Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

BALOZI WA UINGEREZA NCHINI BI. SARAH COOK AMTEMBELEA KAMISHNA JENERALI WA MAMLAKA YA KUDHIBITI NA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA BW. ROGERS WILLIAM SIYANGA.

$
0
0
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cook Leo amemtembelea ofisini kwake Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na  Kupambana na dawa za kulevya  Bw. Rodgers William Siyanga na kufanya mazungumzo ya  namna serikali za  Uingereza  na Tanzania zitakakavyoweza kushirikiana katika kudhibiti tatizo la dawa za kulevya . Katika ziara hiyo Balozi Cook aliambatana na maafisa kutoka ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania  Bw. Christopher Kiddle na Bw. Andrew Stephens.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cook (wapili kutoka kushoto) alipomtembelea  Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na  Kupambana na dawa za kulevya  Bw. Rodgers William Siyanga (wa kwanza kulia) ofisini kwake leo asubui Jijini Dar es salaam. Balozi Cook aliambatana na maafisa kutoka ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania Bw. Christopher Kiddle (wa kwanza kushoto) na Bw. Andrew Stephens (wa tatu kushoto), kutoka kulia (wapili) Makamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti na  Kupambana na dawa za kulevya


DC MUHEZA: AHIMIZA WANAFUNZI KUSOMA MASOMO YA SAYANSI KWA BIDII WILAYANI MUHEZA

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo akitubia wananchi wa wilaya ya Muheza na wadau wa elimu katika maadhimisho ya ya Juma la Elimu wilayani Muheza kushoto ni Kaimu Afisa Elimu Msingi wilayani Muheza,Stuart Kuziwa.
Kaimu Afisa Elimu Msingi wilayani Muheza,Stuart Kuziwa akizungumza katika maadhimisho hayo ambayo yalifanyika kwenye viwanja vya Jitegemee wilayani humo.
Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo akikagua maonyesho ya Juma la wiki ya Elimu wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Jitegemee wilayani Muheza.
Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa pili kulia akikagua maonyesho ya Juma la wiki ya Elimu wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Jitegemee wilayani Muheza.

DAKIKA 360 ZA REKODI AZAM FC VS YANGA LIGI KUU

$
0
0

MACHO ya wapenzi wengi wa soka nchini wikiendi hii yatakuwa kwenye viwanja viwili nchini, lakini asilimia kubwa wanausubiria kwa hamu mtanange wa aina yake kati ya wapinzani Azam FC na Yanga, utakaofanyika kesho Jumamosi katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Jumapili vita nyingine itahamia mkoani Kagera, pale wenyeji Kagera Sugar watakapokuwa wakiikaribisha Simba katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, mechi zote hizo zikitarajiwa kuamua hatima ya nafasi nne za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL). 

Wakati Azam FC iliyo nafasi ya tatu kwa pointi 44 ikiwa kwenye vita kali ya kusogelea nafasi mbili za juu kileleni, inapambana na Yanga (53) ambayo ipo kwenye mchuano mkali na Simba (55) wa kuwania taji la ligi hiyo. 

Ushindi wowote wa Azam FC na Kagera Sugar, ambazo nazo zinafukuzana kuwania nafasi ya tatu, utakuwa unaziweka kwenye nafasi nzuri timu hizo kuzisogelea zaidi timu za juu na kuzitibulia mipango ya ubingwa Simba na Yanga. 

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

NAIBU BALOZI WA VIJANA WA EAC ATOA SOMO KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU JIJINI ARUSHA

$
0
0
Naibu Balozi wa vijana wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Suzane William Mollel (kulia), akizungumza katika Warsha ya siku moja kwa Wanafunzi wa vyuo vikuu, ikiwa ni katika kuwahamasifa wanafunzi hao kuufahamu umuhimu wa Ushirikiano wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, iliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Makumira jijini Arusha, Machi 30, 2017. Jumla ya Wanafunzi 190 kutoka vyuo mbalimbali nchini, walihudhulia Warsha hiyo.
Naibu Balozi wa vijana wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Suzane William Mollel, akisikiliza maoni ya mmoja wa wanafunzi waliohudhulia kwenye warsha hiyo, juu ya ufahamu wake wa Ushirikiano wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, iliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Makumira jijini Arusha, Machi 30, 2017.

TUNATAKA POINTI 3 ZA AZAM KESHO - NIYONZIMA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Kuelekea kwenye mtanange wa Ligi Kuu Vodacom kati ya Yanga na Azam, Nahodha msaidizi wa timu ya Yanga kiungo mchezeshaji Haruna Niyonzima ameongelea mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa kesho katika dimba la Uwanja wa Taifa. 

Niyonzima amesema kuwa  wao kama wachezaji wamejiandaa vyema kisaikolojia kushinda mchezo wa kesho dhidi ya Azam  ili kuzipata alama tatu muhimu katika harakati za kulitetea kombe lao wanalolishikilia .

" namshukuru mungu  binafsi nipo vyema kwa ajili ya mchezo wa kesho, mwalimu akinipa nafasi hakika nitatimiza majukumu yangu vyema pamoja na wenzangu ili kuhakikisha timu yetu inashinda ,"amesema Niyonzima 

Amesema kuwa waalimu wanawaandaa vyema kushinda mchezo huo na mingine iliyobaki ili kuhakikisha tunatetea ubingwa wetu . 

Niyonzima alienda mbali zaidi kwa kuwataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kuwapa sapoti ili kuwatia nguvu kwa dakika zote 90. 

" naheshimu sana mchango wa mashabiki wetu katika timu hii  na kulitambua hilo  nawaomba kesho wajitokeze kwa wingi ili kutupa sapoti , ari na nguvu ya kupambana muda wote wa dakika 90 dhidi ya Azam FC kwani ni timu nzuri na sote tunajuana vyema hivyo umakini unahitajika katika kuwakabili, "amesema Niyonzima.

Yanga itawakosa mabeki wake wawili Hassan Kessy na Kelvin Yondani kwa kuwa na kadi  tatu za njano ila mpaka sasa uhakika wa washambuliaji wake wawili Mzimbabwe Donald Ngoma na Mrundi Amisi Tambwe ambao bado  ni majeruhi wa goti.

Yanga kesho tarehe 1 , April watakuwa uwanja wa taifa kupepetana na Azam FC katika mchezo wa 25 wa ligi kuu Tanzania bara kuelekea ukingoni mwa ligi hiyo.

DAWASCO YAONDOA KERO YA MAJISAFI YA MIAKA 30 MANZESE MVULENI

$
0
0
Katika kuhakikisha kero ya Maji inakwisha kwenye maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (DAWASCO) limezindua vizimba 8 vya Majisafi katika mtaa wa Mvuleni uliopo katika kata ya Manzese wilaya ya Kinondoni, ili kuwapunguzia wakazi wa maeneo hayo adhaa ya kutafuta Majisafi na salama kutoka umbali mrefu baada ya kuyakosa kwa takribani miaka 30.

Akizungumza katika uzinduzi huo wa vizimba vya Majisafi, Meneja wa Dawasco mkoa wa Magomeni, Mhandisi Pascal Fumbuka, ameeleza kuwa wameamua kufikisha huduma ya Majisafi katika mtaa huo wa Mvuleni kwa njia ya kujenga vizimba vya Majisafi kutokana na eneo hilo kutoingilika kimtaa, hivyo kupelekea kushindwa kuweka mabomba ya Majisafi ya nyumba kwa nyumba.

Aidha, Mhandisi Fumbuka ameongeza kuwa, wapo kwenye jitihada za kuongeza mradi mdogo wa bomba la inchi 6 ambalo litasaidia kuongeza msukumo wa Majisafi ili kuwahudumia wakazi wengi zaidi wa maeneo hayo ya Mvuleni pamoja na mitaa jirani ya Muungano na Kilimani.

“Katika kutatua kero ya Maji hapa Manzese Mvuleni, tumejenga vizimba vya Majisafi nane na tunatarajia wakazi zaidi ya elfu thelathini na sita watanunufaika na vizimba hivi. Tumeshindwa kufikisha bomba kwa kila mkazi kutokana na ujenzi holela wa makazi ya watu, lakini tuamini kuwa vizimba hivi vitasaidia kuondoa kero ya Maji kutokana na msukumo wake wa Maji kuwa mkubwa, hivyo tunaamini havitaleta msongamano pamoja usumbufu kwa wakazi pale watakapokuwa wanakinga Maji” alisema Mhandisi Fumbuka.

Kwa upande wa mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mvuleni Bw. Mrita Mzee ameishukuru Dawasco kwa kujenga vizimba hivyo vya Majisafi kwani wakazi wa mtaa wake walikuwa wakipata adhaa ya kutafuta Majisafi na salama kutoka umbali mrefu na kwa muda mrefu, amewataka wananchi kuvitunza pamoja na kuvilinda vizimba hivyo vya Majisafi ili viweze kuwasaidia kwa kipindi kirefu zaidi.

“Nawashukuru sana Dawasco Magomeni na uongozi wake kwa kutukumbuka na kujengea vizimba hivi vya Majisafi, naamini vitaondoa kero ya Maji iliyokuwepo awali na niwaombe tu wananchi kushirikiana kwa pamoja katika kuvitunza na kuvilinda vizimba hivi ili kuepuka kurudi tena katika shida ya Maji tuliyokuwa nayo hapo awali” alisema Bw. Mzee.

Naye, mkazi wa mtaa huo wa Mvuleni Bi. Hawa Mohamed amesema kuwa vizimba hivyo vya Majisafi vimekuwa mkombozi mkubwa kwao kwani wanawake ndio ambao wamekuwa wakihangaika kutafuta Majisafi kwa muda mrefu, hivyo kusababisha kushindwa kufanya shughuli zingine za kimaendeleo. Aidha, ameiomba Dawasco kuongeza vizimba katika sehemu iliyobaki ya mtaa huo ili kuepuka msongamano kwenye vizimba hivyo.

“Vizimba hivi vya Majisafi kwa kweli vimetuokoa sisi wanawake wa mtaa wa Mvuleni maana tulikuwa tunapata shida mno kuyapata na tulikuwa tukiyanunua kwa bei ya juu sana, bei ambayo sisi watu wakawaida ilikuwa inatuwia vigumu kuimudu” alisema Bi. Hawa.

WAZIRI NDALICHAKO KUZINDUA MPANGO WA AFRIKACAN CAPACITY UNAOFADHILIWA NA BENKI YA ADB

$
0
0
Habari Picha na Imma Msumba.

Waziri wa Elimu na Sayansi Prof. Joyce Ndalichako mapema leo asubuhi amewasili katika Chuo cha Sayansi na Tekinolojia Nelson Mandela Arusha kwa ajili ya Uzinduzi wa mpango wa African Capacity unaofadhiliwa na Benki ya ADB.
 
Akizungumza na wanafunzi wa Chuoni hapo Profesa Ndalichako amesema Atawachukulia hatua kali waajiri katika sekta ya Elimu watakaowakataza baadhi  ya wafanyakazi waliopata ufadhili wa kwenda masomoni kujiendeleza .

Pia akiwa kwenye uzinduzi huo waziri alifanikiwa kutembelea maabara mbalimbali za idara tofauti za Chuo hicho zinazotumika na wanafunzi kwa ajili ya majaribio na pia alipata wasaaa wakutembelea shamba la migomba lililopo nje kidogo ya chuo hicho.
Waziri wa Elimu akisalimia na watumishi ya Chuo cha Nelson Mandela leo Asubuhi baada ya kuwasili chuoni hapao .Waziri wa Elimu profesa Joyce Ndalichako ( katikati ) Akimsikiliza Mkuu wa Maabara ya Taasisi ya Chuo Kikuu cha Nelson Mandela jijini Arusha .
Pichani ni wanafunzi wa PHD in material science and Energy lub,Agatha Wagotu na Joyce Elisadiki wakiwa ndani ya Maabara wakifanya majaribio.
 
 
  

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 31.03.2017


How Parents Talk About Social Media - Zulfiqar Manzi

KIWANDA CHA DAWA ZA BINADAMU KUJENGWA WILAYANI BAGAMOYO

mpango wa kuboresha makazi yaliyojengwa kiholela Kimara jijini Dar es salaam

$
0
0
Katika mpango wa kuboresha makazi yaliyojengwa kiholela, Kimara imekuwa mojawapo wa maeneo yanayoendelea na zoezi la Urasimishaji. Kwa sasa hatua iliyofikiwa ni ya uwekaji wa barabara za mitaa.

Halmashauri nyingine 6 zilizopangwa kutekeleza mradi huu ni; Manispaa za Musoma, Kigoma-Ujiji, Tabora, Singida, Sumbawanga na Lindi ambapo viwanja 3000 vitapimwa katika kila Halmashauri.

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya  Makazi inatekeleza mradi wa kurasimisha maeneo yaliyojengwa kiholela katika Jiji la Dar es Salaam katika kata ya Kimara kwa kushirikiana na Halmashauri ya Ubungo. Jumla ya viwanja 6,000 vinatarajiwa kupimwa na kumilikishwa. Katika mitaa ya Makongo juu, na Chasimba katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ambapo jumla ya viwanja 6585 vitapimwa.

Urasimishaji utaongeza huduma za jamii na miundombinu katika makazi na kuongeza usalama wa miliki kwa kutoa hati za kumiliki ardhi kwa muda mrefu. Mpango huu unatekelezwa kwa kushirikisha wananchi na viongozi wa maeneo husika.

Katika mpango huu, Wananchi wanawajibika kuonyesha mipaka ya miliki zao pamoja na kuchangia ardhi kwa ajili ya barabara. Aidha kila mwananchi anawajibika kutoa taarifa kwa usahihi ili kurahisisha umilikishaji. Urasimishaji unatekelezwa kulingana na sheria ya Ardhi Namba 4 ya Mwaka 1999 fungu la 56-60

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inawasihi Wananchi kushirikiana vyema katika zoezi hili kote nchini ili kuepuka  Makazi holela kwa Maendeleo ya Taifa.

Vile vile, Wizara itaendelea kushirikiana na Halmashauri nchini kuandaa mipango ya zoezi la Uramishaji. Baada ya Urasimishaji; miji inatarajiwa kuendelezwa kwa kulingana na mapendekezo ya mipango kabambe.

 Mjumbe katika kamati ya Mipango Miji – Chasimba; Bi Hawa Haruna Kimaro akitoa maelezo kwa Wananchi kuhusu zoezi la upimaji linavyoendelea  Chasimba.

 Zoezi la Urasimishaji linavyoendelea Kimara, ambapo zoezi hilo lipo kwenye hatua ya uwekwaji wa barabara za mitaa.

 Afisa Mipango Miji, akiwa katika zoezi la upimaji Chasimba.

 Dhana ya ushirikishwaji wa Wananchi inavyotekelezwa katika zoezi la Urasimishaji; Wananchi wakieleweshwa  na wapima  jinsi upimaji unavyofanyika katika eneo la Chasimba

Wananchi wakishuhudia uwekaji wa Barabara katika mitaa yao – Kimara.


Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini


Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi


UPDATES: RATIBA ZA MSIBA WA PROF. PHILIP HIZA

$
0
0
It is with great sadness, we announce the death of Prof. Philip Robert Hiza, of Makongo Juu, which occurred on Monday, March 27, 2017, at the Muhimbili National Hospital , Dar es Salaam. During this testing moment our heartfelt support and prayers go to the family. May the Lord rest the departed soul of our beloved Professor Philip Robert Hiza in Eternal Peace, Amen. 

THE LORD HAS GIVEN AND THE LORD HAS TAKEN; 
MAY HIS NAME BE BLESSED

For more information, please contact:
1) Caroline Hiza +1 (952) 215-6690 3) Roby Hiza +255 745555554
2) David Hiza +1 (952) 649-2474 4) Paul Meela +255 76790909

Please refer to the below times schedule of events:


RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AMPOKEA WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA ALIYEWASILI MCHANA HUU JIJINI DAR

$
0
0
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akimpokea mgeni wake ,Waziri Mkuu wa Ethiopia ,Hailemariam Dessalegn,aliyewasili hivi punde katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jijini Dar Es Salaam.
 Waziri Mkuu wa Ethiopia ,Hailemariam Dessalegn akipewa maua ikiwa ni ishara ya kumkaribisha kwa upendo nchini Tanzania,mara baada kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mapema leo mchana,na baadae kupokelewa na mwenyeji wake Rais Dkt John Pombe Magufuli,Waziri Mkuu Kassim Majliwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa. 
Waziri Mkuu wa Ethiopia ,Hailemariam Dessalegn akishuka kwenye ndege mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere mapema leo mchana,na baadae kupokelewa na mwenyeji wake Rais Dkt John Pombe Magufuli,Waziri Mkuu Kassim Majliwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa.

Imeelezwa kuwa ujio wa Waziri huyo Mkuu wa Ethiopia ni pamoja na kukuza mahusiano mazuri yaliyopo baina ya Tanzania na Ethiopia pamoja ‎na kujadili fursa zaidi za ushirikiano katika maeneo mbalimbali ikiwemo uwekezaji na biashara.

 Mhe. Dessalegn atakutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa mazungumzo na kushuhudia uwekwaji saini wa mikataba ya ushirikiano kwenye maeneo mbalimbali kabla ya kuzungumza na Waandishi wa Habari.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumpokea mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam.

BOKO BEACH VETERANS YAISAMBARATISHA GYMKANA VETERANS KWA BAO 3-1

$
0
0
 Timu ya Boko Beach Veterans (BBV) imefanikiwa kuwasambaratisha Veterans wa Gymkana kwa ushindi wa mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa jana jioni katika viwanja vya Gymkana, jijini Dar es salaam.

Wakicheza kwa kujiamini na uelewano mkubwa Maveterani kutoka Boko walionekana kuutawala sana mchezo huo na kuwapa tabu wapinzani wao Gymkana walioonekana kuicheza mechi hiyo kwa hofu. 

Boko waliianza karamu hiyo ya mabao mnamo Dakika Saba ya mchezo kufuatia krosi maridadi toka kwa nyota wake machachari Malekano (messi wa Boko) kutua kifuani kwa Charles Palapala na kuutupia nyavuni kwa ufundi mkubwa, Goli hilo lilidumu hadi mapumziko. 

Kipindi cha pili kilianza kwa Veterans wa Gymkhana waliokua wakiongozwa na Nahodha Ally Mayai Tembele, Juma Pinto, Mohd Sebene na kiungo asiekabika Makocha Tembele walilishambulia lango la Boko beach Veterans kama nyuki na hatimae wakasawazisha kupitia kwa Mshambuliaji wao Mohd Sebene baada ya beki wa boko Kitwana Mango kucheza rafu nje ya kumi na nane. 
Baada ya kusawazisha goli hilo, Timu ya Gymkana Veterans walionekana kuridhika kimchezo na hivyo kuwapa nafasi Boko Beach kutawala kiungo iliyokua ikiongozwa na Kudra Omary, Engenier Kamugisha, Elimboto Nkumbi na Hebron Malakasuka na hatimae kuongeza magoli mawili ya haraka haraka katika dakika ya 65 na 78 kwa magoli mazuri ya kiufundi yaliyowekwa kimiani na Elimboto Nkumbi, huku goli la lingine likifungwa na beki Mohamed Mwinchumu baada ya kazi nzuri iliyoanzishwa na kiungo Kudra Omari.

Huo unakuwa ni ushindi wa pili ndani ya siku saba baada ya mchezo wa kwanza kuirarua Timu ngumu ya veteran ya AZAM magoli matatu kwa mawili.

BBV watakua na kibarua kingine kigumu siku ya jumapili (Aprili 2) katika uwanja wake wa nyumbani watakapo ikaribisha Timu nyingine ngumu ya Dar City FC yenye nyota wa zamani kama George Masatu, Akida Makunda, Clement Kahabuka, Ally Mpemba, Zubeir Zatwila, Salvatory Edwards na Kiungo hatari Ernest Nyambo na Ally Kakima.

Balozi wa Italia Nchini Tanzania afanya ziara Kisiwani Mafia

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Mafia, Mbaraka Dau (kulia) akimuleza jambo, Balozi wa Italia nchini Tanzania, Roberto Mengoni wakati alipotembelea bandari ya Kilindoni, iliyopo katika Kisiwa cha Mafia Mkoani Pwani. Balozi Mengoni, amefanya ziara ya siku 2 katika kisiwa cha Mafia, ambapo aliweza kutembele bandari ya Kilindoni, soko la samaki, hospitali ya wilaya na shule ya Sekondari Kitomondo.
Balozi wa Italia nchini Tanzania, Roberto Mengoni (kulia) akizungumza jambo na Mbunge wa Jimbo la Mafia, Mbaraka Dau (kushoto), walipokuwa katika bandari ya Kilindoni, iliyopo katika Kisiwa cha Mafia Mkoani Pwani. 


Shirika la Meli la Ethiopia kuanza kutumia Bandari ya Dar es Salaam

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, TPA
Waziri Mkuu wa Shirikisho la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ethiopia, Mhe. Hailemariam Desalegn amesema Shirika la Meli la Ethiopia (Ethiopian Shipping Line) lipo tayari kuanza kuitumia Bandari ya Dar es Salaam kutokana na kutoa huduma nzuri.

“Shirika letu la Meli ambalo ni la kihistoria na lililobaki pekee katika ukanda wa Afrika likiwa linamilikiwa na Serikali ya Ethiopia sasa lipo tayari kufanya kazi na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania,” amebainisha Mhe. Desalegn.
Ameongeza kuwa mbali na shirika hilo la meli kuwa tayari kuanza kuleta meli zake Bandari ya Dar es Salaam pia Shirika Kongwe la Ndege la Ethiopia (Ethiopian Airline) lenye mafanikio makubwa nalo litaanza kusafirisha mizigo inayopitishwa katika Bandari ya Dar es Salaam.
Kwa upande mwingine Mhe. Desalegn amepongeza jitihada kubwa zinazofanywa na Menejimenti ya TPA katika kuboresha huduma zake ambapo amesema jitihada hizo sio tu zitanufaisha Serikali zote mbili bali pia ustawi wa maisha ya watu wa Tanzania na Ethiopia nao utaimarika.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Kassim amemshukuru Waziri Mkuu wa Ethiopia kwa kuja nchini ambapo amemuahidi kwamba mahusiano mazuri yaliyopo baina ya nchi hizi mbili yatadumishwa kwa maslahi mapana ya mataifa yote.

Awali akimkaribisha Waziri Mkuu wa Tanzania, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Makame Mbarawa amesema TPA itaendelea na mipango iliyopo ya kuhakikisha inaboresha Bandari zake ili ziweze kuhudumia vyema wateja wote kwa wakati.

“Tutaendelea kuboresha huduma zetu za Bandari na za sekta ya uchukuzi kwa ujumla ili tuweze kufikia malengo yenu na wateja wetu ya kuhakikisha kwamba tunawahudumia vizuri na kwa ufanisi,” amesema Mhe. Mbarawa.

Mapema akitoa taarifa ya utendaji wa Mamlaka, Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko alimweleza Waziri Mkuu wa Ethiopia kwamba kwa sasa TPA inaendelea na mpango wake wa kujenga uwezo wa kuhudumia wateja wake kwa kuzingatia kwamba sekta ya uchukuzi inakuwa kwa kasi.

“Kutokana na kasi kubwa ya ukuaji wa uchumi nchini na Duniani kwa ujumla, TPA inaimarisha uwezo wake wa kuhudumia mizigo na meli kubwa ili kujenga uwezo kabla ya mahitaji makubwa kujitokeza”, amesisitiza Mhandisi Kakoko.

 Waziri Mkuu wa Shirikisho la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ethiopia, Mhe. Hailemariam Desalegn (katikati) akifurahia zawadi ya picha ya Bandari ya Dar es Salaam mara baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPA, Pro f. Ignas Rubaratuka (kulia). Kushoto ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Kassim. 
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Kassim akisalimiana na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPA mara baada ya kuwasili bandari ya Dar es Salaam kumpokea mgeni wake Waziri Mkuu wa Shirikisho la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ethiopia, Mhe. Hailemariam Desalegn hivi karibuni.
Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko akisalimiana na Waziri Mkuu wa Shirikisho la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ethiopia, Mhe. Hailemariam Desalegn mara baada ya kuwasili bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni kwa ziara fupi.

Bamiza Music Chart 1st April 2017

VIKOSI VYA TIMU YA YANGA NA AZAM ZINAZOCHEZA LEO UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR

TIB corporate bank yachangia shilingi milioni 15.3 kwa mkoa wa katavi

$
0
0
 TIB corporate bank katika  kusukuma gurudumu la maendeleo ya nchi leo imechangia Shilingi milioni 15.3 kwa mkoa wa Katavi kusaidia mkoa huu mpya kukabiliana na changamoto mbali mbali ikiwamo miundo mbinu. Pichani wakikabidhi hundi hio kwa Mkuu wa mkoa Katavi Maj Gen Raphael Muhuga ni Mkurugenzi Mkuu wa TIB corporate bank Bw Frank Nyabundege na mkuu wa kitengo cha masoko na mahusiano Bi.Theresia Soka
Pichani ni  Mkuu wa mkoa Katavi Maj Gen Raphael Muhuga (kulia) Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. .Jenista Muhagama (wa pili kushoto), Waziri wa Kazi Na Uwezeshaji Wazee Zanzibar  Mhe. Maudline Castico  (wa tatu kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TIB corporate bank Bw Frank Nyabundege (kushoto)  na Mkuu wa kitengo cha masoko na mahusiano Bi.Theresia Soka (wa pili kulia)



Picha ya pamoja baada ya hafla hiyo fupi.

Injini za Discovery, Defender na Range Rover zinauzwa Dar es salaam

$
0
0
Tunauza injini za Land Rover Discovery, Defender na Range Rover. Pia tunaweza kukupatia Spea ya aina yoyote kutoka Europe kwa bei nafuu. 
Bei ya hiyo Land Rover Discovery  
Engine Td5 ni Tshs 4.7 Milion, 
Gear Box Tshs 2.7 Milion. 
Tunaleta kutoka U.K. 
Zipo Dar es Salaam tayari.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi
on whatswap +447723550406
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images