Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

miondoko ya kumeremeta kwenye mnuso


NAPE AITEKA DONGOBESH NA BASHNET

$
0
0
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akihutubia wakazi wa kata ya Dongo besh na kuwaambia wakati ndio huu kwa wao kuchagua kiongozi atakaye wafaa kwa kuleta maendeleo yao.
 Umati mkubwa wa wakazi wa Dongo besh wakimsikiliza kwa makini Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi kwenye mkutano wa kuhitimisha kampeni za udiwani zilizofanyika Dongobesh.
 Mgombea wa udiwani wa Dongo besh, Joseph almaarufu Cheng Lee akihutubia wakazi wa eneo hilo.Picha zaidi Bofya hapa

JK Mgeni rasmi mechi ya wakuu wa wilaya na wabunge itakayopigwa Juni 29

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mechi ya hisani itakayowakutanisha waheshimiwa wabunge na Wakuu wa wilaya, itakayopigwa Juni 29, katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Mechi hiyo itatanguliwa na ile ya Juni 22 mjini Dodoma, ambapo huko mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambapo lengo la mechi hizo ni kuchangisha fedha za ujenzi wa shule ya albino, huku kukipangwa kuwa na burudani za kila aina, sambamba na wasanii watakaoamua kuungana na serikali juu ya uchangiaji huo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Msemaji Mkuu wa timu hiyo ya wakuu wa wilaya, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, alisema kuwa huku mheshimiwa rais akiwa mgeni rasmi, ila wamejipanga imara kwa ajili ya kuwaonyesha kazi wabunge, ambao baadhi yao wameanza kujigamba dhidi ya mechi hiyo ya aina yake.

Alisema kuwa Watanzania wote watakaopata fursa ya kuhudhuria kwenye mechi hizo wataaburudika kwa kiasi kikubwa, huku wakiamini kuwa licha ya wakuu wa wilaya wengi kuwa mikoani, ila wana nguvu na ari ya kushinda mbele ya wabunge.

“Tupo imara na tutaanza mazoezi yetu kesho Jumatatu kwa kukutanisha wakuu wa wilaya wote waliokuwa kwenye timu hii, huku barua za kuwaombea mialiko kutoka kwa Wakuu wa Mikoa tayari zimeshafika kwa ajili ya kufanikisha zoezi hili.

“Katika mechi hizi, mwamuzi wa kati atakuwa atakuwa Reginald Mengi, ambaye ni Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, huku waamuzi wa pembeni wakiwa ni IGP Said Mwema na Stephen Wassira, ambapo wote watashiriki katika mchezo huu,” alisema.

Aliwataja Wakuu wa wilaya waliotwa kwenye uundwaji wa kikosi hicho kuwa ni pamoja na Venas Mwamoto (Kibondo), Ramadhan Maneno (Kigoma), Norman Sigara (Mbeya), Krispin Meela (Rungwe), Benson Mpesya (Kahama), Deodatus Kinanilo (Chunya), Herman Kapufyi (Same), Francis Isaac ( Chemba), Wilson Mkambaku (Kishapu), Yahya Nawanda (Iramba), Elibariki Kingu (Igunga), Festo Kiswaga (Nanyumbu), Paza Mwamlima (Mpanda), Abdallah Ulega (Kilwa), Seleman Mzee (Kwimba), John Mongela (Arusha), Konstantin Kanyasu (Ngara), Paulo Mzindakaya (Busega), Mrisho Gambo (Korogwe), uhingo rweyemamu handeni, Cristofa Magala( Newala), Erasto Sima (Bariadi), Jordan Rugimbana (Kinondoni), Joseph Mkirikiti (Songea), Ngemela Rubinga (Mpanda) nay eye mwenyewe anayotokea wwilaya ya Handeni, ambaye pia ni msemaji wa timu hiyo.

Aidha, Muhingo alitaja kikosi cha wanawake kuwa kinaongozwa na Beth Mkwasa (Bahi), Sarah Dumba (Njombe), Josephine Mapiro (Makete), Hafsa Mtasiwa (Pangani), Mboni Mgaza (Mkinga), Halima Dendegu (Tanga), Queen Mlozi (Singida), Angelina Mabula (Butiama), Merry Tesha (Ukerewe), Christina Mndeme (Hanang), Anna Magoha (Urambo) Jacqueline Liana ( Magu).

USAHIHI WA TAARIFA KUHUSU MANUNUZI YA ZABUNI YA MASHINE ZA KUKATIA TIKETI KATIKA KIVUKO CHA MAGOGONI

$
0
0
Hivi karibuni kulitolewa taarifa katika chombo kimoja cha habari kikidai kwamba wapo watumishi wa Wizara ya Ujenzi wanaolalamikia ukiukwaji wa sheria ya manunuzi ya umma katika zabuni hiyo. 

Mwandishi wa gazeti hilo ambaye amejitambulisha kama ‘Mwandishi Wetu’ ameendelea kuandika kuwa wapo pia baadhi ya wafanyakazi wa TEMESA wanaodai kuwepo kwa usiri katika manunuzi ya mashine hizo za kukatia tiketi. Aidha, kwa eneo lingine la taarifa hiyo mwandishi anadai kwamba malalamiko yametoka kwa wadau/mdau.

TEMESA inapenda kutoa taarifa rasmi kwamba taratibu zote za manunuzi ya mashine hizo zilizingatiwa kwa kutumia Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2004 na kanuni zake za 2005. Suala la usiri halikuwepo katika zabuni hii kwa kuwa utaratibu wote wa zabuni uliendeshwa na kusimamiwa na Kamati ya Manunuzi pamoja na Bodi ya Manunuzi ya Wakala, vyombo ambavyo vimewekwa kwa misingi ya sheria ya manunuzi. Sheria hiyo pia inaelekeza taratibu za rufaa kwa mzabuni ambaye hajaridhika na tathmini ya zabuni husika.

Aidha, manunuzi yote kuhusu vivuko vya Serikali na huduma zake hapa nchini yanafanywa na TEMESA kupitia Bodi yake ya Zabuni. Wizara kama msimamizi wa Wakala huu hupokea taarifa za utekelezaji. Hivyo, TEMESA ndiyo mamlaka iliyoshughulikia ununuzi wa mashine hizo.

Kwa mujibu wa mkataba, mzabuni aliyefunga mashine hizo yupo katika kipindi cha uangalizi kwa mwaka mmoja. Katika kipindi hicho jukumu lake ni kuangalia mashine alizozisimika na kutoa mafunzo ya uendeshaji kwa watumishi. Mashine hizo za kukatia tiketi zimeanza kufanyakazi tarehe 21/05/2013. Pamoja na kufungwa mashine za kukatia tiketi pia katika kituo hicho kumefungwa kamera maalum za kufuatilia mwenendo wa ukatishaji tiketi katika eneo hilo.

Tofauti na taarifa ya gazeti hilo kuwa, tangu kufungwa kwa mashine hizo za kukatia tiketi mapato yamekuwa yakishuka kwa kasi, ukweli ni kwamba makusanyo yamekuwa yakiongezeka kwa kiwango cha kuridhisha tangu kufungwa kwa mashine hizo ikilinganishwa na hapo awali. Aidha, TEMESA ndiyo inayokatisha tiketi na kukusanya mapato hayo na wala sio mzabuni anayeifanya kazi hiyo kama mwandishi wa gazeti hilo alivyodai katika taarifa yake.

Kwa kutambua majukumu ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kwa mujibu wa Sheria za Wakala Namba 30 ya 1997, Wakala unapenda kuarifu kwamba utaendelea kusimamia masuala ya manunuzi yote kwa misingi na taratibu za sheria, na utaendelea kuelekeza nguvu katika kuhakikisha mapato yatokanayo na vivuko yanakusanywa kwa ufanisi. Tayari Wakala umekwishaa anza kutumi portable electronics machines katika vivuko vingine.

Kutokana na mafanikio ya mfumo huu ulioonekana katika Kivuko cha Magogoni, Wakala unakusudia kueneza mfumo huu (electronic ticketing) katika vivuko vingine hapa nchini hatua kwa hatua.

Taarifa hii imetolewa na:

Eng. Marcellin Magesa
MTENDAJI MKUU

Tumepigwa 4-2 na wa Ivory Cost,lakini na sie chenga tumewala za kutosha...

$
0
0
 Kiungo machachari wa Taifa Stars,Mwinyi Kazimoto akiwachachafya mabeki wa Timu ya Taifa ya Ivory Cost,wakati wa mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu kucheza Kombe la Dunia,uliomalizika hivi punde kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Taifa Stats imefunga bao 4-2.
 Amri Kiemba wa Taifa Stars kiondoka na mpira.
 Golikipa wa Timu ya Ivory Cost,Barry Boubacar akidaka mpira ukiokuwa umepigwa na Mshambuliaji Machachari wa Taifa Stars,Thomas Ulimwengu.
 Mshambuliaji Machachari wa Taifa Stars,Thomas Ulimwengu akiondoka na mpya huku mabeki wa timu ya Ivory Cost wakimfuata kwa kasi ya ajabu bila ya mafanikio.Mpira umekwisha muda mfupi uliopita na na Matokeo ni Taifa Stars 2-4 Ivory Cost.

PICHA ZAIDI ZA MATUKIO MBALI MBALI YA MECHI HII ZITAFUATA

Article 24

President Kikwete tours Sunderland Association Football Club

$
0
0
 President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete and Chairman and owner of Sunderland Association Football Club Mr.Ellis Short pose with some students who study football skills at the club’s Academy of Light in Sunderland this afternoon. The Club in collaboration with Symbion Power Tanzania Limited have agreed to build a state of the art football academy in Dar es Salaam at the request of President Kikwete. President Kikwete is Londo for a three days working visit.
 President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with Sunderland’s Association Football Club  Chairman and owner Mr.Ellis Short at the Club’s Stadium of Light in Sunderland this afternoon.
 President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete talks to pupils attending  some lessons on football skills AND HEALTH  at Sunderland’s Association Football Club Academy of Light in Sunderland this afternoon.
 President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete and his delegation pose with some students who attend football training at Sunderland’s  Association Football Club Stadium of Light Academy this afternoon. Others in picture from left are Symbion’s Power Limited CEO Mr.Paul Hinks(left), Ilala member of parliament Hon. Musa Zungu(Second left), Minister for Information,Youth ,Culture and Sports Dr.Fenella Mukangara(fourth left) and Minister for Land and Human Settlement Prof.Anna Tibaijuka(right).
President  Dr.Jakaya Mrisho Kikwete unveils Sunderland’s Association Football plaque at the club’s Academy of Light this afternoon when the President and his delegation toured the club. On the left, looking on, is the Club’s Chairman and Owner Ellis Short.(photo by Freddy Maro).

Life Without Care: Losing Haydom Hospital, Tanzania


Wadau singida wakiangalia gemu la stars na ivory coast

$
0
0
...Hadi mwisho wa gemu hakuna aliyefurahi kama ambavyo Stars walipopata goli la kwanza

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Ngoma ya Bibie Roberta Flack ya 'Killing Me Softly With His Song' haichuji...

mkataa kwao mtumwa

miondoko ya kumeremeta kwenye mnuso

MAENDELEO YA MSIBA WA JEROME DAVID MPEFO

$
0
0
MAREHEMU JEROME DAVID MPEFO

NDUGU WANAJUMUIA,

 KAMATI ya msiba inapenda kutoa shukurani za dhati kwa Wanajumuia wote wa Houston na vitongoji vyake,watanzania waishio nje ya Texas na mataifa mengine kwa kufanikisha shughuli nzima za harambee ya kutafuta pesa za kupeleka mwili wa marehemu nyumbani Tanzania.

Moyo wa upendo na ushirikiano mkubwa ulioonyeshwa ni mafanikio makubwa ya umoja wetu wa jumuia yetu.

Kutakuwa na MISA ya kumuombea marehemu Jumanne,tarehe 6/18/13 saa kumi jioni,na baadaye kutoa heshima ya mwisho kwa marehemu.

Anuani ya kanisani:

St.Cyril of Alexandria Catholic Church
10503 Westheimer Rd
Houston Tx 77042
Simu: 713 789 1250
Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kwenda nyumbani kati ya Alhamisi na Ijumaa ya tarehe 6/20 au 6/21 baada ya mipango yote kukamilika.
Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa hapo baadaye.
Asanteni,
Juma Maswanya.
Kamati ya msiba.

WAKAZI WA KIJITONYAMA ALI MAUA WALIA NA DAWASCO

$
0
0
Uncle Kayfal Haal,

Kwanza nimshukuru mungu na kutoa shukrani zangu kwa globu ya jamii, maana nilipotoa malalamiko haya kipindi cha nyuma hwa jamaa wa DAWASCO walirekebisha hili tatizo la kutunyima hii haki ya maji safi na tukawa tunapata maji angalau kila weekend kwa muda wa miezi kama minne hivi.

Ila cha kushangaza kwa muda kama wa miezi miwili iliyopita sasa mchezo umerudia upya, ukifungua bomba matokeo ni hewa tu.

Uncle tunajua una mambo mengi ila usichoke kutusaidia maana ndio tegemeo letu, Globu inasikika na inasaidia, pengine waziri au mkuu mwengine anaehusika atasikia kilio chetu na kutusaidia, tunalia na huduma ya maji.
 
Ahsante,
 
Mdau.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, AFUNGA TAMASHA LA ASILI LA WATU WA MANGAPWANI UNGUJA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mlezi wa Tamasha la asili la Watu wa Mangapwani, Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Mwinyi Jamari Ramadhan Nasib, pamoja na baadhi ya viongozi wakati akiwasili kwenye viwanja vya Mangapwani jana Juni 15, 2013 kwa ajili ya kufunga rasmi Tamasha hilo lililoanza Juni 14.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia bidhaa zinazotengezwa na vikundi vya akina mama wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho katika Tamasha la Asili la Watu wa Mangapwani, alipofika kufunga rsmo tamasha hilo jana Juni 15, 2013, mjini Munguja.
  Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiingia shimoni wakati alipofika Mangapwani Kutembelea na kujionea Kisima cha Chini kwa Chini, kilichokuwa kikitumiwa na Wakoloni kupitishia Watumwa. Kisima hicho kilicho chini ya Ardhi huko ndani kuna Njia tatu, mbili zinatokezea Baharini na moja inatokezea katika moja ya Kijiji cha Mangapwani, ambayo hadi leo haijajulikana mwisho wa njia hiyo inapotokezea. 
 Katika Tamasha hilo kulikuwa na mashindano ya michezo mbalimbali ya asili, kama Bao la Kete, Kufua Nazi, na kama mchezo huu pichani vijana wakishindana kukwea Minazi, ambapo kwa upande wa michezo Tamasha hilo lilihitimishwa kwa mchezo wa fainali ya Soka.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mlezi wa Tamasha la asili la Watu wa Mangapwani, Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Mwinyi Jamari Ramadhan Nasib, pamoja na baadhi ya viongozi, kwa pamoja wakifurahia mchezo wa kukwea minazi wakati wa Tamasha hilo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Press Statement from U S Ambassador Alfonso E Lenhardt Condemning Bombing in Arusha

$
0
0
The United States of America strongly condemns the June 15, 2013 bombing at a public rally organized by the Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) political party in Arusha, which according to reports killed at least three people and injured over 40 victims. 

 We offer our deepest condolences to the families of those killed and to those injured by this heinous crime. This cowardly act follows the May 5, 2013 bombing at Saint Joseph's Roman Catholic Church in Arusha that reportedly killed three people and injured more than 60 victims. We call for the arrest, prosecution and conviction of those responsible.

Tanzania is a land known for its cultural richness, tolerance, and diversity. Violent actions of this nature, whatever their origin, threaten to tarnish and undermine the peace and security of this majestic land. The United States stands as a committed partner to all Tanzanians and we urge them to continue to denounce violence committed by those who threaten the security of their fellow citizens.

Finally, we call on all citizens to build on the values of wisdom, unity, and peace so carefully nurtured by Mwalimu Julius K. Nyerere, the Father of the Nation, which are forever enshrined in this nation's national anthem. Values which are equally cherished and admired by all Tanzanians and their fellow peace loving peoples around the world.

Athman Bawji Mbwana ashinda Udiwani kata ya mianzini

$
0
0
 Mgombea wa Udiwani wa Kata ya Mianzini, Athman Bawji Mbwana ameibuka mshindi wa uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata ya Mianzini uliofanyika jana kwa kupata kura 1283, huku Mgombea wa Cuf akipata kura 494, Chadema wakiambulia kura 315 na ADC walipata kura 26, NRA kura 9 na Mgombea wa NCCR Mageuzi akiambulia kura 1. Bawji amemzidi mshindi wa pili kwa zaidi ya nusu ya kura.
 Mara baada ya matokeo kutangazwa na tume kupitia kwa Afisa Mtendaji wa Kata, Wanachama wa CCM waliletewa matokeo yale na kusomwa na Mkurugenzi wa uchaguzi wao ambaye ni Katibu kata wa Mianzini wa CCM, Abdallah Kihuku mbele ya hadhara ya Wana CCM waliofurika katika ofisi za kata .  
 Mshindi mteule wa Udiwani wa Kata ya Mianzini, Athman Bawji Mbwana akiongea machache kwa Wana CCM mara baada ya kutawazwa kuwa mshindi. Bawji anaziba nafasi iliyokuwa wazi kufuatia kifo cha diwani wa kata hiyo.
 Mwenyekiti wa Mkoa wa CCM, Ramadhan Madabida akiwashukuru wana CCM kwa umoja na mapambano ya dhati yaliyopelekea ushindi wa CCM. Huu ndio uchaguzi wake wa kwanza tangu awe Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es Salaam na ni uchaguzi mdogo wa pekee wa udiwani kwa Mkoa wa  Dar Es salaam.
 Katibu wa Mkoa wa CCM, Abdillah Mihewa naye pia akitoa yake ya moyoni.
 Katibu wa Wilaya ya Temeke wa CCM, Ndg Robert Kihaka akiwashukuru Wana CCM kwa uvumilivu wao na jitihada zao zilizozaa matunda mema.Picha na Emmanuel Shilatu wa http//: www.ndgshilatu.blogspot.com

Fly540 signs interline deal with Qatar Airways

$
0
0
Fly540 has signed a deal with Qatar Airways to extend the reach of the Qatar national airline to a range of domestic and regional destinations currently served by Fly 540. Under the terms of the agreement, Qatar Airways’ passengers will be able to connect with a Fly540 Kenya flight at Jomo Kenyatta International Airport in Nairobi and fly to destinations within Fly540 Kenya’s network using one itinerary.

This will ensure that passengers have seamless, through-baggage and hassle-free onward connections to some of Kenya’s most beautiful destinations, including Eldoret, Kisumu, Lamu, Lodwar, Malindi and Mombasa and also across the border into Juba and Zanzibar’.

Qatar Airways flies twice daily between Nairobi and Doha, where travellers can connect with flights to cities across Europe, the Middle East and Asia Pacific. Qatar Airways said its choice of Fly540 Kenya as a interline partner reflects the Doha-based carrier's investment in East Africa as a strategic region.

A spokesperson for Fly540 Kenya said the deal demonstrated that the carrier is a credible airline that can offer a lot to airlines such as Qatar Airways. "We are delighted to have signed this interline agreement with Qatar Airways, which is our first such agreement," said Don Smith, CEO of Fly540 Kenya. "This deal expands our flight network beyond Africa and to a key growth-area of the Middle East."

Meanwhile,Fastjet’s executive chairman David Lenigas stepped down with immediate effect on June 10, and will be replaced by CEO Ed Winter on an interim basis, said the airline. Winter said Lenigas is leaving the post to concentrate on his other business ventures. Lenigras said his decision reflected a looming shift in the carrier’s operations and ownership.

"This is a time of transition for Fastjet both operationally and in terms of shareholder structure as its major shareholder, Lonrho, is likely to have a new owner in the coming weeks as a result of the current offer for Lonrho," he said. "It therefore seems to be a good time for me to step down to pursue my other interests and hand over the reins as Fastjet moves to the next stage of growth." FS Africa, representing a group of Swiss investors, agreed last month to take over Lonrho for £175m.

Lenigras’s resignation also follows the carrier’s announcement a few days back of its decision to terminate a securities deed with Bergen Global Opportunity Fund. In March, Fastjet closed a deal with the New York-based fund for £15.68m to support the airline’s growth.

AIRTEL YATOSHA YAINGIA MTAANI KWA MBWEMBWE!!!

$
0
0
Wakwanza ni muhamasishaji wa huduma ya Airtel Yatosha aliyevalia kijamii ya maasai Bw Petro Abraham Lucas akiwa na Wafanyakazi wa Airtel wakiwa wameshikana mikono kama ilivyo katika tangazo lao la gazeti na televisheni kuashiria kuwa huduma ya Airtel Yatosha kifurushi cha SIKU imeboreshwa na sasa ni masaa 25, ishara hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki kwenye barabara ya Ali Hassan Mwinyi.
Mkuu wa kitengo cha Biashara mpya cha Airtel Bw, Godfrey Mugambi akiwa na wafanyakazi wenzake wakiwa wameshikana mikono kuonyesha kweli Airtel Yatosha.
Wafanyakazi wa Airtel Tanzania makao makuu Dar es salaam wakiingia barabarani huku wameshikana mikono kwa maandamano ikiwa ni tukio maalum la kuitambulisha TOSHA 24+1=25.
Kikundi cha Airtel yatosha kikitoa burudani katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi wakati ambapo wafanyakazi wote wa Airtel jijini Dar e salaam waliposhikana mikono kuashiria kuboreshwa kwa huduma yao ya Airtel Yatosha kwa wateja ambayo sasa imeboreshwa zaidi ili kumuongezea mteja muda zaidi wa kutumia kifurushi chake cha siku kwa masaa 25 toka alipojiunga. Ili mteja kujiunga anatakiwa kupiga *149*99# , tukio hili lilifanyika mwishoni mwa wiki katika barabara hiyo.
Wafanyakazi wa Airtel toka vitengo mbalimbali wakiwa wamejipanga na kushikana mikono kuashiria kuboreshwa kwa huduma yao ya Airtel Yatosha kwa wateja ambayo sasa imeboreshwa zaidi ili kumuongezea mteja muda zaidi wa kutumia kifurushi chake cha siku kwa masaa 25 toka alipojiunga. Ili mteja kujiunga anatakiwa kupiga *149*99# , tukio hili lilifanyika mwishoni mwa wiki katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi,jijini Dar.

Article 10

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images