Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1650 | 1651 | (Page 1652) | 1653 | 1654 | .... | 3278 | newer

  0 0

  East Africa’s music giants Bebe Cool (Uganda) and Sauti Sol (Kenya) are thrilled to announce the release of their new collabo titled ‘MBOZI ZA MALWA’, luganda for conversations that usually take place when friends are having a drink at their local joint. Written by Yesse Oman Rafiki and Sauti Sol, the song has a dancehall vibe and was recorded in Kampala, Uganda. Produced by Danz, co- arranged by Sauti Sol the song was mixed and mastered by Ogopa Inc.

  Bebe Cool explains that: ‘In many African Communities if you want to know the latest gossip in around the communities, visit a local bar or high end bar with friends for a drink and all talk will rotate around what is making news in the community.’

  ‘We had an amazing time working with Bebe Cool. Our East African fans have been requesting for this and we hope they will love it as we do.’ Sauti Sol added in their statement.

  This to announce an online dance contest between Kenyan girls and Ugandan girls as we eagerly await the video which will be out on the 24th of this month. Using the hashtag #MboziZaMalwa, the winner/s from each country will get to go head-to-head with each other. The ultimate winner/s will be announced by Bebe Cool on April 26th and will get the bragging rights of "The Best Dancer/s in East Africa, a chance to hang out with an artist of their choosing between Sauti Sol and Bebe Cool and take home a whopping $500. The contest will run from April 17th - April 26th.  Follow @sautisol and @bebecool_ug for more details.


  0 0

  Makamu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu ya Halotel Pham Dinh Quan (kulia) akiwaongoza wafanyakazi wenzake kutoa zawadi kwa mmoja wa mama wa watoto wenye vichwa vichwa vikubwa na mgongo wazi waliolazwa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI).
  Meneja Mawasiliano wa kampuni ya simu ya Halotel, Stella Pius (kulia) na wafanyakazi wenzake wakitoa zawadi kwa mmoja wa mama wa watoto wenye matatizo ya vichwa vichwa vikubwa na mgongo wazi waliolazwa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI)
  Wafanyakazi wa kampuni ya simu ya Halotel wakiwa katika picha ya pamoja nje ya wodi ya watoto ya Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI) kabla ya kutoa zawadi ya Pasaka kwa watoto hao.    

  Wito umetolewa kwa jamii ya watanzania kuacha mila potofu inayopelekea tabia ya baadhi ya wazazi kuwaficha watoto wenye matatizo mbalimbali hasa tatizo la kichwa kikubwa na mgongo wazi bali wawapeleke hospitali mapema ili wapate matibabu kwani wanaweza kupona endapo wakiwahishwa hospitali.

  Wito huo umetolewa na Afisa Mawasiliano mwandamizi wa Hospitali ya Mifupa (MOI) Bi. Mary Ochieng, wakati akitoa maelezo kwa wafanyakazi wa kampuni ya simu ya Halotel walipotembelea wodi za watoto hao pamoja na kutoa misaada ya kijamii, akizungumza na wafanyakazi hao Ochieng, amesema kuwa licha ya Taasisi hiyo kufanya jitihada kubwa za kutoa elimu na kufanya upasuaji kwa watoto hao bure bado kuna baadhi ya wazazi wameendelea na tabia ya kuwaficha watoto wao.

  “Tangu Taasisi yetu ichukue jukumu hili imefanya kazi kubwa sana, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tumeweza kutoa matibabu kwa watoto wengi, ila changamoto kubwa bado inabaki kwa baadhi ya wazazi ambao wanawaficha watoto wao pale inapotokea wakagundua watoto wao wana matatizo ya vichwa vikubwa au mgongo wazi” Alisema nakuongeza.


  0 0
  0 0

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akiwasili katika eneo la Miti mitatu ndani ya Ngorongoro Crater.
  Watangazaji Baby Kabaye na Hassan Ngoma ,wakifanya mahojiano na Naibu Waziri Ramo Makani.
  Mkurugenzi wa Utalii wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Ibrahim Musa (kulia) pamoja na Meneja Mawasiliano wa TANAPA,Pascal Shelutete wakifuatilia kipindi hicho katika eneo la Crater.
  Wananchi wa jamii ya Masai pia walijumika na askari wa Hifadhi hiyo kufuatilia kipindi hicho.
  Mhandisi Ramo Makani akizungumza jambo na viongozi wa TANAPA na Ngorongoro Crater

  0 0

  Na Stella Kalinga, Simiyu

  Serikali mkoani Simiyu imeomba kuwepo kwa kikundi cha ulinzi cha kijeshi katika Wilaya ya Busega ili kusaidia mapambano dhidi ya vitendo vya uhalifu ikiwemo uvuvi haramu na kuwezesha ufugaji wa samaki ndani ya Ziwa Victoria kufanyika kwa usalama.

  Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka wakati wa Hafla ya kumpongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi hapa nchini, Jenerali Venance Mabeyo iliyoandaliwa na ndugu zake kijijini kwao Yitimwila ‘A’ katika Kata ya Kiloleri Wilayani Busega.

  “Tumepata changamoto nyingi sana kwenye ziwa, matukio mengi ya kihalifu liliwemo la uvuvi haramu , sisi kama mkoa tulikuja na wazo kwamba tungehitaji tupate ‘detouch’ moja eneo la Ziwa ili ukanda huu baada ya kufanya kazi kubwa ya kuchoma makokoro ya wananchi, tuwapeleke kwenye uvuvi wa kisasa hususani ufugaji wa samaki ziwani, jambo ambalo Mheshimiwa Rais analipa kipaumbele sana; na namna pekee ya kufanya ufugaji ule wa samaki ziwani, suala la ulinzi na usalama ni muhimu sana; ” alisema Mtaka.

  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo (katikati) akionesha siaha alizokabidhiwa na Wazee wa Busega kama ishara ya ushujaa kwake wakati wa hafla iliyoandaliwa na ndugu zake kijijini kwao Yitimwila A wilayani Busega kumpongeza kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Magufuli.

  Aidha, Mtaka amesema pamoja na kufanya ufugaji wa samaki katika Ziwa Victoria, Serikali ya Mkoa imefanya makubaliano na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF kuwawezesha wananchi wa Busega kufanya kilimo cha Umwagiliaji kwa kutumia maji ya ziwa hilo ambayo ni ya uhakika.

  “Tumeongea na NSSF kwa ajili ya kuanzisha mradi ambao hautazidi bilioni moja, tutaleta mbegu za aina ya nyanya na pilipili zinazotakiwa ili wananchi wa Busega wazalishe kwa wingi. Hatutakuwa tayari kuona wananchi wanalima nyanya na kuuza ndoo moja shilingi 500, tumepanga kuanzisha mradi wa kuzalisha ‘chill sauce’ na ‘tomato source’ .”alisema Mtaka.

  Ameongeza kuwa Wataalam wa Wilaya na Mkoa kwa kushirikiana na Wataalam wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji , Kituo cha Utafiti wa Kilimo Ukiriguru wanafanya upembuzi yakinifu kuona namna miundombinu ya umwagiliaji itakavyojengwa ili kuwawezesha wananchi wa Busega kulima muda wote kupitia kilimo cha Umwagiliaji badala ya kutegemea mvua.
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na viongozi na waalikwa katika hafla ya kumpongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Salvatory Mabeyo, kijijini kwao Yitimwila A wilayani Busega, kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Magufuli kwa nafasi hiyo.

  Mtaka amesema Serikali mkoani Simiyu imedhamiria kuhakikisha katika kipindi cha miaka mitatu ijayo Mkoa hauingizi bidhaa kutoka mikoa mingine na badala yake wananchi wake watazalisha na kutumia bidhaa zao wenyewe, hivyo ameomba Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuona namna ya kuweka vituo vya kuuza zana za kilimo katika maeneo ya kanda ya Ziwa ili wananchi wapate zana bora za kisasa zitakazowasaidia kulima kisasa.

  Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi hapa nchini, Jenerali Venance Mabeyo amewataka wananchi wa Busega kubadili mtazamo wao na kutumia maji ya ziwa Victoria kwa manufaa yao kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji ili wasikumbwe na tatizo la upungufu wa chakula kunapotokea ukame.


  0 0

  Msanii nyota wa filamu Tanzania, Kajala Masanja, kulia akishiriki katika droo ya kwanza ya bahati nasibu ya Ijue Nguvu ya Buku inayoendeshwa na Kampuni ya Biko ambapo ilimpata mshindi wake wa kwanza wa Sh Milioni 10 ambaye ni Christopher Mgaya, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Juhudi Ngolo.

  0 0

  #BMGHabari

  Lile tamasha la burudani la Nyanza Festival 2017, lililopaswa kufanyika hii leo April 16,2017 katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza limeahirishwa kwa kile kinachodaiwa kwamba ni aliyepewa tenda ya muziki kuingia mitini.


  "Taarifa Muhimu, Tamasha la Nyanza Festival limeahirishwa kutokana na sababu zisizozuilika na litafanyika baada ya wiki mbili yaani 29/4/2017". Amebainisha mratibu wa tamasha hilo, Fabian Fanuel.
  Awali Afisa Habari wa Nyanza Festival 2017, George Binagi, alibainisha kwamba zaidi ya wasanii 30 kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa tayari wamethibitisha kupanda jukwaa la Nyanza Festival 2017 hivyo niwasihi wapenzi wa burudani wakae tayari kwa burudani hiyo ambapo kiingilio itakuwa elfu tano tu.
  Nyanza Festival ni tamasha lililoasisiwa na Wanatasnia mbalimbali kutoka Kanda ya Ziwa wakiwemo wanamuziki, watangazaji, waandishi wa habari, Madjz na wadau wengine wengi kupitia umoja wao wa Mwanza.Com chini ya kampuni ya Famara Entertainment, lengo likiwa ni kuukuza na kuuendeleza zaidi muziki wa Kanda ya Ziwa.

  0 0

  Na Mwamvua Mwinyi,Mkuranga

  MKUU wa wilaya ya Mkuranga,mkoani Pwani, Filberto Sanga,ametoa mwezi mmoja kwa vyama vya ushirika vya msingi vya korosho(AMCOS), ambavyo vimehusika kufanya ubadhilifu wa fedha za korosho kwa wanunuzi,kuzirudisha ndani ya muda huo.

  Amesema ameshakubaliana nao na wameahidi kuzirejesha kabla hajawachukulia hatua kali za kisheria. Sanga amechukua hatua hiyo kufuatia mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo,kuvipa wiki mbili vyama hivyo ,kwenda kujieleza kwa wakuu wa zao ikiwemo Rufiji,Kibiti na Mkuranga .

  Akizungumza na baadhi ya wananchi wilayani hapo katika kata ya Msonga,Njianne,kitomondo na Mwarusembe,alisema hujuma hizo hazivumiliki. Aidha Sanga, alisema mfumo wa stakabadhi ghalani ni mfumo wenye tija kwa wakulima hivyo haupaswi kuchezewa. 

  Alitoa rai kwa wakulima wa korosho kuacha kukubali kurubuniwa na madalali ama wanunuzi wachache hali inayosababisha kukosa mapato kulingana na korosho zao. Mkuu huyo wa wilaya ,alikemea tabia ya baadhi ya  watu wanaosafisha mashamba kwa kutumia kuchoma moto.

  Alisema kitendo cha kuchoma moto mashamba kunaharibu mazingira ikiwemo kukata miti ovyo. Katika hatua nyingine, Sanga aliwaasa wananchi,kila familia kulima heka mbili za zao la mhogo. Alihimiza kupanda mazao yanayostahimili ukame na kukomaa haraka ikiwemo mhogo, mtama, viazi vitamu na mikunde.

  Sanga alieleza kwamba, akiwa na timu yake watapita kuhakiki kila familia kama imefuata agizo hilo. 

  0 0

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, waandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama (wa nne kushoto), akimkabidhi Tuzo aliyomtunuku Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Mgeni rasmi wa tamasha hilo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba aliyeipokea kwa niaba yake, wakati wa tamasha hilo.  
  Wachungaji walioohudhuria tamasha hilo, wakimwombea mwimbaji, Solly Mahlangu (chini aliyepiga magoti), kutoka Afrika Kusini, wakati alipotumbuiza kwenye tamasha hilo jana jijini. 
  Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Martha Mwaipaja, akitumbuiza katika tamasha hilo.  
  Mashabiki waliohudhuria katika Tamasha la Pasaka wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitendeka na kupiga picha za selfi, uwanjani hapo. 
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, waandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama (kulia), akiimba sambamba na mwimbaji wa nyimbo za Injili, Martha Mwaipaja, wakati akitumbuiza katika tamasha hilo. 
  Mgeni rasmi wa tamasha hilo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba, akipongezwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto), mara baada ya kumaliza kutoa hotuba yake. Katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, waandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama.


  0 0
 • 04/17/17--12:11: TAARIFA KWA UMMA


 • 0 0

   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongea na wanachama wa tawi la Muungoni mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi ya Tawi la Muungoni lililopo Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja.

   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiondoka eneo inapojengwa shule ya watoto ya awali iliyopo Kajengwa, Makunduchi mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi.
   Sehemu ya wajumbe 535 waliohudhuria mkutano wa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye amehitimisha ziara yake ya kuimarisha chama katika Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja.
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wajumbe wa kamati za siasa kuanzia matawi mpaka mkoa kwenye mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari ya Makunduchi ambapo aliwasihi wazee kutoa elimu kwa vijana katika historia ya Mapinduzi kisha kuwapa nafasi vijana zaidi ambao kasi yao ni ya 4G.
   Vijana wa Makunduchi wakionesha juu picha za Viongozi wao wakati wa ziara ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

   BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI  0 0


  Wakazi wa maeneo ya Mbagala na viunga vyake jana jumapili walipata burundani ya aina yake iliyoongozwa na wasanii kutoka kundi la Wasafi Classic Harmonize pamoja na mwenzake Rich Mavoko. Tamasha hilo lilikuwa ni maalum kwa kutoa elimu kwa wananchi juu uhuru wa kutuma pesa bila mipaka ambao ni muungano wa makampuni matatu ya simu za mikononi kupitia huduma za Airtel Money, Togo Pesa na Ezypesa.

  Mbali na wasanii hao kutoka Wasafi Classic, Young Killer ambaye ni msanii wa hip hop pia alikonga nyoyo za mashabiki wake pale aliponda jukwaani akiwa ni msanii wa mwisho katika tamasha hilo.

  Akiwa na kibao chake cha matatizo, msanii Harmonize alikuwa akilalizimiki kurudia kila wimbo alikuwa akiimba kwa mara tatu kutokana na maombi ya mashabiki ambao walikuwa wamejikoteza kwa wingi.

  Akiongea kwenye tamasha hilo Liginiku Milinga ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Fern Tanzania ambao ndio walikuwa waratibu na waandaaji wa tamasha hilo alisema kutokana na wingi wa mashabiki waliojitokeza, elimu ya uhuru wa kutuma pesa bila mpaka kupitia kampeini ya Taifa Moja limefanikiwa.

  ‘Nia ya kuandaa tamasha hili ilikuwa ni kufika Watanzania wengi. Kama mnavyoona hapa kwa siku ya leo mtakubali kuwa elimu ya uhuru wa kutuma pesa bila mipaka imefanikiwa, alisema Milinga’.

  Watanzania wengi wanapenda burundani, natoa shukrani za dhati kwa wakazi wote wa Dar es Salaam na sana sana Mbagala na viunga vyake kwa kujitokeza kwa wingi na kuja kushuhudia burundani hii licha ya kuwa na hali ya mvua, aliongeza Milinga.

  Milinga aliongeza kuwa kampeini ya Taifa Moja itaendelea nchi nzima kwa matamasha mbali mbali hili kuwafikia Watanzania na kuweza kujikomboa kiuchumi kwa kutumia vyema fursa ya uhuru wa kutuma pesa bila mipaka tofauti na hapo zamani ambapo kulikuwa na changamoto nyingi pale mtumiaji wa mtandao mmoja alikuwa anatuma pesa kwenda kwenye mtandao tofauti.  Msanii wa Bongo Fleva Harmonize akitumbuiza wakati wa tamasha la Taifa Moja lililofanyika Jumapili ya Pasaka kwenye viwanja wa Mbagala Zakhem Jijini Dar es Salaam. Tamasha la Taifa Moja lina lengo ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya fursa ya uhuru wa kutuma pesa bila mipaka. 
  Msanii wa Bongo Fleva Rich Mavoko akitumbuiza wakati wa tamasha la Taifa Moja lililofanyika Jumapili ya Pasaka kwenye viwanja wa Mbagala Zakhem Jijini Dar es Salaam. Tamasha la Taifa Moja lina lengo ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya fursa ya uhuru wa kutuma pesa bila mipaka. 
  Msanii wa Hip Hop Young Killer akitumbuiza wakati wa tamasha la Taifa Moja lililofanyika Jumapili ya Pasaka kwenye viwanja wa Mbagala Zakhem Jijini Dar es Salaam. Tamasha la Taifa Moja lina lengo ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya fursa ya uhuru wa kutuma pesa bila mipaka. 

  0 0

  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu ametembelea na kukagua kivuko cha MV PANGANI II ambacho kinafanyiwa ukarabati na Kampuni ya Songoro Marine Boatyard ya jijini Mwanza katika eneo la Pangani. Awali kivuko hicho kilikuwa kikitoa huduma kati ya Pangani na Bweni kabla ya ujio wa kivuko kipya cha MV TANGA.

  Dkt. Mgwatu amejionea kazi zilizokamilika zikiwa ni pamoja na matengenezo ya milango mipya ya kupandia abiria na magari na sasa kiko katika hatua za mwisho za ukarabati wake. Aidha, Dkt. Mgwatu aliweza pia kusafiri kutoka upande wa Pangani hadi Bweni kwa kutumia boti mpya ya MV BWENI iliyojengwa hivi karibuni kwa ajili ya matumizi ya dharura katika eneo hilo.

  Akiwa katika ukaguzi huo, Dkt. Mgwatu aliambatana na Meneja wa TEMESA Mkoa wa Tanga Mhandisi Margaret Gina, Mkuu wa Kivuko cha Pangani Bw. Abdulrahman Amier pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa TEMESA mkoani Tanga.

  Vile vile, Dkt. Mgwatu alipata wasaa wa kuzungumza na wafanyakazi wa Kivuko cha MV TANGA ambacho kinaendelea kutoa huduma katika eneo hilo na kuwaasa kufanya kazi kwa bidii na weledi na kuhakikisha wanaongeza mapato. Aliwaomba wafanyakazi hao kuitunza boti ya MV BWENI ambayo itatoa huduma za dharura hasa wakati wa usiku kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa na pia kutoa usafiri mbadala pale changamoto mbalimbali zitakapojitokeza.

  Nae Mhandisi Gina alimueleza Dkt. Mgwatu kero mbalimbali wanazokumbana nazo kivukoni hapo ikiwemo kukosekana kwa vyumba vya ofisi kwa ajili ya wafanyakazi na kumuomba awasaidie kupata eneo kwa ajili ya kujenga ofisi. Dkt. Mgwatu alikuwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Tanga.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu katikati akishuka kutoka kwenye chumba cha kuongozea kivuko cha MV Pangani kilichoko Pangani Tanga alipokuwa akikagua maendeleo ya ukarabati wa kivuko hicho. Nyuma yake ni Mkuu wa Kivuko Bw. Abdulrahman Ameir.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu wa pili kulia akikagua Kivuko cha MV Pangani kilichoko Pangani Tanga kinachofanyiwa ukarabati na kampuni ya MS Songoro Marine Boatyard ya jijini Mwanza wakati wa ziara yake mkoani Tanga.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu aliyesimama katikati akisisitiza jambo wakati akizungumza na wafanyakazi wa Kivuko cha MV Tanga kinachoendelea kutoa huduma kati ya Pangani na Bweni mkoani Tanga.


  0 0


  Mwanasheria wa Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake na Watoto (WLAC) Abia Richard, akizungumza wakati wa Tamasha la Vijana la kupinga Ukatili wa Kijinsia lililofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Picha Zote na Nasma Mafoto

  Na Karama Kenyunko

  Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake (WLAC), kimeanzisha bonanza maalum la michezo kwa ajili ya kuhamasisha jamii kupinga ukatili wa kijinsia. Bonanza hilo, limefunguliwa na mratibu wa WLAC, Abia Richard jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Bonanza hilo uliofanyika Mwembe Yanga,Temek, Abia amesema lengo la kuanzishwakwa bonanza hilo ni kutaka kuwaunganisha watanzania kupambana na vitendo hivyo bya ukatili wa kijinsia. 

  Amesema, katika kampeni nyingine ambazo wamekuwa wakiendesha, kundi kubwa ambalo limekuwa likihamasika ni wanawake na wasichana kwa hiyo wanaamini kuanzisha kampeni hiyo kutasaidia kuwahamasisha na wanaume.

  Ameongeza, kati ya kundi linalotajwa katika kutenda vitendo vya ukatili wa kijinsia na wanaume pia wamo, lakini katika kampeni nyingi zinazoendeshwa za kuhamasisha kupambana na vitendo hivi, kundi la wanaume wamekuwa wakijiweka pembeni.

  " Tunaamini katika kampeni hii kupitia bonanza, wanaume watashiriki kwa wingi kwa sababu wanapenda michezo,” amesema Abia.

  Ameongeza kuwa, vitendo vya ukatili wa kijinsia vinapaswa kupambanwa na kila mtu katika jamii kwa kuwa vinaathiri sana jamii yetu. Wanaume hawapaswi kukaa pembeni, tunawaomba kupitia michezo hii nao washiriki kupambana navyo. 

  Katika kampeni hiyo michezo mbalimbali imepangwa, kuwamp ikiwemo ya mpira wa miguu, pete, na mingine mingi, itakayowapa fursa na wanaume kushiriki. Pia alisema wanatarajia kuanzisha timu baina ya madereva wa boda boda, bajaji na za vijana kutoka sehemu mbalimbali kwa ajili ya kuwahamasisha kuelimisha jamii kupinga vitendo hivyo.

  Katika uzinduzi wa kampeni hiyo, timu ya mpira ya wanawake ya Simba gueen na Mburahati queen zote za jijini Dar es Salaam, zilimenyana na kutoka sare ya bila kufungana.
  Wachezaji wa timu za Simba Queens na Mburahati Queens, wakichuana kuwani mpira wakati wa mchezo wao kwenye Bonanza hilo. Katika mchezo huo Mburahati Queens, waliibuka washindi kwa mikwaju ya penati 4-2.
  Viongozi wakikagua timu kabla ya kuanza kwa mtanange wa Soka kwa upande wa wanaume.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Related image
  Na Mwandishi wetu, Vijmambo Blog.
  Kwanza kabisa namshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutujalia siku nyingine tena na nimatumaini yangu upo vizuri tu na mchaka mchaka wa kila siku.

  Leo napenda nizungumze na wewe au nikumegee machache kuhusu uhalisia wa maisha ya ughaibuni ambayo kama leo utabahatika kwenda ughaibuni basi ujue huku ni kazi tu na sio kweli kwamba pesa inadondoka kutoka kwenye mti kama yalivyo mawazo ya vijana wengi wanaokimbilia nje kwa ajili ya kutafuta maisha na baadae maisha yanageukia kuwa majanga.

  Mimi mwenyewe nilikua na mawazo kama ya kwako na ya vijana wengi wanavyofikiria ughaibuni ni kuku tu, ni kweli kwa wakati mwingine ikilinganisha masikini wa Dunia ya kwanza thamani ya maisha ya masikini wa Dunia ya tatu ni tofauti na jambo la kwanza ambalo ndio vijana wengi ulitizama ni mwonekano wa vijana wanaorudi likizo Tanzania akiwa ameng'aa juu mpaka chini kila kitu kipya wala hakijakanyaga vumbi

  Siri kubwa ya nyuma ya pazia vitu hununuliwa mtu anapojiandaa kusafiri kuelekea Tanzania lakini anapokuwepo ughaibuni katika maisha yake ya kila siku mwonekano wake ni mtu wa kawaida hasa katikati za wiki maisha ni ya kawaida sana na hasa kwenye pamba wewe wa Bongo unang'aa zaidi yake. Na hii nazungumzia Mbongo wa ughaibuni wa hali ya kawaida sio mbongo aliyebahatika akaenda shule na kazi yake nzuri ya ofisi.

  Kama kijana ukibahatika kwenda uhgaibuni kwa masomo  au kitu kingine kilichokuleta kwanza jua maisha ya ughaibuni ni mchakamchaka mno, ughaibuni siku, miezi  hadi miaka inakimbia kupita kiasi hii ni kwa sababu maisha ni mbio mbio unakuta mtu anafanyakazi 1- mpaka 4 kutokana na uhitaji wa maisha aliyoyachagua, ukichagua kuishi kifahari maisha yako yatakua ni mateso ya kazi kwa sababu ya uweze kumudu gharama za maisha uliyojichagulia. Kama nilivyosema hapo awali kama umebahatika kuja kwa masomo au chochote kilicho kupeleka tafadhali jikite nacho mara nyingi vijana wengi wameharibu nafasi zao za masomo kutokana na kuhadaika na watu waliokutana nao au kwa lugha nyepesi waliowapokea.

  Kama utapata mwenyeji mzuri atakae kujali atakuongoza vizuri lakini wakati mwingine unakutana na wenyeji wenye roho mbaya wao wameharibikiwa na wao wanataka na wewe uharibikiwe, watu kama hawa wapo sana tu ughaibuni kwa hiyo kabla hujatumbukia kichwa kichwa ongea na watu wawili watatu wengine usikie nao maoni yao ili nayo uyaweke kwenye mizani.

  Dunia ya sasa imebadilika Ugaidi umebadilisha sheria nyingi ughaibuni tafauti na miaka ya iliyopita, maisha yamezidi kuwa magumu tofauti na miaka ya nyuma, ughaibuni ya zamani sio ya sasa kwa hiyo kabla hujasafiri usikurupuke kaa chini ufikirie mara mbili, jitathmini na ujiridhishe angalia maisha uliyonayo nyumbani, jiulize je nina nyumba au pakulala?, je nina gari au nauli ya kwenda kokote nakotaka?, je nina kazi au biashara?, je nina lala njaaa? kama kila kitu hapo na vitu vingine upo powa ughabuni wewe sio kwa kukimbilia labda kama umepata shule kupanua elimu hapo sitakua na kipinganizi na wewe.

  Kwa wadau wa ughaibuni tusiridhike na mafanikio tuliyofikia daima tupende kujiendeleza na hii ipo tangia nyumbani tunarizika sana na maisha tuliyonayo, inabidi tuwe na wivu wa maendeleo. Unaweza kufanyakazi pamoja na makabila mengine wewe utajikuta miaka 10-15 upo pale pale mataifa mengine miaka hiyo aishapanda cheo.Kama kuna uwezekano nenda shule na jiwekee malengo kila baada ya miaka fulani unataka ufike wapi.

   Michongo inapotokea jambo la maendeleo au manufaa ni vizuri kupeana fursa na mwenzako kama mataifa mengine yanavyofanya, hii ni muhimu kwa maendeleo ya familia na jumuiya zetu katika sekta mbalimbali ikiwemo nchi yetu itanufaika.

   Inapotokea majanga ya misiba kwa wale wasiokua na bima, mara nyingi inakua vigumu hasa kama ulikua mtu usiyejichanganya na yote ni kwa sababu kuu moja ya hatujajiandaa kufia ughaibuni kwa sababu tumeweka kwenye fikra zetu tumekuja kuchuma na ipo siku tutarudi nyumbani. Mawazo ni mazuri lakini usisahau dhamana ya maisha yako ameishikilia Mwenyezi Mungu yeye ndiye anayejua kesho utakua wapi, tujitahidi japo uwe na bima ya maisha hii itasaidia kuondoa matatizo kwako na jamii.

  Naona niishie hapo kwa leo tukutane wiki ijayo

  Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Diaspora.

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

  Katika Bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18, Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara imejipanga kujenga Kituo cha Ushonaji chenye lengo la kukuza sekta ya viwanda na kutoa ajira kwa vijana. 

  Mpango huo umebainishwa hivi karibuni na Afisa Vijana wa Halmashauri hiyo, Mwakajila Emmanuel alipokuwa akizungumza katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii juu ya maendeleo ya vijana waliopo katika Mradi wa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi (YEE) unaoratibiwa na Shirika la Plan International. 

  Mwakajila amesema kituo hicho kitachukua vijana mahiri katika ushonaji ambapo asilimia kubwa ya vijana ni wale waliopata mafunzo katika chuo cha VETA chini ya Mradi wa YEE kwani  wengi wao wanafanya  kazi nzuri lakini hawana vitendea kazi wala maeneo ya kufanyia kazi.

  “Kituo hiki kitaajiri vijana wataalam wa ushonaji watakaokua wanashona sare za wanafunzi wa shule zote za Msingi na Sekondari za Wilaya yetu jambo ambalo litasaidia kulinda mzunguko wa fedha za ndani ya Halmashauri yetu badala ya kuzipeleka katika maeneo mengine,” alisema Mwakajila.

  Afisa Vijana huyo ameongeza kuwa ili kuhakikisha jambo hilo linatimia, Halmashauri itatoa agizo kwa Wakuu wa Shule zote kuhakikisha wanaandika jambo hilo katika fomu za kujiunga na shule ili wazazi waweze kufahamu mahali ambapo sare hizo zinapatikana.

  Amefafanua kuwa kazi ya Afisa Vijana ni kuhakikisha changamoto zinazowakabili vijana katika shughuli zao za uzalishaji pamoja na upatikanaji wa huduma stahiki kwa ustawi wao zinatatuliwa.

  Aidha, ametoa rai kwa vijana kutumia fursa za mikopo inayotolewa na Halmashauri ili waweze kuimarisha biashara zinazowasaidia kupata fedha kwa ajili ya kukidhi mahitaji yao mbalimbali.

  Pia ameyaomba mashirika binafsi kuendelea kujitolea kwa wingi kushirikiana na Serikali kusaidia vijana hasa wanaoishi katika mazingira magumu kwani misaada hiyo imekuwa ikiwawezesha vijana kupata mafunzo na ajira kwa ajili ya kuendeleza maisha yao na kusaidia kukuza uchumi wa nchi.

  Mradi huo wa miaka mitatu 2015 hadi 2018 unatekelezwa kwa ushirikiano wa mashirika ya VSO, CCBRT, VETA, UHIKI, CODERT pamoja na Serikali ya Tanzania huku ukiratibiwa na Shirika la Plan International chini ya ufadhili wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU).

  0 0

  Mother & Child Gala inatarajiwa kufanyika April 22, 2017 pale katika ukumbi wa Danken House Mikocheni. Ni Kwa ajili ya Wamama, mama wadogo, Shangazi, walezi Na watoto wa miaka 8-12 wa kike Na wa kiume. Watoto wakianza kupevuka wanapata mabadiliko mbali mbali physically and mentally Na kupitia stage mbali mbali Za mabadiliko hayo. Je Kama mama umesha ongea Na mwanao kuhusu mabadiliko hayo? Je umemtayarishaje mtoto wako kupitia kipindi hiki? Changamoto gani mtoto anazipata kipindi hiki huko shuleni, Kwa marafiki, Kwa familia Na Kwa jamii Kwa ujumla? Vunja ukimya ongea Na mwanao.

  0 0


  0 0

  Mkuu wa Wilaya Morogoro, Regina Chonjo (wa pili kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris W. Mollel (wa pili kulia), baada ya kupokea msaada ya vitanda vitatu vya kujifungulia wakinamama pamoja na mashine maalum za kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati "Njiti" kupumua, Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro. Wengine pichani ni Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Simon Tarimo (kulia), Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt. Ritha Liamue (kushoto), pamoja na Meneja Masoko wa Benki ya CBA, Solomon Kawishe ambao ndio waliofadhili upatikanaji wa vifaa hiyo.
  Mkuu wa Wilaya Morogoro, Regina Chonjo (wa pili kushoto) akikabidhi kwa Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Simon Tarimo (wa tatu kulia) sehemu ya vifaa tiba (vitanda vitatu vya kujufungulia wakina mama pamoja na mashine maalum za kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati "Njiti" kupumua), vilivyotolewa na Taasisi ya Doris Mollel kwa ufadhili wa Benki ya CBA kwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, mwishoni mwa wiki. Wengine pichani kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris W. Mollel, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Morogoro, Dkt. Ritha Liamue, Meneja Masoko wa Benki ya CBA, Solomon Kawishe na kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro, Ruth John.
  Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro, Ruth John, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris W. Mollel pamoja na Meneja Masoko wa Benki ya CBA, Solomon Kawishe wakipanda mti katika eneo la Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, baada ya kukabidhi sehemu ya vifaa tiba (vitanda vitatu vya kujufungulia wakina mama pamoja na mashine maalum za kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati "Njiti" kupumua), vilivyotolewa na Taasisi ya Doris Mollel kwa ufadhili wa Benki ya CBA kwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, mwishoni mwa wiki.
  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris W. Mollel kwa pamoja na Meneja Masoko wa Benki ya CBA, Solomon Kawishe wakimsikiliza mmoja wa wakinamama waliojifungua watoto kabla ya wakati "Njiti" katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, walipotembelea wadi hiyo kutoa zawadi za Sikukuu ya Pasaka kwa wakinamama hao, baada ya kukabidhi sehemu ya vifaa tiba (vitanda vitatu vya kujufungulia wakina mama pamoja na mashine maalum za kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati "Njiti" kupumua), vilivyotolewa na Taasisi ya Doris Mollel kwa ufadhili wa Benki ya CBA kwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, mwishoni mwa wiki.

  0 0

  Wapalestina kila mwaka hunaadhimisha siku ya mateka inapofika tarehe 17 April kila mwaka, kufuatia kupitishwa kwa Azimio la Bunge la Palestina mwaka 1974 katika vikao vyake vya kawaida, kwamba siku ya tarehe 17 April ni siku ya kitaifa ya kuwaenzi mateka na hatua yao ya kujitoa muhanga. Hilo ni kuzingatia kuwa ni siku ya kupangilia mambo muhimu na kuunganisha juhudi mbalimbali, pia ni siku ya kuwakomboa, kuwasaidia na kuunga mkono haki yao ya kuwa huru.

  Aidha ni siku ya kuwakirimu na kusimama nao na hata jamaa zao, kama ilivyokuwa ni siku ya kuwaenzi pia waliopoteza maisha katika juhudi za kitaifa.Tokea siku hiyo imekuwa na inaendelea kuwa siku ya mateka wa kipalestina ni siku rasmi, wanayoadhimisha wapalestina nchini humo na maeneo mengine duniani na kwa namna mbalimbali.
  Suala la mateka linazingatiwa ni miongoni mwa masuala muhimu na yenye uzito mkubwa kwa taifa la Palestina, hilo ni kutokana na ukubwa wa kujitolea muhanga kulikofanywa na mateka wa kipalestina, katika kufanikisha uhuru na ukombozi wa taifa lao la Palestina kutokana uvamizi wa kimabavu wa Israel. Taasisi za mambo ya mateka na wakombozi wa kipalestina, klabu ya mateka na Taasisi kuu ya takwimu, katika ripoti yao ya pamoja ya mwaka huu zimetaja idadi ya wapalestina waliotekwa ambao wapo katika jela za Israel,wanafikia zaidi ya 6500, wakiwemo wanawake 57 na watoto 300.

  Aidha ripoti hiyo ya pamoja, imetaja pia uwepo wa taasisi zinazojihusisha na haki za binaadamu zilizo rasmi, ambazo zimeorodhesha pia zaidi ya mateka laki moja (100,000) tokea mwaka 2000, huku zaidi ya watoto elfu kumi na tano (15,000) walio chini ya umri wa miaka kumi na nane (18), wanawake elfu moja na mia tano (1,500), mawaziri wa zamani na manaibu wao wapatao (70).Kipindi ambacho serikali ya Israel tayari imetoa maazimio zaidi ya elfu ishirini na saba (27,000) ya kukamatwa bila ya tuhuma na kuwekwa ndani bila ya kuhukumiwa.

  Kwa mujibu wa ripoti ya pamoja, wameripotiwa zaidi ya watu milioni moja waliokamatwa, katika kipindi cha uvamizi wa kimabavu tangu kianze mnamo mwaka 1948, ripoti pia ikiongezea kusema kwamba serikali hiyo ya Israeli ilizidisha ukamataji tokea mwezi Oktoba mwaka 2015, ukafikisha zaidi ya watu waliokamatwa Ukingoni mwa Magharibi huku wengi wao wakiwa kutoka Jerusalemu.
  Ripoti pia imetaja kwamba idadi ya mateka wanawake wa kipalestina wamefikia 57 katika jela za Israel,wakiwemo wasichana wanaoongozwa na mkongwe wao aitwae “Lin Jarbuniy” kutoka katika ardhi inayokaliwa kimabavu tangu mwaka 1948, ambae ameachiwa huru siku ya Jumapili ya jana tarehe 16 April 2017. Ripoti imetilia mkazo ya kwamba, serikali ya Israeli imewakamata watoto wa kipalestina zaidi ya mia tatu (300), huku taasisi mbalimbali zikifuatilia aina mbalimbali ya adhabu na mateso yawapatayo watoto hao wakiwa Jela.

  Takwimu zinaonesha kwamba, zaidi ya asilimia themanini (80%) ya mateka wa kipalestina wamekumbana na mateso hayo wakati wa uchunguzi, mateso hayo yamefanywa na wanajeshi waisraeli wanaosimamia uchunguzi huo. Aidha kuna aina mbalimbali ya mateso hayo wanayofanyiwa mateka wa kipalestina katika Jela hizo za Israeli, ikiwemo kuzuiliwa kulala, kuvuliwa nguo wakati wa usiku, kupigwa, kutikiswa na kadhalika ukiacha mateso ya kinafsi na kukamatwa bila ya tuhuma na kuwekwa ndani bila ya kuhukumiwa.

  Hukumu inatolewa bila hata ya kutakiwa kukiri au kuthibitisha kosa, huku ikifikia idadi ya watu mia tano (500), waliokamatwa bila ya tuhuma na kuwekwa ndani bila ya kuhukumiwa. Ukiongezea kitendo cha serikali ya Israeli kubomoa nyumba zaidi ya mia mbili na thelathini (230) za mateka wa kipalestina, kama ni sehemu ya hukumu yao kwa kujiingiza kwao katika mapambano ya kisiasa yanayolenga kuleta ukombozi na uhuru wa nchi yao ya Palestina.

  Aidha wengine wapatao thelathini na tano (35) wametengwa mjini Gaza, huku vikosi vya Israeli vikiwashambulia kinyume cha sheria mateka wengine wa kipalestina zaidi ya elfu moja na mia tano (1,500), baada ya kuwakamata.

  Vile vile wapo mateka wa kipalestina zaidi ya elfu moja (1,000) wanasumbuliwa na magonjwa sugu mbalimbali hawapati matibabu, huku wengine zaidi ya mia moja na themanini (180) wakipoteza maisha tangu mwaka 1967 na familia za kipalestina zaidi ya elfu mbili haziwezi kuwatembelea watoto wao, kwa sababu ya zuio la kijeshi. Aidha mateka wengine wapatao mia tatu na sabini (370), bado wapo katika Jela za Israeli tokea kabla hata makubaliano ya Oslo mwaka 1993, wakiwemo ishirini na moja waliokaa zaidi ya miaka ishirini (20) hawajatoka hadi leo.
  Kwa upande mwingine, kufuata mnasaba huu zaidi ya mateka wa palestina ndani ya Jela za Israeli wametangaza mgomo wa kula, wakitaka kuboreshewa hali ya Jela walipo na hali zao za kibinaadamu. Hatua hiyo ya kutangaza mgomo inakwenda sambambana maadhimisho ya Siku ya Mateka wa kipalestina ambayo ni 17 April kila mwaka.

  Kwa mnasaba huu, Ubalozi wa Palestina nchini Tanzania unatilia mkazo ya kwamba, suala la mateka na wote waliotiwa nguvuni waliopo katika Jela na kambi za Israeli, ni katika masuala muhimu mno yanayoshughulikiwa na utawala wa Palestina, katika ngazi ya kikanda na kimataifa kwa mtazamo wake wa kisiasa, kitaifa na kibinaadamu.

  Jambo ambalo ni wajibu lipewe umuhimu na wote, kufuatia na kugusa suala hilo haki za msingi za binaadamu, zilizodhaminiwa na sheria, kanuni, desturi na mikataba yote ya kimataifa, hasa ule mkataba wa nne wa Geneva unaohusu haki za binaadamu, tangazo la kimataifa la haki za binaadamu na maazimio mengine mengi pia mikataba ya kimataifa ihusuyo suala hili. 

  Ubalozi pia unatilia mkazo ya kwamba, siku ya mateka wa kipalestina imekuja kuukumbusha Ulimwengu mateka hao na wanayokumbana nayo miongoni mwa aina mbalimbali za adhabu na mateso, yanayogusa utukufu wa binaadamu yaliyozidia na  kukiuka mikataba yote ya kimataifa na kibinaadamu,ukiwemo mkataba wa nne wa  Geneva na misingi yote ya haki za binaadamu ambayo nchi zote duniani zimekubaliana kuziheshimu.

  Ubalozi  wa Palestina hapa nchini pia kupitia mnasaba huu, unaziomba jumuiya zote  za kimataifa na taasisi za haki za binaadamu, kuibana serikali ya Israeli iache kuwaadhibu mateka wa kipalestina na hatimae kuwaacha huru.

older | 1 | .... | 1650 | 1651 | (Page 1652) | 1653 | 1654 | .... | 3278 | newer