Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1639 | 1640 | (Page 1641) | 1642 | 1643 | .... | 3282 | newer

  0 0

   Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoji kutoka kulia ni Naibu Kamishna Billy Mwakatage, Kaimu Kamishana Usalama dhidi ya moto Fikiri Salla, Mhasibu Mkuu Chakala, Kaimu Kamishna wa Operesheni Christom Manyologa na Kamishana Msaidizi Hamadi Muhando wakimfuatilia kwa karibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Charles Kichere hayupo pichani, alipofanya ziara katika Jeshi hilo mapema leo asubuhi tarehe 06/04/2017
   Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (kushoto) akimfuatilia kwa karibu huku akiandika, Kamishana MKuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Charles Kichere, Kamishna huyo aliambatana na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Bw. Richard Kayombo (kulia) alipofanya ziara Makao Makuu ya Jeshi hilo mapema leo Asubuhi.
   Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (kushoto) akimpatia zawadi ya Kalamu ya Jeshi yenye namba ya dharura 114, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Charles Kichere (kulia) mapema leo asubuhi alipofanya ziara Makao Makuu ya Jeshi hilo mapema leo asubuhi.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasilisha Makadirio ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa Fedha 2017/2018, bungeni mjini Dodoma Aprili 6, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   

  0 0

   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akisalimiana na Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Mhe.Tundu Lissu  walipofika na Ujumbe kutoka TLS kumtembelea ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma.
   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akizungumza na Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Mhe.Tundu Lissu  na  ujumbe wake walipomtembelea ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma.
   Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Mhe.Tundu Lissu  akimueleza jambo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai alipofika kumtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma pamoja na viongozi wengine wa TLS.
   Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Mhe.Tundu Lissu  akimuonesha kitabu chenye nyaraka kadhaa za Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS)  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai alipofika kumtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma pamoja na viongozi wengine wa TLS.
   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akipokea  kitabu chenye nyaraka kadhaa za Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS)kutoka kwa Rais wa chama hicho Mhe.Tundu Lissu wakati viongozi wa Chama hicho walipofika kumtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma pamoja na viongozi wengine wa TLS.
   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) wakiongozwa na Rais wao Mhe.Tundu Lissu  walipofika kumtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma pamoja na viongozi wengine wa TLS. 

  (PICHA NA OFISI YA BUNGE.)

  0 0


  • ATOA SIKU 10 KWA YEYOTE ANAYEJIHUSISHA NA BIASHARA YA MOVIE, KUDOWNLOAD KAZI ZA WASANII KUACHA MARA MOJA

  • BAADA YA SIKU 10, OPARESHENI KUBWA KUANZISHWA JIJI ZIMA KUWABAINI WOTE WANAOFANYA BIASHARA HIYO.

  • AFISA BIASHARA KUFANYA TADHMINI YA MADUKA HALALI YA KAZI ZA WASANII WA FILAMU JIJINI NA KUWABAINI WOTE WANAOUZA KAZI FEKI ZA WASANII WAZAWA WA FILAMU.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda amepiga marufuku kuanzia leo tarehe 06 Aprili, 2017 uuzwaji, uingizwaji na usambazaji wa CD, flash, DVD na filamu za ngono katika mkoa wa Dar es Salaam.

  Hali kadhalika Mhe. Makonda ametoa siku kumi kwa wote wanaojihusisha na biashara isiyo halali ya ku-download filamu na kazi za wasanii jijini waache mara moja kwani baada ya siku hizo, ofisi yake kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kanda Maalum wataendesha msako wa kuwakamata wote watakaokuwa bado wanajihusisha na biashara hiyo isiyonufaisha wasanii na Kuzorotesha pato la Taifa.

  Mhe. Makonda pia amemuagiza Afisa Biashara wa Mkoa kufanya tathmini ya haraka kubaini ni maduka mangapi yanayouza mikanda ya filamu kihalali jiji Dar es Salaam.

  Mhe. Makonda ametoa maagizo hayo baada ya kutembelewa ofisini kwake na wawakilishi wa wasanii na wasambazaji, watengenezaji wa Filamu jijini Dar es Salaam, ambao walifikisha kilio chao cha kutonufaika na kazi zao za uzalishaji na usambazaji wa filamu nchini kutokana na kuwepo kwa maharamia wanaoziiba kazi hizo kwa kuzi-download kisha kuzisambaza kimagendo kwa bei ya kutupa bila ridhaa yao na zikiwa hazina stempu ya mamlaka ya mapato!

  Wasanii hao wakiongozwa na Jacob Steven - JB, Vicent Kigosi - Ray walimuomba Mkuu wa Mkoa kuingilia kati tatizo lao hilo kwa maslahi ya tasnia nzima ya sanaa nchini.
   Mkuu wa Mkoa Mh,Paul Makonda akijadiliana jambo na Kamanda Sirro
   Kikao kikendelea
  RC Makonda akiwa katika picha na Msanii wa Filamu aitwae Rado.

  0 0


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali kwa kushirikiana na kampuni ya Viettel ya Vietnam inatekeleza mradi wa ujenzi wa miundombinu ya mawasiliano vijijini ambao umefanikisha kuweka miundombinu ya mtandao wa intaneti kwenye shule 417 hapa nchini. 

  Amesema mradi huo ambao unatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2015-2017, umewezesha pia ofisi za Halmashauri za Wilaya 123, Hospitali za Wilaya 74, Vituo vya Polisi vya Wilaya 131 na Ofisi za Posta 68 kufikiwa na mtandao huo. 

  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Aprili 6, 2017) Bungeni mjini Dodoma wakati akiwasilisha taarifa ya mapitio ya utekelezaji wa kazi za Serikali kwa mwaka 2016/2017 na mwelekeo wa kazi za Serikali kwa mwaka 2017/2018 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake ukiwemo Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2017/2018 

  Waziri Mkuu amesema katika mwaka 2016/2017, baadhi ya kazi zilizofanyika kwenye sekta ya mawasiliano ni pamoja na ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano; Mradi wa Anuani za Makazi na Postikodi; na kuanzisha huduma ya kituo cha Jamii Centre kitakachorahisisha utoaji wa huduma muhimu katika kituo kimoja. Huduma hizo ni kulipa pensheni, ankara na huduma za kibenki. 

  “Sekta ya mawasiliano inatekeleza Programu ya Miundombinu ya Kikanda ambayo inahusisha Mradi wa Shule Mtandao (e-school), Mradi wa Video Conference ambao unahusisha ununuzi, usimikaji na ufungaji wa vifaa vya TEHAMA katika mikoa 26 na taasisi za Serikali,” amesema. 

  0 0


    Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) unatoa pongezi kwa Wabunge wa Bunge Tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutumia haki yao ya kidemokrasia, kikatiba na kikanuni kufanikisha uchaguzi wa Wabunge wa Afrika Mashariki uliofanyika tarehe 4/4/2017 bungeni mjini Dodoma.

  Pia unawapongeza Wabunge waliochaguliwa kuiwakilisha nchi yetu katika Bunge la Afrika Mashariki, tunawataka kuwa wazalendo, waadilifu, wachapakazi na wenye kutanguliza maslahi ya nchi yetu Tanzania kwanza.

  Pia, UWT imeridhishwa na hatua za mchakato wa uchaguzi huo ndani ya Bunge na inapongeza demokrasia pana, komavu na shirikishi iliyooneshwa na wabunge kwa kupiga kura ya HAPANA kwa wagombea waliotokana na CHADEMA kwa sababu uteuzi wao haukuzingatia misingi ya demokrasia, uwakilishi wa Kitaifa wala jinsia.

  Uteuzi uliofanywa na CHADEMA hata baada ya kushauriwa, unadhihirisha dharau kubwa na kutothamini mchango wa Wanawake wa Tanzania katika maendeleo ya nchi yetu.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhe. Alexander Mnyeti akihojiwa mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge baada ya kuitikia wito wa kamati hiyo, Bungeni mjini Dodoma leo, kujibu tuhuma zinazomkabili za kuingilia Haki, Uhuru na Madaraka ya Bunge kutokana na Matamshi aliyoyatoa mapema mwaka huu Wilayani Arumeru Mkoani Arusha yaliyokuwa na madai ya kuidharau Bunge. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)
  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhe. Alexander Mnyeti akihojiwa mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge baada ya kuitikia wito wa kamati hiyo, Bungeni mjini Dodoma leo, kujibu tuhuma zinazomkabili za kuingilia Haki, Uhuru na Madaraka ya Bunge kutokana na Matamshi aliyoyatoa mapema mwaka huu Wilayani Arumeru Mkoani Arusha yaliyokuwa na madai ya kuidharau Bunge. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara ya Dodoma-Babati yenye urefu wa kilometa 188.15 ambayo inajengwa kwa kiwango cha lami na kusisitiza kuwa ujenzi huo utakamilika mwezi Oktoba mwaka huu.

  Akizungumza mkoani Manyara mara baada ya kukagua barabara hiyo, Waziri Prof. Mbarawa amewataka Makandarasi M/S China Railyway Seventh Group anayejenga barabara ya Mela-Bonga KM88.8 na M/S China Henan International Cooperation Group anayejenga barabara ya Mayamaya-Mela Km 99.35 kuzingatia viwango vya ubora katika ujenzi wao kama ilivyo kwenye mkataba, ili idumu kwa muda mrefu na kwa manufaa ya vizazi vijavyo.  "Barabara hii ni kiungo muhimu kwa mikoa ya Arusha, Manyara, Dodoma, Iringa na nchi za Ukanda wa Afrika, hivyo naamini kukamilika kwake kutaibua fursa nyingi za uchumi na kuchochea maendeleo ya wananchi", amesema Profesa Mbarawa.  Aidha, Waziri Mbarawa amewataka wananchi wa mkoa wa Manyara na Dodoma kutumia fursa ya kukamilika kwa barabara hiyo kujiendeleza kiuchumi na kuilinda ili iweze kudumu kwa muda mrefu kwani ujenzi wake una gharama kubwa.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), akifuatilia taarifa ya ujenzi wa mradi wa barabara ya Mela-Bonga KM 88.8 inayojengwa kwa kiwango cha lami, wakati alipokagua barabara hiyo mkoani Manyara, leo, Kushoto ni Mhandisi Mshauri wa mradi huo Eng. Kini Kuyonza.
   Muonekano wa sehemu ya barabara ya Mela-Bonga KM 88.8 inayojengwa kwa kiwango cha lami na kuunganisha mikoa ya Dodoma na Manyara. Barabara hiyo inayojengwa na  Mkandarasi M/S China Railyway Seventh Group, imebaki KM 18 kukamilika.
   Mhandisi Mshauri wa ujenzi wa barabara ya Mela-Bonga KM88.8, Eng. Kini Kuyonza, akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), tabaka la juu la kokoto kabla barabara hiyo kuwekwa lami, mkoani Manyara, leo.
   Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Manyara Eng. Bashiru Rwesingisa, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu ujenzi wa mradi wa barabara ya Mela-Bonga KM 88.8  inayojengwa kwa kiwango cha lami. Barabara hiyo inaunganisha mikoa ya Manyara na Dodoma ambayo ni sehemu ya barabara kuu ya Afrika Great North Road, inayoanzia Capetown (Afrika kusini) hadi Cairo (Misri).
   Muonekano wa Daraja la Kelema lenye urefu wa mita 220, linaounganisha Wilaya ya Chemba na Kondoa katika barabara kuu ya Dodoma-Babati likiwa katika hatua za mwisho za ujenzi.
  Muonekano wa barabara ya Mayamaya-Mela KM 99.35 ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami upo katika hatua za mwisho kukamilika. Barabara hiyo inaunganisha mikoa ya Manyara na Dodoma ambayo ni sehemu ya barabara kuu ya Afrika Great North Road, inayoanzia Capetown (Afrika kusini) hadi Cairo (Misri).

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  Muhadhiri wa chuo kikuu cha Afya na Tiba Muhimbili,Profesa Projestine Muganyizi akifafanua jambo mbele ya wadau na watafiti mbalimbali wa Afya,alipokuwa akitoa mrejesho wa utafiti walioufanya mkoani Njombe,uliohusu Afya ya Mama na Mtoto,jijini Dar.

  Prof.Muganyizi alisema kuwa walikwenda Mkoani Njombe na kukutana na Wafanyakazi na viongozi wa Afya mkoani humo,mwaka jana mwezi wa sita na kufanya utafiti katika suala zima la Afya ya Mama na Mtoto.

  Katika utafiti huo,anaema walibaini mambo makuu manne,kwanza 
  ilikuwa suala la usafi katika hospitali zenyewe,kwa mazinginra ya nje vituo vingi vilikuwa vikionekana ni visafi,lakini kwa ndani ilibainika kuwa na mapungufu makubwa hasa katika eneo la usafi,Pili ni Katika uelewa wa kutoa huduma ya Afya,huduma za Mama na Mtoto zilikuwa na Mapungufu,wafanyakazi wengi walikuwa hawana weredi wa kutosha,

  Anasema na kuongeza kuwa eneo la tatu ni katika suala la ufautiliaji wa hali ya Mama akiwa Mja mzito,vituo vingi havikuwa na uelewa wa kutumia hizo kadi ,akina Mama wengi walikuwa hawafuatiliwa kwa ukaribu wakiwa na uchungu, Mwisho ni suala la kuweka Kumbukumbu za Mama akiwa kwenye uchungu,ikabainika vituo vingi hazitumii zile kumbu kumbu na jambo lingine ni suala la Huduma inayotolewa kwa Mama Mzazi,Je meridhika vipi huduma aliyopewa kutoka kwa wale wahudumu wa afya,Iakabainika kuwa akina Mama wengi walikiri wazi kuwa walihudumiwa vizuri.

  Shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia watoto (UNICEF) lilipokea mrejesho huo,na kwa kuwa Shirika hilo lilikuwa likisaidia kuendeleza huduma ya Afya ya Mama na Mtoto,tayari limeanza kuzifanyia kazi changamoto zote zilizo ainishwa kwenye utafiti huo,ikiwemo na kuwaelemisha wahusika wote katika suala zima la Afya la kupunguza vifo vya mama na Mtoto.
  Baadhi ya wadau na Watafiti wa Afya wakifuatilia mrejesho wa utafiti uliofanywa mkoani Njombe,uliohusu Afya ya Mama na Mtoto.
  Mmoja wa Wakilishi kutoka UNICEF,akichangia mrejesho wa utafiti huo uliofanywa mkoani Njombe Mwaka jana, UNICEF wamekuwa wakishiriki kwa kiasi kikubwa katika kusaidia kuendeleza huduma ya Afya ya Mama na Mtoto mkoani Njombe.
  Mhadhiri wa chuo kikuu cha Afya na Tiba Muhimbili,Profesa Projestine Muganyizi akichangia jambo mbele ya wadau na watafiti mbalimbali wa Afya,mara baada ya kutoa mrejesho wa utafiti walioufanya mkoani Njombe,uliohusu Afya ya Mama na Mtoto,jijini Dar.
  Mkurugenzi wa kuratibu na kutunza utafiti kutoka Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu nchini Tanzania (NIMR),Dkt Julius Massanja akitoa ufafanuzi wakati wa kusikiliza Mresho wa Utafiti uliofanyika Mkoani Njombe uliohusu Afya ya Mama na Mtoto.Dkt Massanja alisema kuwa katika utafiti huo .kazi ya mwanzo ilikuwa ni kujua na kubaini tatizo gani,hivyo Kufuatia mrejesho wa utafiti huo wa Afya ya Mama na Mtoto uliofanywa Mkoani Njombe,Shirika la UNICEF limeanza kurekebisha mambo mbalimbali yaliyobainishwa katika tafiti hiyo ikiwemo na kuwaelemisha wahusika wote katika suala zima la Afya la kupunguza vifo vya mama na Mtoto. 

  0 0


  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imendelea kuwajengea uwezo madaktari wa ndani na nje ya hospitali kwa kufanya upasuaji wa njia ya matundu madogo (laparoscopic surgery).

  Miongoni mwa madaktari walioshiriki kwenye upasuaji huo ni kutoka hospitali ya za jijini Dar es Salaam zikiwamo Kairuki, Tumaini, Regency na Agha kan. Madaktari wengine ni kutoka hospitali za umma zikiwamo Hospitali ya Temeke, Amana pamoja na hospitali za mikoa ya Mbeya, Mwanza, Arusha, Morogoo na Dodoma.

  Lengo ni kuwaongezea ujuzi madaktari hao ili waendelee kufanya upasuaji wa kutumia njia ya matundu madogo kwa wagonjwa mbalimbali.
  Upasuaji huo unafanywa na madaktari wa muhimbili kwa kushirikiana na Daktari Bingwa aliyebobea katika magonjwa ya kinamama na uzazi, Profesa Rafique Parkar ambaye amekuwa akifanya upasuaji huo nchini Afrika Kusini, Kenya na nchi mbalimbali barani Afrika.

  Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kina mama na Uzazi, Vicenti Tarimo wa hospitali ya Muhimbili amesema wagonjwa wanne wamefanyiwa upasuaji na kwamba wengine watatu walikuwa wakiendelea kufanyiwa upasuaji huo leo.
   Daktari Bingwa aliyebobea katika Magonjwa ya Kinamama na Uzazi, Profesa Rafique Parkar akifanya upasuaji wa kutumia njia ya matudu madogo kwa kushirikiana na madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili leo. 
   Baadhi ya madaktari kutoka katika Hospitali za umma na binafsi nchini wakifuatilia mubashara upasuaji wa njia ya matundu madogo uliofanyika leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Nasri Bakari, Dar es salaam

  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo amekabidhiwa madarasa matatu yaliyokamilika na mkandarasi katika shule ya msingi Msakuzi.

  Makabidhiano ya madarasa hayo ambapo ujenzi wake umegharimu shillingi millioni sitini na mbili (62 Mil) yamefanyika katika shule hiyo iliyopo katika Kata ya Mbezi Manispaa ya Ubungo.

  Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mkurugenzi Kayombo amesema kuwa amefurahi kuona ujenzi wa madarasa hayo umemalizika kwa wakati na kutoa ahadi mbalimbali katika shule hiyo.

  "Kwanza napenda nichukue fursa hii kukupongeza mkandarasi kwa kumaliza ujenzi ndani ya muda tuliokubaliana kwa hakika umeonyesha ni jinsi gani unajali kazi yako" Alisema MD Kayombo.

  MD Kayombo amesema kuwa mpaka kufikia kesho tarehe 06/04/2017 madawati 120 yanapaswa kufikishwa kwenye shule hiyo huku akisema kuwa kila darasa yanapaswa kukaa madawati arobaini(40) kila chumba katika vyumba vitatu vya madarasa alivyokabidhiwa.

  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisaini kitabu cha wageni Mara baada ya kuwasili shule ya Msingi Msakuzi katika dhifa ya makabidhiano ya madarasa
  Madarasa matatu ya shule ya Msingi Msakuzi yaliyokabidhiwa kwa MD Kayombo

  Baadhi ya watumishi wa Manispaa ya Ubungo walioshiriki kwenye dhifa ya makabidhiano ya madarasa ya shule ya Msingi Msakuzi


  0 0


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Walimu wa Skuli za msingi na Sekondari za Serikali na Binafsi katika Mikoa ya Pemba leo katika Ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro Wilaya ya Chakechake Pemba akiwa katika ziara yake kisiwani humo.
    Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mmanga Mjengo Mjawiri mara alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) kuzungumza na Walimu wa Skuli za msingi na Sekondari za Serikali na Binafsi katika Mikoa ya Pemba  leo katika Ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro Wilaya ya Chakechake, akiwa katika ziara yake kisiwani humo.
    Baadhi ya  Wakuu wa Wilaya za Mikoa ya Pemba na Afisa Tawala wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipozungumza na  Walimu wa Skuli za msingi na Sekondari za Serikali na Binafsi katika Mikoa ya Pemba leo katika Ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro Wilaya ya Chakechake, akiwa katika ziara yake kisiwani humo.
   Baadhi ya Walimu wa Skuli za msingi na Sekondari za Serikali na Binafsi katika Mikoa ya Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipozungumza nao leo katika Ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro Wilaya ya Chakechake, akiwa katika ziara yake kisiwani humo(Picha na Ikulu).

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  Na: Nuru Juma & Husna Saidi – MAELEZO
  WATANZANIA waalikwa kushiriki katika mdahalo baina ya Diaspora na  wenzao waishio nchini ili kujadili nafasi ya Diaspora katika uchumi wa nchi, unaotarajiwa kufanyika tarehe 11 na 12 April katika ukumbi wa Mzalendo Pub Jijini Dar es Salaam.

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa kampuni ya  Ikolo Investiment Bw Maggid Mjengwa wakati akiongea na waandishi wa habari, leo jijini Dar es Salaam.

  Mjengwa amesema kuwa Mdahalo huo umeandaliwa kwa lengo mahususi la kuwakutanisha kwa pamoja wadau wa maendeleo kwa ajili ya kusukuma mbele jitihada za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda.

  “Lengo la mdahalo huu ni kuwakutanisha watanzania waliopo Ughaibuni, watanzania waliokua wakiishi Ughaibuni na kwa sasa wamerudi na watanzania ambao hawakuwahi kufika Ughaibuni ili kuweza kujadili maendeleo ya nchi” alisema Mjengwa.

  Aliongeza kuwa katika mdahalo huo pia utatumika kama sehemu ya maadhimisho ya miaka kumi ya kuanzishwa kwa mtandao wa Mjengwa Blog, mtandao ambao kimsingi ndiyo umekuwa daraja la kuwakutanisha Diaspora.

  “Mdahalo huu ni pamoja na kuadhimisha miaka kumi ya Mjengwa Blog hivyo tumeona kuyafanya maadhimisho hayo kuwa ya tofauti kwa utofauti  kuwajumuisha watanzania kujadili kwa pamoja mambo kadhaa kuhusu uchumi kwa lengo la kufanikisha maendeleo ya nchi kwa haraka zaidi.” Alisisitiza.

  Nae Mratibu wa Vikoba Kimataifa Mwinyirwaka Hatibu alisema  mdahalo huo pia  utahusisha na mafunzo ya ujasiriamali kwa watanzania ili kuweza kufanikiwa kimaisha binafsi na kufanikiwa kwa taifa kiujumla.

  “Katika kuhakikisha Tanzania inanufaika na Diaspora,yapata miaka mitatu sasa Serikali imekuwa ikiendesha mikutano kama hii kila mwezi wa nane kwa kuwaita watanzania waishio nje ya nchi kujadili uchumi na maendeleo ya nchi na kwa mara ya mwisho mkutano kama huu ulifanyika Zanzibar” alisema Hatibu.

  Hata hivyo aliwasihi wanahabari na wananchi kwa ujumla kufika katika tukio hilo kwani watapata fursa ya kukutana na watu kutoka mataifa mbalimbali na kuweza kujifunza vitu vingi kutoka kwao.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Ikolo Investment Ltd Bw. Maggid Mjengwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mdahalo wa Diaspora kuhusu uchumi na maendeleo ya Taifa leo Jijini Dar es Salaam. Mdahalo huo utafanyika tarehe 11 mwezi April katika Ukumbi wa Mzalendo Pub uliopo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mratibu wa Vikoba Kimataifa Bw. Mwinyirwaka  Hatibu.
   Mratibu wa Vikoba Kimataifa Bw. Mwinyirwaka  Hatibu akifafanua jambo na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mdahalo wa Diaspora kuhusu uchumi na maendeleo ya Taifa leo Jijini Dar es Salaam. Mdahalo huo utafanyika tarehe 11 mwezi April katika Ukumbi wa Mzalendo Pub uliopo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Ikolo Investment Ltd Bw. Maggid Mjengwa.
   Baadhi ya waandishi wa habari wakifatilia uongozi wa Ikolo Investiment LTD wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari kuhusu mdahalo wa Diaspora leo jijini Dar es Salaam. Picha na Frank Shija– MAELEZO.

  0 0

  Sir Jayantilal Keshavji "Andy" Chande KBE a.k.a Andy Chande (born 7th  of  May,  1928) who was a prominent Tanzanian businessman, philanthropist and a freemason,  has passed away at the Aga Khan hospital in Nairobi, Kenya early in the morning today. What a great life !   Sir Andy, Dar es salaam and Tanzania have a lot to thank you for.
  Among his many services to the nation, he was for a long time chairman of the board of the TANGANYIKA STANDARD (newspapers) limited,  one i worked for. He was also a great personal friend. At one time, he was a board member of 28 big firms like the RAILWAYS, HARBOURS, KIO LTD etc. 
  He will be remembered and missed for a very long time. 
   May his soul rest in peace. 
  Om Shant Shanti Shanti.

  By
  Asif Walji

  0 0

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimlaki balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Mhe. Roeland Van de Geer alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo April 6, 2017.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na  balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Mhe. Roeland Van de Geer alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo April 6, 2017.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifanya mazungumzo na Balozi wa Israel hapa nchini Mhe. Yahel Vilan alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo April 6, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea ujumbe maalumu toka kwa Waziri Mkuu wa Israel Mhe. Benjamin Netanyahu uliowasilishwa kwake na Balozi wa Israel hapa nchini Mhe. Yahel Vilan alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo April 6, 2017.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0  0 0  hag1
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizukumza na Makatibu Wakuu wa Ofisi yake nje  ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya kuhairishwa kwa mkutano wa 11 Aprili 6, 2017 wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Erick Shitindi, katikati Dkt.Hamisi Mwinyimvua (Sera na Uratibu) na Bi.Maimuna Tarishi (Bunge na Waziri Mkuu).
  hag2
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akipitia taarifa ya Kambi ya Upinzani Bungeni wakati wa Uwasilishwaji wake katika mkutano wa 11 wa Bunge la Bajeti kulia ni Naibu wake (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde.
  hag3
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akipongezana na baadhi ya wabunge nje ya Ukumbi wa Bunge wakati wa Bunge la Bajeti  kushoto kwake  ni Naibu wake  Mhe. Antony Mavunde (Kazi, Ajira na Vijana) na wa kwanza kulia ni Mhe. John Heche (Tarime).
  hag4
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akiwa na baadhi ya wabunge nje ya Viwanja vya Bunge Dodoma Aprili 6, 2017.

  (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU-DODOMA)

  0 0  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake Kinondoni,jijini Dar es salaam kuhusiana na  maandalizi ya tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika Aprili 16 kwenye uwanja wa Uhuru na kutumbuizwa na waimbaji wa muziki wa injili kutoka mataifa mbalimbali na nchini Tanzania.

  Msama amesema mwimbaji nguli kutoka nchini Afrika ya Kusini Solly Mahlangu atakuwa ni mmojawapo wa waimbaji kutoka nje ya nchi wakiwemo wengine kutoka nchini Kenya, Ameongeza kuwa tamasha hilo litafanyika pia katika mikoa ya Mwanza na Simiyu, hata hivyo tamasha hilo halitafanyika katika mkoa wa Dodoma kama ilivyotangazwa awali kutokana na uwanja wa Jamhuri ambao ulikuwa utumike siku hiyo kuwa na shughuli nyingeni. 
  Msama amesema kuwa katika tamasha hilo la Pasaka litakalofanyika katika Uwanja wa Uhuru,Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani,Mh.Mwigulu Nchemba,baada ya tamasha hilo kurindima jijini Dar litahamia Simiyu na jijini Mwanza ambako mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula .
  Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia taarifa iliyokuwa ikitolewa na Bw. Alex Msama katika mkutano huo.
  Baadhi ya Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama alipokuwa akisisitiza jambo kuhusiana na maandalizi ya tamasha la Pasaka

  0 0


older | 1 | .... | 1639 | 1640 | (Page 1641) | 1642 | 1643 | .... | 3282 | newer