Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA NA SERIKALI YATEMBELEA WALENGWA WA TASAF KATIKA KIJIJI CHA MLANDA IRINGA VIJIJINI.

0
0
NA ESTOM SANGA-TASAF

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wametembelea kijiji cha Mlanda wilaya ya Iringa Vijijini mkoani Iringa kukagua shughuli zinazotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF- kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini-PSSN.

Wakiwa kijijini hapo wajumbe wa kamati hiyo wameonyesha kuridhishwa kwao na namna Mpango huo ulivyohamasisha wananchi kuboresha maisha yao ikiwemo ujenzi wa nyumba za mabati,kusomesha watoto,kuanzisha miradi midogo midogo ya kuichumi na kuboresha afya za familia za kaya hizo.

Akizungumza na walengwa wa Mpango huo na viongozi, Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Venance Mwamoto, ametaka serikali wilayani humo kuhakikisha kuwa wataalamu wa ugani wanawatembelea walengwa wa Mpango huo kuwapa ushauri wa namna bora ya kuendesha miradi wanayoianzisha.

‘’Tusiiachie TASAF kwani nyie ndiyo mko karibu na walengwa hao,ili waweze kufanikiwa zaidi wanahitaji hamasa na utaalamu wenu’’ alisisitiza Mhe. Mwamoto.
 Baadhi ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na  Serikali za Mitaa wakionyeshwa  mabati aliyoyanunua mmoja wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji cha Mlanda ,Iringa Vijijini ,Bi. Konjeta Lyambafu aliyevaa kitambaa kichwani. Kushoto kwake Mwenyekiti wa kamati hiyo Venance Mwamoto akimkabidhi fedha zilizochangwa na wajumbe kuongeza uwezo wa mlengwa huyo kukamilisha mabati ili aezeke nyumba yake iliyoko nyuma yao kwa bati.
 ‘’Ninaishukuru serikali kupitia TASAF kwa kuniwezesha kuboresha maisha kwa kujenga nyumba ya bati na kumudu kuwatunza na kuwasomesha wajukuu zangu wanane ’’ ndivyo mmoja wa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini Bi. Claudia Kanyita mkazi wa kijiji cha Mlanda, wilaya ya Iringa Vijijini anavyoelekea kuwaeleza wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki .

 Mmoja wa walengwa wa TASAF katika kijiji cha Mlanda wilaya ya Iringa Vijijini Claudia Kanyita akiwa na wajukuu zake watatu alioachiwa baada ya watoto wake kufariki, akitoa maelezo kwa kamati ya kudumu ya bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa iliyotembelea kijiji hicho kuona utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na TASAF. Nyumba inayoonekana nyuma yao imejengwa na Mlengwa huyo kwa ruzuku ya TASAF.Wa  kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Ladislaus Mwamanga.

 ‘’Mgeni njoo mwenyeji apone ’’ndivyo ilivyo kwa mlengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini wa  kijiji cha Mlanda wilaya ya Iringa vijijini  Konjeta Lyambafu aliyechangiwa fedha na wajumbe wa  kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa ili aweze kuongezea fedha anazozipata kupitia ruzuku inayotolewa na TASAF kuanzisha mradi wa kujiongezea kipata. Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Venance Mwamoto akimkabidhi fedha hizo mlengwa, kulia kwao ni Waziri Angellah Kairuki . Nyumba iliyoko nyuma yao imeezekwa na mlengwa huyo kwa bati alizozinunua kupitia ruzuku kutoka TASAF  na hivyo kuboresha makazi yake.


KIGOMA YANUFAIKA NA TAASISI YA MKAPA

0
0
Mkoa wa Kigoma umenufaika na nyumba mpya 30 za watumishi wa Afya pamoja na vitendea kazi (baiskeli 200, mabegi 225, mabuti 25 na makoti ya mvua 25) kwa ajili ya wahudumu wa Afya ngazi ya jamii vikiwa na ujumla wa thamani ya Shs 1,806,985,822 billioni kutoka kwa Taasisi ya Benjamin W. Mkapa. 

Akizungumza wakati wa ukabidhiwaji wa nyumba na vitendea kazi hivyo Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brigedia Jenerali (Mstaafu) Emmanuel Maganga, alisema ya kuwa mkoa wa Kigoma unakabiliwa na upungufu wa watumishi wa afya kwa asilimia 65 ya mahitaji kamili na moja wapo ya sababu zinazopelekea upungufu huo ni ukosefu wa mahali pazuri pa kuishi. 

Hivyo nyumba hizi zilizojengwa na Serikali kwa usimamizi wa Taasisi ya Mkapa zitasaidia kupunguza makali ya uhaba wa watumishi kwa mkoa wa Kigoma na nchi nzima kwa ujumla. 

Mkuu wa mkoa aliwasisitizia Wananchi pamoja na watumishi wa afya wanaotumia nyumba hizo kuzitunza na kuzithamini kwani zimejengwa kwa faida yao. Hivyo hivyo kwa upande wa vitendea kazi aliwasisi wahudumu wa afya ngazi ya jamii kuvitumia kwa lengo lililokusudiwa ambalo ni kuwafikia wana jamii ndani ya jamii zao na kuweza kuwapa huduma bora za afya. 

“Napenda kutoa wito kwa mashirika yanayojenga nyumba kama vile shirika la nyumba la Taifa, Mifuko ya hifadhi ya jamii, watumishi ujenzi n.k wafirikie zaidi kujenga kwenye vituo vyetu vya Afya na Zahanati ambapo Serikali inaweza kuwapangishiwa watumishi wake” alisisitiza, Mh. Maganga



Mfano wa moja kati ya nyumba mpya 30 zilizojengwa na kukabidhiwa kwa mkoa wa kigoma na Taasisi ya Mkapa.
Dkt. Ellen Mkondya-Senkoro, Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Mkapa akitoa ufafanuzi wa jiwe la ufunguzi kwa Mhe. Brigedia Jenerali (Mstaafu) Emmanuel Maganga, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma wakati wa halfa ya ukabidhishwaji wa nyumba mpya 30 za watumishi wa Afya iliyofanyika katika zahanati ya Kalinzi mkoani kigoma. 

Kikundi cha kina mama wa mkoa wa kigoma wakiimba kwa furaha mbele ya Mkuu wa Mkoa, Mhe. Brigedia Jenerali (Mstaafu) Emmanuel Maganga wakati wa hafla ya kukabidhiwa nyumba mpya 30 za watumishi wa afya zilizojengwa na Taasisi ya Mkapa mkoani Kigoma. 
Watu waliohudhiria hafla ya ukabidhiwaji wa vitendea kazi vitendea kazi (baiskeli 200, mabegi 225, mabuti 25 na makoti ya mvua 25) kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii 

SERIKALI KUTENGENEZA MWONGOZO WA KUWARUDISHA SHULE WALIOPATA MIMBA

0
0
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

Serikali imejipanga kutengeneza mwongozo wa kuwarudisha shuleni wanafunzi waliopata mimba wakiwa masomoni ili kuhakikisha wanapata elimu hadi kufikia ngazi za juu.

Hayo yamesemwa jana Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi Masuala Mtambuka kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Venance Manori alipokuwa akifungua warsha ya kuwawezesha Maafisa Waandamizi wa Serikali kutoka nchi sita za Afrika katika kutengeneza mipango inayozingatia jinsia katika elimu kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Prof. Joyce Ndalichako.

Manori amesema Serikali ya Tanzania inajitahidi kuzingatia jinsia katika utoaji wa elimu ambapo takwimu zinaonyesha kuwa elimu ya Msingi na Sekondari uwiano wake ni moja kwa moja japo kuwa idadi ya wasichana hupungua kutokana na changamoto mbalimbali zinazowakumba hivyo lengo la warsha hiyo ni kuwasaidia wadau kuweka mipango ya elimu inayozingatia usawa wa kijinsia.

“Serikali yetu imejipanga kuhakikisha wasichana wanapata elimu hadi ngazi za juu lakini mpango huo unakumbwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za mimba na ndoa za utotoni hivyo ili kuhakikisha mtoto wa kike anafikia ngazi za juu za elimu tuko kwenye mchakato wa kuandaa mwongozo kwa ajili ya wanafunzi waliopata mimba wakiwa bado wanasoma kupata nafasi ya kuendelea na masomo,”alisema Manori.
Mkurugenzi Msaidizi Masuala Mtambuka kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Venance Manori akiwa katika picha ya pamoja na waandaaji wa warsha ya kuwawezesha Maafisa Waandamizi wa Serikali kutoka nchi sita za Afrika katika kutengeneza mipango inayozingatia usawa wa kijinsia katika elimu kutoka shirika la Plan International- Tanzania, Global Partnership for Education (GPE), Dubai Cares pamoja na United Nations Girls’ Education Initiative (UNGEI) mara baada ya ufunguzi wa warsha hiyo uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Plan International- Tanzania, Jorgen Haldorsen akitoa neno fupi kwa ajili ya kuwakaribisha Maafisa Waandamizi wa Serikali kutoka nchi sita za Afrika katika ufunguzi wa warsha ya kuwawezesha kutengeneza mipango inayozingatia usawa wa kijinsia katika elimu. Ufunguzi wa warsha hiyo ulifanyika jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Serikali wanaohusika na elimu kutoka nchi sita za Afrika wakisikiliza hotuba ya Mkurugenzi Msaidizi Masuala Mtambuka kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (hayupo pichani), Venance Manori wakati wa ufunguzi wa warsha ya kuwawezesha maafisa hao katika kutengeneza mipango inayozingatia usawa wa kijinsia katika elimu.Warsha hiyo ya siku tatu imefunguliwa jana jijini Dar es Salaam.

DIWANI VINGUNGUTI AJUMUIKA KUSAMBAZA KIFUSI MTAA WA MTAKUJA

0
0
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti , Omary Kumbilamoto akishiriki kusambaza kifusi katika barabara ya Mtakuja mara baada ya eneo hilo kuwa korofi kutokana na kuwepo kwa mashimo mengi ambayo yamekuama yakituama maji muda wote pindi mvua zinaponyesha
 Baadhi ya Vijana na Wakazi wa Vingunguti wa mtaa wa mtakuja wakijitolea kuchimba mitaro na kusambaza kifusi katika barabara ya mtaa wa Mtakuja
 Omary Kumbilamoto akisambaza kifusi katika mtaa wa mtakuja  Vingunguti kuziba mashimo akiwa na watoto wadogo kwa lengo la kuwafundisha umuhimu wa  kuwa wazalendo kujitolea katika shughuri za wananchi pindi watakapokuwa wakubwa

MAAFISA MAENDELEO YA JAMII WA MIKOA WAJENGEWA WELEDI KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO NCHINI

0
0

Na erasto ching’oro- Msemaji: Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto leo imefungua kikao cha siku mbili cha Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Mikoa kwa ajili ya kuwajengea uwezo kuhusu utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kuzuia na Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (2017-2022).

Akifungua kikao hicho, Mwakilishi wa Katibu Mkuu Bw. Julius Mbilinyi ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia aliwashukuru Washirika wa Maendeleo katika kuhakikisha kuwa tatizo la ukatili dhidi ya wanawake na watoto linatokomezwa hapa nchini. Aliyataja mashirika haya kuwa ni pamoja na UN-WOMEN, Shirika la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Haki na Ustawi wa Watoto (UNICEF).

Mgeni Rasimi Kaimu Mkurugenzi wa Jinsia, aliwapongeza Maafisa Maendeleo ya Jamii kwa shughuli mbalimbali ambazo wamekuwa wakizitekeleza katika maeneo yao ya kazi, juhudi ambazo zimekuwa na mchango katika kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto nchini. Alifafanua kwamba, baada ya mafunzo haya, maafisa hao wataendelea kutekeleza majukumu yao kikamilifu ili kupunguza ukatili kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2021/20122.

Wanawake na watoto wamekuwa wakifanyiwa ukatili kwa kisingizio cha mila na desturi. Aidha, mfumo dume umesababisha wanawake kutoshiriki kikamilifu katika maamuzi yanayohusu maendeleo yao, katika ngazi ya kitaifa, katika ngazi ya jamii na hata katika familia zao. Mara nyingi tumesikia wanawake na watoto wakipigwa, kubakwa na wakati mwingine kuuwawa na watu wa karibu. Vitendo hivi ni ukatili wa hali ya juu na vinaleta simanzi na madhara makubwa katika jamii yetu.

Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia Julius Mbilinyi akifungua Kikao Kazi cha Maafisa wa Maendeleo ya Jamii wa Mikoa (hawapo pichani) katika cha siku mbili kinachoanza leo katika Hotel ya Edema Mkoani Morogoro.
Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia Julius Mbilinyi akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Mikoa wanaohudhuria kikao kazi kuhusu utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika mkutano unaofanyika Hotel ya Edema Mkoani Morogoro.
Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha Maafisa Maendelo ya Jamaii wa Mikoa wakifuatilia maelezo ya wawezeshaji kuhusu utekelezaji wa Mpango Kazi wa taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Hotel ya Edema, mkoani Morogoro.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA PROF PALAMAGAMBA KABUDI AWASILI OFISINI MJINI DODOMA

0
0
Waziri wa Katiba na Sheria Prof.Palamagamba Kabudi amewasili katika Ofisi za Makao makuu ya Wizara zilizoko ndani ya Chuo Kikuu cha Dodoma na kulakiwa na watumishi wa Wizara walioko makao makuu ya Serikali mjini Dodoma. 

Prof Kabudi aliapishwa tarehe 24/03/2017 Ikulu jijini Dar Es Salaam kuchukua nafasi hiyo baada ya Mhe.Rais kufanya mabadiliko madogo kwenye Baraza la Mawaaziri ambapo Dkt. Harrison Mwakyembe alihamishiwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. 

Nje ya Ofisi za Wizara Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi alilakiwa na Naibu Katibu Mkuu, Bw. Amon Mpanju, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bw. Aloyce Mwogofi, Jaji Mfawidhi Kanda ya Dodoma na wafanyakazi wengine wa Wizara waliopo Makao Makuu ya Serikali mjini Dodoma.

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi akipokea shada la maua kutoka kwa mtumishi Joyce Mtuma mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi akiangaalia kadi ya Pongezi iliyoasiniwa na watumishi wa wizara mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma
WaziriwaKatibanaSheriaMhe. Prof.Palamagamba Kabudi akisalimiana naNaibu Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma


Waziri wa Katiba na SheriaMhe. Prof.Palamagamba Kabudi akisalimiana na Jaji mfawidhi Kanda ya Dodoma Mhe. Mwanaisha Kwariko alipowasili Wizarani mjini Dodoma




Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi akisikiliza maelezo mbalimbali alipokutana na watendaji wa Wizara na Mahakama katika ukumbi wa mikutano Wizarani mjini Dodoma

Tanzania Day - Dallas, Texas

WACHIMBAJI WADOGO WAMUOMBA RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI KUACHIA MCHANGA ULIOKAMATWA BANDARINI

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Wachimbaji wadogo wa madini wamemuomba Rais Dk. John Pombe Magufuli kuwaachia mchanga wa madini uliozuiwa bandarini ,
kutokana na kuwepo kwa mchanga katika bandari kavu huku wakiendelea kutozwa ushuru wa kuhifadhi.

Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wamesema kuwa mchanga uliozuiwa na bandarini sio wa dhahabu ambao mashine za kuchanjulia ziko hapa nchini.

Mmoja wa wachimbaji hao , King Selemani amesema kuwa mchanga wanaosafirisha kwenda nje ni shaba, Nickel ,Manganise ore ,Zinc ore, Galena pamoja na lead ore ambapo hapa nchini hakuna mtambo wa kuchenjua mchanga huo.

Selemani amesema kuzuiwa kwa mchanga huo kumewaathiri pamoja na kusitisha ajira kwa baadhi ya wafanyakazi katika machimbo ya madini hayo.

Aidha amesema kuwa Rais Dk. John Pombe Magufuli amekuwa mstari mbele hivyo wamemuomba kuwachia kuendelea na biashara hiyo.
Mchimbaji Mdogo wa Madini, King Selemani akizungumza leo na waandishi wa habari juu ya kumuomba Rais Dk.John Pombe Magufuli kutoa ruhusa ya kuwaachia mchanga wa madini uliozuiwa katika bandari ya Dar es Salaam.
Mchimbaji Mdogo na msafirishaji wa Madini , Paul Kalyembe akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuwaruhusu kufanya biashara hiyo huku serikali ikisubiri kufanya taratibu zungine za kuwa na kiwanda cha kufanya kazi ya kuchenjua madini katika mchanga wa Nickel, Shaba na madini megine leo jijni Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Glob ya jamii.
Sehemu ya waandishi habari wakiwasikiliza wachimbaji wadogo wa madini leo jijini Dar es Salaam . 

Kampuni za ujenzi kutoka China zaaswa kushirikana

0
0
KAMPUNI za ujenzi nchini zimeshauriwa kuungana na kushirikiana na kampuni za ujenzi kutoka China ili kujifunza namna wanavyofanya kazi kwa ufanisi.

Akizungumza ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Asasi ya Ushirikiano kati ya Tanzania na China, Bwana Joseph Kahama alibainisha kuwa kampuni za ujenzi nchini bado zina safari ndefu ya kuongeza ujuzi na mbinu za kibiashara.

“Wachina ndio wanaoongoza katika ujenzi duniani, mataifa mengi yaliyoendelea majengo yao yanasimamiwa na kampuni za kichina, hivyo hakuna namna kwa kampuni za Kitanzania kushindana nazo wakitaka kufanikiwa wajipenyeze na kuomba ushirikiano hapo watajifunza mengi.

“Kujifunza kuna njia nyingi, ni utaratibu mzuri katika biashara kujipanga,” alisisitiza Bw. Kahama na kuongeza: “zaidi ya asilimia 80 ya kampuni kubwa za ujenzi duniani zinatoka China, na hapa nchini zipo nyingi kwa sasa huu ndio wakati wetu wa kuchota ujuzi.”

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC East Africa Limited), Bwana Yigao Jiang alisema kampuni yake imekuwepo nchini tangu miaka ya 1960 na wapo tayari kuwasaidia Watanzania katika nyanja zote ikiwemo masuala ya kijamii.
Mkuu wa wilaya ya Chato, Bw Elias Makory akimkabidhi cheti Mkurugenzi wa Operesheni wa kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) Bw.An Yi kwa kutambua mchango wa kampuni hiyo kwa jamii mara baada ya kupokea madawati 50 kwa matumizi ya wanafunzi 150. Kampuni hiyo imeshatoa jumla ya madawati 150 yenye thamani ya milioni 30 na itaendelea kuchangia huduma mbalimbali za kijamiii.
Mkuu wa wilaya ya Chato, Bw Elias Makory (wapili kushoto) akipokea rasmi madawati 50 toka kwa Mkurugenzi wa Operesheni wa kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) Bw.An Yi (watatu kushoto). Kampuni hiyo imeshatoa jumla ya madawati 150 yenye thamani ya milioni 30 na itaendelea kuchangia huduma mbalimbali za kijamiii.


makamishna wapya wa uhamiaji waapishwa leo mjini dodoma

0
0
 Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr. Anna Peter Makakala ,akimvisha cheo kipya Kamishna wa Uhamiaji Utawala na Fedha,  Edward Peter Chogero  katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma. Anayeshuhudia ni Naibu Kamishna wa Uhamiaji Chrispin Ngonyani. Tukio hili linehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira  na Naibu  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi  Hassan Simba Yahaya.

 Kamishna mpya wa Uhamiaji Divisheni ya Sheria Hannerole Morgan Manyanga akila kiapo cha Utii mbele ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr.  Anna Peter Makakala katika hafla iliyofanyika  leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma. Hafla hiyo imehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara  ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira   na Naibu  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Hassan Simba Yahaya.

 Kamishna wa Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma , Jaji Mstaafu Harold Nsekela wa kwanza kushoto akiwaongoza  Makamishna wapya wa Uhamiaji kuapa  kiapo cha Maadili ya Viongozi wa  Utumishi wa Umma baada ya Makamishna hao wapya kuvalishwa vyeo vipyakatika hafla iliyofanyika  leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma. 

 Makamishna wapya wa Uhamiaji wakisaini Fomu za Maadili ya Viongozi wa Umma baada ya Makamishna hao kula kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Utumishi wa Umma,katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara  ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira   akizungumza jambo na Makamishna wapya wa Uhamiaji baada ya kumalizika shughuli ya kuapishwa Makamishna hao  leo katika viwanja vya Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.   

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi awasili ofisini kwake dodoma

0
0
 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi akipokea shada la maua kutoka kwa mtumishi Joyce Mtuma mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma.  
 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma
 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi akiangalia kadi ya Pongezi iliyoasiniwa na watumishi wa wizara mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma
 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi akisalimiana na Jaji mfawidhi Kanda ya Dodoma Mhe. Mwanaisha Kwariko alipowasili Wizarani mjini Dodoma. Picha zaidi BOFYA HAPA

TAIFA STARS YAITANDIKA BURUNDI BAO 2-1 TAIFA LEO

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars' imefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya timu ya Taifa ya Burundi kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika leo Jijini Dar es salaam.
Katika mchezo huo uliofanyika kwenye dimba la Uwanja wa Taifa, timu ya Taifa Stars ndiyo ilikuwa ya Kwanza kuanza kufunga baada ya winga Simon Msuva kuipatia timu yake goli la kwanza katika dakika ya 20 akimaliza pasi safi ya Mohamed Hussein 'Tshabalala'.

Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza Taifa Stars walienda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1 - 0 dhidi ya Burundi.

Kipindi cha Pili kilianza kwa kila timu kulisakama lango la mwenzake na katika dakika ya 54, mshambuliaji wa Burundi Laudit Mavugo alitumia makosa ya beki kati Abdi Banda aliyepoteza mpira na kuifungia timu yake goli la kusawazisha.

Kocha Salum Mayanga anaamua kufanya mabadiliko mbalimbali kwa ikiwemo kumtoa Farid Musa na kuingia Mbaraka Yusuph ambaye aliweza kubadili matokeo na katika dakika ya 76 aliifungia Taifa Stars goli pili na la ushindi.

Mpaka dakika 90 zinamalizika Taifa Stars wanatoka kifua mbele kw goli 2-1 dhidi ya Burundi na inakuwa ni mchezo wa pili mfululizo kwa Taifa Stars kushinda baada ya mwishoni mwa wiki hii kuifunga Botswana kwa goli 2-0.






HUDUMA ZITOLEWAZO NA MAABARA ZA WAKALA WA JIOLOJIA TANZANIA (GST)

MAHAKAMA YASHAURIWA KUWAJENGEA UWEZO WATUMISHI WAKE WA NGAZI ZOTE

0
0

 Na Lydia Churi
Mahakama, Tanga


Mahakama ya Tanzania imeshauriwa kuwa na Mpango endelevu wa kuwajengea uwezo watumishi wake wa ngazi zote ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Tanga Mhe. Imani Abood (pichani) alitoa ushauri huo leo jjini Tanga alipokuwa akielezea utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Miaka Mitano wa Mahakama ya Tanzania katika Kanda yake.

Alisema pamoja na kuwa Mahakama inaendesha mafunzo mbalimbali kwa watumishi wake lakini mafunzo hayo hayana budi kutolewa kwa watumishi wote kuanzia ngazi ya chini mpaka ngazi ya juu kabisa katika Mahakama.

Akizungumzia nguzo ya pili ya Mpango Mkakati wa Mahakama inayohusu upatikanaji wa haki kwa wakati, Mhe. Abood alisema ni muhimu suala la mafunzo likapewa kipaumbele hasa kutokana na kukua kwa sayansi na Teknolojia.

Alisema , hivi sasa katika Mahakama  upo ushahidi wa kielekitroniki unaotolewa hivyo ni muhimu mafunzo yakatolewa ili kuleta ufanisi katika suala zima la utoaji wa haki.

Akizungumzia mikakati iliyowekwa na kanda yake ili kuondosha mashauri mahakamani kwa wakati, Jaji Abood alisema wanakusudia kuziwekea umeme Mahakama za Mwanzo kupitia Mradi wa REA na kuwapatia Mahakimu wote katika kanda yake vitendea kazi kama vile laptops na printer ili ziwarahisishie kutoa hukumu kwa wakati.

Alisema hivi sasa Mahakimu katika Mahakama za Mwanzo hulazimika kupeleka hukumu walizoandika kwa mkono ili zikachapishwe kwenye Mahakama za wilaya ambapo kuna umeme.


Alisema licha ya changamoto hizo, bado watumishi wa Mahakama Kuu kanda ya Tanga wanakuwa wakifanya kazi kwa bidii na Mahakimu kuhakikisha hukumu zinatolewa kwa wakati ikiwa ni pamoja na na wananchi kupatiwa nakala za hukumu ndani ya siku 21 zilizopangwa.

Mkakati mwingine uliowekwa ili kuondosha mashauri mahakamani ni pamoja na, kufanya vikao na Mahakimu wafawidhi wa wilaya pamoja na wadau wa Mahakama ili kurahisisha kazi kwa kuwa kila mdau anaposhughulikia eneo lake shauri huisha mapema.


MHE. NAPE MOSES NNAUYE AKABIDHI RASMI OFISI KWA WAZIRI MWAKYEMBE

0
0

 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Nape Moses Nnauye wakitia saini hati za makabidhiano rasmi ya Ofisi yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara Mjini Dodoma akishuhudia makabidhiano hayo ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof Elisante Ole Gabriel.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Nape Moses Nnauye wakibadilishana  hati za makabidhiano rasmi ya Ofisi yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara Mjini Dodoma.



RAIS WA ZANZIBAR AONGEA NA WALIMU WAKUU WA SKULI ZA SEKONDARI UNGUJA LEO

0
0
 Baadhi ya Walimu wa wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa Mkutano na Walimu wa Skuli za Sekondari za Mikoa mitatu ya Unguja,uliofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja Mjini Unguja
 Baadhi ya Walimu wa wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa Mkutano na Walimu wa Skuli za Sekondari za Mikoa mitatu ya Unguja,uliofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja Mjini Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa Mkutano na Walimu wa Skuli za Sekondari za Mikoa mitatu ya Unguja,uliofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja Mjini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa Mkutano na Walimu wa Skuli za Sekondari za Mikoa mitatu ya Unguja,uliofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja Mjini Unguja. 
Picha na Ikulu. Picha zaidi BOFYA HAPA

uzinduzi wa Kitaifa wa Tovuti za Mikoa na Halmashauri

0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( OR-TAMISEMI) , Mhe. George Simbachawene akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Tovuti za Mikoa na Halmashauri uliofanyika katika  Ukumbi wa HazinaMjini Dodoma 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR-TAMISEMI) , Mhe. George Simbachawene akizindua tovuti za Mikoa na Halmashauri uliofanyika jana katika ukumbi wa Hazina Ndogo  mjini Dodoma. Kulia kwake ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison Mwakyembe. (Kushoto)  ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa, Mhe. Said Meck Sadick wakifuatilia uzinduzi huo.

 Msanii Mrisho Mpoto akitoa burudani wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Tovuti za Mikoa na Halmashauri uliofanyika jana katika Ukumbi wa Hazina mjini Dodoma.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) , Mhe. George Simbachawene,  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison Mwakyembe pamoja na viongozi mbalimbali katika Mikoa na Halmashauri wakifuatilia uzinduzi wa Kitaifa wa Tovuti za Mikoa na Halmashauri uliofanyika  jana Mjini Dodoma katika Ukumbi wa Hazina. Tovuti hizo zinalenga katika kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi na kwa haraka ikiwa ni pamoja na kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa haraka.

 Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa, Mhe. Said Meck Sadick akiongea katika uzinduzi huo.

DIRA YA DUNIA YA BBC SWAHILI MACHI 28, 2017

Neema Wambura Amshukuru Rais Magufuli, Awapongeza Madaktari na Wauguzi

0
0
Na John Stephen, MNH
Mgonjwa Neema Wambura ambaye alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) amemshukuru Rais John Pombe Magufuli baada ya afya yake kuimarika na kuruhusiwa leo kurejea nyumbani.
Neema amemshukuru rais kwa kumwezesha kupata matibabu tangu alipofikishwa katika hospitali hiyo Februari 23, mwaka huu.
“Namuomba Mwenyezi Mungu amuepushe Rais Magufuli na mambo mabaya yote. Sasa nipata nguvu, nina furaha na naoga mwenyewe tofauti na awali,” amesema Neema.
Pia, Neema amewashukuru madaktari na wauguzi wa Muhimbili kwa kumpatia huduma bora na kumwezesha kupona majeraha ya moto.
Neema ambaye ni Mkazi wa Mkoa wa Mara alimwagiwa maji ya moto na mumewe wakati alipokuwa akichemsha maji kwa ajili ya kupika ugali na kuungua sehemu ya kifuani, shingo na mkono.
Mkuu wa Idara ya Upasuaji na Daktari Bingwa wa Upasuaji, Dk Ibrahim Mkoma  amesema afya ya Neema inaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji sehemu ya shingoni ili kutenganisha shingo na sehemu ya kifua na kuziba majera ya moto.
“Neema anaendelea vizuri sasa anaweza kunyanyua shingo vizuri kabla ya hapo alikuwa hawezi kuinyanyua wala kuizungusha,” amesema.
Daktari bingwa wa Upasuaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dkt. Ibrahim Mkoma akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu kuruhusiwa kwa mgonjwa aliyekuwa anapatiwa matibabu kutokana na majeraha ya kuunguzwa na maji ya moto kifuani, shingoni na mkononi, Bibi. Neema Mwita maarufu kama mgonjwa wa Magufuli. Neema alikuwa akipatiwa matibabu katika hospitali hiyo kufuatia msaada wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kuguswa na taarifa za mgonjwa huyo mapema mwezi wa pili mwaka huu hali iliyompelekea kuchukua jukumu la kumsaidia.Mkuu wa Jengo la Sewahaji Bibi. Salome Mayenga (kushoto) na Mkuu wa Wodi namba 24 Sewahaji, Muhimbili Bibi. Georgina Kabaitileki.
 Dkt. Mkoma akionyesha  baadhi ya sehemu ambazo Neema amefanyiwa upasuaji  baada ya kupata majeraha makubwa baada ya kumwagiwa maji ya moto na mume wake huko mkoani Mara.
Neema Mwita akimshukuru Rais Dkt.  John Magufuli pamoja na wa watoa huduma wa  Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya afya yake kuimarika na leo ameruhusiwa kurudi nyumbani.

MWENDO KASI LAPARAMIA TAA ZA BARABARANI LEO

0
0
 Basi la mwendo kasi asubuhi ya leo, limeacha njia na kugonga taa za magari barabarani katika eneo la Fire, Kariakoo. chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika.

Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images