Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109606 articles
Browse latest View live

MV KAZI YASHUSHWA MAJINI

0
0
 Kivuko cha MV KAZI kikielea majini baada ya kushushwa kwa mara ya kwanza tayari kwa kufanyiwa ukaguzi wa mwisho kabla ya kuanza kazi. Kivuko hicho kitakua kikitoa huduma zake kati ya Magogoni na Kigamboni na kitakua na uwezo wa kubeba abiria 800 na magari 22 kwa wakati mmoja.

 Muonekano wa kivuko kipya cha MV KAZI mara baada ya kushushwa majini kwa mara ya kwanza tayari kwa kufanyiwa ukaguzi wa mwisho kabla ya kuanza kazi, kivuko hicho kitatoa huduma zake kati ya Magogoni na Kigamboni na kitakua na uwezo wa kubeba abiria 800 na magari 22.

 Kivuko cha MV KAZI kikisubiri kushushwa kwa mara ya kwanza majini kufanyiwa ukaguzi wa mwisho, kivuko hicho kitakua kikitoa huduma zake kati ya Magogoni na Kigamboni na kitakua na uwezo wa kubeba abiria 800 na magari 22.

 Kivuko cha MV KAZI mara baada ya kushushwa majini kwa mara ya kwanza tayari kwa kufanyiwa ukaguzi wa mwisho kabla ya kuanza kazi, kivuko hicho kitatoa huduma zake kati ya Magogoni na Kigamboni na kitakua na uwezo wa kubeba abiria 800 na magari 22.

Mkurugenzi wa kampuni ya MS Songoro Marine Boatyard ya jijini Mwanza Major Songoro mwenye kofia akiwa kwenye kivuko cha MV KAZI mara baada ya kukishusha majini kwa mara ya kwanza tayari kwa ukaguzi wa mwisho. Kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba abiria 800 na magari 22 kitakua kikitoa huduma zake kati ya Magogoni na Kigamboni.

PICHA ZOTE NA LAFRED MGWENO (TEMESA)




RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA AFYA WA KENYA KUHUSU TANZANIA KUPELEKA MADAKTARI 500(WASIO NA AJIRA SERIKALINI) KWENDA KUFANYA KAZI NCHINI KENYA

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu aliyefika Ikulu pamoja na ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu kuhusu Tanzania kupeleka madaktari 500 nchini Kenya, Ajira za Madaktari hao zitatangazwa mara moja na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu na zitawahusu Madaktari ambao hawajaajiriwa Serikalini(hawapo katika utumishi wa umma au taasisi za serikali) waliomaliza mafunzo kwa vitendo na ambao wamesajiliwa na Baraza la Madaktari la Tanganyika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na ujumbe kutoka nchini Kenya uliongozwa na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu Ikulu jijini Dar es Salaam.



Introducing Dr. Asha- Rose Migiro by Wasanii Tanzania Uingereza (WASATU)

SIMU TV: YALIYOJIRI KATIKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI LEO

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AONDOKA NCHINI KWENDA MOURITIUS KUMWAKILISHA JPM KATIKA UZINDUZI WA JUKWAA LA UCHUMI LA AFRIKA

0
0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kwenye uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam kabla ya kuondoka nchini kwenda Port Louis, Mauritius kumwakilisha Rais John Magufuli katika Uzinduzi wa  Jukwaa la Uchumi la Afrika (The Inaugural  Session of The African Economic Platform) , Machi 18, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA MKUTANO WA DHARURA WA WAKUU NCHI NA SERIKALI WA JUMUIYA YA SADC.

0
0



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo March 18,2017 amehudhuria mkutano wa dharura wa  Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa Afrika SADC akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, mkutano huo umefunguliwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mfalme Mswati wa III wa Swaziland mjini Mbabane Swaziland ambapo amezitaka Nchi wanachama wa SADC kuimarisha ushirikiano katika utekelezaji wa maendeleo ya Jumuiya hiyo kama hatua ya kuwakwamua wananchi na umasikini

WASHINDI MICHUANO YA GOFU YA BRITAM WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO

0
0
Zaidi ya wachezaji 100 walishiriki michuano hiyo ya gofu ya Britam huku Adam Ngamilo akiibuka mshindi wa jumla baada ya kupata pointi 39 katika mashimo 18 aliyocheza katika klabu ya Gymkhana Dar es Salaam.

Aidan Nziku alikuwa mshindi kwa upande wa wanaume, akipata pointi 37 na Mary Kinusia akiibuka mshindi kwa upande wa wanawake baada ya kupata pointi 38.

Mkurugenzi Mtendaji wa Britam Tanzania, Steven Lokonyo amesema watadhamini tena michuano hiyo ili kuendeleza gofu na michezo mingine klabuni hapo.
" Kampuni yetu ipo Afrika yote ya Mashariki na huko kote tunadhamini michezo".

" Nchini Kenya tunadhamini michuano ya wazi ya Safari ya Tennis ( Safari Open ) na klabu ya Mathare United, Hii ni sehemu tu ya mchango wetu", alisema bosi huyo wa kampuni hiyo inayojihusisha na aina zote za bima.

Amesema kampuni yake ina wataalamu waliobobea katika masuala ya bima zote na siku zote wateja wao wamekuwa katika mikono salama.
"Popote upo salama ukiwa na Britam, tunatoa aina zote za bima kwawatu binafsi, vyombo vya moto, bima kwa wasafiri, wachezaji, majengo na vingine vingi ikiwa bima ya afya ambayo iko mbioni kuanzishwa", alisema Lokonyo.

magazeti ya leo jumapili machi 19, 2017


TANZANITE ONE WATOA MILIONI 20 KWA SACCOS YA MADALALI WANAWAKE WA MADINI ARUSHA

0
0

ANDREA NGOBOLE, PMT

Kampuni ya Tanzanite One, imetoa msaada wa Sh 20 milioni kwa chama cha Madalali wanawake,wanaouza madini ya Tanzanite mkoani Arusha .

Wakurugenzi wa kampuni hiyo, inayomilikiwa kwa pamoja na kampuni ya Sky Associate Ltd na shirika la madini la taifa(STAMICO), Faisal Shabhai na Hussein Gonga walitangaza uamuzi huo wakati wakizungumza na madalali , katika ukumbi wa polisi jijini hapa.

Faisal alisema kampuni yao ambayo inachimba Tanzanite, imetoa msaada wa sh 20 milioni,ili kuendelea kutekeleza mahusiano mema na wadau wa Tanzanite na jamii ya wanawake ambao wanajihusisha na biashara ya kuuza madini hayo.

Alisema msaada huo, umetokana na maombi ya wanawake hao, kusaidiwa waliyotoa katika mkutano wa mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na viongozi wa Tanzanite One.

Katika hatua nyingine kampuni hiyo imetenga kiasi cha sh 200 milioni kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa hospitali ya kisasa Mererani.

Madini ya Tanzanite ambayo yanapatikana eneo la mererani pekee duniani yakiwa tayari yamekatwa na kusanifiwa sasa yatauzwa kimataifa katika kituo kitakachonjengwa Arusha
Mtaalamu wa kukata madini Adam Idd Lacha akiwa anakata na kusanifu madini ya Tanzanite ya kampuni ya Tanzanite one ambayo ndio inatoa mafunzo hayo. 
Waziri wa nchi ofisi ya Rais (TAMISEMI) George Simbachawene akiwa anapewa maelezo juu ya madini ya Tanzanite , na wakurugenzi wa Tanzanite One, Faisal Juma na Hussein Gonga. Alipokuwa katika kituo cha kuuza madini cha kampuni hiyo. 


mgogoro wa ardhi wa mipaka uliodumu kwa takribani miaka 33 watatuliwa wilayani ikungi

0
0
MKUU wa Wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu (mwenye miwani) amefanikiwa kutatua mgogoro wa ardhi wa mipaka uliodumu kwa takribani miaka 33 sasa kati ya wananchi,kituo cha kufundishia wanyama kazi(OTC) na kituo cha utafiti wa mifugo(Veterinary)vilivyopo katika kijiji cha Muungano wilayani humo.

Machi 4 mwaka huu Mtaturu alifanya kikao cha awali  na familia zipatazo 21 ambazo zilieleza kutoridhishwa na kitendo cha  kituo kumiliki hekari 320 ambapo mipaka yake iliongezwa bila ya kuwashirikisha  hali iliyomlazimu kuamua kutembelea eneo husika ili kuona namna ya kutatua mgogoro huo.

Baada ya saa nne za mjadala akiwa eneo la tukio alibaini uwepo wa mipaka iliyosogezwa  kwenye maeneo ya wananchi bila ya kuwashirikisha ikiwemo kuingilia makaburi na hivyo kushauri wananchi kurejeshewa hekari 100 kutoka kituo cha OTC na eneo la mita za mraba 3,093 kutoka kituo cha Veterinary..
 “Ili mgogoro huu umalizike inabidi tufanye maridhiano na katika maridhiano kuna utaratibu hufanyika wa nipe nikupe yaani give and take na katika maeneo ambayo wananchi wameingia kwenye mpango mji ufidiwaji utazingatiwa kwa mujibu wa sheria namba 4 ya mwaka 1999,”alisema Mtaturu.

Baada ya maridhiano hayo wataalam wa ardhi waliweka alama kwa kupima upya kwa GPS mbele ya wananchi  ambapo aliwashukuru wazee,viongozi na wananchi kwa ushirikiano uliosaidia kufikia maridhiano  na kumaliza mgogoro huku akitoa agizo kwa halmashauri kupitia idara ya ardhi na kilimo kuweka alama za kudumu kwenye mipaka zitakazosaidia kuondoa migogoro isiyo ya lazima.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Muungano Hussein Galawa kwa niaba ya wananchi alimshukuru mkuu huyo kwa kukubali kusaidia kutatua mgogoro huo wa muda mrefu na kumuomba kwenda kutatua mgogoro wa mipaka kati ya shule yao ya msingi na sekondari Unyahati na wananchi na kusisitiza wananchi kuwa watulivu badala ya kutuhumiana na kuchafua viongozi pindi inapotokea migogoro.

Wakizungumzia historia ya kituo cha OTC mwenyekiti mstaafu wa kijiji hicho mzee Emmanuel Humme,mwenyekiti wa zamani wa kamati ya uendeshaji kituo cha OTC mzee Juma Mwati na mzee Andrea Chima walisema kituo hicho kilianzishwa mwaka 1970 kikiwa na lengo la kufundisha wakulima na wafugaji ili kuleta tija na kilitumiwa kama kituo cha kugawa pembejeo mbalimbali za kilimo.

MEYA WA JIJI LA DAR KUCHANGIA MABATI NA MIFUKO YA SARUJI 100 UJENZI WA MADARASA YA SHULE YA MSINGI MAWENI, KIGAMBONI

0
0
MEYA wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ameahidi kuchangia mifuko 100 ya Saruji pamoja na Mabati 100 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi Maweni iliyopo Kata ya Mjimwema wilayani Kigamboni. Shule hiyo ambayo inaupungufu mkubwa wa madarasa pamoja na uzio wa shule , inajumla ya wanafunzi 1300 ikiwemo na wale wenye ulemavu.

Akizungumza katika hafla hiyo  ya chagizo kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, Meya Isaya alisema kwamba hatua hiyo ni kwa ajili ya kuzisaidia shule ambazo zinaupugufu wa madarasa ili kuwawezesha wanafunzi wasome katika mazingira salama.

Alisema kwamba wakati alipokuwa akiwania nafasi ya Udiwani Kwenye kata yake ya Vijibweni , na kisha kupata nafasi ya kuwa Meya wa jiji, moja ya vipaumbele vyake ilikuwa ni kuzisaidia shule ili  kuondokana na changamoto ya wanafunzi kukaa. 

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mjimwema, Selestine Maufi pamoja na mambo mengine alimpongeza Meya Isaya kwa kuunga mkono jitihada hizo zinazofanywa kwa ajili ya kujenga madarasa katika shule hiyo. Hata hivyo Diwani huyo aliahidi kuchangia matofali 500 ,madawati 60 kwa ajili ya vyumba viwili vya madarasa .

Hata hivyo awali akisoma lisara kwa mgeni rasmi iliyoandaliwa na uongozi wa shule hiyo, Mwalimu Selemani alisema kwamba shule hiyo inakabiliwa na upungufu wa vyumba kadhaa vya madarasa ambapo vilivyopo havikidhi mahitaji ya wanafunzi waliopo.

Alifafanua kwamba kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa wananfunzi wenye ulemavu wamelazimika kusomea kwenye chumba cha darasa kimoja jambo ambalo linawapa shida walimu kwenye ufundishaji.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita akizungumza katika mkutano na wananchi wa mtaa wa Maweni wakati wa harambee ya kuchangisha ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi ya Maweni iliyopo wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Mkuu wa Shule ya Msingi ya Maweni,Zuhura Mwaliko na Kushoto kwake ni Diwani wa Kata ya Mji Mwema,Celestine Maufi (Chadema) na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Maweni,Sylvester Roche.PICHA NA ELISA SHUNDA

Balozi wa Tanzania Nchini Ujerumani Amvisha Cheo Kanali wa JWTZ

0
0
Katika hali ambayo haijazoeleka na iliyoonekana kuwa ngeni, Balozi wa Tanzania Mhe. Philip Marmo alimvisha Cheo Kanali Joseph Bakari aliyepandishwa Cheo hivi karibuni kutoka Luteni kanali.
Hafla hiyo fupi iliyohudhuriwa na  ujumbe wa Watanzania waliohudhuria Maonesho ya Kimataifa ya Utalii Jijini Berlin Ujerumani akiwemo Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma, Mshauri wa Rais wa Zanzibar mambo ya Utalii na Utamaduni Mhe. Chimberi Heri, Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania  Mhe. Geofrey Meena, Maafisa wa Ubalozi na wageni wengine ilifanyika karibuni katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania zilizopo Berlin nchini Ujerumani.
Akitoa maelezo mafupi kuhusu tukio hilo  Mhe. Balozi Marmo alitanabaisha kuwa kwake ni tukio la kwanza na la aina yake kupewa dhamana hiyo  na kwamba amepokea maelekezo husika kutoka Makao Makuu ya Jeshi kupitia Wizarani. 
Akisoma sehemu ya maelekezo hayo alisema: “ kwa kawaida Afisa anapopanda cheo akiwa nje ya nchi, na  iwapo hataweza kwenda Tanzania kuvalishwa cheo hicho na viongozi husika wa JWTZ, cheo hicho kipya huvishwa na Afisa Mkuu au Balozi wa Tanzania katika Nchi aliyopo”. 
 Balozi wa Tanzania Mhe. Philip Marmo na  Acting Colonel Joseph Bakari wakisikiliza maelezo kabla ya hatua ya kumvua cheo cha zamani na kumvika kipya.  Kanali Joseph Bakari ni mwakilishi wa JWTZ katika Sekretarieti ya Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (International Military Sports Council-CISM) kama Mshauri na msaidizi wa Mkurugenzi wa Michezo katika Baraza hilo katika makao makuu yake Brussels, Ubelgiji.
 Balozi wa Tanzania Mhe. Philip Marmo akimvisha cheo kipya Colonel Joseph Bakari 
Balozi wa Tanzania Mhe. Philip Marmo akimvisha kofia ya cheo kipya Colonel Joseph Bakari 
 Balozi wa Tanzania Mhe. Philip Marmo akipikea zawadi maalumu ya  Sekretarieti ya Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (International Military Sports Council-CISM)  toka kwa Kanali Joseph Bakari wakati wa hafla hiyo

 Balozi wa Tanzania Mhe. Philip Marmo akiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma (kushoto)  Mshauri wa Rais wa Zanzibar mambo ya Utalii na Utamaduni Mhe. Chimberi Heri (wa pili kulia) Colonel Joseph Bakari na mkewe 
 Tukio hilo la kuvisha Cheo  lilihitimishwa na kuimbwa wimbo wa Taifa wa Tanzania.
 Picha ya pamoja na ujumbe wa Watanzania waliohudhuria Maonesho ya Kimataifa ya Utalii Jijini Berlin Ujerumani akiwemo Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma, Mshauri wa Rais wa Zanzibar mambo ya Utalii na Utamaduni Mhe. Chimberi Heri, Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania  Mhe. Geofrey Meena, Maafisa wa Ubalozi na wageni wengine katika hafla fup iliyofanyika karibuni katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania zilizopo Berlin nchini Ujerumani.

WAKAZI WA MJI WA KIBAHA WATAKIWA KUTUNZA MIUNDOMBINU YA MIRADI YA MAJI

0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

MHANDISI wa maji katika halmashauri ya Mji wa Kibaha,Grace Lyimo,amewataka wakazi wa mji huo kulinda na kuitunza miundombinu na mifumo ya miradi mbalimbali ya maji safi kwani maji ni uhai kwa afya na maisha yao.

Amesema baadhi ya watu wamekuwa wakiharibu miundombinu hiyo kwa kuikata ama kupasua kwa makusudi hali inayosababisha uchafuzi wa mazingira ikiwemo matope na kusababisha hasara .

Akizungumza wakati akiwa kutembelea miradi mbalimbali ya maji Grace alisema ,miradi mingi inatumia fedha nyingi kutoka bank ya dunia na mengine serikali kuu hivyo kila mmoja athamini miradi hiyo.

Alieleza kwamba ujumbe wa maadhimisho ya wiki ya 29 ya maji 2017 unaenda sambamba na  shughuli zitakazofanywa mjini hapo. Hata hivyo mhandisi huyo wa maji alisema,walianza kutembelea  kituo cha maji cha jumuiya ya maji Zojosa ,kituo ambacho kinalisha maji mitaa mitatu ya Zogowale,Jonung’ha na Saeni na kupanda miti 50.

"Tutakagua pia miradi mbalimbali na viwanda ikiwemo kiwanda cha ngozi na kiwanda cha viuadudu vya kuzuia mazalia ya mbu  ambapo march 22 tutaadhimisha wiki ya maji kwenye mradi wa maji Saeni huko Viziwaziwa " alibainisha Grace.

Nae katibu wa kituo  cha jumuiya ya maji ZOJOSA, Said Kondo alisema,mradi huo umefadhiliwa na bank ya dunia kwa gharama ya mil .109. Alielezea watumiaji maji hadi sasa ni 2,500 kwa siku wanalisha lita  50,000 na kupampu maji masaa  sita.

Kondo alisema walianza na vituo 8 sasa vipo 56 na malengo yao  ni kufikia wanachi kwa asilimia 80 na zaidi ya hapo . "Tunachangamoto ya wateja wetu kutolipa bili  kwa wakati lakini tuna zaidi ya mil.3.4 bank kwa sasa " alisema Kondo .

Mgeni rasmi ambae ni mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Kibaha,Leonard Mloe aliomba mradi huo utunzwe na kusimamia makusanyo.

Uzinduzii wa wiki ya maji duniani umeanza march 16 na kilele chake kitakuwa march 22 .

MAKADA WA CCM WACHUKUA FOMU KUWANIA NAFASI YA UBUNGE, BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI.

0
0
 Katibu Msaidizi Idara ya Organizeshen CCM Ofisi ndogo Dar es Salaam, Said Bakari Is-hak (kulia) akimkabidhi fomu za kugombea nafasi ya Ubunge, Bunge la Afrika Mashariki, Kada wa CCM, Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani, Dkt. Egina Makwabe, wakati wagombea hao walipofika kuchukua fomu hizo kwenye Ofisi ndogo za CCM zilizopo Lumumba jijinin Dar es Salaam, leo. 
 Katibu Msaidizi Idara ya Organizeshen CCM Ofisi ndogo Dar es Salaam, Said Bakari Is-hak (kulia) akimkabidhi fomu za kugombea nafasi ya Ubunge, Bunge la Afrika Mashariki, Kada wa CCM, Leonce Nicholaus Mulenda, wakati wagombea hao walipofika kuchukua fomu hizo kwenye Ofisi ndogo za CCM zilizopo Lumumba jijinin Dar es Salaam, leo. 
 Katibu Msaidizi Idara ya Organizeshen CCM Ofisi ndogo Dar es Salaam, Said Bakari Is-hak (kulia) akimkabidhi fomu za kugombea nafasi ya Ubunge, Bunge la Afrika Mashariki, Kada wa CCM, Zainab Kawawa, wakati wagombea hao walipofika kuchukua fomu hizo kwenye Ofisi ndogo za CCM zilizopo Lumumba jijinin Dar es Salaam, jana. Katikati ni dada zake Mariam Kawawa na Zamaradi Kawawa.  Picha na Mafoto Blog
 Katibu Msaidizi Idara ya Organizeshen CCM Ofisi ndogo Dar es Salaam, Said Bakari Is-hak (kulia) akimkabidhi fomu za kugombea nafasi ya Ubunge, Bunge la Afrika Mashariki, Kada wa CCM, anayetetea nafasi yake, Charles Makongoro Nyerere, wakati wagombea hao walipofika kuchukua fomu hizo kwenye Ofisi ndogo za CCM zilizopo Lumumba jijinin Dar es Salaam.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MBUNGE WA JIMBO LA TANGA AENDELEA KUTATUA KERO ZA WANANCHI JIMBONI KWAKE,AKABIDHI BAISKELI KWA MLEMAVU

0
0
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF),Alhaj Mussa Mbaruku akiendeseha baiskeli hiyo kabla ya kumkabidhi mkazi wa Makorora Mbwana Hamisi leo kwa ajili ya matumizi yake kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Makorora Ally Kivurande 

Mbunge wa Jimbo la Tanga(CUF), Alhaj Mussa Mbaruku akizungumza na wananchi wa Makorora Jijini Tanga leo wakati wa Hafla ya Makabidhiano hayo
Mbunge wa Jimbo la Tanga(CUF),Alhaj Mussa Mbaruku kushoto akimkabidhi Baiskeli Mlemavu wa miguu Mbwana Hamisi Mkazi wa Makorora Jijini Tanga ili iweza kumsaidia kutembea kwenye shughuli zake ambapo baiskeli hiyo ina thamani ya zaidi ya milioni moja.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Makorora Ally Kivurande aliyevaa kanzu akimshukuru Mbunge huyo aliyesimama kulia akisalimia na mama mzazi wa Mlemavu huyo Mariam John.

USIKU WA MISS PENDO KISAKA NA MWANAHABARI GEORGE BINAGI WAFANA

0
0
Ijumaa March 17, 2017 kuamkia  ilikuwa ni siku muhimu kwa Malikia wa nguvu, Pendo Kisaka, ambapo ndugu, jamaa na marafiki zake walijumuika naye kwenye Sendoff yake kuelekea kwenye ndoa anayotarajiwa kufunga na mwanahabari/ mwanablogu, George Binagi, March 26, 2017 Jijini Mwanza.

Shughuli ilifanyika katika ukumbi wa Heinken, Mbagala Kijichi Jijini Dar es salaam. Ni mwendeleo wa kuelekea kwenye ndoa takatifu ya wawili hao iliyotangazwa March 12, 2017 kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza.
BMG
Bibi harusi mtarajiwa akimvisha saa mmewe mtarajiwa
Bibi harusi mtarajiwa (kulia) na best lady wake (kushoto)
Bibi harusi mtarajiwa akiwakabidhi keki wazazi wake na kusema ahsante kwa malezi yenu bora
Bibi harusi mtarajiwa, Pendo Kisaka (katikati), akimtambulisha mumewe mtarajiwa, George Binagi (kushoto).

MAULID YA KUMSALIA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) YAFANA SEGEREA MWISHO, DAR ES SALAAM

0
0
 Siku ya jumamosi ya 11 Machi 2017 katika viwanja vya Madrasat Rahman iliyopo Segerea Mwisho  jijini Dar-es-salaam palikuwa hapatoshi kwa mkusanyiko wa waumini wa dini ya Kiislam waliokusanyika katika shughuli ya kisomo cha Maulid ya kumsalia mtume Muhammad (S.A.W). Shughuli hiyo ya Maulid ilifana sana kwa kuhudhuriwa na wingi wa waumini , wanazuoni na viongozi mbali mbali wa dini hiyo. 
Unaweza kujumuika nao katika at  Rahman Madrasa Segerea





WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR MHE. MAHMOUD THABIT KOMBO AFUNGUA KITUO CHA AFYA NUNGWI

0
0
 Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akisalimiana na Dk,Ameesh Mehta mara baada ya kuwasili katika Ufunguzi wa Hospitali ya Dk,MEHTA(DR MEHTAS HOSPITAL)Ilioko Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
 Waziri wa Afya Mahmoud Thabit kombo akikunjuwa kitambaa ikiwa ni ishara ya Uwekaji wa jiwe la msingi la Hospitali ya Dk,Mehta(DR MEHTAS HOSPITAL)Ilioko Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
 Waziri wa Afya Mahmoud Thabit kombo akikata utepe ikiwa ishara ya Ufunguzi wa  Hospitali ya Dk,Mehta(DR MEHTAS HOSPITAL)Ilioko Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
 Waziri wa Afya Mahmoud Thabit kombo akipata maelezo kuhusiana na dawa kutoka kwa Dokta Mkuu Ameesh Mehta katika Ufunguzi wa  Hospitali ya Dk,Mehta(DR MEHTAS HOSPITAL)Ilioko Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja. 
Dokta Mkuu wa Hospitali ya Dk,MEHTA,Ameesh Mehta akitoa hotuba katika Ufunguzi wa Hospitali hio Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.​

NAIBU KATIBU MKUU WA CCM-BARA RODRICK MPOGOLO AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA CHINA HAPA NCHINI, LEO JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akizungumza na Balozi wa China hapa nchini, Dk. Lu Youqing, nyumbani kwa Balozi huyo, jijini Dar es Salaam, leo, Machi 19, 2017. Mazungumzo hayo yalihusu zaidi kuhusu juhudi za kuongeza ushirikiano baina na CCM na Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) katika nyanja mbalimbali ikiwemo uhusiano wa kidundugu uliopo kwa siku nyingi baina ya vyama hivyo na uchumi. (Picha na Bashir Nkoromo).
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akizungumza na Balozi wa China hapa nchini, Dk. Lu Youqing, nyumbani kwa Balozi huyo, jijini Dar es Salaam, leo, Machi 19, 2017. Mazungumzo hayo yalihusu zaidi kuhusu juhudi za kuongeza ushirikiano baina na CCM na Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) katika nyanja mbalimbali ikiwemo uhusiano wa kidundugu uliopo kwa siku nyingi baina ya vyama hivyo na uchumi. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga.
 Baadhi ya viongozi aliofuatana nao, Naibu Katibu Mkuu wa CCM wakifuatilia mazungumzo hayo. Kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga .
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akiwa na Balozi wa China hapa nchini, Dk. Lu Youqing, nyumbani kwa Balozi huyo, baada ya mazungumzo yao jijini Dar es Salaam, leo, Machi 19, 2017. Kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akimshukuru Balozi wa China hapa nchini, Dk. Lu Youqing, baada ya mazungumzo yao, nyumbani kwa Balozi huyo, jijini Dar es Salaam, leo, Machi 19, 2017. (Picha zote na Bashir Nkoromo).

WAZIRI MKUU MAJALIWA AWASILI MAURITIUS KUMWAKILISHA RAIS DKT. MAGUFULI KATIKA UZINDUZI WA JUKWAA LA UCHUMI LA AFRIKA

0
0



WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasili nchini Mauritius leo (Jumapili, Machi 19, 2017) kwa ajili ya kumuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli katika mkutano wa kuzindua Jukwaa la Uchumi Barani Afrika (AEP).
 Kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Sir Seewoosagur Ramgoolam Waziri Mkuu amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mauritius Mheshimiwa Vishnu Lutchmeenaraidoo. Uzinduzi wa jukwaa hilo unatarajiwa kufanyika kesho mjini Port Louis ambapo utawakutanisha viongozi wakuu wa nchi za Afrika, wanazuoni, wafanyabiashara pamoja na watu kutoka kwenye asasi mbalimbali za kiraia barani Afrika.
 Pamoja na kuhudhuria mkutano huo, pia Waziri Mkuu ambaye ameambatana na mkewe Mama Mary Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Mauritius litakalofanyika Machi 23, 2017. 
 Aidha, Waziri Mkuu mara baada ya kumaliza mkutano huo anatarajia kutembelea maeneo maalumu ya uwekezaji, viwanda vya sukari na nguo. Waziri Mkuu ameambatana na Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Dkt. Khalid Salum Mohammed na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mheshimiwa . Charles Mwijage pamoja na maofisa wengine wa Serikali.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiogozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mauritius, Bw. Vishnu Lutchmeenaraidoo wakati alipopokelewa kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Sir Seewoosagur Ramgoolam nchini Mauritius kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi la Africa mjini Port Luis kuanzi Machi 20, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mauritius, Bw. Vishnu Lutchmeenaraidoo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Sir Seewoosagur Ramgoolam nchini Mauritius kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi la Africa mjini Port Luis kuanzi Machi 20, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mauritius, Bw. Vishnu Lutchmeenaraidoo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Sir Seewoosagur Ramgoolam nchini Mauritius kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi la Africa mjini Port Luis kuanzi Machi 20, 2017. Kulia ni mkewe Mary.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Viewing all 109606 articles
Browse latest View live




Latest Images