Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1648 | 1649 | (Page 1650) | 1651 | 1652 | .... | 3278 | newer

  0 0


  0 0


  Waziri Charles Mwijage akizungumza na wadau wa Sekta Binafsi katika Mkutano maalum kati ya Sekta hiyo na Serikali.Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilikutana na wadau wa Sekta Binafsi mapema wiki hii katika mkutano maalum ulioandaliwa na Chemba ya Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo nchini (TCCIA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF).
  Kutoka kushoto ni Godfrey Simbeye, Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Gotfrid Muganda Mkurugenzi Mtendaji TCCIA, Octavian Mshiu, Makamu wa Rais TCCIA ambao ni waandaaji wa Mkutano huo maalum baina ya Serikali na Sekta Binafsi wakiwa na Hussein Kamote, Mkurugenzi wa Huduma na Uanachama-CTI.Lengo la mkutano huo maalum baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi ulikuwa na lengo la kuboresha mazingira ya biashara nchini, kukuza ushirikiano kati ya Serikali na Sekta Binafsi pamoja na kuongeza njia za kukuza uchumi utakaochochea ya azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda.
  Mkutano huo uliofanyika mjini Dodoma katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango (Treasury Square) uliongozwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji (MB) Mh. Charles Mwijage pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango (MB), Mh. Dkt. Philip Mpango na kuhudhuriwa na wabunge, makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu, Kamishna wa TRA, Mwenyekiti wa TPSF Makamu wa Rais- viwanda wa TCCIA, Mwenyekiti wa TRADEMARK EAST AFRICA, Wafanyabiashara wa Sekta mbalimbali nchini na wawekezaji, viongozi wa ACT, ATE, MOAT, TASOA pamoja na wajumbe wedau wengine wa biashara.
  Makamu wa Rais Sekta ya Viwanda TCCIA Octavian Mshiu akizungumza jambo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage (MB) katika Mkutano huo. 
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage (MB) kushoto, akifurahia jambo na Mwenyekiti wa TPSF Bw. Reginald Mengi kulia, anayeshuhudia ni Waziri wa Fedha na Mipango Mh. Philip Mpango (MB). 
  Mkutano huo uliipa Serikali fursa ya kusikiliza changamoto zinazoikabili Sekta Binafsi na kukusanya maoni ya wadau wa sekta hiyo na kuahidi kuzifanyia kazi na kuzitatua ili kuweza kuimarisha mahusiano, umoja, mshikamano, ushiriakiano na uaminifu baina ya sekta hizi muhimu katika uchumi wa taifa la Tanzania.
  Akizungumza katika Mkutano huo, Waziri Mwijage aliwashukuru wadau wa Sekta Binafsi kwa kujitokeza kwa wingi ili kuzungumza na Serikali na kuwa njia hii ya kukutana kwa vile imeonekana kuwa njema basi itaendelea kutumika ili kuhakikisha sekta hizi zinakutana mara kwa mara. Waziri aliahidi kushughulikia kero zinazokabili mazingira ya biashara kama kuwepo kwa kodi na kuahidi upunguzwaji wa kodi utitiri ambazo zimekuwa kero kwa wafanyabiashara na pia kuweka mazingira rafiki baina ya Sekta Binafsi na Serikali. 
  Kwa upande wake Waziri Mpango alisema, “Tulipofikiria wazo hili hatukutegemea muitikio huu na kwamba ni utaratibu muafaka na napendekeza kwa kuanzia tuendeleze huu utaratibu na tukutane angalau mara moja katika kila robo ya mwaka, asanteni sana. Mmeipongeza serikali na hata mmetuelezea changamoto ambazo ni za msingi sana, mmeifanya siku hii kuwa na thamani kubwa katika kujenga Tanzania mpya”. 
  Waziri Philip Mpango akizungumza na wadau wa Sekta Binafsi katika Mkutano maalum kati ya Sekta hiyo na Serikali.
  Maofisa waandamizi wa Serikali na wadau wa Sekta Binafsi wakifatilia mazungumzo katika Mkutano maalum baina ya Serikali na Sekta Binafsi uliofanyika mjini Dodoma wiki hii.

  0 0

  Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke amesema nchi yake ipo tayari kuisaidia Tanzania katika kutoa mafunzo maalum ya Menejimenti ya Maafa kwa wataalamu wetu.

  Ameyasema hayo hivi karibuni wakati alipomtembelea Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama ofisini kwake mjini Dodoma.

  Akielezea lengo la ziara hiyo, Balozi Cooke alisema Serikali yake inataka kuiunga mkono Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha inajipanga kukabili na kurejesha hali pindi  yanapotokea maafa.

   “Masuala ya maafa yapo nchi nyingi ikiwemo kwetu Uingereza ingawa mafuriko na ajali za moto zimekuwa zikiikumbaa nchi yetu mara kadhaa.”Alisema Balozi.

  Aliongeza kuwa,  Serikali ya Uingereza  imevutiwa na juhudi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania katika kukabili na kurejesha hali ikiwa pamoja na  kuwasaidia wananchi na mali zao pindi yanapotokea maafa.

  Kwa upande wake, Waziri Mhagama alimpongeza Balozi huyo kuona umuhimu wa kuja Tanzania na kuonesha nia ya kuisaidia nchi kwa namna mbalimbali.

  “Nishukuru kipekee kwa ujio wako na kuona umuhimu wa kuunga mkono jitihada za Serikali ya Tanzania katika maswala mazima ya maafa na kumhakikishia kuwa Tanzania ipo tayari na itajiandaa kuwaunga mkono kwa utayari wa kuisaidia nchi”Alisema waziri Mhagama.

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Balozi wa Uingereza Nchini Mhe.Sarah Cooke alipomtembelea waziri Ofisini kwake Bungeni Dodoma 
   Balozi wa Uingereza Nchini Mhe.Sarah Cooke akiongea jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipomtembelea Ofisini kwake Bungeni Dodoma.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiteta jambo na Balozi wa Uingereza Nchini Mhe.Sarah Cooke alimtembelea Ofisini kwake Bungeni Dodoma.

  0 0  0 0


  0 0  0 0  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  KLABU ya Soka ya Kagera imeaiandikia barua Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) kulalamikia maamuzi yaliyotolewa na kamati ya saa 72 kwa kuipatia pointi tatu timu ya Simba ikidaiwa wamemchezesha mchezaji mwenye kadi tatu za njano.

  Braua hiyo iliyopelekwa moja kwa moja kwa Mtendaji Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa imeandikwa na Mwenyekiti wa klabu hiyo  Hamis Mdaki na kuelekeza malalamiko yao ya kutokubaliana na maamuzi ya kamati ya saa 72.

  Hukumu ya kuipatia Simba alama hizo ilitoka jana usiku naada ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Mohamed Yahya  alitoa maamuzii hayo mbele ya waandishi wa habari na kusema kuwa kamati imethibitisha kuwa Mchezaji Mohamed Fakhi alikuwa na kadi tatu za njano alizozipata katika michezo dhidi ya Prisons, Majimaji na African Lyon.

  Hukumu hiyo imeonekana kutokukubalika kwani kamati ilishindwa kupitia ripoti za waamuzi baada ya kuonekana kutofautiana baina ya mwamuzi na kamisaa wa mchezo na kuamua kuwaita waamuzi waje kuthibitisha kama ni kweli Fakhi alipewa kadi ya njano.

  Kagera wamemtaka katibu mkuu kuiangalia upya hukumu hiyo kwani wana uhakika kuwa Fakhi alikuwa na kadi mbili za njano na sio tatu kama wanazodai Simba. Katika mchezo huo wa Kagera walifanikiwa kutoka na ushindi wa goli 2-1 dhid ya Simba uliochezwa kwenye dimba la Uwanja wa Kaitaba Mkoani Kagera.

  Baaada ya maamuzi hayo Simba wamejikita kileleni zaidi wakiwa na alama 61 wakifuatiwa na Yanga wenye alama 56.


  0 0

  mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Ruvuma ABEL SWAI atoa Mambo mawili ya kuzingatia kuelekea sikukuu ya pasaka kwa madereva wa vyombo vya moto na wazazi kwa watoto wao.

  0 0


  0 0


  Ofisi ya Rais TAMISEMI na baadhi ya wabunge wameongoza vikundi vya Jogging Mkoani Dodoma kufanya mazoezi kuunga mkono agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Sluhu Hassan wa kufanya mazoezi.


  Akizungumza baada ya mazoezi hayo Afisa Tawala kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bibi Rose Lugendo amewaomba wakazi wa Dodoma wajitokeze kwa wingi kufanya mazoezi kwa afya zao na kuimarisha mahusiano baina yao.

  “Napenda kuwashauri wakazi wa Dodoma kujiunga na Jogging Clubs na kuwa na Utamaduni wa kufanya mazoezi kwa Afya zao” alisisitiza Bibi Rose.

  Kwa upande wake Mbunge Wa Mtera Mhe. Livingstone Lusinde amewaasa vijana kujitokeza kufanya mazoezi kila siku na sio kusubiri kufanya mazoezi mara moja kwa mwezi kwasababu mazoezi ni sehemu ya maisha.

  “Vijana tumieni fursa hii kufanya mazoezi na kujenga afya zenu mazoezi yawe sehemu ya maisha yenu” alisisitiza Mhe. Lusinde.

  Naye Mbunge wa Buyungu Mhe. Kasuku Bilago amevipongeza vikundi vya Jogging Dodoma kwa kuleta mwamko wa mazoezi katika mkoa wao na kujenga desturi ya watu kupenda mazoezi na michezo.

  Aidha Mkuu wa Polisi Wilaya ya Dodoma Mjini Daniel Shija amewahakikishia ulinzi wanamazoezi na michezo kwa ujumla katika sehemu mbalimblai ambazo watakuwa wanafanya michezo.


   

  Mbunge wa Buyungu Mhe. Kasuku Bilago(kushoto) Mbunge wa Kiwani (Zanzibar) Mhe. Abdalla Haji Ali (kulia) wakifanya mazoezi ya viungo katika katika viwanja vya Kilimani Club Mjini Dodoma ikiwa ni kuunga mkono wito wa Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan wa kufanya mazoezi.
   Mratibu wa Michezo Kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. Salum Mkuya akizungumza navikundi vua Jogging Club wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika Viwanja vya Kilimani Club Mjini Dodoma.


  0 0
  0 0

  Meneja Mwandamizi Kitengo cha Amana, Bima na Huduma za ziada wa Benki ya NMB, Bw. Stephen Adili (kushoto) akitoa maelezo namna benki hiyo inavyowakumbuka vijana katika bidhaa zao mbalimbali kwa wageni waalikwa, Mkurungenzi Mkuu wa UN CDF Tanzania, Peter Malika (wa kwanza kulia) na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) walipotembelea banda hilo kwenye uzinduzi wa mjadala kujadili changamoto mbalimbali na kuhamasisha vijana nchini kupata uelewa wa masuala ya fedha. Mkurungenzi Mkuu wa UN CDF Tanzania, Peter Malika (kushoto) akimkabidhi Meneja Mwandamizi Kitengo cha Amana, Bima na Huduma za ziada wa Benki ya NMB, Bw. Stephen Adili (kulia) cheti kilichotolewa na UN-CDF Tanzania, kwa NMB kwenye kampeni kuwahamasisha vijana kupata uelewa wa masuala ya fedha wakiwa ndani ya banda la Benki ya NMB kujua huduma anuai zinazotolewa na benki hiyo na kuwagusa vijana. NMB imeshiriki kufanikisha kampeni hizo. Baadhi ya wageni waalikwa katika kongamano la kampeni zilizowakutanisha vijana kujadili changamoto mbalimbali, wakipokea vipeperushi ndani ya banda la NMB kwenye kongamano hilo.


  0 0

  Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bw. Rabikira Mushi akikabidhi zawadi za Pasaka kwa niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa sista Stella Selugenge wa Kituo cha Kulelea watoto cha Msimbazi Center leo Jijini Dar es Salaam.
  Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bw. Rabikira Mushi akikabidhi zawadi za Pasaka kwa niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa Afisa Ustawi wa Jamii wa Mahabusu ya Taifa ya watoto Upanga Bi Isabella Shitindi leo Jijini Dar es Salaam.
  Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bw. Rabikira Mushi akikabidhi zawadi za Pasaka kwa niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa Bibi Sherry Mavura Mlezi wa kituo cha kulelea watoto cha SOS Children village Cha Ubungo Jijini Dar es Salaam.
  Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bw. Rabikira Mushi akikabidhi zawadi za Pasaka kwa niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa Bibi Veronika Msanjila wa Makazi ya Wazee wasiojiweza Nunge leo Jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Frank Mvungi-Maelezo)

  Na Anthony Ishengoma

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa zawadi zenye thamani ya Shilingi milioni 11,782,000/= kwa jumla ya vituo 9 katika Mkoa wa Dar es Salaam, 2 Zanzibar na 21 kutoka kwenye mikoa ya Tanzania Bara kwa ajili sikukuu ya Pasaka .

  Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Mhe. Rais,Kamishna wa Ustawi wa jamii Bw. Rabikira Mushi amesema utoaji wa zawadi hizi umekuwa ni utaratibu wa kawaida kwa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutoa zawadi za vyakula kama vile mchele, mbuzi na mafuta ya kupikia ili kuwawezesha makundi yenye mahitaji maalum kufurahi na kusherehekea sikukuu kama ilivyo kwa watu wengine.

  Akifafanua Mushi amesema Mikoa ingine iliyofaidika na zawadi hizo ni Kilimanjaro, Mbeya, Arusha, Tanga, Shinyanga, Morogoro, Kigoma, Ruvuma, Mara, Kagera, Manyara, Tabora, Lindi Mtwara, Singida, Mwanza, na Pwani. Aidha vitu vilivyofaidika na zawaidi hizo kwa mkoa wa Dar es Salaam na Zanzibar ni,Makao ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini,Makao ya Watoto Mburahati,Makao ya Watoto Msimbazi.Makao ya Watoto Kijiji cha Furaha,Makao ya Watoto SOS Children’s Village Tanzania.

  Viuo vingine ni Makao ya Watoto Yatima Group Trust Fund, Temeke.Makao ya Watoto Dar Al Arqum (International Islamic Relief Organization),Mahabusu ya Watoto Dar es Salaam, Upanga,Makazi ya Wazee Wasiojiweza na wenye Ulemavu Nunge Kigamboni. Kwa upande wa Zanzibar Bw. Mushi alitaja Vituo vilivyonufaika na zawadi hizo,Kituo cha Watoto Istima - Chakechake, PembaMakazi ya Wazee Wasiojiweza Sebleni – Unguja.

  Aidha kwa Mikoa ya Tanzania Bara jumla ya vituo 21 vimefaidika na zawadi ya Mhe. Rais na baadhi yake ni Mahabusu ya Watoto Moshi,Makazi ya Wazee Wasiojiweza Njoro – Kilimanjaro,Mahabusu ya Watoto Mbeya,Mahabusu ya Watoto Arusha,Mahabusu ya Watoto Tanga,Makao ya Wazee Wasiojiweza Mwanzage Tanga,Makazi ya Wazee Wasiojiweza Misufini Tanga.

  Utoaji wa zawadi umekuwa ni utaratibu wa kawaida wa Waheshimiwa Marais tangu awamu ya kwanza makundi haya maalum yamekuwa yakipatiwa zawadi za vyakula kama vile mchele, mbuzi na mafuta ya kupikia ili kuwawezesha kufurahi na kusherehekea sikukuu kama ilivyo kwa watu wengine.

  0 0

  Na Richard Mwaikenda 
  Moto Umeibuka katika duka kubwa la GSM Mall ililopo Barabara ya Nyerere eneo la Mtava, Dar es Salaam. Kwa mujibu wa mashuhuda duka hilo lilianza kuungua majira ya 8:30. Hadi sasa chanzo cha moto huo hakijaweza julikana. 
  Magari ya zimamoto na uokoaji yalijazana eneo hilo kunusuru mali na maisha ya watu waliokuwemo kwenye jengo hilo lenye ghorofa nne.
  Watu wengi wakiwemo wafanyakazi wa duka hilo walionekana walikimbia nje ya duka kuokoa maisha yao. Baadhi yao walitolewa wakiwa mahututi na kukimbizwa hospitali kwa kutumia magari ya polisi.
  Duka hilo kubwa la kisasa lenye yenye aina mbalimbali za bidhaa ni moja kati ya maduka makubwa yaliyopo jijini Dar es Salaam.
  Waokoaji waliokuwepo wamepata wakati mgumu kuzima moto kutokana na giza nene ndani ya jengo lililotawaliwa na wingu kubwa la moshi uliosababishwa na moto huo.
  Waokoaji walijitahidi kupata mwanga kwa kuwasha taa za magari karibu na lango kuu la kuingilia ndani lakini changamoto ilikuwa kubwa kutokana na vikwazo vya giza na moshi mnene.
   Magari ya Zimamoto na Uokoaji yakiwa nje ya Duka kubwa la GSM Mall tayari kuzima moto uliokuwa unaunguza duka hilo katika Barabara ya Nyerere eneo la Mtava, Dar es Salaam. Chanzo cha moto huo hakikuweza kujulikana mara moja. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
   Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo akiwahishwa hospitali.
   Pilikapilika katika lango kuu la kuingilia duka hilo

   Mmoja wa majeruhi akitolewa kwenda kwenye gari ili awahishwe hospitali kwa matibabu
  Wananchi wakishuhudia ajali hiyo ya moto uliokuwa ukiwaka ndani ya jengo hilo.  0 0


  0 0

   Mshindi wa Pikipiki ya Sanmoto katika shindano la Shika Ndinga lililoandaliwa na Efm Radio kwa Wilaya ya Ilala, Jane Honga akinyoosha mkono juu kuonyesha furaha yake baada ya kutangazwa kuwa mshindi katika shindano hilo lililofanyika mchana wa leo katika uwanja wa Shule ya Msingi Tabata, Jijini Dar es salaam.
   Mkuu wa Vipindi wa Redio ya Efm 93.7, Dikson Ponela 'Dizo' akikabidhi mkataba wa pikipiki kwa mshindi wa shindano la shika ndinga Wilaya ya Ilala, Jane Honga.
    Mshindi wa Pikipiki ya Sanmoto katika shindano la Shika Ndinga lililoandaliwa na Efm Radio kwa Wilaya ya Ilala, Jane Honga akitokwa na Machozi ya kutoamini kama yeye ndiye aliyeibuka mshindi katika shindano hilo.
   Mshindi wa Shindano la Shika ndinga ambaye ameweza kujinyakulia pikipiki ya Sanmoto , Amani Juma akishangilia kwa furaha mara baada ya kutangazwa mshindi wa shindano hilo katika Wilaya ya Ilala lililofanyika katika uwanaj wa Tabata shule.


  0 0

   Mwenyekiti wa Bodi ya Parole  Augustino Mrema


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


  Mwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa Bodi ya Parole  Augustino Mrema amesema kuna changamoto nyingi sana katika kuendesha bodi hiyo na kumuomba Rais Dr John Pombe Magufuli  kumwezesha ili atimize majukumu yake.


  Akizungumza  kupitia kipindi maalum cha Radio UFM (ya Azm Tv),Mrema amesema kuwa anaiomba serikali kuiangalia upya bodi hiyo kuhusu hali ya wafungwa nchini na mchakato wa kuwatoa wafungwa walio katika hatua za kisheria za Parole.

  Mrema amesema , anaukumbusha umma kuwa kila mtu ni mfungwa mtarajiwa na serikali haiwezi kufanya mambo yote hivyo watanzania wakiwa na utamaduni wa kuyasaidia magereza yetu itasaidia  kupata angalau virago kwa ajili ya wafungwa. Aliongeza kuwa utaratibu wa Parole ni mchakato unaohitaji gharama hivyo bodi yake inajitahidi kupata fedha ili kufanikisha  majukumu yao.

   Akizungumzia hali ya kisiasa nchini, Mrema amesema kuwa viongozi waliopo madarakani na wale waliomaliza muda wao kufanya kazi pamoja na Rais ikiwemo na kumpa ushauri utakaojenga nchini na sio kumbeza kama watu wanavyofanya.

  Watanzania waache kukosoa kazi za Rais na kuacha kuandika mabaya yake kwani siku hizi mtu akiongelea kitu kibaya ndite anaonekana anafaaa lakini kitu hicho kinajenga taswira mbaya na zaidi hata katika Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere aliongea mambo mazito  lakini hakuna chombo cha habari kilichoandika.

  Mrema  amesema, katika wazalendo wa nchi hii yeye ni mmoja wao kwani anafanya kazi hiyo pasipo kujali mshahara ama posho yoyote pia alitumia nafasi hiyo kumuomba radhi Rais mstaafu wa awamu  ya tatu Mhe Benjamini William Mkapa kwa makosa aliyowahi kumfanyia katika kipindi chake kwa kumsingizia kuwa aliiba Tshs Milioni 900,  akasema ule ulikuwa ni mpango wa makusudi ingawa walipoenda mahakamani alishinda.

  0 0  Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii 

  VIJANA wanaoandaliwa na chuo cha kodi nchini wanatakiwa kuangaliwa kwa jicho pana zaidi kwani hao  ni hazina kwa taifa katika masuala ya kodi na ushuru wa Forodha. 

  Hayo ameyasema leo , Meneja wa Mafunzo na Maendeleo ya Watumishi wa TRA, Yassini Mwita wakati siku ya wanafunzi wa Chuo cha Kodi kilichopo Mwenge jijini Dar es Salaam, amesema kuwa wanafunzi wameonyesha umahiri katika masuala ya kodi ambapo ni hazina ya taifa watapotoka katika chuo hicho.

  Amesema wanafunzi wamewasilisha maada mbalimbali juu ya ukusanyaji wa kodi na forodha kwa kile ambacho walifundishwa darasani na kufanyia kazi kwa mazingira na sheria watakayokutana nayo pindi wanapohitimu katika chuo hicho .

  Mwita amesema wanafunzi hao wakitoka wanaweza kusaidia makampuni juu ya ukokotoaji wa kodi kuliko kampuni ikawa inafanya yenyewe bila kuwa na mtaalamu wa masuala ya kodi.

  Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo cha Kodi, Nadhiru Juma amesema siku ya wanafunzi wa chuo hicho ni muhimu kutokana na wanafunzi kuonyesha uwezo wa darasani na jinsi watavyofanyia kazi kile ambacho wanakisomea.

  Amesema kuwa wanafunzi wameonekana kuiva kwa kile kinachofundishwa katika chuo hicho na kuweza kufanyia kazi kwa weledi taifa lao katika masuala ya kodi na ushuru wa forodha.
  Meneja wa Mafunzo na Maendeleo ya Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Yassini Mwita akizungumza na waandishi habari juu siku ya wanafunzi wa chuo cha kodi wakizungumzia namna ya kuwaandaa wanafunzi hao kuja kuhakikushha wanazisaidia makampuni katika Ukokotoaji wa Kodi leo jijini Dar es Salaam.
  Jaji Mkuu wa Kutoa Alama kwa Wanafunzi wa Chuo Kodi Tanzania , Pili Marwa akizungumza katika siku ya wanafunzi wa Chuo cha Kodi na kuwataka kujiandaa kuja kuisaidia serikali katika ukusanyaji wa kodi na ushuru wa Forodha leo jijini Dar es  Salaam.
  Mwanafunzi wa Chuo cha Kodi , Charloite Adamu akionyesha umahiri wakati wa kuwasilisha mada katika siku ya wanafunzi wa chuo hicho uliondeshwa na Mamlaka na Mapato Tanzania (TRA) leo  jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya wanafunzi wa Chuo cha Kodi wakifatilia maada katika siku ya kodi ya chuo hicho leo jijini Dar es Salaam.


  Afisa Uhusiano wa TRA, Oliver Njunwa akizungumza wakati ushereheshaji wa Siku ya Wanafunzi wa Chuo cha Kodi leo jijini Dar es  Saalaam

  0 0


older | 1 | .... | 1648 | 1649 | (Page 1650) | 1651 | 1652 | .... | 3278 | newer