Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

UJUMBE WA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KWA WATANZANIA KUHUSU SERENGETI BOYS


Article 0

SIMBA ILIVYOINGIA GEITA NA KUPOKELEWA KWA SHANGWE NA MASHABIKI WA MKOA HUO

$
0
0
MSAFARA wa Kikosi cha timu ya Simba kimewasili salama jana jioni mkoani Geita ambapo watakaa kwa muda wa siku tatu kabla ya kueleka Jijini Mwanza kwa mechi mbili za ligi kuu Vodacom.

Simba waliotokea Mkoani Kagera walipokuw ana mechi dhidi ya Kagera Sugar waliingia mkoani Geita na kulakiwa kwa shangwe kubwa na wanachama pamoja na mashabiki wa timu hiyo na kuwataka wajihisi wapo nyumbani.

Kikosi cha wanamsimbazi kitaweka kambi ya siku tatu pia kinaweza kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Geita ya mkoani humo ikiwa ni moja ya maandalizi ya mchezo wao wa ligi kuu 


 Gari ya timu ya Simba ikiingia Mkoani Kagera wakiongozwa na msafara wa mashabiki wa timu hiyo.
 Mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Laudit Mavugo akishuka kutoka katika gari ya wachezaji wa timu hiyo wakiwa wanasili Mkoani Geita.
 Mwinyi Kazimoto akishuka kutoka katika gari ya wachezaji wa timu hiyo wakiwa wanasili Mkoani Geita
 Beki wa timu ya Simba raia wa Kongo Besela Bukungu akishuka kutoka katika gari ya wachezaji wa timu hiyo wakiwa wanasili Mkoani Geita.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

BARABARA ZA ARUSHA KUKAMILIKA MWAKA HUU

$
0
0
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akikaza nati katika daraja la Nduruma lenye urefu wa mita 60 linalojengwa katika barabara ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa KM 14.1 wakati alipokagua barabara hiyo, mkoani Arusha leo.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto), akikagua moja ya daraja lililopo katika barabara ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa KM 14.1 inayojengwa na Mkandarasi wa Kampuni ya M/S Hanil Jiangsu J/V wakati alipokagua barabara hiyo, mkoani Arusha leo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na wakazi wa eneo la Sakina mkoani Arusha mara baada ya kukagua barabara ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa KM 14.1.


Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akifafanua jambo kwa uongozi wa Kampuni ya ujenzi ya Chicco, wakati alipokuwa akikagua barabara ya Kia-Mererani yenye urefu wa KM 26, mkoani Arusha, leo. 

TRA YAKUSANYA TRILIONI 10.87 KWA KIPINDI CHA MIEZI TISA

$
0
0
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipakodi ,Richard Kayombo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo juu ya mafanikio katika kukusanya kodi.

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), imefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi Trilioni 10.87katika kipindi cha miezi tisa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/2017 kuanzia juni 2016 hadi March 2017.

Hayo yamesemwa mapema leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa huduma na Elimu kwa mlipa kodi, Richard Kayombo na kutaja kuwa makusanyo hayo ni ukuaji wa asilimia 9.99 ukilinganisha na makusanyo yaliyopita katika mwaka wa fedha uliopita.

“katika mwezi wa machi 2017 TRA imekusanya trilioni 1.34 ukilinganisha na trilioni 1.31 ya mwezi machi mwaka 2016 ambao ni sawa na ukuaji wa asilimia 2.23 ,mamlaka ya mapato Tanzania inawashukuru walipa kodiwote ambao wameitikia wito wa kulipa kodi ya serikali kwa hiari kila wakati na hivyo kuiwezesha mamlaka kutimiza wajibu wake kisheria”Amesema Kayombo.

Amesema kuwa pamoja na mafanikio tuliyopata katika kipindi cha miezi tisa iliyopita mamlaka kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2016/2017 na cha miezi mitatu kinachoanza April mpaka juni itaelekeza juhudi zake katika kukusanya kodi mbalimbali.

MAMA SALMA KIKWETE AAPISHWA KUWA MBUNGE

$
0
0
Spika wa bunge, Job Ndugai akimwapisha Mama Salma Kikwete kuwa mbunge, bungeni mjini Dodoma Aprili 4, 2017.
Mama Salma Kikwete akiapa kuwa mbunge, bungeni mjini Dodoma Aprili 4, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Mama Salma Kikwete baada ya kuapishwa kuwa mbunge, bungeni mjini Dodoma Aprili 4, 2017.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Jakakaya Mrisho Kikwete akishiriki kuimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza kwa kikao cha bunge mjini Dodoma Aprili 4, 2017. Mheshimiwa Kikwete alikwenda bungeni kushuhudia kuapishwa kwa mkewe mama Salma. Kushoto ni mwanae Ali Kikwete na kulia ni msaidizi wake Bw. Togolani Mavula.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RWANDAIR KUANZISHA SAFARI ZA LONDON

$
0
0
Shirika la Ndege la RwandAir linataji kunzisha safari zake mara tatu kutokea Jijini Dar es Salaam kuelekea London Gatwick, kuanzia Mei 26, 2017 huku bei ikiwa ni kuanzia dola 200 bila gharama za viwanja. 
Akilizungumza hilo, Meneja mkazi wa Shirika la RwandAir hapa nchini, Ibrahim Bukenya amesema shirika lake limekuwa likizidi kukua siku siku hadi siku na kuendelea, kwani jana April 3, 2017 Shirika hilo limeanzisha safari zake kuelekea Bombay nchini India na Harare Zimbabwe. Shirika hilo la RwandAir litaanzisha safari zake nyingine nyingi katika mwaka huu wa 2017 na pia kuongeza ndege nyingine kubwa.

DENI LA TFF, SERENGETI BOYS WAPIGWA CHINI WAKIELEKEA KWA MAKAMU WA RAIS

$
0
0


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

MAMALAKA ya Mapato Tanzania (TRA) kupitia kampuni ya Yono, wamelikamata basi la timu ya Taifa linalomikiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) ambalo kwa sasa linatumiwa na timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys. 

Gari hiyo imechukuliwa katika Hotel ya Urban Rose likiwa linawasubiri wachezaji wa Serengeti Boys liwapeleke kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Sulu

Akizungumza na Michuzi Globu, Mkurugenzi Mtendaji wa Yono Scolastica Kevela amesema kuwa wamelikamata gari za Taifa Stars leo mchana na wataendelea kuzikamata mali zingine zinazomilikwa na Shirikisho hilo.

Mama Kevela amesema kuwa, maagizo ya kuzikamata mali za TFF ni maagizo kutoka mamlaka ya Mapato na wataendelea kuzishikilia mpaka pale watakapolipa deni hilo sugu wanalodaiwa.

"tumeendelea kuzishikilia mali za TFF mpaka pale watakapolipa deni lao sugu, takribani wiki tatu tulifunga ofisi zao na uwanja pae Karume na tutaendelea kuzitafuta mali zao popote zilipo,"amesema Kevela.

Deni la TFF linatokana na kodi za mishahara ya aliyewahi kuwa kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars, Marcio Maximo kwa takribani miaka minne tokea 2016 hadi 2010 pamoja na mechi ya Brazili na Taifa Stars mwaka 2010 ambapo kodi yake haikulipwa mpaka leo.



Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) wamethibitisha hilo na kusema kuwa Wakati Serengeti Boys wakielekea kwenda nyumbani kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kupata naye chakula cha jioni kwa mwaliko wake, maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wamekamata basi wanalotumia na kuwashusha njiani. Viongozi wa Serengeti Boys wanatafuta basi jingine kuitikia mwaliko wa Mama Samia na huenda wakachelewa mwaliko kutegemea kupatikana kwa usafiri mwingine.

Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo Selestine Mwesigwa amesema kwamba deni hilo si la kwao peke yao kwani Wizara na Hazina ndio walengwa wakuu na wanaoathirika ni wao TFF na wamejaribu kumtafuta Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo, Profesa Ole Gabirel ili kukutana kutatua tatizo hilo, lakini kwa bahati mbaya hawajafanikiwa.

Timu ya achezaji wa Serengeti Boys wamealikwa nyumbani kwa Mama Samia kwenye hafla maalum ya kuagwa kabla ya safari ya Morocco kesho kwenda kuweka kambi ya mwezi mmoja kujiandaa na fainali za U-17 Afrika nchini Gabon Mei mwakani na inatarajiwa kuondoka kesho Saa 10: 45 jioni kwa ndege ya Emirates kwenda Morocco kupitia Dubai, ambako watalala siku moja.

Kauli ya Zitto Kabwe juu ya uteuzi wa prof Kitila....

$
0
0
Uteuzi wa Prof. Kitila Mkumbo kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji

Leo asubuhi Rais John Pombe Magufuli amemteua Mshauri wa Chama chetu Prof. Kitila Mkumbo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji. 

Chama cha ACT Wazalendo kimepokea kw mikono miwili taarifa juu ya uteuzi wa mshauri wa chama chetu Kwa sababu imeonyesha kuwa Rais ameona kuwa hata Watanzania walio kwenye Vyama vya Upinzani wana uwezo, weledi na uzalendo wa kutumikia nchi yetu.

Kwa nafasi hii ya Ukatibu Mkuu wa Wizara, ndugu Kitila hawezi kuendelea kuwa Mshauri wa Chama nafasi ambayo inamfanya kuhudhuria vikao vyote vya Chama ikiwemo Kamati Kuu. Ndugu Mkumbo ameandika barua ya kujiuzulu nafasi yake ya mshauri wa Chama na kubaki kuwa mwanachama wa kawaida tu. Nimeipokea barua yake na kumkubalia Kwa maslahi mapana ya nchi yetu.

ACT Wazalendo tunamshukuru ndugu Kitila Mkumbo kwa mchango wake katika uongozi wa Chama chetu kwa wakati wote ambao alikitumikia Chama chetu kama mshauri wa chama. Msimamo wa chama chetu ni utumishi wa kizalendo kwa Taifa utokanao na kila mwananchi, ndio msingi wa kaulimbiu yetu ya 'Taifa Kwanza, Leo na Kesho', hivyo basi tunamtakia kila la kheri ndugu Kitila katika utumishi wake kwa Taifa letu katika nafasi yake hii mpya. 

Wizara Hii ni kubwa na muhimu Sana kwa nchi yetu. Maji ni tatizo moja kubwa ambalo wananchi wetu wanakumbana nalo na Kama Taifa hatujaweza kulimaliza. Tunamtakia kila la kheri ndugu Mkumbo katika kuongeza nguvu kumaliza kero ya maji na kuhakikisha tunaimarisha Kilimo cha Umwagiliaji nchi nzima. 

Tunamsihi aanze na ajenda ya Mfuko wa Maji Vijijini na kuanzishwa Kwa Wakala wa Maji Vijijini utakaosimamia upatikanaji wa Maji Kwa wananchi wetu.

Kwa hatua hii, tunaona Rais ameamua kuunganisha nchi yetu Kwa kufanya kazi na watu wote bila kuwabagua Kwa itikadi zao za vyama. Watanzania ni wamoja na kauli za kuwagawa zinaumiza zaidi Taifa kuliko kuliweka pamoja. Tunaamini kuwa Rais Ana nia njema katika uteuzi huu na sisi tumempa baraka zote Mwanachama wetu mwanzilishi wa Chama kwenda kwenye nafasi ya juu zaidi ya utumishi wa umma. Tunaamini hatamwangusha Rais na muhimu zaidi hatawaangusha Watanzania.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama - ACT Wazalendo
Aprili 4, 2017
Dodoma

DAR CITY YAICHAPA BOKO VETERANS BAO 3-2

$
0
0
Mchezaji wa timu ya Dar City, Shadrack Nsajigwa akiondoka na huku akisindikizwa na Mchezaji wa Timu Boko Veterans wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Boko Veterani mwishoni mwa wiki. Katika mchezo huo Dar City ilishinda mabao 3-2, kupitia kwa wachezaji wake Makocha Tembele na Salvatory Edward. Kikosi cha Dar City kinaundwa na wachezaji mbalimbali waliowahi kutamba katika Ligi Kuu Tanzania miaka ya nyuma pamoja na .
Kiungo hodari wa Dar City, Shaffih Dauda akiwania mpira na Mchezaji wa Timu Boko Veterans wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Boko Veterani mwishoni mwa wiki. Katika mchezo huo Dar City ilishinda mabao 3-2, kupitia kwa wachezaji wake Makocha Tembele na Salvatory Edward. Kikosi cha Dar City kinaundwa na wachezaji mbalimbali waliowahi kutamba katika Ligi Kuu Tanzania miaka ya nyuma pamoja na baadhi ya wadau wa soka na wanahabari.
Kiungo wa Timu ya Dar City, Tippo Athuman al maarufu Zizzou ambaye ni muasisi wa timu hiyo, akitafuta namna ya kuwatoka mabeki wa Timu ya Boko Beach Veterans, wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Boko Veterani mwishoni mwa wiki. 
Nahodha wa Timu ya Boko Beach Veterans, John Dilinga a.k.a Dj JD akiajiandaa kuachia shuti.
Makocha Tembele (katikati) akiwasakata wachezaji wa Boko Veterans, Godfrey Ngonyani (kushoto) na John Dilinga 'Dj Jd'.

WAZIRI MKUU MAJALIWA MGENI RASMI MAONESHO YA MIFUKO YA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI

$
0
0
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa atafungua maonesho ya Mifuko ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi yatakayofanyika mkoani Dodoma katika viwanja vya mashujaa kuanzia tarehe 18-22 April 2017. 

Akizungumza na waandishi wa Habari Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC) Bi.Beng’i Issa amesema Maonyesho hayo yameandaliwa na Baraza hilo kwa lengo la kutoa elimu kwa umma juu ya huduma mbalimbali zitolewazo na mifuko yote ya uwezeshaji wananchi kiuchumi. 

“Tumeamua kufanya maonesho haya kwa mara ya kwanza kwa sababu changamoto kubwa tuliyonayo ni kuwa mifuko hii haifahamiki sana na wananchi, wengi walikuwa hawajui wafanye nini ili waweze kupata fursa ya kupata mitaji na kusaidiwa na mifuko hii ambayo imeanzishwa na Serikali kwa ajili yao”,Aliongeza Bi.Beng’i. 

Amesema maonyesho hayo yatawapa wananchi fursa ya kuonana na watu ambao wamefanikiwa katika kipindi kilichopita na hasa kujua jinsi gani watafaidika na mikopo ambayo inapatikana kupitia mifuko hii. 

Ameitaja mifuko ambayo itashiriki ni pamoja na Mfuko wa kuendeleza wajasiriamali wananchi, Mfuko wa Uwezeshaji wa Mwananchi, Mfuko wa Pembejeo za Kilimo , Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Mfuko wa Dhamana za mikopo kwa wajasiriamali wadogo na wa kati na Mfuko wa Dhamana za Mikopo kwa Mauzo ya Nje ya Nchi. 

Mifuko mingine ni Mfuko wa kuwasaidia makandarasi,Mfuko wa Maendeleo ya Jamii,Mfuko wa Misitu Tanzania,SELF Microfinance Fund na PASS Trust Fund. 

Kauli mbiu ya Maonyesho haya ni “WEZESHA WANANCHI KIUCHUMI ILI KUJENGA UCHUMI WA KATI NA TANZANIA YA VIWANDA” 

 Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi.Beng’I Issa akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya Maonesho ya Mifuko ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi yatakayofanyika katika viwanja vya mashujaa kuanzia tarehe 18-22 April 2017.
 Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi.Beng’I Issa akimsikiliza Mhasibu Mkuu kutoka Mfuko wa Rais wa kujitegemea Bw.Ahazi Kibona juu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo.
Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi.Beng’I Issa akizungumz ana waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya Maonesho ya Mifuko ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi yatakayofanyika katika viwanja vya mashujaa kuanzia tarehe 18-22 April 2017.

MAMA SAMIA AWATAKA WAFARANSA KUENDELEA KUWEKEZA TANZANIA.

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa Tanzania ni Moja ya nchi salama kwa ajili ya uwekezaji barani Afrika kwa sababu haina matatizo ya migogoro ambayo yanaweza kuhatarisha usalama wa mali ya wawekezaji ikilinganishwa na nchi nyingine barani Afrika.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati akifungua maonyesho ya Kibiashara kati ya Ufaransa na Tanzania yanayofanyika Jijini Dar es Salaam.

Makamu Rais Mhe Samia Suluhu Hassan pia amewakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchini Ufaransa kuja kuwekeza katika maeneo mbalimbali hasa katika kilimo, nishati, utalii,usafiri kutokana na hali ya amani na utulivu iliyopo nchini.

Makamu wa Rais amesema maonyesho hayo ya kibiashara ambayo yataambatana na kongamano kubwa la Kibiashara kati ya nchi hizo Mbili ni fursa ya kipekee kwa wafanyabishara wa Tanzania na Ufaransa kukutana na kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali ya kibiashara na uwekezaji.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Kongamano la kwanza la Biashara kati ya Ufaransa na Tanzania lililoandaliwa na Balozi wa Ufaransa nchini Bi. Malika BERAK (kulia), kushoto ni Mwenyekiti wa TPFS Dkt. Reginald Mengi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Balozi wa Ufaransa nchini Bi. Malika BERAK kabla ya kukaribishwa kuhutubia hotuba ya ufunguzi wa Wiki ya Kongamano la kwanza la Biashara kati ya Ufaransa na Tanzania lililoandaliwa na Balozi wa Ufaransa nchini linalo fanyika jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia moja ya picha ya majengo yaliosanifiwa na wataalamu wa majengo kutoka nchini Ufaransa kwenye maonyesho ya Bisahara kati ya Ufaransa na Tanzania lililoandaliwa na Balozi wa Ufaransa nchini.

ZANZIBAR FOOTBALL ASSOCIATION YAFANYA UCHAGUZI KUJAZA NAFASI ZILIZOACHWA WAZI

$
0
0
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama cha soka (ZFA) wilaya ya Magharibi A Unguja wamemchagua Haji   Issa Kidali kuwa Mjumbe wa ZFA Taifa kufuatia uchaguzi mdogo uliofanyika April 4 mwaka huu kujaza nafasi iliyoacha wazi na Mussa Suleiman Soraga aliefariki dunia Februari 24 mwaka huu.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika katika ofisi za ZFA Magharibi A, Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi huyo Othman Ali Hamad alimtangaza Kidali baada ya kupata kura 33 kati ya 43 zilizopigwa huku mpinzani wake Abdallah Bakari Abdallah akipata kura 10.

Uchaguzi huyo uliohudhuriwa na Katibu Mkuu wa ZFA Taifa Mohammed Ali Hilal Tedy na make wa mbunge wa jimbo la Mfenesini Mziwanda Ibrahim Abdallah aliekua Mgeni rasmi, pia aliekuwa Katibu wa timu ya Umoja Mbuzini Abrahman Saleh Rajab alichaguliwa kuwa Katibu Msaidizi wa ZFA hiyo kwa kupata kura 26 dhidi ya 16 alizopata mpinzani wake Mwajuma Ali Kombo kati ya kura 42 zilizopigwa.

Akizungumza kabla na baada ya kukamilika kwa uchaguzi huyo Mziwanda aliwapongeza wajumbe wa mkutano huyo na wagombea kwa kufanya uchaguzi guru na wa haki na kuwataka washindi hao kuendeleza umoja na mashirikiano ili kuongeza kazi ya maendeleo ya soka wilayani humo.

Katibu Mkuu wa ZFA Taifa Tedy aliwaasa viongozi wa chama hicho kufanya kazi kwa pamoja ili maendeleo ya soma ndani na nje ya wilaya hiyo yapatikane kwa haraka na kuwapongeza wagombea walioshinda na walioshindwa kwa kuoneaha ukomavu wa michezo na kuahidi kuwapa ushirikiano washindi. 
Akifunga mkutano huo Mwenyekiti wa ZFA hiyo Kheri Adam Ali aliwakumbusha wajumbe wa mkutano huo umuhimu wa kuendelea mshikamano kati yao na kusahau mambo vote yanahusiana na uchaguzi humo ili kuendelea na ligi ya wilaya hiyo iliyopo katika hatua ya 12 bora.

Katika hatua nyengine Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mziwanda Ibrahim Abdallah alitoa ahadi ya kuzipatia timu zilizofuzu kucheza hatua ya nne bora ya wilaya hiyo seti moja ya jezi kila moja ili kuziongezea ari na motisha wa kushiriki ligi hiyo ambayo mshindi wa kwanza na wa pili wataiwakilisha wilaya hiyo katika mashindano ya ngazi ya Taifa.

Uchaguzi humo umefanyika ili kuziba pengo lililoachwa na Soraga aliefariki kwa ajali ya barabarani na kujiuzulu kwa Bakari katika wadhifa aliokuwa akiushikilia kabla ya kuomba kuchaguliwa katika uchaguzi humo..

KAMPUNI YA SIMU YA TTCL INAONGOZA KWA KUTOA HUDUMA ZA INTANET BORA NA ZA UHAKIKA

$
0
0

Kwa sasa, juhudi za Rais Dkt. Magufuli kufufua huduma bora na za uhakika katika Mashirika na Makampuni ya Umma zinazidi kuleta Matokeo chanyA+ Kampuni Simu ya TANZANIA -TTCL ndiyo kampuni pekee inayoongoza kwa sasa kwa kutoa huduma za intanet bora na za uhakika. Rais wangu... *mzalendo na mchapakazi..* Nchi yangu... *Matokeo chanyA+*

TAARIFA YA UTEUZI WA WAGOMBEA WA UJUMBE WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0
1.   Tarehe 17 Machi, 2017 nilitoa Tangazo kwenye Gazeti la Serikali Namba 376 kuhusu Siku ya uteuzi na Siku ya Uchaguzi. Katika Tangazo hilo, nilipanga Siku ya tarehe 30 Machi, 2017, saa Kumi (10.00) Jioni kuwa Siku ya Uteuzi wa Wagombea na pia siku ya tarehe 04 Aprili, 2017 saa Tano (5.00) Asubuhi kuwa Siku ya Uchaguzi wa Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki.


2.   Aidha, natoa shukrani zangu za dhati kwa wadau wote hususan Vyama vyote vya siasa nchini kwa ushirikiano mzuri nilioupata kutoka kwao katika zoezi zima la mchakato wa uteuzi wa wagombea.


3.   Vile vile, navipongeza na kuvishukuru vyama vyote vya siasa vyenye haki ya kushiriki uchaguzi kwa kuendesha mchakato wa uteuzi wa wagombea kwa uwazi na demokrasia kubwa.


4.   Pia navishukuru vyombo vya habari na wanahabari wote kwa ujumla kwa kuhabarisha umma kuhusu mchakato huu muhimu kwa Bunge na Taifa kwa ujumla.


5.   Kipekee nawashukuru na kuwapongeza wananchi wote waliojitokeza kupitia vyama vyao kugombea katika uchaguzi huu ambapo jumla ya Watu 505 walijitokeza kugombea kupitia vyama vifuatavyo:


Kauli ya Zitto Kabwe juu ya Uteuzi wa Prof. Kitila Mkumbo kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji

$
0
0

Leo asubuhi Rais John Pombe Magufuli amemteua Mshauri wa Chama chetu Prof. Kitila Mkumbo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji. Chama cha ACT Wazalendo kimepokea kw mikono miwili taarifa juu ya uteuzi wa mshauri wa chama chetu Kwa sababu imeonyesha kuwa Rais ameona kuwa hata Watanzania walio kwenye Vyama vya Upinzani wana uwezo, weledi na uzalendo wa kutumikia nchi yetu.
Kwa nafasi hii ya Ukatibu Mkuu wa Wizara, ndugu Kitila hawezi kuendelea kuwa Mshauri wa Chama nafasi ambayo inamfanya kuhudhuria vikao vyote vya Chama ikiwemo Kamati Kuu. Ndugu Mkumbo ameandika barua ya kujiuzulu nafasi yake ya mshauri wa Chama na kubaki kuwa mwanachama wa kawaida tu. Nimeipokea barua yake na kumkubalia Kwa maslahi mapana ya nchi yetu.
ACT Wazalendo tunamshukuru ndugu Kitila Mkumbo kwa mchango wake katika uongozi wa Chama chetu kwa wakati wote ambao alikitumikia Chama chetu kama mshauri wa chama. Msimamo wa chama chetu ni utumishi wa kizalendo kwa Taifa utokanao na kila mwananchi, ndio msingi wa kaulimbiu yetu ya 'Taifa Kwanza, Leo na Kesho', hivyo basi tunamtakia kila la kheri ndugu Kitila katika utumishi wake kwa Taifa letu katika nafasi yake hii mpya. Wizara Hii ni kubwa na muhimu Sana kwa nchi yetu. Maji ni tatizo moja kubwa ambalo wananchi wetu wanakumbana nalo na Kama Taifa hatujaweza kulimaliza. 
Tunamtakia kila la kheri ndugu Mkumbo katika kuongeza nguvu kumaliza kero ya maji na kuhakikisha tunaimarisha Kilimo cha Umwagiliaji nchi nzima. Tunamsihi aanze na ajenda ya Mfuko wa Maji Vijijini na kuanzishwa Kwa Wakala wa Maji Vijijini utakaosimamia upatikanaji wa Maji Kwa wananchi wetu.
Kwa hatua hii, tunaona Rais ameamua kuunganisha nchi yetu Kwa kufanya kazi na watu wote bila kuwabagua Kwa itikadi zao za vyama. Watanzania ni wamoja na kauli za kuwagawa zinaumiza zaidi Taifa kuliko kuliweka pamoja. Tunaamini kuwa Rais Ana nia njema katika uteuzi huu na sisi tumempa baraka zote Mwanachama wetu mwanzilishi wa Chama kwenda kwenye nafasi ya juu zaidi ya utumishi wa umma. Tunaamini hatamwangusha Rais na muhimu zaidi hatawaangusha Watanzania.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama - ACT Wazalendo
Aprili 4, 2017
Dodoma

Balozi Seif Ali Iddi atoa pole wananchi wa Kazole Kwagube walioathirika na upepo mkali jumapili

$
0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwapa pole Wananchi wa Kijiji cha Kwagube Kazole walioathiriwa Nyumba zao kutokana na upepo mkali uliovuma Jumapili iliyopita.
 Balozi Seif  akikabidhi fedha kwa mmoja wa Wananchi walioathirika na Upepo Mkali katika Kijiji cha Kwagube uliotokea Jumapili iliyopita.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimkagua Mkuu wa Mkoa wa zamani Bwana Pemba Juma Khamis alipofika nyumbani kwake Bububu Kijichi kuangalia hali yake kiafya baada ya kupata matibabu nchini India.
Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa Mjini Magharibi Bibi Johari Akida akibadilishana mawazo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alipofanya ziara ya kumkagua hali yake  Nyumbani Kwake Mwanakwerekwe. Picha na OMPR – ZNZ. 

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 04.04.2017

RAIS WA ZANZIBAR, DKT. SHEIN AZINDUA KITUO KIPYA CHA UNUNUZI WA KARAFUU ZSTC - PEMBA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akikata utepe kuzindua Kituo Kipya cha Shirika la ZSTC cha Ununuzi wa karafuu katika Kijiji cha Mgelema leo, Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba akiwa katika ziara ya kikazi,(kushoto) Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la ZSTC Dkt.Said Seif Mzee.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimina na Viongozi mbali mbali mara alipowasili katika Kijiji cha Ngomeni Wilaya ya Cheke Chake Mkoa wa Kusini Pemba leo,kuzindua Jengo la Kituo ZSTC,ujenzi wa Kituo cha Afya na Umeme kijijini hapo akiwa katika ziara maalum ya kikazi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na ujumbe wake walipokuwa wakipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Ardhi,Makaazi Maji na Nishati Mhe,Salama Aboud Talib wakati Dk.Shein alipofika katika kijiji cha Ngomeni Wilaya ya Chake chake leo kuangalia Umeme kijijini hapo sambamba na kuzindua Jengo la Kituo cha Ununuzi wa Karafuu cha ZSTC
Baadhi ya Mawaziri na Viongozi wengine waliohudhuria katika Uzinduzi wa Kituo Kipya cha Shirika la ZSTC cha Ununuzi wa karafuu katika Kijiji cha Ngomeni Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba,wakimsikiliza Waziri wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko Mhe,Amina Salum Ali alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,kuzungumza na Wananchi Kijijini hapo leo akiwa katika ziara ya kikazi
Transfoma Mpya iliyowekwa katika kijiji cha Ngomeni Wilaya ya Cheke Chake Mkoa wa Kusini Pemba,ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na ujumbe wake akiwa katika ziara zake za kikazi katika Mkoa wa Kusini Pemba leo alifika katika kijiji hcho kuangalia Umeme kijijini hapo sambamba na kuzindua Jengo la Kituo ZSTC. Picha na Ikulu, Zanzibar.

BALOZI WA ISRAEL MHE. YAHEL VILAN ATEMBELEA IDARA YA URATIBU WA MAAFA OFISI YA WAZIRI MKUU, DODOMA

$
0
0
Mwambata Jeshi wa Israel Barani Afrika Bw. Aviezer Segal akionesha michoro ya muundo wa Ofisi yake wakati wa ziara ya Balozi wa Israel Mhe. Yahel Vilan alipotembelea Idara ya Maafa ili kuangalia eneo lililotengwa kwaajili ya Ujenzi wa Kituo cha Kitaifa na Kimataifa cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura, Dodoma.

 Mratibu wa Maafa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Charles Msangi akionesha muundo wa Idara hiyo wakati wa ziara ya ya Balozi wa Israel Mhe. Yahel Vilan katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma Aprili 4, 2017.

 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (wa kwanza mwenye miwani) akifuatilia mada ya muundo wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa Ziara ya Balozi wa Israel Mhe. Yahel Vilan Dodoma.


 Waziri Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (wa pili kutoka kushoto) akizungumza na baadhi wa wageni walioambatana na Balozi wa Israel Mhe. Yahel Vilan alipotembelea Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Aprili 4, 2017 Dodoma.

 Mkurugenzi wa Idaya ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Brig. Jenerali, Mbazi Msuya (wa kwanza kushoto) akimuonesha Balozi wa Israel Mhe. Yahel Vilan ramani ya  eneo lililotengwa kwaajili ya Ujenzi wa Kituo cha Kitaifa na Kimataifa cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura, Dodoma.

 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na baadhi ya Watendaji wa Serikali walioshiriki katika ziara ya Balozi wa Israel Mhe. Yahel Vilan mara baada ya kumpokea Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images