Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 161 | 162 | (Page 163) | 164 | 165 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Bw. Nyirembe Munasa, akisisitiza jambo katika ufunguzi wa Mafunzo ya usimamizi wa Sheria ya Mazingira na Udhibiti wa biashara haramu ya bidhaa zinazoharibu tabaka la Ozoni. Mafunzo haya ya siku mbili yanayafanyika katika Chuo cha Utalii Arusha na yanahusisha washiriki kutoka mikoa ya Arusha, Tanga na Kilimanjaro. Wa kwanza kulia na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Rogathe Kisanga na Bw. Japhet Kanizius Afisa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais.
  Sehemu ya washiriki wa Mafunzo hayo kutoka Sekta za mbalimbali wakiwemo Maafisa Forodha, Maafisa Biashara, Polisi, Mahakama, Waendesha Mashtaka, Uhamiaji, Wataalamu wa Mazingira na Vyombo vya Habari wakifuatilia hotuba ya ufunguzi katika kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Bw. Nyirembe Munasa.
  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Bw. Nyirembe Munasa (Kulia) akiongea na mmoja wa washiriki wa mafunzo ya usimamizi wa Sheria ya Mazingira na Udhibiti wa biashara haramu ya bidhaa zinazoharibu tabaka la Ozoni. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Bi. Rogathe Kisanga. (Picha Na Lulu Mussa).

  0 0

  Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi

  ZANZIBAR ALHAMISI JUNI 13, 2013. Jeshi la Polisi Zanzibar Jumamosi Juni 15, 2013 litafanya matembezi (Route March) ya pamoja kati yake na Askari wa Vikosi vya SMZ.

  Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, ameyataja makundi mengine yatakayoshiriki kwenye matembezi hayo kuwa ni pamoja na , Vikundi vya Mazoezi ya Viungo pamoja na Vikundi vya Ulinzi Shirikishi.

  Amesema matembezi hayo ambayo yataanza saa 12.00 alfajiri siku hiyo, yataanzia kwenye Viwanja ya Polisi Ziwani na kuishia nje ya Uwanja wa Michezo wa Amani saa 3.00 asubuhi.

  Kamishna Mussa amesema matembezi hayo yenye sura ya amani yatapokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Maghari Unguja Bw. Abdallah Mwinyi Khamisi na washiriki wake watatoka katika mikoa mitatu ya Unguja.

  Katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari, Kamishna Mussa amewaomba wananchi wa mji wa Zanzibar na Viunga vyake wameombwa kufika nje ya Uwanja wa Amani kuanzia saa 2.00 asubuhi ili kupata ujumbe utakaotolewa siku hiyo.

  Viongozi mbalimbali kutoka Vyombo vya Ulinzi na Usalama Zanzibar watahudhuria katika mapokezi hayo.

  Aidha Waandishi kutoka vyombo mbalimbali wa Habari, wameombwa kuhudhuria ili kusaidia kutoa elimu kwa umma juu ya yale yote yatakayoelekezwa kwa manufaa ya Taifa letu.

  IMETOLEWA NA INSP. MOHAMMED MHINA, AFISA HABARI MKUU WA JESHI LA POLISI ZANZIBAR.

  0 0
 • 06/13/13--06:51: Mapitio ya Magazeti leo

 • 0 0
 • 06/13/13--07:27: KUTOKA BUNGENI DODOMA LEO
 • Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Seriklai za Mitaa, Hawa Ghasia kwenye ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma Juni 13, 2013.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani Emmanuel Nchimbi kwenye viwanja vya Bunge Mjini dodoma Juni 13, 2013.
  Wabunge Batrice Shelukindo wa Kilindi (kushoto) ana Aza Hilal wa Viti Maalum wakitoka kwenye ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma Juni 13, 2013.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizunguma na Wabunge Lolesia Bukwimba wa Busanda (katikati) na Felisita Bura wa Viti Maalum kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni13, 2013. (Picha na Ofisi yaWairi Mkuu).

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Dr.Ad Koekkoek,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar,kumuaga Rais leo asubuhi baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Dr.Ad Koekkoek,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar,leo asubuhi kuaga Rais baada ya kumaliza muda wake wa kazi .[Picha na Ramadhan Othman, Ikulu.]

  0 0

  TAARIFA ILIYOTUFUKIA CHUMBA CHA HABARI CHA GLOBU YA JAMII,INAELEZA KUWA MSANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYADA LANGA KILEO A.K.A LANGA AMEFARIKI DUNIA MUDA MFUPI ULIOPITA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI ALIKOKUWA AMELAZWA.

  LANGA AMBAYE INADAIWA KUWA ALIPATWA NA MALARIA KALI SANA HALI ILIYOPELEKEA KUKIMBIZWA HOSPITALI SIKU YA JANA.

  TAARIFA KAMILI ITAKUJA BAADAE.

  0 0

   Muandaaji wa Tamasha la Michezo lijulikanalo kwa jina la Castle Lager Soka Fest 2013,Evans akizungumza na waandishi wa juu Tamasha hilo litakalofanyika siku ya jumamosi katika Viwanja vya Posta,Kijitonyama jijini Dar es Salaam
   Nyanda wa zamani wa timu ya Yanga na Taifa Stars,Perer Manyika akizungumzia uwepo wake kwenye Tamasha hilo la Michezo litakalofanyika siku ya jumamosi katika Viwanja vya Posta,Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
  kwa upande wa Wadhamini wakuu wa Tamasha hilo,Peter Zacharia alisema Castle Lager imeamua kudhamini hilo ikiwa na lengo la kuwakutanisha wafanyakazi wa makampuni mbali mbali ili waweze kukutana na kufurahi pamoja.Tamasha hilo litafanyika siku ya jumamosi katika Viwanja vya Posta,Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

  0 0

  1. INTRODUCTION
  1. Madam Speaker, I beg to move that this esteemed House now resolves to debate and approve Government proposals for Revenue and Expenditure estimates for Fiscal Year 2013/14. Together with this speech, there are four volumes of books which provide detailed explanation of the budget estimates: volume one presents revenue estimates; volume two describes recurrent expenditure estimates for Ministries  and Independent Government Departments, Institutions and Agencies while volume three provides for recurrent expenditure estimates for Regions and Local Government Authorities; and volume four presents development expenditure estimates for Ministries, Independent Government Departments, Institutions and Agencies, Regions and Local Government Authorities.  There is also the Finance Bill of the year 2013 which is part of this budget.

  0 0

  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ujumbe maalumu toka kwa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt Donald Kaberuka ulioletwa kwake na mwakilishi mkazi wa Benki hiyo nchini Mhe Tonia Kandiero leo Juni 13, 2013 katika Ikulu Ndogo Dodoma.
  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na mwakilishi mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) hiyo nchini Mhe Tonia Kandiero leo Juni 13, 2013 katika Ikulu Ndogo Dodoma baada ya kupkkea ujumbe maalumu toka kwa Rais wa Benki ya hiyo Dkt Donald Kaberuka. PICHA NA IKULU

  0 0


  0 0


  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NBC na pia Mkuu wa Hazina wa Benki hiyo, Pius Tibazarwa (wa pili kushoto), Mkuu wa Kitengo Huduma za Kibenki kwa kufuata sheria za Kiislamu (NBC Islamic Banking), Yassir Masoud (kulia), Mkuu wa Huduma za Rejareja, Mmoloki Legodu (wa pili kulia) na Naibu Mufti, Ali Muhidini Mkoyogore wakizindua promosheni ya pili ya Hija ya benki ya NBC jijini Dar es Salaam leo.
  Mkuu wa Kitengo Huduma za Kibenki kwa kufuata kanuni za Kiislamu (NBC Islamic Banking), Yassir Masoud (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi wa promosheni ya pili ya Hija kwa wateja wake jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NBC na pia Mkuu wa Hazina wa Benki hiyo, Pius Tibazarwa na Mkuu wa Huduma za Rejareja, Mmoloki Legodu.
  Mmoja wa washindi wa awamu ya kwanza ya promosheni ya Hija ya NBC, Hamisi Hamza Mwanga (kushoto) akizungumza kuhusu safari yao ya kwenda hija mjini Makkah ambayo yeye na mama yake walikwenda kwa gharama za NBC.

  0 0


  0 0


  Aliyekuwa kocha Simba Patrick Liewig (pichani) amerejea nchini na kuitaka klabu hiyo imlipe malimbikizo ya mshahara wake kisha iachane naye kwa amani.

  Simba iliachana na  Liewig baada ya kutoridhishwa na matokeo ya mechi za msimu uliopita na kuishia kukamata nafasi  tatu.

  Akizungumza na Ripota wetu mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam jana alfajiri,Liewig alisema,hawezi kulazimisha Simba imwongezee mkataba  isipokuwa anachohitaji ni malipo ya malimbikizo ya mishahara yake.

  "Nimekuja hapa kwaajili ya kutaka kujua kinachoendelea, sababu nimesikia tu  juu juu kuwa sitakiwi kwenye timu na sijaambiwa rasmi.

  "Pamoja na hayo mimi sina tatizo,kama wameamua hivyo kuachana na mimi sawa isipokuwa wanilipe fedha zangu ninazodai kwani ni haki yangu na ndio maana nimekuja Tanzania"alisema Liewig

  Aliongeza" Mkataba wangu umeisha Juni lakini kuna fedha zangu bado nawadai hivyo siwezi kuziacha hivi hivi, lazima wanilipe ndipo tumalizane kwa amani".

  Kocha huyo aliichukua Simba mikononi mwa kocha aliyetimuliwa Milovan Cirkovic na alianza kuinoa timu hiyo kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

  Kocha huyo alisifika kwa ukali wake kwa wachezaji na hivyo kuamua kufanya uamuzi mgumu wa kuwasimamisha baadhi ya wachezaji nyota wa timu hiyo kwa madai ya utovu wa nidhamu na kuwatumia vijana katika michezo  10.

  Hata hivyo habari za ndani zinadai kuwa kocha huyo anaidai klabu hiyo malimbikizi ya mshahara wa miezi mitatu unaofikia kiasi cha dola 36,000.
  Kaimu Makamu mwenyekiti wa Simba Joseph Itangare alisema hawana taarifa ya ujio wa kocha huyo lakini wanasubiri kama atawasiliana nao basi watamsikiliza.

  "Sisi hatujui kama amefika hapa nchini lakini tunangoja kama atawasiliana na sisi tutafanya mazungumzo naye" alisema.

  0 0
 • 06/13/13--10:10: Lost Passport

 • Passport No. AB 017956 for SILAS JOHN BURA (pictured above) Has got lost in Melbourne, Australia.

  Whoever has any information leading to the recovery of this passport may please report immediately to the nearest police station in Tanzania or Australia.

  Please Contact +61411 223295 or +255 784 608301

  0 0  BARAZA la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), imeziteuwa timu ya Mamlaka ya Mapato Uganda (URA), Elect Sports ya Chad na Rayon Sports ya Rwanda kuziba nafasi ya timu za Tanzania zilizojitoa kwenye mashindano hayo yatakayoanza kutimua vumbi Juni 18 hadi Julai 2  Durfur nchini Sudan.
  Mbali na timu hizo kuziba nafasi za timu za Tanzania pia baraza hilo linalazimika kupangua upya ratiba ya mashindano hayo na kupanga upya kesho kutwa Jumapili.
  Katibu Mkuu wa Cecafa Nicholaus Musonye alisema wana timu nyingi hawawezi kubabaishwa na timu za Tanzania ambazo zimeshawishika na siasa na kuamua kujitoa katika mashindano hayo na kwamba maandalizi yote yamekamilika na mashindano yatafanyika kama yalivyopangwa.
  "Tumeziteua timu hizo kwa vile tumejitaidi kuzishawishi timu tatu za Tanzania kushiriki michuano hii lakini zimegoma kwa kisingizio cha usalama licha ya kuwambia Sudani ni salama lakini hazijataka kutuamini.
  "Mabadiliko ya ratiba yatafanyika wikiendi hii tutakapokutana mjini Khartoum na wajumbe wa Cecafa na waandaaji ambao ni viongozi wa Shirikisho la Soka la Sudan. 
  "Mashindano ni mazuri kwa ukanda wetu lakini siasa naona zimeingia kwenye soka na timu kujitoa bila ya sababu, hata hivyo mashindano yatafanyika kama kawaida, na maandalizi yanaendelea vizuri na serikali ya Sudan imeendelea kutusisitizia kutupa ulinzi wa  hali ya juu.
  Musonye alidai kuwa kitendo hicho ni sawa na hujuma  huku akidai kuwa timu kubwa za El Merriekh na El Hilal zilijitoa kabla ya ratiba ya makundi kupangwa.Timu hizo zilijitoa kwa kuhofia hali ya usalama nchini Darfur na pia zikawa tayari kushiriki michuano hiyo kama ingefanyika Khartuom.
  Hata hivyo Musonye alidai kuzichukulia hatua kali za kinidhamu timu zilizojitoa dakika za mwisho kwenye michuano hiyo wakati ratiba tayari imeshapangwa.
  Timu zilizojitoa ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo Yanga, Simba, Super Falcon ya Zanzibar na Tusker ya Kenya kutokana na hali duni ya usalama wa Darfur.
  Timu hizo za Tanzania zimejitoa baada ya serikali kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Nje Benard Membe wakati akihitimisha hotuba ya bajeti ya wizara yake hivi karibun, alisema  anashangaa kuona Sudan ikipewa uenyeji wa michuano hiyo licha ya kuwa na usalama mdogo na kuhoji busara iliyotumika kupeleka michuano hiyo huko.
  Kauli hiyo ya Membe iliungwa mkono na msuluhishi wa mgogoro wa jimbo la Darfur nchini Sudan, Dk Salim Ahmed Salim ambaye alisema Sudan hamna usalama wa kuaminika licha ya vikundi kutokuwa na uadui na wachezaji na kutaadharisha kuwa vikundi hivyo vinaweza kufanya mashambulio kwa lengo la kufikisha ujumbe kama bado wapo na wanasilaha na kudai hakuna mantiki ya timu za Tanzania kushiriki michuano hiyo.
  Hata hivyo jitihada za Mwenyekiti wa Cecafa Leodegar Tenga kutaka huruma ya serikali kuziruhusu timu za Tanzania kushiriki michuano hiyo ziligonga mwamba baaada ya juzi Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Amos Makalla kudai serikali haiwezi kuziruhusu timu za Simba, Yanga na Falcon kushiriki michuano hiyo kwa vile wana taarifa za  kutosha kuwa Sudan Kusini hakuna usalama na nchi nyingine zimeendelea kujitoa, hivyo msimamo wao  kama serikali, hawawezi  kupeleka timu sehemu isiyo na usalama
  Timu zitakazoshiriki michuano hiyo sasa ni Al Ahly Shandi (Sudan), Al Nasir (South Sudan), Al-Hilal Kadugli (Sudan), Express FC (Uganda), URA FC (Uganda), Ports FC (Djibouti), Vital’O  (Burundi), Merriekh El Fasher (Sudan), APR (Rwanda), Elman (Somalia), Rayon Sport  (Rwanda) Elect Sport (Chad) na Gor Mahia (Kenya).

  0 0

  Hakika, MBUZI MMOJA TU anaweza Kufanya Mabadiliko!
  Mbio za Hisani za Mbuzi za Dar 2013 zimeweka rekodi kwa kufanikiwa kukusanya Shilingi milioni 130 zitakazosaidia mashirika mbalimbali ya hisani ya ndani ya nchi, imeelezwa na waandaaji leo. 
   Kwa maana hiyo basi, hadi sasa mbio hizo zilizoanza tangu mwaka 2001, zimekwishakusanya zaidi ya Shilingi milioni 790 kwa ajili ya mashiriki zaidi ya 60 ya hisani. Takribani watu 4,700 waliingia getini ili kushuhudia mashindano ya 13 ya Mbio za Mbuzi za Hisani katika Viwanja vya The Green, Kenyatta Drive jijini Dar es Salaam siku ya Juni 1 mwaka huu. 
  Mwenyekiti wa Kamati ya Mbio za Mbuzi, Karen Stanley alisema: “Tuna furaha kubwa sana kutangaza kuwa kwa mara nyingine mwaka huu pia tumefanikiwa kukusanya fedha nyingi kuliko hata mwaka jana baada ya kupata Shilingi milioni 130 kwa ajili ya mashirika yaliyochaguliwa. “Shukrani ziwaendee watu 4,700 waliofika kushuhudia tukio hilo kwa mwaka huu, na sasa tunaweza kusema kwamba tumeongeza idadi ya mashirika yatakayonufaika kwa makusanyo hayo mwaka 2013 kutoka tisa ya awali hadi 16. Miongoni mwa mashirika hayo, yapo yale ambayo yamekuwa yakinufaika kila mwaka lakini pia yapo mapya. 
   “Fedha zinazokusanywa kutokana na mashindano ya Mbio za Mbuzi huleta mabadiliko kwenye mashirika madogo madogo ya hisani yasiyo na fursa pana za kupata fedha nyingi. Mbali na furaha na burudani zinazopatikana siku ya tukio, kitu kikubwa katika mbio hizi ni kusaidia vikundi na mashirika haya ya hisani yanayopambana kuyabadili maisha ya mtu mmoja mmoja. “Tunawashukuru maelfu ya watu walioshiriki, wakatuunga mkono na kuja kwenye tukio hili la burudani, pamoja na wafadhili kwa moyo wao wa ukarimu na kujitoa kwani bila wao haya yote yasingefanikiwa.” Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti yetu www.goatraces.com

  : Mwenyekiti wa Kamati ya  Mbio za mbuzi za Hisani Dar es Salaam, Karen Stanley (kulia) akikabidhi mfano wa hundi ya shs milioni 35 kwa Boniventure Mchovu zitakazopewa kwa mashirika ya kujitolea 16 ambazo
  zilipatikana wakati wa mashindano ya bio za mbuzi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam Juni 1 Mwaka huu. Hafla hiyo ilifanyikan jijini Dar es Salaam

  Mwenyekiti wa Kamati ya  Mbio za mbuzi za Hisani Dar es Salaam, Karen Stanley (katikati aliyevaa gauni jekundu) akipozi kwa picha pamoja na baadhi ya wadhamini na wawakilishi wa mashirika ya hisani 16 katika hafla ya kuyakabidhi mashirika hayo shs milioni 35 zilizopatikana wakati wa mashindano ya mbio za mbuzi yaliyofanyika
  jijini Dar es Salaam Juni 1 Mwaka huu. Hafla hiyo ilifanyikan jijini Dar es Salaam

  Wasanii wa kikundi cha Kigamboni Community Centre wakitoa burudani katika hafla ya kuvikabidhi vikundi 16 vya hisani msaada wa fedha wa shs milioni 35 zilizopatikana wakati wa mashindano ya mbio za mbuzi ya mwaka huu. Hafla ilifanyika jijini Dar es Salaam

   Mashirika yanayonufaika mwaka huu:  • Matumaini Day Care Center for Disabled Children – www.holyuniontanzania.co.ok

  • Zanzibar Outreach Program (ZOP) – www.zopzanzibar.org

  • Bibi Jann's Centre – www.bibijann.org

  • Fahari Zanzibar – www.fahari-zanzibar.com

  • CCBRT (Comprehensive Community Based Rehabilitation in Tanzania) -  www.ccbrt.org.tz

  • Malaika Kids –  www.malaika-kids.net

  • AC-AF – www.ac-af.com

  • Foxes' Community and Wildlife Conservation Trustwww.foxesngo.org

  • The Daughters of Mary Immaculate and Collaborators (DMI) - www.dmimissionafrica.org

  • Sea Sense – www.seasense.org

  • Ramat – www.ramat-tz.org

  • Wonder Workshop – www.wonderwelders.org

  • Molly’s Network – www.mollysnetwork.org

  • Kidzcare Kerege Children’s Home and Pre-School – friends@cats-net.com

  • St Paul’s English Medium Primary School – Wilfred_muhogolo@yahoo.com

  • The Mango Tree Orphan Trust – www.themangotree.org  0 0

  Roboti inayokamua Ng'ombe maziwa Uholanzi. Mtambo huu unauzwa Euro laki moja na wakulima wa Uholanzi wanakopeshwa na Mabenki kwa riba ya asilimia tatu kwa mwaka na wanatakiwa kurejesha mkopo ndani ya miaka thelathini. Mtambo huu umeonyeshwa leo kwa Mabalozi wa Nchi za Afrika Uholanzi wanaotembelea maeneo mbalimbali ya Uholanzi.
  Mabalozi wa Afrika Uholanzi Wakimsikiliza Mkurugenzi  Msaidizi wa Afrika wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uholanzi akiwaeleza jinsi Serikali ya Uholanzi inavyosaidia Wafugaji wa Ng'ombe wa Maziwa. Mwenye tai ya rangi ya taifa ni Balozi wa Tanzania Uholanzi, Ubelgiji, Luxemborg na Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala.

  0 0

  Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga, akisoma hotuba yake wakati wa sherehe ya siku ya wanachama wastaafu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Meneja Kiongozi Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa NSSF, Eunice Chiume na Mkurugenzi wa Uendeshaji, Crescentius Magori. 
  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori akizungumza wakati wa sherehe ya siku ya Wanachama wastaafu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF, Abubakar Rajabu, Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga na Meneja Kiongozi, Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume. 

  Mstaafu wa NSSF, Justina Lyela akitoa ushuhuda wa athari za fao la kujitoa wakatti wa sherehe za wastaafu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Abdallah Ulega akifungua mafunzo ya siku moja kwa Madiwani kuhuisiana na Sheria ya Maadili ya Viongozi Wa Umma.
  Kamishna wa Maadili Jaji mstaafu Salome Kaganda akitoa taarifa fupi ya Sekritereti ya Maadili ya Umma kwa Madiwani wa Halmashauri ya wilaya Kilwa.
  Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa wakiwa katika mafunzo.
  Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya Ya Kilwa Abdallah Ulega akiwa katika picha ya Pamoja na Kamisshna wa Maadili Jaji Mstaafu Salome Kaganda na Madiwani wa Halmashauri ya Wiaya ya Kilwa waliohudhuria mafunzo ya Maadili katika Ukumbi wa Jumba la Maendeleo.

  Picha na Habari na Abdulaziz Video -Kilwa.

  Madiwani Nchini wametakiwa kutambua kuwa wanajukumu kubwa la kusimamia maadili katika maeneo yao pamoja na Halmashauri kwa kuwa karibu na Wananchi ikiwa pamoja na kutatua kero zinazowakabili badala ya wao kujiona ni sehemu ya Halmashauri pekee.

  Akifungua semina ya Mafunzo kwa Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa kuhusu Sheria na Maadili ya Viongozi wa Umma,Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi,Abdallah Ulega alieleza kuwa ili kudumisha demokrasia na Utawala Bora na kuimarisha imani kwa Jamii ni Vema.

  Viongozi kusimamia Utekelezaji wa sheria maadili ikiwa Pamoja na Ujazaji wa Tamko linabainisha na Rasilimali Ulizonazo Aidha Ulega aliwataka Madiwani hao kutoa Maamuzi sahihi kwa kufuata sheria ,Kanuni na taratibu kwa kufuata Miongozo na ikiwa Pamoja na Kubainisha Mali alizonazo kama sheria Namba 13 ya maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995 inavyoelekeza.

  'Ngd zangu Waheshimwa Madiwani lazima mfahamu kuwa suala la Maadili na Utawala Bora ni jambo linalopewa nafasi ya pekee katika Serikali yetu na ili kufikia mafanikio ni muhimu kwenu kuwa na maadili mema ikiwa pamoja na kuwa karibu na jamii hii itaongeza ufanisi katika utoaji wa huduma bora na watumishi wa serikali wawajibike kwa wananchi na vyombo vya habari visaidie ili jamii nayo iwe katika Uadilifu...Alimalizia Ulega.

  Akifunga Mafunzo hayo Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Umma,Jaji mstaafu Salome Kaganda alieleza kuwa Mafunzo hayo yameendeshwa chini ya mradi wa Elimu kwa UMMA Unaofadhiliwa na Shirika la kutoa Misaada la Kimarekani(USAID)na kuwezeshwa na Sekretarieti ya Maadili ya Umma alibainisha kuwa Kuongezeka kwa Halmashauri na Madiwani na kufikia Halmashauri 162 na kuwa na Madiwani 4461 ni Baadhi ya Changamoto kwa kutoweza kuwafikia kutokana na ufinyu wa Bajeti hali iliyofanya Halmashauri hiyo kutopatiwa mafunzo hayo toka mwaka 2006.

  'Kwa kumbukumbu zangu semina ya kwanza kwa wilaya ya Kilwa ilifanyika mwaka 2006 na semina ya pili mwaka 2009 hii inamaanisha madiwani waliochaguliwa mwaka 2010 hii inamaanisha kuwa madiwani hao hawajapata uelewa kuhusiana na mambo mbalimbali ikiwa utoaji wa Tamko la Mali kwa Viongozi wa Umma kwa hiyo naomba Ushirikiano kwa Halmashauri kusaidia kuwezesha utoaji wa Elimu ili kutatia baadhi ya Changamoto isije kutokea Diwani au kiongozi wa Umma akapoteza sifa za kuwa Kiongozi..Alibainisha Jaji Mstaafu Salome Kaganda.

  Kufuatia Mafunzo hayo ya Siku Moja yaliyofanyika katika Ukumbi wa Jumba la Maendeleo wilayani Kilwa Baadhi ya Madiwani akiwemo wa Kata ya Miguruwe,Mitole na Lihimalyao wilayani Humo waliiomba Serikali kubadili Sheria hiyo kwa kuongeza na Watumishi wa Umma kufuatia Kuongezeka kwa Ubadharifu Huku Sheria ya Kutowabana na Kama Viongozi wa Umma huku wakiendelea kijilimbikizia mali muda mfupi baada ya kuanza kazi.

older | 1 | .... | 161 | 162 | (Page 163) | 164 | 165 | .... | 3348 | newer