Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live

Kilimanjaro wonders hotel at your service in Moshi


BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 13.04.2017

WABUNGE MJINI DODOMA WAHAMASIKA KUNUNUA HISA ZA VODACOM TANZANIA PLC

0
0
 Mkurugenzi Mtendaji  Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao,akitoa semina kwa wabunge kuhusu uuzaji wa hisa za kampuni hiyo, bungeni Dodoma
  Mkurugenzi Mtendaji  Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao, akiendelea kutoa semina kwa wabunge 
 Mkurugenzi  mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao, akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Rais Tamisemi  kuhusu umuhimu wa kununua hisa za kampuni hiyo, mjini Dodoma

 Mkurugenzi  mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao, akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Rais Tamisemi  kuhusu umuhimu wa kununua hisa za kampuni hiyo, mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi, Suleiman Jafo akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Rais Tamisemi  kuhusu umuhimu wa kukunua hisa za kampuni  ya Vodacom Tanzania PLC, mjini Dodoma

 Mkurugenzi  mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao, akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Rais Tamisemi  kuhusu umuhimu wa kununua hisa za kampuni hiyo, mjini Dodoma.

THBUB yalaani mauaji ya Askari Polisi 8 Mkoani Pwani

0
0
Bahame Tom Nyanduga -

Mwenyekiti
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imepokea kwa masikitiko taarifa ya kuuwawa kwa askari wanane (8) wa Jeshi la Polisi, katika tukio lililotekelezwa na watu wasiofahamika jioni ya Aprili 13, 2017 katika kijiji cha Jaribu Mpakani, Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani. 

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inalaani vikali mauaji haya ya kikatili ya askari polisi waliokuwa kazini na wasiokuwa na hatia. Aidha, tunaungana na Watanzania wengine kuwapa pole familia za wafiwa na Jeshi la Polisi kwa ujumla.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa matukio ya mauaji ya askari polisi na wananchi wengine maeneo tofauti Mkoani Pwani tangu mwaka 2015 yamekuwa yakiongezeka na kusababisha uvunjifu wa haki za binadamu, hususan haki ya uhai inayolindwa na Katiba ya nchi, na madhara mengine kwa familia za wahanga, kwa jamii na taifa kwa ujumla. 

Haki ya kuishi kama zilivyo haki nyingine, inalindwa kisheria, na pia inalindwa na mikataba mbalimbali ya kimataifa na kikanda ambayo Tanzania imeridhia. Hakuna mtu anayepaswa kuporwa haki hii ya msingi kiholela. Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) Ibara ya 14, kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata kutoka katika jamii hifadhi ya maisha yake, kwa mujibu wa sheria.

Ikumbukwe kwamba askari polisi wanapokuwa kazini wanatekeleza majukumu muhimu ya kulinda raia na mali zao, kwa hiyo usalama wao unategemewa na Watanzania wote. Yeyote yule anayewaua askari polisi siyo tu anataka kuwachonganisha askari polisi na raia, bali pia anawaweka raia hao katika hofu kubwa ya usalama wao na mali zao.

Hivyo basi, kwa mara nyingine, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inashauri kwamba:

1. Katika kuhakikisha kuwa haki ya kuishi ya askari polisi na wananchi wote inalindwa, Jeshi la Polisi na Serikali kwa ujumla wafanye uchunguzi wa kina ili kubaini sababu za mauaji haya kutokea kwa kujirudia Mkoani Pwani, na kuhakikisha wahusika wote wanapatikana na wanafikishwa kwenye vyombo vya sheria, ili sheria ichukue mkondo wake.

2. Tume inawakumbusha wananchi kuwa vitendo vya ukatili, mauaji, na matendo yote yanayokiuka Sheria yanayofanywa na raia wasio wema ni ukiukwaji wa Sheria, haki za binadamu na misingi ya utawala wa sheira; Hivyo Tume inakemea matendo haya na kutaka yapigwe vita.

3. Aidha, inawataka wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuhakikisha upelelezi wa matukio hayo unakamilika ili hatua za kisheria zichukuliwe kwa watakaobainika kuhusika na matukio haya.


Imetolewa na:

Bahame Tom Nyanduga

Mwenyekiti
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Aprili 14, 2017

WAIMBAJI WA TAMASHA LA PASAKA WAANZA KUWASILI LEO,SOLLY MAHLANGU KUWASILI KESHO JIJINI DAR

0
0
Pichani kulia ni Mwimbaji mahiri wa nyimbo za injili kutoka nchini Kenya,Mercy Masika akiimba moja ya wimbo wake ulioitwa Mkono wa Bwana, mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani),leo mchana,jijini Dar,Mercy tayari amekwisha wasili jijini Dar tayari kutumbuiza katika tamasha la pasaka litakalofanyika April 16,2017 ndani ya Uwanja wa uhuru,ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa mambo ya Ndani Mh.Mwigulu Nchemba.Pichani shoto ni Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions,Alex Msama,ambayo ndio waandaaji wa tamasha hilo.
 Mwimbaji mahiri wa nyimbo za injili kutoka nchini Kenya,Mercy Masika akielezea namna alivyojiandaa kuwakonga mashabiki wake mbalimbali watakaofika katika tamasha la Pasaka hapo Jumapili ndani ya uwanja wa Uhuru,Mercy amesema amejiandaa vyema na amewaomba wapenzi wa Injili wakiwa na familia zao kujitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo adhimu ikiwemo kumtukuza na Kumuabudu Mungu kwa njia ya Uimbaji.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions ,Alex Msama akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo mchana kuelekea kwenye kilele cha tamasha la Pasaka,linalotarajiwa kufanyika jumapili hii April 16,2017,katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar.Msama amesema kuwa kila kitu kimekamilika na Waimbaji watakaotumbuiza katika tamasha hilo wanaendelea kujiandaa vilivyo,na walioko nje ya nchi tayari wameanza kuwasili akiwemo Muimbaji Mercy Masika kutoka nchini Kenya,na kesho wanawasili waimbaji wengine akiwemo muimbaji nyota kutoka Afrika Kusini Solly Mahlangu na skwadi lake.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions ,Alex Msama,Muimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchini Kenya,Mercy Masika na Mdau wa nyimbo za injili wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzungumza na wana habari,mapema leo mchana jijini Dar.

Nakala Nyeti za Mazoezi na Maelekezo ya Uimbaji Bora

WATANZANIA WAISHIO ALGERIA WAUPOKEA MSAFARA WA YANGA KWA SHANGWE

0
0
 Kikosi cha wawakilishi watanzania katika michuano ya kimataifa ya kombe la Shirikisho barani Afrika Yanga wamewasili salama nchini Algerai kwa ajili ya mchezo wao marudiano dhidi ya MC Alger utakaochezwa kesho majira ya saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Katika msafara huo uliiongozwa na Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa umefika salama na ukipokelewa na watanzania wanaoishi nchi Algeria na kufurahishwa na mapokezi hayo na kuahidi ushindi kwa watanzania.
Msafara wa wachezaji hao uliingia kwa mafungu mawili ambapo kundi la kwanza liliwasili likiongozwa na benchi la ufundi la timu hiyo likiwa na kocha Mkuu George Lwandamina huku kurudi la pili likiwasili  na Katibu Mkuu.
Mtanzania Hamis Mwampese anayeishi nchini Algeria amesema kuwa timu ya Algers wameingia uoga hasa baada ya kuona Yanga wamechelewa kuingia nchini humo na zaidi kwa kufanya hivyo wameepusha sana kufanyiwa hujuma na wenyeji wa nchi hiyo.
Yanga wamefikia katika Hotel ya nyota tano inayojulikana kwa jina la Sultan ambapo si mbali sana na Uwanja ulipo utakaochezewa kesho katika mechi hiyo ya marudiano ambapo Yanga wanatakiwa kupata ushindi wa aina yoyote au sare.

Mtanzania Hamis Mwampese akisalimiana na Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa baada ya kuwasili Jijini Algeria  kwa ajili ya mechi ya marudiano ya hatua ya mtaoano wa Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Mc Alger ambapo katika mechi ya awali Yanga walitoka na ushindi wa goli 1-0..

Mtanzania Hamis Mwampese  akiwa katika picha mbalimbali na wachezaji wa timu hiyo baada ya kuwasili nchini Algeria kwa ajili ya mechi ya marudiano ya hatua ya mtaoano wa Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Mc Alger ambapo katika mechi ya awali Yanga walitoka na ushindi wa goli 1-0.

KIPINDI CHA CLOUDS 360 CHARUKA MUBASHARA KUTOKA NGORONGORO

0
0
Mtangazaji Sam Sasali akifungua kipindi katika eneo la Olduvai Gorge ,kipindi cha 360 kilichokuwa kikirushwa moja kwa moja kutoka Ngorongoro.
Gari maalumu la kurushia matangazo la kituo cha Clouds TV likiwa katka eneo la Bonde la Olduvai Gorge kwa ajili ya kurusha matangazo ya moja kwa moja.
Mtangazaji wa kipindi cha Couds 360 ,Baby Kabaye akifanya mahojiano na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani wakati kipindi hicho kiliporushwa moja kwa moja kutoka Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro.
Mtangazaji wa Sport 360 ,James Tupatupa akifanya mahojiano na moja ya washindi wa nafasi ya kutembelea vivutio vya utalii ,leo katika kipindi cha Clouds 360 kilichorushwa moja kwa moja kutoka Hifadhi ya Ngorongoro.
Mtangazaji wa kipindi cha Clouds 360 Sam Sasali (katikati) akizungumza na moja ya Couple ya washindi waliofanikiwa kupata nafasi ya kutembelea vivutio va utalii leo wakati wa kipindi hicho kiliporushwa moja kwa moja kutoka katika Bonde la Oduvai Gorge lililopo katika Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.





DKT. RWAKATARE ATEULIWA MBUNGE WA VITI MAALUM KUJAZA NAFASI YA SOPHIA SIMBA

EASTER WISHES FROM SPEAKER HON. JOB NDUGAI

ASKOFU DK.ALEX MALASUSA AONGOZA IBADA YA IJUMAA KUU KATIKA KANISA LA KKKT USHARIKA WA AZANIA FRONT JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Muumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Azania Front, Moses Kombe (katikati) na wenzake wakiigiza igizo la kumbukumbu ya kuambwa msalabani kwa Yesu Kristo miaka 2000 iliyopita katika ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika kanisa hilo jijini Dar es Salaam leo jioni.
 Igizo likiendelea.
 Askofu mstaafu Dk. Alex Malasusa akisalimiana na waumini wa kanisa hilo baada ya ibada ya Ijumaa Kuu.
 Muonekano wa waumini wakati wa ibada hiyo.
 Kwaya Kuu ya Ushairika huo ikitoa burudani ya nyimbo za kifo chake Yesu Kristo wakati wa kuhitimisha ibada hiyo.
 Waumini wa kanisa hilo wakiwa nje kwa kuhitimisha ibada hiyo.
Waumini wakitakiana kheri ya Ijumaa Kuu baada ya ibada hiyo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

SHERIA ISEMAVYO KUHUSU HAKI NA WAJIBU WA MMILIKI ARDHI, NA GHARAMA ZA KUKIUKA SHERIA ZA UMILIKI

0
0
Mwananchi yoyote ana haki ya kupatiwa Hatimiliki ambayo ni nyaraka halali ya umiliki wa ardhi baada ya kupata ridhaa ya Kamishna au Kamati na kulipa ada stahili. Hatimiliki hutolewa ndani ya siku 90 mpaka 180 baada ya ridhaa husika. 
Katika fungu la 32 la Sheria ya Ardhi ya namba 4 ya mwaka 1999, masharti ya umiliki wa ardhi yanaainishwa kuwa ni ya aina tatu, ambayo ni; Umiliki wa miaka 33, umiliki wa miaka 66 na umiliki ulio mkubwa zaidi ni wa miaka 99. 
Aidha, katika fungu la 33 la Sheria ya Ardhi ya namba 4 ya mwaka 1999, inaeleza sharti la mmiliki wa ardhi katika kutoa malipo ya pango la Ardhi kwa kila mwaka wa fedha unapoanza. 
Mwananchi hana budi kutimiza masharti ya ulipaji kodi ya pango la Ardhi kwa wakati. Mwananchi anapokiuka sharti hili; fungu la 49 – 50 la Sheria ya Ardhi ya namba 4 ya mwaka 1999 inaeleza gharama zake ni pamoja na kutozwa tozo au riba, Kupelekwa Mahakamani na Kufutiwa umiliki wa ardhi. 
 Mwananchi zingatia ulipaji wa Kodi la Pango la Ardhi, kutimiza wajibu wako, kuondoa usumbufu na kuongeza pato la Taifa Letu. Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mwanasheria Rachel Kilasi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , akifafanua sheria ya Ardhi na. 4 ya mwaka 1999 sambamba na Umiliki wa Ardhi (Haki, Wajibu na uzingatiaji wa ulipaji wa Pango la Kodi ya Ardhi kwa Mmiliki). 

WANACHAMA WA GIRL GUIDE RUVUMA WAPEWA ELIMU YA USTADI WA MAISHA NA ATHARI ZA KUFANYA NGONO KATIKA UMRI MDOGO

0
0
Twendeni tukajenge taifa serikali GIRL GUIDE maua chanua kauli mbiu ya wimbo wa kundi la wanafunzi toka chama cha girls guide hapa mkoani Ruvuma waliopata elimu jinsi ya kujikinga na maradhi na stadi ya maisha elimu iliyotolewa na walimu kutoka shule ya sekondari MFARANAYAKI

RTO RUVUMA - WATAKAO PANDISHA NAULI KUELEKEA SIKUKUU KUKIONA

0
0
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Ruvuma ABEL SWAI atoa Mambo mawili ya kuzingatia kuelekea sikukuu ya pasaka kwa madereva wa vyombo vya moto na wazazi kwa watoto wao.

HAKUNA VIKWAZO TENA TAMASHA LA "NYANZA FESTIVAL" JIJINI MWANZA

0
0
Baadhi ya wadau wanaosaidia kufanikiwa kwa Tamasha la Nyanza Festival 2017 ni SBL-Pepsi, Delta Media Studios, Kali Boy Music, Lake Fm, Passion Fm, Metro Fm, City F, Barmedas Tv, Binagi Blog-BMG, Tanzania Bloggers Network-TBN na Tamara Entertainment.

BMGHabari
Hatimaye uongozi wa Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza, umethibitisha kwamba tamasha la burudani la Nyanza Festival 2017 litafanyika katika uwanja huo kama ilivyokusudiwa.
Meneja wa uwanja huo, Steven Shija, ameyathibitisha hayo baada ya kutokea figisu figisu kwamba siku ya tamasha hilo kutakuwa na mchezo wa soka wa Ligi Kuu nchini na hivyo kusababisha tamasha hilo kutofanyika.

"Ndugu Wasanii na Waandaaji wa Nyanza Festival napenda kuwajulisha kuwa ratiba ya Tamasha ipo pale pale hakuna kitakachoiathiri, tunasimamia utaratibu na misingi ya haki kwa tunaowahudumia. Nawatakia maandalizi mema ya Tamasha lenu". Amebainisha Shija.
Tamasha la kwanza na la aina yake kuwahi kufanyika Jijini Mwanza la Nyanza Festival 2017, litafanyika wikendi hii April 15 na 16 kwa kiingilio cha 5,000 tu ambapo wasanii zaidi ya 30 watapanda jukwaani.
Kumbuka Nyanza Festival ni tamasha lililoasisiwa na Wanatasnia mbalimbali kutoka Kanda ya Ziwa wakiwemo wanamuziki, watangazaji, waandishi wa habari, Madjz na wadau wengine wengi kupitia umoja wao wa Mwanza.Com chini ya kampuni ya Famara Entertainment, lengo likiwa ni kuukuza na kuuendeleza zaidi muziki wa Kanda ya Ziwa.

JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 167

MAAFISA UGAVI KUWENI NA MASHAMBA YA MFANO ILI WAKULIMA WAIGE

0
0
Mkurugezi wa halimashauri ya wilaya namtumbo mkoani Ruvuma MARCO KILUNGU amewaagiza maafisa ugavi wa vijiji hadi wilaya, kuwa na mfano wa shamba darasa ili kuongeza amasa kwa wananchi badala ya kupiga morojo mtaani.

WANAFUNZI WA DARASA LA TATU WA SHULE YA MSINGI YA AGA KHAN WATEMBELEA AIRTEL

0
0
Mkurugenzi wa Raslimali Watu wa Airtel Tanzania, Patrick Foya akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Aga Khan, waliofanya ziara ya mafunzo katika makao makuu  ya Airtel eneo la Morocco, jijini Dar es Salaam.
 Afisa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Stephen Makongoro akifafanua jambo Wanafunzi wa Shule ya Msingi Aga Khan waliofanya ziara ya mafunzo katika makao makuu ya Airtel eneo la Morocco, jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari wa Airtel Tanzania, Franky Filman akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Aga Khan waliofanya ziara ya mafunzo katika makao makuu ya Airtel eneo la Morocco, jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Aga Khan  wakiangalia bidhaa mbalimbali katika duka la kisasa la Airtel lilipo makao makuu ya Airtel eneo la Morocco, jijini Dar es Salaam
Maafisa wa Airtel wakiwa katika picha ya pamoja na Walimu na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Aga Khan waliofanya ziara ya mafunzo katika makao makuu ya Airtel eneo la Morocco, jijini Dar es Salaam

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba atembelea eneo walipouwawa askari polisi nane

Viewing all 109607 articles
Browse latest View live




Latest Images