Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1611 | 1612 | (Page 1613) | 1614 | 1615 | .... | 3285 | newer

  0 0


  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, Dodoma

  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Millao amewataka Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kuuza huduma zitolewazo na Wizara au Taasisi husika kwa lengo la kutekeleza shughuli za Serikali.

  Bibi Nuru Millao ameyasema hayo leo mjini Dodoma katika Ukumbi wa Hazina ndogo wakati wa Kikoa Kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kilicholenga kuwajengea uwezo Maafisa Mawasiliano Serikalini.

  “Katika kikao hiki tutapata nafasi ya kujadiliana namna bora ya kuboresha mawasiliano katika maeneo yetu ya kazi, kuisemea Serikali, kuitendea haki Serikali katika kuwasilisha taarifa mbalimbali za Serikali” alisema Bibi. Millao.

  Kwa upande wake Mhadhiri Msaidizi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Bw. Dotto Paul alisema kuwa wajibu mkuu wa Maafisa Mawasiliano Serikalini ni Kufuatilia kwa ukaribu nini kimeripotiwa kwenye vyombo vya habari kwa lengo la kuwa tayari kujibu au kufuatilia habari zinazohusu Serikali.

  Bw. Paul aliyasema hayo wakati akiwasilisha mada kuhusu wajibu wa Maafisa Mawasiliano Serikalini katika kutoa taarifa za Serikali kwa Umma kupitia vyombo vya habari na Wajibu wa vyombo vya habari katika kutoa habari za Serikali kwa Umma.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari Dkt. Hassan Abbass akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nuru Millao (hayupo pichani) wakati wa Kikao Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini mapema hii leo Mjini Dodoma.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nuru Millao akizungumza na Maafisa Mawasiliano wa Serikali (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi cha maafisa hao mapema hii leo mjini Dodoma, kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Dkt. Hassan Abbass .
  Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakiendelea na kikao kazi mapema hii leo mjini Dodoma.
  Bw. Dotto Paul toka Shule Kuu ya Uandishi wa Habari (IJMC) akitoa mada kwa Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakati wa kikao kazi cha maafisa hao (hawapo pichani) mapema hii leo mjini Dodoma.
  Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Bw. Theophil Makunga akitoa mada kwa Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakati wa kikao kazi cha maafisa hao (hawapo pichani) mapema hii leo mjini Dodoma.
  Afisa Mawasiliano toka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Bw. Innocent Mungi akichangia mada wakati wa kikao kazi cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali mapema hii leo mjini Dodoma.Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo  0 0
  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (wa nne kulia), akiwa katika picha ya pamoja na diwani wa Vigwaza Mohsin Bharwani (kulia kushoto kwake) pamoja na uongozi wa Lions club dar es salaam-Panorama baada ya kambi ya siku mbili ya huduma ya macho Vigwaza.

   Na Mwamvua Mwinyi, Vigwaza

  WAKAZI zaidi ya 20 wa kata ya Vigwaza, wilayani Bagamoyo,Pwani, wanatakiwa kufanyiwa upasuaji ili kutibu ugonjwa  wa mtoto wa jicho. Akitoa taarifa katika kambi ya macho iliyofanyika shule ya msingi Vigwaza, mratibu wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Lions Club Dar es salaam -PANORAMA, Prash Bhatti, alisema huduma ya macho waliyoitoa imegharimu kiasi cha mil. 30.

  Alisema mbali ya kutoa huduma za macho, pia waliwahudumia wagonjwa wa kisukari, presha na kusaidia huduma za kijamii. Hata hivyo Bhatti alisema kambi hiyo ilikuwa ni ya siku mbili ambapo watu 2,000 walijitokeza kupima macho na kupata huduma ya miwani bure na zaidi ya 20 walikutwa na mtoto wa jicho.
  "Shida kubwa ni ugonjwa wa mtoto wa jicho ambao kitaalamu tunaita cataract ugonjwa huu ndio unaoongoza kwa kuharibu jicho, dawa  yake  ni upasuaji"alisema.

  Bhatti alielezea,watu hao waliogundulika na mtoto wa jicho watafanyiwa upasuaji na gharama zote zitatolewa na lions club.

  Nae mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo,alitoa wito kwa jamii kupima macho mara kwa mara ili tatizo libainike mapema na kutibiwa. Aliiasa jamiii kufanya matibabu ya mtoto wa jicho  hospitali badala ya kukaa majumbani bila kujitibia.

  Mhandisi Ndikilo, alisema tiba ya ugonjwa huo ni upasuaji na kuwa ulaji mzuri wa chakula na matunda hukinga macho dhidi ya magonjwa mbalimbali.

  "Nampongeza diwani wa kata hii Mohsin Bharwani kwa kuona umuhimu wa kuwatumikia wananchi wake ikiwemo masuala ya kiafya"alisema mhandisi Ndikilo.

  Diwani wa kata ya Vigwaza, Mohsin Bharwani aliishukuru taasisi hiyo kwa kujitolea kutoa huduma mbalimbali za afya na vitabu mashuleni.

  Alifafanua kwamba watu wengi huwa hawapendi kuchunguza afya zao hivyo lions club imekuwa mkombozi kwao.

  Bharwani, alishukuru pia kupokea msaada wa vitabu na madaftari kwa wanafunzi wa shule zilizopo Vigwaza.

  0 0

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (wa kwanza kushoto), Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kushoto), Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mhe.Hamoud Jumaa (wa nne kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-hanga wakifurahia uzinduzi wa mradi wa Usambazaji Umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Pwani. Hafla ya Uzinduzi huo ilifanyika katika kijiji cha Msufini mkoani humo.

  Na Teresia Mhagama

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amezindua mradi wa Usambazaji Umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Pwani ambao utawezesha vijiji mbalimbali katika mkoa huo kupata huduma ya Umeme.

  Hafla ya Uzinduzi huo ilifanyika katika kijiji cha Msufini mkoani humo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo, Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete na Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mhe.Hamoud Jumaa.

  Uzinduzi wa mradi huo ulienda sambamba na utambulishaji wa Mkandarasi atakayetekeleza sehemu ya kwanza ya Mradi huo ambaye ni kampuni ya Steg International Services.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa Tatu kushoto), Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (wa kwanza kulia), Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kulia), Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mhe.Hamoud Jumaa (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-hanga (wa kwanza kushoto) wakifunua Jiwe la Msingi kuashiria uzinduzi wa mradi wa Usambazaji Umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Pwani. Hafla ya Uzinduzi huo ilifanyika katika kijiji cha Msufini mkoani humo.

  Kabla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-hanga alieleza kuwa Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini wa Awamu ya Tatu unahusisha vipengele Mradi vitatu vya utekelezaji.

  Alisema kuwa kipengele cha kwanza cha utekelezaji kitahusisha kufikisha umeme kwenye vijiji ambavyo havijafikiwa kabisa na miundombinu ya umeme wa gridi na kipengele cha Pili kitahusika na kuongeza wigo wa usambazaji umeme kwenye vijiji ambavyo vimefikiwa na miundombinu ya umeme.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0
 • 03/14/17--04:47: In Loving Memory
 • Born 06/04/1935 – Died 15/03/2016

  One year has passed since that sad day you departed from our midst to be with the Lord on 15/03/2016 . The heartbreak and pain that we felt has not and will never cease. However, God continues to be our refuge and inspiration.

  Though you are physically gone, spiritually you remain fresh in our hearts and thoughts everyday. Our heart are broken, but the beautiful memories will never disappear. The love you placed within our hearts no one can ever replace. In life we loved you dearly, in death we love you still, in our hearts you hold a place that no one could ever fill.

  We thank you for all the love, support and wisdom that you showed to us. We have so many wonderful memories of the times we shared together. You cared for us all so much and were always there to help. You taught us well, and told us to love each other. We will love and cherish you forever.

  You are sincerely missed and affectionately remembered by your beloved Wife, your children, your – in - laws, grandchildren, relatives and friends. LORD HAS GIVEN AND LORD HAS TAKEN, PRAISE BE TO THE NAME OF LORD,

  AMEN

  0 0

  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa Kikao kazi cha 12 cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali kinachofanyika Mkoani Dodoma.Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi.Nuru Milao,Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi Bi.Elizabeth Kitundu,Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt.Hassana Abbas na Mwenyekiti wa TAGCO Bw.Innocent Mungy.

  Na: Lorietha Laurence – WHUSM, Dodoma.

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amewataka Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini kuzisoma, kuzielewa na kuzifanyia kazi sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 na ile ya Haki ya kupata Taarifa ya mwaka 2016 ili kuweza kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi katika kuuhabarisha umma.

  Waziri Nape ameyasema hayo leo Mjini Dodoma alipokuwa akifungua mkutano wa Maafisa Mawasiliano Serikalini ambapo licha ya kuwataka kuzijua sheria hizo pia amewataka kuwa wabunifu kuendana na maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia katika utendaji kazi wa kila siku.
  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akizungumza na Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakati akifungua kikao kazi cha 12 cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali kinachofanyika Mkoani Dodoma.

  Aidha aliongeza kuwa kuwepo kwa sheria hizo mbili kutatengeneza daraja litakalounganisha na kuwezesha utekelezaji wa majukumu ya Serikali kwa wananchi. “Ni wajibu wa Maafisa Mawasiliano kuzijua na kuzitendea kazi sheria hizi ili kurahisisha upatikanaji wa mawasiliano baina ya serikalini na umma hivyo kuondoa ugumu uliokuwepo hususani katika kupatikana kwa taarifa muhimu kwa wananchi” alisema Waziri Nape.

  Aliongeza kwa kufafanua kuwa endapo utekelezaji wa sheria hizi mbili muhimu utasimamiwa na kuzingatiwa basi kutakuwepo na matokeo chanya ya kiutendaji na hivyo kuleta mafanikio makubwa yanayotarajiwa na umma.


  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa suti) akiongozwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) Dkt. Juma Malewa (mbele), kuingia ukumbini kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza pamoja na Wakuu wa Vituo vya Magereza Tanzania Bara, uliofanyika Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake ya ufunguzi, Masauni aliwataka Maafisa wa Jeshi hilo, kuongeza kasi zaidi ya kuzalisha katika kilimo, miradi ya ufugaji pamoja na vyanzo vingine ili kulilitea mapato zaidi Jeshi hilo. Aidha, alisema kwa Maafisa watakaozembea katika uzalishaji wataondolewa katika nyadhifa zao. (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza naWakuu wa Vituo vya Magereza yote Tanzania Bara (hawapo pichani) katika Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo, Masauni aliwataka Maafisa wa Jeshi hilo, kuongeza kasi zaidi ya kuzalisha katika kilimo, miradi ya ufugaji pamoja na vyanzo vingine ili kulilitea mapato zaidi Jeshi hilo. Aidha, alisema kwa maafisa watakaozembea katika uzalishaji wataondolewa katika nyadhifa zao.

  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) Dkt. Juma Malewa akitoa hotuba yake ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) kwa ajili ya kuja kuufungua Mkutano wa Wakuu wa Vituo vya Magereza Tanzania Bara ambao pia ulihudhuriwa na Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo kutoka Makao Makuu, ulifanyika Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Hata hivyo, Dkt Malewa katika hotuba yake alimshukuru Rais John Magufuli kwa kutatua kwa kiasi kikubwa changamoto ya uhaba wa nyumba za Makazi ya Askari wa Jeshi hilo pamoja na juhudi za Serikali yake za ununuzi wa magari 450 kwa awamu ya kwanza ambapo jeshi hilo linatarajia kuyapata. Katikati ni Naibu Kamishna wa Jeshi hilo, Edith Mallya.


  0 0

  Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeelezwa kuwa jalada la kesi  ya uhujumu uchumi na kusababisha hasara ya bilioni 1.16 inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA), Dickson Maimu na wenzake lipo kwa  (DPP)

  Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Leonard Swai, amesema kuwa, jalada hilo liko kwa DPP kwa ajili ya kufanyiwa tathmini ya upelelezi uliofanyika

  Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage  ameiahirisha kesi hiyo hadi Aprili 20,2017 kwa ajili ya kutajwa. 

  Maimu anashtakiwa pamoja na  Meneja Biashara wa (NIDA), Avelin Momburi na Mkurugenzi wa TEHEMA, Joseph Makani.

  Wengine ni Mhasibu Mkuu wa NIDA, Benjamin Mwakatumbula, Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers,  Astery Ndege, Ofisa Usafirishaji, George Ntalima, Mkurugenzi wa Sheria, Sabina Raymond na Xavery Kayombo.

  Wanakabiliwa na tuhuma za kutumia madaraka vibaya, kula njama, kutumia nyaraka za uongo kumdanganya mwajiri na kuisababishia Serikali hasara ya milioni 1,169,352,931.

   Maimu na Mwakatumbula wanadaiwa kutumia madaraka yao vibaya kati ya  Januari 15 hadi 19,  mwaka 2010 katika makao makuu ya NIDA   wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.

  Wanadaiwa kuidhinisha malipo kwa Gotham International Limited (GIL) ya Dola za Marekani 2,700,00 bila ya kutumia viwango vya kubadilisha fedha za kigeni vilivyowekwa na BOT.

  Aidha wanadaiwa kuidhinisha malipo ya USD 1.8 kwa  GIL bila kuzingatia viwanjo vya fedha.


  Ilidaiwa kuwa, Juni 20, 2014, waliidhinisha USD  675,000 kwa GIL bila ya kuzingatia viwango vya kubadilisha fedha, hivyo kuifanya kampuni hiyo kupata faida ya Sh 42,471,000.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) , Bw. Edwin Rutageruka akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya biashara na ujasiriamali kwa maofisa watendaji kata wa manispaa ya Temeke kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuwahamasisha wananchi katika maeneo hayo kutambua fursa mbalimbali za biashara zinazotolewa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(Tan Trade). Kushoto ni Mchumi wa Manispaa ya Temeke Bw. Erick Kilangwa. Na kulia ni Mkurugenzi wa Ukuzaji Biashara wa TANTRADE, Bi.Anna Bulondo.
  chumi wa Manispaa ya Temeke Bw. Erick Kilangwa (katikati) akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya biashara na ujasiriamali kwa maofisa watendaji kata wa manispaa hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuwahamasisha wananchi katika maeneo hayo kutambua fursa mbalimbali za biashara zinazotolewa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TANTRADE). Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa TANTRADE,Bw.Edwin Rutageruka. Na kushoto ni Mchumi wa TANTRADE, Bw.Emmanuel Miselya. Mafunzo hayo yameratibiwa na TANTRADE.
  Watendaji Kata wa Manispaa ya Temeke wakifatilia mada kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TANTRADE) , Bw. Edwin Rutageruka katika ufunguzi wa mafunzo ya siku moja ya biashara na ujasiriamali lenye lengo la kuwajengea uwezo kuwahamasisha wananchi katika maeneo hayo kutambua fursa mbalimbali za biashara zinazotolewa kuwahamasisha wananchi katika maeneo hayo kutambua fursa mbalimbali za biashara zinazotolewa na TANTRADE.
  Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TANTRADE) , Bw. Edwin Rutageruka akifurahi jambo na Mchumi wa Manispaa ya Temeke Bw. Erick Kilangwa mara baada ya kumalizika kwa mafunzo ya biashara na ujasiriamali kwa maofisa watendaji kata 23 za manispaa hiyo kwa lengo la kuhamasisha wananchi katika maeneo yao kutambua fursa za biashara zinazotolewa na TANTRDE.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  KIUNGO mshambuliaji wa Mwadui FC, Hassan Salum Kabunda amechaguliwa kuwa  Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa mwezi Februari, mwaka huu.

  Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas Mapunda amesema leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam kwamba, Kabunda amewapiku washambuliaji wa Simba, Mrundi Laudit Mavugo na mzalendo Ibrahim Hajibu baada ya mechi tatu za Februari kushinda tuzo hiyo.

  Hassan Salum Kabunda ndiye Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa mwezi Februari, mwaka huu

  “Kabunda amecheza dakika 270 katika mechi tatu ambazo Mwadui wameshinda mbili na kupoteza mechi moja, hivyo kujikusanyia pointi 6 na kupanda kutoka nafasi ya nane hadi ya sita,”amesema Mapunda.

  Lucas amesema mtoto huyo wa beki wa zamani wa Yanga na timu ya taifa, Taifa Stars, Salum Kabunda enzi zake akiitwa Ninja au Msudan, katika mechi hizo tatu alifunga mabao manne kati ya sita ambayo Mwadui ilifunga.

  Na kwa ushindi huo, Kabunda atazawadia Sh. Milioni 1 na wadhamini wa Ligi Kuu, kampuni ya Vodacom.

  0 0

   Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku (aliyevaa shati la draft) wa kwanza kulia akiangalia namna uchimbaji wa mfereji wa kupitishia maji wakati wa mvua unavyochimbwa wakati alipofanya ziara ya kuutembelea leo.
   Kazi  zikiendelea kama inayoonekana kwenye eneo hilo
   Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku wa tatu kutoka kushoto akisisitiza jambo kwa msimamizi wa mradi huo Ephahim Lucas wakati alipotembelea ujenzi wa mfereji huo ili kuona kasi yake ya utendaji kama inakidhi viwango.
  Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akiingia kwenye moja ya chemba zilizopo kwenye ujenzi wa mfereji huo.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Brazil katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Carlos Alfonso lglesias Puente alipofika Ikulu Mjini Unguja leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi wa Brazil katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Carlos Alfonso lglesias Puente alipofika Ikulu Mjini Unguja leo.

  0 0

   Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika ziara ya kukagua sehemu zilizokumbwa na mafuriko katika bonde la Mto Msimbazi, baada ya mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam.

  Na Ripota wa globu ya jamii

  Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewatahadharisha wakazi wa bonde la mto msimbazi kuwa mvua zinazo nyesha zitaweza kuendelea kuleta madhara kwa wakazi waishio mabondeni kutokana na uharibifu wa miundombinu ya maji.

  Makonda amesema hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa bonde la mto Msimbazi ambao walikusanyika kumsikiliza wakati alipokuwa akitembelea maeneo hayo.

  "kulingana na utabiri wa hali ya hewa mvua hizi zipo kati ya Milimita 30 hadi 35 na zikiendelea kuongezeka mpaka Milimita 50, maana yake hali itakuwa ni mbaya zaidi hivyo waswahili husema kinga ni bora kuliko tiba "Amesema Makonda

  amesema kuwa wao kama Serikali chini ya Rais Magufuli wanategemea kupata fedha kutoka benki ya Dunia ili kuweza kudhibiti na kutengeza mto msimbazi ili kupunguza Madhara, kwani yanayo onekana leo ni tabia mbaya za kwetu wenyewe wanadamu kuwa wakaidi pindi tunapoambiwa tusijenge mabondeni tunakuwa wabishi, pia tunaambiwa tuhakikishe kuwa hatuharibu zile kingo za maji sisi tunaharibu na kuziba kisha kujenga
   Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika moja ya nyumba zilizopo kando ya bonde la mto Msimbazi kukagua wakazi wa eneo hilo ambao wamepitiwa na adha ya mafuriko yaliyotokana na mvua ilinyosha jana.
   Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikatiza kuvuka upande wa pili wa bonde mto msimbazi kujionea jinsi maji yalivyofanya uharibifu
   Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na jopo la watumishi na wakazi wa jiji katika bonde la Mto Msimbazi.

  0 0

  Na Lucas Mboje, Dar es Salaam

  KAMISHNA Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa(pichani) ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kufanikisha mchakato wa ununuzi wa magari 450 ya Jeshi hilo ambayo yanatarajiwa kupokelewa muda wowote kuanzia sasa.

  Kamishna Jenereli Malewa ameyasema hayo leo katika ufunguzi rasmi wa mkutano wa wakuu wa magereza yote Tanzania Bara unaofanyika kwa siku moja katika Bwalo kuu la Maafisa magereza, ukonga jijini Dar es Salaam.
  Jenerali Malewa amesema kuwa upatikanaji wa magari hayo utapunguza tatizo kubwa la uhaba wa magari kwa ajili ya shughuli za uendeshaji na utawala pamoja uboreshaji wa utekelezaji wa majukumu ya Jeshi hilo.

  “Nichukue nafasi hii kumshukuru kwa dhati Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na serikali yote kwa ujumla kwa namna inavyoshughulikia utafutaji wa ufumbuzi wa changamoto tulizonazo,” alisema Jenerali Malewa.

  Aidha kuhusu madeni ya Watumishi wa Jeshi hilo na wazabuni, Kamishna Jenerali Malewa amesema serikali imetoa kiasi cha zaidi ya Bilioni 8 za pesa ya kitanzania kwa ajili ya kulipa madeni hayo ambapo madeni yote yaliyokwisha kuhakikiwa tayari yameanza kulipwa na wahusika wamekwishaanza kupata fedha wanazodai Jeshi hilo.

  Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Mhandisi Hamad Yusuph Masauni akizunguza katika ufunguzi wa Mkutano huo ametoa rai kwa jeshi hilo kutumia vyema fursa zilizopo katika katika maeneo mbalimbali ya jeshi hilo kwa kuanzisha na kuimarisha viwanda vidovidogo vilivyopo ili kuongeza uzalishaji hivyo kuchangia pato la taifa.

  Masauni amesema kuwa Jeshi la Magereza linazo fursa nyingi sana za uzalishaji yakiwemo maeneo makubwa yanayofaa kwa kilimo, miradi ya ufugaji na miradi mengineyo ya kiuchumi.

  “Nisisitiza kwamba wekeni mikakati yenye lengo la kuongeza uzalishaji katika maeneo yenu kwani nataka kila mmoja wenu katika gereza alilopo aweke malengo ya kuongeza uzalishaji kulingana na fursa zilizopo,” alisema Mhe. Masauni.

  Mkutano huu wa Wakuu wa Magereza yote Tanzania Bara unajumuisha Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Magereza na Wakuu wa vituo vya Magereza yote nchini ambapo lengo kuu ni kujadiliana kwa kina hali halisi ya utendaji kazi magerezani na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto zilizopo ili kuongeza tija na ufanisi. Kauli mbiu ya mkutano huo ni JESHI LA MAGEREZA KATIKA JITIHADA ZA KUFANIKISHA KUELEKEA TANZANIA YA UCHUMI WA VIWANDA.

  0 0

  Jumla ya wagonjwa 11 wamefanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ushirikiana na madaktari wenzao wa Taasisi ya Open Heart International ya nchini Australia.

  Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Upasuaji wa Moyo ambaye pia ni Daktari bingwa wa upasuaji wa Moyo Bashir Nyangasa wakati akielezea jinsi kambi hiyo ya upasuaji inavyoendelea kutoa matibabu kwa wagonjwa.

  Dkt. Nyangasa alisema, “Kwa kushirikiana na washirika wetu wa OHI tulianza kambi maalum ya upasuaji kuanzia tarehe 10/03/2017 hadi leo  tarehe 17/3/2017 tumefanya  upasuaji kwa wagonjwa 11 ambao wanaendelea vizuri,  kati ya hao watoto ni tisa na watu wazima ni wawili”,.  

  Dkt. Nyangasa alisema  katika kambi hiyo  ambayo inamalizika tarehe 17/3/2017 walipanga kufanya upasuaji kwa wagonjwa 25 kati ya hao watoto ni 15 na watu wazima ni 10.

  Kuhusu uhitaji  wa damu kwa wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji wa Moyo Dkt. Nyangasa alisema wagonjwa hao wanahitaji damu nyingi hivyo basi aliwaomba wananchi wajitokeze kuchangia  damu ambayo itatumika kwa wagonjwa.

  “Tunaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kuchangia damu na  uchangiaji huu wa damu  usifanyike mara moja bali  uwe endelevu  kwani Taasisi inatoa huduma kwa wagonjwa wakati wote siyo wakati wa kambi maalum za matibabu ya moyo pekee yake”, alisisitiza Dkt. Nyangasa.

  Tangu kuanza kwa mwaka huu  wa 2017 JKCI kwa kushirikiana na baadhi ya washirika wake wa nje ya nchi ambao ni  Madaktari  Afrika wa  Marekani, Hospitali za  Apolo Bangalore na BLK zote za nchini  India na Open Heart International ya Australia wamefanya  matibabu ya moyo ya kufungua na bila kufungua kifua kwa wagonjwa wa moyo wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.
  Madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Open Heart International ya nchini Australia (OHI) wakifanya upasuaji wa kuziba matundu ya moyo kwa mgonjwa wakati wa kambi maalum ya matibabu ya moyo inayoendelea katika Taasisi hiyo. Tangu kuanza kwa kambi hiyo tarehe 12/03/2017 hadi leo tarehe 14/03/2017 jumla ya wagonjwa 11 wamefanyiwa upasuaji kati ya hao watoto ni tisa na watu wazima wawili.
  Madaktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Taasisi ya Open Heart International ya nchini Australia (OHI) wakifanya upasuaji wa kuvuna mshipa wa damu mguuni kwa mgonjwa wa moyo na kuupandikiza katika mishipa ya moyo iliyoziba kwa jina la kitaalamu Coronary Artery Bypass Graft (CABG). Tangu kuanza kwa kambi hiyo tarehe 12/03/2017 hadi leo tarehe 14/03/2017 jumla ya wagonjwa 11 wamefanyiwa upasuaji kati ya hao watoto ni tisa na watu wazima wawili. Habari/Picha na Anna Nkinda – JKCI.

  0 0

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imezindua Duka la Huduma ya wateja mjini Shinyanga kwa lengo la kurahisha huduma zinazotolewa na kampuni hiyo kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga.


  Mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa duka hilo la huduma kwa wateja lililopo karibu na uwanja wa Shycom mjini Shinyanga alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro.

  Awali akizungumza wakati wa kuzindua duka hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel nchini Sunil Colaso alisema wamezindua duka hilo ili kuongeza wigo wa soko mkoani Shinyanga na kuwasogezea huduma wananchi.

  “Tunafuraha kubwa kufungua duka hili leo ambalo ni miongoni mwa maduka sita ambayo yanafunguliwa mkoani Shinyanga,hili ni duka la pili Mjini Shinyanga na tunatarajia kufungua maduka mengine ndani ya mwezi huu”,alieleza Colaso.

  Aidha Colaso alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wakazi wa Shinyanga kufika katika duka hilo la huduma kwa wateja ili kupata huduma mbalimbali ikiwemo kurudisha namba zilizopotea,kuuza laini,simu,kurekebisha namba za siri za Airtel Money na huduma nyinginezo.

  Naye mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alisema uwepo wa duka hilo utaongeza ajira kwa vijana na pia itarahisisha upatikanaji wa huduma muhimu za simu kwa wananchi ikiwemo huduma za pesa.

  “Yanapofunguliwa maduka mengi inasaidia kupunguza umbali wa wananchi kufuata huduma,nawaomba wananchi kila mtu asajili simu yake kwa majina yake halisi ili kupunguza vitendo vya uhalifu",alisema Matiro.

  “Nawaomba wananchi mtumie maduka haya kupata huduma mnazohitaji badala ya kutumia watu wa kati ambao baadhi yao siyo waaminifu,kumbukeni mawasiliano ni maendeleo,bila mawasiliano maendeleo yanakuwa ni shida,na sisi tunapoangalia vipaumbele vya maendeleo huwa tunaangalia pia kuna mawasiliano gani”,aliongeza Matiro.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania bwana Sunil Colaso akimkaribisha mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro katika duka la huduma kwa wateja wakati wa uzinduzi wa duka hilo lililopo katika mtaa wa Buzuka karibu na uwanja wa Shycom mjini Shinyanga leo Jumanne Machi 14,2017.
  Meneja wa kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania Kanda ya Kati bwana Stephen Akyoo akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka la huduma kwa wateja mjini Shinyanga. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania bwana Sunil Colaso akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma kwa wateja.Katikati ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro na Afisa mtendaji wa kata ya Shinyanga Mjini Simon Mashishanga wakimsikiliza mkurugenzi huyo wa Airtel.Picha zote na Kadama Malunde

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  Kikosi cha Yanga kimeendelea na mazoezi yake leo kwenye Uwanja wa Taifa ikiwa ni maandalizi ya kuelekea mechi ya marudiano ya michuano ya  klabu Bingwa Afrika dhidi ya Zanaco utakaofanyika mwishoni mwa wiki hii.

  Mechi hiyo inayotarajiwa kuwa Jumamosi Machi 18, itachezwa Nchini Zambia ambapo katika mchezo wa awali timu hizo zilitoka sare ya 1-1.

  Akizungumza na mtandao huu, Meneja wa Yanga Hafidh Saleh amesema kuwa kikosi kinaendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo huo wa marudiano utakaofanyika nchini Zambia huku washambuliaji wawili wa kimataifa wakiwa hawajajiunga na wenzao.

  Saleh amesema, Amisi Tambwe na Donald Ngoma bado wapo katika uangalizi wa daktari na hawajajiunga na wenzao katika mazoezi kuelekea mechi ya marudiano.

  "Kwa sasa tunaendelea na mazoezi hapa Uwanja wa Taifa, Tambwe na Ngoma wakiwa hawajajiunga na wenzao kwani bado wapo chini ya uangalizi wa daktari, wachezaji wengine wote wapo fiti wakiendelea kujifua" amesema Saleh.

  Kesho kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina anatarajia kutaja kikosi kitakachoondoka siku ya Alhamis kuelekea nchini Zambia kwa ajili ya marudiano na Zanaco na Yanga inahitajika kupata ushindi wa goli 1-0 ili iweze kusonga mbele kwenye hatua ya makundi ya klabu Bingwa Afrika.

  0 0


   BancABC, ambayo ni sehemu ya Atlas Mara, leo imezindua bidhaa adimu itakayokuwezesha kuvuna riba hadi asilimia 16% kutokana na akiba maalum utakayojiwekea.

  Katika hali ya kawaida kama tulivyozoea, amana za muda maalum zimekuwa kivutio kwa wateja wengi wa mabenki. Kwa kuanzia amana hii yenye riba kubwa ni nzuri kuliko kufungua akaunti ya akiba ya kawaida kwani unapata riba nzuri zaidi.

  Faida nyingine ni  uhakika wa mapato ya riba na uwezo wa kuamua namna gani ya kuitumia, kukopa au kuweka akiba zaidi, utakavyopenda mwenyewe.

  BancABC imechukuwa hatua kubwa zaidi kwa kutoa riba ya asilimia 16%, vilevile utapata riba hii bila ubabaishaji.

  Akiongea jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya benki hiyo, Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wale wafanyabiashara wa kati. Mama Joyce Malai alisema hakuna tena nafasi nzuri ya kunufaika na huduma za benki kama hii iliyopo sasa.

   “Tunathamini mchango mzuri wa wateja wetu, kwa hiyo kama benki makini kupata ruzuku tunatoa huduma hii ya kipekee kama zawadi maalum”.

  Hii haina tofauti ya kupata faida ya biashara hata kabla hujaianza!  Tunaamini tumeileta huduma hii kwa wakati muafaka, katika muda inayohitajika haswa.  Tuna hakika bidhaa hii mpya ya kibenki itawavutia wateja wengi  hasa wale walio makini”, alisema Joyce.
   Bi. Joyce Malai (kushoto) Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wafanyabiashara wa kati wa BancABC, akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa akaunti maalum ya JIONGEZE MARADUFU uliofanyika katika makao makuu ya benki hiyo. Kulia ni Bi. Upendo Nkini Mkuu wa kitengo cha masoko wa BancABC.


   Bi. Joyce Malai (kushoto) Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wafanyabiashara wa kati,  na  Bi. Upendo Nkini Mkuu wa kitengo cha masoko wa BancABC wakionyesha (bidhaa) Akaunti mpya na ya kipekee JIONGEZE MARADUFU iliyozinduliwa na BancABC.


  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala  ameitisha kikao na viongozi Dini na mila kuwaomba msaada wa kukemea vitendo vya kishirikina katika mkoa huo. Makala amesema hayo katika kikao chake na Viongozi hao pamoja na wenyeviti wa mitaa na vijiji katika mkoa wa Mbeya.

  "matukio ya watu kufukua maiti au kutozika kwa imani ya kuwafuafua  hayapaswi kuachwa yaendelee , Biblia na Qurhan imeandikwa kuna kufufuliwa, kuna kiama ,kuna pepo ni baada ya kufa nawaomba  mnisaidie   kutoa Elimu na mafundisho yenye kuondosha matukio hayo" Amesema Makalla.

   Makalla awaomba pia kusaidia serikali katika mapambano ya Dawa ya Kulevya kwa kutoa Elimu na hamasa ya kuelimisha madhara ya dawa ya kulevya.

  Amesema Mbeya itangazwe kwa sifa nzuri kama Mkoa unaotegemewa kwa uzalishali wa Chakula, Mkoa wa tatu kitaifa kuchangia pato la Taifa na ni Mkoa unapiga hatua kubwa kimaendeleo.
   Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza na viongozi wa Dini, viongozi wa mila, na mitaa katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mkapa leo jijini Mbeya.
   Baadhi ya viongozi wa dini na serikali za mitaa na mila wakiwa katika ukumbi wa mkapa kumsikiliza mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makalla.
  Mkuu wa mkoa wa mbeya Amos Makalla watatu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya mbeya mh.William Ntinika (kushoto) Pamoja na viongozi wa Dini mkoa wa Mbeya.

  0 0

  Na Karama Kenyunko.
  Upande wa Mashtaka katika kesi ya kujeruhi inayowakabili wabunge na makada wa Chadema wamefunga ushahidi wao. Katika kesi hiyo wabunge hao wanadaiwa kumjeruhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresa Mmbando. 

  Wakili wa Serikali, Flontina Sumawe amefunga ushahidi  wa upande wa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi. Wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo iliyopo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  upande wa mashtaka ulileta mashahidi wanne waliofika na kueleza kuwa washtakiwa walitenda kosa la kujeruhi.
  Mahakama imewataka upande wa utetezi kuwasilisha hoja za kuomba washtakiwa wasionekane wana kesi ya kujibu Machi 21, wakati upande wa mashtaka utawasilisha majibu kinzani  Machi 28. Kesi hiyo itatajwa Aprili 5, mwaka huu. Washtakiwa katika kesi hiyo ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea, Halima Mdee, Kawe, Mbunge wa Jimbo Ukonga Mwita Waitara, diwani wa Kata ya Kimanga, Manase Njema, kada wa chama hicho, Rafii Juma na Diwani wa Kata ya Saranga Kimara, Ephreim Kinyafu.

   Wanadaiwa kuwa Februari 27, 2016 katika Ukumbi wa Karimjee wilaya ya Ilala jiji la Dar es Salaam walimjeruhi Theresia na kumsababishia majeraha. Akitoa ushahidi wake, Mmbando alieleza jinsi alivyovamiwa, kujeruhiwa na kupokonywa faili lililokuwa na ajenda na muongozo wa uchaguzi wa Meya na Naibu Meya wa jiji la Dar es Salaam uliopaswa kufanyika  Februari 27,2016. Alidai kuwa siku hiyo ya Februari 27, 2016 alipewa jukumu la kuusimamia uchaguzi huo wa Meya na Naibu Meya ambao ulipaswa kufanyika Karimjee.

  Kama Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam alikuwa ni Mwenyekiti  wa uchaguzi huo, wajumbe wote walifika , Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam, Salehe Yohana ambaye alikuwa Katibu alifungua uchaguzi  huo kwa idadi ya wajumbe ilikuwa inajitosheleza. Baada ya kikao kufunguliwa alipata taarifa ya zuio la mahakama na kuwatangazia wajumbe wote kuwa uchaguzi hauwezi kufanyika. Baada ya uchaguzi huo kuahirishwa , wajumbe wa CCM walitoka nje lakini wajumbe wa vyama vingine wakiwamo Ukawa walimvamia wakisema aendeshe uchaguzi huo.

  “Walinifuata mezani nilipokuwa nimekaa wakitaka niendelee na uchaguzi huo, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee alilivuta faili lililokuwa na muongozo wa uchaguzi huo na katika tukio hilo niliweza kuwafahamu walionivamia kwa wengine kwa majina, wengine kwa sura.”Alisisitiza kusema Mmbando wakati akitoa ushahidi wake.

  Aliongeza kuwa kuna mwanamke mmoja alimkoa konzi kichwani na wengine wakimgonga gonga huku na kule Aliieleza mahakama watu wengine aliowatambua siku hiyo ya tukio kuwa ni Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akimwambia kuwa yeye ni Kibaraka wa CCM, hawawezi kuendesha serikali kama mali yao, akae aendeshe huo uchaguzi. Mbunge wa jimbo la Ukonga, Mwita Waitara yeye alikuwa akimsisitiza kuwa hakuna kuondoka hapa kaa uendeshe kikao.

  Mheshimiwa Hakimu, walinikamata kwa nguvu nisitoke , wengine walinishika maziwa hadi sketi yangu iling’oka zipu na kwamba baada ya tukio hilo aliokolewa na askari wa jeshi lapolisi na wafanyakazi wa jiji  kupitia mlango wa nyuma   na hakujua kilichoendelea nyuma yake. “Katika tukio hili nilipata madhara, utu wangu nilidhalilika na mwili wangu ulivia damu”. Alimaliza kutoa ushahidi wake Mmbando.

older | 1 | .... | 1611 | 1612 | (Page 1613) | 1614 | 1615 | .... | 3285 | newer