Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110153 articles
Browse latest View live

RAIS WA ZANZIBAR AKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO WIZARA YA ELIMU ZANZIBAR.

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Ali Mohammed Shein katikati akimkabidhi Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Riziki Pembe Juma Jezi pamoja na Mipira kwa ajili ya mashindano ya maskuli vifaa vilivyotolewa na Muakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Ali Mohammed Shein katikati akimkabidhi Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Riziki Pembe Juma Viatu vya mpira wa Miguu kwa ajili ya mashindano ya maskuli vifaa vilivyotolewa na Muakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Ali Mohammed Shein katikati akimkabidhi Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Riziki Pembe Juma Kikombe cha kushindaniwa katika mashindano ya maskuli vifaa vilivyotolewa na Muakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Ali Mohammed Shein akitowa hotuba katika hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali vifaa vilivyotolewa na Muakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza Zanzibar. 
Baadhi ya Walimu na viongozi wa michezo katika maskuli waliohudhuria katika hafla ya Rais wa Zanzibar Dk,Ali Mohd Shein ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali vilivyotolewa na Muakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza Zanzibar. PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

SERIKALI KUWEKEZA KWENYE VIFAA TIBA VITOKANAVYO NA PAMBA.

$
0
0

Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.

Serikali kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unakamilisha taratibu za uwekeza kwenye vifaa tiba vitokanavyo na pamba na bidhaa za maji ya dripu(Infusion Fluids).

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge mjini Dodoma.

“Gharama za miradi hii inakadiriwa kufikia dola za kimarekani milioni 36.5 na kutoa ajira za moja kwa moja 1600 na zisizo za moja kwa moja 5000”, Alisema Mhe.Mwijage.

Amesema mradi huu unakadiriwa kutumia pamba tani elfu 50 kwa mwaka na Serikali ya Mkoa wa Simiyu inaendelea na jitihada za kutenga maeneo ya uwekezaji kwa kuwalenga wajasiriamali wadogo,wa kati mpaka wakubwa bila kujali kama ni wa kutoka ndani au nje ya nchi.

Aidha amesema kuwa azma ya Serikali ya ujenzi wa uchumi wa viwanda imeainishwa vyema katika mpango wa pili wa Maendeleo wa miaka mitano wa mwaka 2016/17-2020/21 wenye dhima ya kujenga uchumi wa viwanda ili kuleta mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya watu.

Pamoja na hayo ameainisha kuwa ili kufikia azma hiyo ushiriki wa mchango wa mtu mmoja mmoja,makundi ya watu,taasisi za umma na taasisi binafsi unahitajika.

Amebainisha mikakati minne ambayo imeanza kufanyiwa utekelezaji ni ya ngozi,mafuta ya kula,nguo na mazao jamii ya kunde uku wakati huohuo mpango wa wilaya moja,zao moja na uhamasishaji wa ujenzi wa viwanda chini ya SIDO unaendelea nchini kote.

VIJANA WAHAMASISHWA KUJIUNGA NA KILIMO CHA MBOGAMBOGA,MATUNDA NA NAFAKA.

$
0
0

Na Nuru Juma na Husna Saidi-MAELEZO

Umoja wa Kilimo cha Mbogamboga, Matunda na Nafaka umeanzisha Kampeni ya Kijana Inuka na Kilimo cha Mbogamboga na Matunda kwa lengo la kuepukana na kilimo cha mvua na vijana waweze kujiajiri wenyewe.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Umoja huo Wilaya ya Temeke Joseph Kunguru alipokutana na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.

Kunguru alisema kuwa kilimo hicho ni kilimo biashara na kinahitaji maji na miundombinu ya uhakika ili kuwafanya wananchi kulima kilimo chenye tija badala ya kulima kwa kutegemea mvua.

“Kilimo hiki kinaonekana ni kilimo ghari sana kwani ujenzi wa Green House unaonekana ni kilimo cha watu wenye pesa lakini ukweli ni kwamba wananchi wakiungana pamoja katika kilimo hiki wanaweza kufanikiwa badala ya kulima kwa kutegemea mvua,” alisema Kunguru.

Aidha alisema kuwa vijana wengi mtaani hawana ajira hivyo viongozi kupitia kampeni hii watumie fursa hiyo kuwaelimisha kuhusiana na kilimo hiki cha umwagiliaji ili waweze kujiajiri wenyewe.

Umoja huo wa kilimo cha Mbogamboga na Matunda na Nafaka umesajiliwa kisheria na ulianza na wanachama 17 mpaka sasa wapo 100 ila wanachama hai wapo 74 hivyo wanawasihi wananchi waendelee kujitokeza kujiunga.

Kwa upande wake mmoja wa wanakikundi hicho Sifa Karuka alisema alihamasika kujiunga na kikundi hicho baada ya kupata taarifa kuhusu kilimo hicho cha kisasa licha ya kuwa na shughuli zake binafsi hivyo anawasihi wakinamama na wasichana wajitokeze kwa wingi ili waweze kujiendeleza kiuchumi.

Nae Diwani wa Kata ya Buza James Raphael Mkude aliwahamasisha madiwani wenzie kuweza kuunda vikundi kama hivyo katika kata zao ili wananchi wao hasa vijana wasiokuwa na ajira waweze kujikwamua kiuchumi.

Kikundi hicho kimeiomba Serikali kupitia Maofisa Ugani kutoa mafunzo kwa vijana ambao hawana ajira kuhusiana nakilimo hicho ili kupunguza ukosefu wa ajira kwa kujitegemea wao wenyewe. 

Mwenyekiti wa Umoja wa Kilimo cha Mbogamboga Wilaya ya Temeke, Joseph Kunguru (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Kampeni ya kuwahamasisha Vijana kujihusisha na kilimo cha kisasa cha Mbogamboga na Matunda leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Diwani wa Kata ya Buza, Manispaa ya Temeke, James Raphael Mkude na Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo Waziri Pembe Waziri.
Diwani wa Kata ya Buza Manispaa ya Temeke James Raphael Mkude akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusiana Kampeni ya kuwahamasisha vijana kujihusisha na kilimo cha kisasa cha Mbogamboga na Matunda leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifatilia kwa umakini mkutano baina yao na viongozi wa Umoja wa Kilimo cha Mbogamboga na Matunda leo Jijini Dar es Salaam. Picha na: Husna Saidi – MAELEZO. 

RC MAHENGE AWATOLEA UVIVU MAAFISA KILIMO WAZEMBE

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt BILINITH MAHENGE ameamua kutema cheche kwa Maafisa kilimo wazembe ambao hawajui majukumu yao habari kamili hii hapa chini

TRA Yaja na Mikakati Mipya Ya Ukusanyaji Kodi

$
0
0

Na Husna Saidi na Nuru Juma- MAELEZO

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya Trilioni 10.87 mpaka kufikia Machi mwaka huu kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Hayo yamesemwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Charles Edward Kichere wakati wa mahojiano na mtangazaji wa TBC1 Rashid Salum katika kipindi cha Tunatekeleza kinachorushwa kila siku za Jumatatu saa moja kamili jioni na Alhamisi saa tatu na nusu usiku.

Kichere alisema, mwaka huu wa fedha 2016/2017 TRA inatakiwa kukusanya Trilioni 15.105 na hadi kufikia Machi mwaka huu TRA imefanikiwa kukusanya Shilingi Trilioni 10.87.

Aliendelea kwa kusema kuwa mpaka kufikia Juni mwaka huu TRA itahakikisha inatimiza lengo la kukusanya Shilingi Trilioni 15.105 ili kusaidia Serikali kuleta maendeleo kwa wananchi wake.

Alisema kuwa TRA ina waajiriwa wapya ambao wamepewa mafuzo ya miezi sita katika chuo cha kodi juu ya mifumo mbalimbali ya ukusanyaji kodi ambao waliajiriwa moja kwa moja na mamlaka hiyo kwaajili ya kutekeleza majukumu ya ukusanyaji kodi ndani ya nchi.

“Tunatumia mfumo wa Tehama kukusanya kodi na mifumo mingine mbalimbasli kama vile Tigo Pesa , Airtel Money na MPesa ili kurahisishia watu kulipa kodi wakiwa nyumbani na kuepuka usumbufu,” alisema Kichere.

Kichere aliongeza kuwa kwa mwaka huu wa fedha mapato yameongezeka mpaka kufikia asilimia 9.9 hadi 10 licha ya kuwa kuna baadhi ya maeneo hawakuweza kukusanya.

Aidha Kichere alisema Mamlaka kwa sasa imejipanga kuwa na mahusiano mazuri na wafanyabiashara ili kuhakikisha wafanyabiashara wanalipa kodi stahiki na kwa mujibu wa sheria bila kutumia nguvu au uonevu wowote.

Hata hivyo mamlaka hiyo imekuwa ikitoa elimu kwa walipa kodi kwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari, kutoa semina kwa watumishi wa umma , kuandaa makongamano ambayo yanatoa elimu, kupitia mitandao ya kijamii na ziara mbalimbali ambazo wamekuwa wakizifanya ili kuhakikisha wafanyabiashara wanapata elimu pamoja na kujua wajibu wao katika kulipa kodi ili kuleat maendeleo nchini.

TAMKO LA WAZIRI UMMY MWALIMU KATIKA KUADHIMISHA SIKU YA MALARIA DUNIANI MJINI DODOMA

WATAKAOTOZA FEDHA KUPIMA MALARIA NA KUUZA DAWA MSETO KUCHUKULIWA HATUA

$
0
0
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa Serikali haitosita kuwachukulia hatua mtumishi yoyote katika vituo vya Afya vya Umma nchini watakaobanika kutoza fedha katika kutoa huduma ya vipimo vya malaria na kuuza dawa za Mseto kwa ajili ya kutibu ugonjwa huo.

Ameyasema hayo Mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa Habari kutoa tamko la Siku ya Malaria Duniani na kusisitiza kuwa wananchi wanatakiwa kupata huduma ya kupima malaria pamoja na dawa za kutibu malaria bure katika vituo vya Afya vya Umma.

“Huduma ya kupima Malaria na dawa za Mseto zinatakiwa kutolewa bure katika vituo vyote vya Umma vya Huduma za Afya nchini na hatutosita kuwachukulia hatua watakaokiuka kutekeleza agizo hili.Alisistiza Mhe. Ummy.

Aidha amwewaagiza Waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya kutekeleza agizo hilo na kulisimamia kwa karibu ili kuondoa usufumbu kwa wananchi wanapotaka kupatiwa huduma hiyo.

Mhe Ummy Mwalimu amewashukuru wadau wote waliochangia kwa hali na mali katika mafanikio yaliyofikiwa ya mapambano ya dhidi ya Malaria nchini.

Siku ya Malaria Duniani uadhimishwa kila Aprili 25 ya kila mwaka na kwa mwaka huu kauli mbiu ni “ Shiriki kutokomeza Malaria kabisa kwa Manufaa ya Jamii”.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa tamko kuhusu Siku ya Malaria Duniani kwa waandishi wa Habari Mjini Dodoma na kusisitiza kuwa vipimo vya Malaria na Dawa za Mseto ni bure kwa vituo vyote vya Afya vya Umma nchini.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikata utepe kuzindua Kitabu cha Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Malaria katika kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na Wawakilishi kutoka kamouni ya Gullin Pharma mara baada ya kuzindua Kitabu cha Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Malaria katika kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani. Picha zote na Raymond Mushumbusi Dodoma MAELEZO.

LUKUVI ATANGAZA KIAMA KWA WASIOLIPA KODI YA PANGO LA ARDHI


Simbu arejea nyumbani kishujaa, aahidi kujipanga upya kwa mashindano ya dunia mwezi Agosti!

$
0
0
Balozi maalum wa DStv na Mwanariadha pekee wa Tanzania aliyeshiriki mashindano ya London Marathon 2017 Alphonce Simbu amerejea nyumbani na kutoa onyo kali kwa wale atakaokabiliana nao kwenye mashindano yajayo ya dunia  yatakayofanyika mwezi Agosti jijini London.
Simbu ambaye alishika nafasi ya tano katika mashindano hayo na kujishindia kitita cha dola za marekani 10,000 aliwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro na kulakiwa na maafisa mbalimbali akiwemo Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania Johnson Mshana na Meneja wa mwanariadha huyo Francis John.

 Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Arusha muda mfupi baada ya yeye kuwasili Simbu aliwashukuru sana watanzania wote kwa moyo wao na jinsi walivyomuunga mkono na kumtakia kila la heri katika mashindano hayo. Amesema alifarijika sana na pia kupata moyo zaidi alipokuwa akipokea salamu kutoka kwa watanzania kote ndani nan je ya nchi.
Akizungumzia mashindano hayo, Simbu amesema yalikuwa na changamoto kama yalivyo mashindano mengine makubwa ya kimataifa kwani yalishirikisha vigogo ambao wengi wao wana uzoefu mkubwa katika mashindano mbalimbali na wengine pia ni washindi wa mashindano ya hapo awali.


Alphonce Simbu akilakiwa katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro na  Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania Johnson Mshana (kulia) na Meneja wa mwanariadha huyo Francis John
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ambaye aliwakilishwa na mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Idd Kimanta (kulia) alisema mkoa mzima wa Arusha umepokea kwa Furaha habari za mkazi wao kufanya vizuri katika mashindano makubwa kama hayo na kwamba wataendelea kushirikiana na Simbu na kumsaidia kwa kadiri itakavyowezekana ili kumuwezesha kuendelea kuuwakilisha vizuri mkoa na taifa kwa ujumla kwenye michuano ya kimataifa.
Amesema kuwa ushindi wa simbu uwe ni chachu kwa vijana wengine wa kitanzania wenye vipaji na wasibaki nyuma bali wajitokeze na watie nguvu katika kuonyesha vipaji vyao. “Tuna vipaji vingi sana tena siyo kwa riadha tu, bali vya kila aina, cha mshingi ni kushirikiana kwa karibu na wadau ili kuhakikisha vipaji hivyo vinaibuliwa na kuendelezwa kwa manufaa ya taifa kwa ujumla” alisema mkuu huyo wa mkoa
.
Naye Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania Johnson Mshana amesema wao kama wadhamini wa Simbu wamepokea kwa Furaha kubwa matokeo hayo ambayo yanaonyesha kuimarika kwa kiwango cha Simbu. “Tuliamua kumdhamini Simbu tukiamini kabisa kuwa atakuwa nyota na atailetea Tanzania sifa. Tuna dhamira kubwa nay a dhati kabisa ya kuhakikisha kuwa siku moja wmbo wetu wa taifa unapigwa katika mashindano ya Olimpiki. Bila shaka hili lipo karibu kutokea”.alisema Mshana
Multichoice Tanzania inamdhamini Simbu kwa muda wa mwaka mzima kwa lengo la kufanikisha maandalizi yake ya kushiriki katika mashindano ya Dunia ya mwaka huu. Udhamini huu ulianza tangu mwaka 2016 ambapo Multichoice humpatia Alphonce posho ya kujikimu pamoja na kusaidia kambi yake ya mazoezi.
Alphonce, ambaye ni Mtanzania wa kwanza kushinda medali ya dhahabu katika mashindano maarufu ya Standard Chartered Mumbai Marathon, anatarajiwa kushiriki mashindano ya riadha ya dunia yatakayofanyika London mnamo mwezo Agosti mwaka huu.

JAMHURI YAOMBA KUONDOA KESI YA KUJIFANYA AFISA USALAMA ALIYEKUWA MWENYEKITI UVCCM ARUSHA

$
0
0
Na Wankyo Gati, ARUSHA 
 UPANDE wa Jamuhuri umeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi  ya jijini Arusha kuiondoa kesi ya kujifanya Afisa usalama wa Taifa  na kujipatia chakula  katika hotel moja ya kimataifa jijini Arusha inayomkabili aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa huo  Bw.
Lengai ole Sabaya. 
Akitoa ombi hilo Wakili wa Serikali Bi. Grace Madikenya mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha, Mhe. Gwantwa Mwakuga, alisema upande wa Jamhuri hauna nia ya kuendelea na kesi hiyo sababu shahidi mmoja muhimu yupo nje ya nchi kwa miezi 18. 
 “Sasa tumeona tutamtesa mteja wetu. Hivyo kwa nia njema kabisa tumeamua kuiondoa mahakamani kesi hii, maana miezi hii 18 ni  mwaka mmoja na miezi sita,”alisema. 
 Ombi hilo lilipingwa vikali na Wakili wa utetezi, Bi. Edna Haraka na kuiomba mahakama hiyo iendelee na kesi hiyo, kwa madai kuwa upande wa mwendesha mashitaka unatumia Mahakama kama kichaka cha kumnyima haki mteja wao na kumnyanyasa. 
Alisema upande huo hauna nia njema na mshitakiwa na kwamba kitendo cha kuiondoa kesi hiyo mahakamani sio mara ya kwanza ni mara ya pili, ambapo ya kwanza waliomba hivyo na mahakama ilipofuta walimkamata mteja wao na kumnyima dhamana. 
“Sasa leo tupo katika kusikiliza shahidi wa tatu na badala ya kuleta shahidi walileta maelezo ya shahidi na leo wanakuja na stori ya kuiondoa ili waendelee kumyanyasa mteja wetu. Hapana! Ofisi hiyo ya Mwanasheria Mkuu inatumika vibaya kwa kivuli cha Mahakama,”alisema Edna
Wakili huyo alisema serikali ya sasa inasisitiza mpango wa kuharakisha mashauri kusikiliza wa BRN, sasa wakati inafanyika hivyo wengine wanachelewesha kwa sababu zao. 
Hakimu Gwantwa Mwakuga baada ya kusikiliza pande zote mbili, alisema atatoa uamuzi Aprili 28 mwaka huu, ya  kama anakubali shauri liondolewe au la. Bw.  Lengai anakabiliwa na shitaka la kujifanya Afisa Usalama wa Taifa na kujipatia huduma ya chakula na malazi kwenye Hotel ya kimataifa ya Highway ya jijini Arusha.
Kutoka maktaba: Aliyekuwa Mwenyekiti  wa UVCCM mkoa wa Arusha Bw. Lengai Ole Sabaya (katikati) na wakili wake na wakitoka mahakamani siku za nyuma.

NGOMA AFRICA BAND INAWAKATIKIA WATANZANIA WOTE HERI YA MIAKA 53 YA MUUNGANO

$
0
0
Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani Ulaya The Ngoma Africa band inawatakia kila la heri na fanaka Watanzania wote popote walipo duniani katika kusherekea miaka 53 ya Muungano Day, na kusema siku hii adhimu na iwe na Baraka na mafanikio kwa wadau wote. 
Msikose kupata burudani kamili ya muziki wao at www.ngoma-africa.com

Kamanda wa polisi mstaafu Suleiman kova atunukiwa tuzo ya heshima na apec

$
0
0
Shirika lisilo la kiserikali la APEC limempatia tuzo ya heshima aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam Suleiman Kova katika sherehe za uzinduzi wa chuo jijini Dar es salaam. 
Kabla ya kutolewa kwa tuzo hizo, Mkuu wa APEC Bw.Respicius Timanya alitoa wito na kuhamasisha wananchi hasa madereva bodaboda kulaani mauaji ya polisi na kujenga utamaduni wa kuwakinga na majanga kwa kuhakikisha wanatoa taarifa za maovu kwa wakati.
Amesema tukio la mauaji ya polisi  lililotokea Aprili 13, mwaka huu,Mkengeni Kata ya Njawa wilaya ya Kibiti mkoani Pwani ni la kulaaniwa na kwamba ana imani halitotokea tena.
Amesema, ana imani kwamba mafunzo hayo ya bodaboda itawawezesha kutambua kuwa ulinzi na usalama ni wajibu wa kila mtanzania hivyo  kila mtu mwenye taarifa, tukio ama mtu anayemtilia shaka apeleke taarifa polisi.
Amewaomba waendesha bodaboda 350,000 waliopatiwa mafunzo ya usalama barabarani na Shirika hilo nchini kuzindua kampeni ya kulaani mauji ya polisi na kuhamasisha wananchi kuwa ni wajibu wao kuwakinga.
Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam Suleiman Kova akiongea machache katika sherehe za uzinduzi wa chuo cha APEC  jijini Dar es salaam. 








 Kamishna wa kazi Hilda Kabisa akiangalia sola ya kuchemshia maji wakati wa uzinduzi wa chuo cha Apec jijini Hapa.
Kamanda mstaafu Suleiman Kova akionesha cheti cha heshima alichopewa na chuo hicho 

TANGAZO KWA UMMA LA UUZWAJI VIWANJA KATIKA ENEO LA MKUNDI MOROGORO

MISS TANZANIA SUPERMODEL ATEMBELEA BUNGE MJINI DODOMA

$
0
0
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Harrison Mwakyembe,Naibu Waziri wake Mhe.Anastazia Wambura,Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Mwigulu Nchemba,baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  wakiwa katika picha ya pamoja na Mshindi wa Miss Tanzania Supermodel Bi.Asha Mabula katika viwanja vya Bunge mara baada ya mrembo uyo kutembelea Bungeni hapo  Mjini Dodoma. Picha na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.

KKKT DAYOSISI YA KASIKAZINI JIMBO LA HAI USHARIKA WA UDURU, MACHAME KATI - TANGAZO LA MKUTANO

$
0
0

Bwana asifiwe.

Mchungaji kiongozi wa Usharika  wa Uduru pamoja na wajumbe wa Baraza la wazee wanaomba kukutana na Washarika wote wa Uduru wanaoishi mikoa  ya Dar es salaam na Pwani, ili kuwapa taarifa za Usharika wao, pamoja na kushiriki nao chakula cha jioni kwenye Ukumbi wa Golden Resort Sinza (Lion Street) tarehe 30 April 2017 saa 10.00 jioni.


Kushiriki kwako ni muhimu sana kwa maendeleo ya Usharika wetu. Taarifa hii mpe na mwenzako.


MUNGU AWABARIKI SANA.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:  

 Mzee Manaseh Mwana Ndanshau    0754 284 926                                                               
Bw. Niko Semu Mushi                        0715 310 995


BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 25.04.2017

Balozi Dkt. Asha Rose Migiro aongoza Watanzania Waishio Nchini Uingereza kwenye Ibada ya Kuliombea Taifa Kuadhimisha Miaka 53 ya Muungano

$
0
0
Jumanne Aprili 25, 2017 Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Dkt Asha-Rose Migiro, amewaongoza Watanzania waishio Uingereza kushiriki Ibada Maalum ya kuliombea Taifa iliyofanyika katika Kanisa maarufu la Westminster Abbey jijini London.

Ibada hiyo ilifanyika kama sehemu ya kuadhimisha miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Ikiwa mwanachama wa Jumuiya ya Madola, Tanzania hufanyiwa maombi maalum kanisani hapo katika siku hii adhimu kila mwaka.

Pamoja na kusoma maandiko matakatifu, Ibada hiyo ilihusisha maombi maalum kwa ajili ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli na Serikali yake, Mahakama na Bunge kama mihimili mikuu ya Amani na Mshikamano wa Taifa la Tanzania na Wananchi wote wa Tanzania ndani na nje ya Nchi.
Ubalozi wa Tanzania London Uingereza unawatakia kheri Watanzania wote waishio Uingereza na Jamhuri ya Ireland katika maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Taifa letu.
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Dkt Asha-Rose Migiro, akiwa amewaongoza Watanzania waishio Uingereza kushiriki Ibada Maalum ya kuliombea Taifa iliyofanyika katika Kanisa maarufu la Westminster Abbey jijini London leo.

MFANYAKAZI BORA WA WIZARA, IDARA KUU YA MAENDELEO YA JAMII 2017

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Hamisi A. Kigwangalla akimtunuku zawadi mfanyakazi Bora wa Wizara yake (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) mwaka 2016/17, Bi Emiliana Nyarufunjo, mtalaamu wa TEHAMA wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika katika ukumbi wa Chuo kikuu cha Dodoma, hivi karibuni.

ZANZIBAR YAJIANDAA KUMALIZA KABISA MALARIA 2023

$
0
0
Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar 

Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman amesema pamoja na mafanikio makubwa katika kupambana na Malari Zanzibar, bado shehia tano zinaendelea kutoa wagonjwa wa maradhi hayo zaidi ya asilimia tano.

Akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho ya siku ya Malaria Dunia katika ukumibi wa mikutano wa Wizara ya Afya Mnazimmoja, amezitaja shehia hizo kuwa ni Tumbatu Jongowe, Miwani, Micheweni, Chukwani na Kiwengwa.

Hata hivyo amesema maambukizi ya malaria katika maeneo hayo yanasababishwa na wasafiri wanaoingia na kutoaka nje ya Zanzibar mara kwa mara ambapo mwaka jana asilimia 55 ya wagonjwa waliogundulika walikuwa na tabia hiyo.
Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt, Fadhil Mohd Abdalla akimkaribisha Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman kuzungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani katika ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar. 
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Bi. Harusi Said Suleiman akizunguza na waandishi wa habari katika maadhimisho ya siku ya Malaria Dunia katika ukumibi wa mikutano wa Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar. 
Mwandishi wa habari wa ITV/Radio One Farouk Karim akiuliza swali katika maadhimisho hayo yaliyofanyika kwa mkutano wa waandishi wa habari katika Wizara ya Afya Mnazimmoja. 
Meneja Kitengo cha Kumaliza Malaria Zanzibar Mwinyi Issa Khamis akijibu maswali ya waandishi wa habari katika maadhimisho ya siku ya malaria yaliyoadhimishwa kwa mkutano wa waandishi wa habari Wizara ya Afya Zanzibar .Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar. 


SERIKALI YAWATAKA WAAJIRI KUHAKIKISHA MITAMBO NA VIFAA VYA KAZI VINAFANYIWA UKAGUZI MARA KWA MARA.

$
0
0

Serikali imewataka waajiri wote na wadau kwa ujumla kuhakikisha kuwa sehemu za kazi, mitambo na vifaa vya kufanyia kazi vinafanyiwa ukaguzi mara kwa mara ili kuhakikisha kuwa havileti madhara kwa wafanyakazi.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Antony Mavunde wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo mjini Dodoma kuhusu maandalizi ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya mahali pa kazi.

“Kwa upande wa Serikali jukumu letu kubwa ni kuweka na kusimamia sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi, kutunga na kusimamia Sheria za Usalama na Afya Mahali pa Kazi, na kuweka viwango mbalimbali vya usalama na afya sehemu za kazi” alisisitiza Mavunde.

Mavunde alisema kuwa kwa sasa kanuni ya kuripoti ajali na magonjwa imekamilika na kuanza kutumika tangu mwezi Septemba, mwaka 2016.

Ambapo ameshauri wafanyakazi kuwasaidia waajiri wao kusimamia mifumo iliyopo, kujilinda wao binafsi ili wasiumie ama wasipate magonjwa yatokanayo na kazi sambamba na kutumia ipasavyo vifaa vyote vya kujikinga wawapo kazini.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde akitoa hotuba yake wakati wa mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA) kuhusu  maandalizi ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya mahali pa kazi uliofanyika Aprili 25, 2017 Dodoma. 
Baadhi ya Watumishi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA) wakimsikiliza Naibu wake Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Antony Mavunde (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Ofisi hiyo ikiwa ni maandalizi ya ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya mahali pa kazi uliofanyika Mjini Dodoma. 
Kaimu Mtendaji Mkuu OSHA Bi. Khadija Mwenda akizungumza wakati wa mkutano na Waandishi wa habari juu ya maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya mahali pa Kazi uliofanyika Mjini Dodoma Aprili 25, 2017. 
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw.Peter Kalonga akichangia hoja wakati wa Mkutano na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya mahali pa Kazi uliofanyika Mjini Dodoma Aprili 25, 2017. 

Viewing all 110153 articles
Browse latest View live




Latest Images