Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 160 | 161 | (Page 162) | 163 | 164 | .... | 3278 | newer

  0 0
 • 06/12/13--06:14: mapitio ya magazeti leo

 • 0 0

  Mjumbe wa NEC Phares Magesa akisalimiana na Mwenyekiti wa WAZAZI Temeke mama Sophia Kinega ambaye pia in Mwenyekiti wa TEWO Saccos mara baada ya mazungumzo yenye lengo la kusaidia kuimarisha Saccos hiyo kwa miradi ya kiuchumi kwa faida ya Watanzania wote. UMOJA NI USHINDI !!!!

  0 0

  Timu ya Benki ya NMB ipo kwenye maandalizi makubwa ya mechi kati yao na wabunge ambayo itachezwa siku ya jumamosi kwenye viwanja vya Jamhuri  hapa Dodoma. Ili kufanikisha mtanange huo Benki ya NMB imekabidhi jezi kwa Nahodha wa timu ya Bunge ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Kassim Majaliwa. Ni mtanange wa kukata na shoka ambao umesubiriwa kwa hamu na kwa muda mrefu na mashabiki wa timu hizo mbili.
   Mheshimiwa Kassim Majaliwa akipokea jezi kwa ajili ya mechi hiyo kati ya Wabunge na NMB  kutoka kwa Nahodha msaidizi wa timu ya NMB, Hezbon Mpate. Makabidhiano haya ya Jezi zenye thamani ya shilingi milioni tatu na laki saba yamefanyika katika viwanja vya bunge jijini Dodoma.


  Mheshimiwa Fatma Mikidadi akipokea jezi za mpira wa pete kutoka kwa nahodha wa timu ya mpira wa pete ya NMB Josephine Kulwa. Mechi zote zinatarajiwa kuchezwa siku ya jumamosi katika viwanja vya Jamhuri mjini Dodoma.
   Waheshimiwa wabunge pamoja na maofisa wa NMB wakizifurahia jezi mara baada ya makabidhiano rasmi.


  0 0

  Tanzania kupitia Mpango wa Damu Salama Tanzania itaungana na nchi nyengine Duniani katika sherehe za Kuwashukuru na kuwatambua Wachangia Damu Duniani siku ya Ijumaa ya tarehe 14 Juni, 2013 ambapo kitaifa sherehe hizo zitafanyika katika viwanja vya Mkendo Wialyani Musoma, mkoani Mara huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri mwenye dhamana Katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Mh. Dk. Hussein Mwinyi.

  Kwa Mujibu wa Mpango wa Damu Salama Tanzania, wananchi ambao wako katika mikoa mengine nje ya kanda ya ziwa wanaweza kujumuika na vituo vya Damu Salama vilivyo katika kanda zao ili kuweza kusheherekea na kujitolea damu siku hiyo.

  Aidha, sehemu zilizoanishwa na Mpango wa Damu Salama Tanzania ambapo sherehe hizo zitafanyika Kimkoa ni Makao Makuu ya Mpango wa Damu Salama Tanzania, Ilala Mchikichini kwa Mkoa wa Dar es salaam, Viwanja vya Tangamano kwa Mkoa wa Tanga, Mkoani Tabora Katika Kituo cha Damu Salama Kitete, Viwanja vya Luanda Nzovwe Jijini Mbeya, Kwa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi sherehe zitafanyika katika Bustani ya Mkapa, Morogoro katika Kituo cha Damu Salama Rwegosore, na Mkoani Lindi katika kituo cha Damu Salama Ilulu.

  Sherehe hizo za Kila mwaka zinalengo la kuamsha ari pamoja na kuongeza uwelewa juu ya mahitaji ya damu na umuhimu wa kuchangia damu kwa hiari ili kuokoa maisha ya watu wanaohitaji damu duniani ikiwa pamoja na kuwashukuru na kuwapongeza wachangia damu wote duniani.

  Kidunia sherehe hizi zitafanyika Jijini Paris, Ufaransa chini ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ikishirikiana na Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu (IFRC), Shirikisho la Kimataifa laTaasisi za Kuchangia Damu (IFBDO), na Jumuiya ya Kimataifa Mpango wa Damu Salama (ISBT). Ujumbe wa Mwaka huu ni TOA ZAWADI YA MAISHA. CHANGIA DAMU.

  Rafiki wa Damu Salama Tanzania inawaomba watanzania wote kujitokeza kwa wingi siku ya Ijumaa kuweza kujumuika pamoja katika sherehe hizi muhimu ambazo zinagusa moja kwa moja maisha ya mwanadamu. Mahitaji ya damu nchini bado ni makubwa na wahitaji wamekuwa wakiongezeka kila siku kutokana na Uzazi kwa kina mama, ajali na magonjwa ya saratani. Kama asilimia 1% tu ya watanzania watajitolea kutoa damu kwa mwaka basi Tanzania itaweza kuondokana na tatizo hili la upungufu wa damu.

  0 0

  Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati wa uzinduzi wa Kilimanjaro Music Tour unaotarajiwa kuanza wiki ijayo Mkoani Dodoma,wakati wa mkutano uliofanyika leo katika Hoteli ya Holiday Inn jijini Dar es Salaam.Kulia ni Rais wa Bendi ya Mashujaam,Charles Baba na Muimbaji wa nyimbo za kizazi kipya, Diamod Platinam.
  Mwimbaji wa nyimbo za nyimbo za kizazi kipya,Diamond Platinam (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Kilimanjaro Tour uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe na Rais wa Bendi ya Mashujaam,Charles Baba.
  Mwimbaji wa nyimbo za kizazi kipya,Kala Jeremier (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Kilimanjaro Tour uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Wengine pichani toka kutoka kulia ni Rais wa Bendi ya Mashujaam,Charles Baba, Mwimbaji wa nyimbo za nyimbo za kizazi kipya,Diamond Platinam na Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe.
  Rais wa Bendi ya Mashujaam,Charles Baba(kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Kilimanjaro Tour ulifanyika Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe na Mwimbaji wa nyimbo za nyimbo za kizazi kipya,Diamond Platinam.
  Waimbaji na washindi wa tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013 wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Bia ya Kilimanjaro wakati wa uzinduzi wa Kili Muzic Tour uliofanyika leo katika Hotel ya Holiday Inn jijini Dar es Salaam.

  0 0


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Dkt. Idrisa Muslih Haji (kulia) akikabidhi sehemu ya Compyuta 15, kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya jimbo la Chwaha Bw. Muhammed Ali Selemani, ikiwa ni sehemu ya ahadi ya Mhe. Makamu, kwa Kituo hicho cha Chwaka Computer Training Center. Makabidhiano hayo yalifanyika jana Juni 11, 2013, kwenye Kituo hicho. Kulia ni Mtendaji Mkuu Ofisi ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Bw. George Mulamula.
  Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya jimbo la chwaka wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kusini Uguja, (hayupo pichanio) wakati alipokua akizungumza baada ya makabidhiano hayo, alipomwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dkt. Bilal.
  Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Dkt. Idrisa Muslih Haji (kulia) akikabidhiwa sehemu ya Compyuta 15, na Mtendaji Mkuu Ofisi ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Bw. George Mulamula, ambapo Mkuu huyo wa mkoa wa Kusini unguja, alizikabidhi kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya jimbo la Chwaha Bw. Muhammed Ali Selemani, kwa niaba ya Mhe. Makamu wa Rais Dkt. Bilal, kwa ajili ya Kituo cha Chwaka Compyuter Training Center, ikiwa ni sehemu ya ahadi ya Mhe. Makamu Dkt. Bilal kwa kituo hicho. Makabidhiano hayo yalifanyika jana Juni 11, 2013, kwenye Kituo hicho. Kulia ni . Kushoto ni Naibu Katibu wa Makamu wa Rais, Mohamed Khamis.
  Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Dkt. Idrisa Muslih Haji, akizungumza na Wajumbe wa kamati ya Maendeleo ya Jimbo la Chwaka mara baada ya makabidhiano ya Computer 15, ikiwa ni sehemu ya ahadi ya Makamu wa Rais Kwenye Kituo cha Chwaka Computer Training Center. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Chwaka Bw. Muhammed Ali (kushoto) ni Shekha wa Shehia ya Chwaka Bw. Msaraka Pinja na Mtendaji Mkuu wa Sayansi na Teknolojia Bw George Mulamula. Makabidhiano hayo yalifanyika jana Juni 11, 2013, kituoni hapo. Picha na OMR.

  0 0

  Pata majibu na maelezo ya maswali yafuatayo na matibabu ya njia rahisi kutoka blog ya Afya Njema; Mafanikio Na Utajiri (www.mtsimbe.blogspot.com)

  ·       Je Una Maumivi Ya Gouts (Viungo)?
  ·       Je Una Maumivu Ya Uti Wa Mgongo?
  ·       Je Una Tatizo la Kisukari?
  ·       Je Una Upara?
  ·       Je Ungependa Kuondoa Mabaka Mabaka Kwenye Ngozi?
  ·       Je, Nywele Zako Zinanyonyoka?
  ·       Je Una Fibroids Au Uvimbe Katika Kizazi?
  ·       Je Una Matatizo Ya Kushika Mimba?
  ·       Je Una Matatizo Na Siku Za Hedhi Au Maumivu?
  ·       Jinsi Ya Kupunguza Unene
  ·       Jinsi Ya Kuzuia Kumaliza Mapema
  ·       Je Jogoo Wako Hapandi Mtungi?
  ·       Je, Unapoteza Kumbukumbu?
  ·       Je, Ungependa Kuondoa Michirizi Katika Ngozi?
  ·       Jinsi Ya Kufanya Meno Yawe Meupe
  ·       Jinsi Ya Kuondoa Makunyanzi Ya Ngozi
  ·       Jinsi Ya Kufanya Matiti Yasimame (Yasilale)
  ·       Jinsi Ya Kuondoa Nywele Usoni
  ·       Je, Ungependa Kuwa Na Matiti Makubwa?
  ·       Je Macho Yako Hayaoni Vizuri?
  ·       Je, Una High Blood Pressure?
  ·       Je Una Allergies Na Kitu Chochote?
  ·       Jinsi Ya Kuondoa Vipele Vya Kunyoa Ndevu
  ·       Jinsi Ya Kuondoa Chunusi Usoni
  ·       Je Wewe Unakoroma Usiku Na Ungependa Uache?

  Kwa maoni tuandikie: mtsimbe@gmail.com

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Mh. Mwantumu Mahiza akihutubia katika mkutano wa wadau wa kuhamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Biama ya Afya uliofunguliwa leo mjini Kibaha,mkoani Pwani.
  Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dk. Mohammed Hashim (kulia) akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mh. Mwantumu Mahiza baada ya kufungua mkutano wa wadau wa mkoa huo wa kujadili uhamasishaji wananchi kujiunga na mfuko huo, leo mjini Kibaha. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba.
  Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba akielezea mikakati mbalimbali ya kuboresha mfuko huo nchini,wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa kuhamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Biama ya Afya uliofunguliwa leo mjini Kibaha,mkoani Pwani.


  0 0


  0 0

  Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Sera Uratibu na Bunge Mhe. William Lukuvi akipata maelezo kutoka wa Josephine Mwakapugi kuhusu huduma zipatikanazo katika simu za kiganjani za TTCL "SMART PHONE" pamoja na punguzo kubwa la bei ya Intarnet kwa simu zenye waya na zisizotumia waya "wireless".
  Waheshimiwa wabunge wakipata maelezo kuhusu mkongo wa taifa wa mawasiliano.
  Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akisikiliza maelezo kutoka kwa Bi. Sikitu Mwanakatwe kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na TTCL.
  Naibu waziri wa Nishati na madini Mheshimiwa Steven Masele akiweka saini katika kitabu cha wageni baada ya kupata maelezo kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na TTCL.

  0 0

  Meneja Masoko wa Steps Entertainment, Kambarage Ignnatus akionyesha moja ya tuzo zitakaotolewa kwa wasanii sikuya Jumamosi kwenye ukumbi wa Blue Pearl, Ubungo Plaza, kulia ni Mwakilishi wa kampuni ya Steps Solar, Johnson Mwamba.
  Mwakilishi wa kampuni ya Steps Solar, Johnson Mwamba (mwenye koti) akizungumzia udhamini wa kampuni yao katika tuzo za Steps Movie Award zilizopangwakufanyika Jumamosi kwenye ukumbi wa Blue Pearl.

  Kampuni ya usambazaji wa filamu Tanzania ya Steps Entertainment limited Jumamosi itatoa tuzo kwa wasanii, Watayarishaji, Waongozaji, na wadau mbalimbali waliopo katika tasnia ya filamu Tanzania.

  Mratibu wa tuzo hizo, Carlos Johns Silondwa alisema kuwa tuzo hizo zitafanyika kwenye ukumbi wa Blue Pearl Ubungo Plaza na zitawahusisha zaidi wasanii wanaofanya kazi na kampuni yao tu.

  Silondwa alisema kuwa kutakuwa na vipengele nane ikiwa pamoja na Filamu Bora ya Mwaka, Kampuni iliyotengeneza filabu bora, msanii anayependwa na watu ndani na nje ya mwisho, msanii bora chipukizi, muigizaji bora wa kike, muigizaji bora wa kiume, muongozaji bora wa filamu na mwandishi bora wa filamu.

  Silondwa alisema kuwa wameandaa tuzo hizo kwa lengo la kuanzisha tuzo hizo ni kuleta ushindani na kukubali mchango wa wasanii, watayarishaji na wadau wote kampuni inatumia fursa hii ya kuwatambua na kujali mchango wa wasanii katika ukuzaji wa filamu nchini Tuzo ni kichocheo kitakacholeta ushindani unaoweza kujenga tasnia ya filamu na kujenga ajira kwa jamii kubwa.

  Alisema kuwa tuzo hizo zimezingatia michango mbalimbali kutoka kwa wadau mbalimbali ambao wamekuwa mbele katika kutangaza tasnia ya filamu ndani na nje ya nchi kupitia njia mbalimbali, pia kutakuwa na tuzo za heshima kwa waliotangulia kuitambulisha tasnia ya filam u Tanzania.

  “Tunaamini kuwa tuzo zitakuwa kichocheo kikubwa cha kukuza tasnia ya filamu kuongeza ushindani katika kutengeneza filamu Bora, hadithi nzuri zinazoelimisha, kukuza na kuitangaza lugha ya Kiswahili nje ya mipaka ya Tanzania lugha ambayo imekuwa ikukua kila siku kwa kupitia filamu za kitanzania zinazopenyeza na kuvuka mipaka ya nchi,” alisema Silondwa.

  Alisema kuwa wanaarajia kuwa na Tuzo kubwa zitakazoshirikisha wadau wote kwa baadae, na kuwa ni moja kati ya moja ya kampuni wadhamini wa tuzo zenye mlengo wa kimataifa, mwaka huu kampuni imeandaa tuzo hizo pasipo kuwatumia wadhamini wa nje ya kampuni ikipata udhamini kwa kampuni ya Steps Solar pekee.

  0 0

  SAFARI ya kumpata Redd’s Miss Tanzania kwa mwaka huu, inazidi kunoga kwani kesho (Ijumaa) na keshokutwa (Jumamosi), kutakuwa na vinyang’anyiro katika sehemu mbalimbali nchini.

  Kazi kubwa inatarajiwa katika kumsaka Redd’s Miss Changombe, pale warembo zaidi ya 12 watakapopanda jukwaani, kumsaka mshindi kati yao.

  Kwa mujibu wa Mratibu wa Redd’s Miss Chang’ombe, kila kitu kimekamilika na shindano hilo linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa TCC Club, uliopo Chang’ombe, Dar es Salaam.

  Burudani katika onyesho hilo ambalo kiingilio chake kitakuwa Sh 20,000 inatarajiwa kutolewa na FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’.

  Pia kutakuwa na shindano la Redd’s Miss Iringa ambapo warembo watapanda jukwaani kusaka mwakilishi wa mkoa huo. Shindano hilo linatarajiwa kufanyika Ukumbi wa Highland.  Redd’s Miss Morogoro itafanyika Nashera Hotel, huku Redd’s Miss Mwanza ikiwa ndani ya Yacht Club na Redd’s Miss Central Zone, itafanyika katika Ukumbi wa Kilimani, Dodoma.

  Shindano hilo linatarajiwa kuendelea tena keshokutwa (Jumamosi) ambapo kutakuwa na Redd’s Miss Kilimanjaro na Redd’s Miss Kagera.

  Shindano la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original.

  0 0


  0 0

  Mr. Gerd akipanda katika basi la ABOOD kuangalia namna shughuli za usafirishaji wa abiria katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo ikiwa ni sehemu ya ziara hiyo katika kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi kati ya Jeshi la Polisi Nchini na Jeshi la Polisi Nchini Ujerumani Jimbo la Bavaria. Aliyesimama chini ni Mr. Wolfgang Sommer akiwa na Mkuu wa Polisi Usalama Barabarani Mkoa wa kipolisi wa Kinondoni SSP. Ibrahim Mwamakula. Kikosi kilitembelewa tarehe 11/06/2013.
  Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini DCP. Mohamed R. Mpinga akiwa eneo la taa za kuongozea magari za TAZARA akiwa na ugeni toka Bavaria Polisi Nchini Ujerumani akiwapa maelezo wageni wake namna askari wa usalama barabarani wanavyoongoza magari na changamoto wanazokutana nazo katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku. Kikosi kilitembelewa tarehe 11/06/2013.
  Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani DCP. Mohammed Mpinga wa (pili kutoka kulia) akifafanua jambo kwa wageni waliofika Nchini kwa ziara ya kikazi kujionea namna kikosi cha usalama barabarani Nchini kinavyoendesha kazi zake katika kusimamia suala zima la usalama barabarani. Kutoka kulia kwa kamanda ni ACP. Nyambabe wa Polisi Makao Makuu DSM, Mr.wolfgang Sommer na Mr. Gerd Enkling kutoka Polisi Bavaria Ujerumani, wakifuatiwa na Mr. Conrad wa Hans siedel Foundation na Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Kipolisi wa Temeke ASP. Prackson Rugazia. Kikosi kilitembelewa tarehe 11/06/2013.
  Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania DCP- Mohammed Mpinga (katikati) akiwa kituo kikuu cha mabasi Ubungo pamoja na wageni kutoka Polisi wa Bavaria Nchini Ujerumani waliofika Nchini kwa ziara ya kikazi. Hapa kamanda Mpinga akiwapa maelezo kuhusu utendaji kazi wa kila siku wa askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani. Kulia kwa Kamanda ni Mr. Gerd Enkling (Colonel) wa Bavaria Police Ujerumani, Kushoto kwa Kamanda ni Mr.Walfgeng Sommer (Commissioner) Bavaria Police Ujerumani, nyuma ya Kamanda ni Mr. Conrad wa Hans Siedel Foundation na kulia kabisa ni ACP. Nyambabe wa Polisi Makao Makuu DSM. Kikosi kilitembelewa tarehe 11/06/2013.

  0 0

  SIKU moja baada ya Simba kumalizana na mchezaji wake Amri Kiemba (pichani), mchezaji huyo sasa yupo sokoni na atauzwa kwenye timu ya Wydad Casablanca ya Morocco. Kiemba alimwaga wino wa kuichezea Simba kwa miaka miwili jana kwa dau la Sh35 milioni huku atakuwa akikunja mfukoni kitita cha Sh2 milioni kama mshara wake. 
   Awali mchezaji huyo alikuwa akiwaniwa na mahasimu wao Yanga, na Simba ingezubaa basi kiungo huyo angerejea nyumbani kwa mabingwa hao wa Tanzania bara. Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Zakaria Hanspope tayari ametua Morocco akitokea Tunisia ambako alikwenda kufatilia fedha zao za usajili wa mshambuliaji wao Emanuel Okwi anayekipiga kweney timu ya Etoile du Sahel nchini Tunisia. 
   Okwi alijiunga na timu hiyo ya Tunisia mapema mwaka huu baada ya Simba kumuuza kwa dola 300,000 lakini klabu hiyo ya Etoile Du Sahel imekuwa ikizingua kulipa fedha hizo. 
   Lakini jana Hanspope alisema "Nimeshatoka Tunisia nipo Moroco na nimeshafanya mazungumzo ya awali na viongozi wa Wydad Casablanca n kesho tunafanya mazungumzo ya mwisho kabla sijarejea Dar, kila kitu kinaenda vizuri, naamini tutafikia mwisho mzuri." 
   Simba waliingia mchecheto wa kumsajili mchezaji huyo baada ya kutonywa na kigogo mmoja wa TFF ambaye pia ni mnazi mkubwa wa Simba kuhusu timu hiyo kuvutiwa na Kiemba na kushauri asajiliwe haraka ili Simba wapate faida kwa kumuuza. 
   Casablanca walimuona mchezaji huyo wakati wa mchezo kati ya Stars na Morocco ambapo Stars ililala kwa mabao 2-1 goli ambalo la ni kufutia machozi lilifungwa na Kiemba.

  0 0
 • 06/12/13--12:15: Article 2


 • 0 0

  Meneja wa Biashara wa benki ya CRDB tawi la UDOM, Danford Muyango akitoa mada kongamano la kimataifa la vyuo vikuu vya Afrika Mashariki kuhusu ujasiriamali, ubunifu na uongozi. Vijana wasomi walikutana katika Chuo Kikuu cha Dodoma na kupata fursa ya kuelimishwa kuhusu ujasiriamali toka kwa watoa mada mbalimbali. Kongamano hilo liliandaliwa na taasisi ya kuchipua na kuendeleza vipaji vya uongozi kwa vijana (AISEC) na kudhaminiwa na Benki ya  CRDB.
  Meneja wa Benki ya CRDB tawi la UDOM, Emmanuel Chaburuma akifafanua jambo kuhusu kongamano hilo. 
   Rais wa AISEC Tanzania, Frank Mushi
   Mwanafunzi wa mwaka wa tatu  UDOM, Lulu Molel akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kongamano hilo. 
   Baadhi ya wanafunzi wakionesha vipaji vyao 
  Wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali wakiwa katika kongamano la kimataifa la vyuo vikuu vya Afrika Mashariki kuhusu ujasiriamali, ubunifu na uongozi. Vijana wasomi walikutana katika Chuo Kikuu cha Dodoma na kupata fursa ya kuelimishwa kuhusu ujasiriamali toka kwa watoa mada mbalimbali. Kongamano hilo liliandaliwa na taasisi ya kuchipua na kuendeleza vipaji vya uongozi kwa vijana (AISEC) na kudhaminiwa na Benki ya  CRDB.


  0 0

  NA MAGRETH KINABO- MAELEZO

  BARAZA la Uuguzi na Ukunga Tanzania limetoa agizo kwa mtu, kikundi au taasisi inayoendesha mafunzo ya uuguzi na ukunga bila kuwa na kibali kufunga mara moja.

  Aidha baraza hilo limewataka wamiliki wa vyuo hivyo, wafuate taratibu zinazotakiwa ili kuhakikisha vyuo vyao vinasajiliwa.

  Kauli hiyo imetolewa leo na Msajili wa vyuo hivyo kutoka katika baraza hilo, Lena Mfalila wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari- MAELEZO jijini Dares Salaam.

  Alisema baraza hilo ,linafanya kazi chini ya sheria inayoitwa ‘The Nursing and Midwifery Act’ ya mwaka 2010 namba 1 ili kuhakikisha kuwa huduma za afya inayotolewa kwa umma ni bora na salama.

  “Kuanzia sasa baraza halitasita kuchukua hatua za kisheria kwa wle wote watakaokiuka agizo hili, ni vyema tukazingatia wito wa kutii sheria bila shuruti,” alisema Mfalila.

  Aliongeza kuwa kuanzisha mafunzo ya uuguzi bila kibali cha mamlaka husika, ambayo ni baraza hilo ni uvunjaji wa sheria. Hivyo katika sheria ya baraza hilo kifungu namba 41 kinaeleza hatua zinazopaswa kuchukuliwa dhidi ya mtu,taasisi,kikundi chochote kitakachokiuka sheria hii.

  Akifafanua kuhusu kifungu hicho, Afisa Muuguzi Mkuu –Kitengo cha Mipango na Fedha alisema , Andrew Kapaya alisema sheria iko wazi kifungu cha 41 sehemu ya nane inatoa adhabu kwa mtu atakayekiuka kuwa atatoa faini ya sh.milioni tatu au sh. milioni tano au kifungo cha miaka mitano au vyote kwa pamoja.

  Hata hivyo Mfalila alisema wana mpango wa kuanzisha utaratibu mpya wa kufanya kazi kwa pamoja yaani wataalamu kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wa kitengo hicho, baraza hilo na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) ili kuhakikisha vyuo vya taalauma hivyo vimekidhi masharti ya usajili.

  Baraza hilo limewataka wananchi kuacha kuandikisha vijana wao katika vyuo ambavyo vinaendesha mafunzo kinyume na utarati bu kwa kuwa wale wote wanaohitimu katika vyuo hivyo hawatambuliwa na baraza hilo na hawatasajiliwa kama wauuguzi wa wakunga hapa nchini na duniani kote.

  0 0

  Mkurugenzi wa huduma za kibenki kwa wateja wakubwa wa Benki ya KCB Tanzania Frank Nyamundege akitoa mada juu ya huduma za benki hiyo wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam juzi.
  Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya KCB Tanzania Moezz Mir akiwahutubia wageni waalikwa wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam juzi.
  Mwenyekiti wa bodi ya Benki ya KCB Tanzania Dk Edmund Mndolwa (kushoto) akibadilishana mawazo na mjumbe wa bodi Nehemiah Mchechu (katikati) pamoja na mkuu wa kitengo cha sheria na katibu wa benki hiyo Edward Lyimo, muda mfupi kabla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam juzi.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

older | 1 | .... | 160 | 161 | (Page 162) | 163 | 164 | .... | 3278 | newer