Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1649 | 1650 | (Page 1651) | 1652 | 1653 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Na Dotto Mwaibale 

  WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amewatangazia kiama watu wote waliohusika kuwaua askari polisi nane Kibiti wilayani Mkuranga mkoani Pwani.

  Akizungumza wakati wa kuaga miili ya askari hao jijini Dar es Salaam leo asubuhi Mwigulu alisema watu hao watakamatwa wote na kufikishwa kwenye mkono wa sheria. "Kitendo hiki cha mauaji kilichofanyika dhidi ya askari wetu hakivumiliki hata kidogo waliohusika tutawatafuta na kuwakamata" alisema Mwigulu.

  Aliwaomba wananchi wa maeneo husika kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuwapata wahusika wa tukio hilo. Katika hatua nyingine Mwigulu ameitaka wizara husika kuhakikisha inatoa fidia kwa ndugu wa askari hao na majeruhi badala ya kuchukua muda mrefu kuitoa. "Naomba fidia kwa askari hawa tuliowapoteza wakitumikia taifa itolewa haraka bila kucheleweshwa" aliongeza Mwigulu.


  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Ernest Mangu alisema watuhumiwa wote waliohusika kufanya mauaji hayo ni lazima watafikiwa na mkono wa dola. Alisema wananchi wa eneo hilo wanawafahamu wahusika hivyo amewaomba washirikiane na polisi ili kuwapata vinginevyo nguvu itatumika.

  Alisema linapotokea tukio kama hilo kuna baadhi ya watu wamekuwa wakishabikia kupitia mitandao ya kijamii hivyo akatoa onyo kuwa watakao bainika na wao watakamatwa kwa kutenda kosa.

  Askari waliopoteza maisha katika tukio hilo la kinyama wametajwa kuwa ni pamoja na Mkaguzi Msaidizi Peter Kiguu, Koplo Francis, PC Haruna, PC Jackson, PC Zakaria, PC Siwale, PC Maswi na PC Ayoub.

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchini, Mwigulu Nchemba, akitoa heshima za mwisho Dar es Salaam leo mbele ya majeneza yenye miili ya askari nane waliouawa na majambazi Kibiti wilayani Mkuranga mkoani Pwani juzi jioni.Kulia kwake ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Hamad Masauni.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchini, Mwigulu Nchemba, akitoa pole kwa wafiwa.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchini, Mwigulu Nchemba (kulia), akiteta jambo na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu wakati wa kuaga miili hiyo.

  0 0


  Anthony Ishengoma

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa zawadi zenye thamani ya Shilingi milioni 11,782,000/= kwa jumla ya vituo 9 katika Mkoa wa Dar es Salaam, 2 Zanzibar na 21 kutoka kwenye mikoa ya Tanzania Bara kwa ajili sikukuu ya Pasaka .

  Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Mhe. Rais,Kamishna wa Ustawi wa jamii Bw. Rabikira Mushi amesema utoaji wa zawadi hizi umekuwa ni utaratibu wa kawaida kwa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutoa zawadi za vyakula kama vile mchele, mbuzi na mafuta ya kupikia ili kuwawezesha makundi yenye mahitaji maalum kufurahi na kusherehekea sikukuu kama ilivyo kwa watu wengine.

  Akifafanua Mushi amesema Mikoa ingine iliyofaidika na zawadi hizo ni Kilimanjaro, Mbeya, Arusha, Tanga, Shinyanga, Morogoro, Kigoma, Ruvuma, Mara, Kagera, Manyara, Tabora, Lindi Mtwara, Singida, Mwanza, na Pwani.

  Aidha vitu vilivyofaidika na zawaidi hizo kwa mkoa wa Dar es Salaam na Zanzibar ni,Makao ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini,Makao ya Watoto Mburahati,Makao ya Watoto Msimbazi.Makao ya Watoto Kijiji cha Furaha,Makao ya Watoto SOS Children’s Village Tanzania.

  Viuo vingine ni Makao ya Watoto Yatima Group Trust Fund, Temeke.Makao ya Watoto Dar Al Arqum (International Islamic Relief Organization),Mahabusu ya Watoto Dar es Salaam, Upanga,Makazi ya Wazee Wasiojiweza na wenye Ulemavu Nunge Kigamboni.

  Kwa upande wa Zanzibar Bw. Mushi alitaja Vituo vilivyonufaika na zawadi hizo,Kituo cha Watoto Istima - Chakechake, PembaMakazi ya Wazee Wasiojiweza Sebleni – Unguja.

  Aidha kwa Mikoa ya Tanzania Bara jumla ya vituo 21 vimefaidika na zawadi ya Mhe. Rais na baadhi yake ni Mahabusu ya Watoto Moshi,Makazi ya Wazee Wasiojiweza Njoro – Kilimanjaro,Mahabusu ya Watoto Mbeya,Mahabusu ya Watoto Arusha,Mahabusu ya Watoto Tanga,Makao ya Wazee Wasiojiweza Mwanzage Tanga,Makazi ya Wazee Wasiojiweza Misufini Tanga.

  Utoaji wa zawadi umekuwa ni utaratibu wa kawaida wa Waheshimiwa Marais tangu awamu ya kwanza makundi haya maalum yamekuwa yakipatiwa zawadi za vyakula kama vile mchele, mbuzi na mafuta ya kupikia ili kuwawezesha kufurahi na kusherehekea sikukuu kama ilivyo kwa watu wengine.

  Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bw. Rabikira Mushi akikabidhi zawadi za Pasaka kwa niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa sista Stella Selugenge wa Kituo cha Kulelea watoto cha Msimbazi Center leo Jijini Dar es Salaam. 
  Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bw. Rabikira Mushi akikabidhi zawadi za Pasaka kwa niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa Afisa Ustawi wa Jamii wa Mahabusu ya Taifa ya watoto Upanga Bi Isabella Shitindi leo Jijini Dar es Salaam.
  . Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bw. Rabikira Mushi akikabidhi zawadi za Pasaka kwa niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa Bibi Sherry Mavura Mlezi wa kituo cha kulelea watoto cha SOS Children village Cha Ubungo Jijini Dar es Salaam. 
  . Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bw. Rabikira Mushi akikabidhi zawadi za Pasaka kwa niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa Bibi Veronika Msanjila wa Makazi ya Wazee wasiojiweza Nunge leo Jijini Dar es Salaam.

  (Picha zote na Frank Mvungi-Maelezo).

  0 0  0 0


  0 0

  Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), inatarajiwa kukutana Jumanne Aprili 18, 2017 kwa lengo la kupitia uamuzi uliofanywa na Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji Ligi Tanzania maarufu kwa jina la Kamati ya Saa 72.

  Kwa mujibu wa Katiba ya TFF, Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF, ina mamlaka ya kutafsiri sheria na kanuni za mpira wa miguu nchini kama ilivyoainishwa kwenye katiba na sehemu ya utangulizi ya kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. 

  Kamati hiyo inakutana kutokana na ombi la timu ya Kagera Sugar ambayo imeomba kupitiwa upya uamuzi uliofanywa na Kamati ya Saa 72 ambayo kwa mujibu wa kanuni, ilitoa matokeo mapya ya mchezo kati ya timu hiyo na Simba uliofanyika Aprili 2, mwaka huu huko Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera. 

  Katika mchezo huo, Kagera Sugar ilishinda mabao 2-1, lakini Simba ilikata rufaa ikidai kuwa Kagera Sugar ilivunja kanuni ya 37 (4) ya Ligi Kuu ya Vodacom kwa kumchezesha mchezaji Fakhi Mohammed ambaye alidaiwa na Simba kuwa alikuwa na kadi tatu za njano katika mechi tofauti za Liku Kuu ya Vodacom. Hivyo, ikaadhibiwa kwa mujibu wa kanuni ya 37 (37) ambayo ilitoa pointi tatu na magoli matatu kwa Simba.


  0 0


  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wakulima, Wenyeviti wa Vyama vya Msingi na wadau wa zao la tumbaku kwenye ukumbi wa Isike Ngw’ana Kiyungi mjini Tabora Aprili 15, 2017. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na katikati ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Tabora, Hassani wa Kasubi. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wakulima, Wenyeviti wa Vyama vya Msingi na wadau wa zao la tumbaku kwenye ukumbi wa Isike Ngw’ana Kiyungi mjini Tabora Aprili 15, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wakulima, Wenyeviti wa Vyama vya Msingi na wadau wa zao la tumbaku kwenye ukumbi wa Isike Ngw’ana Kiyungi mjini Tabora Aprili 15, 2017. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na katikati ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Tabora, Hassani wa Kasubi.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na wabunge, Mawaziri na viongozi wa mkoa wa Tabora kwenye uwanja wa ndege wa Tabora baada ya kuzungumza na Wakulima, Wenyeviti wa Vyama vya Msingi na wadau wa zao la tumbaku kwenye ukumbi wa Isike Ng’wana Kiyungi mjini Tabora Aprili 15, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo ameweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi magomeni “QUARTERS”, mradi ambao kwa asilimia kubwa unawagusa watanzania wa hali ya chini.
  Aidha Rais Magufuli ameendelea kusisitiza juu ya ahadi aliyoitoa kwa wakazi 644 waliokuwa wakiishi maeneo hayo kupewa nyumba ambapo wataishi bure kwa muda wa miaka mitano.
  Pia, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo (TBA) Msanifu Majengo Elvis Mwakalinga amesema ujenzi wa mradi huo umezingatia miundombinu yote iliyohitajika ambapo itakuwa na sehemu za makazi, biashara, maegesho ya magari na bustani ya kupumzikia.
  Ujenzi wa mradi huo unatarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha mwaka mmoja ambapo ujenzi wake ulianza rasmi Octoba mwaka jana.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi kuashiria kuanza rasmi ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe na viongozi wengine na muwakilishi wa wananchi kuashiria kuanza rasmi ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine na muwakilishi wa wananchi wakishangilia baada ya kukata utepe kuashiria kuanza rasmi ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na muwakilishi wa wananchi wakifunua pazia kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi kuanza rasmi ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo.


  0 0  0 0


  ....Aagiza TCU kutowachagulia Wanafunzi wa Elimu ya Juu Vyuo.

  Na Lilian Lundo na Beatrice Lyimo
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kutowachagulia vyuo wanafunzi wa elimu ya juu na kuwaacha wanafunzi hao kuchagua vyuo wanavyovitaka wenyewe.
  Agizo hilo limetolewa leo, Jijini Dar es Salaam Rais Magufuli alipokuwa akizindua Mabweni mapya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ikiwa ni ahadi yake aliyoitoa Chuoni hapo Juni, mwaka jana.
  “Ninaamini kama wanafunzi wangepewa nafasi ya kuchagua vyuo wanavyovipenda wenyewe, vyuo vya Serikali kama vile Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Chuo Kikuu cha Mzumbe vingekuwa na wanafunzi wengi sana,” alisema Dkt. Magufuli.
  Aliendelea kwa kusema kuwa TCU imekuwa ikiwachagulia wanafunzi vyuo visivyo na sifa na makazi ya wanafunzi hivyo kusababisha wanafunzi hao kusoma katika mazingira magumu na wanapomaliza masomo yao hukosa ajira kutokana na vyuo hivyo kutokuwa na sifa.
  Aidha, Rais Magufuli ameuagiza uongozi wa UDSM kutoza wanafunzi gharama ya shilingi mia tano(500) kama malipo ya makazi ya  mabweni hayo kwa siku badala ya shilingi mia nane(800) inayotozwa kwa mabweni mengine yaliyopo chuoni hapo.
  Alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga kuwekeza katika elimu hivyo itahakikisha wanafunzi nchini wananufaika kwa kupata elimu bora kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu.
  “watanzania walinichagua ili kutatua changamoto zinazowakabili na hivi ndivyo ninavyofanya kutatua changamoto hizo” alisema Rais Magufuli.
  Naye, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amempongeza Rais Magufuli kwa kutoa shilingi bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni hayo ambao kwa kiasi kikubwa yatatatua changamoto ya makazi iliyokuwa ikiwakabili wanafunzi wa chuo hicho.
  Prof. Ndalichako amesema kuwa mabweni hayo yamejengwa kwa kipindi cha miezi 8 ambayo yatachukua wanafunzi 3840.
  Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo cha Kikuu cha Dar es Salaam Prof. Rwekaza Mukandala ametoa rai kwa wanafunzi wa chuo hicho kuhakikisha wanaimarisha usalama katika maeneo ya mabweni hayo na kulinda miundo mbinu yote iliyoweka.
  “Ni lazima mzingatie matumizi sahihi ya kila kifaa kilichofungwa katika majengo haya, majengo haya ni mapya na yamejengwa kwa gharama kubwa kwa lengo la kutusaidia kuondokana na changamato iliyotukabili kwa muda mrefu,” alisema Prof. Mukangala.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Profesa Rwekaza Mukandala wakati akiwasili kuzindua majengo mapya ya mabweni ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam eneo la Mlimani jijini Dar es salaam. Kiushoto ni Mama Janeth Magufuli na kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Elius Mwakalinga. Mabweni hayo yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 3840, yamejengwa chini ya muda wa mwaka mmoja na yamegharimu shilingi bilioni 10.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Profesa Rwekaza Mukandala wakati akiwasili kuzindua majengo mapya ya mabweni ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam eneo la Mlimani jijini Dar es salaam.Mabweni hayo yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 3840, yamejengwa chini ya muda wa mwaka mmoja na yamegharimu shilingi bilioni 10.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya mchoro toka kwa Rais wa Wanafunzi wakati wa sherehe za kuzindua majengo mapya ya mabweni ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam eneo la Mlimani jijini Dar es salaam. . Mabweni hayo yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 3840, yamejengwa chini ya muda wa mwaka mmoja na yamegharimu shilingi bilioni 10.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa sherehe za kuzindua majengo mapya ya mabweni ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam eneo la Mlimani jijini Dar es salaam. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Elius Mwakalinga. Mabweni hayo yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 3840, yamejengwa chini ya muda wa mwaka mmoja na yamegharimu shilingi bilioni 10.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0
 • 04/15/17--13:32: Article 1


 • 0 0


  Wadau wa Kinyerezi Family kiwa sambamba na Watoto wa kituo cha Watoto waishio katika mazingira magumu,New Hope kilichopo Tabata,wakisali kwa pamoja mara baada ya kuwakabidhi Msaada wa vitu mbalimbali,ikiwemo mchele,nyama,sukari,mayai,nguo na vinginevyo,ili  watoto hao nao wapate kusherehekea vyema sikukuu ya Pasaka
    Kinyerezi Family wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watoto wa kituo cha Watoto waishio katika mazingira magumu chaNew Hope kilichopo Tabata,mara baada ya kuwakabidhi msaada wa vitu mbalimbali,ikiwemo mchele,nyama,sukari,mayai,nguo na vinginevyo,ili na watoto hao wapate kusherehekea vyema sikukuu ya Pasaka
  Pichani kushoto ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Kinyerezi Family ,Leo Joseph Manyara na Mdau wakimkabidhi sehemu ya msaada huo Mwanzilishi na Mlezi wa kituo cha New Hope Organizationi,Bi.Consoler Eliya.Kituo hicho kilichopo Tabata,jijini Dar kinalea watoto zaidi ya 150 ambapo kati yao 32 ndio huishi kituoni hapo na wengine huja na kuondoka.
  Wana Kikundi cha Kinyerezi Family wakiwa katika picha ya pamoja na Mama Mwanzilishi na Mlezi wa kituo cha Watoto waishio katika mazingira magumu.Consoler Eliya
  Mwanzilishi na Mlezi wa kituo cha New Hope Organization,Consoler Eliya akiwashukuru wana Kikundi cha Kinyerezi Family kwa kuwakumbuka watu wenye matatizo mbalimbali kikiwemo kituo chake,kwa kuwapatia msaada wa vitu mbalimbali,ili na wao waweze kusherehekea kwa furaha siku ya Pasakam,Concoler amewaomba wana Kikundi hao na wadau wengine mbalimbali kuwa na moyo wa kujitolea katika suala zima la kusaidia jamii zenye matatizo,kwani kwa kufanya hivyo hata Mungu hawaongezea zaidi palipopungua na kuendelea kuwabariki wao na familia zao
  Katibu Msaidizi wa Kikundi cha Kinyerezi Family,Michael Masota akitoa utambulisho na muongozo mfupi mara baada ya kufika kituoni hapo,kushoto ni Mwanzilishi na Mlezi wa kituo hicho cha New Hope,Bi.Consoler Eliya
  Sehemu ya msaada huo wa vitu mbalimbali
  Mmoja wa wajumbe wa Kikundi cha Kinyerezi Family,Bi Lightness Kweka akizungumza machache katika hafla hiyo fupi ya kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali katika kituo hicho cha New Hope


  0 0
  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira,Vijana na wenye ulemavu Antony Mavunde(katikati)akikata utepe kuashiria Uzinduzi rasmi wa duka jipya la VodacomTanzania Plc lililopo eneo la Kizota mjini Dodoma ,kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa kampuni hiyo ,Jacqueline Maturu na kushoto ni Mkuu wa maduka ya rejareja na mauzo wa kampuni hiyo, Brigita Stephen.

  Naibu Waziri wa Kazi Vijana na Ajira,Mh.Antony Mavunde, ameipongeza kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania Plc kwa kuzidi kuimarisha huduma zake mkoani Dodoma hususani kipindi hiki ambacho Serikali imehamishia makao yake mkoani humo na ofisi nyingi za serikali zikiwa zinazidi kuhamia.

  Akizindua duka jipya na la kisasa  la kampuni hiyo eneo la Kizota mwishoni mwa wiki,Mh.Mavunde alisema kuwa serikali inatambua kuwa sekta ya mawasiliano inachochea maendeleo ya nchi haraka ndio maana imekuwa ikifanya jitihada za kuboresha mazingira ya uwekezaji katika sekta hii ili kuwezesha wawekezaji kusambaza huduma za mawasiliano nchini kote,maeneo ya mijini na vijijini.
  Mkuu wa maduka ya rejareja na mauzo wa Vodacom Tanzania PLC ,Brigita Stephen na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa kampuni hiyo ,Jacqueline Maturu wakimshuhudia Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira,Vijana na wenye ulemavu Antony Mavunde(katikati)akikata keki kuashiria Uzinduzi rasmi wa duka jipya la kampuni hiyo mwishoni mwa wiki lililopo eneo la Kizota mjini Dodoma.

  “Nawapongeza Vodacom kwa kuongeza nguvu ya huduma zenu kwa kufungua duka jipya mbali na maduka yaliyopo,hatua hii inadhihirisha kuwa mnaenda sambamba na kasi ya serikali ya awamu ya tano ya kuhamia Dodoma ambapo tayari shughuli nyingi za serikali zinafanyika mjini hapa na idadi ya wakazi inaongezeka hivyo mawasiliano bora yanatakiwa.”Alisema

  Aliwataka wakazi wa Dodoma kuchangamkia fursa  mbalimbali zinazojitokeza  kama vile kutembelea duka  hili jipya la Vodacom kwa aili ya kupata huduma za mawasilaino ikiwemo kujua  huduma za kubadilisha maisha ya wananchi zinazotolewa na kampuni ya Vodacom bila kusahau kujitokeza kununua hisa zake katika mchakato wa kuuza hisa unaoendelea.
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira,Vijana na wenye ulemavu Antony Mavunde katikati akigongesha glasi wenye mvinyo ikiwa ni ishara ya Uzinduzi wa duka jipya la kisasa eneo la kizota mjini Dodoma.

  Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Jacquiline Materu,alisema Vodacom itaendelea kutekeleza dhamira yake ya kurahisisha  mawasiliano na kufanya ubunifu wa kiteknlojia kupitia mtandao wake  lengo kubwa likiwa ni kuwapeleka watanzania katika ulimwengu wa kidijitali.

   “Tutaendelea kushirikianana na serikali ya awamu ya tano kuhakikisha kuwa sekta ya mawasiliano inakua zaidi na inaleta mabadiliko mengi kwenye maisha ya watanzania na nchi nzima kwa ujumla. Vodacom imejikita kwenye kupanua wigo wa mawasiliano kuhakikisha kila mtanzania popote alipo anaweza kuwasiliana kwa bei nafuu, kupitia mtandao bora na wenye huduma zenye uhakika”.Materu

  Kampuni ya Vodacom ambayo ni ya kwanza kuanza mchakato wa kuuza hisa zake katika sekta ya mawasiliano nchini  imekuwa mstari wa mbele kwenye sekta ya mawasiliano kwa kutoa huduma na bidhaa zenye ubunifu na manufaa makubwa kwa jamii, hivyo kuchangia kwa kiasi kukubwa sana kuendeleza sekta hii muhimu kupitia njia mbali mbali kama kutoa ajira, kuchangia pato la taifa, kuchangia maendeleo ya jamii na kuwezesha watanzania wajiendeleze kiuchumi na kijamii kupitia mawasiliano ya bei nafuu.
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira,Vijana na wenye ulemavu Antony Mavunde(katikati)akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC baada ya kuzindua rasmi duka jipya la VodacomTanzania Plc lililopo eneo la Kizota mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.

  0 0


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli katika Ibada ya Pasaka katika wa Kanisa la Afrika Inland Church Pastorate ya Magomeni  Mapipa jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na waumini wa Kanisa hilo la la Afrika Inland Church Pastorate ya Magomeni Mapipa  jijini Dar es Salaam mara baada ya Ibada ya Pasaka.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Baba Askofu wa Kanisa la Afrika Inland Church Pastorate ya Magomeni Askofu Charles Salala mara baada ya kuzungumza Kanisani hapo.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea Sakramenti Takatifu wakati wa ibada ya Pasaka katika Kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam. Ibada hiyo, ambayo imeongozwa na Paroko wa Parokia ya Oysterbay Padre Asis Mendokta, imehudhuriwa pia na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo na waumini wengi wengine.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyekiti wa Paroko ya Oysterbay DktAdelhelm Meru wakisali baada ya kupokea Sakramenti Takatifu wakati wa  ibada ya Pasaka katika Kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam. Ibada hiyo, ambayo imeongozwa na Paroko wa Parokia ya Oysterbay Padre Asis Mendokta, imehudhuriwa pia na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo na waumini wengi wengine.


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  akimuamkia Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo baada ya  ibada ya Pasaka katika Kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam leo Jumapili Aprili 16, 2016. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0  Salaam na HERI YA PASAKA Ndugu
  Kwa niaba ya KC GLOBAL LINKS tunakutakia wewe mteja wetu na familia yako kila la heri katika PASAKA hii.Tunaamini siku ya leo ni furaha tupu kwetu sote. Kubwa la leo tunakukumbusha kuwa KC bei zetu ni nafuu na sasa tumeboresha huduma zetu. Mizigo yote kwa wakazi wa Dar, Mwanza, Arusha na kule wa akina Asajile Mwaijumba tunaifikisha mpaka nyumbani kwako.

  Mzigo kwa meli kutoka London mpaka mikononi mwako ni £1.60 inclusive clearance na sasa ni wiki tano.  
  Mzigo kwa ndege kutoka London mpaka mikononi mwako ni £3.99 inclusive clearance na sasa ni siku tano tu

  Any car to Mombasa £900
  Saloon Car to Dar £650
  4x4 cars to Dar £800
  DHL from anywhere in UK to anywhere in Africa £25
  Kwa wateja wetu kutuma dawa kwa wagonjwa ni bure.

  TUWASILIANE:
  KC GLOBAL LINKS LTD
  SUITE 2 CLIPPER HOUSE
  TILBURY PORT
  RM18 7SG

  TEL: +447903828119
  OFFICE: +441375858525
  KC TEAM....!

  0 0

   Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi wa CCM Wilaya ya Kati na wa  Mkoa wa Kusini Unguja alipowasili  kwenye ofisi za CCM za Wilaya ya Kati

  Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wajumbe wa kamati za Siasa Tawi , wilaya na mkoa kwenye ukumbi wa TC Dunga, wilaya ya Kati mkoa wa Kusini Unguja.

  Kwenye mkutano huo uliohudhuriwa na wajumbe 590 uliofanyika kwenye ukumbi wa TC Dunga , Mhe. Samia aliwataka wana CCM kukiimarisha chama katika mkoa wa Kusini Unguja , aliwaambia wajumbe hao kuwa CCMsi kadi CCM ni Itikadi, ambapo aliahidi kutoa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha mafunzo ya itikadi mara baada ya chaguzi ndani ya chama kukamilika.

  Alihimiza Vijana waambiwe mambo mazuri ya CCM  alisema  "CCM peke yake, ndio penye misingi,penye historia, na penye Malengo" na kutaka wananchi hao kuunga mkono juhudi na jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein katika kuleta maendeleo nchini.

  Mhe. Samia pia alihimiza Makatibu kufanya kazi zao hasa katika kutoa taarifa sahihi za masuala ya uchaguzi badala ya kubeba watu na alizitaka Jumuiya kufanya kazi zake kwa mujibu wa kanuni na utaratibu.

  Aidha wakati wa kumkaribisha Mhe. Samia , Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Dkt. Abdalla Juma Mabodi alisema Wazanzibar wapuuze porojo za wanasiasa waliopoteza muelekea kwani hata Jumuiya za Kimataifa zinaelewa CCM ndio inayotawala kwa mujibu wa Sheria na Katiba na aliahidi kufanya kazi zaidi na mashina.   Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Dkt. Abdalla Juma Mabodi akihutubia kabla ya kumkaribisha Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa , Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye ukumbi wa TC Dunga wilaya ya Kati mkoa wa Kusini Unguja.
   BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI  0 0

  VIDEO: Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo(juu) na Baba Askofu wa Kanisa la Afrika Inland Church Pastorate ya Magomeni Askofu Charles Salala (chini) wakimuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya Ibada ya Pasaka katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay na  Magomeni jijini Dar es Salaam leo
   Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo  akimuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli baada ya ibada ya Pasaka katika Kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam leo Jumapili Aprili 16, 2017.
  PICHA NA IKULU

  0 0


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Mh Amos Makalla ameupokea Mwenge wa Uhuru kutoka mkoa wa Songwe mapema jana,jijini humo huku vifijo na nderemo za kuwasili mwenge huo vikiwa vimeshamiri,Hafla ya kuupokea Mwenge huo imefanyika Wilayani Chunya April 16,2017.Mwenge huo ukiwa mkoani Mbeya utakimbizwa katika halmashauri saba,ambapo utafanya kazi ya kukagua,kuzindua na kuweka Mawe ya Msingi miradi mbalimbali yenye thamani ya shilingi Bilioni 10.8
   Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh.Amos Makalla akiupokea Mwenge wa Uhuru wilayani Chunya mkoani Mbeya sambamba na kula kiapo cha kuukimbiza mwenge huo katika halmashauri zote za mkoa  wa Mbeya.
   Baadhi ya makamanda wa jeshi la Polisi ambao pia ni miongoni Mwa wakimbiza mwenge wa Uhuru uliowasali hapo mkoani Mbeya
   Baadhi ya wanachama na Wafuasi wa Chama cha Mapindizi (CCM) sambamba na viongozi wa chama wakisherehekea mapokezi ya Mwenge huo wa Uhuru ulio wasili  jana April 16,2017 mkoani Mbeya na kupokelewa na mkuu wa Mkoa wa  Mbeya Mh.Amos makalla 

older | 1 | .... | 1649 | 1650 | (Page 1651) | 1652 | 1653 | .... | 3285 | newer