Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

KUMBILAMOTO AWATAKA CUF KUIMARISHA UMOJA KATIKA KATA YA VINGUNGUTI

$
0
0
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akiwaongoza Wanachama wa Chama cha Wananchi Cuf Buguruni kwenda kuweka bendera katika Matawi mawili ya Sarafina na Aluta, uwekaji huo wa bendera ni sehemu ya ujenzi wa Cuf  wa kuamsha wanachama kujitambua na kujenga umoja baina yao ili wasiyumbishwe.
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala,Omary Kumbilamoto akipandisha bendera katika tawi la Aluta kuashiria ujenzi wa CUF Taasisi na sio mtu ili kurejesha umoja na kuinua hali ya chama
 Wananchama wa Chama cha Wananchi Cuf Vingunguti wakicheza mziki katika mkutano wa chma hicho uliofanyika katika kata ya Vingunguti
 Naibu Meya wa  Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akikabidhi mfuko wa Saruji kwa Mwenyekiti wa tawi la Sarafina Zaid Mohamedi kwa ajili ya ujenzi wa kizmba cha tawi.
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akizungumza na Wanawake wa Chama cha Wananchi Cuf ambao walifika katika mkutano huo
Naibu meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akiwa katika meza kuu na baadhi ya Viongozi wa Chama cha wananchi Cuf katika mkutano wa kujenga Chama katika kata ya Vingunguti

TTCL YAKUTANA NA MAWAKALA ZAIDI YA 50 WILAYA YA TEMEKE

$
0
0
 Meneja Msaidizi wa wa mkoa wa Dar es Salaam Kusini wa mtandao wa simu ya Mkononi ya TTCL, Mwanaisha Semboko  akizungumza na Mawakala wa kuuza laini za Mtandao wa TTCL na kuwaeleza namna ya kuwafikia wananchi ambao hawajapata kuwa na laini za mtandao huo ili waweze kupata kutumia .

Semboko amesema kuwa Mtandao wa TTCL ni mtandao wa bei rahisi na wakizalendo, kwani fedha ambayo watapata kuchangia watanzania ni fedha ambayo inarudi katika maisha yao ya kila siku kwa kuendelea kujenga miundombinu ya mawasiliano ya Taifa hili .
 Baadhi ya Mawakala wakimsikiliza, Semboko wakati wakitoa mada ya faida za kuwa wakala wa mtandao huo
 Mratibu wa mkutano huo kutoka Makangarawe Youth , Ismail Mnikite  akizungumza na Mawakala waliofika katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam
 Afisa Mauzo wa mkoa wa Dar es Salaam Kusini , Amina Salum  akizungumza na mawakala hao juu ya uzwaaji wa laini za TTCL na faida zake na kutaja kuwa ni mtandao wa gharama nafuu katika data kuliko yote
 Mmoja wa mawakala walioshiriki mkutano huo , Monica Harry akiuliza swali juu ya huduma zinazotolewa na matandao wa simu za mkononi wa TTCL
 Baadhi ya mawakala wakisikiliza kwa makini namna ya kuwaunganisha watu katika mtandao wa TTCL

TAASISI YA NAMELOK KUJENGA KITUO CHA ELIMU KWA AJILI YA WAJASILIAMALI WASICHANA WILAYANI KIBAHA MKOANI PWAN

$
0
0
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA.
KATIKA kuunga juhudi za serikali ya awamu ya tano kupambana na wimbi la umasikini taasisi ya Namelok ya Wilayani Kibaha inatarajia kujenga kituo maalumu cha wasichana  na wanawake wajasiriamali ambacho kitakuwa kinajihusisha na masuala ya  utoaji wa mafunzo  mbali mbali kwa lengo la kuweza  kuwapa fursa ya  kuachana na kuwa tegemezi na kujiajiri wao wenyewe.

Akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa kituo hicho zilizofanyika katika Kata ya Mwendapole  iliyopo  katika halmashauri ya mji wa Kibaha  Mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo Janet Mwasuka amesema kukamilika kwa ujenzi  huo kutaweza kuwa ni mkombozi mkubwa wa kuwainua wanawake  hao kiuchumuni  kupitia  mafunzo ya stadi za kazi pamoja na  fursa zilizopo  kutokana na elimu watakayoipata.

Janet alibainisha kuwa anatambau kuwa wanawake wegine katika Wilaya ya Kibaha ambao baadhi yao wameshindwa kutimiza ndoto zao kutokana na kukosa elimu ya ujasiriamali hivyo ana imani kituo hicho kitaweza  kusaidia kwa kiasi kikubwa kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa wanawake pamoja na jamii yote kwa ujumla.
Naye Mkurugenzi wa Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya Purple Planet ya Jijini Dar es Salaam inayojishughulisha na  kuwasaidia katika kuendesha biashara zao na kuwainua kiuchumi wanawake wajasiriamali  Hilda Kisoka  amebainisha kuwa mikakati yao waliyojiwekea ni kufika mbali zaidi na kuuza bidhaa  wanazozizalisha hapa nchini  hadi nje ya nchi kwa lengo la kujitangaza zaidi.

Alisema kwamba ana imani wanawake wengi hapa nchini wana uwezo mkubwa wa kuengeneza bidhaa zenye ubora wa hali ya juu hivyo ameiomba serikali ya awamu ya tano kuwasaidi kwa hali na mali ili kuweza kufika mbali katika kuleta ushindani zaidi  wa masoko katika nchi zingine za nje na kuondokana na kuwa tegemezi.
 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kulia  Happiness Seneda akionyeshwa eneo lililopo kata ya Mwendapole na Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Namelok Janet Mwasuka wa  kushoto ambapo kutajengwa kituo maalumu cha elimu kwa ajili ya wasicahna na wanawake wajasiriamali  waliopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani (PICHA NA VICTOR MASANGU)
 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kulia Happiness Seneda kulia akiwa amemshika mmoja wa watoto huku akisikiliza maelekezo kuhusina na ujezni wa kiutuo hicho maalumu cha elimu kwa ajili ya wasichan na wakinamama kinachijengwa katika kata ya Mwendapole Wilayani Kibaha, kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Namelok Janet Mwasuka.
  Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Nameloc akoinyesha eneo ambalo kutajengwa kituo maalumu cha elimu kwa ajili ya wasichana na wanawake wajasiriamali katika kata ya Mwendapole  Wilayani Kibaha Mkoani Pwani

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RESOLUTION INSURANCE YAZINDUA HUDUMA YA HAKIKA PLAN

$
0
0
Meneja Mauzo wa Resolution Insurance, Nilufar Manalla (kushoto) akiwa na Meneja Masoko wa kampuni hiyo Laura Lyabandi kwenye mkutano na Waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya Hakika Plan ambapo wamama wajawazito, wagonjwa sugu na wadau wengine wanatakiwa kuitumia.
  Meneja Mauzo wa Resolution Insurance, Nilufar Manalla akizungumzia huduma ya Hakika Plan inayotolewa na kampuni kwa wateja wa rika zote
 Wafanyakazi wa Resolution Insurance wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kuzindua huduma yao hiyo ya Hakika Plan

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete atembelewa na Balozi wa Canada Nchini

$
0
0
 Rais Mstaafu Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo amekutana na Balozi wa Canada nchini Mhe. Ian Myles aliyemtembelea ofisini kwake Masaki jijini Dar es Salaam.
 Mheshimiwa Balozi Ian Myles aliwasilisha ujumbe maalum kutoka kwa Mheshimiwa Lloyd Axworthy, Mwenyekiti wa Global Refugee Initiative na Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje wa Canada. 
Mheshimiwa Rais Mstaafu amepokea ujumbe huo na kufanya mazungumzo na Balozi huyo wa Canada nchini kuhusu shughuli zake baada ya kustaafu hususan ushiriki wake katika Kamisheni ya Elimu.

KISHAPU WILAYA YENYE FURSA LUKUKI ZA UWEKEZAJI

$
0
0
Serikali ya Awamu ya Tano iko katika mkakati wake kabambe wa kuhakikisha kuwa Sera ya Tanzania yenye viwanda inafanikiwa, lengo kubwa likiwa ni kukuza na kuinua uchumi wa nchi.

Yote hayo yanafanyika kwa kufufua viwanda mbalimbali ambavyo vilikuwa vimekufa na kusitisha uzalishaji wake kutokana na sababu mbalimbali hatua inayokwenda sanjari na kujenga vipya.

Tunashuhudia juhudi kubwa za Serikali zikizaa matunda katika maeneo kadhaa ya taifa letu ambayo tayari wawekezaji wameanzisha viwanda vya kutengeneza bidhaa mbalimbali. 

Katika kudhihirisha hilo, pia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji inayoongozwa na Waziri Charles Mwijage imejikita katika kuwezesha wajasiriamali ili wainuke na kutambulika katika soko la kitaifa na kimataifa.

Hilo linafanyika kupitia maonesho mbalimbali ya viwanda na biashara ambayo hufanyika kila mwaka lengo ni kuwapa fursa wajasiriamali hao kuonesha bidhaa zao haijalishi kama ni kubwa au ndogondogo. Katika hilo Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu iliyopo katika Mkoa wa Shinyanga magharibi mwa Tanzania haiko nyuma kwani tayari imeanza utekelezaji wa sera hiyo muhimu kwa ustawi wa nchi.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba akizungumza katika moja ya vikao. Wengine pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo, Stephen Magoiga na Mwanasheria wa wilaya, Wilson Nyamunda.
Mmoja wa mafundi wa bidhaa za ngozi katika kiwanda kidogo cha Badimi akiwajibika. 

Sehemu ya mifugo ambayo ni muhimu kwa uwekezaji wa viwanda vya bidhaa za ngozi wilayani Kishapu.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Kumbu kumbu ya Misa ya Marehemu Mwl. Dionis Ndege

$
0
0
Umetimiza miaka 10 na siku 14 toka mwenyezi mungu alipokuchukua katika hospitali ya regency dsm tarehe 05/04/2007 siku ya alhamisi kuu. 
 
Unakumbukwa sana na mkeo mama Helena D. Ndege, wanao: Esaka D. N. Mugasa, James, Lawi, Anna, Mary, Lucy, Catherine, Tabu, Vicent, Joseph, Mwavisu, wanao wengine wote, Wajukuu, Vitukuu, ndugu, Jamaa, marafiki, wanafunzi wako, waalimu wenzio na majirani. 
 
Unakumbukwa pia kwa mchango wako mkubwa wa elimu hapa nchini toka ulipofungua shule ya msingi sirari mwaka 1954 ukiwa mwl. mkuu, na baadaye kufundisha katika shule za utegi, abainano, marasibora na wanyere. sisi tulikupenda sana lakini mungu alikupenda zaidi.
 
Jina la Bwana lihimidiwe. Amen.
 
Misa ya kumwombea marehemu imefanyika leo tarehe 18/04/2017 saa 4.00 asubuhi nyumbani kwake shinyanga mjini - mtaa wa lubaga.

uzinduzi wa kongamano la siku mbili la wadau wa Afya kujadili hali ya upasuaji nchini

$
0
0




Mkurugenzi wa Global Health kutokea Taasis ya GE, Asha Varghese akizungumzia ushiriki wa Taasis hiyo katika kongamano hilo
Mganga Mkuu wa Serikali Professa Muhammed Bakari akizungumza kwenye uzinduzi wa kongamano la siku mbili la wadau wa Afya kujadili hali ya upasuaji nchini (medical operation).
Wadau mbalimbali wa sekta ya Afya wanaoshiriki kongamano hilo wakifuatilia kwa umakini mjadala uliokuwa unaendelea.

 
Washiriki wa kongamano hilo wakiwa kwenye picha ya pamoja. 
======  ======   ======  ======
The Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children and Safe Surgery 2020 officially launch the National Surgical, Obstetrics and Anaesthesia Plan Process.

The Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children (MoHCDGEC) in collaboration with Safe Surgery 2020 officially launched the National Surgical, Obstetrics and Anaesthesia Plan (NSOAP) drafting process by convening Working Groups in Dar Es Salaam.

The Planning process was officially launched by the Permanent Secretary, Ministry of Health Tanzania, Dr. Mpoki Ulisubisya, and Ms Asha Verghese- Director, Developing Health Globally at the General Electric Foundation (GE Foundation) and Deputy Permanent Secretary for health at the President’s Office Regional and Local Government (PORALG), Dr. Zainab Chaula the Director of Health and Nutrition services at PORALG, Dr. Ntuli Kapologwe as well as Regional and District Medical Officers.

The need for a National Surgical, Obstetric and Anaesthesia Plan has been informed by various studies highlighting the urgent need to prioritize safe surgery in Tanzania. A study carried out using the WHO Tool for Situational Analysis to Assess Emergency and Essential Surgical Care in 2012 found that the average travel distance for patients receiving surgical care is 119 km in Tanzania.1 


The Lancet Commission on global surgery recommends that by the year 2030, 80% of the population should have access to emergency surgical care within 2hrs. However, the current proportion of Tanzania’s population that cannot access surgery within two hours is unknown.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

CGI Atembelea Ofisi Ya Mufti Wa Tanzania

$
0
0

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. AP. Makakala akieleza jambo kwa Mufti Mkuu wa Tanzania , Sheikh Abubakary Zubeiry bin Ally, alipomtembelea Mufti Ofisini kwake Kinondoni leo asubuhi.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. A.P. Makakala akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ofisini kwa Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeiry bin Ally, leo asubuhi Makao Makuu ya BAKWATA, Kinondoni, Dar es Salaam. Katikati ni Mshauri wa Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Khalid.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. A.P. Makakalla akiwa katika picha ya pamoja na Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeiry bin Ally, pamoja na baadhi ya Masheikh na Maafisa wa Ofisi ya Mufti leo asubuhi Makao Makuu ya BAKWATA, Kinondoni, Dar es Salaam

SERIKALI KULILIPA SHIRIKA LA POSTA SH. BIL 3.2

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

Serikali imeahidi kuwa italirejeshea Shirika la Posta Tanzania kiasi cha shilingi bilioni 3.2 ambazo ilizitumia kuwalipa wastaafu wa lililokuwa Shirika la Posta na Simu la Afrika Mashariki ifikapo kufikia 30 Juni mwaka huu itakuwa imelipa kiasi cha Sh. Bil.3.2 zinazodaiwa na Shirika la Posta Tanzania

Ahadi hiyo imetole Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na MIpango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ludewa, Mhe. Deo Ngalawa (CCM), aliyehoji Serikali ilikuwa na mpango gani wa kuwalipa Wastaafu hao yenyewe moja kwa moja bila ya kutumia fedha za mfuko wa Shirika hilo.

‘’Shirika linasuasua kujiendesha, fedha ambazo zilikuwa zitumike kwenye operation ndizo hizo zimekuwa zikitumika kuwalipa Wastaafu wa Afrika Mashariki ili kulinusuru Shirika hilo serikali haioni umuhimu wa kulipa deni hilo”.alihoji Mhe. Ngalawa.

Mhe, Ngalawa alitaka kujua kwanini Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), mwaka 2016 ilifungia akaunti za Shirika la Posta Nchini, kutokana na kuliidai Shirika hilo kiasi cha Sh. Mil.600, ikiwa Shirika hilo linaidai Serikali kiasi cha Sh. Bil.5.

Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alisema kuwa, Serikali ipo kwenye mchakato wa kuhakikisha fedha hizo zinalipwa na Serikali yenyewe na sio Shirika.
Naibu Waziri wa Fedha na MIpango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji.

Sehemu ya Mwisho - MAMBO USIYOYAJUA KUHUSU NYERERE

$
0
0

D: MTU WA MISIMAMO
Baada ya kumaliza darasa la nane Tabora, alipata nafasi ya kusoma chuo kikuu cha Makerere Uganda. Alisomea ualimu na alihitimu diploma mwaka 1947. Aliporudi Tanganyika, alipata nafasi ya kazi kutoka misheni na serikalini. Serikalini kulikuwa na mshahara mkubwa na marupurupu mengi kuliko misheni lakini alikataa kufanya kazi serikalini akipinga mfumo wa tofauti kubwa ya malipo.

Misimamo yake ya kupinga sera za kikoloni ilimgharimu kwani serikali ya kikoloni ilikataa kumpa nafasi ya masomo nje ya nchi. Ni kwa utetezi tu wa rafiki yake mkubwa, Father Walsh, ndipo alipokubaliwa kwenda kusoma chuo kikuu cha Edinburgh cha Scotland Uingereza, aliposomea historia, uchumi na falsafa.

E: MTU WA KUJISHUSHA
Chuoni Edinburgh alihitimu na kupata Masters na kuwa mtanganyika mweusi wa kwanza kupata mafanikio hayo. Hata hivyo, hakupata kiburi na aliporudi, akaenda kijijini kwao Butiama ambapo alijenga kwa mikono yake mwenyewe nyumba yake ili afungie ndoa na mchumba wake Maria Magige. Alichanganya saruji na mchanga yeye mwenyewe na kufyatua matofali. Wanakijiji walimshangaa msomi kama yeye kushika tope...wasomi wa wakati huo, wengi wao darasa la nne tu lakiji walikuwa daraja la juu sana.

F: MSHAWISHI
Alijiunga na harakati za siasa chini ya TAA. TAA hakikuwa chama cha siasa moja kwa moja bali kikundi cha kudai baadhi ya haki ambazo zilikuwa za wazungu pekee. Akawashawishi wazee aliowakuta wabadili malengo na kuanzisha chama rasmi cha siasa kitakachodai uhuru kamili badala ya haki fulani pekee. Wazee wakakubali na kuanzisha TANU, Julai 7, 1954 na yeye akawa mwenyekiti. TANU ikafanikiwa kuleta uhuru, 1961.

Lakini ushawishi mkubwa kabisa katika historia yake na ya nchi ni ule wa mwaka 1958 aliposhawishi wajumbe wa TANU kuingia kwenye uchaguzi mkuu wa baraza la kutunga (LEGCO). Vyama mbalimbali vilitakiwa kushiriki na chama kitakachopata wajumbe(wabunge) wengi ndicho kitakachounda serikali.

Huu ndiyo uchaguzi wa kwanza kabisa nchini na mkoloni aliweka masharti magumu kwa waafrika kupiga ili kukandamiza haki zao. Masharti hayo ni kuwepo kwa viti vitatu vitakavyoshindaniwa kwa matabaka(wazungu, waasia na waafrika) huku waafrika wakitakiwa kupiga kura zote tatu. Lengo la mkoloni lilikuwa kuhakikisha baraza la kutunga sheria linakuwa na wajumbe sawa, yaani waafrika, wazungu na wahindi. Kutokana na sharti hili, uchaguzi huu uliitwa UCHAGUZI WA KURA TATU.

Masharti mengine ya kumuwezesha mwafrika kupiga kura ni kuwa na kipato cha pauni mia nne za Uingereza kwa mwaka, pia awe na kiwango cha elimu ya darasa la 12(form four) na awe ameajiriwa katika kazi maalumu.

Masharti haya yaliwakera wazee na wanachama wa TANU. Viongozi wa makao makuu na majimboni wakapanga kuususia. 
Nyerere peke yake alitaka TANU ishiriki uchaguzi huu kwa sababu alihisi kama ingesusa, chama cha wazungu cha United Tanganyika Party(UTP) kingepata mteremko na kuzoa viti vyote na kuingia kwenye baraza la kutunga sheria huku TANU kikibaki nje. Kupitia fursa hiyo, wazungu wangetunga sheria kali zaidi za kuchelewesha uhuru kwa kisingizio kwamba waafrika hawajawa tayari kujitawala huku mfano ukiwa kususia uchaguzi. 

Nyerere aliona mbali zaidi ya wenzake ndani ya chama. 
Uchaguzi huo ulipangwa kufanyika Septemba 1958, TANU ikapanga kufanya mkutano wake mkuu wa mwaka wa 1958 mjini Tabora kuanzia Januari 21-26, 1958 kuamua hatima ya uchaguzi.

cc. Zaka Zakazi

NMB yapata faida ya shilingi bilioni 153.7 kwa mwaka 2016

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker akizungumza.

• Ni ongezeko la asilimia 2.4 la faida • Kwa miaka 10 mfululizo, NMB imeendelea kuongoza kwa faida nchini 

BENKI ya NMB imepata ongezeko la faida la asilimia 2.4 baada ya kodi kwa mwaka 2016. Mkurugenzi Mkuu wa benki ya NMB - Ineke Bussemaker amesema kwamba licha ya changamoto zilizoikabili sekta ya fedha na uchumi kwa ujumla kwa mwaka 2016, benki ya NMB iliweza kufanya vizuri.

“Faida ya benki kwa ujumla iliongezeka kutoka shilling billioni 150.3 kwa mwaka 2015 hadi shilingi bilioni 153.7 kwa mwaka 2016. Ongezeko hili limetokana na kuongezeka kwa pato linalotokana na Biashara ya benki lililokuwa kwa asilimia 16,” alisema Bussemaker. 

Riba katika mikopo ilikua kutoka shilingi bilioni 438.7 kwa mwaka 2015 hadi billioni 551.0 mwaka 2016 ambayo ni sawa na ukuaji wa asilimia 25.6. Pia Rasilimali za benki ziliongezeka kwa asilimia 8 kutoka shilingi bilioni 4,580 kwa mwaka 2015 hadi shilingi Bilioni 4,951 mwaka 2016. 

Mikopo kwa wateja iliongezeka hadi shilingi 2,794 billioni, ikiwa ni ongezeko la asilimia 13% kutoka shilingi bilioni 2,482 kwa mwaka uliotangulia. Ongezeko hili la mikopo ilitokana kwa kiasi kikubwa na ongezeko la mikopo kwa wafanyakazi kwa asilimia 16 kwa mwaka 2015 hadi kufikia shillingi bilioni 1,698 kwa mwaka 2016. 

Pamoja na ukata wa fedha uliozikumba benki nyingi mwaka 2016, ongezeko la amana za benki lilichangiwa kwa kiasi kikubwa na ongezeko la amana za wateja kwa shilingi bilioni 172 billioni, fedha ambayo benki ilikopa kiasi cha shilingi bilioni 312 pamoja na hati fungani ambayo ilipatikana kiasi cha shilingi bilioni 41. Gharama za riba ziliongezeka kwa asilimia 49 kutoka shilingi bilioni 68.5 kwa mwaka 2015 hadi shilingi bilioni 102.2 kwa mwaka 2016. 

“Amana za wateja ambazo kwa kiasi kikubwa ziliwekwa katika akaunti zisizokuwa na riba ziliongezeka kwa asilimia 4.8% kutoka shilingi bilioni 3, 568 kwa mwaka 2015 hadi shilingi bilioni 3,737 kwa mwaka 2016,” alisema. 

Aliongeza, “Idadi ya wateja wetu iliathiriwa sana na hali ya kibiashara kwa mwaka 2016, hali ambayo iliathiri ubora wa mikopo na kuchangia ongezeko la mikopo mibovu (NPL) hadi asilimia 4.8 kwa mwaka 2016 kutoka asilimia 2.4 mwaka 2015,” Ikishikilia asilimia 20% ya soko kwa mikopo na amana za wateja, benki ya NMB ni ambayo ni ya pili kwa ukubwa wa mizania ya Rasilimali za kibenki nchini, kwa miaka 10 mfulululizo benki imekuwa ikiongoza kwa kupata faida kubwa kuliko benki zote nchini.

PROFESA MKUMBO ATINGA DAWASCO NA KUWAMWAGIA SIFA, AWATAKA KUONGEZA USAMBAZAJI WA MAJI

$
0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo (wa kwanza kulia) akiwa ameambatana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco, Mhandisi Cyprian Luhemeja (wa kwanza kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Mhandisi Archard Mutalemwa (katikati) kuelekea katika chumba cha mkutano baada ya kuwasili makao makuu ya Dawasco jana kupokea taarifa ya huduma ya maji jijini Dar es Salaam na Pwani.

KATIBU mkuu  wa Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo amesema  kuwa hakuna sababu ya  taasisi za Serikali kushindwa kulipa bili ya maji wakati taasisi hizo zinapewa fedha kutokana serikalini  na yeye kama katibu aliyepewa dhamana hiyo atahakikisha shirika  hilo linaongeza uwezo wa  kuhudumia wananchi.

Profesa Mkumbo amesema hayo leo katika ziara yake ya kwanza  ya kikazi katika shirika hilo, ambapo pamoja na mambo mengine aliipongeza Dawasco kwa kazi kubwa wanayoifanya  kwani  ukilinganisha na huko nyuma ambapo malalamiko ya maji  yamepungua kwa kiasi kikubwa.

Mkumbo amesema haiwezikani  mwananchi wa kawaida  anamudu kulipa  bili ya maji alafu taasisi za serikali ambazo zinapewa fedha zinashindwa kulipa hivyo lazima wahakikishe wanalipa na Dawasco wanatakiwa wafanye kazi hiyo ya kukusanya bili hizo za maji.


 Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo akizungumza na waandishi wa habari na watendaji wa Dawasco baada ya kupokea taarifa ya huduma ya maji jijini Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani.

‘’ Nawapongeza  Dawasco  kwani mnafanya kazi kubwa  binafsi nimekuwa nikiwafuatilia hata kabla sijaingia wizaani kwakweli mnafanya kazi kubwa na mnastahli kupongezwa  lakini muendelee hivyo na kwakweli wananchi wanataka maji si vinginevyo.’’ Amesema   mkumbo.

Pia alisema pamoja na kazi kubwa nakudai kuwa watoke kwenye lengo  badala yake  wahakikishe tatizo la maji linakwisha kabla ya kufika 2020  kwani kuna miradi mikubwa mno ya maji ambayo inatekelezwa na kwakweli kama ikikamilika basi shida ya maji itakuwa limepata suluhisho.

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco, Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza machache katika mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Mkumbo ameiongeza kuwa lazima shirika litoke kwenye mtazamo na kuingia kwenye uhalisia  n hiyo ndiyo kazi kubwa  iliyopo  na hapo nikuona watu wanapata maji  huku kibainisha maeneo kama Bonyokwa,Pugu,Chanyanyikeni Kinyerezi, maeneo hayo kwa kiasi kikubwa yanakabiliwa na Changamoto kubwa ya maji nay eye kama Katibu amepongeza Dawasco kwa kuliona hilo.

 Akiwasilisha  wake  kwa katibu huyo Ofisa Mtendaji mkuu wa Dawasco  Sypriani Luhemeja alisema kuwa shirika hilo limepiga hatua kubwa ukilinganishana na huko nyuma ambapo uzalishaji ulikuwa chini.
Amesema hivi sasa Dawasco wanazalisha lita milioni 480 kwa siku na hitaji ni milioni 512  na kudai kuwa kiwango hicho ni kikubwa ukilinganisha na huko nyuma na kwamba bado wamejipanga kikamilifu kuhakikisha kwamba wanamaliza tatizo la maji katika mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.
Aidha alifafanua kuwa uzalishaji wa maji  katika ruvu chini ni lita milioni 217, ruvu juu lita mil 196  na kutoka mtoni lita 9000 na vyazo vinginevyo vinachangia kwa asilimi ndogo  huku akibainisha kuwa jumla ya wateja  187,087  wamehudumiwa  na lengo nikuwafikia wateja 400000, ifikapo mwezi  juni 2017.

  Akizungumzia Changamoto Luhemeja alisema ni usambazaji wa maji pamoja na upotevu wa maji  ambapo katika kipindi cha mwaka 2015 maji yalipotea kwa asilimia 57 na kufikia mwezi machi mwaka huu maji yamepotea kwa asilimia 37.8.


Sehemu ya watendaji wa Dawasco wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo  leo jijini Dar es Salaam.Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

MIAKA 20 IMEPITA, YANGA BADO ILE ILE

$
0
0
Mwaka 1998 Yanga ilifuzu kwa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa. Walipangwa kundi B sambamba na Asec Mimosas ya Ivory Coast, Raja Casablanca ya Morocco na Manning Rangers ya Afrika Kusini.

Mchezo wao wa pili ulikuwa ugenini dhidi ya Asec, ulipigwa mpira mwingi mno japo Yanga walipoteza 2-1. Baada ya hapo walitakiwa waende Morocco kucheza na Raja Casablanca. Tiketi zao za ndege ziliandikwa ndege itaondoka Jumanne saa sita usiku. Basi wao wakaitafsiri kwamba walale Jumatatu halafu waamke Jumanne ndiyo usiku wake waondoke...kumbe Jumanne saa sita usiku ni baada ya saa tano usiku ya Jumatatu. Wao.walipoenda Jumanne usiku, wakaambiwa ndege imeondoka usiku uliopita, wakachelewa.
Ndege nyingine ya kwenda Morocco itakuja Jumanne ijayo saa sita usiku. Ikabidi wabaki Ivory Coast mpaka hiyo Jumanne. Ukikutana na mchezaji wa Yanga aliyekuwpo kwenye kikosi kile, akikuhadithia maisha waliyoishi kule utatamani kulia. Haikushangaza walipoenda Morocco wakafungwa 6-0 na Raja Casablanca.
Hatua ya makundi iliendelea na mechi ya mwisho Yanga waliwakaribisha Asec Mimosas uwanja wa Taifa(siku hizi Uhuru). Katika mchezo huo ulioisha kwa kipigo cha 3-0, Yanga walivaa jezi za Taifa Stars kwa sababu jezi zao zilifanan na zile za Asec. Makosa mengine(ila sijui ni ya nani). Pichani hapo, beki wa Yanga, John Mwansansu, akikabana na Abou Dominique wa Asec.

Mwaka 2017, Yanga wanafanya makosa yale yale ya 1998, wanachelewa ndege na kuwalazimu kubaki ugenini wasijue waanzie wapi. Wakitoka huko wana mchezo dhidi ya TZ Prisons robo fainali ya kombe la Shirikisho la Azam Sports. Endapo watapoteza mchezo huo kutokana na uchovu, viongozi hawawezi.kukwepa lawama.

TFF KUTOA MAAMUZI YAKE KUHUSU ALAMA TATU ZA SIMBA NA KAGERA SUGAR


BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 18.04.2017

Mbiu ya KTN: Mkutano wa Mkulima market waandaliwa Dar es Salaam kuwasilisha wakulima

Zulfiqar Manzi: Teens Smoking on Social Media

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

makala ya sheria: MAKAMPUNI YA SIMU YANAUZA HISA, JE UNAJUA LOLOTE KUHUSU HISA ?.

$
0
0
Na  Bashir  Yakub
Ni  kipindi  muhimu  kujua  kuhusu  hisa. Hivi  karibuni  utakuwa  umesikia  makampuni  mbalimbali  hasa  yale  ya  simu  yakiwatangazia  watu  kununua  hisa.  Ni muhimu  kwako  kujua  kuhusu  biashara  hii.  Huenda  ikawa  ya  faida  kwako   au eneo  zuri   kwako  kwa  kuwekeza.

Mapema  niseme  kuwa  usiogope wala usiwe  mwenye  hofu. Biashara  ya  hisa  ni  ya  watu  wote tajiri  au  maskini.  Laki  moja,  laki mbili  nk.  unaweza  kununua  hisa.  Ili umiliki  hisa kwenye kampuni  ya  simu  si  lazima  umiliki  mamilioni  kama  unavyodhani.  Na  hapa  ndipo  tunapokosea na  kuwaacha  matajiri  watambe  nasi  tubaki  kulalamika.


1.HISA  NI NINI.

Hisa  ni  mali  kama  zilivyo  mali  nyingine  unazomiliki. Tofauti  ya  hisa  na mali  nyingine ulizonazo  kama  shamba,  gari,  nyumba  nk.ni  kuwa    mali   nyingine  huweza  kushikika   au  kuonekana  kwa  macho  wakati  hisa  ni  mali  isiyoonekana  kwa  macho.  Yumkini  zote  ni  mali  tu.

Hisa  ni  maslahi  au  haki  fulani  unayokuwa nayo  katika  taasisi au  kampuni  fulani.  Ndiyo  maana  ni  mali  isiyoonekana  kwasababu  huwezi  kuona  maslahi  au  haki  kwa macho.


2.  KUMILIKI  HISA  KATIKA  KAMPUNI.

Kampuni  yoyote  unayoiona huwa  inao  wanahisa.  Wanahisa  ndio  wamiliki  wa  kampuni.  Kwahiyo  hata  wewe  ukinunua  hisa  kwenye  kampuni  yoyote  na  wewe  unakuwa  mmoja  wa wamiliki. 

Haijalishi  ukubwa  wa kampuni  na  kiwango  chako cha  hisa ulichonunua  bali  ni  kuwa  ukishanunua  tu   hapohapo  na  wewe  unakuwa  mmoja  wa  wamiliki. Hata  hisa  za  laki  moja  nazo  zinakufanya kuwa  mmoja  wa  wamiliki.

Kiwango cha  hisa  zako  ndicho  kiwango  cha  umiliki  wako.  Kampuni  ikiwa  na  hisa  100,000   na  wewe  ukamiliki  hisa 50,000  basi  wewe  unaimiliki  nusu  ya  kampuni.  Ukimiliki  hisa  25,000  basi  wewe  unamiliki  robo  ya  kampuni.  Halikadhalika  ukimiliki  hisa  500,  100,  50,  10, 5  au  hata  hisa  3  basi  hichohicho  kiwango  chako  cha  hisa  ulichonunua   ndicho  kiwango  chako cha  umiliki   wa  kampuni  husika. 

Kwahiyo  ukinunua  hisa  100  Vodacom  basi  wewe  utaimiliki  Vodacom  kwa  kiwango  cha hisa hizo  ulizonunua. Isipokuwa  ni  muhimu  kujua  kuwa  anayemiliki  hisa nyingi  kuliko  wote  ndiye  hujulikana  kama  mmiliki  mkuu  wa  kampuni.


3.  JE  UTAFAIDIKAJE  NA  HISA.

Kila  mwanahisa  hupata  gawio  la  faida  pale  kampuni  inapotangaza  faida.  Kampuni  hutangaza  faida  kila  baada  ya  mwaka  au  nusu  mwaka  au  vinginevyo.


 Utapata  mgao  kwa  asilimia  kutokana  na  kiwango  chako  cha  hisa  ulizonazo. Ukiwa  na  hisa  nyingi  utapata mgao  mkubwa,  ukiwa  na  hisa  kidogo  utapata  mgao  mdogo   na  vivyo  hivyo. 


Kusoma zaidi BOFYA HAPA



Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images