Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1640 | 1641 | (Page 1642) | 1643 | 1644 | .... | 3282 | newer

  0 0


  Na Dotto Mwaibale

  WATUMIAJI wa Stendi ya Mabasi ya Mbagala Rangitatu jijini Dar es Salaam wameiomba Manispaa ya Temeke kuboresha miundombinu ya stendi hiyo katika kipindi hiki cha mvua ili kuondoa adha wanayokabiliana nayo ya kujaa maji.

  Ombi hilo limetolewa Dar es Salaam jana na wafanyabiashara na madereva wanaotumia stendi hiyo wakati wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu changamoto hiyo waliyonayo ya kujaa maji hasa katika kipndi hiki cha mvua za masika.

  Mfanyabiashara ndogo ndogo katika stendi hiyo, Afidh Abdallah alisema katika kipindi hiki cha mvua stendi hiyo imekuwa ikijaa maji na kusababisha matope hivyo kuwa kero kwao.

  "Mvua ikinyesha hatuwezi kufanya biashara katika stendi hii tunashindwa kuzunguka kufuata wateja" alisema Abdallah.

  Abdallah alisema kwa kutumia fedha wanazolipa ushuru kila siku manispaa hiyo inaweza kuwawekea hata molamu kwa kipindi hiki cha mvua ili kupunguza madimbwi ya maji wakati wakisubiri kujenga miundombinu ya kudumu.

  Mama Lishe katika stendi hiyo Mwajabu Mohamed alisema maji yanapo jaa katika stendi hiyo wateja wao wamekuwa wakishindwa kufika kupata chakula kutoka maeneo mengine kwa kuhofia madimbwi na matope yanayokuwepo.

  Said Khatibu ambaye ni dereva wa basi la Manshallah linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na mikoa ya kusini alisema wakati huu wa mvua changamoto kubwa inayokuwepo eneo hilo ni kushindwa kupata nafasi ya kupakia na kushusha abiria kutokana na maji yanayojaa.
  Kijana akisukuma tolori huku akipita kwenye matope katika Stendi ya mabasi ya Mbagala Rangitatu jijini Dar es Salaam jana. Watumiaji wa stendi hiyo wameomba Manispaa ya Temeke kuwawekea miundombinu mizuri ili kuruhusu maji kupita katika kipindi hiki cha mvua.
  Muonekano wa stendi hiyo katika kipindi hiki cha mvua.
  Wafanyabiashara wakiendelea na biashara zao kwenye stendi hiyo.


  0 0
  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, Suleiman Nchambi amewataka wananchi kuwa kichocheo cha miradi ya maendeleo katika maeneo yao bila kujali msingi ya tofauti zao.

  Nchambi alisema hayo jana wakati akiongoza kikao cha Kamati ya Mfuko wa Jimbo kilichofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ambapo jumla y ash. Milioni 82 zinatarajiwa kutolewa kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

  Katika kikao hicho kilichohudhuria pia na madiwani, watendaji mbalimbali na viongozi wa dini alisema wananchi wanaoibua miradi ya maendeleo na Serikali kupitia Mfuko wa Jimbo inawapelekea fedha ili zitumike kufanya miradi hiyo.

  Alisema viongozi wa ngazi za kata wakiwemo madiwani na watendaji wana nafasi ya kuhamasisha wanancho wao kushiriki katika shughuli za maendeleo na kutoa elimu kuhusu fedha za mfuko huo.Mbunge huyo alibainisha kuwa katika mwaka huu fedha zinazotarajiwa kutolewa katika jimbo hilo zitasaidia katika kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata mbalimbali. 
  Mbunge wa Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, Suleiman Nchambi akifungua kikao cha Kamati ya Mfuko wa Jimbo kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Kishapu.
  A 1
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akisisitiza jambo wakati akizungumza wakati hicho kikao hicho.
  A 2
  Wajumbe wa Kamati ya Mfuko wa Jimbo kutoka kushoto, Grace Chamila, Mh. Regina, Salma Kalebo na Thomas Ng’ombe wakifuatilia kikao hicho.
  A 5
  Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kishapu ambaye ni Diwani wa Kata ya Uchungani wilayani humo, Paul Makolo akitoa uzoefu wake kuhusu namna ya fedha za Mfuko wa Jimbo zinavyofanya kazi wakati wa kikao hicho.
  A
  Washiriki wa kikaao hicho wakiwemo madiwani, watendaji kata, vijiji, wenyeviti wa vijiji, maafisa tarafa na viongozi wakifuatilia kikao hicho.


  0 0


  0 0
 • 04/07/17--02:03: Article 15


 • 0 0


   Muonekano wa Kiwanja. Ni Kuanzia mwanzo wa Picha mpaka mwisho wa Ukuta upande wa kushoto
  Mwanzo wa Picha Mpaka kwenye ukuta wa Ghorofa kule 

  Kiwanja Kipo KIGAMBONI KIBADA
  Ukubwa wa Kiwanja ni Mita za Mraba (Sq. Meter) 1088
  Kiwanja kina hati safi na hakina mgogoro
  Bei ni Milioni 65 Maongezi kidogo yapo na Kiwanja hiki kinauzwa Na Mwenye Nacho - Karibu mwenye Uhitaji. Biashara Maelewano
  Kwa Mawasiliano 0786 821 613


  0 0

  Timu ya majimaji imeendelea kufanya mazoezi ya kufa mtu katika uwanja wa Majimaji kujiwinda na Afrika Lyion huku Kocha msidizi wa Majimaji Habibu Kondo asema mchezo wao wa jumamosi utakuwa mgumu sana.

  0 0

  Na Fredy Mgunda,Iringa


  Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amewataka wananchi wa wilaya ya iringa kuacha tabia ya kuamini na kujihusisha na maswala ya imani za kishikina pamoja na kujichukulia hatua mikononi.

  Ameyasema hayo baada ya kuwepo kwa taarifa za mtu mmoja mkazi wa kijiji cha mikong’wi kata ya kihologota wilaya ya iringa ameuawa na watu wasiojulikana kwa kukatwa kichwa na kutelekeza kiliwili chake.

  “Kwanini watu wajichukulie hatua mkononi wakati serikali,jeshi la polisi,mahakama,makanisa na misikiti huku ndio unaweza kutatuliwa shida zako zote na haya mambo ya kishikina serikali haiamini da nasikitika sana kwa tukio la leo ni baya sana”alisema Kasesela.

  Kasesela alisema kama wilaya wamepokea taarifa hiyo kwa masikitiko na kuwataka wananchi wote kutojichukulia sheria mikononi kwa kuwa serikali haiamini uchawi na kwamba ameliagiza jeshi la polisi kufanya uchunguzi ili kubaini aliyehusika na tukio hilo.

  “Wilaya ya Iringa ilikuwa imetulia sasa yameanza mambo ya kuuwana kwa keli lazima jeshi la polisi lifanye uchunguzi kwa kina kubaini nini kinachoendelea katika kijiji cha mikong’wi na lazima tukomeshe na kuwa elimu wananchi kutojihusisha na maswala ya kishirikina kwa kuwa serikali haiamini sala hilo”alisema Kasesela 

  Kasesela ameeleza kuwa tukio hilo limetokea asubuhi ya leo na kumtaja aliyefariki dunia kuwa ni hasani nyalusi mkazi wa kijiji cha mikong’wi tarafa ya Isman mkoani Iringa.

  Aidha Kasesela amewaomba viongozi wa dili mbalimbali kutoa elimu ya mungu na kukemea maswala ya kishikina kwa kuwa yanapunguza nguvu kazi za wananchi.

  Kwa upande wake afisa mtendaji wa kijiji cha Mikong’wi Majorino Muyinga Anaeleza kuwa Mnamo tarehe 06/04/2017 huko kitongoji cha Utitiri kijiji cha Mikong’wi kata ya Kihorogota tarafa ya Isimani wilaya ya Iringa vijijini Mkoani Iringa alisema kuwa Hassan Nyalusi alikutwa akiwa ameuawa nje ya nyumba yake na mtu/watu wasiofahamika na mwili ukiwa hauna kichwa na uchunguzi wa daktari umefanyika na kukabidhiwa kwa ndugu wa marehehemu kwa taratibu za mazishi laiki mtu mmoja Jackson Nyalusi anashikiliwa na polisi kuhusishwa na mauaji haya,bado upelelezi unaendelea.
  Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake hii leo


  0 0


  Na.Vero Ignatus .Arusha
   
  Wananchi wametakiwa kulipa kodi ya majengo ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza baadae kutokana na Sera ya serikali inayisema kila mwananchi inayomraka takiwa kulipa kodi ya majengo.


  Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake na kusema kuwa yapo makundi matatu yanayoaanishwa katika ulipwaji wakodi hizo


  Hata hivyo amesema makundi hayo ni Pamoja na wale ambao nyumba zao hazijapimwa wala kufanyiwa tathimini,kundi la pili in wale ambao nyumba zao zimepimwa lakini hazijafanyiwa tathimini kundi la mwisho no wale ambao nyumba zao zimepimwa na kufanyiwa tathimini.


  Hata hivyo amesema kundi la kwanza linatakiwa kulipa shilingi elfu 15,000kwa mwaka,ambapo kundi la pili wanatakiwa kulipa waendelee kulipa Kwa utaratibu waliokuwa wanautumia toka awali,kundi la tatu gharama zao zipo juu kulingana na tathimini mpya iliyofanyika mwaka 2015-2016.


  Vilevile Gambo ametoa onyo kali Kwa wanasiasa wenye tabia ya kupita Kwa wananchi na kuwapotosha kuhusiana na ulipaji wa kodi hiyo amesema hatua Kali za kisheria zitachukuliwa endapo watambaini mmoja wapo.


  Nae meneja wa TRA mkoa wa Arusha Pili Mbaruku amesema kuwa wamejiwekea utaratibu mzuri kuhakikisha wanashirikiana na watendaji wa mitaa ili zoezi la ukusanyaji liwe jepesi kwao badala ya kupanga foleni TRA jambo ambalo litawqchukulia muda wananchi.

  Amewataka wananchi kujitokeza Kwa umoja ili kurahisisha zoezi hilo na kuweza kutekeleza agizo la serikali kulipa kodi.
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza na waandishi wa habarimapema  leo ofisini kwake .Picha na Vero Ignatus Blog.

   Meneja wa TRA Mkoa wa Arusha Pili Mbaruku akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mapema leo katika mkutano ulioitishwa na mkuu wa mkoa  kwa waandishi wa habari.Picha na Vero Ignatus Blog.


  0 0


  Mbunge wa Jimbo la Busega, Mkoani Simiyu, Dk Raphael Chegeni ambaye kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu wa ndani na nje ya nchi amefanikiwa kujenga bweni moja la wasichana katika Sekondari ya Ngasamo ikiwa ni jitihada za kuwanusuru watoto wa kike na ukatishaji masomo unaotokana na mimba pamoja na vishawishi bvingine mbalimbali.
   Vitanda katika moja ya vyumba vya bweni hilo.
  MBUNGE wa Busega Dr. Raphael Chegeni amefanikisha ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya sekondari Ngasamo.

  Bweni hilo lenye uwezo wa kuhudumu wanafunzi wa kike 48 litasaidia wasichana kupata muda wa kujisomea na kujiepusha na adha ya kutembea mwendo mrefu wa kuja na kurudi shuleni.

  Kitendo hicho imekuwa kikwazo  kwa baadhi kuangukia mtego wa kukatisha masomo katokana na bodaboda Au lift kuwasababishia mimba na hivyo kukatisha masomo yao.

  Mbunge huyo ameweka mpango kujenga mabweni kwa shule zilizo katika mazingira hatarishi zikiwemo Malili, Mkula, Kabita na Sogesca.

  Aidha amewashukru wadau wakiwemo ubalozi wa Ireland, Canada, Tanapa na Serikali kwa kuchangia jitihada hiz0.

  0 0


  Katika jitihada za kuhakikisha TMA inashiriki kikamilifu katika kuongeza pato la Taifa, Mamlaka iliandaa mafunzo ya siku tano ambayo yalikuwa yana lengo la kutoa uelewa wa sheria, kanuni na taratibu za ununuzi wa umma katika kuboresha utendaji wa kazi hasa katika usimamizi na utekelezaji wa shughuli za ununuzi na usimamizi wa mikataba.

  Akizungumza wakati akifunga rasmi mafunzo hayo, Mkurugenzi mkuu wa TMA, Dkt Agnes Kijazi alisema wakuu wa idara na vitengo wafanye maboresho kwenye maeneo yaliyokuwa na changamoto na kitengo cha ununuzi waboreshe utendaji wa kazi sambamba na kusimamia vizuri taratibu zote zinazohusu ununuzi kwa mujibu wa sheria na kanuni zake, kama ilivyoelekezwa na washauri waelekezi kutoka PSPTB ili kuisaidia Mamlaka yetu kutekeleza sera na mikakati ya Serikali ya kupunguza gharama za ununuzi kwa lengo la kuboresha pato la Taifa.

  Aidha Dkt. Kijazi aliishukuru Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) kwa kukubali kutoa wataalam katika upande wa sheria ya ununuzi na kuahidi kuendelea kushirikiana na Bodi hiyo kila inapobidi.

  Kwa upande wa Bodi ya utaalam wa ununuzi na ugavi Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Bwana Paul Bilabaye kwa niaba ya Mtendaji Mkuu alitoa pongezi kwa TMA kwa uamuzi wa kutoa mafunzo haya kwa Viongozi wanaohusika na utekelezaji wa Sheria ya Ununuzi na Ugavi.

  Mafunzo haya yamejenga uwezo kwa Idara tumizi, Kamati za tathmini, Kitengo cha Ununuzi na Ugavi pamoja na Bodi ya Zabuni katika kutekeleza majukumu yake.

  Mafunzo hayo ya siku tano yamefanyika katika ukumbi wa mikutano, Makao Makuu ya TMA, Ubungo Plaza na kuhudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu, Wakuu wa idara na wakuu wa vitengo vyote pamoja na wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Mamlaka ya Hali ya Hewa.


  Imetolewa na

  Ofisi ya Uhusiano

  MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

  0 0

  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeipongeze Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kuendesha warsha ya siku tatu kuhusu upasuaji wa matundu madogo (laparoscopic surgery) kwa madaktari kutoka hospitali mbalimbali nchini.

  Warsha hiyo ilianza jumatano na imemalizika leo Ijumaa na kuwashirikisha madaktari kutoka hospitali ya za jijini Dar es Salaam zikiwamo Kairuki, Tumaini, Regency na Agha kan. Madaktari wengine ni kutoka hospitali za umma zikiwamo Hospitali ya Temeke, Amana pamoja na hospitali za mikoa ya Mbeya, Mwanza, Arusha, Morogoo na Dodoma.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akimkabidhi cheti cha ushiriki Dk. Paul Kisanga wa Hospitali ya Selian mkoani Arusha leo.

  Pongezi hizo zimetolewa leo na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba wa Wizara hiyo Dk. Dorothy Gwajima kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara, Dk. Mpoki Ulisubisya wakati akifunga warsha hiyo.

  Dk  Gwajima amewataka washiriki wa warsha hiyo kupeleka ujuzi waliojifunza kwa madaktari wengine ili kupunguza msongamano wa wagonjwa wanakwenda kutibiwa katika hospitali ya Muhimbili.

  “Kwa niaba ya wizara napenda kuipongeza Muhimbili kwa kuandaa mafunzo haya, sisi wizara tunawaunga mkono na msifikiri tumewasahau la hapana kwani tunatambua uwezo wa madaktari. Heshima ya hospitali itabaki pale pale kwani Muhimbili kitovu cha uwanzishwaji wa HospitaOceac road, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na Taasisi ya Mifupa ya Moi,” amesema Dk Gwajima.
  Mkurugenzi wa Huduma za Tiba katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima akifunga warsha ya siku tatu iliyolenga kuwajengea uwezo madaktari nchini kuhusu upasuaji wa matundu madogo (laparoscopic Surgery).

  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru amewashukuru madaktari kutoka hospitali za binafsi na umma kwa kushiriki kwenye mafunzo hayo.

  “Tumeanzisha mafunzo haya na napenda kuwahakikishia tutaendelea kuandaa warsha kwa kada nyingine ili kuwajengea uwezo madaktari wa hospitali za mikoa na wilaya nchini,”amesema Profesa Museru.

  Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kinamama na Uzazi, Profesa Rafique Parkar ameishauri uongozi wa Muhimbili kuendelea kutoa mafunzo hayo na kuendesha ufapasuaji wa njia ya matundu madogo kwa wagonjwa waliopo mikoani kwani wengi wao hawana fursa ya kupatiwa huduma hiyo.
   
  Daktari bingwa wa Magonjwa ya Kinamama na Uzazi, Profesa Rafique Parkar (kushoto) akimfanyia upasuaji mmoja wa kinamama mwenye matatizo ya uzazi leo. Kulia ni Dk. Vicenti Tarimo akishirikiana na Profesa Parkar.

  Washiriki walikabidhiwa vyeti baada ya mafunzo hayo kufungwa.

  Katika hatua nyingine, wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa kutumia njia ya matundu madogo wanaendelea vizuri na baada ya afya zao kurejea katika hali ya kawaida wataruhusiwa kurejea nyumbani.

  Wagonjwa waliofanyiwa upasuaji hadi leo wamefikia wanane.


  0 0


  0 0

   Katibu Mkuu wa Kamati ya Miss Tanzania, Bosco Majaliwa (kulia) akimkabidhi fedha taslim kiasi cha Sh. Milioni mbili (2Mil.), Mrembo mwenye taji wa Tanzania kwa Mwaka 2016 - 17, Diana Edward ikiwa ni sehemu ya stahiki yake aliyotakiwa kuipata baada ya kutwaa taji hilo, mapema mwaka jana. Fedha hizo zimetolewa na Mmoja wa Wadhamini wa shindano hilo, ambao ni Duka Maarufu kwa Uuzaji wa vito vya thamani la Gift Jewellers lililo ndani ya Jengo la City Mall, Jijini Dar es salaam. Kamati ya Miss Tanzania mwezi jana iliahidi mbele ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuwa ingeweza kumalizana na Mrembo huyo mapema mwezi huu na sasa wamekamilisha deni hilo kupitia kwa Mdhamini wao ambaye ni Gift Jewellers. Makabidhiano hayo yamefanyika leo Aprili 7, 2017. Kulia ni Meneja Masoko wa Duka la Vito vya thamani la Gift Jewellers, Faudhia Abdulrahman.

  Mrembo mwenye taji wa Tanzania kwa Mwaka 2016 - 17, Diana Edward (katikati) akipokea zawadi kutoka kwa Meneja Masoko wa Duka la Vito vya thamani la Gift Jewellers, Faudhia Abdulrahman (kushoto) wakati wa hafla fupi ya kumkamilishia fedha za zawadi zake kiasi cha shilingi Milioni 2 alizokuwa akidai Mrembo huyo kwa Kamati ya Miss Tanzania baada ya kushinda taji hilo mapema mwaka jana. Fedha hizo zimetolewa na Mmoja wa Wadhamini wa shindano hilo, ambao ni Duka Maarufu kwa Uuzaji wa vito vya thamani la Gift Jewellers lililo ndani ya Jengo la City Mall, Jijini Dar es salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Kamati ya Miss Tanzania, Bosco Majaliwa.
  Mrembo mwenye taji wa Tanzania kwa Mwaka 2016 - 17, Diana Edward akionyesha sehemu ya zawadi yake aliyopewa kutoka Duka la Vito vya thamani la Gift Jewellers muda mfupi baada ya kukabidhiwa kitita chake. Wengine pichani toka kushoto ni Katibu Mkuu wa Kamati ya Miss Tanzania, Bosco Majaliwa, Meneja Masoko wa Duka la Vito vya thamani la Gift Jewellers, Faudhia Abdulrahman pamoja na Mkuu wa Itifaki na Nidhamu wa Miss Tanzania, Albert Makoye.
   
   Mrembo mwenye taji wa Tanzania kwa Mwaka 2016 - 17, Diana Edward akipozi kwa picha nje ya Duka la Vito vya thamani la Gift Jewellers.


  0 0


  0 0

  A team of twelve Local Engineers from Tanesco have concluded a 2-week Training with Pietro Fiorentini in Italy and Hungary
  In an effort to address the shortage of skills and experience in the Energy & Power sector in the country, Director of Pietro Fiorentini Tanzania Mr. Abdulsamad Abdulrahim has been working very hard to ensure that local engineers, senior managers and operation workers are empowered by building valuable skills, and helping to ensure the sustainable development of the country.
  The need for skills and training are the driving force behind twelve engineers from the Tanzania Electric Supply Company  (Tanesco) attending two-weeks tailor-made training programme at Pietro Fiorentini Italy and Hungary facilities ended 7th April 2017
  Pietro Fiorentini is an Italian company founded in 1940.  The company is operating in Tanzania and has physical presence in other 96 countries worldwide. Its core and operating based on Oil & Gas Upstream, Midstream, Downstream and maintenance.  It is a manufacturing company in Oil & Gas equipment, among other things; design a complete range of solutions for oil and gas streams with collaboration.
  The two-week training provided a complete approach to developing knowledge in various different disciplines including technical design, engineering, assembling, operation, health & safety, maintenance and troubleshooting. At the completion of their training, the team were given official ceritificates and had oporunity for the first time to participate in the Research & Development (R&D) facilities where they witnessed the development of new products while observing engineers tasked with applied research in technological fields for future product development.
  The engineers said that they were extremely pleased with the relevance of tailor-made training offered by Pietro Fiorentini, saying it would bring value to their career, and help Tanesco build more capable and skilled engineers. After completing their training in Italy and Hungary, Tanesco engineers returned to Tanzania very determined to share their knowledge with their fellow engineers and teams they work with.
  Mr Abdulrahim encouraged other investors and reputable companies in the country to follow his example by building Local Content capacity as part of their investments in the country quoting

  that "Any investment that's not geared towards growing Local Content, knowledge and adding value to our people in Tanzania is deceptive investment”. The team will be landing in Daressalaam this weekend from Italy.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Clifford Tandari (kushoto) akisaini mkataba na Naibu Mkurugenzi wa Kampeni  ya China Industrial Forum, Wang Xiangncheng ikiwa ni Makubaliano ya kushirikiana katika sekta ya uwekezaji. Makubaliano hayo yamefikiwa kifuatia ziara iliyoratibiwa na Balozi wa Tanzania nchini China, Balozi Mbelwa Kairuki pamoja na Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Tanzania kupitia TIC.Katika hafla hiyo iliyoandaliwa na TPSF na kudhaminiwa na Exim Bank, Kaimu Mkurugenzi wa TIC alielezea kuwa mkataba huo ni muendelezo wa ushirikiano wa nchi hizi mbili ulioanza zamani na kusisitiza uendelee ili kuleta tija kwa nchi zote mbili. Ametoa wito kwa wawekezaji kuja kuwekeza kwenye sekta za Viwanda, Kilimo, umeme na mafunzo ya ufundi stadi.

  0 0


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akiweka shada la Mauwa katika Kaburi la Marehemu Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume baada ya Dua ya Khitma iliyofanyika Ijumaa  katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini zanzibar.
  Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Mama Samia Suluhu Hassan akiweka shada la Mauwa katika Kaburi la Marehemu Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume baada ya Dua ya Khitma iliyofanyika leo katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini zanzibar.
  Viongozi mbali mbali akiwemo Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhaj Dkt.Amani Abeid Karume (wa pili kushoto) wakiwa katika kisoma Hitma ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Abeid Amani Karume iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar,ambapo Viongozi mbali mbali wa Kitaifa wamehudhuria katika Hitma hiyo
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiongoza kisomo cha Hitma ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Abeid Amani Karume iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar,ambapo Viongozi mbali mbali wa Kitaifa wamehudhuria katika Hitma hiyo.


  0 0

older | 1 | .... | 1640 | 1641 | (Page 1642) | 1643 | 1644 | .... | 3282 | newer