingira mazuri na kumuelimisha mtumishi asifanye makosa.

“Ukiona mtumishi anafanya mambo yanayokinzana na sheria, kanuni na utaratibu, usimkaripie wala kumtega, mtafutie afisa ustawi wa jamii. Kwa vyo vyote afisa ustawi wa jamii atamrejesha kwenye mstari stahiki na mambo yatakwenda vizuri”.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akimkabidhi afisa wa usalama kutoka shirika la TANESCO Mkoa wa Singida Juma Mauba zawadi ya cheti na  TV flat screen baada ya kuchaguliwa kuwa mfanyakazi bora mwaka 2017.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiwa ameshikama na Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi TUCTA Mkoa wa Singida Aaran Jumbe (kulia kwake) na Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo (kushoto kwake) wakiimba wimbo maalumu wa wafanyakazi wa Mshikamano daima pamoja na wimbo wa taifa.
 Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi wakati akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi kwa Mkoa wa Singida.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

FAINALI YA KOMBE LA FA SASA NI JAMHURI STADIUM DODOMA MEI 28, 2017

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


Hatimaye Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) limeweka wazi kuwa uwanja Jamhuri mjini Ddodma ndio utakaotumika kwa ajili ya fainali ya mchezo wa Fainali za kuwania Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup HD - ASFC) mwaka huu.

Hayo yamesemwa leo na Rais wa TFF Jamal Malinzi wakati akifungua kozi ya uamuzi na ukocha inayoendeshwa na Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Ubungo (UFA) na kuweka wazi kuwa fainali ya Kombe la FA itafanyika katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma.
Fainali hiyo  kati ya Simba SC ya Dar es Salaam na Mbao FC ya Mwanza, itafanyika Mei 28, mwaka huu huku kila timu ikiwa ni wageni kwenye uwanja huo ambapo makao makuu ya nchi.
Kwa mujibu wa Kanuni ya 5 ya michuano ya ASFC kuhusu Uwanja wa mashindano inasema: “Uwanja wa mashindano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports HD utakuwa ni uwanja wenye hadhi inayokubalika na TFF.”

Hilo limekuja baada ya jana Rais wa TFF kunukuliwa katika mtandao wake wa kijamii wa Twitter akisema kuwa, kutachezwa kwa droo ya kutafuta wapi fainali ya Shirikisho itachezwa  huku wadau mbalimbali wakionekana kupinga suala hilo na kusema haiwezekani na haijawahi kutokea.

Simba walifanikiwa kutinga hatua ya fainali baada ya kutoka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Azam mchezo ukiofanyika April 29 katika dimba la uwanja wa Taifa, na Mbao kuivua ubingwa  Yanga kwa kuifunga goli 1-0 mechi iliyopigwa April 30 dimba la CCM Kirumba Mwanza.

BALOZI SEIF AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA MCT

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inasubiri kuyapokea kwa ajili ya kuyafanyia kazi mapendekezo yatakayowasilishwa ya Rasimu ya Sera ya Habari Zanzibar katika kuona Sekta ya Habari Nchini inakuwa imara. 

Alisema Taasisi zinazohusika na jukumu la kusimamia masuala hayo ni vyema zikahakikisha kwamba zinaharakisha mapendekezo hayo ili ile dhana ya Uhuru wa kupata Habari bila ya kuogopa inapatikana. 

Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati wa mazungumzo yake na Uongozi wa Baraza la Habari Tanzania { MCT } ulioongozwa na Katibu Mtendaji wake Bwana Kajubi Mukajanga aliokutana nao hapo Afisini kwake Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar. 

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeahidi kutoa kila aina ya msaada katika kuona Sekta hiyo muhimu kwa jamii inawajibika ipasavyo katika kuwapasha Habari Wananchi. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Uongozi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) uliofika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kubadilishana nao mawazo. Kulia ya Balozi Seif ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Bwana Kajubi Mukajanga na Kushoto ya Balozi ni Mkuu wa Ofisi ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) upande wa Zanzibar Bibi Shifaa Hassan .
Mkuu wa Ofisi ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) upande wa Zanzibar Bibi Shifaa Hassan akifafanua jambo mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif walipokutana nae kwa mazungumzo.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Bwana Kajubi Mukajanga Kulia ya Balozi Seif akielezea mikakati ya Baraza la Habari Tanzania inavyofanya kazi Zanzibar katika kuhakikisha Maadili ya Habari yanazingatiwa na Wana Habari wote Nchini.


WAZIRI LUKUVI AZINDUA MPANGO KABAMBE MTWARA

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi amefanya uzinduzi wa Mpango Kabambe (Master Plan) ya 2015-2035 Mkoani Mtwara . Katika shughuli hiyo Mh. Lukuvi aliwataka watendaji wa Mtwara katika sekta ya ardhi kwa kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa mkoa Bi. Halima Dendego kuhakikisha kuwa wanafuata Master Plan hiyo ili kuweza kuipanga Mtwara na kanda ya kusini yote vizuri hatimaye kufikia Tanzania yenye uchumi wa kati na Viwanda.

Katika ziara hiyo, mbali na kuzindua mpango kabambe pia alifanya ukaguzi katika mifumo ya ukusanyaji wa kodi ofisi za ardhi za halmashauri ya manispaa ya Mtwara ili kuhakikisha makusanyo ya kodi ya ardhi yanafanyika kwa malengo mahususi.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi. Halima Dendego akiongea na wananchi mbele ya Waziri Lukuvi, alimhakikishia Mheshimiwa Waziri kuwa atasimamia utekelezaji wa mpango kabambe kikamilifu kwa maendeleo ya watu wa Mtwara  na watanzania kwa ujumla.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akizindua mpango kabambe mkoani Mtwara na Mkukabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi. Halima Dendego.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akikagua masijala ya ardhi halmashauri ya Manispaa ya Mtwara na kuwataka Maafisa Ardhi kuweka kumbukumbu za Hati Miliki za Ardhi katika mpangilio mzuri ili kuepusha migogoro ya ardhi..
 Wananchi wa Mkoa wa Mtwara wakifuatilia Uzinduzi wa Mpango Kabambe (Master Plan) ya Mtwara.ra.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

NMB yapata taarifa bora za hesabu

$
0
0

 Mkurugenzi wa Benki ya NMB - Ineke Bussemaker

 • Yapata faida ya shilingi bilioni 40.9 kwa miezi Mitatu 
 • Ni ongezeko la asilimia 4 

BENKI ya NMB imepatafaida ya shilingi Bilioni 40.9 kwa miezi mitatu ya mwanzo wa mwaka ikiwa ni ongezeko la 4% ya faida ukilinganisha na kipindi kama hicho Mwaka jana – 2016 ambapo NMB ilipata faida ya shilingi Bilioni 39.3. Mkurugenzi wa Benki ya NMB - Ineke Bussemaker alisema mwanzo huu wa Mwaka mzuri katika faida ya benki umetokana na kuimarika kwa pato linalotokana na biashara ya benki na ahueni iliyopatikana katika mikopo mibovu au isiyolipika. 

Bi Bussemaker alisema pato linalotokana na biashara ya benki lilikua kwa asilimia 4.6 hadi kufikia kiasi cha shilingi bilioni 58.7 ikilinganishwa na kiasi cha bilioni 56.1 zilizopatikana katika kipindi kama hicho mwaka jana. 

Alisema ongezeko hili limechangiwa kwa kiasi kikubwa na pato linalotokana na riba katika mikopo na biashara ya fedha za kigeni ambalo limeongezeka kwa asilimia 41 hadi kufikia kiasi cha shilingi bilioni 4.9 katika robo ya kwanza ya mwaka huu ikilinganishwa na shilingi bilioni 3.5 zilizopatikana katika kipindi kama hicho mwaka jana.

 “Robo ya kwanza ya mwaka 2017, pato linalotokana na riba katika mikopo ilikuwa shilingi za kitanzania bilioni 115.9, ikiwa ni ongezeko la asilimia 9.4 ikilinganishwa na kiasi cha shilingi bilioni106.0 katika kipindi kama hicho mwaka jana na pia ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 0.9 hadi shilingi bilioni 114.9 katika robo ya mwisho ya mwaka 2016,” alisema Bi Bussemaker. 

Pia taarifa hii ya hesabu za benki inaonyesha kuwa pato lisilotokana na riba katika mikopo limeongezeka kwa asilimia 5.3 hadi kufikia kiasi cha shilingi bilioni 41.5 katika robo ya kwanza ya mwaka huu ikilinganishwa na kiasi cha shilingi bilioni 39.4 katika kipindi kama hicho mwaka jana na pia ikilinganishwa na ongezeko la asilimia nne kutoka shilingi bilioni 39.9 katika robo ya nne ya mwaka 2016. 

Amana za wateja nazo ziliongezeka kwa asilimia 0.9 hadi kufikia shilingi trilioni 3.75 katika robo ya kwanza ya mwaka huu ikilinganishwa na shilingi trilioni 3.71 katika robo ya mwisho ya mwaka jana. “Ili kuongeza idadi ya wateja na amana, benki imeweza kutumia zaidi NMB wakala, walioponchi nzima. Lengo la benki ni kuwa na mawakala wapatao 4,500 mpaka kufikia mwisho wa mwaka huu," alisema Bi Bussemaker 

Bi Bussemaker pia alisema katika kupambana na changamoto ya ukata katika soko, benki imeweza kuongeza umakini katika kutoa mikopo kwa Wateja. Mikopo iliyotolewa kwa Wateja katika robo ya kwanza yam waka ilipungua kwa 1.2% mpaka kufikia shilingi trilioni 2.76 kutoka shilingi trilioni 2.79 zilizonukuliwa katika robo iliyopita. Uwiano wa mikopo na amana za NMB umeendelea kuwa mzuri kwa Kiwango cha 74.6%, ukusanyaji wa mikopo inadhihirishwa na Kiwango cha mikopo mibaya au isiyolipika ambacho kimepungua mpaka kufikia 4.6% kutoka 4.8% iliyopatikana mwaka jana. 

“Menejimenti imedhamiria kuendelea kutoa hesabu nzuri na mwisho wa siku kuleta matunda kwa wana hisa wa benki ya NMB kwa mwaka 2017,” alisema Bi Bussemaker. Kuhusu NMB: NMB ni benki inayoongoza nchini Tanzania kwa matawi, ikiwa na zaidi ya matawi 189, wateja zaidi ya milioni 2 na laki tano na zaidi ya mashine 700 za kutolea fedha (ATM) nchi nzima. 

NMB imeasisi ubunifu mkubwa katika soko la Tanzania ikiwa ni pamoja na huduma za benki kwa njia ya simu yaani NMB mobile , Pesa Fasta na malipo kwa kutumia mashine za ATM. NMB inaendelea kujikita katika kutoa huduma kwa makampuni makubwa, masoko ya kifedha pamoja na huduma za kusaidia makusanyo ya kifedha na biashara. Lakini Pia imekuwa mstari wa mbele katika maendeleo ya kilimo na imeanzisha mfumo wa stakabadhi ghalani kupitia vyama vya ushirika nchini.

MAMBO YA GADO

RAIS DKT MAGUFULI AREJEA DAR ES SALAAM LEO BAADA YA KUHITIMISHA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU TATU MKOANI KILIMANJARO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiswasili Uwanja wa ndege wa  Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 2, 2017 akitokea mkoani Kilimanjaro alikokuwa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Mhe. Paul Makonda baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 2, 2017 ,akitokea mkoani Kilimanjaro alikokuwa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Mhe. Paul Makonda baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 2, 2017 ,akitokea mkoani Kilimanjaro alikokuwa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dar es salaam  baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 2, 2017 ,akitokea mkoani Kilimanjaro alikokuwa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dar es salaam  na kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya mkoa huo Kamishna Simon Sirro baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Aprili 2, 2017 akitokea mkoani Kilimanjaro alikokuwa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.


PICHA NA IKULU

Vicoba Moshi wanufaika na mafunzo ya ujasiriamali

$
0
0

Wajasiriamali wa Kilimanjaro Vicoba Network (KIVINET) wamepata elimu ya ujasiriamali baada ya kupata mafunzo yaliyoandaliwa na FINCA Microfinance Bank mjini Moshi mwishoni mwa wiki.

“Lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha wajasiriamali wa KIVINET kuwa na uelewa wa kutosha wa kukuza miradi na mitaji yao hivyo kushiriki kikamilifu katika kukuza uchumi”, alisema Mkurugenzi wa biashara wa FINCA Microfinance Bank Bw. Gershom Mpangala.

KIVINET inajumuisha zaidi ya wanachama 10,000 kutoka vikundi mbalimbali mjini Moshi ambavyo vimesaidia kuwawezesha kushiriki katika fursa za kiuchumi na kuwawezesha kuboresha biashara zao na kuinua kiwango cha maisha yao. “Mafunzo haya yametuwezesha kubadilishana mawazo na kupeana uzoefu. Naamini sasa watafanya biashara zao mafanikio zaidi”, alisema Mpangala.

Katika mafunzo hayo, maofisa wa Finca waliweza kutoa ufafanuzi wa huduma ambazo wanaweza kupata na masuala ya kutilia manani katika kukuza biashara zao. “Tumejaribu kuwaonyesha mikopo yetu ya elimu ambayo imeandaliwa maalum kwa ajili ya kumsaidia mjasiriamali na namna ya kuepuka kuvuranga mtaji wake pale ambapo anatakiwa alipe karo ya mtoto wake,’ alisema Mpangala.

Naye Meneja wa Benki ya FINCA Mkoani Kilimanjaro Sebastiani Timothy amesema wao wanahusika na utoaji wa elimu ya ujasiriamali pamoja na mikopo yenye riba nafuu kwa wajasiriamali wadogowadogo na wale wa kati lengo likiwa ni kuhakikisha wanaweza kujikwamua kiuchumi. Vikundi vya Vicoba kwa hapa Moshi tunawahudumia sana kwa sababu mbali na kuwapa mikopo yenye riba nafuu lakini pia tunatoa elimu jinsi ya kutunza fedha na pia jinsi ya kufanya biashara kwa mafanikio, aliongeza Timothy.

Kwa upande wake, Matia Mathiasi Mwingira ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa Kilimanjaro Vicoba Network (Vicoba) amesema ni vigumu kwa wafanyabiashara kufanikiwa bila kupata mikopo yenye riba nafuu hivyo ni vyema taasisi za kifedha zikatoa mikopo yenye riba nafuu ili wajasiriamali waweze kumudu na kuboresha maisha yao. ‘Nawapongeza sana Benki ya Finca kwani licha ya kusikia kilio chetu sisi Vicoba na kuamua kutupatia mikopo nafuu lakini pia wanatupa mafunzo bure ya jinsi ya kutumia vyema mikopo yetu, alisema Mwingira.

Mwingira pia ametoa wito kwa akinamama ambao hawapo kwenye vikundi vidogo vidogo yaani VICOBA kujiunga ili wapate fursa za mikopo ikiwepo mikopo kwa ajili ya ada za shule.

Wanachama wa Kilimanjaro VICOBA Network (KIVINET) wakiwa kwenye mafunzo ya jinsi ya kutumia mikopo wanayopata kutoka FINCA Microfinance Bank. Mafunzo hayo yaliandaliwa na benki hiyo na kufanyika mjini Moshi mwishoni mwa wiki.

SHIRIKA LA ANGA ETIHAD LAMTEUA GAVIN HALLIDAY KUWA MKURUGENZI MTENDAJI WA HALA GROUP

$
0
0
Shirika la Anga la Etihad (EAG) limetangaza uteuzi wa Gavin Halliday kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hala Group ikiwa ni sehemu ya kuboresha utendaji wake na kuimarisha huduma zake ulimwenguni.

Halliday ataliongoza shirika hilo katika kuendana na huduma bora ulimwenguni ikiwa ni pamoja na kuwasogeza karibu wateja na kuendelea kufurahia huduma bora zinazotolewa na shirika hili pamoja na washirika wake wa ndege. Pia, atawajibika kuwa karibu na wabia wa EAG pamoja na kushiriki vikao vya utawala ambavyo ni ndiyo nguzo muhimu kwa mipango na maendeleo ukuaji wa biashara ya usafirishaji Abu Dhab na Nchi za Falme za Kiarabu.

Halliday anaungana na Shirika la Anga la Etihad baada ya kufanya kazi na kuwa na uzoefu mkubwa akifanya kazi kwa miaka 30 katika Shirika la Ndege la Etihad na kwenye Shirika la IAG. Kwa miaka mitatu ya hivi karibuni amekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Avios, ambayo ni programu maarufu ulimwenguni. Pia amewahi kuwa katika nafasi ya juu akihusika na masuala ya biashara kwenye Shirika la IAG, Iberia, British Midland na British Airways.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Anga la Etihad, H.E Mohomed Mubarak Fadhel Al Mazrouei alisema, “Hala ni nembo muhimu kwa Etihad ambayo imekuwa ikihakikisha inawaunganisha wabia wetu kwenye biashara ya usafiri wa anga. Pia ni idara muhimu ambayo imekuwa kiungo muhimu kwa wasafiri wa Abu Dhab na Nchi za Famlme za Kiarabu kwenye biashara na usafirishaji wa uhakika. Gavinni ni miongoni mwa watu muhimu kwenye sekta hii ya usafiri wa anga, hivyo tunafurahia kujiunga na timu ya uongozi wa EAG.

“Tumefurahishwa na uzoefu wa Gavin na tunaamini ataendeleza programu za masoko ulimwenguni jambo ambalo ndiyo mpango wetu mkubwa.”
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hala Group Gavin Halliday .

 
Viewing all 110129 articles
Browse latest View live




Latest Images