Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

UZINDUZI WA MICHUANO YA MPIRA WA MIGUU YA MAJIMBO YA CCM ZANZIBAR

$
0
0
 Vijana wa CCM Family wakipita kwa  maandamano wakati wa  Uzinduzi wa Mashindano ya michuano ya Majimbo ya CCM Mpira wa Miguu katika uwanja wa Amaan leo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwnyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohanmed Shein
 Vijana wa CCM Jimbo la Jang'ombe wakipita kwa  maandamano wakati wa  Uzinduzi wa Mashindano ya michuano ya Majimbo ya CCM Mpira wa Miguu katika uwanja wa Amaan leo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwnyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohanmed Shein
 Vijana wa CCM Afisi Kuu Kisiwandui wakipita kwa  maandamano wakati wa  Uzinduzi wa Mashindano ya michuano ya Majimbo ya CCM Mpira wa Miguu katika uwanja wa Amaan leo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwnyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohanmed Shein
 Rais wa Zanzibar na Mwnyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohanmed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake ya Uzinduzi wa Mashindano ya michuano ya Majimbo ya CCM Mpira wa Miguu katika uwanja wa Amaan leo
Baadhi ya wanakamati ya maandalizi ya michuano ya Majimbo ya CCM Mpira wa Miguu katika uwanja wa Amaan uliofanyika leo wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwnyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohanmed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake ya Uzinduzi wa michuano hiyo. Picha na Ikulu.

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 24.03.2017

HAFLA YA KUAPISHWA MAWAZIRI, MABALOZI, KATIBU MKUU NA KAMISHNA IKULU DAR ES SALAAM

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi Dkt. Harrison Mwakyembe baada ya kumuapisha kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo  Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017.
Profesa Palamagamba kabudi akila kiapo mbele ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ,kuwa Waziri wa Sheria na Katiba Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017
  Waapishw wakila kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Umma Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017. Kutoka kushoto ni Mhe Jaji Stella Esther Mugasha ambaye ameapishwa kuwa kamishna wa Tume ya Mahakama, Mhe  Sylvester Mabumba (Balozi wa Tanzania nchini Oman), Mhe Job Masima (Balozi wa Tanzania nchini Israel), Mhe. Dkt Abdallah Possi (Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani), Mhe Profesa palamagamba Kabudi (Waziri wa sheria na katiba) na Dkt Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea machache  baada ya kuhitimisha hafla ya kuwaapisha mawaziri, mabalozi na Kamishna Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza Dkt. Harrison Mwakyembe baada ya kumuapisha kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, huku Waziri mpya wa Sheria na katiba Profesa palamagamba kabudi akiwa pembeni baada ya kuhitimisha hafla ya kuwaapisha mawaziri, mabalozi na Kamishna Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na  waapishwa baada ya kuhitimisha hafla ya kuwaapisha mawaziri, mabalozi na Kamishna Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017. Waapieshwa hao ni Mhe Jaji Stella Esther Mugasha ambaye ameapishwa kuwa kamishna wa Tume ya Mahakama, Mhe Sylvester Mabumba (Balozi wa Tanzania nchini Oman), Mhe Job Masima (Balozi wa Tanzania nchini Israel), Mhe. Dkt Abdallah Possi (Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani), Mhe Profesa palamagamba Kabudi (Waziri wa sheria na katiba) na Dkt Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wanahabari wa vyombo mbalimbali baada ya kuhitimisha hafla ya kuwaapisha mawaziri, mabalozi na Kamishna Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wanahabari wa vyombo mbalimbali baada ya kuhitimisha hafla ya kuwaapisha mawaziri, Katibu Mkuu, mabalozi na Kamishna Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

TANZANIA YAHUDHURIA MKUTANO WA 18 WA MWAKA WA BENKI YA DUNIA WA MASUALA YA ARDHI NA UMASIKINI

$
0
0
Na Mboza Lwandiko, Wshington DC
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Imeshiriki Mkutano wa mwaka wa 18 wa Benki ya Dunia unaohusu masuala ya Ardhi na Umaskini, Machi 20 – 24, 2017 – Washington DC – Marekani.

Mkutano huo unaobeba ujumbe; “Utawala bora wa Ardhi”, umejumuisha zaidi ya wajumbe 1,200 kutoka nchi wanachama, zilizohusisha Serikali, taaluma, jamii na Sekta binafsi mbalimbali.

Pamoja na mambo mengine; Mkutano huo umejikita zaidi katika Maboresho mbalimbali yanayoendelea kufanyika katika Sekta ya Ardhi Duniani, ikiwa ni pamoja na kuzingatia nafasi ya takwimu na shuhuda zinazoashiria maboresho katika Sera za Ardhi, na kuainisha Mikakati ya Maendeleo katika kuboresha zaidi Sekta ya Ardhi.

Aidha, Mada ambayo imewasilishwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imewasilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara; Dkt. Yamungu Kayandabila, ambayo ilibeba ujumbe -  “Ardhi; Ufunguo wa Utawala Bora na Maendeleo ya Uchumi kwa Tanzania”. Alieleza kuwa utawala wa Ardhi Tanzania unazingatia; Sheria, Uwazi, Uwajibikaji na Ushirikishwaji wa Wananchi. Pamoja na mengine Dkt. Kayandabila alieleza jitihada mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanyika kuboresha sekta ya ardhi nchini na juhudi ambazo zinaendelea kuboresha utawala bora wa Ardhi nchini. 

 Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dkt. Yamungu Kayandabila akiwasilisha mada: “Ardhi; Ufunguo wa Utawala Bora na Maendeleo ya Uchumi kwa Tanzania”. Katika Mkutano wa 18 wa Benki ya Dunia wa masuala ya Ardhi na Umaskini; Washington DC, Marekani.

 Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dkt. Yamungu Kayandabila, akiwa ameambatana na Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Mipango Miji na Vijiji; Immaculate Senje, Kaimu Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya ; Amina Rashidi, wakijadili jambo na wajumbe wenzao wa Mkutano wa 18 wa Benki ya Dunia wa masuala ya  Ardhi na Umaskini; Washington DC, Marekani 

 Wajumbe kutoka Tanzania katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Finland kwenye mkutano wa 18 wa Benki ya Dunia kuhusu masuala ya Ardhi na Umaskini uliofanyika mjini Washington DC, Marekani

 Wajumbe kutoka Tanzania wakifanya mazungumzo ya pamoja na mtaalamu mwelekezi wa Benki ya Dunia kutoka nchini Uganda; Bwn. Moses Kibirige (aliyevaa miwani) kwenye mkutano wa 18 wa Benki ya Dunia kuhusu masuala ya Ardhi na Umaskini uliofanyika mjini Washington DC, Marekani

Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dkt. Yamungu Kayandabila, akiwa na wajumbe wengine kutoka nchi mbalimbali katika vikao vinavyoendelea katika Mkutano wa 18 wa Benki ya Dunia kuhusu masuala ya Ardhi na Umaskini uliofanyika mjini Washington DC, Marekani. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

GLOBAL TV LIVE: Event ya Malkia wa Nguvu, Ukumbi wa High Spirit Dar es salaam

Waziri Mwakyembe Apokelewa na Wafanyakazi Wa Wizara Yake

$
0
0
PLO
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akipokelewa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Annastazia James Wambura katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO mala baada ya kutoka kula kiapo leo Jijini Dar es Salaam.
PLO 1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea shada la maua kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Wizara hiyo Bi. Flora Mwnyenyembegu wakati wa mapokezi ya Waziri huyo yaliyofanyika katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Annastazia James Wambura(wapili kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel.
PLO 2
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Nuru Khalfan Milao wakati wa mapokezi ya Waziri huyo yaliyofanyika katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam.
PLO 3
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari – MAELEZO Bibi. Zamaradi Kawawa wakati wa mapokezi ya Waziri huyo yaliyofanyika katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam.
PLO 4
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo  Yusuph Omary wakati wa mapokezi ya Waziri huyo yaliyofanyika katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam.
PLO 5
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa OElisante Ole Gabriel akimtambulisha Kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo (kushoto) wakati wa mapokezi ya Waziri huyo yaliyofanyika katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam.
PLO 6
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiweka saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kupokelewa na watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Taasisi zake mapokezi yaliyofanyika katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Annastazia James Wambura.
Picha zote na Frank Shija – MAELEZO.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MACHI 25,2017

WAZIRI MAKAMBA:RASIRILIMALI ZA NCHI ZITUNZWE KWA FAIDA YA SASA NA VIZAZI VIJAVYO

$
0
0
Akizungumza katika katika ziara yake mkoani Tanga iliyoingia siku ya tano Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. January Makamba amesema kuwa ni vema rasilimali za nchi hii zitunzwe kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo.”hatuwezi kufanikiwa kama tutaharibu mazingira” Makamba alisisitiza.

Waziri Makamba amesema ofisi yake ya imedhamiria kuchukua swala la mazingira kwa uzito wa kipee ikiwa ni pamoja na kuweka hifadhi ya mazingira katika mipango ya maendeleo.” Uwekezaji wote lazima uende sambamba na hifadhi ya mazingira”

Aidha, uongozi wa Halmashauri ya Mji Korogwe imetakiwa kuwachukua hatua kali wananchi wote wanaofanya shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji, kwa kutumia sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 na ile ya maji ya mwaka 2009. Waziri Makamba amesema kuwa ofisi yake iko katika hatua za mwisho za kuteua wakaguzi wa mazingira 200 ambao watapata mafunzo na kusambazwa katika Halmashauri mbali mbali nchini.

Pia Waziri Makamba amesema kuwa katika kikao kijacho cha Bunge Ofisi ya Makamu wa Rais itatoa waraka juu ya usimamizi na uchimbaji wa mchanga nchini pamoja na umiliki wa “Chain-saw” kwa lengo kuweka utaratibu utakaowezesha kutambua na kutoa vibali maalumu kwa shughuli hizo ili kulinda mazingira.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. January Makamba ameendelea na ziara yake maalumu ya kukagua shughuli mbalimbali za kimazingira nchini na hii leo amepokea taarifa ya hali ya mazingira katika Halmashauri ya Mji Korogwe na Same.

Awali akimkaribisha Waziri Makamba, Mwenyekiti wa Halmashauri ya hiyo Bw. Hillary Ngonyani amesema kuwa katika kutekeleza sheria ya mazingira zoezi la uzoaji na utupaji wa taka ngumu na taka maji umewekewa mkakati maalumu na kutekelezwa kikamilifu pia usafi wa mazingira umefanyika kwa kufanya ukaguzi wa nyumba hadi nyumba na kutoza faini kwa wananchi wasio na vyoo.

Bw. Ngonyani amebainisha kuwa wananchi wanaokiuka taratibu hizo hushtakiwa kwenye mabaraza ya kata na kupewa muda maalumu wa kujenga vyoo, kusisitizwa kuvitumia pia kuamriwa kusafisha mazingira yao chini ya uangalizi wa maafisa afya.

Aidha Bw. Ngonyani amesema kuwa wananchi wamekumbusha pia kutofanya shughuli za maendeleo kando ya mito na vyanzo vya maji ili kupunguza athari kwa mazingira, na kuunda kwa kamati za mazingira.

Katika hatua nyingine Bw. Ngonyani ameinisha changamoto zinazojitokeza katika Halmashauri ya Korogwe mji kuwa ni pamoja na Ukosefu wa wakaguzi wa Mazingira na athari za mabadiliko ya tabianchi yanayosababisha vipindi vya mvua kubadilika na kuongezeka kwa joto.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiandaa mti kwa ajili ya kuupanda ikiwa ni jitihada za kuunga mkono kampeni ya upandaji miti nchini. Zoezi hilo limefanyika leo katika Halmashauri ya mji Korogwe.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiongea na wawakilishi wa wananchi, watumishi na Watendaji wa Halmashauri ya Mji Korogwe (hawapo pichani). Waziri Makamba amesisitiza umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji na hifadhi ya mazingira kwa ujumla wake.
Sehemu ya wawakilishi wa wananchi, watumishi na Watendaji wa Halmashauri ya Mji Korogwe wakimsikiliza Waziri Makamba alipofanya ziara ya kikazi kutembelea Halmashauri hiyo, kusikiliza na kujionea changamoto za kimazingira na kuainisha namna bora ya kukabiliana nazo.

MASAUNI AWATAKA WANANCHI WAISHIO MPAKANI MWA TANZANIA NA MSUMBIJI KUFUATA SHERIA ZA UHAMIAJI, ATEMBELEA KIWANDACHA KUCHAKATA GESI ASILIA MADIMBA

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kushoto) akimsikiliza Meneja wa Kiwanda cha Kuchakata Gesi Asilia Madimba wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), mkoani Mtwara, Mhandisi Sultan Pwaga, wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara kiwandani hapo kuangalia jinsi gesi inavyozalishwa. Hata hivyo, Masauni alitoa ahadi, Jeshi lake litafanya taratibu kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda (katikati) pamoja na TPDC kufanikisha uwepo wa Kituo cha Polisi kama walivyoomba uongozi wa Kiwanda hicho kwa ajili ya kuimarisha ulinzi kiwandani hapo pamoja na wananchi waishio jirani na kiwanda hicho. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia) akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Kilambo kilichopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji. Masauni aliwataka wananchi hao kudumisha amani mpakani hapo pamoja na kufuata sheria za uhamiaji za nchini pamoja na za Uhamiaji Msumbiji endapo watahitaji kuvuka mpaka huo. Masauni baada ya kukagua mpaka huo aliwataka maafisa wakekuimairisha ulinzi zaidi mpakani hapo. Wapili kulia ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mtwara, Rose Mhagama.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(katikati) akiiangalia moja ya nyumba za askari wa Jeshi la Magereza ambazo zinahitaji marekebisho katika Gereza Lilungu mkoani Mtwara. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa huo, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi hilo mkoani humo, Ismail Mlawa.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wapili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kuhitimisha ziara yake kukagua mpaka wa Tanzania na Msumbiji uliopo katika Kijiji cha Kilambo, mkoani Mtwara. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda. Wapili kulia ni Afisa Uhamiaji mkoa huo, Rose Mhagama, na Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoa huo, Neema Mwanga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akiwapa maelekezo maafisa wake wakati alipokuwa Mto Ruvuma, Kijiji cha Kilambo kilichopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji, mkoani Mtwara.Wapili kushoto ni Afisa Uhamiaji mkoa huo, Rose Mhagama, na anayefuata ni Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoa huo, Neema Mwanga.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akikaribishwa na Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Mtwara, Ismail Mlawa kwa ajili ya kwenda kukagua nyumba za askari Magereza wa Gereza Lilungumkoani humo ambazo zinahitaji marekebisho kutokana na kuharibika. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

DKT KEBWE AONGOZA KIKAO CHA MAANDALIZI YA MAONESHO YA KILIMO

$
0
0

Na Mathias Canal, Morogoro

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen Kebwe ameongoza kikao cha Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) Kanda ya Mashariki inayounganisha Mikoa ya Dar es salaam, Tanga, Pwani na Morogoro.

Kikao hicho kilichokuwa na Agenda sita kimefanyika Katika Ukumbi wa JKT Nane Nane Manispaa ya Morogoro ambapo kwa kauli moja kimepitisha Agenda zote sita ikiwemo kupitia Taarifa ya Tathmini ya Maonesho ya Nane Nane 2016 sawia na Taarifa ya Maandalizi ya Maonesho ya Nane Nane ya mwaka 2017 ambayo Kitaifa yanayotaraji kufanyika Mkoani Morogoro.

Akizungumza wakati Akifungua kikao hicho Dkt Kebwe ameitaka kamati inayoratibu shughuli hizo ya TASO kuweka wazi mapato na matumizi ya fedha wanazozipata kwani kufanya hivyo ni kujenga zaidi uaminifu kwa wananchi na kujihuisha kwa pamoja na wadau mbalimbali ili kukuza uchumi nchini kupitia Kilimo.

Dkt Kebwe alisema kuwa TASO kutofanya hivyo ni njia mojawapo ya kuzifanya Halmashauri zingine kutochangia kwa kuhofia fedha zao kutumika pasina weledi uliokusudiwa.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen Kebwe akizungumza wakati wa kikao cha Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) Kanda ya Mashariki
Baadhi ya washiriki wa kikao cha Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) Kanda ya Mashariki wakifatilia kikao hicho kwa makini
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisikiliza kwa makini wakati wa kikao cha Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) Kanda ya Masharikikilichofanyika Mkoani Morogoro
Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe Godwin Gondwe akifatilia kwa makini kikao cha Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) Kanda ya Mashariki kilichofanyika Mkoani Morogoro, Kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg James Mkumbo
Mkuu wa Wilaya ya Muheza Hajat Mhandisi, Mwanasha Tumbo akichangia jambo wakati wa kikao cha Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) Kanda ya Mashariki.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MPIGA CHAPA MKUU ASISITIZA KAMPUNI KUENDELEA KUJISAJILI

$
0
0

Leonce Zimbandu

MPIGACHAPA Mkuu wa Serikali, Cassian Chibogoyo ameendelea kusisiti za na kuzitaka taasisi za serikali, binafsi za uchapishaji  kuendelea kujisajili katika ofisi hiyo na kuepuka usumbufu wa kubainika kwenye msako.

Kauli hiyo imetolewa baada ya kutoridhishwa na kasi ya kampuni za uchapishaji zilizojitokeza tangu wito huo utolewe Februari 13, mwaka huu, kampuni 24 tayari zimejitokeza.

Chibogoyo  aliyasema hayo alipokuwa akizungumza jijini Dar es Salaam leo  wakati akijibu swali kuhusu kampuni za uchapishaji zilizotii sharia kujisajili  bila shuruti.

Alisema amesikitishwa na mwitikio mdogo wa usajili wa kampuni na taasisi za uchapishaji, hivyo akiwa muungwana ameamua kutumia fursa ya  kuwakumbusha  watimize wajibu wao kisheria.

“Inawezekana katika mkutano wangu  sikueleweka vizuri lakini usajili unahusu kampuni binafsi na serikali kwa lengo la  kutambua shughuli zao na kuepuka kujificha,” alisema.

Alisema baada ya muda uliotolewa kukamilika na ofisi hiyo ikapata  taarifa kuwa ipo taasisi au kampuni inajihusisha na uchapishaji, Ofisi itachukua hatua ya kuifuatilia.

Hivyo kabla ya hali hiyo ya ufuataliaji, itakuwa busara kwa wachapishaji hao kujisajili  ndani ya siku tano zilizobaki tangu wito huo ulipotolewa. 

Aidha, alisema   ili kuondoa usumbufu kwa kampuni za uchapishaji za mikoani, zinaweza kujisajili kwa kupitia mtandao wa Ofisi ya Mpigachapa.

Alisema Wachapishaji   halali watakaojiorodhesha watakaribishwa na kupewa fursa ya kutoa mawazo ya kuiweka nchi mahali salama kupitia nyaraka.

Hatua hiyo imechukuliwa  ili kuendeleza vita dhidi ya wachapishaji wa nyaraka bandia kwa kuwasaka nyumba kwa nyumba, iwapo watashindwa kujitokeza na kujisajili kwa hiari.
Mpigachapa Mkuu  wa Serikali,Cassian Chibogoyo akionesha waandishi wahabari (hawapo pichani) katika moja ya mikutano yake  rangi sahihi  ya bendera yaTaifa, kulia ni Afisa Habari wa Idara Habari Maelezo, Frank Shija.

WAZIRI MBARAWA AKAGUA MIUNDOMBINU BUKOBA MKOANI KAGERA

$
0
0



Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  Profesa Makame Mbarawa ameipa miezi miwili  Kampuni ya Simu Tanzania  (TTCL), kuhakikisha kuwa inapata Dola za Kimarekani milioni 50 ili kuongeza pato kwa Kampuni na Taifa kwa ujumla kupitia Mkongo wa Taifa.

Akitoa agizo hilo leo, wilayani Bukoba mkoani Kagera, Waziri Prof. Mbarawa amesema agizo hilo limetokana na Serikali kuongeza masafa kwa kampuni hiyo kutoka 10 hadi 200 (MHZ) ambayo yana uwezo wa kuunganisha wateja wengi na wakubwa zaidi.

Amesisitiza makampuni ya Simu nchini kuchangamkia fursa ili kupata masafa yenye uwezo mkubwa kupitia mkongo huo.

“Hakikisheni mnajipanga kuipata hiyo fedha ndani ya miezi miwili na kuwapatia masafa ya kutosha wateja mlionao ndani na nje ya nchi na kujitahidi kuongeza wateja wengi zaidi”, amesema Prof. Mbarawa.

Aidha, ameitaka TTCL kusogeza  wigo wa kuwasiliana na wateja wakubwa ili kuwashawishi kununua masafa hayo  kulingana na mahitaji yao na hivyo kutanua wigo wa kibiashara  na kuiwezesha kampuni hiyo kupata faida zaidi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), akioneshwa taarifa ya mapato na Meneja wa Kampuni ya Simu Nchini (TTCL), mkoa wa Kagera, Bw. Salum Mbaya, wakati alipotembelea ofisini hapo leo.

ML 1
Fundi Mitambo kutoka Kampuni ya Simu Nchini (TTCL), Eng. Godfrey Mbise, akimpa maelezo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), kuhusu mfumo wa utoaji huduma katika mkongo wa taifa mkoani humo.
ML 2
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa uongozi wa Kampuni ya Simu Nchini (TTCL), mkoa wa Kagera, leo, mara baada ya kukagua mitambo na mifumo iliyopo ofisini hapo.
ML 3
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akishuka katika ndege ya Kampuni ya Ndege Nchini (ATCL), katika uwanja wa ndege wa Bukoba, mkoani Kagera alipowasili kwa ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo.

RC MAKALA AWATAKA WANANCHI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO ZILIZOPO KATIKA MAENEO YAO

$
0
0


Na Fadhili Atick Globu ya Jamii Mbeya

 Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala amefanya mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi mtaa wa Shewa kata ya Mwakibete mkoani Mbeya,na kuwataka wananchi kushirikiana na serikali katika kutatua Changamoto mbalimbali zinazo wakabili.

Makala ambaye ametembelea Shule ya Msingi Shewa na kushuhudia msongamano wa wanafunzi,  amepongeza wananchi kwa kushiriki ujenzi wa madarasa kupunguza msongamano wa wanafunzi, ambapo halmashauri ya jiji la Mbeya walichangia shilingi milioni 6.3 kuunga Mkono jitihada za wananchi.

Makala ameahidi kufuatilia kwa Karibu ujenzi wa madarasa mpaka yakamilike, kwani wananchi wamekuwa wakichukizwa na baadhi ya watu wachache wanaopita kushawishi wananchi wasichangie

Makala amewaonya wote wanaoshawishi wananchi kutochangia Maendeleo kuacha tabia hiyo mara moja katika  na kuamua kuonyesha mfano wa kuchangia milioni moja katika ujenzi wa choo cha Shule msingi shewa

Pia ameagiza Tanesco na Mamlaka ya Maji kushughulikia haraka matatizo ya  Umeme na Maji katika mkoa wa Mbeya hili kupunguza kero kwa Wananchi.
 Rc Makalla akizungumza na wananchi wa kata ya mwakibete jijini mbeya
Akishangazwa na wingi wa wanafunzi katika shule ya msingi mwakibete ambapo idadi ilionesha wanafunzi ni wengi kuliko madarasa.
Moja kati ya Wakazi wa shewa kata ya mwakibete wakitoa kero zao mbele ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya.
Mmoja wa Wananchi akitoa duku duku lake kwa RC Makala.
Baadhi ya wakazi wa Mwakibete wakifuatilia mkutano huo.

NEWZ ALERT;SEHEMU YA KITUO CHA MAFUTA CHA GAPCO CHAPIGWA 'NYUNDO'.

$
0
0
Sehemu ya Kituo cha Mafuta cha Gapco kilichopo karibu na kamata jijini Dar ikibomolewa mapema leo kwa kuwa ndani ya eneo la reli.Zoezi hilo ambalo limeanza hivi karibuni linaendeshwa na kampuni ya reli Tanzania (TRL) dhidi ya watu waliofanya maendelezo ndani ya eneo la reli.

Article 10


PAC YATEMBELEA MRADI WA NYUMBA ZA WATUMISHI BUNJU B ZILIZOJENGWA NA TBA

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali Kuu na Mashirika ya Umma (PAC) imetembelea miradi ya ujenzi wa nyumbaza watumishi zilizojengwa na Wakala wa Majengo (TBA) .

Kamati hiyo imeitaka TBA kuendelea kubuni miradi ya nyumba kwa gharama nafuu ili watumishi waweze kupata nyumba hizo kutokana na viwango vyao.

Akizungumza wa wakati wa Kutembelea miradi ya TBA Bunju B, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya PAC , Joseph Kasunga, amesema kuwa mradi ni ya gharama kubwa.

Kamati hiyo imesema TBA wamefanya kazi katika kufanya utatuzi wa nyumba kwa watumishi wa serikali wanavyostaafu wanakuwa na makazi bora.

Afisa Mtendaji Mkuu wa TBA , Arch , Elius Mwakalinga amesema kuwa wanaendelea kufanya ujenzi katika kuhakikisha kila mtumishi anaweza kupata makazi bora .

Amesema kuwa changamoto za baadhi ya viwanja walinunua na muda lakini kuna watu wanakaa ambapo wameweza kukaa nao jinsi ya kusaidiana.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),Mhandisi Elius Mwakalinga (wa tatu kulia), akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Fedha za Serikali (PAC), kabla ya kutembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za Bunju B jijini Dar es Salaam jana zinazojengwa na wakala huo. Wa pili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Josephat Asunga.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),Mhandisi Elius Mwakalinga (wa pili kushoto), akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Fedha za Serikali (PAC), walipotembelea mradi wa ujenzi wa nyumba Bunju B jijini Dar es Salaam jana. Wa nne kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Josephat Asunga.
 Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Josephat Asunga, akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa majumuisho ya ziara hiyo.
 Baadhi ya nyumba zinazojengwa katika mradi  wa Bunju B
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),Mhandisi Elius Mwakalinga, akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo.
 Baadhi ya nyumba zinazojengwa kwenye mradi wa Bunju B

WAZIRI MUHONGO AZINDUA MRADI WA UMEME VIJIJINI MKOANI SINGIDA

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Muhongo akizinduzia Mradi wa umeme Vijijini Mkoa wa Singida. Uzinduzi huo umefanyika jana Machi  24/2017 na kuhudhuriwa na wafadhili kutoka WB, EU, Norway na Denmark ambao wwnafadhili mradi mkubwa wa Backbone unaoanzia Iringa- Dodoma-Singida hadi Shinyanga. Mradi huo wa REA III unatekelezwa kuziba mapengo ya maeneo vijiji ambavyo vimepitiwa na mradi mkubwa wa Backbone na vilirukwa katika Awamu ya REA II.

MAKAMANDA WA POLISI KUKUTANA DODOMA KUPANGA MIKAKATI YA KUPAMBANA NA UHALIFU

$
0
0
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi.

MAOFISA Wakuu wa Jeshi la Polisi wanatarajia kukutana mkoani Dodoma kuanzia Jumatatu tarehe 27-29/03/2017 katika kikao kazi cha siku tatu kujadili na kupanga mikakati mbalimbali ya kukabiliana na uhalifu na wahalifu hapa nchini.

Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Advera Bulimba (pichani) alisema kikao hicho kitawakutanisha maofisa wakuu wa makao mkauu ya Polisi, makamanda wa Polisi wa mikoa na Makamanda wa vikosi bara na Zanzibar ili kujadili mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika utendaji katika kipindi cha mwaka uliopita na kuweka mikakati mipya ya kupambana na uhalifu kwa mwaka 2017.

Aidha, Bulimba alisema mbali na utaratibu wa mawasiliano ya kila siku katika kuimarisha usalama wa raia na mali zao, Jeshi la Polisi pia lina utaratibu wa kukutana kila mwaka kwa pamoja ili kubadilishana uzoefu kukabiliana na wahalifu kwa lengo la kuhakikisha kuwa usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarika hapa nchini.

“Katika kikao hicho Inspekta Jenerali wa Polisi IGP Ernest Mangu atatoa maelekezo ya kiutendaji ambayo lengo lake ni kuhakikisha kuwa kila ofisa, mkaguzi na askari anawajibika kwa nafasi yake katika kuhakikisha uhalifu unapungua hapa nchini” Alisema Bulimba.

Bulimba alisema kikao kazi hicho kinatarajiwa kufunguliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba ambapo kauli mbiu katika kikao hicho ni “Zingatia maadili tunapopambana na uhalifu ili kuimarisha usalama kwa maendeleo ya Taifa”.

NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI AKUTANA NA BALOZI WA UJERUMANI NCHINI NA UJUMBE WAKE JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
NIS1
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (mbele) akiongoza kikao kilichoshirikisha Balozi wa Ujerumani Nchini, Egon Kochanke na ujumbe wake, wawekezaji kutoka Denmark na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini. Mambo yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na ujenzi wa kiwanda cha mbolea Kilwa mkoani Lindi.
NIS2
Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wakifuatilia maelekezo  yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (hayupo pichani) katika kikao hicho.
NIS3
Sehemu ya ujumbe kutoka Ujerumani na wawekezaji kutoka Denmark wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa unatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (hayupo pichani) katika kikao hicho.
NIS4
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo akifafanua jambo katika kikao hicho.
NIS5
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akisalimiana na Balozi wa Ujerumani Nchini, Egon Kochanke (kushoto) kabla ya kuanza kwa kikao hicho.

UONGOZI CHALINZE WAUJIA JUU UONGOZI WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI MAZINGIRA KWA KUSHINDWA KUSAMBAZA MAJI

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete pamoja na madiwani wa halmashauri ya Chalinze ,wameujia juu uongozi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Chalinze CHALIWASA kwa kushindwa kusambaza maji ili kuondoa kero hiyo .
 
Amesema mradi huo ulitakiwa kukabidhiwa mwezi huu jimboni hapo lakini unasuasua.Ridhiwani aliyasema hayo kwenye baraza la Madiwani lililofanyika Lugoba.Alisema tatizo la ukosefu wa maji, bado ni kubwa hivyo inaonekana uongozi wa Mamlaka hiyo umeshindwa kutatua.
Ridhiwani alifafanua kwamba hadi sasa hakuna matenki yaliyojengwa na mabomba hayajafukiwa hivyo ni ndoto za alinacha mradi huo kukamilika mwezi huu.Kwa mujibu wake, waziri wa maji anapaswa kulieleza bunge na wananchi wa Chalinze fedha za maji zilizopelekwa kwa ajili ya mradi huo na mwezi wa kuumaliza .
"Kama mradi huu utaendelea kusuasua wananchi na wawekezaji wanaokimbilia kuwekeza Chalinze watashindwa kutimiza malengo yao na kuendelea kuishi kwenye adha hii inayowapa wakati mgumu "alisema Ridhiwani.Nao madiwani walisema, kama uongozi wa mamlaka hiyo umeshindwa kazi basi wawapishe .Diwani wa Lugoba, Rehema Mwene,aliiomba serikali imsimamie mjenzi wa mabomba na matenki amalize kazi hiyo.
Nae Hassan Mwinyikondo, alieleza hatari kubwa kwa wananchi wa maeneo ya Bwilingu na Chalinze ambao wanatumia maji yasiyo safi wala salama.
Alisema mradi wa maji wa CHALIWASA hauna faida, kutokana na wananchi kukosa maji kwa kipindi kirefu.
Hussein Hading'oka aliweka hofu katika kipindi kinachokuja kuwa cha mvua za masika na kuongeza kwamba mara kadhaa viongozi wa CHALIWASA wamekuwa wakisema kipindi cha mvua mitambo yao huwa inasumbuliwa na tope.hivyo kushindwa kufanyakazi za kusukuma maji.
Alimshangaa Meneja wa Mamlaka hiyo Mhandisi Christer Mchomba kushindwa kuhudhuria kikao hicho kama alivyotakiwa na Mkurugenzi Edes Lukoa .
Meneja huyo alitakiwa kwa ajili ya kuwapatia Madiwani hao maelezo ya kina kuhusiana na tatizo sugu la maji linalowakabili wananchi wa Halmashauri hiyo kwa miaka mingi sasa.Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Edes Lukoa alisema Halmashauri imetenga bajeti iwa ajili ya maeneo ambayo hayafikiwi na CHALIWASA hivyo mamlaka hiyo lazima iwe na mpango wake.
Hivi karibuni Waziri wa Mazingira Januari Makamba alipofanya ziara ndani ya Halmashauri hiyo alifika eneo la chanzo cha maji Wami na kutoa maagizo kwa wilaya na mkoa.Aliagiza Mkuu wa wilaya Alhaj Hemed Mwanga kuhakikisha na Mkoa wanakutana na wenzao wa Morogoro kuzungumzia suala la wafugaji wanaotokea Morogoro kuvamia kando ya mto WAMI na kuhakikisha wakulima wanaolima kando ya mto wondolewe mara moja.
Mbunge wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akizungumza na madiwani wa halmashauri hiyo katika baraza la madiwani. (picha na Mwamvua Mwinyi).
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images