Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1626 | 1627 | (Page 1628) | 1629 | 1630 | .... | 3278 | newer

  0 0


  0 0

   Waziri mstaafu Profesa Mark Mwandosya akiwa ameamka alfajiri na mapema ili kufanya mazoezi na kuzunguka katika ziwa Nyasa hususan kwenye fukwe maarufu na mwanana za Matema wilayani Kyela mkoani Mbeya. Fukwe hizo ni mojawapo ya vivutio vikubwa vya utalii kwa kuwa na mandhari ya kupendeza, samaki wa kila aina pamoja na utengenezaji wa vyungu, magudulia na mitungi vya udongo. Profesa Mwandosya ameiambia Globu ya Jamii kwa njia ya mtandao kwamba Matema Beach pia ni location nzuri sana kwa watengeneza filamu za muziki, tamthiliya na kadhalika. 
    Waziri mstaafu Profesa Mark Mwandosya akiwa anafurahia Matema Beach
  Waziri mstaafu Profesa Mark Mwandosya akiwa anafurahia Matema Beach ndani ya mtumbwi unaoteleza juu ya maji tulivu na masafi ya Ziwa Nyasa.

  0 0

  Na Kareny Masasy- Malunde1 blog
  Inaelezwa kuwa tangu kuibuka kwa mauaji ya watu wenye ualbino mwaka 2007 takribani makaburi 22 nchini  Tanzania yamefukuliwa na watu wasiojulikana.
  Chama hicho kimeiomba serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Pombe Magufuli kuweka mkazo katika mapambano dhidi ya ukatili wa watu wenye ulemavu wa ngozi kama ilivyoonesha nguvu za kutosha katika vita ya dawa za kulevya na pombe aina ya viroba. 
  Akizungumza juzi kwenye kikao cha viongozi wa chama watu wenye ualbino kutoka mikoa ya kanda ya Ziwa ambayo ni Mara,Mwanza na Shinyanga na wanachama wengine Afisa mahusiano na habari TAS taifa Josephat Torner vitendo vya kufua makaburi ya watu wenye ualbino yanatishia amani yao 
  Torner alisema wanaiomba serikali kuelekeza nguvu katika masuala ya mauaji na ufukuaji wa makaburi ili kuwafanya watu wenye ualbino waishi kwa amani ndani ya nchi yao. 
  Katikati ni Afisa mahusiano na habari wa chama cha watu wenye ualbino nchini Tanzania (TAS )Josephat Torner akizungumza wakati wa kikao cha viongozi na wanachama wa chama hicho ambapo walilaani vitendo vya ufukuaji wa makaburi ya watu wenye ualbino.Kulia ni Mwenyekiti TAS mkoa wa Mara  Joseph Sinda,kushoto ni mwenyekiti TAS mkoa wa MwanzaAlfred Kapole 
  Baadhi ya wanachama wa chama cha watu wenye ualbino nchini Tanzania wakiwa katika kikao hicho. Picha na Suzy Butondo-Malunde1 blog.

  0 0

   Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh Angelina Mabulla Akifafanua  namna Fomu ya Umiliki Ardhi inavyo tumika ili kupata taarifa za awali za Mwananchi anaye andaliwa Hati ya Kumiliki Ardhi mbele ya Wajumbe wa kamati ya Bunge Ardhi Maliasili na Mazingira na Wananchikatika kijiji cha Mikoleko  Wilaya ya Kilombero- Morogoro  
   Mratibu wa Mradi wa Kuwezesha Umilikishaji wa Ardhi Godfrey Machabe akisoma Ripoti ya maendeleo ya mradi huo mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Mazingira wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya  Mradi huo Wilayani Kilombero-Morogoro

  Mwenyekiti wa kijiji cha Mikoleko Wilaya ya kilombero akielezea ushiriki wa Wanakijiji katika zoezi la kumilikisha ardhi ndani ya kijiji hicho Mbele ya Wajumbe wa kamati ya Bunge Ardhi, Maliasili na Mazingira. 

  0 0  Na Lulu Mussa

  Mwanga - Kilimanjaro 
  Imebainika kuwa Ziwa Jipe liko hatarini kutoweka endapo hatua za haraka hazitachukuliwa katika kulinusuru. Hayo yamesemwa  na Waziri mwenye dhamana ya usimamizi wa Mazingira Mh. January Makamba alipofanya ziara ya kukagua ziwa hilo ambalo sehemu kubwa imezungukwa na magugu maji.

  Waziri Makamba amesema kuwa ziwa hilo ni rasilimali muhimu na hivyo ni lazima kuwe na mpango wa muda mfupi na ule wa muda mrefu. Kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamiza wa Mazingira (NEMC) ameazimia kutangaza kupita Tangazo la Serikali kuwa eneo hilo ni eneo nyeti kimazingira."Tutatanga eneo hili kuwa eneo nyeti kimazingira na tutaweka masharti ya matumizi katika eneo hili" Alisisitiza Makamba

  Azimio hilo la kutangaza kuwa eneo mahsusi ama nyeti kimazingira itasaidi katika kuandika maandiko mbalimbali ya miradi na kupata fedha kutoka kwa wadau na washirika wa maendeleo. Pia litawekwa chini ya uangalizi maalumu na kuweka masharti ya matumizi bora ya eneo hilo. " Tutaweka masharti makali na magumu zaidi ili watakao kiuka wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria" Aliongezea Waziri Makamba.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akizungumza na Mtendaji wa Kijiji cha Butu, Kata ya Jipe Wilayani Mwanga Bw. Nassor Abdul wakati Waziri Makamba alipotembelea Ziwa Jipe ambalo limeathiriwa kwa kiasi kikubwa na magugu maji ambayo yanasababisha kupungua kwa shughuli za uvuvi ambazo ndio chanzo kikubwa cha mapato kwa wakazi wa eneo hilo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Bw. Aron Mbogho.

   Mifano kwa vitendo: Pichani Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiwa amembeba mtoto Meshack Ombeni  katika Kijiji cha Butu pembezoni mwa Ziwa Jipe. Waziri Makamba amewaasa wananchi hao kulinda Ziwa hilo ili liweze kunifaisha vizazi vijavyo na kuwatahadharisha kuwa uharibifu wa mazingira utahatarisha uhai wa ziwa hilo. .

  Upungufu mkubwa maji katika bwawa la nyumba ya Mungu. Inasemekana kupungua kwa kina cha maji kunatokana na ukame wa muda mrefu na uharibifu mkubwa  wa mazingira kutokana na shughuli za binadamu katika vyanzo vya maji vinavyopeleka maji katika bwawa hilo ukiwemo Mto Kikuletwa. Kwa tarifa kamili BOFYA HAPA


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dr. John Pombe Joseph Magufuli amewapandisha cheo Maafisa sita wa Uhamiaji kuwa Makamishna wa Uhamiaji kuanzia tarehe  28 mwezi Februari mwaka 2017, Wakati huo huo amewateua kushika  nyadhifa  mbalimbali katika Jeshi la Uhamiaji. 

  Walioteuliwa kushika nyadhifa hizo ni Mrakibu wa Uhamiaji (SI) Edward Peter Chogero kuwa Kamishna wa Divisheni ya Fedha na Utawala, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji (SSI) Samwel Rhobby Magweiga kuwa Kamishna wa Divisheni ya Udhibiti na Uongozi wa Mipaka, Mrakibu Mwandamizi (SSI) wa Uhamiaji Gerald John Kihinga kuwa Kamishna wa Divisheni ya Pasipoti na Uraia, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji (SSI) Musanga Mbusuro Etimba kuwa Kamishna wa Divisheni ya Hati za Ukaazi na Pasi, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji (SSI) Hannerole Morgan Manyanga kuwa Kamishna wa Divisheni ya Sheria. 
  Aidha Mh.Rais amemteua pia Naibu Kamishna wa Uhamiaji Mourice David Kitinusa kuwa Kamishna Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA).  Uteuzi huo unaanzia tarehe 28 mwezi Februari mwaka 2017.


  Imetolewa na

  Meja Jenerali Projest Rwegasira

  Katibu Mkuu

  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi  


  26 Machi 2017


  0 0  0 0


  Na  Bashir  Yakub

  Kutelekezwa  ni  pamoja  na  kunyimwa  huduma  za  muhimu  ambazo  kama  mke  alistahili  kupata. Huduma  muhimu  ni  kama  chakula, mavazi  ,  makazi,  matibabu, hela  ya  kujikimu  kwa  matumizi  ya  kawaida  ya  mwanamke,  pamoja  na  kila  hitaji  ambalo  kama  mwanamke  alitakiwa  kulipata.

  Ifahamike  kuwa  habari  ya kutelekeza  inawahusu  wote  mke  na  mme  kwa  maana  ya kuwa  mme  anaweza  kumtelekeza  mke  halikadhalika  mke  anaweza  kumtelekeza  mme. Hata  hivyo  makala  yatazungumzia   mme  kumtelekeza  mke  ambapo sura  ya  29 ,  Sheria ya  ndoa  iliyofanyiwa  marekebisho  mwaka  2010  itarejewa.


  1.AINA  ZA  KUTELEKEZA.    

  ( a ) Aina  ya  kwanza ni  kutelekeza  ambako  mume  anaondoka  kabisa  ndani  ya  nyumba  ambayo  alikuwa  akiishi  na  mke  wake kama  wanandoa  na  kwenda  kuishi  kwingine. Haijalishi huko  alikoenda   panajulikana  ni  wapi au  hapajulikani  suala  la  msingi  ni  kwamba  hayupo  katika  makazi  yake  ya  kawaida  ya familia.

  Aidha  ikiwa  hayupo  nyumbani  lakini  kwa  sababu  za  msingi  na za  kisheria  huko  sio  kutelekeza.  Sababu  hizo  ni kama  kuwa  jela, kuwa  hospitali, kuwa  amehamishiwa  sehemu  nyingine kwasababu  ya  matibabu   kwa  mfano  wengine  huamishiwa  mikoani, na pia  kuwa  vitani  labda  baadae  mkapoteza  mawasiliano  na  mazingira  mengine  ya  dharula  za  kibinadamu  na  ambayo  siyo  ya  makusudi   hayawezi  kuitwa  kutelekeza.


  ( b ) Aina  nyngine  ya kutelekeza  ni   hatua  ya  kuwa  mme  na  mke  wanaishi  wote  katika  nyumba   moja  au  chini  ya paa  moja lakini  mume  huyo  hajishughulishi  na  kutoa  matumizi  au  matunzo  kwa  mke  huyo  kwa  namna  yoyote  ile. Hajui  anakula  nini,  hajui  anavaa  nini, hajui  anapata  vipi  matibabu,  kwa ufupi  hajui  lolote  zaidi  ya  kumuona  tu  kama  binadamu  wengine  ambao  anawaona  mitaani  na  hana  uhusiano  nao.

  Pia kuishi  chini  ya  paa  moja  lakini  vyumba  tofauti  nako  ni kutelekeza    hata  kama   mke  anapewa  matumizi  yote  yanayostahili. Zaidi,  hata  kulala  chumba  kimoja  lakini  vitanda  tofauti  kwa  muda  mrefu  tena  kwa  makusudi  kwasababu  ya  mgogoro  wowote  nako  ni kutelekeza.  Lakini  pia  kulala  kitanda  kimoja  bila  kushiriki  tendo  la  ndoa kwa  makusudi  kwa muda mrefu   bila  sababu  za  msingi  za  kiafya au  vinginevyo nako  ni  kutelekeza.


  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko akimpa muhtasari Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai ambaye ameongoza wajumbe wa Kamati za kudumu za Bunge za Nishati na Madini pamoja na Kamati ya Bajeti bandari ya Dar es salaam kujionea makontena yenye shehena ya mchanga kutoka migodini iliyokuwa imezuiwa kusafirishwa nje ya nchi kwa agizo la serikali leo Machi 26, 2017
  Sehemu ya  makontena yenye shehena ya mchanga kutoka migodini ambayo imezuiwa  kusafirishwa nje ya nchi kwa agizo la serikali 
    Sehemu ya wajumbe wa Kamati za kudumu za Bunge za Nishati na Madini pamoja na Kamati ya Bajeti wakitembelea bandari ya Dar es salaam kujionea makontena yenye shehena ya mchanga kutoka migodini ambayo  imezuiwa kusafirishwa nje ya nchi kwa agizo la serikali leo Machi 26, 2017
    Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko akimpa maelezo  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai na wajumbe wa Kamati za kudumu za Bunge za Nishati na Madini pamoja na Kamati ya Bajeti bandari ya Dar es salaam juu ya makontena yenye shehena ya mchanga kutoka migodini iliyokuwa imezuiwa kusafirishwa nje ya nchi kwa agizo la serikali leo Machi 26, 2017
   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiwa na wajumbe wa Kamati za kudumu za Bunge za Nishati na Madini pamoja na Kamati ya Bajeti akiongea na wanahabari katika bandari ya Dar es salaam baada ya kujionea makontena yenye shehena ya mchanga kutoka migodini ambayo imezuiwa kusafirishwa nje ya nchi kwa agizo la serikali leo Machi 26, 2017

  0 0


  6

  0 0

  Na Veronica Simba – Dodoma

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesaini leseni za madini kutoka kwa wawekezaji mbalimbali waliowasilisha maombi na kutimiza taratibu zote zinazotakiwa kwa mujibu wa sheria.

  Leseni ya kwanza iliyosainiwa ni ya uchimbaji wa kati wa dhahabu katika eneo la Masagalu, Handeni yenye namba ML 570/2016. Leseni hiyo imehamishwa kutoka kwa mmiliki wake wa awali ambaye ni Najim & Company Ltd kwenda kwa Shale Investments Tanzania Ltd.

  Aidha, Waziri Muhongo alisaini leseni namba ML 572/2017 ya Sisti Mganga. Leseni hiyo ni ya uchimbaji wa kati wa madini ya ujenzi katika eneo la Itiso, Chamwino mkoani Dodoma.

  Leseni nyingine iliyosainiwa na Waziri Muhongo ni ya uchimbaji wa kati wa madini ya ujenzi aina ya kokoto, ambayo mmiliki wake ni Said Abdallah. Leseni hiyo namba ML 573/2017 ipo eneo la Chipite, Masasi.

  Profesa Muhongo aliwataka waombaji na wamiliki wote wa leseni za madini nchini, kuhakikisha wanatekeleza ipasavyo taratibu zote kama zilivyobainishwa katika Sheria ya Madini ikiwemo ulipaji wa mrabaha na kodi mbalimbali, kujenga mahusiano mema na jamii zinazowazunguka pamoja na kuzingatia utunzaji na uhifadhi wa mazingira.

  Zoezi hilo la utiaji saini lilifanyika hivi karibuni, Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma na kushuhudiwa na wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), akisaini leseni za madini za wawekezaji mbalimbali waliowasilisha maombi na kukamilisha taratibu zote zinazotakiwa. Anayeshuhudia ni Mwanasheria wa Wizara, Khadija Ramadhan.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kutoka kulia), akikabidhi leseni iliyohamishwa kutoka kwa mmiliki wake wa awali Najim & Company Ltd kwenda kwa Shale Investment Tanzania Ltd.


  0 0

  Madaktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Saifee ya nchini India wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa moyo . Katika ziara aliyoifanya nchini mwishoni mwaka jana kiongozi Mkuu wa Madheebu ya Bohora Duniani Mtakatifu Dkt. Syedna Aliqadr Mufaddal Saifuddin alimuahidi Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuleta madaktari wa Moyo nchini ambao watashirikiana na Madaktari wa JKCI kufanya upasuaji kwa wagonjwa. Timu ya wataalam hao ambao idadi yao ni sita imeshawasili nchini na tayari wameanza kufanya upasuaji ambao utachukuwa siku tano na wanatarajia kufanya upasuaji wa kuvuna mishipa ya damu mguuni na kuipandikiza katika mishipa ya moyo iliyoziba ( CABG-Coronary Artery Bypass Graft) na upasuaji wa milango miwili hadi mitatu ya moyo ambayo inamatatizo na inahitaji kubadilishwa kwa wagonjwa 15.
  Daktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Evarist Nyawawa (kushoto) kwa kushirikiana na mwenzake wa Hospitali ya Saifee ya nchini India Ali Oscar Behranwala wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa moyo . Katika ziara aliyoifanya nchini mwishoni mwa mwaka jana kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtakatifu Dkt. Syedna Aliqadr Mufaddal Saifuddin alimuahidi Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuleta madaktari wa Moyo nchini ambao watashirikiana na Madaktari wa JKCI kufanya upasuaji kwa wagonjwa. Timu ya wataalam hao ambao idadi yao ni sita imeshawasili nchini na tayari wameanza kufanya upasuaji ambao utachukuwa siku tano na wanatarajia kufanya upasuaji wa kuvuna mishipa ya damu mguuni na kuipandikiza katika mishipa ya moyo iliyoziba ( CABG-Coronary Artery Bypass Graft) na upasuaji wa milango miwili hadi mitatu ya moyo ambayo inamatatizo na inahitaji kubadilishwa kwa wagonjwa 15.
  Madaktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Saifee ya nchini India wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa milango ya moyo ambayo inamatatizo na kuweka milango mingine. Picha na Anna Nkinda – JKCI

  0 0
 • 03/27/17--07:45: NAY WA MITEGO AACHIWA HURU
 • Msanii wa Muziki wa kizazi kipya, Emmanuel Elibariki maarufu kama Nay wa Mitego, ambaye alikuwa amekamatwa na kushikiliwa na maafisa wa polisi nchini, kuhusiana na wimbo wake wenye jina la "Wapo", ameachiliwa huru mchana wa leo.

  Nay wa Mitego ameachiliwa huru kufuatia uamuzi wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe baada ya kupokea ushauri wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli. 

  Hata hivyo Waziri Mwakyembe alimtaka Nay wa Mitego auboreshe zaidi wimbo wake.

  Wimbo huo mpya wa Ney wa Mitego, ulianza kusambaa katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alikuwa amesema mwanamuziki huyo alikamatwa kwa kosa la kutoa wimbo wenye maneno ya kashfa dhidi ya serikali.

  0 0

  Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii

  Timu ya Tanzania "Taifa Stars" inatarajiwa kushuka tena kesho Machi 28 katika mchezo wa pili wa kirafiki unaotarajiwa kuanza majira ya saa 10:00 jioni kumenyana na timu ya taifa ya Burundi.

  Stars inaingia tena Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kucheza na Intamba Murugamba ya Burundi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa, kwa mujibu wa kalenda ya wiki ya mechi za kimataifa ya FIFA.

  Huu ni mchezo wa pili kwa Taifa Stars kucheza ndani ya wiki moja baada ya ule wa awali dhidi ya The Zebras ‘Pundamilia’ wa Botswana uliofanyika Uwanja huo wa Taifa, jijini Dar es Salaam Jumamosi iliyopita.

  Katika mchezo huo wa Jumamosi, Taifa Stars ambayo kwa sasa inanolewa na Salum Mayanga akisaidiwa na Patrick Mwangata ambao ni makocha wapya wa kikosi hicho, walishinda kwa mabao 2-0.

  Tayari Intamba Murugamba wametua nchini tangu jana Jumapili saa 4.30 asubuhi na kufikia Hoteli ya De Mag iliyoko, Kinondoni, Dar es Salaam na jioni yake walifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijini. Leo Jumatatu, inafanya mazoezi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

  Kwa upande wake, Mayanga alifurahishwa na ushindi wa Jumamosi iliyopita dhidi ya The Zebras ya Botswana na hivyo amehimiza Watanzania kujitokeza kwa wingi katika mchezo wa kesho.

  Katika kuunga mkono wito wa Kocha Mayanga, TFF imebakiza viingilio vya mchezo huo kuwa sawa na vile vya Jumamosi iliyopita kwani katika mzunguko ambao unachukua mashabiki wengi kiingilio kitakuwa ni Sh 3,000.

  Kwa upande wa VIP “A” Kiingilio kitakuwa ni Sh 15,000 wakati VIP “B” na VIP “C” kiingilio kitakuwa ni Sh 10,000. Viingilio hivyo vimelenga kuwaalika Watanzania wengine kwenda uwanjani.

  0 0

   Askari wawili wanaodaiwa kuiba mafuta ya ndege ya serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na raia wengine wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo kujibu tuhuma za kula njama na kuhujumu nchi.

  Mwendesha Mashtaka wakili wa serikali mwandamizi Nassoro Katuga akisaidiana na wakili Leornad Chalo waliwataja askari hao kuwa ni F. 8419 Koplo Bahati Nyerema Msilimani (33), mkazi wa Ukonga Kota za Airwing na F.9901 PC Benaus (34), anayeishi Ukonga Madafu.

  Wengine ni  Iddy Juma Nyangas (42), mlinzi wa Moko mkazi wa Vingunguti kwa Mnyamani na Ramadhani Bakari Mwinshehe (52), fundi wa ndege mkazi wa Yombo Buza.

  Mbele ya Hakimu Voctoria Nongwa imedaiwa kuwa, kati ya Machi 1 hadi 17 mwaka huu, katika uwanja wa ndege wa mwalimu Julius Nyerere washtakiwa wote kwa pamoja walikula njama ya kutenda kosa la kuhujumu.

  Iliendelea kudaiwa kuwa, siku na mahali hapo washtakiwa hao kwa ajali ya kuhujumu manufaa ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, bila kuwa na uhalali kisheria walitoboa ndege kukinga lita 280.6 kutoka kwenye ndege ya ATCL namba 5-HMWF-DASH 8 Q 300.

  Iliendelea kudaiwa kuwa kitendo hicho kilikuwa ni kuingilia utoaji wa huduma maalumu kwa jamii ya ndege.
  Watuhumiwa wa Uhujumu uchumi wa mafuta ya ndege ya serikali (ATCL) wakiwa kizimbani.

  Hata hivyo, washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mashtaka yao yako chini ya sheria ya uhujumu uchumi na DPP hajatoa kibali cha kuipa mamlaka Mahakama ya Kisutu Kusikiliza kesi hiyo.

  Hata hivyo, Mahakama imewaachia washtakiwa hao kwa dhamana kwa vila hakuna kibali cha DPP  kinachopinga dhamana na pia mahakama ya kisutu inayomamlaka ya kutoa dhamana kwa kesi isiyozidi shilingi milioni kumi na katika mashtaka yanayowakabili washtakiwa haionyeshi garama za mafuta washtakiwa wanazodaiwa kuhujumu.

  Kesi hiyo imeahirishwa hadi April 27,mwaka huu,.

  Wakili Katuga ameiarifu mahakama kuwa, upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na washtakiwa wako nje kwa dhamana ya wadhamini wawili kila mmoja walioweka dhamana ya shilingi milioni moja.

  Aidha mahakama imewataka washtakiwa kutosogelea maeneo yao ya kazi na vilevile kutyosafiri nje ya Dar esSalaam bila kibai cha mahakama.

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) kimesaini makubaliano ya Mradi wa East Africa and Investiment Hub kwa ajili ya uchocheaji wa uwekezaji nchini.

  Akizungumza wakati wa makubaliano hayo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TIC, Cliford Tandari amesema kuwa makubaliano hayo yatachochea uwekezaji pamoja na upatikanaji wa masoko nje ya nchi.

  Tandari amesema katika kufanya kazi ya mradi huo utasaidia Tanzania kupata wawekezaji kutokana na wigo uliopo katika mradi unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Watu wa Marekani (USAID).

  Aidha amesema mradi huo ni wa miaka mitano ambao TIC  inaingia katika makubaliano, tayari  miaka mitatu umefanya kazi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  Aliongeza kuwa mpaka kumalizika kwa mradi huo nchi itanufaika na kodi pamoja na kuongezeka kwa ajira kwa  vijana.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Cliford Tandari akizungumza na Mkurugenzi wa Mradi wa East Africa and Investiment Hub, Kanini Mutooni baada ya kusaini makubaliano ya mradi huo leo jijini Dar es Salaam.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TIC, Cliford Tandari akibadilishana hati na Mkurugenzi wa Mradi wa East Africa and Investiment Hub, Kanini Mutooni leo Jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya Watendaji wakuu wa Kituo cha Uwekezaji nchini, wakiwa katika mkutano huo.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TIC, Cliford Tandari akiwa katika picha ya pamoja na watu wanaotekeleza mradi East Africa and Investiment Hub pamoja na watendaji wa TIC leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massak,Globu ya jamii.

  0 0

  Na Lydia Churi- Mahakama, Tanga.

  Mahakama Kuu Kanda ya Tanga inakusudia kuwanunulia Mahakimu wake 67 kompyuta Mpakato (Laptops) ili kurahisisha kazi zao na kuondosha mashauri kwa wakati katika Mahakama mbambali za mkoa wa Tanga.

  Akizungumza kwa niaba ya Mtendaji wa Mahakama Kuu kanda ya Tanga, Afisa Utumishi wa Kanda hiyo, Bwana Farid Mnyamike amesema kompyuta hizo zitawasaidia waheshimiwa Mahakimu katika kuandika hukumu ili wananchi waweze kupati haki kwa wakati.
  Alisema katika kanda yake, baadhi ya Mahakama zina uhaba wa watumishi hasa Makatibu Muhtasi pamoja na vitendea kazi jambo ambalo limekuwa likichelewesha utolewaji wa hukumu pamoja na upatikanaji wa nakala za hukumu kwa wakati. Aliongeza kuwa kwa Mahakimu kupatiwa kompyuta hizo kutarahisisha upatikanaji wa haki.

  Aidha, Afisa Utumishi huyo alisema hivi sasa Mahakama Kuu kanda ya Tanga inao mpango wa kuhakikisha inazipatia umeme baadhi ya Mahakama za Mwanzo kupitia Mradi wa Umeme vijijini (REA) ili kurahisisha upatikanaji wa nakala za hukumu kwa wakati.

  Mahakama ya Tanzania ilimwekea malengo kila Hakimu nchini ya kuhakikisha  anasikiliza kesi zaidi ya 250 kwa mwaka  ili kuondosha mrundikano wa mashauri yaliyoko kwenye Mahakama mbalimbali nchini.

  Bwana Mnyamike aliitaja mipango mingine iliyowekwa na Kanda yake katika kuitekeleza nguzo ya pili ya Mpango Mkakati wa Miaka Mitano wa Mahakama ya Tanzania kuwa ni kuwapeleka Mahakimu wenye mashauri machache kwenye Mahakama zenye mashauri mengi ili kuhakikisha mashauri yote ya muda mrefu yanaondoshwa na yaliyofunguliwa yanamalizika kwa wakati. 

  Ili kuleta mabadiliko ndani ya Mahakama, Mahakama ya Tanzania iliandaa Mpango Mkakati wa Miaka mitano 2015-2020 unaotekelezwa kupitia nguzo tatu ambazo ni Utawala bora, Upatikanaji wa Haki kwa Wakati na pamoja na kurudisha na kujenga imani ya wananchi kwa Mahakama. 

  0 0  0 0

  Jana March 26,2017 ilikuwa siku muhimu kwa mwanahabari wa 102.5 Lake Fm Mwanza na mwanablogu wa BMG, George Binagi wa Tarime Mara pamoja na Miss Upendo Kisaka wa Moshi Kilimanjaro baada ya kuuaga ukapera.
  Wapendanao hao walifunga pingu za maisha katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza na baadaye hafla kufanyika Ukumbi wa Sun City Hotel, Ghana Green View Jijini Mwanza.
  "Ahsanteni nyote mliotusaidia kutimiza ndoto yetu kubwa katika maishani yetu. Familia yangu, ndugu, jamaa na marafiki zangu. Waumini wote wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza chini ya Mchungaji Daniel Kulola na kila mmoja kwa nafasi yake, Mungu awabariki. 
  Mmenionesha upendo wa ajabu mno.
  Wazazi wangu hususani mama mpendwa, nimetimiza deni mliloniachia duniani. Hakika sasa mtapumzika kwa amani, pahali pema, peponi, Amina. Ndoa na iheshimiwe na watu wote. Mungu atuongoze vyema". Mr & Mrs George Binagi.
  Shukurani za pekee pia ziwaendelee best man na Best Lady, Mr and Mrs. Joel Maduka kutoka Storm FM Geita na Maduka Online kwa kufanikisha shughuli hiyo kwenda vyema.
  BMG inakusihi uendelee kutazama picha za awali za shughuli hiyo wakati wataalamu wetu wakiendelea kukuandalia picha nyingine ikiwemo picha za kanisani. BOFYA HAPA

  0 0

   Zao la korosho nchini lipo hatarini kuporomoka kufuatia kugundulika kwa ugonjwa mpya wa mnyauko wa mikorosho ambao umeua mikorosho zaidi ya elfu 40 hadi sasa katika mikoa ya LINDI na MTWARA. Fungua video kupata taarifa kamili

older | 1 | .... | 1626 | 1627 | (Page 1628) | 1629 | 1630 | .... | 3278 | newer