Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

HALMASHAURI YA HANDENI YAZIPONGEZA SHULE KUMI ZA MSINGI NA SEKONDARI KWA KUFANYA VIZURI KWENYE MITIHANI YA DARASA LA SABA NA KIDATO CHA NNE 2016

$
0
0
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imepongeza na kutoa zawadi kwa shule kumi za Msingi na    moja Sekondari kwa kufanya vizuri kwenye mitihani ya darasa  la saba na kidato cha nne mwaka 2016. Zawadi hizo zilitolewa kwenye kilele cha maadhimisho ya juma la elimu yaliyofanyika kiwilaya Wilayani Handeni kwenye shule ya Msingi Kabuku nje.

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Handeni   ambaye pia alikuwa mgeni rasmi Mh. Godwin Gondwe aliwapongeza walimu na wadau wengine wa elimu kwa kazi nzuri wanazofanya na wanazoendelea kufanya katika kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora.

“elimu ni ufunguo wa maisha na kwamba Handeni hakuna mtoto mjinga, wazazi na walezi himizeni  watoto kutumia fursa ya Elimu bure inayotolewa na Raisi wa Tanzania” Alisema.

Aidha ameeleza kuwa atahakikisha fedha zinazohusu madai ya walimu  zinapofika  Halmashauri zinawafikia walengwa kwa wakati uliopangwa. Aliwataka wakuu wa shule na Maafisa elimu Kata kusimamia haki ya msingi ya wanafunzi kupata elimu wanayostahili.

Wakati huohuo amepiga marufuku watoto walio na umri wa kuwepo shuleni kuacha kuchunga mifugo hasa kwa siku za shule baada ya kubainika watoto wengi wa jamii ya wafugaji wanatumiwa kuchunga mifugo badala ya kwenda shule. 

Amewaonya wazazi na jamii ya wafugaji ambao wanakwamisha watoto kupata haki yao ya msingi ya kupata elimu na kwamba sheria itachukua mkondo wake kwa yeyote atakayebainika kwenda kinyume. Amewaeleza pia wazazi ambao wanawatoto waliovuka umri wa kwenda shule kupelekwa kwa utaratibu wa MEMKWA. 
  Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe akikabidhi zawadi kwa mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Tewe iliyokuwa ya kwanza kiwilaya na ya sita kimkoa
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe na Mkurugenzi Mtendaji Bw William Makufwe wakisomewa namba na wanafunzi wa shule ya awali kabuku nje
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe na Mkurugenzi Mtendaji wakisikiliza mwanafunzi alipokuwa akielezea tense za somo la kiingereza 
 wanafunzi wa shule ya sekondari kabuku akielezea mifumo ya kibaiolojia Kwa viongozi.


SERIKALI KUTEKELEZA MRADI WA MAJI CHALINZE

$
0
0
Serikali kwa kushirikiana na  Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, Benki ya Maendeleo ya Waarabu(BADEA),Washirka wa Maendeleo (DPS), na Serikali ya India  kwa pamoja wametoa jumla ya Shillingi Billion 164 kawa ajili ya kutekeleza mradi wa maji Chalinze kwa awamu tatu.

Akijibu Swali Mbunge wa Chalinze (CCM) Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete lililouliza kuwa Wakazi wa Chalinze wamekuwa katika sintofahamu ya kukamilka kwa mradi wa maji Chalinze?

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Gerson Lwenge ameeleza kuwa Serikali ipo katika utekelezaji wa mradi huo na gharama za utekelzaji wake ni Shillingi Billioni 23.4 kwa awamu ya kwanza na Shillingi Billioni 53.7 kwa awamu ya pili ya mradi na kwa awamu ya tatu itagharimu Shillingi Billioni 86.9.

Ameongeza kuwa kukamilika kwa awamu ya kwanza na utekelezaji umekamilika na kwa awamu ya pili ya mradi huo jumla ya vijiji 88 vimenufaika na kupeleka hali ya upatikanaji wa maji katika mji wa Chalinze na Vitongoji vyake kufikia asilimi 88 ya wakazi wote waishio katika eneo lote linalopitiwa na mtandao wa maji.

“Mradi upo katika hatua nzuri na umekamilika kwa awamu ya kwanza na awamu ya pili ipo katika utekelzeaji na wanachi wameanza kunufaika na mradi huu kwa kupata huduma ya maji” alisisitiza Mhe. Lwenge.

Pia ameleza kuwa katika awamu ya pili vijiji 12 vya Mwindu,Visakazi, Lulenge, tukamisasa,Kinonko, Bwawani, Sinyaulime, Gwata, Ngerengere, Kidugalo, Kambi ya Kinonko na Sangasanga vitaanza kupata huduma ya maji ifikapo mwishoni mwa mwezi Aprili mwaka 2017 baada ya kukamilika kwa majaribio ya bomba kuu.

Vijiji vitatu vya Kwang’andu,kifuleta na Kwaruhombo vitaanza kupata maji mara baada ya mkandarasi kufanya maboresho ya pampu ambazo zimeonekana hazifanyi kazi kama inavyotakiwa  na mkandarasi huyo ameagizwa kuhakikisha pampu  hizo zinafanya kazi kabla ya Juni 2017.

Aidha kwa sasa Serikali inatekeleza mradi huu kwa awamu ya tatu ambapo upanuzi wa mtambo wa kuzalisha maji, ujenzi wa mabomba makuu ya kusafirisha maji (KM 115), Ujenzi wa mfumo wa manomba ya kusambaza maji(KM 1022), Ujenzi wa matanki makubwa 19 na ujenzi wa vituo 9 vya kuchotea maji na ujenzi wa vioski 351 vya kuchotea maji vinatekelzwa.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Gerson Lwenge akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha pili cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.

Wabunge, wasomi waja juu Chadema kutoenzi demokrasia uchaguzi EALA

$
0
0
WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na wasomi mbalimbali nchini wameeleza kushangazwa na chama cha upinzani nchini, Chadema, kushindwa kuenzi demokrasia na misingi ya haki kufuatia chama hicho kuwasilisha majina ya wagombea wawili tu katika nafasi zao mbili za ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA).

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Dodoma na wabunge hao na wasomi wengine mbalimbali wakati wa Mahojiano Maalum na Mwandishi wa habari hizi kuhusu uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki uliofanyika jana Mjini Dodoma.

Akizungumzia kuhusu Uchaguzi huo Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Amina Mollel alisema Bunge la Tanzania kama yalivyo Mabunge mengine duniani yameendelea kuzingatia suala la usawa wa kijinsia, na hivyo hatua ya Wabunge wa CHADEMA waliokuwa wawili tu katika nafasi mbili kukataliwa ilikuwa ni sawa.

Katika majina ya Chadema, hakukuwa na uwakilishi wa kijisia wala pande mbili za Muungano, ambapo badala yake, wagombea wote wa chama hicho walikuwa wa jinsia moja na kutoka mkoa na wilaya moja.

Mbunge Mollel ameongeza kitendo kilichofanywa na CHADEMA ni kukiuka kanuni za Bunge hilo na la Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambayo yote kwa pamoja yamesisitiza suala la usawa wa kijinsia katika nafasi za uteuzi wa Chombo hicho cha kutunga Sheria.

“Serikali ya awamu ya nne ilijitahidi sana katika kusimamia suala la usawa wa kijinsia kwa kuwa hata katika maazimio ya Mkutano wa Wanawake uliofanyika Jijini Beijing China mwaka 1995 ulizitaka nchi zote ulimwenguni kuheshimu haki na usawa wa wanawake” alisema Mhe. Mollel.

Aliongeza kuwa pamoja na idadi kubwa ya wagombea waliofikia 400, CCM ilipata majina ya wagombea 12 kuwania nafasi sita hatua iliyodhirisha kuwa Chama hicho kimekomaa kisiasa tofauti na vyama vingine vya upinzani vilivyopo nchini.

Naye Mbunge waSingida Mjini (CCM) Musa Sima aliwapongeza Wabunge wapya wa Bunge la Afrika Mashariki  na kusifu ukomavu wa kisiasa ulionyeshwa na Wabunge wa Bunge la Tanzania wakati wa mchakato wa uteuzi wa Wabunge.

Mmoja wa wagombea wa nafasi za uongozi katika chaguzi za nyuma wa Chadema Bi Esther Wassira amekaririwa na mitandao ya kijamii akilaumu mfumo wa uchaguzi ndani ya chama hicho kwa kutozingatia misingi ya demokrasia.

Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliyeomba jina lake lisiwekwe hadharani akiwa na ngazi ya cheo cha Profesa ametabiri kuzidi kutokea kwa hatima ya Chadema katika siasa za kitaifa.

“Ni chama ambacho kinadidimia. Kila siku ukitazama misingi ya kuanzishwa kwake, sera zilizowafanya kuwepo walipo na sababu za kufika walipo zote wameanza kuzisigina,” alisema msomi huyo aliyebobea katika sayansi za siasa.

Benki ya EXIM yapata faida ya bilioni 83.6

$
0
0
 BENKI ya Exim imepata faida ya Tsh bilioni 83.6 (kabla ya kodi) kwa mwaka wa fedha 2016 ikiwa imejumuisha faida ya Tsh bilioni 46.4 ya kuuza hisa ilizowekeza. Faida itokanayo na uendeshaji wa shughuli mbalimbali za kibenki ni Tsh 37.2 Bilioni.

Mapato yatakanayo na riba yaliongezeka kwa asilimia 25 mpaka Tsh 90.9 bilioni, ikiwa imechangiwa na ongezeko la mikopo pamoja na mkazo katika amana zenye riba nafuu.

Aidha katika kipindi hicho hicho, mapato yatokanayo na tozo mbalimbali za huduma za kibenki yaliongezeka kwa asilimia 14 mpaka Tsh bilioni 35.7 ukilinganisha na Tsh bilioni 31.3 kwa mwaka uliopita. Ukuaji huu umechangiwa kwa kiasi kikubwa na ufanisi kwenye utoaji huduma kwa wateja wakubwa na wale wa kati.

Faida hiyo imeongeza mtaji wa benki kufika Tsh bilioni 227 na kuongeza uwezo wa benki kuweza kufanya miamala ya kibiashara mikubwa zaidi.

Katika kuongeza uwezo wa kutoa huduma nzuri kwa wateja na kujiandaa kwa ukuaji wa kasi, Benki ya Exim ametelekeza miradi mbalimbali ya kiteknolojia. “Nina furaha kubwa kuwataarifu kwamba kati ya miradi 8 ya kiteknolojia, miradi 7 imemalizika kwa mafanikio”. Alisema Afisa Mkuu wa fedha wa benki hiyo Bw. Selemani Ponda na kusisitiza kuwa kutokana na ukuaji wa teknolojia, benki itaweza kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake.

Utekelezaji wa miradi hiyo kwaajili ya kubadilisha mifumo ya kiutendaji umepelekea uwekezaji mkubwa katika rasilimali watu na teknolojia na hivyo kusababisha gharama za uendeshaji kupanda. Katika taarifa yake ya fedha jumla ya gharama ya uendeshaji ilipanda  kwa asilimia 24 hadi kufikia Tsh bilioni 99.

Benki ya Exim imejiandaa kuwahudumia wateja wa kada zote kutokana na kuongezeka kwa uwezo wa kuhudumia wateja wote mara baada ya kutekeleza miradi ya kiteknolojia na kuongezeka kwa mtaji.

Akizungumzia mafanikio ya benki tanzu za Exim zilizopo katika nchi tatu: Komoro, Djibuti na Uganda, Bw. Ponda alisema kuwa Komoro na Djibuti wamefanya vizuri na kuweza kupata faida mara 3 ya mwaka uliopita na kufikia Tsh bilioni 8 kutokana na ukuaji mzuri wa uchumi na huduma bora. 

Na benki tanzu mpya ya Uganda ilipata hasara ndogo ya Tsh milioni 177, na inategemewa kufanya vizuri zaidi mwaka huu baada ya kuteleza mikakati mipya baada ya Benki ya Exim kununua hisa zaidi ya 58.6%.  

Chief Financial Officer of Exim Bank Tanzania, Mr Selemani Ponda as he shares with journalists that Exim Bank Group has achieved a pre-tax profit of TZS 83.6 Billion for the year 2016. The Group recorded a 25% growth in net interest income, fueled by asset book growth, better yields and reduction in cost of funds. Seated beside him are Senior Finance Manager, Joseph Mrawa [Left] and Deputy Finance Officer, Issa Hamisi [Right].

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZUNGUMZA NA MAWAKALA WA PEMBEJEO ZA KILIMO

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na mawakala wa pembejeo za kilimo kwenye ukumbi wa Spika, bungeni mjini Dodoma Aprili 5, 2017. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji na wapili kulia kwake ni Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvu Tete Ole-Nasha. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mkuu wa Mkoa wa Arusha afanya mkutano watendaji wa Kata na Mitaa

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akizungumza na watendaji wa Kata na Mitaa(hawapo pichani) wakati wa Kikao kazi cha Ukusanyaji wa Kodi ya Majengo.
  Wajumbe wa Kikao wakifuatilia kikao kazi walichofanya na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Mtendaji wa Mtaa wa Panga, Kata ya Kati Bi. Maria M. Singo(Aliyesimama) akichangia hoja kwenye kikao kazi kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kuhamasisha ukusanyaji wa Kodi ya Mapato.

TAFITI YA HAKI ELIMU YABAINI ELIMU BURE IMEKUWA NA MAFANIKIO MAKUBWA

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Rais John Pombe Magufuli alipongia madarakani alitangaza elimu bure kwa shule za msingi na sekondari.

Taasisi ya Haki Elimu ni moja ya taasisi ambayo imefanya utafiti katika swala la elimu na kuja na majibu ambayo yameonesha kuwepo kwa mafanikio makubwa katika swala la elimu bure.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mapema leo,Mkurugenzi Mtendaji wa Haki Elimu, John Kalage ametaja kuwa tafiti hiyo imebaini kuwa Sera ya elimu bila malipo imesababisha ongezeko la wanafunzi wa darasa la kwanza hasa kwa shule za msingi.

“kulikuwa na ongezeko la asilimia 43 na asilimia 10 kwa shule za Sekondari ,hali iliyosababisha msongamano madarasani na pia kuongezeka kwa uwiano wa mwalimu kwa mwanafunzi kwa darasa la kwanza hadi kufikia mwalimu mmoja kufundisha wanafunzi 164 kwa wastani badala ya wanafunzi 45 wanaotakiwa” amesema Kalage.

Amesema kuwa utafiti huo ambao ulifanyika Wilaya za Njombe ,Mpwapwa , Sumbawanga ,Kilosa , Korogwe ,Tabora Mjini na Muleba kwa kuhusisha shule 28 na Msingi na 28 za Sekondari.
Mkurugenzi wa Haki Elimu nchini , John Kalage akizungumza na wadau mbalimbali wakati wa hafla ya uzinduzi wa tafiti juu ya mpango wa elimu bure nchini.
Aliyekuwa Mwenyekiti ya bodi ya taasisi ya Haki elimu nchini, Profesa Martha Qorro akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ripoti ya elimu bure iliyofanyiwa utafiti na tasisi ya Haki eleimu nchini
Baadhi ya washiriki wakisikiliza ripoti hiyo kwa makini.

SERIKALI YASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO WA ANGA

$
0
0
Serikali ya Tanzania na Uganda zimesaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano (BASA), katika usafiri wa anga utakaowezesha nchi hizo kutoa huduma bora za anga na kufungua fursa za kibiashara kwa wananchi wake.

Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo jijini Arusha, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema mkataba huo utaruhusu ndege za nchi hizo mbili kutua na kuruka bila vikwazo vyovyote katika nchi hizo.

"Naamini ushirikiano huu utaboresha huduma zinazotolewa na Mamlaka za usafiri wa Anga na hivyo kuongeza viwango vya usalama wa usafiri huu", amasesema Prof. Mbarawa.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Sam Kutesa, amesisitiza kuwa mkataba huo ni muendelezo wa ushirikiano mwema baina ya Tanzania na Uganda na hivyo kuchochea maendeleo ya uchumi kwa raia wa nchi hizo.

Ushirikiano wa Tanzania na Uganda ni sehemu ya mkakati wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuwezesha wananchi wake kunufaika na fursa za kijamii, kiuchumi, kiusalama na kiutamaduni.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Sam Kutesa (kushoto), wakisaini mkataba wa ushirikiano katika masuala ya anga baina ya nchi hizo mbili, jijini Arusha leo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), akibadilishana hati za makubaliano na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Sam Kutesa (kushoto), kuhusu ushirikiano katika masuala ya anga baina ya nchi hizo mbili, jijini Arusha leo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Sam Kutesa (kushoto), wakionesha hati zao za makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya anga baina ya nchi hizo, jijini Arusha leo. Mkataba huo utaimarisha huduma za usafiri na usalama wa anga.


Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

MANISPAA YA UBUNGO YAFANYA OPERESHENI MAALUM YA UKUSANYAJI MAPATO MANZESE

$
0
0
Kamati ya fedha na uongozi kwa kushirikiana na wakuu wa  idara na timu ya ukusanyaji mapato halmashauri ya Manispaa ya Ubungo wamefanya operesheni maalum ya kukagua leseni za biashara, leseni za vileo, kodi ya huduma ya jiji (city service levy), ushuru wa nyumba za kulala wageni ( hotel levy), ushuru wa  mabango, vibali vya ujenzi, TFDA,  ukusanyaji wa mapato na kuelimisha wafanyabiashara juu ya umuhimu wa kulipa kodi katika mitaa mbalimbali ya Kata ya Manzese.

Kamati hiyo inayoongozwa na mwenyekiti Mstahiki Meya Boniface Jacob na katibu ambaye ni Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndg. John Lipesi Kayombo kwa kushirikiana na watumishi hao imefanya  operesheni hiyo leo kwa lengo la kuhamasisha ulipaji wa  kodi, ada na tozo mbalimbali za Manispaa ya Ubungo.

Wakati wa  operesheni hiyo changamoto mbalimbali zimejitokeza zikiwemo wafanyabiashara kutokuwa na uelewa juu ya ukataji wa leseni, kutokukata leseni kwa wakati na kutokuweka leseni katika eneo la biashara.

Akizungumza wakati wa operesheni hiyo mwenyekiti wa kamati Mstahiki Meya Boniface Jacob aliwasisitiza wafanyabiashara kulipa kodi kwa wakati na hatimaye kuleta maendeleo katika Manispaa ya Ubungo na taifa kwa ujumla.

"Ndugu wafanyabiashara kulipa kodi ni wajibu wenu kwani itawasaidia ninyi wenyewe na vizazi vyenu na  unapolipa kodi ndipo tutaweza kujenga zahanati, shule, masoko na huduma muhimu katika Manispaa yetu" alisema Meya Boniface Jacob.

PROFESA MUHONGO AZINDUA JUKWAA LA NISHATI TANZANIA

$
0
0

Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo amesema nishati ya uhakika ya umeme itatokomeza umasikini nchini Tanzania ifikapo mwaka 2030.

Profesa Muhongo aliyasema hayo alipokuwa akizindua Jukwaa la Nishati Tanzania (TEP) pamoja na mkutano wa siku mbili kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu mapema leo jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo unaolenga kujadili upatikanaji wa nishati endelevu ya kutosha kwa bei nafuu kwa ajili ya uchumi wa viwanda Tanzania, unakutanisha wadau mbalimbali zikiwemo kampuni za utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi nchini kama vile Statoil, BG na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

Wadau wengine ni pamoja na kampuni za kuzalisha umeme kama vile Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Songas pamoja na mabalozi wa nchi mbalimbali, taasisi za kifedha na viongozi wa kiserikali.

Profesa Muhongo alisema kuwa Serikali imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha nishati ya uhakika inapatikana itakayopelekea Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kama Dira ya Maendeleo ya Taifa inavyofafanua. 
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ( wa tatu kutoka kulia) na Balozi wa Uholanzi Nchini, Jaap Frederiks ( wa pili kutoka kushoto) wakifurahia uzinduzi wa Jukwaa la Nishati Tanzania (TEP). Kushoto kabisa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Florens Luoga (katikati) wakifurahia jambo katika mkutano huo . Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo na kulia ni Balozi wa Uholanzi Nchini, Jaap Frederiks
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa mwakilishi kutoka Chuo cha Twente kilichopo nchini Uholanzi, Profesa Tom Veldkamp (kulia) mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi huo. Katikati ni Balozi wa Uholanzi Nchini, Jaap Frederiks

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati waliokaa mbele) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo ( wa pili kutoka kushoto waliokaa mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya washiriki wa mkutano huo. 

RAIS DKT MAGUFULI AAPISHA MAKATIBU WAKUU, MABALOZI NA KAMISHNA WA TRA IKULU, DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Leonard Akwilapo kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia Ikulu jijini Dar es salaam leo April 5, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Kitila Alexander Mkumbo kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Umwagiliaji Ikulu jijini Dar es salaam leo April 5, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Ave Maria Semakafu Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia Ikulu jijini Dar es salaam leo April 5, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Sylvester Ambokile Mwakinyuke kuwa Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Ikulu jijini Dar es salaam leo April 5, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Baraka Luvanda kuwa Balozi wa Tanzania nchini India Ikulu jijini Dar es salaam leo April 5, 2017 -Rais akimkabidhi nyezo za kazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Charles Edward Kichere kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Ikulu jijini Dar es salaam leo April 5, 2017.

RAIS MAGUFULI AAPISHA MAKATIBU WAKUU, MABALOZI NA KAMISHNA WA TRA

TANZANIA YAPANDA HADI NAFASI YA 135, BRAZIL YASHIKA NAMBA MOJA DUNIANI

$
0
0
SHIRIKISHO la Soka Duniani (FIFA) limetoa viwango bora vya soka duniani kwa nchi zote huku Brazil wakiwashika namba moja wakifuatiwa na Argentina na Ujerumani iliyoshika nafasi ya tatu.

Katika viwango hivyo bora vya soka, timu ya Misri iliweza kuingia katika 20 bora kwa kushika nafasi ya 19 na Senegal kushika nafasi ya 30 duniani.

Kulingana na ratiba ya mechi za Kirafiki za kalenda ya FIFA, Tanzania imefanikiwa kupanda kwa nafasi 22 kutoka 157 mpaka nafasi ya 135 .


Kwa upande wa nchi za Afrika Mashariki, Uganda imeendelea kuongoza lakini wakipanda  kwa nafasi 2 kutoka 74 mpaka 72 akifuatiwa na Kenya iliyo nafasi ya 78, Rwanda nafasi ya 117 na Burundi 141.

Viwango vingine vitatolewa Mei mwaka huu.


MATAIFA YA AFRIKA 10 YENYE VIWANGO BORA VYA FIFA AFRIKA MWEZI HUU . 

1. Misri ( 19 )

2. Senegal ( 30 )

3. Cameroon ( 33 )

4. Burkinafaso ( 35 )

5. Nigeria ( 40 )

6. Congo DR ( 41 )

7. Tunisia ( 42 )

8. Ghana (45 )

9. Ivory Coast ( 48 )

10. Morocco ( 53 )

MATAIFA 10  YENYE VIWANGO BORA VYA FIFA MWEZI HUU

1Brazili 

2.Argentina 

3.Ujerumani

4.Chile

5.Colombia

6.Ufaransa

7.Ubelgiji

8.Ureno

9.Uswisi

10.Hispania

NAIBU MEYA KUMBILAMOTO AUNGANA NA WANANCHI KUFUKIA SHIMO LILILOACHWA NA DAWASCO

$
0
0
Naibu Meya wa Manispa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akiwa amebeba toafali wakati wa zoezi la kufukia shimo katikati ya barabara ya Vingunguti kwa Mnyamani mara baada ya shimo hilo kutelekezwa na Dawasco kwa zaidi ya wiki mbili.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti, Omary Kumbilamoto akisogeza mchanga katika shimo lililochimbwa katika barabara ya Vingunguti kupitia kwa Mnayamani.
Roli la Mchanga likimwaga mchanga katika shimo hilo lilitolekezwa na Dawasco
Wananchi wakifukia shimo lililoachwa na Dawasco baada ya kulichimba na kubadirisha bomba jipya la maji safi vingunguti.
Wananchi wakifukia shimo lililoachwa na Dawasco baada ya kulichimba na kubadilisha bomba jipya la maji safi vingunguti.

JSI WATOA ELIMU YA MALEZI KWA WATOTO WANAOISIHI MAZINGIRA MAGUMU WILAYA YA TEMEKE

$
0
0
Wadau wa malezi ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi (JSI) wametoa mafunzo ya mfumo jumuishi kwa watendaji na wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke. 

Mfumo huo umewekwa na serikali kwa kushirikiana na wadau kama WAMATA na (JSI) ili kutoa huduma kwa pamoja kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi pamoja na watu wanaoishi na virusi vya ukimwi na sio kila mdau kwenda au kupeleka huduma kipekee 

Akitoa mafunzo hayo Asia Jingu amesema mfumo huu ni muhimu kwani utawezesha kuweka taratibu za utoaji wa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na si kila taasisi ama mdau kuwa na utaratibu wake jambo ambalo lilikuwa likisababisha baadhi ya watoto kukosa huduma kutokana na sababu mbalimbali. 

Pia Mfumo huu utahamasisha ushirikiano wa karibu kati ya wadau na taasisi zinazojihusisha na kuhudumia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi. 

Asia Jingu pia amesema watoa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu wanatakiwa kutoa huduma kwa uweledi mkubwa kwani kazi hii ni ya kujitolea,kwa hiyo kwa wale wote watakaopata mafunzo kwa ajili ya huduma hiyo katika Mitaa mbalimbali wawe waadilifu kwa watoto na pia kutoa huduma bila ubaguzi kwa watoto wala kutowadhuru watoto hao walio katika mazingira magumu.
Mkufunzi wa masuala ya malezi ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi (JSI), Asia Jingu akitoa mafunzo hayo kwa viongozi mbalimbali, watendaji na wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.


watendaji na wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke wakiwa makini.

Wateja wa ENGEN kupata ofa ya mafuta bure wakilipa kwa M-PESA

$
0
0
Wateja watakaojaza mafuta ya magari kuanzia shilingi 50,000 na kuendelea kwenye vituo vya mafuta vya kampuni ya ENGEN nchini kote kuanzia leo na kulipia kupitia huduma ya Lipa kwa M-Pesa ya Vodacom Tanzania Plc watajipatia ofa papo hapo ya mafuta ya bure yenye thamani ya shilingi 5,000/-.

Wateja watakaojaza mafuta ya magari kuanzia shilingi 50,000 na kuendelea kwenye vituo vya mafuta vya kampuni ya ENGEN nchini kote kuanzia leo na kulipia kupitia huduma ya Lipa kwa M-Pesa ya Vodacom Tanzania Plc watajipatia ofa papo hapo ya mafuta ya bure yenye thamani ya shilingi 5,000/-.

Ofa hii inatokana na kampeni ya Vodacom Tanzania Plc inayohamasisha wananchi kuacha utaratibu wa kutumia fedha taslimu wanapofanya manunuzi ya bidhaa mbalimbali badala yake watumie huduma ya Lipa kwa M-Pesa ambayo hivi sasa imerahisishwa zaidi na mtandao huo kuwa salama katika masuala ya kibiashara.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa ofa hii, Mkurugenzi wa huduma za kifedha wa Vodacom Tanzania Plc, Sitoyo Lopokoiyit alisema “Huduma ya Lipa kwa M-Pesa imeboreshwa zaidi; mbali na kuwawezesha wateja kulipa bila makato yoyote, malipo yamerahishwa zaidi kupitia M-PESA APP mpya yenye teknolojia ya QR codes na wateja wa Vodacom watazawadiwa dakika za BURE kila wanapolipa. Kizuri zaidi ni kwamba sasa wateja wa mitandao mingine pia wanaweza kuwalipa wafanyabiashara waliosajiliwa na huduma hii moja kwa moja kutoka kwenye akaunti za simu za mitandao yao au akanti za benki’.

Alisema kampeni hii inaambatana na ofa mbalimbali kwa sekta tofauti kama ambavyo wateja watakaonunua mafuta kwenye vituo vya ENGEN watakavyozawadia mafuta BURE kila wanapolipia kwa M-PESA. Aliwashauri wateja kupakua APP mpya ya M-Pesa inayorahisha malipo Kwa kwenda Google Playstore na kutafuta ‘MPESA TANZANIA’ kisha wajionee urahisi wa kulipa kwa QR codes kwenye vituo vya ENGEN na maeneo mbalimbali.

“Natoa wito kwa wateja wetu na watanzania kuachana na utamaduni wa kubeba mabulungutu ya fedha wanapotaka kununua bidhaa badala yake waweke fedha kwenye simu zao na kulipia kutumia kupitia M-Pesa, njia rahisi na salama inayorahisisha maisha kwa wateja na wafanyabiashara.Tunandelea na kampeni itakayofanyika nchini kote kuwaelimisha wananchi sambamba na kuwezesha wafanyabishara wengi zaidi kupokea malipo kwa M-Pesa’’. Alisema Sitoyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Engen Tanzania,Paul Muhato alisema “Wakati tunaendelea na wiki ya huduma kwa wateja kwa wateja wetu ambapo tunafanya shughuli mbalimbali, tunayo furaha kushirikiana na Vodacom katika kuhamasisha wananchi matumizi ya njia za kupata huduma bila kutumia fedha taslimu kama hii ya Malipo kwa M-Pesa njia ambayo ni rahisi na salama kwa watoa huduma na  wapata huduma.”

Alisema, Engen Tanzania ikiwa moja ya kampuni inayoongoza kutoa huduma za kuuza mafuta nchini itaendelea kuwaletea ubunifu wa huduma bora wateja wake na kuwapatia ofa mbalimbali kama ambavyo inawaletea ofa hii maalumu ya kupata mafuta ya bure kwa kushirikiana na Vodacom na lengo kubwa likiwa ni kuhakikisha wateja wetu wanaishi maisha ya kisasa kupitia mapinduzi ya kiteknolojia.

Mbali na ENGEN, huduma ya lipa kwa M-Pesa imeendelea kupokelewa vizuri na wafanyabiashara wengine kutoka sekta mbalimbali kama mahoteli na migahawa, bar na clubs, maduka ya rejereja, maduka ya madawa, maduka ya vifaa vya ujenzi, saluni n.k
Mkurugenzi wa huduma za kifedha wa Vodacom Tanzania Plc, Sitoyo Lopokoiyit(kushoto) Mfanyakazi wa kituo cha mafuta cha Engen,Mikocheni jijini Dar es Salaam,Abdalah Shomari, wakimshuhudia Mkurugenzi mtendaji wa Engen Tanzania,Paul Muhato akijaza mafuta kwenye gari la mteja baada ya kulipia kwa huduma ya Lipa kwa M-Pesa na kujipatia ofa ya mafuta ya bure yenye thamani ya shilingi 5,000/-wakati wa Uzinduzi wa ofa hiyo leo.
Mkurugenzi wa huduma za kifedha wa Vodacom Tanzania Plc, Sitoyo Lopokoiyit(katikati)akijadiliana jambo na Mkurugenzi mtendaji wa Engen Tanzania,Paul Muhato(kulia)wakati wa Uzinduzi wa huduma ya Lipa kwa M-Pesa kwa wateja watakaojaza mafuta ya magari kuanzia shilingi 50,000 na kuendelea kwenye vituo vya mafuta vya kampuni ya ENGEN nchini kote kuanzia leo na kujipatia ofa ya bure yenye thamani ya shilingi 5,000/- anaeshuhudia kushoto ni Meneja Masoko wa Vodacom Tanzania PLC,Noel Mazoya.

CHANGIA SERENGETI BOYS KUPITIA AIRTEL MONEY

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Shirikisho la mMpira wa Miguu Nchini (TFF) limewaomba watanzania na wadau wa mpira kuichangia timu ya vijana chini ya miaka 17 Serengeti Boys ili kuiwezesha kuweka kambi ya mwezi mmoja nchini Moroco.

Serengeti Boys wameondoka nchini jana saa 8 mchana kueleka nchini Moroco kwa ajili ya kambi kabla ya kuelekea Gabon kwa ajili ya fainali za vijana zitakazoanza Mei 14.

Kabla ya kwenda Gabon, Serengeti inatarajiwa kucheza mechi mbili za kirafiki kwa ajili ya maandalizi zaidi ya kujipima na wamepangwa kundi B wakiwa na mabingwa watetezi wa kombe hilo Mali.

Timu mbili za juu za kila kundi zitawakilisha Afrika katika fainali za Kombe la Dunia nchini India 

Kauli mbiu 

Gabon mpaka kombe la Dunia...........................

WAZIRI MAHIGA AZUNGUMZA NA MKURUGENZI WA UN WOMEN KWA KANDA YA MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake cha Umoja wa Mataifa (UN Women) kwa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Izeduwa Derex-Briggs alipofika Wizarani tarehe 06 Aprili, 2017. Katika mazungumzo yao, Bi. Derex-Briggs alimweleza Mhe. Waziri maendeleo ya utendaji wa Kitengo hicho kwa Kanda na umuhimu wa uwepo wao hapa nchini. Pia alimtambulisha Bi. Hodan Addou, Afisa Msimamizi mpya wa Kitengo hicho hapa nchini. 
Mhe. Mahiga akiendelea na mazungumzo na Bi. Derex-Briggs huku Bi. Hodan Addou (kushoto), Afisa Msimamizi mpya wa Kitengo cha Wanawake cha Umoja wa Mataifa hapa nchini na Bi. Sekela Mwambegele (kulia), Afisa Mambo ya Nje wakifuatilia. 
Bi. Derex-Briggs nae akimweleza jambo Mhe. Waziri 
Hapa Bi. Derex-Briggs (katikati) akimtambulisha rasmi Bi. Addou kwa Mhe. Mahiga 
Picha ya pamoja 

NAIBU SPIKA AKUTANA NA CHAMA CHA WANASHERIA WA TANGANYIKA (TLS) MJINI DODOMA

$
0
0
  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Mhe.Tundu Lissu  na  ujumbe wake walipomtembelea ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma.
  Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Mhe.Tundu Lissu  akimueleza jambo Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson alipofika kumtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma pamoja na viongozi wengine wa TLS.
 Makamu wa Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Godwin Ngwilima akifafanua jambo Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson alipofika kumtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma pamoja na viongozi wengine wa TLS.
Viongozi wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) wakiwa pamoja na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson wakijadiliana masuala mbalimbali viongozi hao walipomtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma.

PICHA NA OFISI YA BUNGE.​

MICHUZI TV:RC MBEYA AFUNGUA KONGAMANO LA ELIMU MKOANI HUMO

$
0
0
 - Wadau wa Elimu wapongeza na wamejitokeza kwa Wingi 

- Kongamano labainisha changamoto za elimu na mikakati ya kukabiliana Na changamoto zatajwa
- Lengo la KONGAMANO  ni kuongeza ufaulu na elimu bora katika Elimu YA msingi na sekondari
- Serikali ya Mkoa wakusudia kuanzisha mfuko wa Elimu kwa lengo la kusaidia Vifaa vya Maabara, ununuzi wa vitabu, motisha kwa walimu na wanafunzi wanaofanya vizuri na kuingiza Umeme mashuleni
- Mkuu wa mkoa aelekeza  wazazi na walezi kuchangia Chakula mashuleni na kushirikiana na serikali ktk ujenzi wa hostel
- Aagiza madai ya walimu yashughulikiwe kuanzia ngazi ya halmashauri kwa Yale ambayo yapo ndani ya uwezo wa halmashauri
- Mkoa umejipangia malengo ya  kuwa Miongoni mwa mikoa KUMI bora kitaifa
 - Maazimio ya kongamano yatakuwa ndiyo dira ya Elimu kimkoa na yataelekezwa katika ngazi zote.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images