Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1625 | 1626 | (Page 1627) | 1628 | 1629 | .... | 3285 | newer

  0 0


  Wachimbaji wa mchanga unaodhaniwa kuwa na madini ya almasi ‘Wabeshi’ wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wameiomba serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Pombe Magufuli iwatengee eneo maalum kwa ajili ya uchimbaji ili waache vitendo vya kuvamia mgodi wa almasi wa Williamson (Williamson Diamonds Ltd).


  Wachimbaji hao wa madini ambao wamekuwa wakivamia mgodi na kuambulia kupigwa,kunyanyaswa na hata kuuawa na walinzi wa mgodi huo,walisema yapo maeneo ambayo hayatumiki hivyo ni vyema serikali ikawakatia maeneo ili iwe suluhu ya mgogoro kati yao na uongozi wa mgodi.

  Wakizunguza na waandishi wa habari hivi karibuni kwa nyakati tofauti Wabeshi walisema wananchi wanaozunguka mgodi huo wamekuwa hawanufaiki nao kabla na baada ya uhuru hivyo wanaamini serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais Magufuli itatatua kero yao ya muda mrefu.

  Walisema vijana wengi wanategemea shughuli ya uchimbaji hivyo wakipewa eneo la uchimbaji wataweza kumudu gharama za maisha ikiwemo kutunza familia zao.

  Mmoja wa wabeshi hao Mabula Njile mkazi wa kijiji cha Nyenze kata ya Mwadui Luhumbo alisema endapo serikali itawapatia maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo hawatavamia tena mgodi wa Williamson kwenda kuchimba mchanga unaodhaniwa kuwa na madini ya almasi.

  Mkazi wa kijiji cha Nyenze kata ya Mwadui Lohumbo akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea kijiji hicho .


  0 0

   Timu ya Tanzania "Taifa Stars" imefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Timu ya Botswana katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika leo Jijini Dar es salaam.

  Mchezo huo uliochezwa leo kwenye dimba la Uwanja wa Taifa ilifanikiwa kutoka na ushindi huo baafa ya Mshambuliaji wa Kimataifa anayecheza soka la kulipwa nchini Ubelgiji Mbwana Samata kufunga magoli yote.

  Dakika ya pili ya kipindi cha Kwanza Samata aliweza kuipatia Stars goli la kuongoza lililodumu mpaka mapumziko huku kila timu ikionekana kutafuta goli kwa udi na uvumba.

  Kipindi cha pili kinaanza ambapo Botswana wanafanya mabadiliko lakini wanshindwa kutumia nafasi walizozipata.

  Katika dakika ya 87, Mbwana Samata anaiandikia Stars goli la 2 kwa faulo ya nje ya 18 akiupiga mpira huo moja kwa moja ambapo mpala dakika 90 zinamalizika Stars 2-0 Botswana.

   Stars wanatarajiwa kucheza tena Jumanne dhidi ya Burundi ikiwa ni muendelezo wa mechi za kirafiki za kimataifa.
   Kiungo wa Timu ya Taifa Stars, Himid Mao akiruka juu sambmba na Beki wa Botswana kuwania mpira wa juu, katika Mchezo wa kirafiki wa rekodi za FIFA, uliochezwa jionu ya leo katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam leo. Taifa Stars imeshinda bao 2-0.
   Beki wa kati wa Botswana , Mosha Galemonthale akimchezea vibaya Mbwana Sammata.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakwembe akisalimiana na Nahodha wa Timu ya Taifa "Taifa Stars", Mbwana Ally Samatta  kabla ya kuanza kwa mchezo dhidi ya Timu ya Taifa ya Botswana, katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam leo.


  0 0
 • 03/25/17--14:11: GLOBAL TV MUBASHARA


 • 0 0


  0 0

  Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imeushauri uongozi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) kuelekeza nguvu ya uwekezji katika mji wa Dodoma ili kuziba kukidhi ongezeko la huduma za kumbi za kufanyia muikutano linalosababishwa na serikali kuhamia katika mji huo.

  Akizungumza katika kikao cha majumuisho baada ya Kamati ya PIC kutembelea AICC mwishoni mwa wiki na kukagua miradi miwili, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Albert Obama ameshauri AICC kuupa kipaumbele mkoa wa Dodoma katika mkakati wa kujenga kituo kingine cha kisasa cha Mikutano.

  “Tunahitaji kuiona taasisi hii ikipanuka na kujenga vituo vingine vya mikutano huko mikoani na moja ya mikoa ambayo tungependa muipe kipaumbele ni Dodoma maana huko ndio serikali inahamia na mahitaji ya huduma ya kumbi za mikutano yanakwenda kuongezeka”, alisisitiza Obama.

  Nae Mjumbe wa Kamati hiyo, Amina Mollel alieleza kufurahishwa na juhudi za uongozi wa AICC kumilisha ujenzi wa mradi wa nyumba za kisasa (apartment) 48 ambapo azote zina wapangaji na kuwa sehemu muhimu ya kuongeza mapato ya shirika.
  Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma wakiwa katika mradi wa nyumba za kisasa za kupangisha za AICC ambapo mradi huu umekamilika na tayari nyumba hizo zimeisha pata wapangaji. 

  Mkurugenzi wa Miliki na Miradi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), Victor Kamagenge (kushoto) akitoa maelezo kwa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji Mitaji ya Umma, juu ya ujenzi wa ukumbi wa kisasa wa maonesho. Kamati hiyo ilitembelea AICC mwishoni mwa wiki kukagua miradi miwili ya ujenzi wa ukumbi wa maonesho ambapo ujenzi wa unaendelea na mradi mwingine wa nyumba za kisasa 48 ambao tayari umekamilika.  0 0
  0 0

  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini Tanzania  Jenerali Venance Mabeyo akizungumza na wanahabari kuhusu Jeshi hilo kuanza kulipa deni wanalodaiwa na Shirika la Umeme nchini TANESCO kuanzia kesho. Mkutano huo umefanyika katika Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi Ngome jijini Dar es Salaam  leo Machi 26, 2017.

  0 0

  Kamati ya kudumu ya bunge Utawala na Serikali za Mitaa imetembelea mkoani Njombe na kukagua baadhi ya miradi inayotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF,TAMISEMI, Mfuko wa Rais wa Kujitegemea na MKURABITA na kuridhishwa na mchango wa taasisi hizo katika kupiga vita umasikini kwa kuwawezesha wananchi kiuchumi.
  Wakiwa mkoani humo,wajumbe wa Kamati hiyo walikutana na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaotekelezwa na TASAF ambapo licha ya kuvutiwa na hatua ya kujiongezea kipato kutokana na ruzuku kwa kuanzisha miradi midogo midogo, lakini pia walipongeza mafanikio makubwa yaliyopatikana katika sekta za elimu, afya na lishe katika kaya za walengwa hao.
  Aidha wajumbe wa kamati hiyo ambao waliongozana na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki pia wamepongeza hatua ya TASAF ya kupunguza tatizo la makazi ya walimu kwa kujenga nyumba katika kijiji cha Uwemba nje kidogo ya mji wa Njombe.
  Akizungumza katika ziara hiyo, Mhe.Kairuki amesema serikali itaendelea kuweka mkazo katika miradi inayolenga kuwapunguzia wananchi adha ya umasikini hivyo akataka wananchi kuitumia fursa hiyo vizuri ili waweze kuboresha maisha yao.Waziri huyo alionyesha kuridhika na baadhi ya wananchi mkoani Njombe kwa kutumia fursa zilizowekwa na serikali kuendesha shughuli za kiuchumi kikiwemo kilimo,ufugaji ,biashara na uanzishaji wa vikundi vya kuweka akiba.

   Wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali Mitaa wakipata maelezo ya mradi wa ujenzi wa nyumba ya Walimu katika kijiji cha Ulembwe inayojengwa TASAF ikiwa ni jitihada za serikali za kutatua tatizo la makazi kwa walimu.

   Wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya utawala na serikali za mitaa wakipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wananchi walionufaika na fedha kutoka mfuko wa Rais wa kujitegemea katika mji wa Makambako mkoani Njombe ambaye anaendesha kilimo cha viazi mviringo.

   Waziri Kairuki na Wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Utawala bora na Serikali za Mitaa wakiangalia bidhaa za ususi zinazofanywa na baadi ya wanawake kupitia kikundi chao kilichowezeshwa na Mfuko wa Rais wa Kujitegemea mjini Njombe.

   Baadhi ya Wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya utawala na serikali za mitaa wakipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wanufaika wa Mfuko wa Rais wa kujitegemea mkoani Njombe aliyetumia fedha alizokopeshwa na mfuko huo kuanzisha mradi wa kufuga n’gombe. 

  Waziri Angellah Kairuki watatu kutoka kushoto mstari wa mbele akiwa na Mhe.Magreth Sitta na Mhe.Ruth Mollel ambao ni wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge wa utawala na serikali za mitaa wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Walengwa wa TASAF katika kijiji cha Ulembwe nje kidogo ya mji wa Njombe.

  0 0  0 0


  0 0

  Kuna ukomo wa nafasi. Jiandikishe sasa kupitia ukurasa huu, kwa kuchagua hapo chini kulia ' Going' au hata ' Maybe' kama huna hakika... Bofya https://www.facebook.com/events/250673922060000/ 

  0 0

   Mkurugenzi Miradi wa Kamuni ya Kimataifa ya Uhandisi wa Miundombinu ya Ujenzi ya Garware ya Nchini India  Bwana Deepak Menghnani kati kati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika Hoteli ya Kimataifa ya Eros Mjini New Delhi India. Kulia ni Balozi Seif na wa kwanza kutoka Kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya wadhamini ya Kampuni ya Garware Bwana Jatindery V. Sehgal.
   Mkurugenzi wa Miradi wa Kampuni ya Garware Bwana Deepak Mnghnani Kushoto akifafanua jambo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyekaa kati kati na wa kwanza kulia ni Mjumbe wa Bodi ya wadhamini ya Kampuni ya Gaware Bwana Jatindery V. Sehgal.
   Balozi Seif Ali Iddi wa Pili kutoka Kulia akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Kampuni ya Garware mara baada ya kumaliza mazungumzo yao katika Hoteli ya Kimataifa ya Eros Mjini New Delhi India. Wa kwanza kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Miradi wa Kampuni ya Garware Bwana Deepak Mnghnani na kulia ya Balozi Seif ni Mjumbe wa Bodi ya wadhamini ya Kampuni ya Gaware Bwana Jatindery V. Sehgal pamoja na Kaimu Balozi wa Tanzania Nchini India Balozi Mohamed Hija Mohamed. Picha na OMPR  Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

  Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani Ulaya The Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni yenye makao yake nchini Ujerumani imemtakia kila la heri balozi wa Tanzania nchini ujerumani anayemaliza muda wake Mhe. Philip Marmo.

   "Tunamtakia kila la heri mheshimiwa Bw.Philip Marmo amekaa na sisi na kutuwakilisha hapa ujerumani si haba" alisema kiongozi wa bendi hiyo mwanamuziki nguli Kamanda Ras Makunja.
  Pia alitumia muda huo huo kwa kusema "karibu Ujerumani balozi  Dkt.Abdallah Possi" 
  Kamanda Ras Makunja alisema kwa kuwa sera ya serikali ya awamu ya tano ni ya Tanzania ya kujenga uchumi wa viwanda,ni wakati muafaka kwa balozi zetu kuwashirikisha wasanii katika kutangaza soko la Tanzania kimataifa kuvutia wawekezaji na watalii. 
  Ngoma Africa band imeitangaza Tanzania zaidi ya miaka ishirini kimataifa na milango ipo wazi kama balozi zitazishirikisha bendi hiyo "tunajua wapi pa kuitangaza na walipo wawekezaji wenye upendo na Tanzania alisema Kamanda Ras Makunja. wasikilize at www.ngoma-africa.com

  0 0


  Afisa Mahusiano na habari kutoka chama cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS) Josephat Torner akitoa elimu kuhusu masuala ya ualbino katika kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria
  Kushoto ni Mkurugenzi wa wanawake,Watoto na Diakonia katika kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Martha Ernest Ambarang'u akiwatambulisha viongozi kutoka TAS.Wa pili kutoka kushoto ni Afisa Programu kutoka TAS Severin Edward ,akifuatiwa Happiness Ngaweje na afisa mahusiano na habari (TAS)Josephat Torner.Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA
  0 0

  Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Msalala Simon Berege akimwongoza Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya siku ya Kifua kikuu duniani mkoa wa Shinyanga kwenda kukagua mabanda yaliyokuwa yanatoa huduma za kupima VVU,uchunguzi wa kifua kikuu,tohara na huduma zingine za afya sambamba na zoezi la kuandikisha watoto ili wapate vyeti vya kuzaliwa
  Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu (mwenye suti nyeusi) na Meneja wa AGPAHI kanda ya ziwa Dkt. Nkingwa Mabelele(kulia) wakisikiliza maelezo ya wataalamu wa afya katika banda la kupimia VVU
  Ndani ya banda la uchunguzi wa ugonjwa wa kifua kikuu-Wataalamu wa afya wakitoa maelezo kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu 
  Zoezi la tohara kwa wanaume linaendelea-Katikati ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akiwa katika banda la kutolea huduma ya tohara kwa wanaume bure. Kwa Taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0  0 0


  1 Arusha - Elias Mpanda
  2 Dar - Saad Kusilawe
  3 Dodoma - Jamila Yusuf
  4 Geita - Adam Ngalawa
  5 Iringa - Christopher Magala
  6. Kagera- Rahel Degeleke
  7. Katavi- Kajoro Vyahoroka
  8. Kigoma- Naomi Kapambala
  9. Kilimanjaro- Jonathan Mabihya
  10. Lindi-Mwanamasoud Pazi
  11. Manyara -Paza Mwamlima
  12. Mara -Innocent Nanzabar
  13. Mbeya -Wilson Nkhambaku
  14. Morogoro- Kulwa Milonge
  15. Mtwara -Zacharia Mwansasu
  16. Mwanza- Raymond Mwangala
  17. Njombe- Hossea Mpagike
  18. Pwani- Anastanzia Amasi
  19. Rukwa- Loth Ole Nesere
  20. Ruvuma- Amina Imbo
  21. Shinyanga -Haula Kachambwa
  22. Simiyu- Donald Etamya
  23. Singida- Jimson Mhagama
  24. Tabora- Janeth Kayanda
  25. Tanga- Allan Kingazi.

  0 0

   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Mhe. Seleman Mzee, wakati alipokuwa anawasili wilayani humo, Mkoa wa Mtwara kwa ajili ya ziara ya kikazi.  
   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akiongozwa na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mtwara (RPO), Ismail Mlawa (kulia), kuingia Gereza la Kilimo na Mifugo Lamajani lililopo wilayani Masasi kwa ajili ya ukaguzi wa Gereza hilo ambalo lina wafungwa ambao wanafanya shughuli za kilimo na ufugaji. 
   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mtwara (RPO), Ismail Mlawa, alipokuwa anamfafanulia jambo mara baada ya kutoka ndani ya Gereza la Kilimo na Mifugo Lamajani lililopo wilayani Masasi kwa ajili ya ukaguzi wa Gereza hilo ambalo lina wafungwa ambao wanafanya shughuli za kilimo na ufugaji. 
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiiangalia moja ya nyumba za askari magereza zilizopo jirani na Gereza la Kilimo na Mifugo Lamajani wilayani Masasi, Mkoa wa Mtwara. Katikati ni Mkuu wa Magereza Mkoa huo (RPO), Ismail Mlawa. Kushoto ni Ahmed Bakari, Kaimu Mkuu wa Gereza hilo. Masauni alimaliza ziara yake ya mikoa ya kusini kwa kutembelea Gereza hilo. 
  Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


  0 0

  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe. Jaji (R) Semistocles Kaijage amewataka watumishi wa tume hiyo wazingatie maadili na kanuni za utawala bora ili kutekeleza kwa ufanisi jukumu la Tume katika kukuza na kuimarisha demkorasi na utawala bora nchini.

  Jaji Kaijage ameyasema hayo alipoalikwa kuwa mgeni rasmi kufungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Tume kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima jijini Dar es Salaam.

  “Jukumu kubwa la Tume ni kukuza na kuimarisha demkorasi na utawala bora nchini, kwa maana hiyo ni muhimu kwamba watumishi wa Tume wazingatie maadili na kanuni za utawala bora ili kutekeleza kwa ufanisi jukumu hili” alisema na kuongeza kuwa:

  “Ni muhimu kwa watumishi wa Tume katika utendaji kazi wao kuepuka vitendo vya ukiukwaji wa maadili kama vile rushwa, upendeleo na au ubaguzi wa aina yoyote katika sehemu ya kazi”

  Mbali na hayo, Mhe. Jaji Kaijage aliipongeza Tume kufanikisha uchaguzi mdogo uliofanyika mwezi Januari mwaka huu katika jimbo la Dimani na kata 20 za Tanzania Bara kwa kuufanya kuwa wa amani na utulivu pamoja na changamoto mbalimbali zilizoukabili uchaguzi huo.

  Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi  wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ambaye ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani akimkaribisha Mgeni Rasmi wa Ufunguzi wa Kikao cha baraza hilo ambaye ni Mwenyekiti wa NEC Mhe. Jaji (R) Semistocles Kaijage baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima jijini Dar es Salaam ambako kikao hicho kilifanyika.Kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) Taifa Bw. Heri Mkunda.
   Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani (aliyesimama) akitoa neno la ukaribisho kwa Mgeni Rasmi wa ufunguzi wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Tume hiyo Mhe. Jaji (R) Semistocles Kaijage (kulia kwake) kabla ya kufungua kikao hicho.Kulia ni Katibu Mkuu wa (Tughe) Taifa Bw. Heri Mkunda na kushoto ni Katibu wa Baraza hilo Bi. Rose Malo. 
  Mgeni Rasmi Mhe. Jaji (R) Semistocles Kaijage akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume (hawapo pichani) kabla ya kufungua kikao hicho kwenye ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima jijini Dar es Salaam.Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Baraza Bw. Kailima Ramadhani, Katibu Mkuu wa Tughe Taifa Heri Mkunda na kulia kwake ni Katibu wa Baraza hilo Bi. Rose Malo na Naibu Katibu Bi. Uddy Sadick. 

  Katibu Mkuu wa Tughe Taifa        Bw. Heri Mkunda (kulia) akitoa neno la shukrani kwa Mgeni Rasmi wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe. Jaji (R) Semistocles Kaijage (kushoto).Katikati ni Mwenyekiti wa baraza hilo Bw. Kailima Ramadhani 
   
   Katibu wa Baraza la Wafanyakazi  wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  Bi. Rose Malo akiwasilisha muhtasari wa kikao kilichopita cha baraza hilo huku Mwenyekiti wa Baraza Bw. Kailima Ramadhani (katikati) na Naibu Katibu Msaidizi Bi Uddy Sadiki wakifuatilia muhtasari wa kikao hicho.
  Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 1625 | 1626 | (Page 1627) | 1628 | 1629 | .... | 3285 | newer