Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

NSSF YASAIDIA UJENZI WA ZAHANATA KATIKA KIJIJI CHA MATAMA MKOANI RUVUMA

$
0
0

SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limetoa msaada wa vifaa vya ujenzi wa kituo cha Afya katika Kata ya Muhukuru, Kijiji cha Matama, Mkoani Ruvuma.

Vifaa hivyo, ni mifuko 800 ya saruji na nondo 400 zitakazosaidia kufanikiwa ujenzi wa kama njia yakuleta maendeleo katika jamii.Katika kufanikisha ujenzi huo, NSSF imetoa mifuko 800 ya saruji pamoja na nondo zipatazo 400.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo Meneja wa NSSF Mkoa wa Ruvuma, Mariam Muhaji, alisema NSSF ni shirika kubwa la hifadhi ya jamii lenye ofisi katika kila mkoa wa Tanzania na wilaya zake.

Mpango wa ujenzi wa zahanati hiyo umetokana na ombi la Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwa NSSF kuona jinsi ya kusaidia jamii inayoshi katika Kata ya Muhukuru ambao walikuwa wanatumia kilometa 62 kufika katika zahanati ya Muhukuru.

Msaada huo wa NSSF, unalenga kufanikisha mpango huo wa kuwapa wananchi unafuu wa kupata huduma za afya, hivyo kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo ya kukabidhi vifaa vya ujenzi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Songea Mjini, Oraleti Komando aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.

Naye Diwani wa Kata ya Muhukuru, Manfred Mzuyu alisema msaada huo umekuja kwa wakati muafaka kwani baada ya kukamilika, utapunguza kero wanayopata wakazi wa kijiji cha Matama.

Aidha, diwani huyo aliongeza kuwa ujenzi huo utasimamiwa kwa ukaribu kuhakikisha hakuna atakayehujumu ujenzi wa kituo hicho na kutoa wito kwa wengine kuiga mfano huo wa NSSF.
Mkuu wa Wilaya ya Songea, Oraleti Komando, akipokea sehemu ya msaada wa mifuko 800 ya saruji na nondo 400 kutoka kwa Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Ruvuma, Mariam Muhaji. Hafla hiyo ilifanyika mkoani Ruvuma mwishoni mwa wiki.

Mkuu wa Wilaya ya Songea Mjini, Oraleti Komando, akimkabidhi sehemu ya msaada uliotolewa na NSSF kwa Diwani wa Kata ya Muhukuru, Manfred Mzuyu. Kulia ni Meneja wa NSSF Mkoa wa Ruvuma, Mariam Muhaji.

Meneja wa NSSF Mkoa wa Ruvuma, Mariam Muhaji (wa tatu kulia), Ofisa Mwandamizi wa Masoko na Uhusiano, Amina Mmbaga (wa pili kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na maofisa wengini wa NSSF baada ya kukabidhi mifuko 800 ya saruji pamoja na nondo 400 kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati katika Kijiji cha Matama, Songea.
Wakzi wa Kijiji cha Matama Kata ya Mahukuru wakiwa katika hafla hiyo.
Sehemu ya msaada wa mifuko ya saruji iliyotolewa na NSSF kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Matama, Songea mkoani Ruvuma.

MBEYA CITY YAPATA MDHAMINI WA VIFAA VYA MICHEZO

$
0
0
Timu ya soka ya Mbeya City imepata mfadhili mpya wa timu hiyo ambaye atakuwa anasimamia maswala yote ya vifaa vya michezo ikiwemo jezi zote za timu hiyo zitakazotumiwa na wachezaji na zile za mashabiki kuanzia mwezi wa saba mwaka huu. Viongozi hao wamesaini mkataba wa udhamini huo uliofanyika katika ukumbi mdogo wa hoteli ya Mbeya Hill View kwa kuwaalika wadau wa mbeya city na vyombo vyote vya habari.
Mwenyekiti wa Timu ya Mbeya City, Mussa Mapunda (kushoto) akipokea mkataba kutoka kwa Kiongozi wa Sports Master ambao ni wadhamini wapya watakaosimamia maswala yote ya vifaa vya michezo vya Timu hiyo, Fadhili Nsemwa, baada ya kusainiana makubaliano.
Mwenyekiti wa Timu ya Mbeya City, Mussa Mapunda akisaini mkataba wa makubalino na uongozi wa Kampuni ya Sports Master chini yake Fadhili Nsemwa (kulia).
Mfano wa Vifaa vya michezo vitakavyotumiwa na Timu ya Mbeya City kuanzia msimu ujao.
Picha ya pamoja.

WAZIRI MAGHEMBE AZIPA HADHI HOTEL ZA DAR ES SALAAM

$
0
0
 Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akizungumza kabla ya kukabidhi vyeti vya kutambua hadhi za Hotel zilizopo jijini Dar es Salaam na kwa kuzipa madaraja mpaka nyota tano  katika soko la utali hapa nchin, katika hafla fupi iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe  akikabidhi cheti kwa Mkurugenzi wa  Masoko na Mauzo wa Serena Hoteli, Seraphin Lusala baada ya Hoteli hiyo kutambuliwa kuwa na hadhi ya Nyota tano katika mkoa wa Dar es Salaam, katika hafla fupi iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
 Majaji ambao waliokuwa wakitoa maksi ya hadhi za hoteli hapa nchini wakisimama kujitambulisha kwa wageni waliofika.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Generali Gaudence Milanzi akizungumza na Wamiliki wa Mhoteli jijini Dar es Salaam leo kabla ya kukabidhi vyeti vya madaraja ya hotel zao.
Afisa utalii kutoka bodi ya Utalii Tanzania (TTB),Irene Mville akitoa maelekezo kwa wadau wa mahoteli ambao walifika katika hafla ya ugawaji wa madarajana viwango katika Hoteli zilizopo jijini Dar es Salaam .
  Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akiwa katika picha ya pamoja na wamiliki wa Hotel jijini Dar es Salaam.

Wafanyabiashara Dar wanufaika na mafunzo ya kijasiliamali

$
0
0
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es salaam na Pwani, Vick Bishubo (kulia) akizungumza kwenye mkutano wa wafanyabiashara wa Dar es Salaam "NMB Business Club' waliokutanishwa na benki hiyo jana jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutoa mafunzo ya biashara pamoja na kodi ili kukuza biashara zao. Afisa Mkuu wa NMB Kitengo cha Wateja wadogo na wakati, Abdulmajid Nsekela (kulia) akizungumza kwenye mkutano wa wafanyabiashara wa '"NMB Business Club' waliokutanishwa na NMB jana jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutoa mafunzo ya biashara pamoja na kodi ili kukuza biashara zao. Baadhi ya wafanyabiashara walioshiriki mkutano huo wakizungumza kuelezea mafanikio yao juu ya huduma za mikopo na ukuaji wa biashara zao.

BENKI ya NMB imekutanisha wafanyabiashara zaidi ya 500 wa jijini Dar es Salaam waliopo katika jumuia ya wafanyabiashara wa NMB "NMB Business Club" kwa lengo la kutoa mafunzo mbalimbali ya biashara pamoja na mafunzo ya kodi ili kukuza biashara zao. 

Kundi hilo la NMB Business Club mkoa wa Dar es Salaam limekutanishwa kwa pamoja ili wafanyabiashara hao waweze kujuana na kubadilishana uzoefu katika shughuli zao jambo ambalo litachangia wao kushikamana na kunufaika zaidi na huduma zinazotolewa na benki hiyo. 

Akizungumza na wafanyabiashara katika mkutano huo, Afisa Mkuu wa NMB Kitengo cha Wateja wadogo na wakati, Abdulmajid Nsekela alisema katika semina hiyo wataalam wa biashara wa Benki ya NMB watatoa mafunzo mbalimbali ya namna ya kukuza biashara na kuelezea fursa anuai zilizopo ndani ya benki hiyo ili wateja wao waendelee kunufaika nazo. Alisema mbali ya kutoa mafunzo ya biashara na kodi wana NMB Business Club walioshiriki katika mkutano huo watapata fursa ya kutoa mrejesho dhidi ya huduma wanazopewa ili benki iangalie namna ya kuzishughulikia. Sehemu ya wafanyabiashara walioshiriki mkutano huo.

Kijana aliyetoka Dar hadi Arusha kwa baiskeli azindua rasmi kitabu chake

$
0
0
Mheshimiwa Nabii Mkuu Dr GeorDavie Royal Mkuu ,   jana amezindua rasmi kitabu cha " KUKIWA NA FOLENI" kilichoandikwa na Wiseman Luvanda.
Pia Nabii Dr.GeorDavie alimpongeza kwa kitendo chake  alichoamua kufanya kwa kuwa balozi wa barabarani  kwa kutoka Jijini Dar es salaam hadi mkaoni Arusha wa usafiri wa baiskeli.

Akizungumza na wadau waliohudhuria hafla hiyo mtunzi wa kitabu hicho alisema vijana wanapaswa kutumia vipaji vyao kwa kujituma, kuthubutu na kufanya kazi kwa nguvu  na si kulalamika kila siku,  jambo linalopelekea kuibuka kwa makundi mbalimbali kama vile Panya Road na mengineyo.

Aidha mwandishi huyo amewataka wadau mbalimbali kumuunga mkono katika kukinunua kitabu hicho cha " KUKIWA NA FOLENI" , ambacho pia amekiandika kwa lugha ya Kiswahili  ili kuweza kukisambaza nchi nzima.
Tazama baadhi ya picha za tukio hili hapo chini
Pichani ni Mwandishi wa kitabu hicho Wiseman Luvanda, Akizungumza na baadhi ya wadau waliohudhuria kongamano hilo jana Jijini Arusha. Picha na msumbanews blog
Nabii Mkuu Dr GeorDavie Royal Mkuu akipokea kitabu kutoka kwa Mwandishi Wiseman Luvanda.Picha na msumbanews blog
Baadhi ya wadau mbali waliojitokeza kwenye kongamano  la kuinuliwa viwango na uzinduzi wa kitabu hicho.Picha na msumbanews blog
Mwandishi Wiseman Luvanda akifuatilia kwa makini kongamano la kuinuliwa viwango ambalo lilifuatana na uzinduzi wa kitabu chake.Picha na msumbanews blog

VODACOM YATOE ELIMU YA HISA SAUT MWANZA

$
0
0
Meneja wa wateja wakubwa kutoka wakala wa hisa(Orbit Securities) Godfrey Gabriel,akiwasilisha mada ya umuhimu wa kununua hisa kwa wanafunzi wa chuo cha Mtakatifu Augustine Mwanza leo, wakati wa semina iliyofanyika chuoni hapo leo. 
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano Vodacom Tanzania Jacqueline Materu,akizungumza na wanafunzi wa chuo cha Mtakatifu Augustine Mwanza leo, wakati wa semina ya elimu ya ununuzi wa hisa. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Oparesheni wa Kampuni ya uwakala wa hisa ya Oarbit Security Juventus Simon, akijibu maswali ya wanafunzi wa chuo cha Mtakatifu Augustine Mwanza leo, wakati wa semina ya umuhimu wa ununuaji wa hisa iliyofanyika chuoni hapo leo. 
Rais wa Serikali ya wanafunzi wa chuo cha Mtakatifu Augustine Makamba Bahati,akizungumza jijini Mwanza leo,wakati wa semina ya umuhimu wa ununuaji wa hisa iliyofanyika chuoni hapo. 
Wanafunzi wa chuo cha Mtakatifu Augustine, wakijisomea vipeperushi vinavyoonyesha jinsi ya kununua hisa za Vodacom Tanzania, wakati wa semina ya umuhimu wa ununuaji wa hisa iliyofanyika chuoni hapo jijini Mwanza leo.

WATCH THIS SPACE!

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AWASILI MKOANI KILIMANJARO

$
0
0
 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Kilimanjaro na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Said Meck Sadik pamoja na viongozi wengine wa Serikali pamoja na Chama Cha Mapinduzi katika uwanja wa ndege wa KIA. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).Makamu wa Rais atahudhuria sherehe za wafanya kazi Mei Mosi zitakazofanyika kitaifa mkoani Kilimanjaro.



Dkt. Harrison Mwakyembe awataka Vijana kutenga muda wao kujisomea Vitabu.

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka vijana kutumia muda wao kujenga utamaduni wa kujisomea vitabu badala ya kupoteza muda wao mwingi katika mitandao ya kijamii kwakuwa kusoma vitabu ndiyo msingi mzuri wa elimu.

Kauli hiyo ameitoa leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akizindua Kitabu cha “Colour of Life” kilichoandikwa na Mwandishi Bi. Ritha Tarimo ambapo katika hotuba yake aliyoitoa mbele ya wageni waalikwa amesisitiza suala la vijana kujenga utamaduni wa kupenda kusoma vitabu ili kukuza elimu yao.

Mhe. Mwakyembe ameeleza kuwa, baadhi ya vijana siku hizi wamekuwa wakitumia muda wao mwingi katika mitandao ya kijamii badala ya kujisomea, hivyo amewashauri wajifunze kutoka kwa Mwandishi wa Kitabu hicho ili waje kuwa waandishi hodari wa kutegemewa na Taifa.

Sambamba na rai hiyo, Waziri Mwakyembe amempongeza Bi. Ritha Tarimo kwa juhudi zake kubwa na maarifa katika kutunga na kuandika kitabu hicho ambacho amesema kuwa kitabu hicho ni kizuri na kina maudhui mazuri kwa vijana hususani wanafunzi, hivyo ameitaka jamii kumuunga mkono kwa kukisoma ili jamii ipate kuelimika.

“Ukimkuta mtu kama Ritha Tarimo anaandika kitabu katika kipindi hiki ambapo vitabu vinaonekana kuondolewa kwasababu ya maendeleo ya teknolojia, ni vema kumpa moyo na kumuunga mkono kwakuwa yeye ametuonyesha Watanzania kuwa hata sisi tunaweza, na kitabu hiki niwaambie ukweli kina maudhui ya kumtia moyo kijana ya kutokata tamaa katika maisha”, alisema Dkt. Mwakyembe.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mkwakyembe akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu cha "Colour of Life" kilichoandikwa na Mwandishi wa vitabu Bi. Ritha Tarimo. 30 Aprili, 2017 Jijini Dar es Salaam. 



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mkwakyembe akiongea na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa kitabu cha "Colour of Life" kilichoandikwa na Mwandishi wa vitabu Bi. Ritha Tarimo 30 Aprili, 2017 Jijini Dar es Salaam.

Mwandishi wa vitabu Bi. Ritha Tarimo akiongea na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa kitabu chake cha "Colour of Life"leo 30 Aprili, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mkwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na familia ya Mwandishi wa vitabu Bi. Ritha Tarimo pamja na wageni waalikwa mara baada ya uzinduzi wa kitabu hicho 30 Aprili, 2017 Jijini Dar es Salaam. (PICHA/HABARI NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM).

Ujio mpya wa Rico Single na video ya wimbo ‘Halindwa’.

$
0
0


Msanii wa muziki wa Bongo Fleva anayefanyia shughuli zake za muziki visiwani Zanzibar, Rico Single, amefungua mwaka 2017 kwa kuachia video ya wimbo wake mpya uitwao ‘Halindwa’.

Muimbaji huyo ambaye alifunga mwaka 2016 na video ya wimbo ‘Yaani Raha’, amesema mwaka 2017 ni mwaka ambao atafanya mapinduzi makubwa katika muziki wake.

“Kwanza nimeanza na video ya wimbo wangu mpya ‘Halindwa’ ni kazi ambayo kila Mtanzania anatakiwa kuiangalia. Audio ya wimbo imeandaliwa na producer Aloneym kutoka Island Record Zanzibar na video ameandaa na director Ivan na amefanya mambo makubwa sana,” alisema Rico.

Aliongeza, “Kwa mwaka huu bado kuna mambo makubwa yanakuja, hapo ni kama nimefungukua kurasa moja kuna mambo mengine mengi yanakuja, video kali, audio kali mpaka kieleweke,”

Muimbaji huyo ambaye ni mmoja kati ya wasanii wa muziki kutoka Zanzibar ambao wanafanya vizuri, amewataka Watanzania kuipokea kazi yake hiyo mpya.

Katika hatua nyingine, Rico ameweka wazi kwamba, kuimba wimbo wa harakati kama alivyofanya Emmanuel Elibarik (Nay wa Mitego) ni vigumu kwa Zanzibar, kwa madai kwamba mitazamo ni tofauti.

Rico Single alisema siasa visiwani humo ina nafasi kubwa mno na kama msanii atajaribu kuimba wimbo kama huo, huenda akakutana na matatizo makubwa kutoka kwa mtu mmoja mmoja hata kama si mlengwa aliyeimbiwa wimbo huo.

“Huku bana watu wanapenda siasa kuliko fedha, ukiimba harakati kama za wimbo wa Ney utajikuta katika matatizo, maana mtu tu mwenye mapenzi na unayemuimba anaweza kukudhuru kabla hata mlengwa mwenyewe hajakufikia, ndiyo maana harakati huku zimepungua kwa wasanii,’’ alieleza Rico Single.

Rico Single aliongeza kwamba, baadhi ya wasanii wa bongo fleva walishawahi kuimba nyimbo zenye ujumbe wa harakati kwa kuikumbusha serikali mambo maovu yanayofanywa na watu visiwani humo, lakini mapokeo yake yakawa tofauti.

DKT. NCHIMBI AZITAKA KAMATI ZA MAJI KUSIMAMIA KIMAMILIFU MIRADI YA MAJI MANISPAA YA SINGIDA.

$
0
0

Kamati za maji za visima kumi vya maji katika manispaa ya Singida zimekuwa sababu ya miradi hiyo iliyokamilika kwa asilimia miamoja kutofanya kazi na kuwanufausha wananchi huku ikiwa imegharimu fedha nyingi za serikali na wahisani hasa benki ya dunia.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi mwishoni mwa wiki hii mara baada ya kukagua miradi hiyo na kujiridhisha kuwa miradi hiyo imekamilika licha ya kutofanya kazi.

Dkt. Nchimbi amesema sababu kubwa ya kutofanya kazi miradi hiyo ni udhaifu wa kamati za maji na wanasiasa katika maeneo ya miradi kutojali shida ya wananchi ya kukosa maji na hivyo kuitelekeza miradi hiyo badala ya kuisimamia.

Amesema lengo la miradi hiyo ni wananchi wapate maji safi na salama kwa umbali usiozidi kilometa nne kama ilivyoagizwa na serikali.

“Katika ukaguzi wangu nimebaini mifumo katika miradi hii ya maji ipo vizuri sana. Baadhi inaendeshwa kwa umeme na mingine kwa mafuta ya dizel. Makubaliano yalikuwa baada ya kukamilika miradi hii iendeshwe na kamati za maji kwa asilimia mia moja”, amesema.

Dkt. Nchimbi amesema wajibu wa kamati hizo ni pamoja na kukusanya fedha zinazotokana na kuuza maji kwa wateja pamoja na matengenezo ya miundombinu ya visima hivyo ili miradi hiyo iwe endelevu.

“Fedha zinazopatikana ndizo zitakazoendesha mradi husika ikiwemo kugharamia matengenezo ya mashine, pampu, miundombinu, kununulia dizel, umeme na kumlipa mhudumu wa mradi. Makubaliano ni miradi ikikamilika inabaki mikononi mwa wananchi kupitia kamati zao za maji. Serikali na wafadhili hawatahusika tena”, amesisitiza Dkt. Nchimbi.

RAIS DKT MAGUFULI AHUDHURIA IBADA YA JUMAPILI MAKANISA MAWILI TOFAUTI MJINI MOSHI

$
0
0


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiungana na waumini  katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini katika ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
 Waumini wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli aliposalimia waumini katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini katika ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
 
 Waumini wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na  Askofu Isaac Amani akisalimia waumini katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini katika ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiombewa na Askofu Isaac Aman katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini alikohudhuria ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na watawa katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini baada ya  ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017

 Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo akitoa mahubiri wakati wa ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo  Aprili 30, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na waumini wengine wakimsikiliza Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo akitoa mahubiri wakati wa ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo  Aprili 30, 2017

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akikaribishwa na Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo kuongea na wananchi baada ya  ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo  Aprili 30, 2017

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea na waumini na wananchi baada ya  ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo  Aprili 30, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiombewa sala maalumu na Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo kuongea na wananchi baada ya  ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo  Aprili 30, 2017. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

TPDC yang’oa vikombe lukuki Mei Mosi.

$
0
0

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) lafanikiwa kubeba vikombe vinanena na medali nne katika michuano ya mashindano ya Maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani-Mei Mosi yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Ushirika Mkoani Kilimanjaro. 

Katika mashindano hayo yaliyoanza tarehe 19 hadi 29 Aprili, 2017 yaliyoandaliwa na COTWU(T) yalihusisha mashindano katika michezo ya kuvuta kamba, mbio za marathon, mbio za baiskeli, bao, kalata, draft, mpira wa pete na mpira wa miguu kama sehemu ya maandalizi ya siku ya Mei Mosi. 

Akizungumza na vyombo vya habari Mwenyekiti wa Michezo wa TPDC ndugu Nelson Rwechunguraalieleza kuwa timu yake imezidi kuwa bora zaidi kwakuwa mashindano yaliyopita ilifanikiwa kuchukua jumla ya vikombe vitano na medali tatu lakini katika mashindano ya safari TPDC imefanikiwa kuchukua vikombe vinane na medali nne. 

“Tumeweza kuchukua kikombe cha mshindi wa wa tatu katika mashindano ya kuvuta kamba kwa wananume, kikombe cha mshindi wa pili katika mashindano ya kuvuta kamba kwa wanawake, kikombe cha mshindi wa tatu katika mbio za baiskeli kwa wanawake na kikombe cha mshindi wa pili kwa upande wa wanaume, kikombe cha mshindi wa pili katika mashindano ya marathon kwa wanaume na kikombe cha mshindi wa kwanza kwa upande wa wanaume na kikombe kwa mshindi wa tatu katika mchezo wa draft’’ alieleza mwenyekiti wa TPDC. 

Kwa mujibu wa ndugu Rwechungura wafanyakazi wa TPDC walioipatia timu vikombe ni Diana Byonge na Peter Ngalu kwa upande wa baiskeli, Neema Mdegela na Darush Shija kwa upande wa mbio ndefu na Diana Byonge katikamchezo draft. 

Aidha akizungumzia kushindwa kuchukua ubingwa wa mpira wa miguu, Mwenyekiti alieleza kuwa pamoja na kufungwa na timu Geita Gold Mining, kwake yeye timu yake ndiyo bingwa wa mashindano kutokana na mpira mzuri walioonyesha katika mtanange huo pamoja na kuwa pungufu kwa muda mrefu. 

“Pamoja na kushindwa kuchukua ubingwa wa mpira wa miguu, bado kwangu mimi naichukulia timu yangu kama ndiye bingwa wa mashindano hayo kwakuwa tumecheza kwa kiwango bora zaidi na hata watazamaji wameshuhudia hilo na hivyo tumepata faraja na pia tunawapongeza Geita kwa ushindi walioupata ingawa changamoto zilikuwepo kwa upande wa maamuzi lakini ndio mchezo na tunatumaini zitafanyiwa kazi katika mashindano yajayo’’ alieleza mwenyekiti. 

Kwa upande wake Kapteni wa timu ya mpira wa miguu TPDC ameeleza kuwa hatua waliyofikia ya kuwa washindi wa pili ni ya kumshukuru Mungu kwakuwa timu bora zilikuwa nyingi lakini ‘wao walifanikiwa kufika hatua ya fainali. 

“Kiukweli najivunia kuwa na timu bora zaidi kwenye mashindano haya na hiiimedhihirishwa na ushindi tuliokuwa tukiupata hadi kufikia hatua na tumecheza vizuri saana pamoja ya kuwa pungufu kwa zaidi ya dakika 76 lakini bado tumeweza kuwadhibiti wa pinzania wetu kwa muda mrefu hadi walipoweza kutufunga gori la pili ambapo hadi mwisho wa mchezo tulitoka gori mbili kwa moja’’ alichambua kapteni wa TPDC. 

Aidha alisisitiza kuwa waajiri wanapaswa kuzingatia na kusisitiza michezo kwa wafanyakazi ili kuboresha afya za wafanyakazi, kuleta umoja na kutangaza shughuli za Mashirika kwa wananchi.
 
Timu za michezo za TPDC zikiwa na mafuriko ya vikombe vya ushindi zilizoupata kwenye mashindano mbalimbali ya Mei Mosi. 
Shamrashamra za ushindi mnono na vikombe kwenye michezo minane kati ya kumi ambayo timu za michezo TPDC ilishiriki katika mashiondano ya Mei Mosi. 

SHIRIKA LA NDEGE TANZANIA LAZINDUA RASMI USAFIRI WA ANGA DAR – SONGEA

$
0
0
Wafanyakazi wa shirika la ndege Tanzania (ATCL) wakigawa wine kwa viongozi ambao wamehudhuria uzinduzi wa usafiri wa anga Dar es Salaam – Songea, kupitia shirika hilo katika uwanja wa ndenge wa songea mkoani Ruvuma.Kwa undani wa habari hii tiazama video yake hapo chini.

DKT. HARRISON MWAKYEMBE AZINDUA KITABU 'COLOUR OF LIFE'


BALOZI WA VIJANA WA EAC ATOA SOMO KWA WANAFUNZI WA IJA JUU YA UMUHIMU WA JUMUIYA YA EAC

$
0
0
Naibu Balozi wa vijana wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Suzane William Mollel (kushoto), akizungumza katika Mkutano wa Wanafunzi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA), Lushoto Mkoani Tanga, wakati alipokuwa akiwahamasisha wanafunzi hao kuufahamu umuhimu wa Ushirikiano wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo amewataka kutumia maarifa yao yote kuhakikisha ushirikiano huo unakuwa wa kudumu.
 Naibu Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) anayesimamia Elimu, Utafiti na Ushauri, Fahamu Mtulya akizungumza jambo katika warsha hiyo.
Sehemu ya Wanafunzi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA), Lushoto Mkoani Tanga wakimsikiliza Naibu Balozi wa vijana wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Suzane William Mollel (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao juu ya umuhimu wa Ushirikiano wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Ukafika muda wa maswali.
Picha ya pamoja.

VIDEO: SALAAM ZA MEI MOSI KUTOKA KWA KAIMU MKURURUGRNZI MKUU WA NHIF

MAGAZETI YA LEO JUMATATU MAY MOSI 2017

SMZ YAAHIDI KUUNGA MKONO JUHUDI ZA ZANUSO KATIKA SEKTA YA UJASIRIAMALI

$
0
0
Mshiriki wa Mashindano ya ujasiriamali kwa Vyuo vikuu, Tahani Said akipokea zawadi kutoka kwa Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Viwanda Zanzibar, Saleh Suleiman Hamad katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Zanzibar(ZANUSO).
Mshiriki wa Mashindano ya ujasiriamali kwa Vyuo vikuu, Issah Eugenio ambaye mradi wake wa Handbags made in Jeans umechukua nafasi ya mwanzo, akipokea zawadi kutoka kwa Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Viwanda Zanzibar, Saleh Suleiman Hamad katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Zanzibar(ZANUSO).
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Viwanda Zanzibar, Saleh Suleiman Hamad akiutubia wakati wa kufunga mashindano yaliyoandaliwa na jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Zanzibar(ZANUSO) huko ZU kampasi kuu ya Tunguu.
Mlezi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar(ZU), Mhadhiri wa Chuo hicho Juma Rashid Khamis wakati akizungumza katika uzinduzi wa mashindano ya miradi ya Ujasiriamali kwa wanafunzi wa vyuo vikuu Zanzibar yaliyofanyika katika kampasi ya chuo hicho huku Tunguu, Unguja.

MICHUZI TV: MAMBO YALIVYONOGA KATIKA SHEREHE ZA MEI MOSI KATIKA UWANJA WA USHIRIKA MJINI MOSHI LEO

$
0
0
Kutoka VIWANJA VYA USHIRIKA MOSHI -  ambapo leo tarehe 01 Mei 2017 kuanzia  asubuhi hii, Mhe. Rais Magufuli ni Mgeni Rasmi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi (MEI MOSI) ambayo kitaifa yanafanyika katika manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro

Fuatilia moja kwa moja kupitia tovuti rasmi ya Rais, BOFYA hapa;


Kwa kusikiliza BOFYA HAPA;



Pia fuatilia kupitia katika Televisheni za 

TBC1

AZAMTV 

AZAMTV

CLOUDSTV

STARTV

ITV

na katika Radio ya Taifa TBC Taifa
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live


Latest Images