Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

MAKALA YA KUMBUKIZI LA KUZALIWA MWALIMU NYERERE

0
0

Na Judith Mhina-MAELEZO

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ulikuja hapa duniani Aprili 13, 1922 kupitia kwa Mpendwa Marehemu Bibi Mgaya wa Buritho kama zawadi kwa nchi ya Tanzania.

Mwalimu tunamshukuru Mungu kwa kutupa wewe ambaye umeitendea mambo makubwa Tanzania, Afrika na Dunia kwa ujumla.

Mwalimu wakati nakumbuka kuzaliwa kwako nimepata fursa ya kuangalia kazi ulizozifanya mara baada ya kuacha madaraka ya Urais na kujikita katika kazi kuu tano; Mosi pamoja na kubaki na kofia moja ya Uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ya kuimarisha Chama na alianza maandalizi ya kukabidhi Uenyekiti huo kwa Rais aliyepokea madaraka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye alikuwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi.

Pili, mwaka 1986 baadhi ya Viongozi wa nchi za Kusini mwa Dunia, walikuomba kuanzisha Tume ya Uchambuzi wa maendeleo ya nchi za Kusini tangu miaka 30 iliyopita na kuweza kuona hatua za maendeleo na changamoto zilizopo katika mataifa hayo na mapendekezo ya nini kifanyike ili kuboresha ustawi wa wananchi.

Mwalimu Nyerere alikubali jukumu hilo, ndipo alianza kutembelea nchi 19 katika Bara la Asia na Marekani ya Kusini kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa majukumu hayo mapya. Safari ya kutafuta maoni hayo ilikuwa ni pamoja na kupata uthibitisho wa kuwaelewesha wananchi na nchi hizo kuhusu majukumu ya Tume na aina ya maoni yanayokusanywa.

Kazi hiyo aliifanya kwa miaka mitatu na kutoa ripoti kuwa nchi za Kusini zifanye maendeleo yao yenyewe yalenge maslahi ya wananchi walio wengi kwa kielelezo kuwa ili nchi za Afrika ziweze kupiga hatua za maendeleo ni vyema ziwe na mshikamano kama zinahitaji kushindana na nchi za Kaskazini.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA KITUO CHA KUFUA UMEME CHA MTERA

0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewaagiza Viongozi wa mikoa wa mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya kukabiliana na tatizo la kilimo karibu na mito ambacho kimechangia kupungua kwa maji kwenye bwawa la Kufua Umeme la Mtera.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo baada ya kufanya ziara fupi katika bwawa la Kuzalisha umeme la Mtera wakati akielekea Dar es Salaam ili kujionea utendaji kazi wa Bwawa hilo baada ya kumaliza ziara ya kikazi ya Siku Tatu mkoani Iringa.

Makamu wa Rais amesema uharibifu mkubwa unaondelea kwenye mito inayotiririsha maji kuelekea Bwawa la Mtera ndio chanzo cha maji kuendelea kupungua mwaka hadi mwaka hivyo hatua za kukabiliana na hali hiyo ni lazima zikuchuliwe ili kukokoa bwawa hilo kukauka.

Amesema bwawa la kufua umeme la Mtera ni muhimu kutokana na uzalishaji wake wa umeme ambao unatumika katika shughuli mbalimbali za kiuchumi hivyo Serikali haitakubali hata kidogo bwawa lisitishe kuzalisha umeme kutokana na uharibifu huo wa mazingira.

Makamu wa Rais amewahimiza wafanyakazi wa kituo hicho kufanya kazi kwa uzalendo ili kuhakikisha kituo hicho kinaendelea kufanya kazi kwa kiwango kinachotakiwa pamoja na changamoto zinazojitokeza.

Akitoa Taarifa ya Hali ya Uzalishaji Umeme kwenye kituo hicho kwa Makamu wa Rais, Meneja wa Kituo cha Kufua Umeme cha Mtera Mhandisi John Sikauki amemueleza Makamu wa Rais kuwa hali ya mitambo ni nzuri ambapo mpango wa matengenezo kwa kuzingatia umri wa mitambo wa miaka 28 umekwiza anza.

Amesema matengenezo makubwa katika kituo hicho yamefanyika ikiwa ni pamoja na ukarabati wa Jenereta Mbili.

Mhandisi Sikauki ameeleza kuwa kina cha maji kwa sasa katika bwawa hilo hadi kufikia Aprili mwaka 2017 ni mita 693.76 juu ya usawa wa bahari na kina hicho cha maji kina uwezo wa kuzalisha umeme hadi mwisho mwa Octoba mwaka huu.

Meneja wa Kituo cha Kufua Umeme cha Mtera amesema jitihada za sasa zinazofanywa na Serikali za kunusuru Hifadhi ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu maana ndio chanzo cha kuaminika cha kufanya Bwawa la Mtera kuwa na maji ya uhakika na hivyo kutaleta ufanisi katika ufuaji wa umeme katika kituo hicho na cha Kidatu kwa mwaka mzima.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Iringa 13-April-2017.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akipokea taarifa ya kina cha maji katika kituo cha kufua umeme cha Mtera kutoka kwa Meneja wa Kituo hicho Mhandisi John Sikauki wakati akiwa njiani kuelekea Dodoma baada ya kumaliza shughuli za kuzindua Kikosi Kazi cha Taifa cha kunusuru ikolojia ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu mjini Iringa. (PichA na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wafanyakazi wa kituo cha kufua umeme cha Mtera akiwa njiani kuelekea Dodoma baada ya kumaliza shughuli za kuzindua Kikosi Kazi cha Taifa cha kunusuru ikolojia ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu mjini Iringa.

MKUU WA WILAYA YA KISHAPU AFANYA ZAIARA KATA YA MASANGA NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI, APIGA MARUFUKU UUZAJI WA CHAKULA

0
0
Mkuu wa Wilaya Kishapu mkoani Shinyanga, Nyabaganga Taraba amepiga marufuku wananchi kuuza mazao ya chakula wanayovuna hususan mtama na badala yake waweke akiba. 

Taraba alipiga marufuku hiyo jana wakati akifanya ziara katika kata za Lagana, Mwamashele, Mwakipoya na Masanga baada ya kubaini kuwepo kwa baadhi ya wananchi kufanya biashara hiyo. 

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Masanga alisema kuna baadhi ya watu huwahadaa na kununua mtama kwa bei ya juu hali inayowafanya wananchi wabaki bila chakula. 

“Nasikia hapa kuna baadhi watu wanapita kwenu wananchi na kununua debe moja la mtama kwa shilingi elfu ishirini na tano msidanganyie na kuuza wewkeni akiba,” alisisitiza mkuu huyo wa wilaya. 

Aidha alionya tabia ya baadhi ya watu kuuza mazao yakiwa shambani baada ya kukadiriwa kiasi cha mazao yao kabla ya kuyavuna aliwataka wananchi wakatae kufanya hivyo. 

Kwa upande mwingine aliwataka kuandaa mashamba yao mapema na kupanda mazao yanayohimili ukame yakiwemo mtama ili yaweze kustawi na kuwapa chakula. 

Taraba aliwataka wananchi hao kuwatumia wataalamu wa kilimo kwenye kata zao ili kupata ushauri wa kutumia mbegu zilizo bora ambazo zinaweza kuota na kukua kwa haraka.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba (katikati) akizungumza na wananchi (hawapo pichani) katika mkutano wa hadhara kata ya Masanga. kulia ni Afisa Kilimo (Ubora wa mbegu), Maduhu Masunga 
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba (katikati) akizungumza na wananchi (hawapo pichani) katika mkutano wa hadhara kata ya Masanga. Wengine pichani kulia ni Afisa Kilimo (Ubora wa mbegu), Maduhu Masunga na Mwenyekiti wa kijiji cha Masanga, Gambishi Malele. 
Mwananchi wa kata ya Masanga akitoa kero yake kwa Mkuu wa Wilaya, Nyabaganga Taraba wakati wa mkutano wa hadhara. 

OFISI YA MDHIBITI NA MKAGUZI WA MAHESABU YA SERIKALI YAWASILISHA RIPOTI YAKE KWA MWAKA WA FEDHA UNAOISHIA 2015/2016.

0
0
  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) Prof Musa Assad na Mwenyeketi Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe.Naghenjwa Kaboyoka  wakiangalia moja ya kitabu cha Ripoti kutoka Ofisi yake wakati alipokutana na  na waandishi wa Habari(hawapo Pichani) kuhusu Ripoti ya Ofisi yake kwa mwaka wa Fedha unaoisha 2015/2016 Leo Aprili 13,2017 Mjini Dodoma.Picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO Dodoma.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) Prof Musa Assad akizungumza na waandishi wa Habari(hawapo Pichani) kuhusu Ripoti ya Ofisi yake kwa mwaka wa Fedha unaoisha 2015/2016 Leo Aprili 13,2017 Mjini Dodoma.

TTB YAWAPELEKA NGONGORO WASHINDI WA KUTUMA PICHA KATIKA KUTEMBELEA UTALII WA NDANI

0
0
 Washindi wa shindano la kupiga picha wakiwa mbugani kutangaza utalii wa ndani wakiwa wameongoza na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya utalii Tanzania(TTB) ,Devotha Mdachi (katikati) wakiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JNA Dar es Salaam kwa ajili ya Safari ya kuelekea Ngorongoro  na Serengeti kujionea vivutio zaidi ili kuweza kuwavutia watanzania wengine kutembelea vivutio hivyo.
 Washindi wa shindano hilo wakiwa na wenza wao wakijadili jambo kabla ya kuondoka na ndege ya shirika la ndege nchini Air Tanzania kuelekea katika mbuga za wanyama za Ngorongoro na Serengeti,ikiwa ni moja ya sehemu ya Safari zilizoratibiwa na bodi ya utalii nchini (TTB) kwa ajli ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa Watanzania
Afisa uhusiano wa Bodi ya utalii Tanzania  akizungumza jambo na washindi wa shindano la kutuma picha kwa wapenzi ambao walishawahi kutembelea mbuga za wanyama ambao walipata kushinda tena fursa ya kutemmbelea Mbuga ya Ngorongoro na Serengeti.

KUMBUKUMBU YA DKT. AARON DAUDI CHIDUO

0
0

Tarehe 23 May 1933 – 13 April 2007


Baba yetu mpendwa, Masaa, Siku, Wiki, Miezi na sasa ni miaka 10 tangu Mungu wetu mwenye wingi wa rehema na upendo alipodhihirisha utukufu na mapenzi yake makubwa kwako hadi akaamua kukuchukua alfajiri ya siku ya Ijumaa terehe 13/04/2007. 

Huzuni na majonzi bado vimebaki kuwa ni sehemu ya maisha yetu katika familia lakini tunalo lile tumaini la Neno la Mungu kuwa siku moja tutaufikia ule ufufuo wa milele ndani ya Kristo pamoja. Matendo yako mema yamebaki kuwa lulu na mwanga uiangaziayo familia yetu. Maisha yako ya upendo, unyenyekevu, uadilifu, utu wema na bidii katika kazi ndiyo dira inayotuongoza: mke wako Mama Ahilai, watoto wako Sydney, Sarah, Oripa, Geoffrey, Rodney, wakwe zako Pascal, Joel, Eunice na Salome pamoja na wajukuu zako Dennis, Karen, David, Samantha, Jovin na Daniel. Tutakukumbuka siku zote kwa kukukosa katika mengi.


Dada zako, kaka zako na familia zao na ndugu wengine wote wa koo za Chiduo, Chitemo, Chigongo, Mheta, na Msele nao pia wanakukumbuka sana. Kwetu sote imebaki kumbukumbu ni jinsi gani ulikuwa mhimili wa familia na ukoo mzima kwa ujumla.


Baba, kwako tulijifunza uaminifu, uadilifu, unyenyekevu na kupenda haki vitu ambayo viliyokujengea heshima kubwa miongoni mwa jamii.

Mchango wako mkubwa ulioutoa katika kulitumikia Taifa hili utakumbukwa siku zote na wachapa kazi wote.


Bwana alitoa na Bwana ametwaa. Jina la Bwana Lihimidiwe.


1 Wathesalonike 4:13-14 Neno: Bibilia Takatifu



13 Ndugu wapendwa, hatupendi mkose kujua kuhusu wale wanaokufa, au mhuzunike kama watu wasiokuwa na tumaini. 14 Tunaamini kwamba Yesu alikufa na kufufuka, kwa hiyo tunaamini kwamba Mungu atawainua wale waliokufa pamoja na Kristo wakiwa ndani yake.

SALAMU ZA PASAKA KUTOKA KWA MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM KWA WAKAZI WA MKOA WA DAR ES SALAAM

0
0
 
Ndugu wananchi wa Jiji la Dar es Salaam.

Napenda kutumia nafasi hii kwanza kabisa kumshukuru mwenyezi mungu kwa kuniwezesha kuwa mzima hadi siku hii ya leo. Ni dhahiri kwamba mmekuwa pamoja tangu nilipochaguliwa kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam. 


akini pia mmekuwa bega kwa bega na mimi Meya wenu wa Jiji, katika juhudi kubwa za kulifanya jiji letu kuwa la kuvutia. Hivyo nina kila sababu ya kuwashukuru na kuwapongeza sana.

Ushirikiano ambao mnaunyesha na kuendelea kuuonyesha unanipa matumani makubwa kwamba tuko pamoja katika kuhakikisha kwamba tunaleta mabadiliko makubwa katika jiji letu na hivyo kuondokana na changamoto mbalimbali zinazo likabili jiji letu. hivyo naomba tuendelee kushirikiana na kuzidi kuniombea Meya wenu niweze kufanya kazi ambazo mmenituma katika jiji letu la Dar es Salaam.

Ni wazi mnafahamu kwamba, maendeleo ya jiji letu hajawezi kuletwa bila ya nyinyi wannachi kuonyesha ushirikiano kwa viongozi wenu ambao mmetuchagua kuanzia ngazi za Mitaa, Kata, Halmashauri pamoja na jiji.

Ndugu wananchi wa Jiji la Dar es Salaam.

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imekuwa na mipango mingi mizuri ambayo imelenga kuboresha maendeleo ya wananchi wake. Miongoni mwa mambo ambayo niweka na kuendelea kusimamia ili kuhakikisha kwamba wakazi wa jiji la Dar es Salaam wanapata huduma mbalimbali za kijamii kwa uhakika.

Ndugu wananch wa Jiji la Dar es Salaam.

Hivi sasa tunaingia kwenye kipindi cha sikuu ya pasaka. Tunapoungana na wenzetu Wakristo katika kusherehekea Sikukuu ya Pasaka, niwaombe wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuendeleza kushirikiana na vyombo vyetu vya usalama katika suala zima la uimarisha wa usalama wenu.

Vyombo vya usalama vimekuwa rafiki kwa kipindi chote jambo ambalo limefanya kupungua kwa matukio ya kiuhalifu ndani ya jiji letu.

Hivyo basi nitoe rai kwa wakazi wote wa jiji la Dar es Salaam, kusherehekea siku kuu hii kwa Amani na utulivu bila kuwepo kwa vurugu zozote. Salamu zangu za upendo katika sikukuu hii ya Pasaka ziwe chachu ya kuendelea kutunza amani katika jiji letu, huku mki hakikisha kwamba kila eneo ambalo watoto wenu watashiriki kwa namna moja ama nyingine kuwe na usalama wa uhakika. Tusijenge utamaduni wakukubali matukio ya kuvunja amani kwenye siku kuu maana hizi ni sherehe sio vita.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WAKAZI WA JIJI LA MWANZA KULIPOKEA TAMASHA LA "NYANZA FESTIVAL" KWA KISHINDO

0
0




Judith Ferdinand, BMGHabari


Wakazi wa Jiji la Mwanza na viunga vyake, wanatarajia kupata burudani ya kukata na mundu kutoka kwa wasanii mbalimbali Kanda ya Ziwa katika tamasha la burudani "Nyanza Festival 2017".

Burudani hiyo ambayo itakua ya aina yake kwa kuwakutanisha wasanii kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa, itafanyika Siku Kuu ya Pasaka kuanzia saa nne asubuhi mpaka majogoo kwa kiingilio cha shilingi 5,000 tu katika Uwanja wa CCM Kirumba.

Mratibu wa tamasha hilo, Fabian Fanuel, amesema mbali na burudani ya mziki pia kutakua na mchezo wa mpira wa miguu kati ya Waandish wa habari za michezo Kanda ya Ziwa LASPOJA Fc na Bongo Movie, na Madjs na Watangazaji wa vipindi vya burudani watacheza na wafanyakazi wa halmashauri ya Jiji la Mwanza.

Naye Afisa Habari wa tamasha hilo, George Binagi, amebainisha kwamba wanatasnia wa burudani hususani wanamuziki mastaa na chipukizi kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa, wameahidi kudondosha burudani kali siku hiyo.

"Zaidi ya wasanii 30 kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa tayari wamethibitisha kupanda jukwaa la Nyanza Festival 2017 hivyo niwasihi wapenzi wa burudani wakae tayari kwa burudani hiyo ambapo kiingilio itakuwa elfu tano tu". Amesema Binagi.

Nyanza Festival ni tamasha lililoasisiwa na Wanatasnia mbalimbali kutoka Kanda ya Ziwa wakiwemo wanamuziki, watangazaji, waandishi wa habari, Madjz na wadau wengine wengi kupitia umoja wao wa Mwanza.Com chini ya kampuni ya Famara Entertainment, lengo likiwa ni kuukuza na kuuendeleza zaidi muziki wa Kanda ya Ziwa.

AHADI ZA SERIKALI YA MKOA WA DAR ES SALAAM ZAZIDI KUKAMILIKA.

0
0
Makonda atembelea hospitali ya Koica Chanika leo jijini Dar es Salaam.
Hospitali ya Koica Chanika ya Mama na Mtoto inatarajia kuzinduliwa Juni mwaka huu, ambayo inawezo kuendesha oparesheni nne kwa siku.

Hospitali hiyo imejengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Korea Kusini ambapo kujengwa hospitali hiyo kulitokana na ombi la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipokutana na Balozi wa Korea Kusini nchini.

Akizungumza wakati alipotembea hospitali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa hospitali hiyo ni mkombozi kwa wanawake na watoto kutokana na kuwa vifaa vya kisasa.

Amesema azma ya serikali ya awamu ya tano ni ya kuhakikisha wananchi wanyonge na masikini wanapata huduma za afya zilizo bora inatimia.

Makonda amesema hakuna kitu kinachoshindikana kama viongozi kufanya kazi za kujitoa kwa wananchi hasa katika sekta ya afya ambayo ndio msingi wa maisha ya watanzania.

Amesema hospitali hiyo ina hadhi yake kutokana na kuwa na vifaa vya kila aina zote ambapo hakuna mama atakayepoteza maisha kutokana na kujifungua ikitokea ni mipango ya Mungu.

Makonda amesema wanawake wakiwa na ujauzito walikuwa wanafikiri huduma wakati wa kujifungua lakini serikali ya awamu ya tano imeweka kipaumbele chini ya Rais wa Awamu ya Tano, Dk.John Pombe Magufuli.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amesema kuwa kujengwa kwa hospitali hiyo kutapunguza msongamano katika hospitali ya Amana.Amesema kutokana na vifaa huduma ambazo zitatolewa katika Hospitali hiyo kwa mama na mtoto zitakuwa ni za kiwango cha juu.
Mkuu wa Wilaya , Mjema amesema kuwa moja huduma hizo ni kuwa na mashine za kisasa za kufulia ambazo zinaweza kufua kilo 70 kwa saa.

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimsikiliza Mganga wa Manispaa ya Ilala,Willy Sangu (hayupo pichani) alipokuwa akitoa maelezo ya vifaa mbalimbali vilivyofungwa katika hospitali hiyo mapema leo jijini Dar,kulia ni Mkuu wa wilaya ya Ilala,Mh Sophia Mjema.

Majengo ya hospitali hiyo kama yaonekanavyo pichani, iliyojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Korea Kusini,ampapo inatarajiwa kuzinduliwa Juni 2017 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipata maelekezo ya vifaa kutoka kwa Daktari wa Manispaa ya Ilala, Willy Sangu leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akitazama baadhi ya vifaa vya kisasa vilivyofungwa katika hospitali hiyo,alipotembelea mapema leo kuangalia vifaa mbalimbali katika Hospitali ya Koica Chanika, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Vifaa vya kisasa ambavyo tayari vimeishafungwa katika hospitali hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimsikiliza Mganga wa Manispaa ya Ilala,Willy Sangu (hayupo pichani) alipokuwa akitoa maelezo ya vifaa mbalimbali vilivyofungwa katika hospitali hiyo mapema leo jijini Dar.

BALOZI WA KUWAIT AZINDUA KISIMA CHA 27 KATIKA SHULE YA MSINGI MAJANI YA CHAI JIJINI DAR

0
0

Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Jasem Al-Najem amezindua kisima cha 27 katika shule ya msingi Majani ya Chai iliyopo Vingunguti ikiwa ni ka

Katika tamati ya awamu ya kwanza ya mpango wa Ubalozi wa Kuwait wa kuchimba Kisima kwa kila shule mpaka sasa kumezinduliwa visima vya maji 27 katika shule 27 mbalimbali katika kipindi cha miezi mitatu tu jijini Dar es salam.

Mpango huo wa Ubalozi wa Kuwait umeweza kufanikiwa ambapo visima 16 kati ya hivyo vilichimbwa na Jumuiya ya mwezi mwandamo ya Kuwait (Kuwait Red Crescent Society ).

Visima vingine vilichimbwa na wasamaria wema wa Kuwait kwa kushirikiana na asasi nyingine za nchin Tanzania na Kuwait.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Jasem Al-Najem akizindua kisima katika Shule ya Msingi Majani ya Chai iliyopo ya Vingunguti akiwa pamoja na wanafunzi wa Shule hiyo na walimu ikiwa ni mpango wa kwanza wa ubalozi wa nchi hiyo kuchimba kisima katika Shule za Msingi Jijini Dar es salaam

BODI YA ZABUNI YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YAIPA WIKI TANO KAMPUNI YA UJENZI YA KOBERG KUKAMILISHA UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAMISHNA WA UHAMIAJI, JIJINI D’SALAAM

0
0
Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imeipa muda wa wiki tano Kampuni ya Ujenzi ya Koberg Construction Co.Ltd kukamilisha ujenzi wa nyumba za makazi za Makamishna wa Idara ya Uhamiaji hapa nchini zilizoko katika eneo la Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam ambazo zitatumiwa na Makamishna hao. 

Uamuzi wa Bodi hiyo umekuja baada ya Kampuni ya Koberg Construction ya nchini hapa kuonyesha kusuasua na kushindwa kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo kwa wakati.

Bodi hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga na Katibu wake Bw. David Mwangosi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi cha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imefanya maamuzi hayo baada ya kufanya ukaguzi na kujionea hatua zilizofikiwa katika ujenzi wa nyumba hizo.

Kwa upande wake Katibu wa Bodi hiyo amesema kitendo cha Mkandarasi huyo kusuasua kukamilisha kwa wakati kazi ya ujenzi wa nyumba hizo ulioanza tangu mwaka wa Fedha wa 2014/2015 ndicho kilichoifanya Bodi ya Zabuni ya Wizara hiyo kuamua kutembelea eneo ambalo kazi ya ujenzi wa nyumba hizo unaendelea na kumpatia wiki tano tu kuhakikisha anakamilisha kazi hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga (watatu kushoto), Katibu wa Bodi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara hiyo, David Mwangosi wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Majengo wa Idara ya Uhamiaji, Hamza Shabani (kushoto), wakati wajumbe wa Bodi hiyo walipotembelea nyumba za makazi za Makamishna wa Uhamiaji, Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam. Bodi hiyo ilitoa wiki tano kwa Kampuni ya Ujenzi ya Koberg kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo.
Katibu wa Bodi ya Zabuni, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara hiyo, David Mwangosi akiwafafanulia jambo Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Wizara hiyo, wakati wajumbe hao walipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa nyumba za makazi ya makamishna wa Uhamiaji zilizopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, Wajumbe wa Bodi hiyo walitoa wiki tano kwa Kampuni ya Ujenzi ya Koberg kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga.

Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga (kushoto) akiangalia kabati la nguo katika moja ya chumba cha nyumba za makamishna wa Uhamiaji zilizopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam. Wajumbe wa Bodi hiyo walizikagua nyumba hizo na kutoa wiki tano kwa Kampuni ya Ujenzi ya Koberg kukamilisha ujenzi.

Makao Makuu ofisi ya Taifa ya Takwimu kukamilika baada ya miezi kumi

0
0
Benjamin Sawe-Maelezo,Dodoma.

MKURUGENZI Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dk. Albina Chuwa ametaka ujenzi wa makao makuu ya ofisi hiyo unaoendelea mjini Dodom ukamilishwe kwa wakati.

Akizungumza mjini hapa jana baada ya kukagua ujenzi wa ofisi hiyo, Dk. Chuwa alisema ni wakati sasa kwa NBS kuwa na ofisi yenye hadhi kwa ajili ya kuboresha na kuimarisha shughuli za takwimu nchini.Dk. Chuwa alisema NBS ni miongoni mwa taasisi kongwe nchini na ambayo imekuwa ikibadilika na kwenda na wakati hivyo kupatikana kwa jengo hilo ni jambo linalopaswa kutimia haraka.

“Jengo letu ni la ghorofa tano tu, kwa kuwa mkandarasi umepewa muda wa miezi 10 sioni sababu ya kuchelewa kukamilishwa.“Hivi karibuni nilizungumza na wenzetu wa Uganda wao walijenga jengo lao la ghorofa 12 kwa mwaka mmoja tu sasa sioni sababu kwa nini letu lisikamilike kwa wakati,”alisema.

Kwa mujibu wa Dk. Chuwa jengo hilo litakuwa ni la ghorofa tano na kwamba kwa kuwa wanazo ofisi katika kila mkoa nchini, makao makuu hayo yatatumika kuratibu uendeshaji wa shughuli za takwimu na mambo mengine ya maendeleo yanayohusiana na NBS.

Dk. Chuwa alisema jengo hilo litagharimu sh. Bilioni 11.6 hadi kukamilika kwake fedha ambazo zinatokana na mkopo kutoka Benki ya Dunia.

Kwa upande wake, Msimamizi Mkuu wa ujenzi huo, Mtumwa Shomvi kutoka kampuni ya Y&P Achtects Limited, alisema watahakikisha wanatekeleza majukumu yao kikamilifu katika kuusimamia mradi huo.Shomvi  alisema jukumu kubwa wanalolisimamia ni kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati, gharama na ubora uliokubaliwa.

Aidha, Msimamizi kutoka kampuni inayotekeleza mradi huo ya Hainani International Limited ya China, Lan Shuiqing alisema kazi ya ujenzi inaendelea vyema na kwamba anaamini kila kitu kitakamilika kwa wakati.


Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Albina Chuwa akitoa maelekezo wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo jipya la Makao Makuu ya Ofisi hiyo unaondelea Mkoani Dodoma leo (jana), wa kwanza kulia ni Injinia Lan Shuiqing kutoka Kampuni ya Hainan Internationa.
Msimamizi Mkuu kutoka Kampuni ya Y and P Bw. Mtumwa Somvi wa kwanza kulia akitoa maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Albina Chuwa wakati menejimenti ya Taasisi hiyo ilipokagua maendeleo ya ujenzi mkoani Dodoma leo (jana).
Baadhi ya mafundi wakiendelea na ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu lenye urefu wa ghorofa tano linaloendelea kujengwa Mkoani Dodoma.
Muonekano wa ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu unavyoendelea mkoani Dodoma.(Picha na Benjamin Sawe -Maelezo) .
 

MATUKIO YA AJALI BARABARANI NA KAMERA YA GLOBU YA JAMII

0
0
Ajali mbalimbali zilizonaswa na kamera ya Globu ya jamii katika barabara ya Iringa.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

Taifa Moja kunogesha Pasaka kwa matamasha

0
0
Kampeini ya Taifa Moja inatarajiwa kuendelea mwishoni mwa wiki hii kwa matamasha ambayo yatafanyika kwenye mikoa mitano hapa nchini ikiwa na lengo ya kuendelea kutoa burundani pamoja elimu kwa Watanzania juu ya kutuma na kupokea fedha kutoka kwenye mtandao wowote kwa gharama ile ile.

Taifa Moja ni kampeini ambayo imedhaminiwa na taasisi za Financial Sector Deepening Trust of Tanzania (FSDT) pamoja na Bill & Melinda Gates Foundation huku ikiratibiwa na International Finance Corporation (IFC) chini ya muungano ya makampuni matatu ya simu za mkononi za Airtel Tanzania, Tigo Tanzania na Zantel kupitia huduma zao za Airtel Money, Tigo Pesa na Ezy Pesa.

Akizungumza jijini leo Jijini Dar es Salaam, Liginiku Milinga ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Fern Tanzania ambao ndio waratibu na waandaaji wa matamasha hayo alisema maandalizi yote yamekamilika na kuwaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kupata burundani toka kwa wasanii wakali hapa nchini na pia kupata elimu juu ya kutuma na kupokea pesa kwenda mtandao wowote hapa Tanzania kwa gharama ile ile.

Milinga alitajwa mikoa ambayo matamasha hayo yatafanyika ni pamoja na Mbeya (Mwenge Primary School), Dar es Salaam (Zakhiem Grounds), Arusha (Kilombero Grounds), Mwanza (Furahisha Grounds na Tabora (Uyui Grounds) huku msanii Chege akitumbuiza Mwanza, Stamina na Jambo Squad wakitumbuiza Arusha, Belle 9 Mbeya, Cassim Mganga Tabora huku Mkubwa na wanae wakifanya yao Jijini Dar es Salaam. Matamasha hayo yatafanyika Jumapili ya tarehe 16 April mwaka huu.

Kuhusu kutoa elimu kwa wananchi juu ya huduma ya kutuma na kupokea pesa kwenda mtandao kwa gharama ile ile Meneja Chapa kutoka kampuni ya Tigo Tanzania William Mpinga, Moses Alphonce ambaye ni Meneja wa Airtel Money, Patric Dumulinyi ambaye ni Mobile Money Manager walitoa wito kwa wananchi kwenye mikoa hiyo kujitokeza kwa wingi kwani matamasha haya ni ya wazi na hakuna kiingilio.

‘Natoa wito kwa Watanzania kujitokeza na kupata elimu ya kutosha ya jinsi ya kutuma na kupokea pesa kwenda mtandao wowote kwa gharama ile ile, alisema,’ alisema Mpinga.

Mpinga alisema huduma hiyo itawanufaisha wananchi kupunguza gharama za kutuma fedha kwenda mitandao mingine na upotevu wa fedha uliokuwa ukijitokeza hapo awali.

Alisema kampeni ya Taifa Moja itaongeza uelewa wa watumiaji wa simu za mikononi nchini juu ya namna ya kutuma na kupokea pesa kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine kwa gharama ile ile.

“Watumiaji wa huduma za simu-pesa watatumiana pesa kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine na kuingia moja kwa moja kwenye akaunti za simu –pesa ya mteja aliyetumiwa, hakutakuwa na sababu ya kuhofia pesa hiyo uliyotumiwa kwenda kuitoa haraka ukihofia kumrudia aliyekutumia kama ilivyokuwa hapo awali," aliongeza Moses Alphonce kutoka Airtel Money.

Kwa upande wake, Rukia Mtingwa ambaye ni Meneja Chapa na Mawasiliano alisema njia hii ya sasa ni tofauti na utaratibu wa zamani ambao mteja akimtumia mwenzake ambaye yupo mtandao mwingine hutumiwa ujumbe wa meneno (sms) kwa aliyetumiwa kwenda kuchukua pesa hiyo kwa wakala.

“Kuanzia sasa tutaendelea kutoa elimu kwa watumiaji wa mitandao yetu juu ya utumaji pesa kutoka kwenye mtandao mmoja kwenda mwingine anavyoweza kukatwa kiasi cha fedha kile kile kama ambacho angelikatwa kutoka mtandao kama wake.”Aliongeza Mtingwa.

WATANZANIA WATAKIWA KUCHANGAMKIA UNUNUZI HISA ZA AWALI ZA VODACOM

0
0
Benny Mwaipaja, WFM-Dodoma

Serikali imewataka watanzania kuchangamkia fursa ya ununuzi wa asilimia 25 ya hisa za awali za kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom zinazouzwa kwa watanzania pekee ikiwa ni utekelezaji wa sheria ya fedha ya mwaka 2016 kwa lengo la kuwawezesha watanzania kuwa wamiliki makampuni ya simu za mikononi hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma leo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Bi Beng’i Issa amesema hi ni fursa kubwa na muhimu kwa watanzania kuwa sehemu ya wamiliki wa makampuni ya simu za mikononi kupitia ununuzi wa hisa hizi za awali.

‘’Ni uwekezaji ambao ni salama sana na hauna hasara, kwa kuwa ukiwa hutaki kuendelea kuwa mwanahisa unauza hisa zako na kurudisha pesa zako na unaweza kupata faida’’.

Ununuzi wa hisa hizi utawawezesha Watanzania kuwa wamiliki wa kampuni, watapata gawio la faida, wanaweza kutumia hisa kama dhamana za mikopo benki na wanaweza kuziuza hisa wanapokuwa na shida ya fedha.

Hisa hizi zinauzwa kwa mtanzania mmoja mmoja, watumishi walioajiriwa, wastaafu, makampuni yanayomilikiwa na watanzania, mashirika ya kitanzania, VICOBA, SACCOS, vikundi vya kijamii, wanawake na vijana. Aidha hisa moja inauzwa kwa shilling 850 na kiwango cha chini cha ununuzi ni hisa 100 na hakuna kikomo cha juu cha ununuzi wa hisa.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi. Beng’i Issa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa kununua hisa kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mkoani Dodoma.
Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Bw. Edward Kessy, akitoa ufafanuzi wa namna ya kununua hisa hizo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mkoani Dodoma.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifatilia kwa makini maelezo ya Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi. Beng’I Issa (hayupo pichani) alipokuwa anatolea ufafanuzi kuhusu umuhimu wa kununua hisa kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mkoani Dodoma.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifatilia kwa makini maelezo ya Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi. Beng’I Issa (hayupo pichani) alipokuwa anatolea ufafanuzi kuhusu umuhimu wa kununua hisa kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mkoani Dodoma.(Piha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango).


ENGINE FOR LAND ROVER DISCOVERY AND DEFENDER FOR SALE!

0
0
Tuna Engine za Land Rover Discovery , Defender Range Rover, Puma Engine Tdci 2.4, Td5,Tdi300,Tdi200,P38, na pia tunaweza kukupatia Spare ya aina yoyote kutoka Europe kwa bei nafuu.
Bei ya hiyo Land Rover Discovery  Engine Td5 ni T.sh.4.7 Milion 
Gear Box T.sh. 2.7 Milion
Tunaleta kutoka U.K. na tayari  zipo Dar es Salaam kwa maelezo zaidi wasiliana nasi Tel.+255674782666 +255652444311 
 on whatsapp +447723550406

Mwili wa Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) Hayati Dkt. Elly Macha kuwasili Dar es salaam April 20, 2017

0
0

Mwili wa Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA) Hayati Dkt.  Elly Macha unatarajiwa kuwasili nchini Aprili 20 mwaka huu ukitokea nchini Uingereza.
Dk Macha alifariki dunia Machi 31 mwaka huu katika Hospitali ya New Cross, Wolverhampton nchini Uingereza alikokuwa akitibiwa.
Akitoa ratiba ya msiba huo leo bungeni, Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai alisema taratibu zote za nchi i Uingereza za kurudisha mwili wa Mbunge huo zimekamilika.
“Kule kuna taratibu nyingi za kisheria na kadhalika haikuwa rahisi kuharakisha mchakato huo. Tunashukuru ubalozi wetu wa nchini humo umeweza kufanikisha jambo hili,”amesema
Ndugai amesema mwili wake utawasili Alhamis ya wiki ijayo katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere April 20, mwaka huu saa tisa mchana.

WATANZANIA WANANE WALIOKUWA WAKISHIKILIWA NCHINI MALAWI WAACHIWA HURU

0
0
NA K-VIS BLOG NA MASHIRIKA YA HABARI
WATANZANIA wanane waliokuwa kizuizini nchini Malawi wakituhumiwa kufanya “ushushushu” wameachiliwa huru leo Aprili 13, 2017 na mahakama moja kwenye mji wa Mzuzu nchini humo.
Taarifa za vyombo vya habari vya Malawi zinasema, Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Muzuzi nchini Malawi, amewaachia huru Watanzania hao waliotiwa mbaroni Desemba 20, 2016 kwa tuhuma za kufanya “ushushushu” kwenye mgodi wa madini ya Urani wa Kayekera huko Karonga.
 Kwa mujibu wa vyombo hivyo vya habari, Watanzania hao walikuwa wakishtakiwa kwa kosa la kuingia maeneo ya mgodi bila kibali ikiwa ni pamoja na shikata la kufanya “upelelezi”.
Hata hivyo Watanzania hao walikanusha mashtaka hayo tangu walipotiwa mbaroni.
Kwa mujibu wa Watanzania hao, sababu kuu iliyowafanya kufika kwenye eneo hilo ilikuwa ni ziara ya kimafunzo na wala haikuwa kufanya upelelezi kama ambavyo mamlaka za Malawi zilivyowatuhumu.
Baada ya Watanzania hao kupatikana na hatia, Hakimu huyo Mkuu Mkazi wa mahakama ya Muzuzu, Texious Masoamphambe, aliwahukumu Watanzania hao kifungo cha mwezi mmoja jela kwa kosa la kuingia eneo hilo bila kibali na kifu ngo cha miezi mitatu jela kwa kosa la kufanya “Ushushushu”
Hata hivyo Hakimu huyo aliitupilia mbali hukumu hiyo na kutoa sharti la watu hao kutofanya kosa katika kipindi cha miezi sita. Pia mahakama hiyo iliiamuru serikali kuwafukuza nchini Watanzania hao.
Aidha kuachiwa huru kwa Watanzania hao ambao tayari walikuwa wamekwisha hukumiwa kunatokana na mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea baina ya Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, ambapo Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Dkt.Augustine Mahiga, alinukuliwa wiki iliyopita akitoa hakikisho la kuachiwa huru kwa Watanzania hao.

KARIBU MINI FESTIVAL IN BAGAMOYO ON APRIL 22, 2107

0
0
Burudani bureeeee...unaanzaje kukosaaaaa..... Uongozi wa Karibu Music Festival unawaletea burudani ya muziki bureeeee kwa wakazi wa Bagamoyo na sehemu mbalimbali tarehe 22/4/2017 pale  Baga  Point Bagamoyo. Karibu Min Festival ni sehemu ya maandalizi ya Tamasha kubwa la muziki live litakalofanyika kiwanja cha Mwanakalenge tarehe 3-5, November mwaka huu...
#TwenzetuBagamoyo APRIL 22 #KaribuMiniFestival  #BagaPoint Ni BURE kabisa Hakuna Kiingilio.
#KaribuMiniFestival
#KaribuMusicFestival
100% #LiveMusic Toka Kwa #JagwaMusic ,  #SegereOrignal ,  #JustinGodykaozya , #Tabasamu ,  #ChikayaBuruya
#TukutaneBagamoyo
It's All About #KaribuMusicFestival2017
@karibumusicfestival
FAHARI YA TANZANIA.


KIKWANGUA ANGA KIREFU KULIKO VYOTE JIJINI MBEYA

0
0
MBEYA MUBASHARA: Jengo refu zaidi kuliko majengo yote Jijini Mbeya ni jengo hili la Shirika la Umeme la Taifa (TANESCO) lenye ghorofa 11 ambalo lipo katika eneo la Uhindini mkabara na Stendi ya Zamani ya BP Barabara ya Soko Matola katika barabara ya  kwenda Uyole Jijini Mbeya.
Picha na Mr. Pengo wa Globu ya Jamii, Mbeya.
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images