Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1663 | 1664 | (Page 1665) | 1666 | 1667 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba akizungumza na Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Kilimo-IFAD wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bw. Sana Jatta alipofika Wizarani tarehe 28 Aprili, 2017. Pamoja na mambo mengine walizungumzia namna ya kuendeleza miradi ya kilimo na ufugaji hapa nchini kwa ajili ya kujihakikishia usalama wa chakula na lishe bora kwa maendeleo. 
  Sehemu ya ujumbe kutoka Ofisi za IFAD hapa nchini alioambatana nao Bw. Jatta. Kulia ni Bw. Francisco Pichon, Mwakilishi na Mkurugenzi wa IFAD nchini akiwa na Bi. Mwatima Juma Afisa Miradi Mwandamizi wa IFAD nchini. 
  Bw. Jatta nae akimweleza jambo Mhe. Dkt. Susan wakati wa mazungumzo yao. 
  Sehemu ya ujumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Jestas Nyamanga, Bi. Eva Ng'itu, Afisa Mambo ya Nje na Bw. Charles Faini, Msaidizi wa Naibu Waziri. 
  Mhe. Dkt. Kolimba katika picha ya pamoja na wageni wake. 

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  Timu ya mpira wa wavu (Volleyball) ya wanawake ya Magereza imetwaa ubingwa wa mchezo huo  katika mashindano ya Muungano yaliyofikia tamati  jana katika  uwanja wa Taifa wa Ndani jijini Dar es Salaam.

  Timu ya Magereza ya wanawake licha ya kufungwa mchezo wao wa mwisho dhidi ya Jeshi Stars wanawake kwa seti 3-2 walifanikiwa kuibuka mabingwa kwa tofauti ya pointi.

  Kwa upande wa wanaume, timu ya mpira wa wavu (Volleyball) Jeshi Stars wamefanikiwa kuibuka mabingwa wa mashindano ya Muungano baada ya kufanikiwa kuwafunga Magereza kwa ushindi wa seti 3-1.

  Mabingwa hao wamekabidhiwa zawadi pamoja na kikombe na aliyekuwa mgeni rasmi Katibu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Mohamed Kiganja.

  Mchezaji wa timu ya mpira wa wavu (Volleyball) ya Jeshi Stars, Fordey Edward ameibuka mchezaji bora (MVP)  wa mashindano ya Muungano yaliyofikia tamati jana.

  Fordey ameiwezesha timu yake ya Jeshi Stars kutwaa taji hilo baada ya kuifunga timu ya Magereza katika mchezo huo wa fainali. Fordey ambaye ni mkazi wa mkoa wa Tabora pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya mchezo huo
   Nahodha wa timu hiyo Averine Albert akikabidhiwa kikombe na Mgeni rasmi Ndg. Ahmed Kiganja ambaye ni katibu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
   Nahodha wa timu hiyo ya Jeshi Stars Abel Masunga akikabidhiwa kombe lao.

  0 0

  Na Husna Saidi- MAELEZO

  Takribani shilingi milioni 271 zinadaiwa kwa wakazi wa Manispaa ya Musoma Mjini, Mkoani Mara ikiwa ni kodi ya Pango la Ardhi. 

  Hayo yamebainishwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alipofanya ukaguzi wa mfumo wa kodi ya ardhi hivi karibuni Mkoani humo.

  Waziri Lukuvi alisema kuwa amekagua mfumo wa kodi wa manispaa ya Musoma mjini ili kuhakikisha wamiliki wote wa ardhi nchini wanalipa kodi kwa hiari kabla ya hatua za kisheria hazijafuata dhidi yao.

  “Nimeagiza kesi za madai ya kodi zitolewe hukumu ndani ya siku moja tu ili wadaiwa waweze kuchukuliwa hatua ya kuuzwa kwa mali zao haraka”, alisema Lukuvi.

  Aidha Waziri Lukuvi alimtaka Afisa Ardhi wa Manispaa ya Musoma Bw.Joseph Kamonga kuwasilisha majina ya wadaiwa hao katika Mahakama ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kupiga mnada majengo na mali zao kama wakikaidi kulipa kodi hiyo.

  Kwa upande mwingine Lukuvi alifanya uzinduzi wa mpango kabambe (Master Plan) wa Manispaa ya Musoma na kuwapongeza viongozi na watendaji wa Manispaa hiyo kwa kuwa Manispaa ya kwanza nchini kuweza kuzindua mpango huo kutumia kampuni za ndani katika utekelezaji wa mpango huo.

  Kufuatia hatua hiyo Waziri Lukuvi amezitaka Manispaa nyingine kutumia kampuni za ndani ya nchi ambazo zimesajiliwa na Wizara ya Ardhi katika kutekeleza mipango mbalimbali ya ulipaji kodi za ardhi. 

  Pia Waziri Lukuvi aliiagiza Manispaa ya Musoma kuandaa mpango mkakati wa utekelezaji wa mpango kabambe kwa kutumia wataalam wao (wa serikali) au Makampuni ya ndani na kutoa nakala za kutosha ili mpango huo uwafikie wadau wote na kutaka mpango huo utafsiriwe kwa Kiswahili ili Madiwani na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa waweze kuwafikishia wananchi kwa urahisi.

  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Bi. Ummy Nderinanga wakati wa mkutano wao na Waziri huyo ili kujadili utekelezaji wa majukumu uliofanyika Ukumbi wa mikutano wa ofisi hiyo Bungeni Dodoma.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo wakati wa mkutano wake na Viongozi wa SHIVYAWATA kujadili utekelezaji wa majukumu yao katika Ukumbi wa Ofisi yake Bungeni Dodoma Aprili 27, 2017.
   Wajumbe wa mkutano wa uongozi wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu nchini wakifuatilia maelekezo kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama wakati wa kikao chao Mjini Dodoma tarehe 27 Aprili, 2017.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiendesha mkutano na Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu walipokutana ofisini kwake Dodoma kujadili utekelezaji wa Majukumu yanayowahusu.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa SHIVYAWATA mara baada ya kumaliza mkutano wao, kushoto kwake ni Naibu wake (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde.

  (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU - DODOMA)

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  TEACHER’S Junction imetoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri mtihani wa ujirani mwema kwa shule 19 binafsi.

  Akizungumza katika hafla hiyo Mwalimu Mstaafu na aliyekuwa Mmiliki wa Shule Binafsi, Athuman Ahmed amesema kuwa mashindano upimaji wa wanafunzi kwa mtihani kutaongeza taaluma kwa wanafunzi hao.

  Ahmed amesema kuwa Teacher’s Junction wamekuwa kiungo kwa shule za sekta binafsi katika kuratibu masuala ya mitihani ya ujirani mwema.Amesema kuwa wanafunzi walioshinda wameonesha uwezo wao na wakiendelea watakuwa ni hazina kwa taifa.

  Afisa Miradi wa Teacher’s Junction, Salum Njama amesema kuwa wataendelea kuwa na mitihani mbalimbali katika kuwaandaa wanafunzi kitaaluma na sio ushindani kwa shule.

  Njama amesema shule zilizoshiriki katika mtihani huo 19 ambapo wanatarajia ushiriki wa shule nyingi na kuweza kujua viwango vya taaluma kwa wanafunzi.

  Amesema wamefanya katika Mikoa ya Arusha , Mbeya pamoja na Mwanza na kila sehemu iliyofanyika wanafunzi wameonyesha uwezo kitaaluma.
  Mwalimu Mstaafu, Athuman Ahemed akizungumza wakati wa utoaji zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri mtihani wa ujirani mwema ulioratibiwa na Teachers’s Junction kwa shule binafsi leo jijini Dar es Salaam.
  Afisa Miradi wa Teacher’s Junction, Salumu Njama akizungumza juu ya uandaaji wa mtihani wa ujirani mwema kwa shule binafsi wakati utoaji zawadi kwa wanafunzi iliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Walimu, wanafunzi pamoja na Teacher’s Junction wakiwa katika picha ya pamoja baada ya hafla ya utoaji zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Benki ya KCB Tanzania yadhamini mkutano wa Watanzania wanaoishi nchini Marekani. Mkutano huo utafanyika tarehe 5 – 7 Mei 2017 katika hoteli ya Wyndham Dallas Suites - Park Centrale, Dallas, Texas. Na unategemewa kuhudhuriwa na watanzania elfu moja kutoka majimbo mbalimbali ya Marekani.

  Akizungumza kuhusiana na mkutano huu, Meneja Mahusiano wahuduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya Nchi, Bi. Shose Kombe alisema Texas ni mji wenye watanzania wengi wakiwemo wanafunzi, wafanyakazi na wafanyabiashara wenye mahitaji ya huduma za kibenki kutoka Tanzania.

  “Tunaelewa kuwashughuli za kutafuta kipato na elimu hupelekea watanzania wengi kuenda sehemu mbalimbali duniani na kuishi huko kwa muda mrefu na hivyo huhitaji kuwekeza na kupata huduma za kibenki nyumbani wakiwa mbali na Tanzania.” Alisema Bi. Kombe.

  Meneja huyo alisema kuwa Benki ya KCB inawapatia watanzania wanaoishi nje ya nchi huduma bora za kibenki ikiwemo akaunti za akiba (savings), akaunti za uwekezaji (Investment), akaunti za wanafunzi, akaunti za watoto na fursa ya kununua nyumba (Mortgage) kwa lengo la kuwawezesha watanzania hao kuendesha shughuli zao za kibenki Tanzania huku wakiwa nje ya nchi na kupata akiba zao pindi watakaporudi nchini Tanzania. 
   
  Aliongeza kwamba huduma hizi za kibenki kwa watanzania wanaoishi nje ya nchini za papo kwa hapo (real time transactions), hivyo kuwawezesha wateja wake kufanya mambo kwa wakati na bila kadhia popote pale walipo duniani.

  “Watanzania wanaoishi nje ya nchi wanapaswa kupata huduma za kibenki kwa haraka, usalama na bila usumbufu” alisema Bi. Kombe. Na hivyo tunasema “JIULIZE KWANINI uhangaike kuweka akiba na kuwekeza nyumba ni ukiwa mbali na Tanzania wakati benki ya KCB ipo?”

  Akamalizia kwa kuwataka watanzania wanaoishi nje ya nchi na bado hawajajiunga na benki ya KCB kujiunga leo kupitia tovuti ya www.kcbbank.co.tz na kupata huduma za kibenki wakiwa nje ya nchi.

  0 0


  0 0

  Benki ya KCB Tanzania yadhamini mkutano wa Watanzania wanaoishi nchini Marekani. Mkutano huo utafanyika tarehe 5 – 7 Mei 2017 katika hoteli ya Wyndham Dallas Suites - Park Centrale, Dallas, Texas. Na unategemewa kuhudhuriwa na watanzania elfu moja kutoka majimbo mbalimbali ya Marekani.

  Akizungumza kuhusiana na mkutano huu, Meneja Mahusiano wahuduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya Nchi, Bi. Shose Kombe alisema Texas ni mji wenye watanzania wengi wakiwemo wanafunzi, wafanyakazi na wafanyabiashara wenye mahitaji ya huduma za kibenki kutoka Tanzania.
  “Tunaelewa kuwashughuli za kutafuta kipato na elimu hupelekea watanzania wengi kuenda sehemu mbalimbali duniani na kuishi huko kwa muda mrefu na hivyo huhitaji kuwekeza na kupata huduma za kibenki nyumbani wakiwa mbali na Tanzania.” Alisema Bi. Kombe.

  Meneja huyo alisema kuwa Benki ya KCB inawapatia watanzania wanaoishi nje ya nchi huduma bora za kibenki ikiwemo akaunti za akiba (savings), akaunti za uwekezaji (Investment), akaunti za wanafunzi, akaunti za watoto na fursa ya kununua nyumba (Mortgage) kwa lengo la kuwawezesha watanzania hao kuendesha shughuli zao za kibenki Tanzania huku wakiwa nje ya nchi na kupata akiba zao pindi watakaporudi nchini Tanzania. Aliongeza kwamba huduma hizi za kibenki kwa watanzania wanaoishi nje ya nchini za papo kwa hapo (real time transactions), hivyo kuwawezesha wateja wake kufanya mambo kwa wakati na bila kadhia popote pale walipo duniani.

  “Watanzania wanaoishi nje ya nchi wanapaswa kupata huduma za kibenki kwa haraka, usalama na bila usumbufu” alisema Bi. Kombe. Na hivyo tunasema “JIULIZE KWANINI uhangaike kuweka akiba na kuwekeza nyumba ni ukiwa mbali na Tanzania wakati benki ya KCB ipo?”
  Akamalizia kwa kuwataka watanzania wanaoishi nje ya nchi na bado hawajajiunga na benki ya KCB kujiunga leo kupitia tovuti ya www.kcbbank.co.tz na kupata huduma za kibenki wakiwa nje ya nchi.

  0 0

  Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imezuia wanachama wa CUF kufanya usafi katika makao makuu ya chama hicho yaliyopo Buguruni kutokana na kuwepo kwa viashiria vya uvunjifu wa amani kutokana mvutano wa makundi mawili.

  Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema ombi la kufanya usafi katika mazingira ya ofisi za chama hicho, lililowasilishwa na Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea Aprili 27 mjini Dodoma.

  Amesema kutokana na sababu za kiusalama pamoja na mgogoro wa muda mrefu unaoendelea ndani ya chama hicho, Mbunge huyo pamoja na wanachama wengine na wanashauriwa kila mmoja kufanya usafi katika eneo lake analoishi au analofanyia kazi.

  "Kitendo hicho cha wanachama wa CUF kukusanyika kutoka katika maeneo mbalimbali kwa kigezo cha kufanya usafi kinaweza kusababisha uvunjifu wa amani na atakayethubutu kujitokeza atachukuliwa hatua za kisheria," amesema Sirro.

  Wakati huo huo Kamanda Sirro amesema sakata la watu waliovamia mkutano wa iongozi wa CUF wilaya ya Kinondoni na wanahabari hadi sasa wanawashikilia watu saba akiwemo Mkurugenzi wa Mahusiano wa wa chama hicho, Abdul Kambaya.

  Amesema upelelezi wa kesi hiyo, umefanyika vizuri na tayari jalada limefikishwa kwa Mwanasheria wa Serikali kwa ajili ya hatua zaidi ikiwemo kufikishwa mahakamani.

  Jeshi hilo pia limewataka wananchi waliowahi kuibiwa magari yao kujitokeza katika Kituo cha Polisi Mbezi ili kuangalia kutokana,na kupatikana kwa magari matano yanayodaiwa kuibiwa jijini Dar es Salaam.
  Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Kitendo cha wanachama wa CUF kukusanyika kutoka maeneo mbalimbali kwa kigezo cha kufanya usafi kinaweza kusababisha uvunjifu wa amani atakethubutu kujitokeza atachukuliwa hatua za kisheria leo jijini Dar es Salaam.
  Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro akionesha madumu ya pombe haramu ya Gongo yaliyo kamatwa katika oparesheni ya jeshi la polisi leo jijini Dar es Salaam.

  Picha za magari yanayodaiwa kuibiwa jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka,Globu jamii.


  0 0   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb), leo tarehe 28 Aprili, 2017 amekutana na Bi. Maniza, Mwakilishi Mkazi wa UNICEF nchini. Bi. Maniza aliongozana na Bi. Birgithe Lund-Henriksen, Mkuu wa Ulinzi wa Haki za Watoto na Bi. Manisha Mishra, Mkuu wa Mawasiliano, Uratibu na Ushirikiano. Katika maongezi yao Bi. Maniza amesisitiza kuendeleza ushirikiano na Serikali katika miradi na programu za kulinda haki za watoto. Bi. Maniza alimhakikishia Mhe. Mwakyembe kwamba UNICEF itaendelea kuandaa vipindi vya runinga na redio kuhusu umuhimu wa kulinda haki za watoto na kuviwasilisha kwenye vituo vya runinga na redio ili viweze kuwafikia wananchi. Mhe. Mwakyembe alimshukuru Bi. Maniza na kumuahidi ushirikiano wa karibu kwenye miradi na program  hizo. "Watoto ndio viongozi wa kesho, hivyo hatuna budi kuwalinda na kuwapatia haki zao", alisisitiza Mhe. Mwakyembe. kufuatilia program za kulinda.
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb), amekutana na Mhe. SONG Geum, Balozi wa Jamhuri ya Korea leo tarehe 28 Aprili, 2017,  Dar es Salaam. Mhe. SONG alimhakikishia Mhe. Mwakyembe kuhusu ushirikiano wa karibu kwenye masuala ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Aidha,  Mhe. SONG alitumia nafasi hiyo kumkaribisha Mhe. Mwakyembe kwenye tamasha la filamu za Korea litakalofanyika tarehe 5-6 Mei, 2017 Dar es Salaam na tarehe 19-20 Mei, 2017 Arusha na tamasha muziki wa asili wa Korea litakalofanyika Dar es Salaam tarehe 16 Mei, 2017. Mhe. Mwakyembe alimshukuru Mhe. SONG na kumuahidi kudumisha uhusiano ulipo kati Tanzania na Korea katika nyanja za Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Vilevile Mhe. Mwakyembe alikubali mwaliko wa kuhidhiria kwenye matamasha yeye pamoja na Wizara kwa ujumla.


  0 0    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti  kwa Watumishi wa umma kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Angela Kairuki katika Ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akinyanyua juu Taarifa na vitabu vye majina 9,932 ya watumishi wenye vyeti vya kugushi.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe na kufungua boksi kubwa lenye majina ya watumishi zaidi ya 9,932 waliobainika kuwa na vyeti vya kugushi mara baada ya kupokea Taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti  kwa watumishi wa umma kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Angela Kairuki katika Ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia majina hayo pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan  mara baada ya kufungua boksi kubwa lenye majina ya watumishi hao wa umma ambao wamegushi vyeti vyao .
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisoma jina mojawapo la mtumishi aliyegushi cheti katika taarifa hiyo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa , Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako, Spika wa Bunge Job Ndugai, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Angela Kairuki wakiminya kitufe kuashiria maadhimisho ya miaka 10 ya Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM katika ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akihutubia viongozi mbalimbali, wanafunzi wa UDOM, pamoja na watumishi wa Umma mara baada ya kupokea Taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti  kwa watumishi wa umma kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Angela Kairuki katika Ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.PICHA NA IKULU.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0
  0 0


  WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama ametoa wito kwa waajiri wote nchini kujisajili kwenye Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF) kama sheria inavyotaka.

  Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Mahali pa kazi duniani yaliyofanyika Aprili 28,2017 kitaifa katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika mkoani Kilimanjaro, alisema bado kuna mwamko mdogo kwa waajiri kujisajili katika Mfuko huo. 

  “Serikali inathamini sana juhudi zenu kama waajiri katika kuajiri wafanyakazi, niwaombe sana Chama Cha Waajiri nchini tushirikiane katika kuongeza hamasa ya kujisajili kwenye Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ili hatimaye, Wafanyakazi wenu waweze kupata stahiki (Mafao), zao pindi wapatwapo na matatizo ya kiafya wanapokuwa kazini,” alisema Waziri Mhagama. 

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Matibabu na Tathmini kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi – WCF, Dkt. Abdulssalaam Omary 

  Alisema mwitikio mpaka sasa kati ya waajiri 23,000 waliowabaini 700 pekee ndiyo wamesajiliwa katika mfuko huo hivyo kuiomba serikali isaide kuhamasisha waajiri wajisajili kwenye mfuko huo. 

  Katika hatua nyingine Dkt. Omary alisema katika kipindi cha Mwezi Julai,2016 mpaka Machi 31,2017 wamepokea taarifa ya matukio 478 kutoka kwenye maeneo ya kazi. 

  Alisema kati matukio hayo 478,matukio ya ajali ni 454,magonjwa sita na vifo 18 katika maeneo ya viwandani,migodini na vyombo vya usafiri ambapo waliopata ajali huduma ya fao la matibabu 

  Aidha alisema mfuko huo unatoa mafao 7 ambayo ni mafao ya huduma ya matibabu,malipo ya ulemavu wa muda,malipo ya ulemavu wa kudumu,malipo ya anayemhudumia mgonjwa,huduma za ukarabati na ushauri nasaha,huduma za mazishi na malipo ya wategemezi. Angalia picha za matukio yaliyojiri katika banda la WCF katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama amewataka waajiri nchini kujitokeza kwa wingi kujisajili katika Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (Workers Compesation Fund – WCF) kwa ajili ya kuwawezesha waajiriwa kupata mafao pindi wanapoumia,kuugua au kufariki wakiwa kazini. 
  Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano WCF, Laura Kunenge akimkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama katika banda la WCF wakati wa maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi mwaka 2017 katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro.
  Mkurugenzi wa Huduma za Matibabu na Tathmini kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi – WCF, Dkt. Abdulssalaam Omary akiwasilisha mada fupi kuhusu Mfuko huo ambapo alisema walengwa wa mafao yanayotolewa na WCF kuwa ni wafanyakazi wa sekta ya umma na binafsi ambao wataumia au kuugua kutokana na kazi walizoajiriwa nazo.


  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Kazi, na Watu wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama, akipata maelezo kutoka kwa Kaimu meneja wa Rasilimali watu na Utawala wa Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Bi Amina Ally alipotembelea banda la SSRA wakati wa Maonyesho ya Maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa kazi OSHA yanayoendelea mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.
  Maafisa wa SSRA wakitoa ufafanuzi juu ya Masuala yanayoihusu Sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa wadau waliotembelea banda la Mamlaka hiyo wakati wa Maonesho ya OSHA yanayoendeleaa Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.
  Afisa Uhisiano na Uhamasiahaji wa wa Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Bw Ally Masaninga akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda la SSRA wakati wa Maonesho ya OSHA yanayondelea Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Kazi, na Watu wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama akimkabidhi cheti cha Ushiriki Kaimu meneja wa Rasilimali watu na Utawala wa Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) bi Amina Ally wakati wa kilele cha maonesho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi yanayoendelea Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.
  Wananchi wakisikiliza maelezo kutoka kwa afisa wa SSRA wakati wa maonesho ya OSHA yanayofanyika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo mafupi leo kutoka kwa mmoja wa wataalamu wa mradi huo, kuhusiana na mradi wa maji unaojengwa katika kijiji cha Mabama wilayani Uyui mkoani Tabora,Makamu wa Rais Mama Samia atazindua mradi huo wa maji utakao wafikia watu zaidi ya elfu 40 katika vijiji 32 mradi huu umedhaminiwa na serikali ya Japan kupitia shirika lake la JICA.Picha kwa hisani ya Ofisi ya Makamu wa Rais.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akileza jambo mara baada ya kupata maelezo mafupi leo kutoka kwa mmoja wa wataalamu wa mradi huo, kuhusiana na mradi wa maji unaojengwa katika kijiji cha Mabama wilayani Uyui mkoani Tabora,Makamu wa Rais Mama Samia atazindua mradi huo wa maji utakao wafikia watu zaidi ya elfu 40 katika vijiji 32 mradi huu umedhaminiwa na serikali ya Japan kupitia shirika lake la JICA.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifuatilia yaliyokuwa yakijili kabla ya uzinduzi wa mradi wa maji utakao wafikia watu zaidi ya elfu 40 katika vijiji 32 mradi huu umedhaminiwa na serikali ya Japan kupitia shirika lake la JICA.Kulia ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Inj.Gerson Lwenge na kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mh.Prof.Kitila Mkumbo pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Mh.Aggrey Mwanri.
  Baadhi viongozi na wawakilishi wa wananchi na wadau mbalimbali wakiwa katika tukio hilo la uzinduaji mradi wa maji,ambapo Mgeni rasmi ni Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.
  Baadhi ya vijana wakishiriki kuhudhudia tukiao hilo
  Baadhi ya Wanachama wa CCM na wananchi wa kwa ujumla wakifurahia kwa tukio hilo adhimu la kuzinduliwa mradi mkubwa wa maji unaozindulia katika kijiji cha Mabama wilayani Uyui mkoani Tabora,Makamu wa Rais Mama Samia atazindua mradi huo wa maji utakao wafikia watu zaidi ya elfu 40 katika vijiji 32 mradi huu umedhaminiwa na serikali ya Japan kupitia shirika lake la JICA.

  0 0


  Na Veronica Simba – Dodoma

  Balozi mpya wa Iran hapa nchini, Mousa Farhang amemtembelea Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kwa ajili ya kujitambulisha na kuzungumzia uwezekano wa nchi za Tanzania na Iran kushirikiana katika sekta za nishati na madini.

  Balozi Farhang alimtembelea Profesa Muhongo jana, Aprili 28, 2017 ofisini kwake mjini Dodoma.

  Akizungumzia nia ya nchi yake kushirikiana na Tanzania katika sekta ya nishati, Balozi Farhang alimwambia Waziri Muhongo kuwa Iran inazo sifa stahiki katika sekta hiyo kutokana na maendeleo iliyofikia ambapo alieleza kuwa mbali na kuzalisha umeme wa kutosha kwa mahitaji ya nchi, imejenga viwanda vya umeme katika baadhi ya nchi zinazowazunguka.

  Aidha, aliongeza kuwa, nchi hiyo huzalisha zaidi ya mapipa milioni nne ya mafuta kwa siku moja.

  “Miaka 10 iliyopita, Iran ilikuwa kama nchi nyingine zilizo nyuma kimaendeleo lakini sasa tunazalisha umeme mwingi unaotosheleza mahitaji ya nchi yetu na mwingine tunauza.

  Alisema kuwa, kutokana na utafiti alioufanya yeye binafsi, amegundua kuwa, sekta ya nishati ndiyo yenye nafasi kubwa na nzuri zaidi itakayowezesha nchi za Tanzania na Iran kunufaika endapo zitashirikiana.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), akifafanua jambo kwa Balozi mpya wa Iran hapa nchini, Mousa Farhang (katikati), wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri ofisini kwake mjini Dodoma hivi karibuni. Kulia ni Ofisa kutoka Ubalozini, Maisarah Ally.
  Balozi mpya wa Iran nchini Tanzania, Mousa Farhang (kushoto) akimkabidhi zawadi Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. Balozi Farhang alimtembelea Waziri Muhongo ofisini kwake mjini Dodoma hivi karibuni.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), akiagana na Balozi mpya wa Iran nchini Tanzania, Mousa Farhang (kulia). Katikati ni Ofisa kutoka Ubalozini, Maisarah Ally.


  0 0


  0 0

  Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Raisi muungano na Mazingira Mheshimiwa Luhaga Mpina, amewataka wakazi wa Mkoa wa Morogoro kutunza Vyanzo vya maji na Mazingira kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wameokoa maisha ya binadamu na viumbe hai wengine.
  Naibu Waziri Mpina ameyasema hayo leo alipikuwa katika zoezi la usafi kitaifa Mjini Morogoro ambapo amesisitiza kwa kufanya hivyo wakazi wa mkoa huo watakuwa wamesaidia wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam Pamoja na pwani ambao vyanzo vyao vyingi vya maji vimetokea mkoani Morogoro.
  Mpina pia aliweka msisitizo katika zoezi zima la upandaji miti ambapo kila wilaya inatakiwa kupanda miti milioni moja na nusu, "kutakuwa na ufuatiliaji wa hali ya katika utekelezaji wa zoezi hiyo katika ngazi ya Wilaya." Alisisitiza Mpina.
  Aidha Mpina aliunga Mkono Jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Morogoro katika suala zima la utunzani na usafi  wa mazingira , "Mnae Mkuu wa Mkoa anaetosha, anaujua mkoa vizuri na hwa ndiyo viongozi wa mkoa tunaowataka, wachapakazi na wenyekujituma. Alisema Mpina."
  Akiongelea suala la kuhamishwa wananchi katika milima na vyanzo vya maji, NW Mpina Alisema kuwa  " Tunapowaondoa wananchi katika maeneo hayo aimaaninishi kwamba tunawatesa. tunawapenda ndo maana tunawahamishia katika maeneo salama na rafiki kwa mazingira, RC watoeni wananchi wanaokaa katika maweneo Hatarishi." Alisema.
  Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bwana Kebwe Steven Kebwe, akizungumzia hali ya mazingira ya mkoa huo, alisema kuwa mkoa utajitahidi kupambana na hali ya uharibifu wa mazingira, pamoja na changamoto mkoa unazokumbana nazo akitolea mfano upungu wa vifaa vya kuzolea taka.

  Jumamosi ya usafi wa Mazingira Mkoani Morogoro kwa Jumamosi ya Mwishho wa mwezi wa nne ni utegelezaji wa Agizo la Mhe. Rais la Usafi wa Mazingira. 
   Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akitoa Mchanga katika moja ya Mtaro Mijini Morogoro wakati wa kufanya usafi, Leo.
  Moja ya Mtaro Uliosafishwa katika zoezi la usafi wa mazingira leo Mjini Morogoro

   Kulia Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bwna Kebwe Steven Kebwe akimkabirisha Naibu Waziri Mpina kabla a kuanza kwa zoezi la Usafi kitaifa Mjini Morogoro siku ya Jumamosi ya Mwisho wa mwezi wa nne.
  (Habari na Picha na Evelyn Mkokoi wa OMR)
   

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  TAASISI ya Tulia Trust inayomilikiwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson imewafadhili wanafunzi 27 kwa ajili ya kupata mafunzo ya sanaa.

  Taasisi hiyo imewadhamini wanafunzi hao kutoka Mbeya kusoma kwenye chuo cha Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUBa), kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani.

  Wanafunzi hao watapata fursa ya kujifunza sanaa ya maonyesho ya upigaji ngoma za asili, maigizo na utumiaji jukwaa.Akizungumza kwenye uzinduzi wa kuwakabidhi wanafunzi hao chuoni hapo, Dkt. Tulia amesema lengo la kuwafadhili vijana hao ni kutokomeza tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana.

  Amesema taasisi yake imedhamilia kukuza sanaa kwa vijana nchini ili kutatua tatizo la ajira na kuongeza ufanisi kwenye vipaji vyao walivyokuwa navyo awali.Alisema vijana hao wakipata mafunzo kwenye chuo hicho wataweza kufanya shughuli zao za ngoma za asili kiutaalamu zaidi, hali itakayowaongezea kipato na kuwafungulia fursa nyingi.

  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalum ya Vikundi vya  ngoma za asili kutoka mkoa mbeya yanayofadhiliwa na Tulia Trust.

  Mtendaji mkuu wa chuo cha Sanaa Bagamoyo(TASUBA) akizungumza kumkaribisha Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson
  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson, akicheza ngoma pamoja na Mtendaji mkuu wa Chuo Cha Sanaa Bagamoyo , Dk Herbert Makoye.

  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson akiwasili katika chuo cha Sanaa Bagamoyo kwa jili ya ufunguzi wa mafunzo kwa vikundi vya Sanaa mkoa mbeya.


  0 0

  Uwasa)inapoteza kiasi cha shilingi milioni 13 kila siku kutokana na kuongezeka kwa za shughuli za kibinaadamu zinazofanywa katika vyanzo vya maji vilivyopo katika Mto zigi na Muzii Wilayani Muheza. 

  Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea kwenye vyanzo vya maji,Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa alikiri kuwepo kwa uharibifu mkubwa katika vyanzo hivyo unaosababishwa na wananchi katika maeneo hayo. 


  Mhandisi Mgeyekwa alisema shughuli za uchimbaji wa dhahabu,kilimo na maogesho ya mifugo katika vyanzo hivyo vimekuwa vikichangia kwa kiasi kikubwa kuongeza matope kwenye bwawa la Mabayani linalosambaza maji Mjini hasa kipindi hiki cha mvua za masika. 


  Aidha alisema kuwa awali mamalaka hiyo ilikuwa inazalisha maji kiwango cha ujazo km 29,000 na kupungua hadi kufikia ujazo wa km 20,000 kwa sasa jambo lililopelekea kuanza kutoa huduma hiyo kwa mgao ndani ya Jiji la Tanga. 


  Alisema wao kama mamlaka baada ya kugundua kuwepo kwa tatizo hilo walianza kufanya jitihada mbalimbali ikiwemo kuvitembelea vyanzo vyote vya maji ili kubaini uhalisi uliopo na namna ya kuanza kulishughulikia jambo hilo kwa haraka zaidi ili lisiweze kuleta madhara kwa wananchi. 


  “Ki ukweli tatizo hili la katizo la maji na maji kutoka machafu haliwaathiri wananchi peke yake hata sisi kwenye maeneo yetu tunayokaa limekuwa likijitokeza hivyo tunaangalia namna ya kupambana nalo usiku na mchana kwa lengo la kutatua shida hiyo”Alisema. 


  Mratibu wa shughuli za Mazingira wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga Tanga Uwasa,Ramadhani Nyambukah akizungumza jambo kwa waandishi wa habari kuhusu dawa ambazo zinatumika kuwekwa kwenye maji 
  Mratibu wa shughuli za Mazingira wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga Tanga Uwasa,Ramadhani Nyambukah akiwaonyesha mitambo iliyopo kwenye kituo hicho wakati walipoitembelea kujionea

  Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Citizeni Mkoani Tanga, George Sembony akiwa kwenye vyanzo hivyo vya maji 


  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 1663 | 1664 | (Page 1665) | 1666 | 1667 | .... | 3286 | newer