Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 163 | 164 | (Page 165) | 166 | 167 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Mfalme wa nyimbo za asili nchini Tanzania Costa Siboka akiwa na msanii Atomi Sifa "Senetor" kutoka nchini Kenya anayetamba na wimbo wa Obama wametambiana kuonyeshana umwamba kanda ya ziwa.

  Wasanii hao mwaka jana walikutana mjini Bunda mkoani Mara kila mmoja akiwa na ziara yake mfalme Siboka akidhaminiwa na bia ya Balimi Extra na Konyagi na Atomi Sifa akiwa chini ya udhamini wa bia ya "Senetor" wamekutana tena jana mjini Geita wakiwa katika ziara Atomi Sifa anatarajia kufanya show leo tarehe 15/06/2013 katika uwanja wa Mwaitogole na mfalme Siboka anatarajia kufanya show kubwa mjini Geita tarehe 27/06/2013.

  Wasanii hawa kwa sasa wana washabiki wengi sana ukanda wa Afrika Mashariki na kanda ya ziwa, Atomi Sifa anatamba na wimbo wa Obama, mfalme Siboka anatamba na wimbo wa Ntemelakatoke na Twisile ambazo kwa sasa zimekuwa ni gumzo kwa mashabiki wa muziki huo nchini Tanzania na Kenya . Baada ya ziara hiyo wasanii hao wamekubaliana kufanya nyimbo mbili, kati ya nyimbo hizo mmoja utaitwa Amani yetu ambao wataimba kwa lugha za makabila ya Tanzania na Kenya.

  Mfalme Siboka yuko Kanda ya ziwa katika kusherehekea kundi lake kutimiza miaka mitano na utambulisho wa nyimbo zake mpya, Siboka atafanya show mjini Geita, Ukerewe, Kisiwa cha Ghana na kisiwa cha Ukara kwa udhamini wa KONYAGI, BALIMI EXTRA na CXC Afrika.

  0 0

  Mshindi wa taji la Redds Miss Kanda ya Kati Happiness Watimanywa (Katikati) akiwa na nyuso ya furaha mara baada ya kamati ya majaji kumtangaza mshindi katika kinyanganyiro kilichoshirikisha walimbwendwe 12 kutoka Mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora na Kigoma Wa Kwa Kwanza kulia Ni Mshindi wa Tatu Jackline huku Mshindi wa Pili ni  ( Wa kwanza Kushoto) Sabrina Juma Kutoka Mkoani Tabora
  Jaji Mkuu wa Shindano la Kumsaka Mlimbwende wa Kanda ya Kati Mh Hashim Lundenga Akipungia mikono watanzania waliofika kushuhudia mlimbwende wa Kanda ya kati anapatikana.
   Walimbwende walioingia hatua Ya Tano Bora
  Mratibu na mwandaaji wa Redds Miss Kanda ya Kati akitoa Maneno huku pembeni yake ni Mgeni Rasmi (katikati) Mh John Komba akiwa na baadhi ya wabunge wenzake kutoka Zanzibar
  Mmoja wa mashabiki wakimtunza Mwanamziki wa Kizazi kipya Amin wakati alipokuwa akitoa Burudani Jana katika Kinyanganyiro Cha Kumtafuta Mlimbwende wa Kanda ya Kati.Picha Na Josephat Lukaza Wa Lukaza Blog

  0 0

  Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika Mark Simmonds jijini London Uingereza leo(picha na Freddy Maro).

  0 0


  Mwanamuziki Jady Jay Dee akionyesha umahiri wake wa kulishambilia jukwaa wakati wa show yake ya kutimiza miaka 13 katika Muziki iliyofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Nyumbani Lounge,Namanga jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbali mbali.
  Ilikuwa ni shangwe tupu wakati wa show hiyo.
  Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi akiwa stejini kutoa burudani mbele ya Mashabiki Lukuki waliofika Nyumbani Lounge kuona show ya Miaka 13 wa Mwanamuziki Lady Jay Dee.

  KUONA PICHA ZAIDI
  0 0

   Mtanange mkali kati ya timu za Makampuni ya FastJet pamoja na AIM Group ukiendelea kwenye viwanja hivi vya Posta,Kijitonyamana jijini Dar es Salaam hivi sasa ikiwa ni sehemu ya Bonasha la aina yake la Michezo linalofahamika kama "Castle Lager Soka Fest" chini ya Udhamini Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania kupitia Bia yake ya Castle Lager.Bonanza hili limebamba vilivyo katika viwanja hivi huku Bendi za Twanga Pepeta na Kalunde Band zikiendelea kutoa Burudani.
   Mara nyingi sifa kwa Beki huwa hakuna,kwani hatakiwa kuremba pindi apatapo mpira na hapa ni Beki wa timu ya AIM Group akiondosha hatari langoni mwake.
   Shangwe zikiendelea.
   Wadau wakicheza Game ya Soka walipotembelea kwenye Banda la Castle Lager ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa Bonanza  "Castle Lager Soka Fest" linaloendelea hivi sasa kwenye viwanja vya Posta,Kijitonyama jijini Dar es salaam.
   Mameneja wa Bia za TBL,Toka shoto ni Kabula Nshimo (Meneja wa Bia ya Castle Lage),Pamela Kikuli (Meneja wa Bia ya Ndovu na Castle Lite) pamona na Victoria Kimaro (Meneja wa kinywaji cha Redd's Original).


  0 0

  Na .Tamimimu adam- Jeshi la Polisi ,Moshi

  Mahakama ya hakimu mkazi Moshi, mkoani Kilimanjaro imewahukumu watu watatu kifungo cha miaka 67 jela wakiwemo raia wawili wa Kenya na mwanamke mmoja mtanzania baada ya kupatikana na hatia ya kula njama na kupora shilingi million 239 katika benki ya NMB tawi la Mwanga, Kilimanjaro.

  Uporaji huo ulifanyika julai 11,2007 ambapo watu hao waliiba bunduki aina ya Sub machine gun (SMG) mali ya Jeshi la Polisi nchini, ikiwemo kuuawa kwa askari Polisi Ex- PC Michael Milanzi aliyekuwa lindo.

  Jopo la makakimu watatu wakiongonzwa na Panterine Kente waliwajata washitakiwa hao waliofungwa ni wanaume wawili raia wa Kenya ambao ni Samweli Gitau maarufu kwa jina la Saitoti na Michael Joseph Kimani Pamoja na mwanamke Elizabert Elias marufu kwa jina la bella mkazi wa Kwangulelo mkoani Arusha.

  Katika hukumu hiyo, washitakiwa hao walihukumiwa miaka saba kwa kosa la kwanza ambalo ni kula njama, miaka 30 kila mmoja kwa kosa la uporaji pamoja na mika 30 kwa kosa la wizi wa silaha.

  Hakimu huyo alisema kuwa adhabu hizo zinaenda pamoja hivyo washitakiwa watatumikia kifungo cha miaka 67 jela, mbali na hukumu hiyo mahakama hiyo pia iliwaachia huru ndugu watatu ni ambao ni Devotha Elias Masenza, Ntibasana Elias Masenza na Julian Elias Masenza na mtu mwingine Calist kanje baada ya kutowakuta na hatia katika mashitaka yote matatu.

  Kabla ya kutoa hukumu hiyo , wakili wa Serikali Tamali Mndeme aliomba mahakama kutoa adhabu kali kwa washitakiwa ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye nia kutenda makosa kama hayo.

  0 0

   Mwenyekiti wa Ujoma wa Wanawake Tanzaia (UWT) Sophia Simba akiwalaki Mjumbe wa Kamati Tendaji wa Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO), Jehad Abu Zead na Makamu Mwenyekiti wa POL Tayseer Khalid (mwanaume mwenye miwani) Khalid na ujumbe wake walipowasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo jioni kwa ajili ya sherehe maalum, waliyoandaliwa na UWT kwenye viwanja hivyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Wanne Kushoto ni Katibu Mkuu wa UWT, Amina Makilagi.

   Mwenyekiti wa Ujoma wa Wanawake Tanzaia (UWT) Sophia Simba (wapili kulia), akiwa na  Mjumbe wa Kamati Tendaji wa Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO), Jehad Abu Zead, Makamu Mwenyekiti wa PLO Tayseer Khalid, wakati ujumbe wa chama hicho ulipowasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo jioni kwa ajili ya sherehe maalum, iliyoandaliwa na UWT kwenye viwanja hivyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa UWT, Amina Makilagi 


  0 0


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, marehemu, Timoth Apiyo, aliyefariki dunia nchini Afrika ya Kusini alikokuwa amelazwa kutokana na kusumbuliwa na maradhi. Shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu imefanyika leo Juni 15, 2013 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, na baadaye mwili ulisafirishwa kuelekea Mkoani Mara kwa maziko.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia baada ya kutoa heshima za mwisho mblele ya jeneza lenye mwili wa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, marehemu, Timoth Apiyo, aliyefariki dunia nchini Afrika ya Kusini alikokuwa amelazwa kutokana na kusumbuliwa na maradhi. Shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu imefanyika leo Juni 15, 2013 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, na baadaye mwili ulisafirishwa kuelekea Mkoani Mara kwa maziko.

  Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro, akipita kutoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, marehemu, Timoth Apiyo, aliyefariki dunia nchini Afrika ya Kusini alikokuwa amelazwa kutokana na kusumbuliwa na maradhi. Shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu imefanyika leo Juni 15, 2013 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, na baadaye mwili ulisafirishwa kuelekea Mkoani Mara kwa maziko.
  Makamu wa Rais na Viongozi wengine mbali mbali waliokuwepo kwenye kuaga mwili wa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, marehemu, Timoth Apiyo, aliyefariki dunia nchini Afrika ya Kusini alikokuwa amelazwa kutokana na kusumbuliwa na maradhi. Shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu imefanyika leo Juni 15, 2013 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, na baadaye mwili ulisafirishwa kuelekea Mkoani Mara kwa maziko.
  Viongozi mbali mbali pia walikuwepo.
  Katibu Mkuu Kiongozi,Mh. Balozi Ombeni Sefue akizungumza na waandishi wa habari.Picha na OMR.

  0 0

  TAARIFA ILIYOIFIKIA GLOBU YA JAMII JIONI HII TOKA JIJINI ARUSHA,INAELEZA KUWA KUMETOKEA MLIPUKO KATIKA VIWANJA VYA SOWETO JIJINI HALI NA INAHOFIWA KUWA WATU WAWILI WAMEPOTEZA MAISHA NA WENGINE KADHAA KUJERUHIWA VIBAYA.
  RIPOTA WETU JIJINI HUMO ANASEMA KUWA HALI HIYO ILITOKEA WAKATI WA MKUTANO WA HADHARA ULIOKUWA UKIFANYWA NA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) UKIONGOZWA NA MWENYEKITI WAKE, MH. FREEMAN MBOWE.

  HALI BADO HAIJAKAA SAWA MPAKA SASA NA KUNA GARI LA KUBEBA WAGONJWA LA HOSPITALI YA MOUNT MERU LIMEPASULIWA VIOO NA WAFUASI WA CHAMA HICHO WAKIDAI KUWA LILICHELEWA KUFIKA ENEO LA TUKIO 
  Madaktari wakihudumia majeruhi katika hospitali ya Mount Metu
  Sehemu waliyokuwepo baadhi ya majeruhi katika tukio hilo

  0 0
 • 06/15/13--13:20: Article 14

 • Free social event with free food, drinks and music in MINNESOTA. Limit ya ukumbi ni watu 160, RSVP by sending an email to info@sobernight.com au text the number on the flyer.

  0 0

  Globu ya Jamii na Vijimambo Teams zinawatakia hepi besdei njema  ya siku ya kuzaliwa kwa babu njenje na bibi njenje . Mungu awazidishie uhai.

  0 0


  0 0


  0 0

  Picha hii ya wazee wa kazi, na silaha zao mkononi na mikobani ! Ni wapiganaji wetu...lakini majina yao kama unayajua ?
  andika katika maoni, Lakini silaha zao zinaona mbali.
  Na Desh..Desh.. MSEMAKWELI

  0 0

   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Peter pinda akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi kitabu cha "Sumbawanga Ng'ara" kilichoandikwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya (wa katikati) katika ukumbi wa Dodoma Hoteli Mjini Dodoma, kulia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Sabas Katepa. Kitabu hicho kinaelezea na kutoa muongozo juu ya usafi na uhifadhi wa mazingira katika Manispaa ya Sumbawanga, Mkoa wa Rukwa na taifa kwa ujumla. Kitabu hicho kinauzwa Tsh. 3,500 kwa lengo la kukusanya fedha ya kuchapisha machapisho mengine zaidi.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Peter pinda akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho alitoa wito kwa Uongozi wa Mkoa wa Rukwa kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa mpango waliouanzisha wa Sumbawanga Ng'ara kwa kuweka mikakati na kutengeneza sheria ndogondogo za kusimamia mpango huo.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akisoma hotuba yake ya kumkaribisha Waziri Mkuu kuzindua kitabu cha Sumbawnga Ng'ara ambapo alimshuru kiongozi huyo Mkuu katika nchi kwa kutenga muda wake pamoja na waliohudhuria katika hafla hiyo fupi ya uzinduzi. Zaidi ya vitabu 175 vilinunuliwa baada ya uzinduzi huo.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI


  0 0

  Viongozi wa Wanyarwanda, Waganda na Wakongo Wanaoishi Ubelgiji Wakiwasilisha Ujumbe Maalum kwa Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye tai yenye rangi ya taifa). Viongozi hao wamewasilisha ujumbe wa wenzao 120 walioandamana leo hadi kwenye Ubalozi wa Tanzania Brussels kupongeza na kuunga mkono ushauri uliotolewa na Mhe. Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete wa kushauri Serikali za Rwanda, Uganda na DRC kuzungumza moja kwa moja na wapinzani wao kwa nia ya kupata amani ya kudumu katika eneo la Maziwa Makuu (Great Lakes Region).
  Kiongozi wa Baraza la Taifa la Mabadiliko ya Demokrasia Rwanda (NCDC) Balozi Munyeshyaka Ildephonse akimkabidhi Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye tai yenye rangi ya taifa) ujumbe kwa niaba ya Wanyarwanda, Waganda na Wakongo wanaoishi Ubelgiji ambao wameandamana leo hadi Ubalozi wa Tanzania Ubelgiji kupongeza na kuunga mono ushauri wa Mhe. Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete aliotoa kwa Serikali za Rwanda, Uganda na DRC kuzungumza na wapinzani wao kwa nia ya kupata amani ya kudumu katika ukanda wa Maziwa Makuu. Wanyarwanda, Waganda na Wakongo wapatao 120 wameshiriki katika maandamano hayo.

  0 0

   Wafanyakazi wa Benki ya Barclays wakitoa msaada wa vitu ,mbalimbali katika wodi ya watoto Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, vikiwemo sabuni, vyandaru, miswaki, vinywaji baridi pamoja na dawa za meno, vitu hivyo vimetokana na michango ya wafanyakazi wanawake wa benki hiyo.
   Mwanasheria wa Benki ya Barclays, Farija Ghilas akimkabidhi sehemu ya msaada waliotoa kwa watoto waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam, Sakina Hassani. Vitu hivyo vimetokana na michango ya wafanyakazi wanawake wanaofanyakazi katika benki hivyo. 
   Rahma Said mkazi wa Manzese jijini Dar es Salaam akipokea sehemu ya msaada uliotolewa na wafanyakazi wanawake wa benki ya Barclays wakati walipofika kuwajulia hali wagonjwa waliolazwa katika wodi ya watoto katika hospitali ta Taifa Muhimbili. Vitu vilivyokabidhiwa leo ni pamoja na sabuni, vyandaru, miswaki, vinywaji baridi pamoja na dawa za meno, vitu hivyo vimetokana na michango ya wafanyakazi wanawake wa benki hiyo.
   Mwanasheria wa Benki ya Barclays, Farija Ghilas akimkabidhi sehemu ya msaada waliotoa kwa watoto waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam jana, Sakina Hassani. Vitu vimetokana na michango ya wafanyakazi wanawake wanaofanyakazi katika benki hivyo. 
  Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Barclays, Neema Sengo akizungumza na waandishi wa habari baada kutembelea wodi ya watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam na kwafariji watoto walolazwa katika wodi hiyo na kuwabidhi vitu mbalimbali vikiwemo sabuni, miswaki, vyandarua, mafuta, pamoja na vinywaji baridi kwa watoto waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam, leo. 

  0 0
 • 06/15/13--20:00: Ngoma azipendazo ankal
 • Ngoma ya 'Siku Hazigandi' ya Lady Jay Dee inajieleza yenyewe...

  0 0
 • 06/15/13--22:00: mkataa kwao mtumwa

older | 1 | .... | 163 | 164 | (Page 165) | 166 | 167 | .... | 3270 | newer