Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

MVUA YALETA MADHARA NA KUSABABISHA KAYA 20 KUKOSA MAKAZI CHALINZE

$
0
0
 Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete (mwenye kanzu) akiwa na wananchi wa jimbo hilo wakikagua `Bwawa la Umwangiliaji la Msoga 

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete,ametembelea eneo la Chalinze Mzee lilokumbwa na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika jimbo hilo na kusababisha madhara ya nyumba kubomoka na nyumba 9 kusombwa na maji na kusababisha zaidi ya kaya 20 kukosa pakulala.

Akizungumza Ridhiwani,ametaja  maeneo yaliyokumbwa na  mafuriko ni Chalinze Mzee,Bwawa la umwangiliaji la Msoga ambalo limetoboka na shule ya Sekondari ya Imperial.

Aidha,amesema kuwa madhara makubwa yaliosababishwa na mafuriko hayo ni kuharibika kwa mashamba,nyumba za wananchi kuharibika na kusabbishwa wananchi kukosa pa kulala,na ameongeza kuwa kwasasa wananchi hao wanahitaji msaada. 

Ridhiwani ametoa pole kwa wakazi hao na kuwaomba kuwa vumilivu katika kipindi hiki.
 Baadhi ya Nyumba katika eneo la Chalinze Mzee zikiwa zimearibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
 Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiangalia madhara yaliosababishwa na mafuriko katika jimbo hilo la Chalinze.
 wakazi wa chalinze wakiangalia nyumba zao zilizobomoka kutokana na mafuriko.
 Sehemu ya bwawa la umwangiliaji la Msoga liloaribiwa na mafuriko na kupasua kingo za bwawa hilo.
 Moja ya Nyumba iliyobomoka kutoka na mvua zinazoendelea kuonyesha katika eneo la Chalinze.

Balozi mpya wa Tanzania nchini Kenya Dkt. Pindi Hazara Chana aripoti kwenye kituo chake cha kazi

$
0
0
Balozi mpya wa Tanzania nchini Kenya, Mheshimiwa Dkt. Pindi Hazara Chana ameripoti kwenye kituo chake cha kazi jijini Nairobi na kulakiwa na wafanyakazi wa kituo hicho.
Balozi Chana amekutana na wafanyakazi wa kutoka nyumbani na wale walioajiriwa hapa Kenya. Balozi ameelezea kituo cha Nairobi kama moja ya vituo vyenye shughuli nyingi na vinavyosifiwa kwa utendaji mzuri licha ya mazingira magumu ya kazi. Amewaahidi wafanyakazi kuwa atakuwa kiongozi wa kujichanganya kwani anaamini katika uwazi, umoja na mshikamano kazini.
"Nitajichanganya sana na ninyi kwa sababu nimetumwa kuwatumikia watu. Sera yangu ya kazi ni uwazi, upendo na mshikamano. Tufanye kazi kama familia moja," alisema.
Balozi Chana amesema Kenya ni jirani mwema wa Tanzania na nchi hizo zina historia ndefu ya undugu na ushirikiano, hivyo kazi yake ni kuhakikisha ushirikiano huo unaimarishwa na kudumishwa.
 Balozi Chana akikaribishwa kwenye ofisi za Ubalozi na Mwambata wa Utawala, Bi Aneth Mmari
 Balozi akisalimiana na wafanyakazi wa Ubalozi. Wa kwanza kulia ni Konseli Mkuu wa Tanzania Mombasa, Mheshimiwa Khalifan Shehe Saleh
 Balozi Chana akisalimiana na wafanyakazi wa Ubalozi waliojipanga kumlaki.
Balozi Chana akiongea na wafanyakazi wa Ubalozi.

HIVI NDIVYO MAMBO YALIVYONOGA KATIKA UZINDUZI WA WASATU NORTHAMPTON, UINGEREZA

$
0
0
Na Freddy Macha 
Jumuiya ya wasanii Watanzania Uingereza (WASATU) ilizunduliwa kwa vigelegele na muziki mjini Northampton , katikati ya Uingereza jumamosi iliyopita. Tafrija hiyo ndogo lakini iliyowakutanisha zaidi ya Watanzania mia moja na marafiki zao wa Kenya, Uganda, Kongo , Nigeria, Uingereza nk, ilihudhuriwa na Mheshimiwa Balozi Dk Asha Rose Migiro. WASATU ilibuniwa mwaka jana kati ya wasanii wakiongozwa na mwanamuziki na mcheza sarakasi Fab Moses na promota wa vyakula vya Kitanzania, Bi Neema Kitilya. Asilimia 20 ya kipato cha onesho zilitolewa na WASATU kwa waliofikwa maafa ya mafuriko ya maji karibuni Tanzania.1- Watanzania na marafiki zao wakijimwaga Northampton- pic by F Macha 2017Watanzania na marafiki zao wakijimwaga ukumbi wa The Eastern District Social Club, Northampton.
2-Furaha na shangwe - pic by F Macha 2017Furaha na shangwe ya WASATU3- Balozi Migiro na Mwana WASATU-mcheza ngoma asilia Khadija Ismail ; wa kwanza ni Salma Kashinde- pic by F Macha 2017Balozi Migiro (katikati) na mwana WASATU- mcheza ngoma asilia, Khadija Ismail. Wa kwanza ni Mtanzania, Salma Kashinde4-Muziki moto moto Northampton- pic by F Macha 2017Muziki motomoto, Northampton.

Mdahalo Maalum: Watanzania Wa Nyumbani Na Diaspora Kukutanishwa

$
0
0
Ni Jumanne na Jumatano, Aprili 11 na 12. Ni mdahalo kuhusu nafasi ya Diaspora kuungana na wenzao walio nyumbani kwenye kuchangia kusukuma mbele jitihada za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda kutokana na maendeleo ya viwanda. 
Hivyo, umuhimu wa kujadili fursa na changamoto.Tukio hilo ambalo ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka Kumi ya kuanzishwa kwa mtandao wa ' Mjengwablog' litafanyika Aprili 11 na 12 ( Jumanne na Jumatano) kwenye Ukumbi wa Nyumba ya Makumbusho, Dar Es Salaam. 
Ukumbi upo Mtaa wa Shabaan Robert na utazamana na IFM.Mdahalo utaambatana na maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa Tanzania na wajasiriamali wa Kitanzania. Washiriki wa mdahalo huo wanaotarajiwa kuwa zaidi ya mia mbili wanatazamiwa kuwa katika makundi matatu makuu; Baadhi ya Watanzania waishio ughaibuni, waliokuwa wakiishi ughaibuni na sasa wamerejea nyumbani na Watanzania wa nyumbani. Wote hao wanaunganishwa jambo kuu lenye kuhusu maendeleo ya uchumi wa nchi na kwa ngazi ya mtu binafsi. Hivyo, inahusu kujadili fursa za kufanya biashara na uwekezaji. Mdahalo hauna kiingilio.
Na Alhamisi April 13, kutakuwa na ' Usiku wa Nyumbani Na Diaspora' kwenye ukumbi wa Mzalendo Pub, Kijitonyama. Kutakuwa na chakula cha Kiafrika na maonyesho ya mavazi ya Kiafrika. Baada ya hapo ni mwendo wa kujirusha kwa muziki mchangayiko wa DJ BonyLuv!

Article 14

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) yaishukuru Jumuiya ya Kihindu Mwaminarayan Sanstha (BAPS)

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)  Profesa Mohamed Janabi akimshukuru Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Kihindu Mwaminarayan Sanstha (BAPS) Duniani Mtukufu Mahant Swami Maharaj  alipotembelea Tanzania hivi karibuni na kutoa msaada wa zaidi ya dola za Kimarekani 300,000 kusaidia Taasisi  hiyo kwa ajili ya upasuaji wa watoto 200  Profesa Janabi pia amemshukuru sana Bw.  Subash Patel Mkuu wa BAPS Tanzania kwa kuratibu na kuwezesha kutolewakwa msaada huo.

Introducing "Acha nikae kimya" by Diamond Platnumz

NEWS ALERT: Mabweni ya chuo cha uuguzi Ifisi, Mbalizi jini Mbeya yateketea kwa moto

$
0
0
Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii  inaeleza kuwa Mabweni ya Chuo cha Uuguzi yaliyopo eneo la Ifisi Mbalizi, Mbeya, yameteketea kwa moto. Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lipo eneo la tukio kuhakikisha mambo yanakaa sawa kutokana na moto uliozuka na kuteketeza baadhi ya mabweni hayo. Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana. Habari kamili baadae kidogo
Sehemu ya ndani ya mabweni hayo baada ya kuungua.

WAHESHIMIWA FREEMAN MBOWE NA HALIMA MDEE WAFIKISHWA MBELE YA KAMATI YA MAADILI YA BUNGE

$
0
0
 Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni (KUB), Mhe. Freeman Mbowe akihojiwa mbele ya ya kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kufuatia amri ya Mhe. Spika wa Bunge ya kumtaka afike mbele ya kamati hiyo kujibu tuhuma zinazomkabili za kuingilia Haki, Uhuru na Madaraka ya Bunge kutokana na matashi yasiyo na staha aliyoyatoa mapema mwezi Machi 2017 Bungeni Mjini Dodoma yaliyokuwa na madai ya kudharau Bunge.
 Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni (KUB), Mhe. Freeman Mbowe akihojiwa mbele ya ya kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge k
Mbunge wa Jimbo la Kawe, Mhe. Halima Mdee akihojiwa mbele ​​ya kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kufuatia amri ya Mhe. Spika wa Bunge ya kumtaka afike mbele ya kamati hiyo kujibu tuhuma zinazomkabili za kuingilia Haki, Uhuru na Madaraka ya Bunge kutokana na kutoa matusi Bungeni na kumtukana Spika, matamshi aliyoyatoa mapema mwezi Machi 2017 Bungeni Mjini Dodoma yaliyokuwa na madai ya kudharau. Bunge. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

Bamiza Music Chart 8th April 2017

EFM YAKABIDHI PIKIPIKI MBILI KWA WASHINDI WA SHIKA NDINGA WILAYA YA KINONDONI

$
0
0
  Mshindi wa shindano la Shika ndinga katika Wilaya ya Kinondoni , Alphonce Daudi akisaini mkataba wa kuwa mshindi wa shindano lashika ndinga huku akiwa amesimamiwa na Afisa Uhusiano wa Efm Neema Makarasi
Mshindi wa Shindano la Shika ndinga na Efm kwa Wanawake Wilaya ya Kinondoni Rehema Nassoro akisaini hati ya kumtambua kuwa ndio mshindi wa shindano la Shika ndinga
Afisa Uhusiano wa Efm Neema Makarasi akiwavesha makoti na vifaa vya pikipiki washindi wa shindano hilo
Afisa Uhusiano wa Efm Neema Makarasi akikabidhi pikipiki kwa Alphonce Daudi ambaye ni mshindi
Afisa Masoko wa kampuni ya SanMoto akikabidhi funguo kwa shindi wa shindano hilokwa Wanawake. 
Picha zote na Humphrey Shayo wa Globu ya Jamii.

HIGHLIGHTS ZA MCHEZO WA MAJIMAJI VS AFRICA LYON

$
0
0
Timu ya Maji Maji imelazimishwa sale ya 1 – 1 na Africa Lyon katika mchezo uliochezwa uwanja wa Maji Maji mjini Songea mkoani Ruvuma, Goli la Africa Lyon limepatikana kipindi cha pili dakika ya 61 baada ya shuti kali lililopigwa na Peter Mwalyanzi, huku goli la Maji Maji limepatikana dakika ya 74 na Kelvin Sabato .

NAPE APOKELEWA KWA KISHINDO JIMBONI KWAKE,ASHINDWA KUJIZUIA KUMWAGA CHOZI

$
0
0
Sehemu ya Umati wa watu wakishangilia kwa pamoja mara baada ya Mbunge wa jimbo la Mtama,Mh Nape Nnauye kupanda jukwaani na kuanza kuimba na kucheza kwa pamoja huku miluzi,shangwe na vigele gele vikiwa vimetawala uwanjani hapo.
Mbunge wa jimbo la Mtama,Mh Nape Nnauye akizungumza na Wananchi (hawapopo pichani) katika mkutano wa hadhara uliofanyika mapema leo jioni jimboni kwake,kwenye uwanja wa shule ya msingi Kiwakala,mkoani Lindi.Mh Nape aliwashukuru Wananchi wake kwa kumpigia kura za kutosha na hatimae akachaguliwa kuwa mwakilishi wao Bungeni,akawashukuru kwa mapokezi makubwa waliompa na kumuonesha ni kiasi gani bado wanampena na kumuhitaji kama kiongozi wao mpambanaji katika kuwaletea maendeleo.

''Kilichonitoa machozi ni heshima kubwa mlionipa akina Mama,Mlilala chini,makataka nipite juu yenu,si ambalo nililitegemea,Nawashukuru sana,Niwaahidi nitafanya kazi kwa nguvu zangu zote,kuwatumikieni,usiku na mchana,nitaikumbuka heshima hii mlionipa na sitoisahau",alisema Mh Nape huku sauti yake ikiendana na hisia ya kutoa chozi mbele ya umati mkubwa uliokuwepo pale uwanjani. 

Mh,Nape alizungumza mambo mbalimbali yakiwemo ya kuiletea maendeo jimbo la Mtama,kuzitatua changamoto zilizopo kama vile  Maji,Barabara,Elimu na Afya,amesema katika maeneo hayo atayasimamia kwa spidi kubwa kwa sababu amepata muda wa kutosha wa kuanza kuwahudumia wananchi wa jimbo lake na kuhakikisha anatimiza yale yote aliyokwisha waahidi wakati wa kampeni.

Pia amewataka Wananchi hao kuungana na kuwa kitu kimoja na kuweka itikadi za kisiaza pembeni na kuhakikisha wanashirikiana katika kuhakikisha jimbo la Mtama linapiga hatua kimaendeleo.
Baadhi ya Wananchi na Wafuasi wa chama cha CCM wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza Mbunge wa jimbo lao,Mh Nape Nnauye mapema jioni ya leo.
Mbunge wa Jimbo la Mtama,Mh Nape Nnauye akipita juu ya migongo ya baadhi ya akina Mama walioamua kulala chini ili kiongozi huyo apite juu yao,ambapo imeelezwa kuwa imefanywa vile ikiwa ni sehemu ya heshima kubwa waliompa pamoja na upendo walionao kwa Mbunge wao kwa kusimamia ukweli.Kitendo hicho kilisababisha Mh.Nape ashindwe kujizuia na kuanza kutoa machozi.
Sehemu ya Umati wa watu wakishangilia kwa pamoja mara baada ya Mh Nape kupanda jukwaani na kuianza kuimba nyimbo kwa pamoja huku wakicheza sambamba na shangwe za hapa na pale uwanjani hapo
Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza Mbunge wao Mh Nape,alipowasili jimboni humo mapema leo kwa lengo la kuwashukuru kwa Kumchagua kuwa mwakilishi wao mzuri na pia kuzungumza mipango yao mbalimbali ya kuliletea maendeleo jimbo lake.

KAGERA SUGAR V/S JKT RUVU WATOSHANA NGUVU KAITABA KWA SARE YA 0-0

$
0
0
Kikosi cha Timu ya JKT Ruvu kilichoanza kupambana na Timu ya Kagera Sugar.
Kikosi cha Timu ya Kagera Sugar kilichoanza dhidi ya Timu ya JKT Ruvu leo kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba na kutoshana nguvu kwa kutoka sare ya 0-0.
Mchezaji wa JKT Ruvu Hassan Dilunga akiwa chini ya ulinzi wa Wachezaji wa Kagera Sugar.
Rashid Mandawa mchezaji wa zamani wa Kagera Sugar akijiandaa kuingia wakati wa kipindi cha pili cha mchezo huo kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Vodacom. Picha/Habari na Faustine Ruta - Bukoba
Mchezaji chipukizi Mbaraka Yusuph (kushoto) wa Kagera Sugar akiambaa na mpira huku beki wa JKT Ruvu akimkimbiza kipindi cha pili.


MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA ATOA TUZO ZA RAIS KWA WAZALISHAJI BORA WA VIWANDA 2016

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amelitaka Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) kuongeza kasi katika uwekezaji na uzalishaji wa bidhaa zenye ubora nchini ili tufike tunakotaka yaani uchumi wa viwanda ifikapo 2025.

Akizungumza katika hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016, Makamu wa Rais alisema kwamba Serikali inatambua mchango mkubwa wa sekta binafsi katika kukuza uchumi na kwamba mambo ambayo yamekuwa yakilalamikiwa mengi yanatafutiwa ufumbuzi.

Alisema mwaka wa kwanza wa Serikali ulikuwa ni wa kazi nyingi na hivyo serikali ilikuwa ikitafuta fedha na kwamba sasa wametulia na wataleta nafuu kwa mujibu wa sheria na matakwa ya sasa ya kukuza uchumi.

Alisema Serikali ipo tayari kufanyakazi na wenye viwanda kwa sababu inaamini mchango mkubwa wa sekta binafsi katika kuondoa umaskini, kukuza ajira na kuimarisha mwelekeo kwenda katika uchumi wa kati.


Makamu wa Rais ambaye hotuba yake ilizungumzia mafanikio na changamoto zinazokumba sekta binafsi katika kutekeleza wajibu wake, amesema kwamba serikali ya awamu ya tano inatambua changamoto hizo na imechukua hatua kadhaa kuhakikisha kwamba zinamalizwa.
Hatua hizo ni pamoja na ujenzi wa miundombinu kama bandari na reli na pia kuwapo kwa kamati inayoangalia kero zinazosumbua sekta ili serikali ifanye maamuzi.

Kwa sasa kuna Kamati inayoangalia namna bora ya kuboresha mazingira ya biashara inayofanyakazi chini ya Wizara ya Viwanda , Bisahara na uwekezaji na inakaribia kumaliza kazi yake na kuikabidhi Serikalini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akihutubia wakati wa hafla ya utoaji waTuzo za Rais za Mzalishaji Bora wa Viwanda kwa mwaka 2016 zilizofanyika kwenye Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akimkabidhi mshindi wa jumla Tuzo za Rais za Mzalishaji Bora wa Viwanda kwa mwaka 2016 Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Bw. Devis Deogratius (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa Tuzo za Rais za Wazalishaji Bora wa Viwanda kwa mwaka 2016.

ZAIDI YA WATU 70 WAOKOLEWA LEO KUTOKANA NA MAFURIKO YALIYOTOKANA NA MVUA KUBWA

$
0
0
Katikati ya Makazi ya watu Eneo la Nyakanyasi Mitumbwi imefanya kazi
Okoa okoa ikiendelea eneo la Nyakanyasi Mjini Bukoba leo hii.
Wakaazi wa hapa Tangu usiku saa 9 waliondoka!
Mkazi wa Omukigusha akisaidiwa kuvutwa juu baada ya kuanguka shimoni asubuhi leo kwenye mufda wa saa nne. Picha na habari na Faustine Ruta.







YANGA YAICHAPA MC ALGER 1-0 UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Obrey Chirwa akiwania mpira na Beki wa MC Alger ya nchini Algeria, Hachoud Abdullman, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, unaochezwa hivi sasa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda kwa  bao 1-0 lililowekwa kimyani na Thaban Kamusoko.


Na Zainab Nyamka  Globu ya Jamii
WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya kimataifa ya hatua ya mtoano ya kombe la Shirikisho Yanga wamefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya MC Alger ya Algeria.
Mchezo huo uliopigwa leo majira ya saa 10 Alasiri katika dimba la Uwanja wa Taifa ukichezeshwa na mwamuzi kutoka Burundi Louis Hazikumana.

Kipindi cha kwanza kilianza kwa Kila upande kusaka goli la kuongoza lakini umakini wa safu ya ushambuliaji ya Yanga iliyokuwa ikiongozwa na Mzambia Obrey Chirwa ilishindwa kutumia nafasi walizozipata.
Mpaka mapumziko timu zinaingia vyumbani, matokeo yalikuwa ni 0-0. Kipindi cha pili kilianza kwa MC Alger kulisakama lango la Yanga lakini umakini wa safu ya ulinzi ilikuwa makini na kuondosha hatari langoni mwao.
Kocha George Lwandamina anafanya mabadiliko ya kwanza na kumtoa Deus Kaseke ambapo mabadiliko hayo yanaleta tija na katoka dakika ya 61 Thaban Kamosoku anaipatia Yanga goli la kwanza.
Yanga walianza kubadilika na kuendelea kulisakama goli la MC Alger lakini Chirwa anakosa umakini na kukosa magoli ya wazi.
Baada ya matokeo hayo, mechi ya marudiano inatarajiwa kuwa April 15 nchini Algeria ambaoo Yanga inatakiwa kuhakikisha wanatoka na ushindi au sare ya aina yoyote ili kufuzu kuingia hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho.
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Obrey Chirwa akiongoka na mpira mbele ya Mabeki wa Timu ya MC Alger ya nchini Algeria, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, unaochezwa hivi sasa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. 
 Wachezaji wa Timu ya MC Alger ya nchini Algeria wakimdhibiti Mshambuliaji wa pembeni wa Timu Yanga, Hassan Kessy, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, unaochezwa hivi sasa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. 
 Mchezaji wa Yanga, Thaban Kamusoko akijirabu kuchukua mpira mguuni mwa Beki wa Timu ya MC Alger ya nchini Algeria, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, unaochezwa hivi sasa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. 

BODI YA MAZIWA TANZANIA KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI KUONGEZA IDADI YA NG'OMBE WA MAZIWA KUFIKIA MILIONI 1.5

$
0
0
Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) (wa pili kushoto) akizungumza na Waandishi wa Habari katika moja ya mikutano yake na Vyombo vya Habari.

Na Ismail Ngayonga - MAELEZO

BODI ya Maziwa Tanzania (TDB) imeandaa Mpango Mkakati  wa ushirikiano na Sekta Binafsi ili kuongeza idadi ya ng’ombe wa maziwa kufikia Milioni 1.5 hatua inayolenga kuongeza wa soko la uzalishaji wa mazao ya maziwa katika nchi za Ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Hayo yamesemwa jana Jijini Dar es Salaam na Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa Nchini, Nelson Kilongozi wakati wa mahojiano katika kipindi maalum cha TUNATEKELEZA kinachorushwa hewani na Shirika la Utangazaji Nchini (TBC) na kuratibiwa na Idara ya Habari (MAELEZO).

Kilongozi alisema taasisi hiyo imeandaa mkakati huo wa miaka 5 kuanzia mwaka 2018-23 ili kuhakikisha kuwa viwanda vya Tanzania vinakuwa na uwezo mkubwa wa kusindika maziwa na kushindana na nchi nyingine za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya katika uuzaji na usambazaji wa mazao ya maziwa katika ukanda wa Jumuiya hiyo.

“Kwa sasa Tanzania ina jumla ya Ng’ombe wa maziwa 782,000 kati ya ng’ombe Milioni 28 waliopo, hivyo hawatoshelezi mahitaji yetu, lengo letu ni kushirikiana na sekta binafsi ili kuhakikisha kuwa tasnia ya maziwa inaleta tija inayokusudiwa” alisema Kilongozi.

Kwa mujibu wa Kilongozi alisema uzalishaji wa maziwa nchini kwa sasa ni lita Bilioni 2.1 kwa mwaka ambapo asilimia 70 yanatokana na ng’ombe wa asili, ambapo hata hivyo imekuwa ni vigumu kutoa elimu kwa wafugaji wake kutokana na changamoto ya kuhama mara kwa mara kwa ajili ya kutafuta malisho.

 Aliongeza kuwa kuwa mpaka sasa kuna jumla ya viwanda 82 vyenye uwezo wa kusindika lita laki 652,000, na hivyo Bodi hivyo imejipanga katika kuhakikisha kuwa inaongeza hamasa kwa wawekezaji kwa ajili ya kujenga viwanda vidogo na vya kati ili kulinda ubora wa maziwa ya Tanzania.

“Changamoto iliyopo sasa ni kukosekana kwa vituo vya ukusanyaji wa maziwa pindi yanapozalishwa kwa kuwa vituo hivyo havina vifaa vya kupoozea maziwa pindi yanazalishwa kabla ya kufikishwa kiwandani” alisema Kilongozi.

Alisema Bodi hiyo imekuwa ikitoa elimu kwa wafugaji kuzingatia kanuni za ufugaji bora ikiwemo kuwa na mbegu bora zenye uwezo wa kuzalisha kiasi kikubwa cha cha maziwa ili waweze kujiongezea kipato sambamba na kuimarisha afya.

Akifafanua zaidi Kilongozi alisema Bodi hiyo pia imeendelea kuhamasisha wananchi kujenga tabia ya kunywa maziwa kwa, ambapo kwa mwaka huu wataanzisha Programu maalum ya uhamasishaji unywaji wa maziwa katika mikoa 6 nchini.

Aliitaja Mikoa hiyo kuwa ni Arusha, Kilimanjaro, Dodoma, Iringa, Njombe na Mbeya, ambapo pamoja na mambo mengine program hiyo imelenga pia kukabiliana na magonjwa ya udumavu yanayowakabili watoto wadogo katika mikoa mbalimbali nchini.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI APRIL 9,2017

VIJANA AFRIKA WATAKIWA KUIMARISHA UMOJA ULIOPO

$
0
0
 Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe Maudline Cyrus Castico akizungumza wakati wa kufunga kongamano la Vijana barani Afrika lililoandaliwa na Taasisi ya Unogozi Instute na kuwakutanisha vijana zaidi ya 45 ambao walipata muda wa kukaa na kujadili mustakabali wa maendeleo ya bara la Afrika.


aidha Mh. Castico amewaasa wa Vijana kuacha kukata tamaa na maisha na kujiwekea imani ya kuwa wao ndio viongozi wa Mataifa haya ya Afrika na kuwaomba kuendeleza umoja wetu ambao umeachwa na wasisi ambao walipigania uhuru.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Insitute, Profesa Joseph Semboja akizungumza kabla ya kumakaribisha mgeni rasmi kufunga warsha hiyo ya Vijana Afrika.
 Baadhi ya washiriki wakifurahi mara baada ya kusikiliza maneno mazuri kutoka kwa mgeni rasmi
Vijana wakinyoosha mikono juu kama ishara ya umoja wao katika maendeleo ya Bara la Afrika
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images