Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 162 | 163 | (Page 164) | 165 | 166 | .... | 3278 | newer

  0 0


  0 0

  MKUU WA JKT MEJA JENERALI RAPHAEL MUHUGA ANAWAITA VIJANA 10,849 WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA MWAKA 2013 KUJIUNGA NA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA KAMA IFUATAVYO:-

  1. VIJANA WOTE WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA WALIOPATA DIVISION I NA DIVISION II.

  2. VIJANA WOTE WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA WALIOSOMA MASOMO YA MCHEPUO WA SAYANSI NA KUPATA DIVISION III.

  3. VIJANA HAO WANATAKIWA KURIPOTI KATIKA MAKAMBI YA JKT TAREHE 24 JUNI 2013 BILA KUKOSA. AMBAYE HATARIPOTI ATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.

  4. TANGAZO HILI HALIWAHUSU VIJANA WOTE WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA 2013 KATIKA SHULE ZA SEKONDARI ZA UNGUJA NA PEMBA. AIDHA, SHULE 27 AMBAZO VIJANA WAKE WAMEHITIMU MAFUNZO YA JKT AWAMU YA KWANZA HAZIHUSIKI.

  5. VIJANA HAO WATUNZE TIKETI ZAO KWA AJILI YA KUREJESHEWA NAULI WATAKAZOTUMIA MARA TU WATAKAPORIPOTI VIKOSINI.

  6. TAARIFA ZAIDI ZITATOLEWA KWENYE MAGAZETI MBALIMBALI YA HAPA NCHINI.

  Majina ya waliochaguliwa na vituo watakavyokwenda:


  Kwa maelezo zaidi ya kambi mbalimbali walikopangwa tembelea www.jkt.go.tz

  KUNRADHI/ANGALIZO TOKA MICHUZI BLOG: 
  BANDWITH YA SERVER YA JKT IMEHEMEWA KWA WINGI WA WASOMAJI
  HIVYO LINK HIZO ZINA KWIKWI..

  0 0


  TUNAHITAJI MADEREVA WAWILI WA MAGARI MAKUBWA
  GOOD NEWS FOR TANZANIA
  HUDUMA MPYA YA KIFURUSHI 
  NEW DOOR TO DOOR SERVICE
  TUNACHUKUA MZIGO MLANGONI KWAKO UK NA TUTAUFIKISHA MLANGONI KWAKO DAR
  UKILIPA HAPA UK HAULIPI TENA DAR, SISI TUTAKULETEA MZIGO NYUMBANI KWAKO!
  Baada ya kushughilikia kwa kina mapungufu yaliyojitokeza mwanzo, 
  sasa tumerudi na huduma ya kifurushi tena ikiwa imeboreshwa zaidi.
  BEI ZETU KAMA KAWAIDA HAZINA KIGUGUMIZI NA SI ZA KUUMIZA

  AIR CARGO TO DAR NOW £3.50 INCLUSIVE CLEARANCE!
  AIR CARGO TO ZANZIBAR NOW £3.00 INCLUSIVE CLEARANCE!
  AIR CARGO TO NAIROBI/MOMBASA NOW £2.80 INCLUSIVE CLEARANCE!
  KIFURUSHI KWA KONTENA DAR/ZANZIBAR NOW £2.20 INCLUSIVE CLEARANCE!

  NDEGE ZINAONDOKA KILA WIKI MARA MBILI
  MZIGO WOWOTE LETE TU
  MINIMUM WEIGHT IS 40KILOS
  KAMA UNATAKA KUAGIZA KITU AU KUFANYA BOOKINGS TUWASILIANE KWA NAMBA HAPA CHINI
  40'HC CONTAINER TO DAR/MOMBASA £1,800
  CHEZEA SERENGETI WEWE!
  CHRIS LUKOSI +44 07903828119  & 07404279633 
  SIMON LOUIS (MOHSIN) +44 07950689243
  HASSAN   +44 07404672873
  HQ -  UNIT 92 THAMES INDUSTRIAL PARK, PRINCESS MARGARET ROAD, EAST TILBURY, RM18 8RHRH
  Tell (+44) 01375 855917  Fax (+44) 01708202477

  0 0
 • 06/13/13--20:00: Ngoma zaipendazo Ankal
 • Ngoma ya 'Seya' ya Nguza Viking na mwanae Papii Kocha mwana wa Mfalme haisahauliki kirahisi...

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akionyesha Tuzo ya heshima aliyopewa Rais Jakaya Kikwete na Mtandao wa wabunge wa mabunge wa Afrika wa kupambana na rushwa APNAC ili kutambua mchango wake katika kupambana na rushwa. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye semina na SPNAC iliyofunguliwa na Waziri Mkuu kwenye ukumbi wa Afrian Dream mjini Dodoma Juni 14, 2013. Kushoto ni Spika wa Bunge Anne Makinda.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Spika wa Bunge Anne Makinda (katikati) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Gerge Mkuchika baada ya kufungua semina ya Mtandao wa wabunge wa mabunge wa Afrika wa kupambana na rushwa APNAC iliyofunguliwa na Waziri Mkuu kwenye ukumbi wa Afrian Dream mjini Dodoma Juni 14, 2013. Kushoto ni Spika wa Bunge Anne Makinda.
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiteta na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora, George Mkuchika baada ya kufungua semiana ya Mtandao wa Wabunge wa Afrika waanaopambana na Rushwa APNAC kwenye ukumbi wa Afrian Dream mjini Dodoma Juni 14, 2013.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Jaji Kiongozi, Fakih Jundu (kakatikati) na Mbunge wa Mkanyageni, Mohamed Habib Mnyaa baada ya kufungua semiana ya Mtandao wa Wabunge wa Afrika waanaopambana na Rushwa APNAC kwenye ukumbi wa Afrian Dream mjini Dodoma Juni 14, 2013.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Naibu Waziri wa Habari , Vijana na Michezo, Amos Makala kwenye viwanja vya Hoteli ya African Dream mjini Dodoma Juni 14, 2013.

  0 0

  Na Abdulaziz Video,Nachingwea

  Jumla ya Vijana 63 Waendesha Pikipiki na Bajaj (MAARUFU BODABODA)Wilayani Nachingwea wamekabidhiwa Leseni za Udereva baada ya kuhitimu Mafunzo yaliyotolewa na Veta na Kitengo cha Usalama Barabarani baada ya Kuwezesha na Mbunge wa Jimbo hilo Ambae Pia ni Waziri wa Sheria na Katiba,Mathias Chikawe.

  Katika kufanikisha zoezi hilo Mbunge huyo pia amesaidia kuwalipia Leseni zenye thamani ya Tshs Milioni Tatu ambapo Vijana 50 wamenufaika na mpango huo ambao utakuwa endelevu katika jimbo hilo.

  Mpango huo wa kuwezesha Vijana Hao ni Jitihada za Mkuu wa Wilaya Hiyo Bi Regina Chonjo baada ya kukutana na makundi mbalimbali na kubaini Baadhi ya Changamoto ikiwemo mahusiano mabaya kati ya Polisi wilayni humo na Waendesha Bodaboda hali Iliyokuwa Inachangia Uvunjifu wa AMANI Ikiwemo kutotoa huduma kwa Uaminifu Huku wakiwa ni tegemeo kubwa la Usafiri na Usafirishaji Vijijini Wakiwemo WAGONJWA.
  Mmoja ya Waendesha Boda boda akikabidhiwa leseni yake na Waziri wa Katiba NA Sheria,Mathias Chikawe katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Nachingwea.
  Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Bi REGINA CHONJO akizungumza na Waendesha Boda boda wakati wa hafla ya kukabidhiwa leseni zao mara baada ya kumaliza mafunzo.Wa pili kulia ni Waziri wa Katiba NA Sheria,Mathias Chikawe.
  Furaha baada ya kuhitimu mafunzo.

  0 0

   Hivi ndivyo hali ilivyo ndani ya Ukumbi huu wa Nyumbani Lounge,Namanga jijini Dar es Salaam ambapo leo hii kuna bonge moja la show la Mwanadada mkongwe kwenye tasnia ya muziki hapa nchini,Lady Jay Dee ambaye anatimiza miaka 13 tangu alipoanza kazi yake ya muziki.katika show hii wanamuziki mbali mbali watapanda jukwaani aliwepo Mh. Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu.
   Wadau mbali mbali wa muziki hapa nchini wapo ndani ya ukumbi huu hivi sasa kusuhudia show hii ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa muziki.
   Ndani ni nyomi la hatari,lakini nje nako watu bado wanataka kuingia huku wengi wao wakisema kuwa "hata kama hakuna siti,sie tuko radhi kusimama ilimradi tumsapoti Dada yetu.
   Getini mambo yako namna hii.
   Foleni bado ni ndefu na watu bado wanazidi kuingia ukumbini hapa hivi sasa.
  Burudani ya Utangulizi ikiendelea.

  Kwa picha na video zaidi zitawajia baadae kidogo.

  0 0

  image
  Kufuatia kifo cha ndugu yetu, JEROME MPEFO, kilichotokea juzi tarehe 12, June,2013-,Houston, Texas, mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu kwenda nyumbani Tanzania kwa mizishi inafanyika.

  Tunawaomba ndugu,jamaa, marafiki, watanzania na yeyote aliyeguswa na msiba huu kusaidia kwa michango ya hali na mali ili tuweze kufanikisha kuupeleka mwili wa marehemu nyumbani.

  Kwa wale ambao hawawezi kuleta michango katika pesa taslimu, tunapokea michango kupitia;
  Name of The Bank : Bank Of America
  Account Number: 586033522448
  Routing Number: 113000023
  Name On The Account: STELLA LIMING
  Pia tutakuwa na fundraising siku ya Jumamosi (tarehe 15, June,2013) kuanzia Saa 10 Jioni. Anuani ya mahali Fundraising itakapofanyika ni
  5800, Westheimer Road,
  Houston, Texas, 77057
  Misa ya kumuaga ndugu yetu JEROME MPEFO, itafanyika siku ya Jumanne wiki ijayo. Tutawataarifu juu ya muda na mahali.
  Kwa upande wa nyumbani Tanzania, wasiliana na wafuatao kuhusu msiba na maelekezo yoyote ya jinsi ya kufika nyumbani kwa wafiwa;
  GRACE MPEFO: +255 717 400808
  RAYMOND: +255 714 644964
  Asanteni sana. Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa. Jina lake lihimidiwe.Amen.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapunduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akizungumza na Madakatari wa Kichina waliofika IKulu Mjini Zanzibar, kumuaga Rais baada ya kumaliza muda wao wa kazi,ambapo walikuwa wakishirikiana na Madakatari wazalendo katika kutoa huduma mbali mbali kwa wagojwa katika Hospitali za Unguja na Pemba.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapunduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akizungumza na Madakatari wa Kichina waliofika IKulu Mjini Zanzibar, kumuaga Rais baada ya kumaliza muda wao wa kazi,ambapo walikuwa wakishirikiana na Madakatari wazalendo katika kutoa huduma mbali mbali kwa wagojwa katika Hospitali za Unguja na Pemba.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapunduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akiwa katika picha ya pamoja na Madakatari wa Kichina waliofika IKulu Mjini Zanzibar, kumuaga Rais baada ya kumaliza muda wao wa kazi,ambapo walikuwa wakishirikiana na Madakatari wazalendo katika kutoa huduma mbali mbali kwa wagojwa katika Hospitali za Unguja na Pemba.{Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

  0 0


  Show inaendelea na ni shangwe tupu ndani ya ukumbi huu wa Nyumbani Lounge,Mh. Sugu amemaliza kutoa  burudani muda mfipi uliopita na sasa ni zamu ya TMK Halisi chini yake Kibla Juma Nature.

  0 0

  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete meets and hold talks with Sir. Richard Branson in London this evening . Sir.Richard is a British business magnate best known as the founder and chairman of Virgin Group of more than 400 companies. President Kikwete is in London UK for a three days working visit in which, among other things, he will attend the G8 summit.
  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete and his delegation in conversation with The Chairman of Virgin Group of Companies Sir. Richard Branson in London this evening. Others in the picture are from left are Minister for Transport Dr. Harrison Mwakyembe, Tanzania Tourist Board Managing Director Dr.Aloyce Nzuki, President’s advisor Economic Affairs Dr.Hamis Mwinyimvua and Tanzanian High Commissioner to the United Kingdom Peter Kallaghe(photos by Freddy Maro)

  0 0

  Na Anna Nkinda – New York 
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ametunukiwa tuzo ya Malengo ya Maendeleo ya Milinia ya mwaka 2013 kwa wanawake na Shirika la Voices of African Mothers (VAM) la nchini Marekani kutokana na kazi kubwa anayoifanya ya kusaidia jamii wakiwemo wanawake na watoto. 
   Sherehe ya kukabidhi tuzo hizo zimefanyika jana katika ukumbi wa mikutano uliopo makao makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) mjini New York. Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) amekabidiwa tuzo hiyo kutokana na uongozi wake madhubuti, mafanikio na mchango wake na kujitoa kwake kuwasaidia wanawake na watoto wa Tanzania. 
   Akikabidhi tuzo hizo Nana – Fosu Randall ambaye ni Rais na mwanzilishi wa shirika hilo alisema kuwa tathimini ilitofanyika kwa mwaka 2012 juu ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia wametambua kwamba malengo matatu yamefikiwa nchini Tanzania kabla ya muda uliowekwa wa kikomo wa mwaka 2015. Alisema kuwa wake wa Marais wa Afrika wanamajukumu mbalimbali katika nchi zao ili kufikia Malengo hayo, Taasisi ya VAM imekuwa ikifanya tathimini juu ya hatua zilizofikiwa na Taasisi za wake wa Marais kupitia taarifa za mwaka na zingine zinazowasilishwa.
   “Wanawake hawa wanastahili kutuzwa kwani wamefanya kazi kubwa pamoja na kufanya shughuli zao katika mazingira yenye changamoto nyingi ukilinganisha na wenzao katika nchi zingine. Hafla ya tuzo hizi siyo tu inasherehekea mafanikio ya wake wa marais wa Afrika bali pia inawahamasisha na kuwatia moyo wakati huu ambapo mwaka 2015 unakaribia”, alisema . 
   Alimalizia kwa kusema kuwa mara nyingi vyombo vya habari vimekuwa vikiandika habari zisizokuwa sahihi kutokana na kazi zinazofanywa na wake wa marais lakini vinasahau kuandika mambo mazuri na kazi kubwa wanayoifanya ya kuwasaidia wananchi na kuviomba vyombo hivyo kubadilika na kuthamini kazi kubwa wanayoifanya. 
   Akiongea mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo Mama Kikwete alishukuru kwa tuzo aliyopewa na kusema kuwa Tanzania ni moja ya nchi ambazo zimepiga hatua kubwa sana katika kufikia malengo ya milinia kwani vifo vya watoto vimepungua kwa asilimia 45 na 49 kwa watoto wachanga. 
   Alisema kuwa haya ni mafanikio makubwa sana japokuwa lengo ni kuondoa kabisa vifo ambavyo vinatokana na sababu ambazo zinazuilika na katika malengo mengine maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) yanaendelea kupungua kutoka asilimia 5.7 kwa mwaka 2004 hadi asilimia 5.1 kwa mwaka 2011. Mama Kikwete alisema;
   “Elimu ya msingi inatolewa bure kwa watoto wote walio na umri unaostahili na hatua kubwa imepigwa katika kupunguza ugonjwa wa maralia na vifo vya akina mama vinavyotokana na tatizo la uzazi” Kwa upande wa harakati za kumkomboa mtoto wa kike alisema kuwa ni lazima ziendelee na zizingatie changamoto mpya za mazingira mapya kwani unapompatia elimu unampunguzia changamoto za ujinsia na kumpatia huduma ya afya ikiwemo uzazi wa mpango, unamuwezesha kushiriki zaidi shughuli za maendeleo ya kiuchumi, unasaidia familia yake na jamii kuweza kuendelea. 
   Kwa upande wake Dk. Judy Kuriansky ambaye ni mwakilishi wa Asasi zisizo za Kiserikali zilizo chini ya UN alisema kuwa wake wa marais wanafanya kazi kubwa ya kuisaidia jamii hivyo basi ni jukumu la kila mmoja kuwaunga mkono na kushirikiana kwa pamoja ili kuweza kutimiza malengo ya maendeleo ya milinia. Dk. Kuriansky alisema kuwa ili kufikia malengo ya milinia inatakiwa kuimarisha miundombinu iliyopo jambo ambalo litasababisha kuifikia jamii kwa ukaribu zaidi na kuweza kutatua changamoto zinazowakabili. 
   Tuzo hizo zimetolewa kwa mara ya kwanza na shirika hilo kwa kushirikiana na Taasisi ya The reed for Hope (RFHF) na Bethesda Counsel kwa wake wa marais wa Afrika akiwemo Mke wa Rais wa Burundi Mama Dk. Denice Nkurunziza, Mke wa Rais wa Equatorial Guinea Mama Constancia Mangue de Obiang na Mke wa Rais wa Mali Mama Mintou Doucoure Epse Traore.
   
   Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokea tuzo ya Millenium Development Goals, Women Progress Awards 2013, kutoka kwa Ms Jennie Yeung , Rais wa Shirika la Sun Zhong Shan Foundation lililo chini ya United Nations Education, Science, Cultural and Health Advancement  Foundation la nchini Marekani.  Mama Salma alipokea tuzo hiyo baada ya kutimiza baadhi ya malengo ya Millenia katika masuala ya ukimwi, elimu kwa watoto waliokosa fursa  na kuwawezesha wanawake kiuchumi nchini Tanzania. Kulia ni Katibu wa WAMA, Ndugu Daud Nassib na kushoto ni Dr. Judy Kuriansky, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Columbia nchini Marekani.
   Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete akimkabidhi tuzo hiyo Katibu wa WAMA Foundation , Ndugu Daud Nassib  wakati wa kupokea   tuzo hiyo huko New York nchini Marekani tarehe 13.6.2013.
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipongezwa na Dr. Judy Kuriansky, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Columbia mara tu baada ya kukabidhiwa tuzo yake.
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia  waalikwa waliohudhuria sherehe za utoaji tuzo kwa wake wa Marais wa Bara la afrika zilizofanyika huko New York nchini Marekani. Picha na John Lukuwi  Mama Salma Kikwete akiongea baada ya kutunukiwa tuzo hiyo 

  0 0

  Ukumbi wa Highlands Cinema jijini Iringa unalipuka kwa vifijo mara baada ya Miss Redds Iringa 2013 Neema Mality kutangazwa mshindi usiku huu
  Miss Redds Iringa 2013 Neema Mality akishukuru mashabiki 
  Miss Redds Iringa 2013 Neema Mality akipozi na mshindi wa pili Lucy  George (kushoto), na mshindi wa tatu Lillian Samson baada ya kutwa taji hilo usiku huu. Picha na Francis Godwin

  0 0
 • 06/14/13--20:00: IN LOVING MEMORY
 • REV. K. EPHRAIM AMOS LYIMO

  (17 NOVEMBER 1922 – 15 JUNE 1978)


  It is 35 years since you left us. We, Samwel, Dora, Tabusia, Remi, Vicky, Nechi and Julius pause to reflect how you and our late mother Margaretha shaped our characters, molded our spirits and touched our hearts and souls. May this note be a reminder of the memories we have shared and a symbol of the everlasting impact you have in our lives.


  We remember how you emphasized on education, hard work, patience, and prayers; and we always get thrilled when telling our wives, husbands, in-laws, children, grand children and great grand children of your love, smile and sense of humor.


  You will forever be remembered by the family, friends, co-workers at Lutheran Church of Tanzania and colleagues at Marangu Sembeti. We love you so much and are proud to be part of you. To God be the Glory, in Jesus’ Name – Amen.

  0 0


  0 0
 • 06/15/13--01:41: Article 13


 • 0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kushoto) akisalimiana na Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti wa Chama Cha TLP,Mh. Augustine Mrema wakati wa Harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Chama Cha kuweka na kukopa (saccos) Cha waalimu wa Moshi vijijini.Shughuli hiyo ilifanyika jana kwenye Uwanja wa Chuo kikuu kishiriki Cha ushirika mjini Moshi.
  Mmoja wa Wazee wa Kichaga akimvisha Kofia ya kichifu,Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa ikiwa ni ishara ya kumsimika kuwa Mangi wa Wachagga.
  Mangi wa Wachaga Mh. Edward Lowassa akiwa na Kofia na Fimbo ya umangi.
   Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wabunge na viongozi wa serikali,kuanza kushoto ni Mbunge wa Mkoa wa Kilimanjaro Viti Maalim wanawake, Betty Machangu,Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia,January Makamba,Mbunge wa Moshi vijijini,Dr. Cyril Chami,Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama na Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema.
  Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa jana amefanya maajabu huko Moshi,baada ya kuchangisha zaidi ya shilingi bilioni moja na milioni Mia mbili,katika Harambee ya Chama Cha kuweka na kukopa (saccos) Cha waalimu wa Moshi vijijini.

  Katika Harambee hiyo ya aina yake iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo kikuu kishiriki Cha ushirika mjini Moshi,zaidi ya shilingi milioni 500 zikiwa fedha tasilimu zilipatikana, huku ahadi zikiwa zaidi za milioni 700.

  Akihutubia katika Harambee hiyo iliyohudhuliwa na maelfu ya waalimu wa mkoa wa Kilimanjaro,Mh Lowassa alisema ana ndoto kuwa siku si nyingi, umuhimu wa elimu utaonekana, na waalimu wataboreshewa maisha na maslahi yao, shule zitaboreshwa vifaa, na usumbufu wanaoupata wanafunzi kutokana na kurudi nyumbani utakwisha.

  Mbunge wa Moshi Jimbo la Vunjo (TLP),Mh. Augustine Mrema alimsifu Lowassa kwa uwezo wake na uchapakazi na akamshukuru wa kujitolea kwake katika shughuli za kijamii.

  Lowassa alitawazwa na wazee wa kichagga kuwa Mangi ambapo walimkabidhi silaha na kofia ya kijadi ikiwa ni ishara ya kukabiliana na maadui katika harakati za kuwatumikia Watanzania.

  Ifuatayo ni Hotuba ya Mh. Lowassa wakati wa harambee hiyo


  0 0

  Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi
  ZANZIBAR JUMAMOSI JUNI 15, 2013. Mkuu wa Mkoa wa Mjini Maghari Zanzibar Mh. Abdallah Mwinyi Khamizi, amepongeza Ushirikiano wa Jeshi la Polisi na Vikosi vya SMZ Zanzibar na kuzitaka Idara nyingine kuiga mfano huo ili kuweza kutatua matatizo yanayowakabili.
  Mh, Abdallah ametoa wito huo leo kwenye Uwanja wa Amani mjini Zanzibar wakati akiwahotubia wananchi na Askari wa Jeshi la Polisi na Vikosi vya SMZ walioshiriki kwenye matembezi ya pamoja ya kijeshi (Route March).
  TC 00:54:00 Mh. Abdallah Mwinyi, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi.
  Amesema kwa mfano vikundi kama hivyo vinaweza kushirikishwa katika masuala ya usafi wa mazingira, upandaji wa miti na ustawishaji wa bustani za miti ya vivuli na matunda na mambo mengine kama hayo.
  Akizungumzia matembezi hayo, Mh. Abdallah amesema tukio hilo ni kielelezo kuonyesha utayari wa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama katika kushirikiana na wananchi kwenye mambo mbalimbali yakiwemo ya kimaendeleo.
  Awali Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, amesema madhumuni ya matembezi hayo ni kuonyesha umma kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vina ushirikiano na uwezo mkubwa wa kukabiliana na vitendo vyovyote vya kihalifu.
  TC 00:46:43 CP Mussa Ali Mussa, Kamishna wa Polisi Zanzibar
  Mbali ya Askari, Wakaguzi na Maafisa wa Jeshi la Polisi, Vikosi vya SMZ vilivyoshiki katika matembezi hayo ni Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo (KMKM), Vyuo Vya Mafunzo (Magereza), Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU), Kikosi cha Zimamoto na Uokozi (KZU), Kikosi cha Valantia (KVZ) pamoja na Vikundi 33 vya Mazoezi kotoka mikoa mitatu ya Unguja.
  IMETOLEWA NA INSP. MOHAMMED MHINA, AFISA HABARI MKUU WA JESHI LA POLISI ZANZIBAR.

  0 0


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Waziri wa Ulinzi wa Comoro, Hamada Madi, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, jana Juni 14, 2013 kwa ajili ya kumkabidhi Ujumbe maalum wa Serikali ya watu wa Comoro. Makamu alipokea ujumbe huo kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea Ujumbe maalum kutoka kwa Waziri Ulinzi wa Comoro, Hamada Madi, aliyefika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, jana Juni 14, 2013 kwa ajili ya kumkabidhi Ujumbe maalum wa Serikali ya watu wa Comoro. Makamu alipokea ujumbe huo kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri wa Ulinzi wa Comoro, Hamada Madi, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, jana Juni 14, 2013 kwa ajili ya kumkabidhi Ujumbe maalum wa Serikali ya watu wa Comoro. Makamu alipokea ujumbe huo kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete. Picha na OMR.

older | 1 | .... | 162 | 163 | (Page 164) | 165 | 166 | .... | 3278 | newer