Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

TANZIA:Brigedia Jenerali (mstaafu) Albert Costantino Frisch afariki dunia

$
0
0
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)linasikitika kutangaza kifo cha Brigedia Jenerali Albert Costantino Frisch (mstaafu) kilichotokea tarehe         13 Aprili 2017.

Marehemu Brigedia Jenerali Albert Costantino Frisch(mstaafu)  alizaliwa tarehe 13 Novemba 1944, mtaa wa Uhuru,  Tarafa ya Kariakoo, Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam.  Alisoma na kuhitimu Shule ya Msingi mkoani Dar es Salaam na baadaye kuendelea na masomo ya Sekondari katika Shule ya Sekondari St. Joseph Convert School, Dar es Salaam hadi alipohitimu Kidato cha Nne mwaka, 1963.

Marehemu Brigedia Jenerali Albert Costantino Frisch (mstaafu), alijiunga na JWTZ tarehe 07 Desemba 1964 na kutunukiwa Kamisheni tarehe 22 Juni 1967.  Alistaafu Utumishi Jeshini kwa Heshima tarehe 30 Juni 1999.
Katika utumishi wake Marehemu alishika Nyadhifa mbalimbali Ikiwemo Mkaguzi Mkuu wa Jeshi Makao Makuu mpaka anastaafu.

Mwili wa Marehemu unatarajiwa kuagwa rasmi tarehe 20 Aprili 2017 katika Hospitali ya Jeshi Lugalo kuanzia saa 10:30 Asubuhi.


MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU

BRIGEDIA JENERALI ALBERT COSTANTINO FRISCH (MSTAAFU)

AMINA


Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano

Makao Makuu ya Jeshi, Upanga

S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.


Kwa Mawasiliano zaidi: 0756-716085.


WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFUNGUA MAONYESHO YA MIFUKO YA UWEZESHAJI YA SERIKALI

$
0
0
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na watumishi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) wakati alipotembelea banda la benki hiyo kwenye maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali aliyoyafungua kwenye uwanja wa Mashujaa mjni Dodoma  
 Waziri Mkuu, Kassim majaliwa akizungumza na wanachama wa kikundi cha Juhudi kinachojishughulisha na usindikaji vyakula kabla ya kufungua maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kwenye uwanja wa  Mashujaa mjini Dodoma 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikilza Bi. Evelyne  Mandenje amabaye ni mmoja wa wajasiriamali walionufaika na mikopo inayotolewa na Benki ya TIB wakati alipotembelea banda la wasindikaji vyakula kabla ya kufungua Maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma
 Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira  na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama  wakijadili jambo katika maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi  ya Serikali yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili 28, 2017. Kulia ni Afisa Mwandamizi wa Fedha wa  Benki ya TIB, Kenneth Lusesa.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkurugenzi wa manispaa ya Dodoma, Bw. Godwin Kunambi (wapili kushoto)  hundi ya Shilingi 1, 469, 358,0 00/= kwa ajili ya vijana kabla ya kufungua maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kwenye uwanja wa mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017.  Wanne kushoto ni Wziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kulia ni Naibu Wziri wake, Anthony Mavunde. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini , Christina Mndeme na watatu kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la  Taifa wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng Issa.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na  Mawasiliano wa Benki ya TPB, Noves Moses (kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Sabasaba Moshingi ( wapili kulia) cheti maalum cha kushiriki Maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kabla ya kufungu maonyesho hayo kwenye uwanja wa Mashujaa mjni Dodoma Aprili 18, 2017. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama.



MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA VIONGOZI WA UWT ZANZIBAR

$
0
0
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi wa UWT kutoka mikoa minne ya Unguja.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi wa UWT Unguja ambapo aliwaambia washikamane katika kukitetea Chama kilichobeba maana halisi ya Mapinduzi na alihimiza Vijana wapewe nafasi kwa wingi kwani wao wananguvu na kasi ya siasa ya wakati huu.
Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake,na Watoto Mhe, Maudline Castico akizungumza wakati wa mkutano wa Mjumbe wa Kamati Kuu CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Viongozi wa UWT Unguja .
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akizungumza kwenye mkutano wa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Viongozi wa UWT kwenye ukumbi wa NEC Afisi Kuu Kisiwandui, Zanzibar.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na wasanii wa Filamu nchini maarufu kama Bongo Movie waliopita kumsabahi kwenye Makao Makuu ya CCM, Kisiwandui Zanzibar.

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete atembelewa na Balozi wa Canada Nchini

$
0
0
 Rais Mstaafu Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo amekutana na Balozi wa Canada nchini Mhe. Ian Myles aliyemtembelea ofisini kwake Masaki jijini Dar es Salaam.
 Mheshimiwa Balozi Ian Myles aliwasilisha ujumbe maalum kutoka kwa Mheshimiwa Lloyd Axworthy, Mwenyekiti wa Global Refugee Initiative na Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje wa Canada. 
Mheshimiwa Rais Mstaafu amepokea ujumbe huo na kufanya mazungumzo na Balozi huyo wa Canada nchini kuhusu shughuli zake baada ya kustaafu hususan ushiriki wake katika Kamisheni ya Elimu.

YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA TISA MKUTANO WA SSBA WA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO APRIL 19, 2017.

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson  akiongoza kikao cha nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 18, 2017.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mhe. Suleimani Jafo akijibu maswali ya wabunge mbalimbali  katika kikao cha Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 19,2017.
Naibu Waziri wa Mambo ya nje ya Nchi na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Susan Kolimba akijibu maswali ya wabunge mbalimbali  katika kikao cha Tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 19,2017.
Wabunge wakifuatilia hoja mbalimbali katika kikao cha nane cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 19, 2017.  
Picha na Raymond Mushumbusi Dodoma MAELEZO.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WATU 13 WATAKIWA KUFIKA KITUO CHA KATI WAKIWA NA MITAMBO YAO YA KUZALISHA KAZI ZA WASANII

$
0
0

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema watu 13 wenye mitambo ya kufyatua kazi za wasanii za nje na ndani wakutane kituo cha kati wakiwa na nyaraka za kufanya kazi hiyo.

Akizungumza na Wasanii hao pamoja na Wananchi leo katika mkutano wa kupambana na uharamia wa kazi za wasanii , Makonda amesema kuna watu wanafanya kazi za ujanja ujanja kwa kuwanyonya wasanii.

Amesema kuwa kuanzia leo ni mwisho kwa wale ambao wanafanya kazi za kuuza nyimbo za wasanii na wanaotakiwa kufanya hivyo ni wale ambao wenye mikataba na wasanii wenye nyimbo husika.

Makonda amesema kuwa kazi zote za wasanii za zinatakiwa ziwe na sitika za Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ili nchi iweze kupata mapato kujenga huduma za wananchi.

Aidha amesema kuwa wauza wa kazi za wasanii mkononi zinatakiwa kuwa na stika za TRA pamoja na kuwa na kibali maalumu cha kumtambulisha  kufanya kazi hiyo kutoka  bodi ya filamu.

Hata hivyo amesema kuna watu wanafanya kazi za  kuwarubuni wasanii na kufanya maisha yao yawe duni katika kazi hiyo wakati Nigeria inaongoza kwa kupata mapato kupitia kazi za filamu.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na Wasanii katika mtaa wa Mafya mara baada ya kumaliza maandamano ya wasanii kupinga uuzwaji wa filamu za nje ambazo zinachangia kushuka kwa thamani ya filamu za ndani kutokana na bidhaa hizo kutolipiwa kodi
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda akiwa katika maandamano na wasanii wa Filamu hapa nchini kupinga uuzwaji wa filamu za nje ya nchi ambazo hazilipiwi ushuru. 
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa nchini(BASATA), Godfrey Mwingereza akizungumza na wasanii wa filamu waliofika katika maandamano hayo yaliyoitimshwa katika mtaa wa Mafia Kariakoo
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam , Simon Sirro akizungumza na wasaniii hao.
Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Filamu nchini , Jimy Mafufu akizungumza kwa niaba ya wasanii katika mkutano huo
Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema akizungumza na Wasanii waolifika karikoo mara baada ya maandamano ya kupinga Biashara ya uuzwaji filamu za nje
Kundi la Wasanii wakishangilia

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Bungeni leo

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Mawaziri kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma, Aprili 19, 2017. Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Tekinolojia na Mafunzo ya Ufundi Mhandisi Stella Manyanya, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangalla. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangalla kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Aprili 19, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mbunge wa Rufiji, Mohamed Mchengerwa kwenye jengo la utawala la bunge mjini Dodoma Aprili 19, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

DC LINDI AWATAKA WAZAZI KUSHIRIKI KATIKA KUWAWEZESHA VIJANA

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO.

Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Mhe. Shaibu Ndemanga amewataka wazazi kuacha tabia ya kuiachia Serikali na mashirika binafsi kuwawezesha vijana na badala yake washiriki kuwasaidia vijana hao ili waweze kujitegemea.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu nafasi ya Serikali katika kusaidia maendeleo ya vijana waliomaliza mafunzo ya ufundi chini ya Mradi wa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi (YEE) unaoratibiwa na Shirika la Plan International.

Ndemanga amesema kuwa mradi huo umeleta mabadiliko makubwa kwa vijana katika eneo hilo kwani wamefundishwa sio tu mafunzo ya ufundi bali pia ujasiriamali, namna ya kuweka hisa, kujiwekea fedha kwa ajili ya matumizi ya baadaye pamoja na masuala ya kodi lakini tatizo linalojitokeza ni wazazi kuwaachia Serikali na wadau wengine kushughulikia kila kitu.

“Changamoto ni nyingi katika kusaidia vijana hasa ambao tayari walishapata mafunzo kwa sababu wazazi wakishafahamu kuwa vijana wao wako chini ya mradi basi wanawaachia mzigo wote Serikali na wadau mbali mbali hivyo nawasihi wazazi wawasaidie vijana wao katika kujitafutia ajira”.alisema Ndemanga.

Ametoa rai kwa vijana kujitokeza kwa wakati pindi miradi hiyo inapotokea kwa sababu wengi wao wamekuwa wakichelewesha kuleta maombi hayo mpaka muda wa mafunzo unafika hivyo kwa kuwa mafunzo hayo hufanyika kwa muda maalum, vijana wanatakiwa wajitokeze mapema kwa idadi kubwa.

Aidha, Ndemanga amewataka vijana waliopata mafunzo kuwafundisha wenzao na pia wanaojiajiri wakumbuke kuwaajiri vijana wengine ili kupunguza mrundikano wa vijana wanaozagaa mitaani bila kuwa na kazi za halali.

Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Hamida Mohamed amekabidhi cherehani mbili kwa vijana wawili waliomaliza mafunzo ya ufundi chini ya mradi huo ikiwa ni njia mojawapo ya kuhamasisha ushiriki wa wazazi katika kuwakomboa vijana hasa kwenye masuala ya kiuchumi.

“Mradi huu umetusaidia sana kuwaona vijana wenye mazingira magumu hasa walemavu na kufahamu matatizo yao hivyo kutufanya sisi viongozi wa Serikali kufahamu namna ya kuwasaidia huku tukisaidiana na wadau mbalimbali”, alisema Mhe. Hamida.

Mradi huo wa miaka mitatu 2015 hadi 2018 unatekelezwa kwa ushirikiano wa mashirika ya VSO, CCBRT, VETA, UHIKI, CODERT pamoja na Serikali ya Tanzania huku ukiratibiwa na Shirika la Plan International chini ya ufadhili wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU).

TUME YA KUREKEBISHA SHERIA YAENDESHA MKUTANO WA WADAU KUHUSU MAPITIO YA SHERIA ZINAZOHUSIANA NA USAJILI WA MATUKIO MUHIMU YA BINADAMU TANZANIA BARA

$
0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Mhe. Jaji Aloysius Mujuliza (Kulia) akisisitiza jambo wakati mkutano wa wadau kuhusu Mapitio ya Sheria zinazohusiana na Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu Tanzania Bara, kushoto ni Bw. Albert Msangi.
Sehemu ya washiriki  wa mkutano wa wadau kuhusu Mapitio ya Sheria zinazohusiana na Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu Tanzania Bara.
Mmoja wa washiriki akichangia wakati wa mkutano wa wadau kuhusu Mapitio ya Sheria zinazohusiana na Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu Tanzania Bara

SERIKALI YAAMUA KUWAAJIRI MADAKTARI 258 WALIOTAKIWA KWENDA KENYA

Rais Magufuli, Makomandoo Kupamba Sherehe za Muungano Dodoma

$
0
0
Na: Lilian Lundo - MAELEZO.

Maonesho ya ukakamavu na mbinu za medani katika kupambana na adui hasa kulinda amani ya nchi yetu kutoka Kikosi Maalum cha Makomandoo wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), itakuwa ni sehemu ya shamrasha zitakazopamba maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano yatakayofanyika kwa mara ya kwanza mjini Dodoma Aprili 26 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama maadhimisho hayo yanatarajiwa kuhudhuriwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, pia yatapambwa na burudani nyingine kutoka vikundi mbalimbali.

Taarifa ya Waziri Mhagama ametaja shughuli nyingine zinazotarajiwa kufanyika siku ya Muungano kuwa ni gwaride la heshima lililoandaliwa na vikosi vya ulinzi na usalama (JWTZ,JKT, Polisi na Magereza) na onesho la mbwa na farasi waliofunzwa.

Aidha, Waziri Mhagama aliongeza kuwa mambo mengine yatakayofanyika ni gwaride la uzalendo la wanafunzi wa shule za sekondari za Dodoma, burudani za vikundi vya ngoma za asili kutoka Dodoma na Zanzibar, Yamoto Band, vikundi vya muziki wa kizazi kipya kutoka kwa wasanii Mchungaji Zayumba, Jacob Beats, Mwenge Jazz Band na Mgosi Maturumbeta.

“Kauli mbiu ya sherehe za kutimiza miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni Miaka 53 ya Muungano; Tuulinde na Kuumarisha, Tupige Vita Dawa za Kulevya na Kufanya Kazi kwa Bidii,” alifafanua Waziri Jenista Mhagama.

Ametoa wito kwa wananchi wote nchini kusherehekea siku hiyo muhimu kwa kudumisha amani, upendo, umoja na mshikamano kwa maendeleo ya nchi.“Ninaomba kuchukua nafasi ya pekee kuwaomba wananchi wote waliopo Dodoma kujitokeza kwa wingi uwanja wa Jamhuri siku hiyo ya Jumatano tarehe 26 Aprili 2017 kuanzia saa 12:00 asubuhi ili kusherehekea kwa pamoja maadhimisho hayo muhimu kwa nchi yetu,” alisema Jenista Mhagama.

Maadhimisho ya Muungano yanafanyika kwa mara ya kwanza Dodoma ikiwa ni siku kadhaa tangu Serikali ya Awamu ya Tano iabnze kutumiza azma ya kuhamia katika makao makuu hayo mapya. 

SERIKALI HAIDAIWI NA WAFANYAKAZI WA SEVENTY SEVEN HOTEL ARUSHA

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM-Dodoma

Wizara ya Fedha na Mipango imesema kuwa waliokuwa wafanyakazi wa Hoteli ya Seventy Seven ya mkoani Arusha, walioachishwa kazi mwaka 2000, wameshalipwa mafao yao kwa mujibu wa sheria na taratibu hivyo hawastahili kudai malipo yoyote ya nyongeza.

Hayo yameelezwa Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango (MB), Dkt. Ashatu Kijaji alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maaluum (CCM) Arusha, Mhe. Catherine Magige aliyetaka kujua ni lini Serikali itawalipa mafao waliokuwa wafanyakazi wa hoteli hiyo.

Mhe. Magige aliliambia Bunge kuwa waliokuwa wafanyakazi wa hoteli hiyo ambao waliachishwa kazi mwaka 2000, hawajalipwa mafao yao hadi sasa.

Akijibu swali hilo, Dkt. Kijaji alisema kuwa katika zoezi la ulipaji wa mafao kwa wafanyakazi hao Serikali ililipa Sh. 217,366,296 mwezi Januari, 2000 ambapo baadae walipokea malalamiko kutoka kwa wafanyakazi hao kuwa wamepunjwa.

“Serikali baada ya kupokea malalamiko hayo, ilihakiki na baada ya kujiridhisha mwezi Agosti, 2000, ilitoa idhini ya kulipa tena kiasi cha Sh. 273, 816, 703 kwa ajili ya mapunjo ya mishahara na mafao ya wafanyakazi hao” aliongeza.

Hata hivyo, Mhe. Magige hakuridhishwa na majibu ya Dkt. Kijaji na alipopewa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza alisema kuwa Serikali imewalipa wafanyakazi hao awamu ya kwanza tu na hawakupewa nyongeza yoyote licha ya kuwasilisha malalamiko hayo.

Mhe. Magige aliongeza kuwa Wizara ya Fedha ilishawahi kwenda kufanya uhakiki na kubaini kuwa kulikuwa na mapungufu, na Serikali iliipa jukumu la kusimamia malipo hayo Wizara ya Maliasili na Utalii ambapo mpaka sasa bado haijalipa.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii (MB), Mhe. Ramo Makani aliliomba Bunge limpe muda wa kufuatilia jambo hilo kwa ukaribu ili aweze kutoa majibu sahihi.

MAADHIMISHO YA MIAKA 53 YA MUUNGANO

WAFANYAKAZI WA KUJITOLEA WA KIMAREKANI WA PEACE CORPS HAMSINI NA MOJA (51) WA SEKTA ZA AFYA NA KILIMO WAAPISHWA

$
0
0
Katika hotuba yake, Kaimu Balozi Spera aliieleza hafla hii kama sherehe ya kuthibitisha dhamira ya dhati ya wafanyakazi wa kujitolea kuhudumu na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani.  “Serikali ya Marekani inafanya kazi katika maeneo yote – kuanzia utawala bora hadi maendeleo ya kiuchumi na usalama wa kikanda – lakini msingi wa kila tunachokifanya ni kuwasaidia watu wa Tanzania.  

Tunafanya hivyo vyema zaidi pale panapokuwa na ushirikiano katika ngazi ya mtu na mtu. Dhamira hii hudhihirishwa kila siku na wafanyakazi wa kujitolea wa Peace Corps, wenyeji wao na wafanyakazi wenzao wa Kitanzania,” alisema Kaimu Balozi Spera. 

Toka mwaka 1962, zaidi ya wafanyakazi wa kujitolea wa Peace Corps 2,850 wamehudumu nchini Tanzania. Peace Corps hutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa kujitolea wa Kimarekani wanaopangiwa kufanya kazi katika jamii wakihudumu katika nyanja za elimu ya sekondari (wakifundisha hisabati, sayansi na teknolojia ya Mawasiliano), afya na elimu ya mazingira.

Wafanyakazi wa kujitolea husaidia na kutoa mafunzo kuhusu utunzaji wa mazingira ikiwa ni pamoja na kuzuia kuharibika kwa ardhi, kulinda vyanzo vya maji, kuhifadhi ardhi na matumizi ya mbinu bora za kilimo na uhifadhi wa misitu (agro-forestry) wakiweka msisitizo katika kufanya kazi kwa ubia na wanawake na vijana. Pia watatoa mafunzo na kuwezesha kuanzishwa kwa kilimo hai cha bustani (bio-intensive gardens) ili kuongeza upatikanaji wa chakula, na kuboresha lishe ya kaya pamoja na shughuli nyingine za kujiongezea kipato.

Aidha, wafanyakazi hawa wa kujitolea husaidia katika kuimarisha afya ya umma kwa kufanya kazi na vituo, vikundi vya kijamii na vile vilivyomo mashuleni vinavyotoa huduma na elimu ya afya ikiwa ni pamoja na zile zinazohusu kujikinga dhidi ya VVU/UKIMWI, matibabu na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU/UKIMWI,yatima na watoto walio katika mazingira hatarishi. Wafanyakazi wa kujitolea hufanya kazi kwa karibu na kamati za afya vijiji ili kubaini na kuchambua mahitaji na vipaumbele vya jamii na kushiriki katika shughuli zinazohamasisha mabadiliko ya tabia katika maeneo ya afya ya mama na mtoto, lishe, malaria, maradhi yanayosababishwa na maji yasiyo salama, afya ya uzazi na kinga dhidi ya VVU/UKIMWI.

Peace Corps ni taasisi ya Serikali ya Marekani iliyoanzishwa na Rais John F. Kennedy mwaka 1961 ambayo hivi sasa inahudumia zaidi ya wafanyakazi wa kujitolea zaidi ya 8,000 katika zaidi ya nchi 60 duniani. Kwa miaka 56, Peace Corps imekuwa taasisi inayoendesha shughuli za mabadilishano ya kiufundi na kitamaduni zisizoegemea mrengo wowote wa kisiasa na kidini. Zaidi ya wafanyakazi wa kujitolea 189,000 wamehudumu katika nchi 140. 
Wafanyakazi wa kujitolea wa Kimarekani wa Peace Corps wapatao 51 wamekula kiapo cha utumishi wa miaka miwili nchini Tanzania katika hafla maalum iliyofanyika leo katika ofisi za Peace Corps jijini Dar es Salaam. Wafanyakazi hawa watakaohudumu katika sekta za afya na kilimo watapangiwa kufanya katika wilaya 20 nchini, ikiwa ni pamoja na wilaya za Iringa, Mufindi, Kondoa, Mbinga, Masasi, Ludewa, Lushoto, Songea, Kishapu, Makete na Singida vijijini. Wengine watapangiwa katika wilaya za Same, Njombe, Manyoni, Shinyanga vijijini, Mafinga, Makambako, Wanging’ombe, Mbeya na Lushoto. 


Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Vincent Spera aliwaapisha wafanyakazi hao wapya wa kujitolea mbele ya mgeni rasmi, Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Huduma za Afya na Lishe katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dk. Athumani Amir Pembe, na Mkurugenzi Mkazi wa Peace Corps nchini Tanzania Dk. Nelson Cronyn. 

 Hafla hii ilihudhuriwa pia na waliowahi kuwa wafanyakazi wa kujitolea wa Peace Corps katika maeneo mbalimbali dunia, maafisa kutoka taasisi wabia na familia zilizowahifadhi wafanyakazi wapya wa kujitolea wakati wakiwa mafunzoni.  

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) YATOA HUDUMA YA UPIMAJI WA MOYO KWA MTOTO ALIYEPO TUMBONI KWA MAMA YAKE (FETAL ECHO)

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Prof. Mohamed Janabi akiongea na waandishi wa habari kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo ikiwemo upimaji wa kina mama wajawazito moyo wa mtoto aliyepo tumboni (Fetal ECHO) ili kuangalia kama una magonjwa au la. Kutolewa kwa huduma hiyo kutasaidia kufahamu afya ya mtoto aliyepo tumboni ikiwa ni pamoja na hali ya moyo. 
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Naiz Majani akimpima Mama Mjamzito moyo wa mtoto aliyepo tumboni ili kuangalia kama una magonjwa au la. Mwishoni kwa mwaka jana Taasisi hiyo iliwapima wajawazito 25 kati ya hao watano watoto wao walikutwa na matatizo ya Moyo.Picha na Anna Nkinda – JKCI



WATUHUMIWA 267 WAKAMATWA JIJINI DAR ES SALAAM KWA MAKOSA MBALIMBALI.

$
0
0
Na Ripotawetu Globu ya Jamii.

Jeshi la Polisi limewakamata Jumla ya watuhumiwa 267 kwa Makosa mbalimbali ya kihalifu pamoja na Madawa ya kulevya, Unyang'anyi wa kutumia Silaha katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda Polisi kanda Maalum Dar es salaam Simon Sirro amesema operation hii ni endelevu na jumla ya kete 366 za dawa za kulevya zimekatwa pamoja  puli za bangi 150 na Misokoto ya bhangi 51.

Aidha Sirro amesema kuwa Operatini kali ya kuwasaka wahalifu wa makosa hayo mbalimbali ikiwemo kosa la kupatikana na madawa ya kulevya  bado inaendelea na hivyo tunawaomba raia wema waendelee kutoa Ushirikiano mzuri kwa Jeshi la Polisi ili kufanikisha kukamatwa kwa waalifu.

" Watuhumiwa wote kwa ujumla bado wanaendelea kuhojiwa kulingana na makosa yao na pindi  upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kwa hatua nyingine zaidi" amesema Sirro.

Pia Kamishna huyo ameongeza kuwa mnamo tarehe 15 mwezi huu 2017 majira ya saa moja usiku maeneo ya Kiwalani kwa Ally Mboa, Jeshi la polisi limefanikiwa kukamata silaha moja aina ya Shotgun ambayo imekatwa kitako na mitutu na huku namba zake zikiwa zimefutwa.

" Siraha hiyo ilipatikana wakati Askari wakiwa doria katika maeneo hayo ambapo yaliskia harufu ya bhangi na kuanza kufuatilia ili kubaini ilipokuwa ikitokea. Ghafla watu wawili wasiofahamika walikurupuka na kupanda pikipiki ambayo haikusomeka namba kisha kuangusha begi moja la mgongoni ambalo lilikuwa na Silaha" amesema Sirro.
 Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam Simon Sirro akizungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na watuhumiwa waliokamatwa kwa Makosa mbalimbali ya kiharifu katika jiji la Dar es Salaam.
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam Simon Sirro akionyesha baadhi ya vitu mbalimbali walivyo vikamata leo alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari.

PROFESA KITILA MKUMBO ATEMBELEA MTAMBO WA KUZALISHIA MAJI WA RUVU JUU

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji ametembelea Tenki la Maji la terminal lilipo karibu na chuo kikuu cha ardhi ambalo linapokea maji kutoka mtambo wa Ruvu juu na chini.

Pia ametembelea tenki kubwa jipya la Maji lilipo Kibamba Luguruni ambalo linapokea maji kutoka mtambo wa Ruvu juu na ametembelea Ofisi za Dawasco Mkoa wa Kibaha na kumalizia ziara yake kwa kutembelea mtambo wa kuzalishia Maji wa Ruvu juu ambapo umeanza kuzalisha maji mapya leo.
 Katibu mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo akiwa ameambatana na Ofisa Mtendaji mkuu Dawasco,mhandisi, Cyprian Luhemeja katika ziara ya kutembelea   Mtambo Ruvu juu uliopo mkoani Pwani.
 Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa DAWASA, mhandisi Romanus Mwangingo, akitoa maelezo mafupi kwa Katibu mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo kuhusu tenki jipya la Maji lilipo Kibamba Luguruni ambalo linapokea maji kutoka mtambo wa Ruvu juu mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea Mtambo huo wa uzalishaji Maji wa Ruvu juu uliopo Mlandizi, mkoani Pwani. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii.
 Ofisa Mtendaji mkuu Dawasco, mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa maelezo mafupi kwa Katibu mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo katika ziara ya kutembelea Mtambo Ruvu juu uliopo mkoani Pwani.
 Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MICHUZI TV: DALADALA LAPIGA MWELEKA NA KUINGIA MTARONI JIJINI DAR LEO

$
0
0
Basi la abiria linalofanya safari zake kati ya Makumbusho mpaka Posta, limepiga mweleka na kuingia mtaroni katika eneo la Oysterbay, Kinondoni jijini Dar es salaam mchana wa leo.

imeelezwa kwamba Basi hilo lenye namba za usajili T 958 DEJ aina ya Hino lililokuwa likitokea Posta kuelekea upande wa Moroco, lilijikuta likiingia mtaroni humo, baada ya dereva wake kushindwa mbinu za kulizuia kufuatia gari nyingine iliyoingia ghafla barabarani ikitokea upande wa Kituo cha Polisi Oysterbay, hivyo kutokana mwendo kasi wa basi hilo, ilishindwa kusimama na kuparamia mti uliokuwa kando ya barabara na kuingia mtaroni.

Inadaiwa kuwa abiria wote waliokuwepo kwenye basi hilo walitoka salama na kuendelea na safari zao.
Hivi ndivyo muonekano wa Basi hilo baada ya kuparamia mti.
Mashuhuda wa Ajali hiyo wakiwa katika eneo la tukio.

Article 10

Mtoto Hudhaifa Shatry atoa ujumbe wa kuwasisitiza wazazi Watanzania kuongea na watoto wao Kiswahili Ughaibuni

Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images