Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA BANDARINI NA KUZUIA MAKONTENA 20 YENYE MCHANGA WA MADINI ULIOKUWA USAFIRISHWE NJE YA NCHI

0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam kufatilia maagizo yake ya kudhibiti vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na wafanyabiashara wanaogiza na kusafirisha mizigo ndani na nje ya nchi.
. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akihesabu makontena 20 yenye mchanga wa madini ambapo ameamuru kontena hizo zisisafirishwe mahali popote. 
Makontena 20 yenye mchanga wa madini yakiwa yamezuiwa kusafirishwa nje ya nchi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mara alipofanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar es Salaam. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akikagua nyaraka mbalimbali zenye maelezo kuhusu makontena ambayo husafirishwa nje ya nchi katika Bandari ya Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na IGP Ernest Mangu mara baada ya kufanya ukaguzi Bandarini hapo. PICHA NA IKULU


MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA AKUTANA NA BALOZI WA UFARANSA NCHINI

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameonana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Malika Berak  ambaye aliongozana na Mshauri wa  Uchumi wa Ubalozi  wa Ufaransa  Bi. Beatrice Alperte, Ikulu jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Balozi wa  Ufaransa nchini Mhe. Malika Berak  alipokuwa akifanya mazungumzo nae mapema leo , Ikulu jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza  Mshauri wa  Uchumi wa Ubalozi  wa Ufaransa  Bi. Beatrice Alperte, Ikulu jijini Dar es salaam. alipokuwa akifanua jambo mapema leo , Ikulu jijini Dar es salaam.
 Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Malika BERAK (katikati) akimtambulisha Mshauri wa Masuala ya Uchumi wa Ubalozi huo Bi. Beatrice Alperte (kushoto) kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassanakiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Malika BERAK (kushoto) na Mshauri wa  Uchumi wa Ubalozi  wa Ufaransa  Bi. Beatrice Alperte (kulia), Ikulu jijini Dar es salaam.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


ZANZIBAR KUADHIMISHA SIKU YA KIFUA KIKUU DUNIA LEO MACH 24

0
0
Mkurugenzi kinga na elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Fadhil Mohammed Abdalla akitoa maelezo kwa wandishi wa habari na kumkaribisha Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Bi. Harusi Said Suleiman katika mkutano wake na wandi wa habari uliofanyika ukumbi wa Wizara hiyo Mjini Unguja.
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Bi. Harusi Said Suleiman akitoa maelezo kwa wandishi wa habari kuhusu mapambano zidi ya Kifua Kikuu katika ukumbi wa Wizara ya Afya.
Baadhi ya wandishi wa habari waliofika katika mkutano wa Naibu Wizara ya Afya wakifuatilia mkutano huo.
Mkuu wa kitengo cha Kifua Kikuu (TB) Zanzibar Dkt. Khamis Abubakar Suleiman akijibu maswali yaliyoulizwa na wandishi wa habari katika mkutano wao.

Picha na Makame Mshenga-Maelezo

Watanzania kunufaika na gesi asilia

0
0
Benjamin Sawe-Maelezo

Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limesema mpaka kufikia mwaka 2020 litawawezesha watanzania kutumia gesi majumbani mwao hivyo kupelekea upungufu wa uharibifu wa mazingira nchini.

Kaimu Mkurugenzi wa TPDC Eng. Kapuulya Musomba amesema muda mrefu kumekuwa na uharibifu wa mazingira hivyo kupatikana kwa nishati ya mafuta na gesi kutaiwezesha Tanzania kuwa mahali salama kimazingira ikiwa ni pamoja na ukuaji wa sekta ya uchumi.

Alisema katika robo ya pili ya mwaka 2017 shirika limekamilisha usambazaji wa mabomba ya gesi kwa matumizi ya majumbani jijini Dar es Salaam na zaidi ya viwanda 300 vimeunganishwa na nishati ya gesi hapa nchini hivyo kupelekea upatikanaji wa umeme wa uhakika.

Kuhusu upangaji wa Bei kwa matumizi ya gesi itakayosambazwa majumbani Eng. Musomba amesema Taasisi yake itashirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta (Ewura), kuhakikisha nishati hiyo inapatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu.

Hivi sasa zaidi ya asilimia 50 ya umeme uliopo katika Gridi ya Taifa unatokana na gesi asilia hivyo mipango ya Serikali ni kulifanya Shirika hilo kuchangia zaidi mapato Serikalini yanayotokana na rasilimali hiyo.Alisema Eng. Musomba

Alisema TPDC imejipanga kuwekeza kwenye shughuli za utafutaji, uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa gesi ili Taifa linufaike na rasilimali hiyo.

Akitolea mfano mradi mkubwa wa kusindika gesi asilia (Liqufied Natural Gas-LNG), Eng. Musomba alifafanua kwamba itachukua takribani miaka 8 hadi 10 kabla ya mzigo wa kwanza wa LNG kusafirishwa kwenda katika soko la dunia kwa mauzo.

Alisema kukamilika kwa mradi wa (Liqufied Naturla Gas- LNG)utakuwa ni fursa kwa watanzania kupata ajira katika mradi huo ikiwa ni pamoja na kuchangia pato la mwananchi,wawekezaji na Taifa kwa ujumla.

Alisema uwekezaji katika sekta ya mafuta na gesi ni wa gharama kubwa na hata mafaniko kwa maana ya mapato makubwa kwa Serikali huchukua muda mrefu kuonekana hivyo amewataka wananchi kuwa wazalendo kwa kuilinda miundombinu inayopita maeneo yao.

TPDC inaendelea kutoa elimu kwa wadau mbalimbali ikiwa na lengo la kuongeza uelewa zaidi katika sekta hiyo ya gesi na mafuta.

MUWSA WATUMIA MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI KUOTESHA MITI KATIKA VYANZO VYAKE VYA MAJI.

0
0
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) wakishusha miti tayari kwa ajili ya kuotesha kando ya vyanz vya maji vinavyosimamiwa na mamlaka hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) John Ndetiko akiwa amebeba mti tayari kwa ajili ya kuotesha kando ya chanzo cha maji cha Shiri kilichopo wilayani Hai.

Wafanyakazi wa Airtel kuitambulisha “Hatupimi Bando” Sokoni

0
0

Kufatia kuzinduliwa kwa ofa Kabambe ya Airtel ijulikanayo kama “Hatupimi Bando” ofa inayowapa wateja wake uhuru wa kuongea bila kikomo, wafanyakazi wa Airtel wamejipanga kuingia sokoni na kukutana na wateja kwa lengo la kutoa elimu zaidi juu ya huduma na bidhaa za Airtel

Mpango huu unategemea kufanyaka leo ijumaa ambapo wafanyakazi wa Airtel nchi nzima watakutana na kuzungumza na wateja wao ana kwa ana katika maeneo mbalimbali na kuitambulisha ofa hii ya “Hatupimi Bando” pamoja na kuwaunga wateja wapya kwenye mtandao wa Airtel ili nao pia waweze kufurahia bidhaa na huduma mbalimbali na kujiunga na ofa hii kabambe ya “Hatupimi Bando”

“Tunapenda wateja wetu waelewe vyema ofa hii ya “Hatupimi Bando” itakayowasaidia kuokoa kiasi kikubwa cha gharama katika matumizi yao ya simu kwani ofa hii inawapatia gharama nafuu zaidi za mawasiliano sokoni.

wateja wetu wanaweza kujinga “Hatupimi Bando” Kwa kiasi cha shilingi 1000/= ,shilingi 5000 kwa wiki, na vilevile unaweza kujiunga na kwa mwezi kwa shilingi 10,000/= na kufurahia huduma yakutopimiwa dakika na kuongea bila kikomo”. Alisema Jackson Mmbando, Meneja Uhusiano wa Airtel

Kujiunga na ofa ya HATUPIMI Bando piga *149*99# kisha chagua 1 kupata HATUPIMI kisha chagua bando ya Siku, Wiki, Mwezi kulingana na mahitaji yako “ alisisitiza Mmbando

KAMATI YA BUNGE YAPONGEZA KAZI NZURI YA TPSC TAWI LA TANGA

0
0
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala na Serikali za Mitaa Mwaine Ismail Nchemba (Viti Maalum ) Tabora akifafanua jambo wakati kamati yake ilipozuru tawi la Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) tawi la Tanga leo asubuhi.
Mkuu wa Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Dk.Henry Mambo akifurahia jambo wakati wakiwasilisha taarifa kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala na Serikali za Mitaa waliotembelea Chuo hicho tawi la Tanga leo asubuhi
Wanakwaya wa Chuo wakiimba wimbo maalum mbele ya wajumbe wa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala na Serikali za Mitaa, leo asubuhi chuoni hapo.
Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) tawi la Tanga , Hassanal Issaya, akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala na Serikali za Mitaa Mwaine Ismail Nchemba (Viti Maalum ) Tabora baada ya ujumbe wa Kamati hiyo kuwasili tawini hapo eneo la Nkange Jijini Tanga. wa pili kushoto ni kushoto kwa Mkurugenzi huyo ni Mkuu wa TPSC Dk.Henry Mambo.

KIKAO CHA KAMATI MAALUM CCM LEO.

0
0
Na Is-haka Omar, Zanzibar.

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, leo (jana) amekiongoza kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa..

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya Habari iliyotolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM wa Idara ya Itikadi na Uenezi Bi. Waride Bakari Jabu, amesema kikao hicho cha siku moja kilifanyika Afisi Kuu ya CCM, Mjini Unguja.

Ameeleza kwamba pamoja na mambo mengine, kikao kilipokea na kujadili majina ya wana CCM waliojitokeza kuomba ridhaa ya Chama hicho, ili waweze kuwania nafasi ya Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki, kwa kipindi cha mwaka 2017 - 2022.

“ Kutokana na Chama chetu kuwa Kinara wa Demokrasia wanachama wengi wamejitokeza kuwania nafasi hizo ili waweze kuiwakilisha vyema CCM na serikali inazoziongoza katika Bunge hilo muhimu.

Pia Wana CCM na wananchi kwa ujumla tukumbuke kuwa fursa hizi zisingeweza kujitokeza kama nchi yetu ingekuwa katika mashaka na migogoro, hivyo wito wangu tuendelee kuwa wamoja ili wenzetu waweze kutuwakilisha vyema.”, alisema Bi. Waride.

Kikao hicho kimefanyika kwa kuzingatia Ibara ya 114 (7) (b) ya Katiba ya CCM ya mwaka 1977, Toleo la 2012, ambayo inatoa Mamlaka kwa Kamati Maalum ya H/Kuu yaTaifa ya CCM Zanzibar, kupokea na kujadili na hatimaye kutoa mapendekezo yake kwa Kamati Kuu, kwa hatua zinazofuatia.

Bi. Waride amesema jumla ya wana CCM 33, wakiwemo wanawake 7 na wanaume 26, kutoka Mikoa mbali mbali ya Unguja na Pemba, wamejitokeza kuomba waruhusiwe na CCM kugombea nafasi hizo.

Katibu huyo wa Kamati Maalum ya NEC wa Idara ya Itikadi na Uenezi amefafanua kuwa kwa mujibu wa Katiba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Tanzania inapaswa kuwakilishwa na Wabunge tisa (9).

Aidha kikao hicho kilimtambulisha Ndugu. Abdullah Juma Saadalla (Mabodi) aliyepitishwa na Mkutano Mkuu wa CCM hapo Machi 13, mwaka huu, kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar. Aidha, kimeahidi kumpa kila aina ya mashirikiano ili aweze kutekeleza majukumu yake aliyopewa na Chama ipasavyo.

Hata hivyo Kikao pia kimewapongeza kwa dhati wana CCM hasa Vijana waliojitokeza kuomba kugombea nafasi hizo muhimu za Uongozi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki hali inayoonyesha kuimarika kwa Demokrasia ndani ya Chama hicho.

BALOZI KAIRUKI AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO

0
0
Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Mbelwa Kairuki amewasilisha rasmi Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping tarehe 17 Machi 2017.  

Hafla hiyo iliyofanyika katika Ikulu ya China (Great Hall of the People) ilihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Mhe. Wang Yi na maafisa waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China. 

Katika mazungumzo mafupi baada ya kuwasilisha hati, China na Tanzania zimekubaliana kukuza zaidi mahusiano ya kiuchumi kupitia mpango maalum wa China wa kuhamishia viwanda vyake nje ya China (Production Capacity Cooperation Programme) pamoja na programu ya kukuza ushirikiano wa biashara na ujenzi wa miundombinu ijulikanayo kama Maritime Silk Road initiative. 

Aidha, Tanzania imeihakikishia China kuendelea kuunga mkono sera yake ya ONE CHINA POLICY sambamba na kuunga mkono mtazamo wa China kuhusu mgogoro wa Bahari ya Kusini mwa China.
Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mberwa Kairuki akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Xi Jinping wakati wa hafla ya kuwasilisha Hati za Utambulisho iliyofanyika Ikulu kwenye Ukumbi wa Great hall of the people siku ya Ijumaa tarehe 17 Machi 2017.

Balozi Kairuki (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa China, Mhe. Xi Jinping 

SPIKA WA BUNGE AFUNGUA MKUTANO WA KAMATI TENDAJI YA CPA KANDA YA AFRIKA.

0
0
Katibu Msaidizi wa Chama cha Mabunge Wanachama Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CPA Africa Region ) Bw. Demetrius Mgalami akimuelezea jambo Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 72 wa Kamati Tendaji ya CPA Afrika Jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika kusini Mhe Lindiwe Maseko ( wa pili kushoto) na Katibu wa Chama cha  CPA Afrika ambaye pia ni Katibu wa Bunge la Tanzania   Dkt Thomas Kashililah.
 Wajumbe wa Kamati Tendaji ya CPA Afrika  wakiimba wimbo wa Jumuiya hiyo kabla ya kuanza kwa Mkutano huo.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Wajumbe wa Kamati Tendaji CPA Afrika  wakati wa Mkutano wa Chama hicho uliofanyika Jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Viongozi wa Kamati hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya CPA Afrika ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Kusini Mhe. Lindiwe Maseko akizungumza wakati wa Mkutano huo.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (kulia waliokaa mbele) ambaye pia ni Mwenyejiti wa Bodi ya Chama cha CPA Afrika akiongoza kikao cha Bodi hiyo mara baada ya kikao cha Kamati Tendaji ya chama hicho kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya CPA Mhe. Lindiwe Maseko. Wengine katika picha ni Wajumbe wa Bodi hiyo.(Picha na Ofisi ya Bunge).                                               

WAZIRI MWAKYEMBE APOKELEWA IDARA YA HABARI MAELEZO MARA BAADA YA KUAPISHWA

0
0
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison George Mwakyembe akisalimiana na Naibu wake Mhe. Anastazia Wambura wakati alipowasili katika ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) Jijini Dar es Salaam mara baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel.

Malkia wa Tembo Afunguka Mahakamani

0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

Anayedaiwa kuwa Malkia wa Meno ya Tembo Yang Feng Clan (66), amesema kauli mbiu ya Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania ni hapa kazi tu lakini mbona Mahakamani hamna hiyo kazi tu.

Mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya uhujumu uchumi, Clan ameuliza hayo mahakamani Leo wakati kesi yake ilipokuja kwa ajili ya kusikilizwa.

Kabla Clan hajasema kitu, Wakili wa Serikali Nassoro Katuga ameileza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa kesi hiyo Leo imekuja kwa ajili ya kusikilizwa lakini wakili anayeendesha anamajukumu mengine kikazi.

Baada ya kusikia hayo, mshtakiwa Clan alinyoosha mkono ndipo Hakimu Huruma Shahidi anayesikiliza kesi hiyo akamruhusu kusema naye akalamika, " tumekuja màhakamani mara nyingi, leo mara ya nne hamna kitu, Rais Magufuli alisema hapa kazi tu, hapa court iko wapi hiyo kazi tu" amesema Mshtakiwa Clan kwa kutumia kiswahili chake chenye lafudhi ya kichina.

Hakimu Shahidi amewataka mawakili wa Serikali kuleta mashahidi na kuwaambia kuwa wanataka kesi zote ziishe kwa wakayi.Katika kesi hiyo Clan anashtakiwa pamoja na mfanyabiashara Salvius Matembo (39) na Manase Philemon (39).

Wanadaiwa kujihisisha na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya bilioni 5.4.

Wanadaiwa kati ya Januari Mosi 2000 na Mei 22, 2014 walijihusisha na biashara ya nyara za Serikali bila kibali.Katika kipindi hicho wanadaiwa kufanya biashara ya vipande 706 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 1,889 zenye thamani ya Sh5.4 bilioni bila leseni iliyotolewa na Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Machine 20 na 30, mwaka huu.

TAASISI YA MANJANO FOUNDATION KUWAWEZESHA WANAWAKE WA MTWARA KIUCHUMI

0
0
Mradi wa Kuwawezesha wanawake Kiuchumi Kupitia Tasnia ya urembo ujulikanao kama Manjano Dream-Makers ulioasisiwa na Taasisi ya Manjano Foundation wataendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Mkoa wa Mtwara kuanzia Jumatatu, tarehe 27 March 2017 kwenye ukumbi wa SIDO Mkoani Mtwara. Mafunzo hayo yatatolewa kwa jumla ya wanawake watakaochaguliwa 30 kutoka mkoani Mtwara. 

Baada ya mafunzo hayo wanaweke hao watakuwa chini ya uangalizi wa Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha wanawake wa Mkoa wa Mtwara wanafikia malengo yao waliojiwekea katika kujikita kwenye kujiajiri. Wanawake wakazi wa Mkoa wa Mtwara waliotuma maombi kupitia tovuti ya Manjano Foundation na wanaopenda kunufaika na mradi huo wanaombwa kujitokeza kwa ajili ya usaili siku ya Jumamosi tarehe 25 Machi 2017 kuanzia saa tatu (9:00AM) asubuhi kwenye ukumbi wa wa SIDO Mkoani Mtwara.

Mafunzo yana lengo la kumsaidia mjasiriamali mwanamke kujikwamua na kujiongezea kipato. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya biashara namna ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika mpangilio wa biashara ikiwemo matumizi sahihi ya rasilimali muda, kutokufuja fedha na pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na biashara yake. 

Awamu ya pili itahusu kuwafundisha jinsi ya kupamba ma harusi na matumizi sahihi ya vipodozi vya LuvTouch Manjano. Baada yanawake hawa kuhitimu mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation itawaunganisha na taasisi za fedha zinazotoa mikopo bila riba waweze kupata mtaji wa kununua bidhaa za vipodozi kwa ajili ya kuwawezesha kuanzisha biashara wakiwa chini ya uangalizi maalum wa Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha kila mhitimu wa mafunzo haya anapiga hatua na kuweza kujitegemea.

Wasiliana nasi kwa Simu namba +255 784 661 080 au +255 714 646 322..

BALOZI WA KOREA AKABIDHI MAKTABA YA KISASA KWA SERIKALI YA TANZANIA

0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Serikali ya Korea kupitia mradi wa ''Thank you Small Ribray program'' leo imekabidhi Vifaa na kuzindua maktaba ndogo ya kisasa katika ofisi za makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo balozi wa Korea nchini Song Geum Young amesema kuwa serikali yake licha ya kusaidia serikali katika miradi mingi lakini kwa sasa wameamua kusaidia katika kuwawezesha watoto kupata elimu inayoendana na wakati.

"sisi kama korea tunaamini kuwa ukimpa mtoto elimu umeweza kumpa maisha ya kesho, hivyo vifaa hivi vitaweza kuwasaidia katika kukuza taaluma yao " amesema Balozi.Balozi ametoa wito kwa wazazi kuwaleta watoto waweze kutumia maktaba hiyo kwa kutumia sehemu hiyo kwa ajili kukuza taaluma yao .
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dk Leonard Akwilapo akiwa na Balozi wa Korea nchini , Song Geum Young na Mama Anna Abdalah Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Makumbusho ya Taifa wakikata utepekuashiria uzinduzihuo.

Balozi wa Korea nchini , Song Geum Young akizungumza kabla ya uzinduzi wa wa Maktaba ya kisasa ambayo imetolewa na Serikali ya korea.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dk Leonard Akwilapo, akikabidhi vitabu kwa Mwenyekiti wa bodi ya Makumbusho ya Taifa , Mama Anna Abdalah
Mkurugenzi Mtendaji wa Makumbusho ya Taifa , Audax Mabula akizungumza kabla ya uzinduzi wa Maktaba ya Kisasa katika Makumbusho ya Taifa.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dk Leonard Akwilapo akizungumza kabla ya uzinduzi wa Maktaba ya Kisasa katika ukumbi wa Makumbusho ya taiafa kwa msaada wa Serikali ya watu wa Korea.

WAZIRI MWAKYEMBE AONGEA NA WAANDISHI WA HABARI BAADA YA KUAPISHWA LEO


SERIKALI YASISITIZWA KUONGEZA MASUALA YA MABADILIKO YA TABIANCHI KATIKA MIPANGO NA BAJETI

0
0
FORUMCC imeandaa mkutano na kukutanisha wadau kujadili namna ya kuongeza jitihada katika kuingiza masuala ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi katika mipango na bajeti ya serikali kuu na serikali za mitaa hapa nchini Tanzania. 

Mkutano huo umewakutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta binafsi pamoja na serikali ili kuangalia njia nzuri zinazoweza kusadia Tanzania kuwa na mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ili kupunguza kutegemea zaidi fedha kutoka kwa wafadhili.

Lengo la mkutano huu ni kuwakutanisha wadau kujadili na kuhamasisha jitihada za kuingiza masuala ya mabadiko ya Tabianchi katika mipango na bajeti ya Serikali katika kipindi hiki tunapoelekea katika Bunge la bajeti ya mwaka 2017/18.

Akizungumza kwenye mkutano huo Mkurugenzi Msaidizi, Sekta za Uchumi na Uzalishaji toka TAMISEMI, Dkt. Lucy Ssendi amesema serikali kupitia TAMISEMI iko karibu na wadau mbalimbali wa mabadiliko ya Tabianchi ili kuweza kupunguza majanga mbalimbali hapa nchini, na wao TAMISEMI wana jukumu la kubwa kwenye asasi za kiraia kuingia kwenye miradi inayohusu mabadiliko ya Tabianchi.

Pia Mwenyekiti wa bodi ya ForumCC, Euster Kibona aliwaomba wadau mbalimbali waliofika kwenye mkutano huo kushirikiana na FORUMCC ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea kwenye suala la mabadiliko ya Tabianchi linalotishia maendeleo ya jamii za mbalimbali na ukuaji wa uchumi nchini Tanzania.

Mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa COSTECH (Tume ya Sayansi na Teknolojia) leo uliwakutanisha wadau mbalimbali kutoka asasi za kiraia, maafisa mipango kutoka wizara mbalimbali, watafiti na waandishi wa habari. 
Mkurugenzi Mtendaji wa ForumCC, Rebecca Muna akiwasilisha mada kwa wadau kutoka kwenye asasi za kiraia, maafisa mipango wa wizara mbalimbali pamoja na watafiti kuhusu namna ya kuongeza jitihada katika kuingiza masuala ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi katika mipango na bajeti.
Mkurugenzi Msaidizi, Sekta za Uchumi na Uzalishaji toka TAMISEMI, Dkt. Lucy Ssendi akitoa mada kuhusu kazi za TAMISEMI pamoja na ushirikiano wake kwenye masuala ya mabadiliko ya Tabianchi kwenye mkutano uliofanyika leo kwenye kumbi wa COSTECH (Tume ya Sayansi na Teknolojia) jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa bodi ya ForumCC, Euster Kibona akitolea ufafanuzi baadhi ya maswali pamoja na kutoa maoni kwa maofisa wa wizara kuangalia namna ya kushirikiana ili kupunguza athari za mabadiliko ya Tabianchi.
Mkutano ukiendelea uliowakutanisha wadau mbalimbali uliowakutanisha ili kujadili namna ya kuongeza jitihada katika kuingiza masuala ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi katika mipango na bajeti.

WAZIRI MHAGAMA AFUNGA MKUTANO WA 26 WA WANACHAMA WA MFUKO WA PPF JIJINI ARUSHA LEO

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge, Vijana Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama, akitoa hotuba yake wakati akifunga Mkutano wa 26 wa mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko Pensheni wa PPF uliokuwa na kauli mbiu ya "Tanzania ya Viwanda, Umuhimu na Wajibu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii", uliokuwa ukifanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.
Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa, akizungumza machache katika Mkutano wa 26 wa mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko Pensheni wa PPF uliokuwa na kauli mbiu ya "Tanzania ya Viwanda, Umuhimu na Wajibu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii", uliokuwa ukifanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko Pensheni wa PPF, Ramadhan Khijjah akizungumza wakati akitoa shukrani wa viongozi na washiriki wengine wa Mkutano wa 26 wa mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko Pensheni wa PPF, uliokuwa ukifanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko Pensheni wa PPF, William Erio akizungumza katika Mkutano wa 26 wa mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko Pensheni wa PPF, uliokuwa ukifanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.
 Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Daniel Gabriel Daqarro akichangia moja ya mada zilizowasilishwa katika Mkutano wa 26 wa mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko Pensheni wa PPF, uliokuwa ukifanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (TSSA), Meshack Bandawe akizungumza wakati alipowasilisha taarifa ya maendeleo ya mifuko mbalimbali, katika Mkutano wa 26 wa mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko Pensheni wa PPF, uliokuwa ukifanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

DKT ABBAS: MAAFISA HABARI MUUNGENI MKONO RAIS MAGUFULI KWA KUTANGAZA MAFANIKIO YA SERIKALI

0
0
Maafisa Habari na Mawasiliano katika Wizara, Taasisi, Idara na Mamlaka za Mikoa na Wilaya nchini wametakiwa kutangaza mafanikio ya miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongoozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli. 
Hayo yamesemwa leo Mjini Morogoro na Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas wakati alipokuwa akizungumza na Maafisa Habari na Maafisa TEHAMA katika mafunzo ya uwekaji wa taarifa katika tovuti za Mikoa na Halmashauri yanayofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID) na kusimamiwa na Ofisi ya Rais- TAMISEMI na Wakala ya Serikali Mtandao (EGA).
Kwa mujibu wa Dkt. Abbas alisema Serikali ya Awamu ya Tano inatekeleza miradi mikubwa ya maendeleo katika Mikoa na Halmashauri zake, hivyo ni wajibu wa Maafisa Habari kuhakikisha kuwa taarifa zinazowekwa katika tovuti hizo  zinaonyesha mafanikio ya Serikali katika utekelezaji wa miradi hiyo.
“Ipo miradi mikubwa inayotekelezwa na Serikali ikiwemo miradi ya umeme vijiji, ambapo Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi hiyo, hivyo ni wajibu wa Maafisa Habari kuhakikisha kuwa taarifa za utekelezaji wa miradi inawafikia wananchi” alisema Dkt. Abbas.
Aliongeza kuwa  lengo la Serikali ya Awamu ya Tano inayooongozwa na Rais Dkt. John  Pombe Magaufuli ni kuleta matokeo ya haraka kwa wananchi wake, hivyo ni wajibu wa Maafisa Habari kuhakikisha taarifa mbalimbali za mafaniko katika maeneo yao ya kazi zinatangazwa kwa kuzingatia  muda na wakati.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas akizungumza na Maafisa Habari na Maafisa TEHAMA katika mafunzo ya uwekaji wa taarifa katika tovuti za Mikoa na Halmashauri yanayofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID) na kusimamiwa na Ofisi ya Rais- TAMISEMI na Wakala ya Serikali Mtandao (EGA). Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

ALIYEKUWA MTENDAJI WA KATA YA BWANGA AFUNGWA JELA MIAKA MITATU (3) KWA KOSA LA KUOMBA RUSHWA

0
0

 Mahakama ya Wilaya ya Chato  imemkuta na hatia Aliyekuwa Mtendaji wa kata ya Bwanga Bw. Protase Polycarp Kyakatamba Ambaye ameshitakiwa  kwa makosa mawili ya Kuomba Rushwa ya kiasi cha Tshs. 300,000/= na kupokea Rushwa ya kiasi cha Tshs. 170,000/= kinyume na Kifungu cha 15(1)(a) na (2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, hukumu hiyo imesomwa na hakimu Mfawidhi wa mahakama ya Wilaya ya Chato Mheshimiwa JOVITH KATO.
Akisoma hukumu hiyo, mbele ya mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Bw. AUGUSTINO MTAKI, Mheshimiwa Kato alisema mahakama imemkuta na hatia Mshitakiwa katika makosa yote mawili kama alivyoshitakiwa, na kwamba mahakama imejiridhisha pasipokuwa na shaka lolote na ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa Jamhuri kwamba mnamo tarehe 5/2/2016 Mshitakiwa aliomba kiasi cha Tshs. 300,000/= kutoka kwa Bw. Jackson Madereke ili aweze kumwachia Ndugu yake Bw. Kulwa Charles aliyewekwa chini ya ulinzi katika ofisi ya kata ya Bwanga kwa zaidi ya siku Nne, na kwamba mnamo tarehe 6/2/2016 alimtuma Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyarututu Bw. Silvester Nalompa akutane na Bw Jackson Madereke ili aweze kupokea fedha hizo kwa niaba yake ambazo baada ya makubaliano kwa njia ya simu Mtendaji huyo alikubali kupokea kiasi cha Tshs. 170,000/= badala ya Tshs. 300,000/= alizoomba awali.
Baada ya kusomewa hukumu hiyo mshitakiwa alipewa nafasi ya kujitetea kabla ya kutolewa adhabu ambapo mahakama imempa adhabu ya kulipa faini ya Tshs. 500,000/= kwa kosa la kwanza au kifungo jela miaka mitatu (3) na faini ya Tshs. 500,000/= au kifungo cha miaka mitatu (3) jela kwa kosa la pili, na makosa yote yatatumikiwa kwa pamoja.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Geita Bw. Thobias Ndaro ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Geita kuendelea kuunga mkono TAKUKURU na serikali kwa ujumla katika mapambano dhidi ya Rushwa kwa kutoa taarifa mbalimbali za vitendo vya Rushwa katika ofisi za serikali za mitaa, mahakama na Halmashauri ili watuhumiwa waweze kuchukuliwa hatua za kisheria na hivyo kushiriki kutokomeza vitendo vya Rushwa, Ubadhilifu na Ufisadi katika jamii zetu na hivyo mwananchi atakuwa ameshiriki kukata mnyororo wa Rushwa. 

IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE

NAIBU MEYA WA MANISPAA YA ILALA, OMARY KUMBILAMOTO ATEMBELEA OFISI ZA MICHUZI MEDIA GROUP

0
0
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Mstahiki Omary Kumbilamoto akisalimiana na Msimamizi wa Chumba cha Habari, Cathbert  Kajuna wakati alipotembelea ofsi za Michuzi Media Group (MMG) mtaa wa Chimala jijini Dar es salaam leo, ili kujionea jinsi wanavyofanya kazi. Mgeni huyo alifurahishwa kukuta ofisi hiyo imesheheni vijana wanaoendesha shughuli za tasnia ya habari kwa kuzingatia weledi huku wakiweka maslahi ya nchi mbele kwa kutafuta na kutangaza habari za maendeleo ya Tanzania naMtanzania ndani na nje ya nchi.
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Mstahiki Omary Kumbilamoto, akisalimina na mwandishi mwandamizi na Msimamizi wa Habari za Mahakamani, Karama Kenyunko wakati alipofanya ziara katika ofisi za MMG.
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala  Mstahiki Omary Kumbilamoto akiwa ndani ya ofisi ya MMG.
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Mstahiki Omary Kumbilamoto akifurahi jambo na Mwandishi Mwandamizi wa Michuzi Blog,  Chalila Kibuda
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Mstahiki Omary Kumbilamoto, Akisalimiana na Mkurugenzi wa Michuzi TV, Karim Michuzi,  wakati alipofanya ziara ya kutembelea chumba cha habari cha Michuzi Media Group ili kujionea jinsi wanavyofanya kazi.
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images