Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Ruvuma ABEL SWAI awaasa madereva wa bodaboda

$
0
0
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Ruvuma ABEL SWAI amewataka madereva pikipiki maarufu kama bodaboda kuvaa kofia ngumu katika kujinga na ajali za mara kwa mara wawapo barabarani kwa undani wa habari hii , Hii hapa video yake.

WAZIRI MWAKYEMBE AKUTANA NA WAZIRI WA MICHEZO WA ZANZIBAR MHE. RASHID ALI JUMA

$
0
0
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe.Rashid Ali Juma akizungumza na waandishi  juu ya Maendeleo ya Michezo ya Zanzibar  kwa ujumla leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Harrison Mwakyembe.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari juu ya hatua mbalimbali SErikali  inazofanya  katika kuimarisha Michezo nchini.Kulia kwake ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe.Rashid Ali Juma na Kushoto kwake ni Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Dkt.Hassan Abbas
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Harrison Mwakyembeakifurahia jambo na Waziri wa Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe.Rashid Ali Juma wkati walipokutana Jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo mafupi juu ya hali ya Michezo nchini.Picha zote na Daudi Manongi-MAELEZO.

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

MICHUZI TV: SERENGETI BOYS YAPATA SARE YA BAO 2 - 2 DHIDI YA GHANA 'THE BLACK STARLETS'

RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA MABADILIKO MADOGO KATIKA SAFU YA MAKATIBU WAKUU, PROF. KITILA MKUMBO KUWA KATIBU MKUU MAJI NA UMWAGILIAJI

$
0
0
Prof. Kitila Mkumbo aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 04 Aprili, 2017 amefanya mabadiliko madogo katika safu ya Makatibu Wakuu.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Kitila Alexander Mkumbo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

Prof. Kitila Alexander Mkumbo anachukua nafasi ya Mhandisi Mbogo Futakamba ambaye amestaafu.

Kabla ya Uteuzi huu Prof. Kitila Alexander Mkumbo alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Leonard Akwilapo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Kabla ya Uteuzi huo Dkt. Leonard Akwilapo alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Kufuatia uteuzi huo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bi. Maimuna Tarishi amehamishwa na kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge).

Bi. Maimuna Tarishi anachukua nafasi iliyoachwa na Mussa Uledi ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Ave Maria Semakafu kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambako anajaza nafasi iliyoachwa na Dkt.

Leonard Akwilapo ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.

Kabla ya Uteuzi huo Dkt. Ave Maria Semakafu alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).

Wateule hao wataapishwa kesho tarehe 05 Aprili, 2017 saa 3:00 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, 
IKULU
Dar es Salaam
04 Aprili, 2017

MVUA YATIBUA MIUNDOMBINU JIJINI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Dereva wa bodaboda akikatiza  dimbwi la maji lililopo katika makutano ya barabara ya Bibi Titi  na Morogoro jijini Dar es salaam
 Basi la Mwendo kasi likiwa katika barabara ya Morogoro  ambayo imejaa maji
 Baiskeli za wauza lambalamba  zikiwa zimepaki kutokana na kushindwa kutembea kutokana na mvua kubwa kunyesha

TAHADHARI YA MVUA KUBWA ZINAZOENDELA KUNYESHA/UPDATES OF THE ON-GOING HEAVY RAINS

COUNTDOWN FOR THE PRESIDENT’S MANUFACTURER OF THE YEAR AWARDS

$
0
0
The President’s Manufacturer of the year (PMAYA) Awards scheduled to be held on April 08, 2017 at the Serena Hotel Dar es salaam. The President’s Manufacturer of the year Awards is an annual event that is organized by the Confederation of Tanzania Industries (CTI) in partnership with Bank M. Bank M has been the main sponsor of this event for a second year in a row. HE Samia Suluhu Hassan, Vice President of the United Republic of Tanzania will be the Chief Guest.

Speaking to the press yesterday, The Confederation of Tanzania Industries (CTI) Executive Director Mr. Leodegar Tenga said “PMAYA aims to recognize and appreciate the industrial sector’s important role in Tanzania’s economic development process. For the past twelve consecutive years, CTI has been staging this most prestigious members’ event covering all sectors of production and services”.

“This year’s competition has been improved by including Energy Efficiency Award. The award will also act as an opportunity to publicise the industrial energy efficiency actions across the country. CTI, DANIDA and GIZ are actively involved in promoting energy management and efficiency in industries e.g energy audits in industries recently done throughout Tanzania” added Mr. Tenga.
The Confederation of Tanzania Industries (CTI) Executive Director Leodegar Tenga talking to the press regarding CIT partnership with Bank M in conducting this year’s President’s Manufacturer of the year awards (PMAYA) taking place over the weekend. With him is the Bank M CEO Ms. Jacqueline Woiso & Alaf Marketing manager Theresia Mmassy.

For the first time ever, non-members have also participated in this year’s competition. “In order to accommodate the advice given by our Patron the President of the United Republic of Tanzania H E John Pombe Magufuli, during the last PMAYA, we decided to widen the participation by allowing non-members to participate in the competition to make the contest more competitive” Tenga said.

The main objective of these awards includes recognizing the pertinent role of the industrial sector’s contribution to the national economy, to encourage and motivate investors in the industrial sector, to publicize the importance of the industrial sector in the country, raising the standard of business practices and promote sound corporate governance in the country etc. Also Mr. Tenga thanked Bank M for coming on board once again this year to support the awards as the main sponsors.

Bank M’s CEO Ms. Jacqueline Woiso said that Bank M recognises the government’s efforts to boost the industrial sector in the country. “The Industrial sector plays a central role in the economic growth of Tanzania so we are proud to support the local manufacturing industry not only financially in banking services but also through this prestigious competition.
Bank M’s CEO Jacqueline Woiso giving a brief to the press yesterday in Dsm regarding the Bank in partnership with the Confederation of Tanzania Industries (CTI) in conducting this year’s President’s Manufacturer of the year award (PMAYA) which will be held over the weekend in DSM. She is flanked by the CTI Executive Director Leodegar Tenga (right) and Alaf Marketing manager Theresia Mmassy.

PMAYA competition is one avenue that challenges corporate companies to improve on quality of products and services to the public, therefore, like we have raised the benchmark for provision of banking services in the country, we are positive that our involvement in this event will thereby benefit the community and the nation at large” concluded Ms. Woiso.

The awards introduced in 2005 with the aim of recognizing and appreciating the manufacturing sector’s important role in Tanzania’s economic development process. The Awards are given to companies in small, medium and large manufacturer categories that exhibit a high degree of economic impact. About 400 guests from the private sector and government institutions will attend.

NAIBU WAZIRI DKT. ANGELINE MABULLA AFANYA ZIARA YA UKAGUZI WILAYANI KILOMBERO, MOROGORO

$
0
0
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Angeline Mabulla akikagua majalada katika masijala ya ofisi ya Ardhi, wilaya ya Kilombero – Morogoro. Walioambatana naye ni Kamishna wa ardhi msaidizi; Juliana Pila na Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Bwn. Ezekiel Mpanda.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Angeline Mabulla akitoa maelekezo kuhusu utunzwaji bora wa majalada kwa afisa ardhi mteule wa wilaya ya Kilombero – Morogoro. Walioambatana naye ni Kamishna wa ardhi msaidizi; Juliana Pila na Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Bwn. Ezekiel Mpanda.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Angeline Mabulla akitoa maelekezo kuhusu utunzwaji bora wa machapisho na nyaraka mbalimbali katika ofisi ya ardhi, kwa afisa ardhi mteule wa wilaya ya Kilombero – Morogoro.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Angeline Mabulla katika picha ya pamoja na watendaji wa ofisi ya Kanda ya kati (Morogoro), mradi wa kuwezesha umilikishaji ardhi (LTSP) na Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Bwn. Ezekiel Mpanda.

BIASHARA YA NDIZI KATIKATI YA JIJI

$
0
0
 Mmoja wa Wachuuzi wa ndizi akiuza ndiz kwa mteja wake kama alivyokutwa na kamera yetu ya Mtaa kwa Mtaa katika eneo la Kisutu jijini Dar es Salaam
Dereva wa Guta akiwa na Msaidizi wake wakisukuma Guta lilisheheni ndizi kama walivyokutwa kandokando mwa barabara ya Morogoro

JOSE MARA AONGOZA MAPACHA BENDI KATIKA SHOO YA KUMUAGA KAMISHNA MSTAAFU WA BIMA

$
0
0
 Kiongozi wa bendi ya Mapacha Bendi Jose Mara akiongoza safu wa uimbaji wa bendi hiyo katika shoo ya kumuaga  Kamishna wa TIRA , Islael Kamuzora
 Mpiga Drum wa bendi hiyo , Computer Drama akifanya yake katika shoo hiyo
 Mpiga Tumba wa bendi hiyo Njeki Mponda akipiga tumba katika shoo hiyo ya Mapacha Bendi
 James Bezi akitumbuiza nadani ya ukumbi wa Serena Hotel
 Erasto Mashine mpiga Kinanda wa bendi ya Mapacha Bendi akifanya yake katika shoo hiyo
 Mpiga gitaa , Kombora Solo akionyesha ujuzi wake ndani ya Mapacha Bendi ilipofanya shoo ya kumuaga Islael Kamuzora.

GARI LA SERENGETI BOYS LAACHIWA

Kocha Mwingereza atua nchini kusaka vipaji vya kuogelea

$
0
0
UJIO wa Kocha Sue Purchase kutoka katika shule ya kimataifa ya Mtakatifu Felix Uingereza kusaka vipaji vya mchezo wa kuogelea kwenye mashindano ya taifa kutawanufaisha wachezaji watakaoonyesha uwezo. Mashindano ya klabu bingwa Taifa yanatarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii na kushirikisha wachezaji 172 kutoka klabu 15 za Tanzania bara na Zanzibar.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA) Ramadhan Namkoveka, Purchase ambaye pia  ni Mkurugenzi wa michezo wa kuogelea wa shule hiyo, atahudhuria mashindano hayo dhamira  yake kuu ni kusaka vipaji vya mchezo huo. Alisema kuwa hatua ya Purchase kuja nchini imetokana na uwezo mkubwa wa waogeleaji wa Tanzania wanaosoma katika shule hiyo kwa njia ya ‘scholarship’, ambao ni Sonia Tumiotto, Collins Saliboko, Anjani Taylor,  Smriti Gokarn na Aliasgar Karimjee.

“Wachezaji hawa ambao wanasoma uingereza tayari wameshawasili hapa nchini hivi karibuni tayari kushiriki mashindano ya Taifa na wanaendelea na mazoezi ya mwisho hapa Dar es Salaam,”alisema.

Namkoveka alisema kuwa waogeleaji wameonyesha viwango vya hali ya juu kiasi cha kumfanya Purchase kuamua kufunga safari ya kuja nchini kushuhudia waogeleaji wengine wa Tanzania ili kujionea mwenyewe katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Davis & Shirtliff, CRDB Bank, Mediterraneo Hotel & Restaurant, Cocacola na The Terrace.

“Tunawashaukuru makampuni haya kuweza kutisaidia, kwa hakika mchango wao utasaidia kuinua mchezo wa kuogelea. Tunaomba ushirikiano huu uendelee kwa maslahi ya mchezo wa kuogelea na michezo hapa nchini,”alisema. Alisema kuwa mbali ya kushuhudia mashindano hayo na kusaka vipaji, kocha huyo atakutana pia na wazazi na, makocha, waogeleaji wa klabu ya Dar Swim Club na kufanya  nao mazungumzo.

Alisema kuwa hii ni faraja kwa wadau, wachezaji, vilabu  na viongozi wa mchezo wa kuogelea kwani ujio wa kocha huyo ni ishara ya mchezo kukua. Mashindano hayo yatashirikisha jumla ya klabu 15 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ambazo zitashindana katika staili za backstroke, freestyle, breaststrokes, Butterfly na Individual Medley (IM).

MISA-TAN YAWANOA WANAHABARI KANDA YA KASKAZINI JUU YA SHERIA MPYA YA HUDUMA ZA HABARI

$
0
0
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya The Guardian Ltd, Jesse Kwayu akiwaongoza washiriki wa warsha inayotolewa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN) juu ya changamoto zilizopo katika sheria mpya ya Huduma za Habari.
Baadhi ya Wanahabari kutoka mikoa ya Tanga,Arusha ,Manyara na Kilimanjaro wakishiriki katika warsha hiyo inayofanyika katika Hoteli ya Impala jijini Arusha.
Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Luninga cha ITV mkoa wa Manyara, Charles Masanyika akichangia jambo wakati wa warsha hiyo.

Dkt. Kalemani amtaka Mkandarasi REA kuajiri wazalendo

$
0
0
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (wa pili kutoka kulia), akifunua kitambaa kilichofunika Jiwe la Msingi, kuashiria uzinduzi rasmi wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III), kwa Mkoa wa Shinyanga. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga, Mwenyekiti wa Wabunge wa Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige na Mbunge wa Kishapu, Seleman Nchambi.

Na Veronica Simba – Shinyanga

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, amemtaka Mkandarasi kutoka Kampuni ya M/s OK Electronics and Electric Limited, atakayetekeleza kazi ya kusambaza umeme vijijini Awamu ya Tatu (REA III) kwa Mkoa wa Shinyanga, kuhakikisha anaajiri wananchi wenye sifa kutoka maeneo hayo badala ya kuleta wafanyakazi kutoka mbali.

Alitoa maagizo hayo hivi karibuni katika Kijiji cha Negezi, wilayani Kishapu, Mkoa wa Shinyanga, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) kwa Mkoa huo.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani, akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Negezi, Wilaya ya Kishapu (hawako pichani), wakati wa uzinduzi wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III), kwa Mkoa wa Shinyanga. Uzinduzi huo ulifanyika hivi karibuni.

“Tumia wataalam/vibarua vijana kutoka maeneo haya. Hatutapenda uajiri watu kutoka mbali wakati wafanyakazi wenye sifa wako hapahapa,” alisema Naibu Waziri. Aidha, Dkt. Kalemani, alimwagiza Mkandarasi huyo kuhakikisha anawalipa vibarua mara moja kila wanapokamilisha kazi husika. “Hakuna kulaza malipo kwa sababu sisi tunakulipa vizuri.”

Sambamba na maagizo hayo, Dkt Kalemani, aliutaka uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani humo, kujipanga na kumsimamia Mkandarasi husika ili kuhakikisha anafanya kazi masaa 24 kwa siku. Alisisitiza kuwa, Ofisa yeyote atakayelegalega kumsimamia Mkandarasi husika kadri inavyotakiwa. Atawajibishwa kwa kuondolewa katika nafasi yake.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani, akiwatunza na kujumuika kucheza ngoma pamoja na moja ya vikundi vya burudani kutoka Shinyanga, kilichokuwa kikitumbuiza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III), kwa Mkoa wa Shinyanga hivi karibuni.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

WAZIRI MKUU AWAKARIBISHA WA ISRAEL KUWEKEZA NCHINI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewakaribisha wawekezaji kutoka nchini Israel waje nchini kuwekeza kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya  kilimo.

Ametoa kauli leo (Jumatano, Aprili 5, 2017) alipokutana na Balozi wa Israel nchini Tanzania, Mheshimiwa Yahel Vilan, Ofisini kwake Bungeni mjini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema Tanzania na Israel ni nchini ambazo zina uhusiano mzuri kwa muda mrefu, ambapo ameahidi kwamba Serikali itaendelea kuudumisha.

Pia Waziri Mkuu amewakaribisha raia wa Israel kuitembelea Tanzania kama watalii kwa sababu kuna fursa nyingi za utalii ukiwemo mlima wa Kilimanjaro na mbuga nyingi zilizosheheni wanyama.

Kwa upande wake, Balozi Vilan  ameipongeza Serikali kwa utendaji wake, ambapo amesema viongozi wa makampuni 50 kutoka nchini Israel wanatakuja nchini mwaka huu kushiriki katika jukwaa la biashara na uchumi kati ya Tanzania na Israel.

Amesema mbali na kushiriki katika jukwaa hilo, pia viongozi wa makampuni hayo watapata fursa ya kuangalia maeneo mbalimbali ya uwekezaji nchini.

Pia Balozi Vilan amesema Serikali ya Israel itaimarisha kitendo cha wagongwa mahututi (ICU) katika hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa mkoani Dodoma pamoja na kuwajengea uwezo watumishi wa kitengo hicho.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Israel nchini, Mheshimiwa Yahel Vilan, mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya, kabla ya mazungumzo yao ofisini kwa Waziri Mkuu, Bungeni Mjini Dodoma Aprili 5, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na balozi wa Israel nchini, Mheshimiwa Yahel Vilan, mwenye makazi yake jijini Nairobi Kenya, Ofisini kwa Waziri Mkuu bungeni mjini Dodoma Aprili5, 2017. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu).

WAFICHUENI WASIO NA SIFA YA KUPATA KITAMBULISHO CHA UTAIFA - RC MASENZA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza, amewataka wananchi Mkoani humo, kutoa ushirikiano kwa mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA, ili kuwabaini watu ambao si raiya wa Tanzania na wanalengo la kujipatia vitambulisho vya uraiya kinyume cha sheria za nchi.

Taarifa ya kitengo cha habari na Mawasilino cha halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, imetanabaisha kuwa, Mkuu wa Mkoa ametoa rai hiyo katika viwanja vya Mashujaa mjini Mafinga, wakati akizindua zoezi la uandikishaji vitabulisho vya uraiya kwa wananchi wa Mkoa wa Iringa, zoezi ambalo linaratibiwa na mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA.

Bi. Masenza, amesema, kabla ya ugawaji vitambulisho hivyo, NIDA wataendesha zoezi la kubaini watu ambao si raiya na wanania ovu ya kujipatia vitambulisho, hivyo akawataka wakazi wa Mkoa wa Iringa kuonesha uzalendo kwa kuwafichuo wale wote wasio na sifa za uraiya kwa usalama wa Taifa na watu wake.

Naye kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka wa vitambulisho vya Taifa NIDA Bw. Andrew Masawe, amesema mpaka sasa jumla ya Watanzania milioni 08 laki 04 na 99 elfu wametambuliwa na kukabidhiwa vitambulisho vya uraiya na kuongeza kuwa baada ya kukamilika kwa vitambulisho vya watumishi wa umma, zoezi hilo linaamia rasmi kwa wananchi na akawataka wananchi kuona umuhimu wa kutambuliwa kupitia vitambulisho hivyo.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza akimkabidhi kitambulisho chake mmoja kati ya wakazi wa mji wa Mafinga wakati wa uzinduzi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza akihutubia wananchi katika viwanja vya Mashujaa mjini Mafinga.
Umati wa wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi huo kwenye kiwanja cha Mashujaa Mjini Mafinga.

MZAZI ASIYEPELEKA MTOTO WAKE SHULE HADI SASA KUKIONA - DC SANGA

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi, Mkuranga

MKUU wa wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani, Filberto Sanga amewataka wazazi ambao watoto wao wamefaulu kuingia kidato cha kwanza kuwapeleka shule mara moja, na atakaebainika kukaa na mtoto nyumbani atakiona.

Aidha amewataka wazazi wenye watoto waliofikia umri wa kuanza darasa la kwanza kwenda kuwaandikisha bila kufanya ajizi. Amesema kuanzia sasa ataambatana na timu yake, kupita kuhakiki kijiji hadi kijiji na endapo atakutwa mtoto hajapelekwa shule mzazi wake atafikishwa mahakamani.

Sanga alisema msimamo huo,wakati akizungumza katika kata ya Msonga, Magawa, Njianne, Kitomondo na Mwarusembe wilayani hapo kwenye mikutano ya ndani iliyoandaliwa na Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani.

Alieleza licha ya serikali kuagiza elimu kutolewa bure kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha nne lakini wapo wazazi mpaka sasa wanaoshindwa kuwapeleka shule watoto wao kwa sababu zisizoeleweka.

Sanga alisema atalivalia njuga suala hilo hadi hapo atakapohakikisha watoto hao wameripoti mashuleni. Alifafanua kwamba sekta ya elimu haina utani hata kidogo na ni haki ya mtoto .

Sanga alibainisha kwamba, watoto bila kuwa na elimu wilaya hata mkoa na taifa haitojikomboa. "Asilimia 80 ndio walioripoti mashuleni wengine wapo majumbani ,hivyo wazazi wawe na mwamko wa elimu ili kuwakomboa watoto wao” “Serikali inachangia vitu vyote vya msingi ,sioni sababu ya mzazi kukaa na bila elimu, atakaekaidi agizo hili afikishwe mahakamani”alisisitiza Sanga.

Kwa upande wake,katibu wa siasa na uenezi CCM mkoani Pwani, Zainab Gama, aliwataka wazazi kuwalinda na kuwalea watoto kwa umoja kwani mtoto wa mwenzio ni wako. Alisema vijana wengi wanaharibika kutokana na kuiga maadili ya nchi za nje na kushawishiana.

Gama aliiomba jamii kukemea watoto na vijana ambao wanakiuka mila, desturi na maadili ya nchi bila kuwaonea aibu. Nae katibu wa CCM wilaya ya Mkuranga, Abihudi Shilla alisema anaunga mkono suala la watoto kufikishwa shule kwa wakati kwa kuwa anatambua umuhimu wa elimu.

Shilla anasema, endapo watu wanachangia harusi na sherehe kuna kila sababu ya kuipa kipao mbele elimu ili kuwajengea watoto msingi bora katika maisha yao ya baadae.

PROFESA MUHONGO AZINDUA JUKWAA LA NISHATI TANZANIA

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akifungua mkutano wa wadau wa nishati ulioambatana na uzinduzi wa Jukwaa la Nishati Tanzania (TEP) kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu jijini Dar es Salaam tarehe 05 Aprili, 2017. Lengo la mkutano huo lilikuwa ni kujadili upatikanaji wa nishati endelevu ya kutosha kwa bei nafuu kwa ajili ya uchumi wa viwanda Tanzania.

Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo amesema nishati ya  uhakika ya umeme itatokomeza umasikini nchini  Tanzania ifikapo mwaka 2030. Profesa Muhongo aliyasema hayo alipokuwa akizindua Jukwaa la Nishati  Tanzania (TEP) pamoja na  mkutano wa siku mbili  kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu mapema leo jijini  Dar es Salaam.

Mkutano huo unaolenga kujadili upatikanaji wa nishati endelevu ya kutosha kwa bei nafuu kwa ajili ya uchumi wa viwanda Tanzania, unakutanisha wadau mbalimbali zikiwemo kampuni za utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi nchini kama vile Statoil,  BG na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
Sehemu ya wadau wa nishati wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani) katika mkutano huo.

 Wadau wengine ni pamoja na  kampuni za kuzalisha umeme kama  vile Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Songas pamoja na  mabalozi wa nchi mbalimbali,  taasisi za kifedha na viongozi wa kiserikali.

KESI YA MAUAJI YA DK. SENGONDO MVUNGI KUSIKILIZWA MAHAKAMA KUU, MASHAHIDI 30 KUSIKILIZWA

$
0
0
Na Karama Kenyunko

Jumla ya Mashahidi 30 wanatarajiwa kutoa ushahidi katika Mahakama kuu Kanda ya Dar es Salaam kufuatia kesi ya mauaji ya kukusudia ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk. Sengondo Mvungi.

Mwendesha Mashtaka, wakili wa serikali Patric Mwita ameileza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  leo, baada ya kumaliza usiklilizwaji wa awali kwa kusoma ushahidi wa mashahidi thelesini mbele ya Hakimu Mkazi mkuu Thomas Simba.

Aidha wakili Mwita amedai kuwa wakati wa usikilizwaji pia vielelezo 13 vikiwemo, mapanga, bastola, postmortem ya daktari na hati ya ukamatwaji vitawasilishwa mahakamani hapo.

Jumla ya watuhumiwa 12 walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza mwaka 2013 ambapo wanne waliachiwa huru huku mmoja akifariki dunia.

Watuhumiwa waliofutiwa kesi na kuachiwa huru baada ya DPP kuondoa mashtaka dhidi yao kwa kuwa hana nia ya kuendelea kuwashtaki ni Hamad kitabu, Zacharia Msese na Masunga Makenza. Mshtakiwa aliyefariki alifahamika kwa jina la Chibago Chiuguta. 


Watuhumiwa ambao wanakesi ya kujibu na kesi yao itasikilizwa mahakama kuu baada ya kupangiwa tarehe ya kusikilizwa ni Chibago Magozi, Juma Mangungu, Paulo Mdonondo,  Mianda Mlewa, Msingwa Matonya.
Wengine ni aliyekuwa mlinzi wa marehemu Dk Mvungi, Longishu Losingo na John Mayunda.
Baada ya maelezo ya mashahidi kusomwa, washtakiwa wameileza mahakama kuwa watatotoa maelezo yao mbele ya wakili wao ambaye watepatiwa pindi wakifika mahakama kuu.
Kufuatia hayo kesi hiyo sasa inasubiri kupangiwa tarehe ya usikilizwaji (session). Washtakiwa wamerudishwa mahabusu.

Inadaiwa kuwa Novemba 3, mwaka 2013, huko Mbezi eneo la Msakuzi Kiswegere washtakiwa walimuua Dk. Sengondo Mvungi .
Walitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 196 cha sheria na kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002. Marehemu Mvungi alizikwa baadae kijijini kwao Chanjale Kisangara juu.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images