Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1618 | 1619 | (Page 1620) | 1621 | 1622 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimlaki Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein alipowasili Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2017 kwa mazungumzo
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongozana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein alipowasili Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2017 kwa mazungumzo
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein walipokutana Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein bwakiagana baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2017 PICHA NA IKULU.


  0 0
 • 03/19/17--13:30: mambo ya wasafi dot com


 • 0 0
 • 03/20/17--08:37: TAARIFA KWA UMMA


 • 0 0


  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Naibu meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto ameviomba vikundi vya Jogging kuanza kujisajiri hili waweze kupata fursa za mikopo kutoka Halmashauri zao.

  Kumbilamoto amesema hayo alipokuwa  akizungumza mwishoni mwa wiki na Vikundi mbalimbali vya Jogging katika Bonanza lililoandaliwa na Mzimuni Joger  na kushirikisha vikundi zaidi ya kumi .

  "kila Halmashauri ina mapato ambayo inatakiwa kutoa kwa vijana  ambayo ni asilimia 10 kwa vijana na vikundi vya kina mama hivyo vikundi vya Joging vinahusisha watu wote hao katika hivi vikundi vyetu" Amesema Kumbilamoto

  Amesema ufike wakati wa Halmashauri zote zitenge pesa za vijana na kuacha ujanja ujanja wa kukwepa kulipia fedha hizi kwani kama wanashindwa waje kujifunza Ilala hili waweze kuwakwamua vijana na kinamama.
   Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto, akizungumza wakati wa Bonanza la Klabu ya Mbio za pole za Mzimuni Joging
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Oamry Kumbilamoto akiongoza safu ya Wakimbiaji katika Bonanza la Mzimuni
   Wana vikundi wakikimbia katika Bonanza hilo la klabu ya Mzimuni.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  0 0


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
  BAADA ya kurejea kutoka nchini Zambia kwenye mchezo wa  kombe la Klabu Bingwa Afrika na kuondolewa kwenye michuano hiyo, kikosi cha Yanga kinatarajiwa kesho kuanza mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na michezo ya ligi kuu Vodacom.
  Yanga waliiondolewa kwenye michuano hiyo na kurejea kwenye kombe la Shirikisho barani Afrika ambapo kesho kutakuwa na  droo ya kupanga timu za kucheza hatua ya mtoano ya 32 na timu 16 kuingia makundi.

  Droo hiyo itapangwa kesho na michezo inatarajiwa kuanza kuchezwa Aprili 7 hadi 9 na atakayefanikiwa kushinda ataingia hatua ya makundi ya 16 bora.

  Akizungumza na Globu ya Jamii, Meneja wa timu ya Yanga Hafidh Saleh amesema kuwa kesho kikosi kitaanza mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya ligi na mivhuano mingine kwani hawatakuwa na muda wa kupoteza.

  "sisi  kama benchi la ufundi tunachofahamu ni kuwa tunaendelea na mazoezi kama kawaida lakini kuhusiana na mechi ya kirafiki na timu ya Polisi Dodoma ni suala la utawala labda umuulize katibu mkuu Charles Mkwasa," amesema Saleh baada ya kumuuliza kuhusiana na mechi ya kirafiki na Polisi Dodoma iliyopangwa kuchezwa Machi 25.
  Kwa sasa akili zetu zote ni kukipa muda kikosi kiweze kupata muda wa klupumzika na kujipanga kwa michezo inayofuata kwani wachezaji waliobaki ni wengi kuliko wale walioenda kwenye timu zao za Taifa kujumuika nao, saleh aliweka wazi msimamo wa benchi la ufundi.

  Hizi ndio timu zinazoweza kukutana na Yanga
  1. Maghreb Fez - MOROCCO
  2. Zesco - ZAMBIA
  3. Al Masry - MISRI
  4. Rayon Sports - RWANDA
  5. JS Kabyile - ALGERIA
  6. Plantinum Star - S. AFRICA
  7. Recretivo Libolo - ANGOLA
  8. Asec Mimosas - IVORY COAST
  9. Smouha - MISRI
  10. MC Alger - ALGERIA
  11. CS Sfaxien - TUNISIA
  12. Mbabane Swallows - SWAZILLAND
  13. Club African - TUNISIA
  14. Ittihad Thanger -  MOROCCO
  15. Supersport United - S. AFRICA
  16. Hillal Obayed - Sudan  0 0


  Na Dotto Mwaibale

  Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo inatarajia kufanya kongamano linalolenga maadili kwa Taifa nchini.

  Kongamano hilo litafanyika kesho kuanzia saa nne asubuhi Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Naibu Waziri wa wizara hiyo, Anastazia Wambura amesema ni wajibu kwa kila mwanajamii kuthamini, kuenzi na kuendeleza maadili mema, mila na desturi zinazofaa.

  “Serikali hususani wizara inajukumu la kutoa muelekeo na usimamizi kuhakikisha Taifa linaenzi na kuimarisha utambulisho wake na kujenga utamaduni huru na sio huria” alisemaWambura.

  Aidha Wambura alisema kuna fursa ya kubaini, kuenzi na kukuza, kuhifadhi na kurithisha utamaduni na sanaa vyenye kuzingatia na kuimarisha maadili, mila na desturi kwa kuleta maendeleo.

  “Wananchi wamekuwa wanaendelea kujihusisha na shughuli mbalimbali za Kifani, Sanaa na utamaduni ikiwemo ngoma za asili, filamu, muziki, jando, unyago, matambiko, Sherehe na maadhimisho mbalimbali” alisemaWambura.

  Ameongeza kuwa shughuli hizo ni halali ilimradi zifanywe kwa kuzingatia sheria na kanuni na msingi wa asili yake, kwa maana kwamba kama jambo ni la faragha na usiri libaki kwenye uhalisia wake na kuhusisha rika jinsia na asili yake.


  Naibu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Anastazia Wambura (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kongamano la maadili litakalofanyika kesho Uwanja wa Taifa kuanzia saa nne asubuhi. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa, Leah Kihimbi na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata), Godfrey Mngereza.
  Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata), Godfrey Mngereza (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
  Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

  0 0

   Katibu  wa Bunge ambaye pia ni msimamizi wa Uchaguzi wa Wawakilishi wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki Dkt. Thomas Kashililah  akizungumza na wawakilishi mbalimbali wa Vyama vya Siasa kuhusu uchaguzi wa Wawakilishi wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashiriki. Wa kwanza kulia kwake ni Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi. Kikao hicho kimefanyika leo katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam. 
   Katibu  wa Bunge ambaye pia ni msimamizi wa Uchaguzi wa Wawakilishi wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki Dkt. Thomas Kashililah  akizungumza na wawakilishi mbalimbali wa Vyama vya Siasa kuhusu uchaguzi wa Wawakilishi wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashiriki. Wa kwanza kulia kwake ni Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi. Kikao hicho kimefanyika leo katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
    Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi akifafanua jambo katika kikao hicho.
   Wawakilishi mbambali wa Vyama vya Siasa wakifuatilia kikao hicho.
  Wawakilishi mbambali wa Vyama vya Siasa wakifuatilia kikao hicho.
  (Picha na Ofisi ya Bunge)

  0 0

   Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) imesema zoezi la ubomoaji wa majengo yaliyomo katika hifadhi ya reli linaloendelea nchini limezingatia taratibu na sheria za uendeshaji wa reli na kwamba matangazo ya notisi ya kuwataarifu waanchi waliovamiwa hifadhi hizo zilizotolewa mapema ili wananchi hao waweze kuhama.

  akiongea leo Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi mtendaji RAHCO Bw. Massanja Kadagosi amesema Ubomoaji huo unaoendelea haupo kwa ajili ya kumuonea mtu bali upo kwa ajili ya kulinda miundombinu ya reli ikiwemo pia kujali usalama wa wananchi waliojenga kwenye hifadhi ya reli. ‘’Sheria ya Reli Na.4 ya mwaka 2002,kifungu cha 57 (2) kinabainisha kuwa mtu yoyote haruhusiwi kufanya ujenzi wowote katika hifadhi ya njia ya reli pasipo kibali cha RAHCO, kwani sheria hii inatamka wazi  kuwa mtu yeyote harusiwi kufanya ujenzi wowote katika eneo lilopangwa na mamlaka husika”
  Madagosi amesema kabla ya kuanza kuzibomoa nyumba hizo walitoa notisi mbali mbali ikiwemo tangazo la kuwataarifu wavamizi hao kupitia kwenye vyombo vya habari vya tarehe 25/4/2016, pamoja na kutoa barua kwa mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala ya kuwajulisha wananchi hao kuanza kuhama kabla yauvunjaji kuanza.

  Mbali na Barua hizo, amesema Bw. Kadagosi  tarehe 9 hadi tarehe 10 /2/2017 waliziweka nyumba alama ya X kwa wavamizi hao, analosema kuwa watu wanaosema wananchi hao wanaovunjiwa hakuwapata taarifa za kutakiwa kuvunjiwa nyumba si za kweli kwani taarifa zilitolewa. 

  Bw. Kadagosi amewataka wananchi waliovamia maeneo hayo kuhama mara moja kwani kukaa kwenye maeneo hayo sio tu ni kosa la jinai bali pia linahatarisha usalama wao.
  Mkurugenzi mtendaji  Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) Bw. Masanja Kadogosa akizungumza na waandishi  habari leo jijini Dar es Salaam kuzungumzia  zoezi la ubomoji wa nyumba zilizopo kwenye hifadhi ya reli
  Afisa Uhusiano wa RAHCO,Catherine Moshi  akitoa maelezo kwa waandishi wa habari waliokuwepo kwenye mkutano huo leo jijini Dar es Salaam
  Waandishi wa habari na watendaji wa RAHCO wakimsikiliza Mkurugenzi mtendaji  Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO),Masanja Kadogosa.


  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

   Timu zilizofuzu hatua ya makundi klabu bingwa Africa ni kama ifuatavyo

  1)Zanaco-Zambia
  2)Mamelodi sundwon-SA
  3)Wydad Casablanca-Morroco
  4)USM Alger-Algeria
  5)Cotton Sport-Cameroon
  6)Al-Merreikh-Sudan
  7)Al-Ahly-Egypty
  8)CAPS United-Zimbwabwe
  9)Al-Ahly Tripoli-Libya
  10)St George-Ethiopia
  11)Zamalek-Egypty
  12)As Vita-DRC
  13)Al Hilal-Sudan
  14)Esperence Tunis-Tunisia
  15)Ferroviario Beira-Mozambique
  16)Etoile du Sahel-Tunisia.                        

   Timu zilizotolewa klabu bingwa ambazo zitakwenda kucheza mchezo wa mtoano na timu 16 zilizofuzu caf confederation cup ili kupata team 16 zitakazocheza hatua ya makundi confederation cup ni zifuatazo

  1)Yanga-Tanzania
  2)KCCA-Uganda
  3)CF Mounana-Gabon
  4)CNaPS SPORT-Madagascar
  5)Rail Club Kadiogo-Burkinafaso
  6)Rivers united-Nigeria
  7)Tp Mazembe-DRC
  8)Bidvest Witts-SA
  9)FUS Rabbat-Morroco
  10)Leopard-Congo
  11)ASPL-Mauritious
  12)Enugu rangers-Nigeria
  13)Gambia port-Gambia
  14)Tanda-Ivory Coast
  15)Horoya AC-Guinea
  16)BYC-Liberia

  0 0

   Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Peter Makakala alipofika Ikulu Mjini Unguja kujitambulisha leo akiwa na ujumbe aliofuatana nao.
   Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  akizungumza na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt.Anna Peter Makakala alipofika Ikulu Mjini Unguja kwa ajili  ya kujitambulisha leo
  Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  (kulia) akifuatana na mgeni wake   Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt.Anna Peter Makakala alipofika Ikulu Mjini Unguja leo kujitambulisha  kwa Rais  akiwa na ujumbe aliofuatana nao. 
  Picha na IKULU.

  0 0


  Na Shamimu Nyaki-WHUSM
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye ameunda kamati ya watu watano itayoongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt.Hassan Abbas kuchunguza tukio la uvamizi lilofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika chombo cha habari cha Clouds Media.
  Akiongea katika ziara aliyoifanya  leo  Jijini Dar es Salaam  katika chombo hicho Mhe.Nape amesema Kamati hiyo itafanya kazi ndani ya masaa 24 kuanzia sasa huku akiwataja wajumbe wengine  kuwa ni Bw. Frank Balile,Bibi.Johanes Neng’ida,Bw.Jessy Kwayu na Bibi. Mabel Mabisa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Serikalini (TCRA).
  “Kamati hii ipo kwa ajili ya kupata maelezo ya kutosha kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw.Paul Makonda ili tuwe na taarifa iliyokamilika na kujua hatua itakayofuata” alisema Mhe.Nape
  Aidha Waziri Nape ameeleza kuwa kitendo cha uvamizi kilichofanywa na Mkuu wa Mkoa kipo kinyume na Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari ya mwaka 2016 kwa kuwa sheria hiyo ipo kwa ajili ya kulinda wanatasnia hao.
   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo katika Picha) alipofanya ziara katika Chombo cha Habari cha Clouds leo Jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye Katikati, akimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Nchini (MOAT) Bw. Reginald Mengi (kulia) alipofanya ziara katika chombo cha Habari leo Jijini Dar es Salaam ,kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt. Hassan Abbas.
   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Bw.Joseph Kusaga (wa pili kushoto) alipowasili katika ofisi hizo leo Jijini Dar es Salaam, wengine ni Mkurugenzi wa Idara ya habari Maelezo Dkt.Hassan Abbas (pembeni ya Waziri) na wa kwanza kushoto ni Afisa Mahusiano wa Clouds Bw. Simon Simalenga.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0  0 0

  Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kuondoa Umasikini Tanzania (PFT), Mbunge mstaafu wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (kulia), akibadilishana mawazo na baadhi ya Maofisa wa Benki ya Kiislamu ya Amana, wakati alipofika kwenye ukumbi wa PTA, viwanja vya Sabasaba kuufungua mkutano wa wanachama wa Vicoba wa Wilaya ya Temeke na benki hiyo, mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kuondoa Umasikini Tanzania (PFT), Mbunge mstaafu wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akisalimiana na baadhi ya wanachama wa vikundi mbalimbali vya Vicoba, wilayani Temeke, wakati alipofika kwenye ukumbi wa PTA, viwanja vya Sabasaba kuufungua mkutano wao na Benki ya Kiislamu ya Amana, jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kuondoa Umasikini Tanzania (PFT), Mbunge mstaafu wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akizungumza na wanachama wa vikundi mbalimbali vya Vicoba, wilayani Temeke, alipoufungua mkutano wao mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Edwin Rutageruka na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha biashara cha benki hiyo, Munir Rajab.
  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Edwin Rutageruka, akizungumza na wanachama wa vikundi mbalimbali vya Vicoba, wilayani Temeke, wakati wa ufunguzi, wa mkutano wao, ukumbi wa PTA, Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kuondoa Umasikini Tanzania (PFT), Mbunge mstaafu wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu, wa pili kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha biashara cha benki ya Amana, Munir Rajab na wa kwanza ni Mkuu wa Masoko wa benki  hiyo, Dassu Mussa.
  0 0

  Na Daudi Manongi-MAELEZO
   
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli ametoa wito kwa Watanzania kuulinda mradi wa barabara za juu kwenye makutano ya barabara za Morogoro,Mandela na Sam Nujoma eneo la Ubungo Jijini Dar es Salaam utakaogharimu shilingi bilioni 188 na kukamilika mwaka 2019.
   
  Rais Magufuli ameyasema hayo wakati akitoa hotuba kabla ya kuweka jiwe la msingi la barabara za juu eneo la Ubungo.
   
  “Tutasimamia pesa izi kikamilifu ili tujenge barabara izi za juu vyema,nawataka Watanzania kusimamia mradi huu ili ukamilike haraka na hivyo Wizara,Mkandarasi na Msimamizi wa mradi ili ulete ukamilike na kuleta tija kwa wananchi hawa”,Aliongeza Rais Magufuli.
   
  Amesema katika ujenzi wa mradi huo bilioni 1.9 inatoka Serikalini na bilioni 186 inatoka Benki ya Dunia na ivyo ni muhimu kuulinda kwani ni pesa za Watanzania walipa kodi.
   
  Aidha amesisitiza kuwa nchi ya yetu imepata mkopo huu  kwa sababu tunaaminika katika kukopesheka na tunarudisha kwa wakati,amemuomba rais wa benki ya Dunia  kuendelea kuikopesha Tanzania katika miradi mingine.
   
  Rais Magufuli ameeleza kuwa mkopo huu kutoka benki ya Dunia una riba ya asilimia 0.5 na unalipwa ndani ya miaka 40 ivyo ni vyema kuendelea kushirikiana na Benki ya Dunia.
   

  0 0

  Daktari Bingwa Mshauri Mwandamizi wa Magonjwa ya Moyo Kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Morogoro na Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Mtakatifu Fransisco, Dkt Harun Nyagori, ametunukiwa  Tuzo ya Heshima katika fani hiyo fani (FELLOW OF AMERICA COLLEGE OF CARDIOLOGY) na Kutambuliwa na Chuo Kikuu Cha Maradhi ya Moyo jijinin Washington DC, Marekani,  leo.
  Akiongea baada ya kupokea zawadi  hiyo kwa njia ya simu  Dkt Nyagori anasema leo ilikuwa ni siku pekee ya Kuonyesha Ulimwengu kwamba Tanzania pia inaweza na kwa kutimiza ndoto yake ya kuipatia Heshima Tanzania ili itambulike  kuwa ina Wataalamu wanaoweza kufanya Utafiti Mbali mbali wa Maradhi ya Moyo.
  Dkt Nyagori amepongezwa sana na Watanzania na Wanasyansi mbalimbali Nje na ndani ya nchi. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu mbariki Daktari wetu na wanataalauma Mbalimbali walioonyesha mfano kama Daktari wetu huyu. 

  Dkt Harun Nyagori akipozi baada ya kutunukiwa  tuzo ya Heshima katika fani hiyo fani (FELLOW OF AMERICA COLLEGE CARDIOLOGY)  toka  Chuo Kikuu Cha Maradhi ya Moyo mjini Washington DC, Marekani,  leo. 
  Dkt Harun Nyagori akipongezwa baada ya kutunukiwa  tuzo ya Heshima katika fani hiyo fani (FELLOW OF AMERICA COLLEGE CARDIOLOGY)  toka   Chuo Kikuu Cha Maradhi ya Moyo mjini Washington DC, Marekani,  leo.

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina Mdeme akizungumza na Kamati ndogo ya Mkoa inayoratibu Ujenzi wa mradi wa Uwanja wa Michezo wa Kimataifa utakojengwa katika kata ya Nala Mjini Dodoma.
   Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Mkoa ya Uratibu Mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Kimatafa Bw.Salum Mkuya akitoa mrejesho wa mambo yaliyofanywa na Kamati yake kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina Mdeme (Hayupo Pichani)   katika kuhakikisha Mradi huo unafanikiwa.
    Mjumbe wa hiyo ambaye ni Mwanasheria kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Evordy Kyando akifafanua jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina Mdeme (Hayupo Pichani)  wakati Kamati hiyo ilipokutana na Mkuu huyo wa Wilaya. 
   Mjumbe wa hiyo ambaye ni Afisa Tawala Wilaya ya Dodoma Bw. Hashimu Kitambuliyo akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina Mdeme (Hayupo Pichani) kuhusu mipango na mikakati iliyoweka na Kamati hiyo katika kufanikisha Mradi huo.Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma


  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema nia ya Uongozi wa Shirikisho la Viwanda Nchini India wa kuonyesha muelekeo wa kutaka kuwekeza miradi yao katika sekta ya Kilimo utaleta matumaini makubwa ya kuimarika kwa Uchumi Visiwani Zanzibar. 
  Alisema hatua hiyo itafungua milango ya Uwekezaji kwa Taasisi na Makampuni ya Uwekezaji ya Jimbo la Kerala Nchini India kuanzisha miradi yao Zanzibar hasa ikizingatiwa kwamba Utamaduni pamoja na mazingira ya pande hizo mbili yanafanana. 
  Balozi Seif Ali Iddi akiuongoza Ujumbe wa Viongozi Wawili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika mwanzo wa ziara yake ya Wiki Moja Nchini India alitoa Kauli hiyo wakati wa Kikao cha pamoja kati ya ujumbe wake na Uongozi wa Shirikisho la Viwanda Nchini India {CII} hapo katika Ukumbi wa Hoteli ya Kimataifa ya Crowne Plaza Mjini Kochi katika Jimbo la Kerala. 

   Ujumbe wa Serikali ya Zanzibnar ukiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Kulia ukifanya mazungumzo na Uongozi wa Shirikisho la Viwanda Nchini India {CII} hapo katika Ukumbi wa Hoteli ya Crowne Plaza Mjini Kochi Jimboni Kerala India.

  Balozi Seif wa Pili kutoka Kulia akiuongoza Ujumbe wa Zanzibar katika Mkutano na Uongozi wa Shirikisho la Viwanda Nchini India. Wa kwanza kulia ni Kaimu Balozi wa Tanzania Nchini India Balozi Mohamed Hija, Kulia ya Balozi Seif ni Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri asiye na Wizara Maalum Dr. Sira Ubwa Mamboya na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mihayo Juma N’hunga.
  Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Nd. Juma Ali Juma akitoa ufafanuzi wa Mikakati ya Zanzibar katika uimarishaji wa fursa za uwekezaji kwenye sekta ya Kilimo na Uvuvi kwa Uongozi wa Shirikisho la Viwanda Nchini India. Kushoto ya Ndugu Juma ni Afisa wa Ubalozi wa Tanzania Nchini India Bibi Haika Msuya na Katibu wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd.Abdulla Hassan Abdulla {Mitawi }.
  Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Waziri asiye na Wizara Maalum Dr. Sira Ubwa Mamboya akitoa uzoefu wake katika sekta ya Kilimo kwa Uongozi wa Shirikisho la Viwanda Nchini India ambao haupo pichani.
  Balozi Seif  wa nne kutoka kushoto waliokaa vitini na Ujumbe wake akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Shirikisho la Viwanda Nchini India mara baada ya kumaliza kikao chao cha ushirikiano. Kushoto ya Balozi Seif  ni Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda Nchini India Bwana  George Paul. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0  0 0

older | 1 | .... | 1618 | 1619 | (Page 1620) | 1621 | 1622 | .... | 3272 | newer