Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1627 | 1628 | (Page 1629) | 1630 | 1631 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Mtanzania Lilian Danieli mwenye kampuni yake ya NASHONA amefungua duka la nguo za Kitanzania Goldsboro jimbo la North Carolina nchini Marekani. Uzinduzi wa duka hilo ambalo lipo Center Street katikati ya mji huo wa Goldsboro ulifanyika siku Jumamosi March 25, 2017. Anuani kamili ya duka ni 119 Center Street, Goldsboro, NC na simu ya dukani ni 918 947 1273.

  Katika duka hilo nguo mbalimbali vitenge toka Tanzania ikiwa asilimia 90 ameshona yeye mwenyewe na baadhi ya vingine kuja toka Tanzania. Duka litakua linafunguliwa siku ya Jumanne mpaka Jumamosi. Picha na Vijimambo Blog na Kwanza Production
  Baadhi ya wateja waliokuwepo dukani hapo siku ya uzinduzi wa duka hilo Jumamosi March 25, 2017 Goldsboro, North Carolina nchini Marekani.
  Lilian Daniel Kulia akikinja moja ya nguo zilizo nunuliwa na mmoja ya wateja wake siku ya uzinduzi wa duka lake la nguo za kiTanzania lililozinduliwa siku ya Jumamosi March 25, 2017.
  Kushoto ni Serena Danieli akisaidiana na dada yake Imani Danieli katika kuhakikisha mahesabu ya duka yanaenda sawa.
  Lilian Danieli akiwa na mmoja ya wateja wake akiwaonyesha nguo zake na kuwapa maelekezo. Picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa Taasisi ya Maendeleo ya Elimu inayohusiana na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu,Uti wa Mgomgo na Vichwa maji  Dr.Hosea Piquer akiongoza Ujumbe wa Wataalamu   wa Upasuaji wa Kichwa na Uti wa mgongo   walipofika Ikulu Mjini Unguja kwa mazungumzo na Rais
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Ujumbe wa Wataalamu   wa Upasuaji wa Kichwa na Uti wa mgongo mara walipofika Ikulu Mjini Unguja kwa mazungumzo (wa pili kulia)Rais wa Taasisi ya Maendeleo ya Elimu inayohusiana na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu,Uti wa Mgomgo na Vichwa maji  Dr.Hosea Piquer akiongoza  Ujumbe huo. Picha na Ikulu.

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Juma Abdalla Juma (Mabodi),Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Mhe,Borafya Silima na Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto Mhe,Moudline Cyrus Castico (kulia) wakiwa katika Tamasha la Taarab rasmi ya kusherehekea Ushindi wa CCM na Kumpongeza Dk.Shein kwa kutimiza mwaka mmoja tokea kuchaguliwa kuwa Rais,katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani
   Baadhi ya Viongozi mbali mbali wakiwemo Mawaziri wakiwa Tamasha la Taarab rasmi ya kusherehekea Ushindi wa CCM na Kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein    kwa kutimiza mwaka mmoja tokea kuchaguliwa kuwa Rais,katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani Mjini Zanzibar
   Wasanii wa Kikundi cha Big Star cha Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mjini kikitoa burudani wakati wa Tamasha la Taarab rasmi ya kusherehekea Ushindi wa CCM na Kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein    kwa kutimiza mwaka mmoja tokea kuchaguliwa kuwa Rais,katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani Mjini Zanzibar
  Mwimbaji wa Kikundi cha Big Star cha Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mjini Munira Mngwame Ame alipotoa burudani ya wimbo na Kikundi chake jana wakati wa amasha la Taarab rasmi ya kusherehekea Ushindi wa CCM na Kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein    kwa kutimiza mwaka mmoja tokea kuchaguliwa kuwa Rais,katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani Mjini Zanzibar. 


  0 0

  Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba amewataka maofisa na askari Polisi kote nchini kuendelea kufanya kazi kwa uadilifu ili kujenga taswira nzuri kwa wananchi wanaowahudumia jambo ambalo litaongeza imani na ushirikiano katika kukomesha vitendo vya uhalifu nchini.
  Waziri Nchemba ameyasema hayo wakati alipokuwa akifungua kikao kazi cha Maofisa wakuu wa Jeshi la Polisi kutoka makao makuu, Makamanda wa Polisi wa Mikoa na vikosi kutoka bara na Zanzibar kinachoendelea mkoani Dodoma.
  Alisema Pamoja na Jeshi hilo kufanya kazi nzuri bado linakabiliwa na changamoto ya baadhi ya askari na maofisa wasio waadilifu wanaofanya vitendo vya  kuwabambikia wananchi kesi na wakati mwingine kuwabadilishia kesi ili kujenga mazingira ya kupatiwa rushwa jambo ambalo ni kinyume na maadili ya askari Polisi.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba (kulia) pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu  wakiongozwa na askari wa kikosi cha  bendera kuingia ukumbini  kwa ajili ya ufunguzi wa kikao kazi cha mwaka kinachowahusisha maafisa wakuu wa jeshi la Polisi na makamanda wa mikoa na vikosi kinachofanyika mkoani Dodoma. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba (kulia) akiongea na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu  wakati wa hafla ya ufunguzi wa kikao kazi cha maafisa wakuu wa jeshi la Polisi na makamanda wa mikoa na vikosi kinachofanyika mkoani Dodoma. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.

   Baadhi ya maofisa wakuu wa Jeshi la Polisi wakiimba wimbo wa maadili ya afisa wa polisi wakati wa hafla ya ufunguzi wa kikao kazi cha maafisa hao na makamanda wa mikoa na vikosi kinachofanyika mkoani Dodoma. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.


  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba (kulia) akitoa hotuba ufunguzi wa kikao kazi cha mwaka kinachowahusisha maafisa wakuu wa jeshi la Polisi na makamanda wa mikoa na vikosi kinachofanyika mkoani Dodoma. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi. 

   Picha Na Hassan Mndeme. 
  Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0
  0 0
 • 03/27/17--12:03: IN LOVING MEMORY
 • Dr Henry C. M Nyamubi 

  Born 12 Feb 1958
  Died  28 March 2014

  Seconds become hours, hours into days,days into weeks, week's into months, months into years... 

  It is now two years since you were called by our Lord.. Though your physical gone, your memories remain with us forever.. 

  Remembered by your Parents, Wife, Daughters, Brothers, Sisters, Nephews, Nieces, Grandchildren, Relative's and Friends.. 

  The Lord gave and the Lord as taken away. 

  May the name of the Lord be praised. 

  Rest in peace our beloved till we meet again

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akipokea sehemu ya vifaa vya michezo kutoka kwa Mdau Mkubwa wa Michezo nchini, Athuman Tippo maarufu kama Zizzou, kwa ajili ya kuhamasisha Michezo kwa vijana wa Wilaya hiyo, kupitia Kampeni ya Michezo kwa vijana ya Uchumi Cup iliyoianzisha DC Gondwe kwa ajili ya kuwahamasisha vijana kujikwamua kiuchumi kupitia fursa ya Michezo. Makabidhiano hayo yamefanyika katika Duka la Vifaa vya Michezo la Zizzou Fashion, Sinza Jijini  Dar es salaam.
  Sehemu ya vifaa vya michezo vilivyokabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe.

  0 0

  . Mgeni Rasmi wa Mkutano Mkuu wa Jeshi la Polisi unaoendelea mkoani Dodoma, Waziri wa Mambo ya Ndani Nchini, Mh. Mwigulu Nchemba (katikati) pamoja na Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati wa NMB, Bw. Abdulmajid Nsekela ( wa kwanza kulia) na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, Ernest Mangu (wa kwanza kushoto) wakionesha mfano wa hundi ya shilingi Milioni 50 iliyotolewa na Benki ya NMB kwa ajili ya mkutano huo.
   BENKI ya NMB imekabidhi udhamini wa shilingi Milioni 50 kwa jeshi la polisi kwaajili ya kufanikisha mkutano mkuu wa jeshi la polisi unaoendelea mkoani Dodoma kwa siku tatu. Mkutano huo unajumuisha maafisa waandamizi wa polisi na makamanda wa mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani. 

  Udhamini huu unalenga kufanikisha mkutano huo wenye malengo ya kujadiri changamoto na mafanikio yaliyopatikana na jeshi la polisi kwa mwaka 2016 na kuweka mipango bayana ya usalama kwa mwaka 2017. 
  Akikabidhi hundi ya mfano kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi – Mh Mwigulu Nchemba, Kaimu Afisa Mkuu wa wateja Wadogo na wa Kati wa NMB – Abdulmajid Nsekela alisema kuwa udhamini huo unalenga kutambua umuhimu wa jeshi la polisi si tu kwa NMB bali kwa jamii yote kwa ujumla huku akisisitiza kuwa utendaji kazi mzuri wa jeshi la polisi umekuwa chachu ya maendeleo ya sekta ya kibenki nchini kwani benki zimekuwa zikifanya kazi katika mazingira tulivu bila matukio mengi ya uhalifu. 

  “Niseme tu kuwa jeshi la polisi wamekuwa wadau wetu wakubwa katika nyanja za ulinzi na pia biashara na hivyo hatuwezi kusita kudhamini mkutano huu mkubwa na muhimu kwa nchi yetu, tumekuwa tukitoa mchango kwa miaka kadhaa sasa kwa mkutano mkuu wa jeshi la polisi, na awamu hii, tumetoa mchango wa shilingi Milioni 50 ili kufanikisha mkutano,” alisema Bwana Nsekela. Ndugu Nsekela pia alilishukuru jeshi la polisi kwa kutambua mchango wa NMB na kuwapatia Nafasi ya kufanya kazi pamoja. NMB pia ilitoa wasilisho la huduma mbalimbali ambazo imekuwa ikitoa kwa jeshi la polisi. Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo na Kati, Bw. Abdulmajid Nsekela akitoa wasilisho la huduma za kibenki kwa jeshi la polisi (hawapo Pichani) kwenye mkutano mkuu wa jeshi la polisi mkoani Dodoma. Mgeni Rasmi wa Mkutano Mkuu wa Jeshi la Polisi unaoendelea mkoani Dodoma, Waziri wa Mambo ya Ndani Nchini, Mh. Mwigulu Nchemba pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, Ernest Mangu, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma - Jordan Rugimbana pamoja na Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Abdulrahman Kaniki wakiwa wanatoa heshima kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini kabla ya ufunguzi rasmi.

  Katika wasilisho hilo, NMB iliainisha mafanikio mbalimbali ambayo imeyafikia katika utoaji huduma na kuingizia serikali mapato huku ikielezwa kuwa tangu mwaka 2010, NMB imelipa kwa serikali jumla ya shilingi bilioni 336 kama kodi huku serikali ikinufaika na jumla ya shilingi bilioni 50 kama gawio kutoka NMB tangu mwaka 2010, NMB pia imelipa gawio la zaidi ya shilingi bilioni 174 tangu mwaka 2010.

   Thamani ya hisa serikali zilizoko NMB yaani asilimia 31.8 ni shilingi bilioni 437. Ndugu Abdulmajid aliongeza kuwa “Tumekuwa tukifanya kazi vizuri na jeshi la polisi kwani kwa upande wa mikopo tu, mpaka sasa, mikopo yenye thamani ya shilingi Bilioni 27 imetolewa kwa zaidi ya askari polisi 8,569 kupitia mikopo ya mishahara.” NMB ndiyo benki inayoongoza nchini kwa kuwa na matawi mengi kwani ina matawi zaidi ya 189 yaliyopo karibia kila wilaya, ATM Zaidi ya 700 nchi nzima pamoja na idadi ya wateja inayofikia milioni mbili na nusu.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea taarifa rasmi ya uchunguzi wa kifo cha Faru John kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali, Prof. Samwel Manyele ambaye alikuwa akiongoza tume maalum iliyoundwa na Waziri Mkuu.
  Waziri Mkuu amepokea taarifa hiyo, leo (Jumatatu, Machi 27, 2017) kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam.
  Akisoma taarifa hiyo mbele ya Waziri Mkuu, Prof. Manyele amesema tume yake ilifanya uchunguzi wa kifo cha Faru John kwa kupima vinasaba vya sampuli mbalimbali vikiwemo mzoga, fuvu, mifupa, pembe, damu, ngozi na kinyesi kilichokaushwa ambapo ilibainika kuwa vyote ni vya mnyama mmoja, aina ya faru mweusi ambaye ni dume.
  Prof. Manyele amesema matokeo hayo yamethibitisha kuwa faru John alikufa katika hifadhi ya Sasakwa Grumeti kwa kukosa matunzo na uangalizi wa karibu.

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea  kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele  taarifa ya Tume aliyoiunda ya kuchunguza suala la Faru John, ofisini kwake jijjini Dar es salaam Machi 27, 2017. (Picha na Ofisi ya `Waziri Mkuu)

  “Maabara iliyotumika ni ya Chuo Kikuu cha Pretoria, Afrika Kusini chini ya usimamizi wa timu ya wataalamu kutoka Tanzania, wachunguzi wa Serikali, chini ya Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali. Sababu za kifo chake zilichangiwa na kukosa matunzo na uangalizi wa karibu, kukosa matibabu alipoumwa, mazoea yanayotokana na kutofuata taratibu zilizowekwa kisheria na mapungufu ya kiuongozu kwa Wizara husika, hifadhi na taasisi zake,” amesema.

  Prof. Manyele amesema mapungufu waliyoyabaini kutokana na uchunguzi huo ni kutokuwepo kwa kibali rasmi cha kumhamisha Faru John; kukosekana kwa mkataba wa kupokelewa kwa Faru John hifadhi ya Sasakwa Grumeti na kutofuatiliwa kwa afya na maendeleo ya Faru John baada ya kuhamishwa.  
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kukabidhiwa taarifa ya tume ya kuchunguza suala la Faru John na Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele, Ofisini kwake jijini Dar es salam Machi 27, 2017.

  Mengine ni uchukuaji holela wa sampuli za wanyama pori kwa lengo la utafiti na kuzisafirisha nje ya nchi; migongano ya kimaslahi kati ya watumishi waliolenga kusimamia taratibu na wale wenye kusimamia maslahi binafsi na uwepo wa taasisi nyingi zenye mamlaka sawa juu ya masuala ya uhifadhi wa wanyamapori.

  Pamoja na kwamba mawasiliano yanaonyesha zoezi hilo liliridhiwa na Wizara, hapakuwepo na kibali rasmi kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori cha kuruhusu kumhamisha Faru John kutoka NCAA kwenda Grumeti,” amesema Prof. Manyele katika ripoti yake.  

  Akizungumzia kuhusu uchukuaji holela wa sampuli za wanyama pori kwa lengo la utafiti na kuzisafirisha nje ya nchi, Prof. Manyele amesema kumbukumbu za watafiti na aina ya sampuli wanazochukua haziwekwi vizuri  na kwamba tume inashauri TAWIRI na TANAPA wapewe msisitizo juu ya umuhimu wa kuzingatia majukumu yao.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkemia Mkuu wa Serikali , Profesa Samwel Manyele wakati  alipowasilisha taarifa ya tume ya uchunguzi wa suala Faru John baada ya kukabidhi taarifa hiyo , Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Machi27, 2017.

  Amesema kuna umuhimu wa kudhibiti watafiti na tafiti ili kulinda taarifa muhimu za vinasaba vya wanyamapori (Genetic information) dhidi ya mataifa mengine. “TUME inashauri maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ianzishe kitengo cha Sayansi Jinai na Uchunguzi wa Vinasaba vya Wanyamapori (DNA Forensic Wildlife Laboratory) ili Serikali na vyombo vyake iweze kufanya maamuzi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupata ushahidi wa kimahakama katika kesi za jinai zinazohusu wanyamapori (Expert Witness).

  Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusomewa ripoti huyo, Waziri Mkuu aliishukuru timu ya uchunguzi iliyokuwa chini ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kazi iliyoifanya ikiwemo kuainisha udhaifu uliokuwemo ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii na taasisi zake.

  “Ofisi yangu itaipitia taarifa hii ambayo ni kubwa kiasi na kuifanyia kazi. Matokeo ya kazi hiyo, tutayatoa hivi karibuni ili kuonyesha Serikali imeamua kufanya nini juu ya mapendekezo yaliyotolewa.”

  Alimtaka Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Kupambana na Ujangili wa Wanyamapori, Bw. Robert Mande, afuatilie mapendekezo yaliyoainishwa na tume hiyo na wayafanyie kazi mapema iwezekanavyo.

  Waziri Mkuu aliiunda tume hiyo Desemba 10, mwaka jana baada ya kupokea pembe mbili za faru John na taarifa yenye nyaraka zilizotumika kumhamisha faru huyo. Hatua hiyo ilifuatia agizo alolitoa Desemba 6, 2016, akiwa ziarani mkoani Arusha, ambapo alitoa siku mbili na kuutaka uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), umletee nyaraka zote zilizotumika kumhamisha faru John kutoka kwenye hifadhi hiyo.

  Alitoa agizo hilo alipotembelea ofisi za makao makuu ya NCAA zilizoko wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha na kuzungumza na watumishi wa mamlaka hiyo pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafugaji ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo.


  0 0


  0 0

  Bonge la supermarket jipya lipo katika jengo la kituo kikuu cha daladala  cha Makumbusho jijini Dar es salaam ambako utapata  BIDHAA KIBAO kwa bei  poa kabisaaa kama vile Mikate, keki,  biscuit wanazopika wenyewe pamoja na vyakula vya kila aina vinapatikana hapo
  Usipitwe...Fanya uwatembelee CHOPPIES ukajipatie vitu vingi kwa bei ya kiwandani na wapo wazi kuanzia saa 12:00 kamili asubuhi mpaka saa tatu usiku siku za Jumatatu mpaka Ijumaa.Siku za weekend wako wazi kuanzia saa 03:00 kamili asubuhi mpaka saa 3 usiku. 

  KARIBUNI SANA!
  0 0


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Nakala ya Vitabu vya  Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni, 2016, kutoka kwa CAG  Profesa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es Salaam. 

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akifurahi pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad mara baada ya kupokea ripoti hizo Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad mara baada ya kupokea ripoti hizo za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) 
  Maafisa kutoka katika Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wakifatilia kwa makini wakati wa uwasilishwaji wa Ripoti hizo Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU .


  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza kuachiwa huru kwa Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego (pichani) na wimbo wake kuruhusiwa kupigwa  katika vyombo vyote vya Redio na Televisheni.

  Wimbo huo unaojulikana kwa jina la "Wapo" ulikuwa umefungiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) mapema leo na yeye mwenyewe kukamatwa akiwa mkoani Morogoro alipoenda kikazi.

  Akizungumza na waandishi wa habari mchana huu mjini Dodoma wakati akitoa taarifa hiyo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harison Mwakyembe amesema uamuzi wa kuruhusiwa kupigwa kwa wimbo umetoka kwa Mheshimiwa Rais John Magufuli baada ya kupokea ujumbe wa kumtaka auruhusu  wimbo wa msanii huyo kupigwa katika vyombo vyote.

  "Wimbo unaozungumziwa Rais Magufuli anaupenda sana. Na  ameomba Ney wa Mitego aachiwe huru na aendelee na kazi zake. Ila anaweza kuuboresha zaidi wimbo wake huo kwa kuongeza vitu zaidi, kama vile wakwepa kodi, watumia dawa za kulevya nk". alisema Dk. Mwakyembe.

  Mwakyembe alisema kuwa Rais amefurahishwa na wimbo wa Ney wa Mitego na kumshauri kama inawezekana aendelee kuwataja watu wengine kama vile wauza unga, wakwepa kodi, wabwia unga, wezi na wengine wasio na maadili mema katika jamii.

  0 0

   Mkurugenzi wa Masoko wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Vivian Shaluwa akizungumza na wadau waliofika katika hafla ya ugawaji vyeti kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha nne somo la Sanaa.
   Baadhi ya washiriki waliofika kushuhudia ugawji huo wa vyeti
   Rais wa Shirikisho la Sanaa Maonyesho , William Chitanda akizungumza juu ya umuhimu wa wanafunzi kufanya sanaa pindi wanapokuwa mashuleni
   Baadhi wanafunzi wa Sekondari wakiwa wana fatilia hafla hiyo

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Na Zuena Msuya DSM,

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo amefungua mafunzo ya ufungaji wa migodi yanayotolewa kwa wataalam wa mbalimbali wanaoshiriki katika Kamati ya Kitaifa ya ufungaji wa Migodi.

  Watalaam hao wanatoka katika Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto zinazojitokeza wakati wa ufungaji wa migodi nchini.Mafunzo hayo yanatolewa jijini Dar Es Salaam,na Serikali ya Canada kwa siku tano kuanzia 27-31 machi 2017.

  Akizungumza wakati wa akifungua wa mafunzo hayo, Dkt. Pallangyo alisema kuwa mafunzo hayo yatawawezesha wataalamu wa migodi nchini kuwa na uelewa zaidi juu ya hatua zote zinazotakiwa kufuatwa wakati na baada ya ufungaji wa migodi ili kuondoa changamoto mbalimbali zilizokuwa zikijitokeza baada ya migodi kufungwa.

  Dkt. Pallangyo, alifafanua kuwa, kwakuwa Serikali ya Canada imejikita katika Sekta ya Madini kwa zaidi ya miaka 200, hivyo mafunzo hayo yatawasaidia wataalam wa ndani kufahamu na kujifunza namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza kupitia migodi iliyokwishafungwa katika nchi hiyo ili yasijitokeze hapa nchini.

  ” Tusiwe watu wa kusoma tu na kufunga migodi, tujifunze kwa vitendo kutoka kwao makosa waliofanya wakati wa ufungaji wa migodi kwa kuwa Canada ipo katika Sekta ya madini kwa zaidi ya miaka 200 na tujirekebishe, ili makosa yaliyotokea kwa yasijirudie katika migodi yetu,” alisisitiza Dkt.Pallangyo.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo ( kulia) na Mkuu wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Canada, Sue Steffen,(kushoto) akizungumza wakati wa mafunzo ya kufunga wa migodi yanayotolewa kwa Kamati ya Kitaifa ya ufungaji Migodi.Mafunzo hayo ya siku tano yanatolewa na Serikali ya Canada jijini Dar Es Salaam.
  Washiriki wa mafunzo ya ufungaji migodi ambao ni Kamati ya Kitaifa ya ufungaji Migodi wakifatilia mada mbalimbali wakati wa mafunzo hayo yanayotolewa kwa siku tano jijini Dar es salaam na Serikali ya Canada.

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo ( katika waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Kitaifa ya ufungaji Migodi wakati wa mafunzo ya ufungaji wa migodi yanayotolewa kwa siku tano jijini Dar es salaam na Serikali ya Canada. Kushoto kwake ni Mkuu wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Canada, Sue Steffen, na kulia kwake ni Afisa Rasilimali Watu Mkuu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Suzan Kiwelu.


  0 0


  0 0

  Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii
  Wakala wa Vipimo nchini imewaasa Wajasiriamali kuzingatia Vipimo sahihi katika upimaji wa bidhaa ili kuendana na Uchumi wa Viwanda na kufikia soko la Kimataifa kwa bidhaa husika.
  Akizungumza na Globu ya Jamii katika Maonyesho ya Kimataifa ya Wanawake Wajasiriamali yaliyojumuisha nchi za Tanzania,Rwanda, Burundi, Uganda na Comoro, Kaimu Meneja, Elimu, Habari na Mawasiliano-Wakala wa Vipimo, Irene John amesema kuwa wafanyabiashara wote watumie matumizi sahihi ya vipimo wanapotumia au kufungasha bidhaa zao.
  Irene amesema kuwa si sahihi wafanyabiashara kutumia vikombe, Kopo au Debe  badala ya Mzani katika upimaji wa bidhaa,amebainisha kuwa ni kinyume cha Sheria ya Vipimo, Sura namba 340 mapitio ya mwaka 2002(Faini ya Sh. 10,000) na Maboresho ya sheria ya mwaka 2016 faini  ni  Sh. 100,000 au kifungo cha Mitatu au vyote kwa pamoja.
  Kwa upande wao Wajasiriamali waliohudhuria Maonyesho hayo,Grady John na Glory Shayo wamewashukuru Wakala wa Vipimo kutoa elimu kwa Wajasiriamali hao kutokana kuwafanya wateja wa bidhaa hizo kuwa na uhakika kutokana na vipimo sahihi.
  Kaimu Meneja, Elimu, Habari na Mawasiliano-Wakala wa Vipimo, Irene John akitoa Elimu ya Vipimo kwa Mjasiriamali na Msimamizi wa Mafuta ya Dina Marios Baby Oils, Glory Shayo katika Maonyesho ya Kimataifa ya Wanawake Wajasiriamali jijiniDar es salaam

   Kaimu Meneja, Elimu, Habari na Mawasiliano-Wakala wa Vipimo, Irene John akizungumza na Mwandishi wa Michuzi TV kuhusiana na elimu kwa Wajasiriamali kutumia Vpimo sahihi katika upimaji wa bidhaa.

   Mjasiriamali na Msimamizi wa Mafuta ya Dina Marios Baby Oils, Glory Shayo akielezea bidhaa hiyo katika Maonyesho ya Kimataifa ya Wanawake Wajasiriamali jijiniDar es salaam
  Sehemu ya Wafanyabiashara waliohudhuria Maonyesho ya Kimataifa ya Wanawake Wajasiriamali yaliyojumuisha nchi za Tanzania,Rwanda, Burundi, Uganda na Comoro.

  0 0  0 0


  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
  Kampuni ya kuuza Ving’amuzi ya StarTimes Tanzania inatoa pakacha la pasaka  kwa wateja wake ambapo kampuni hiyo imetangaza kuwa kuanzia tarehe 16 Machi 2017  wateja watakaojiunga na kifurushi cha kuanzia Mambo watapata ofa ya wiki moja  ya kifurushi cha Uhuru.

  Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam  leo Maeneja Masoko wa StarTimes Tanzania, Felix Awino amesema kuwa wateja waliolipia  watafurahia maudhui mazuri yatakayokidhi na kuburudisha familia msimu mzima  wa pasaka.Ambapo ndani ya wiki nne (4) wiki moja ya kwanza mteja atafurahia kifurushi cha juu.
  Maeneja Masoko wa StarTimes Tanzania, Felix Awino akizungumza waandishi wa habari. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini limetoa ratiba ya michezo miwili ya Kombe la Shirikisho maarufu kama Azam Sports Federations Cup (ASFC) kwa timu za Yanga na Azam ambazo zilikuwa hazijapangwa.
  Mechi hizo zilishindikana kuchezwa baada ya Yanga na Azam kuwa wawakilisji katika michuano ya kimataifa ambapo April 95 Azam itashuka dimbani kuvaana na Ndanda kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi.
  Yanga ambao bado wanaendelea kuiwakilisha nchi kwenye kombe la Shirikisho barani Afrika wao mchezo wao utakuwa April 22 watakapovaana na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Taifa.
  Taarifa kutoka TFF zimesema kwamba michezo miwili ya mwisho ya Robo Fainali za ASFC zimepangiwa tarehe na pazia la nane bora litafungwa Aprili 22.
  Tayari Simba ya Dar es Salaam na Mbao FC ya Mwanza zimekwishafuzu hatua ya Nusu Fainali baada ya kuzitoa Kagera Sugar ya Bukoba na Madini FC ya Arusha katika Robo Fainali.
  Mbao FC iliwafunga Kagera Sugar 2-1 Uwanja wa Kaitaba, Bukoba wakati Simba SC iliwafunga Madini FC 1-0 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha bao pekee la Mrundi, Laudit Mavugo.
  Kikosi cha Prisons FC
  Kikosi cha Yanga

older | 1 | .... | 1627 | 1628 | (Page 1629) | 1630 | 1631 | .... | 3283 | newer