Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1610 | 1611 | (Page 1612) | 1613 | 1614 | .... | 3285 | newer

  0 0

  RAIS wa Serikali ya Awamu ya Nne, Dk Jakaya Kikwete kesho anatarajiwa kuzindua Taasisi ya Maendeleo ya Jakaya Mrisho Kikwete (JMKF) .

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na taasisi hiyo, uzinduzi huo utafanyika katika Hoteli ya Hyatt Kempinsk The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam na baada ya uzinduzi huo, Dk. Kikwete ataendesha kikao cha kwanza cha bodi ya taasisi hiyo.

  Taasisi hiyo imeundwa ili kusaidia Tanzania na Afrika katika kuimarisha amani, afya, utawala bora na maendeleo endelevu.Aidha taasisi hiyo itajikita katika maendeleo endelevu kwa kusaidiana na wadau wengine kukabiliana na umasikini, kusaidia mkulima mdogo, kulinda mazingira na kukabiliana na athari za tabianchi.

  Taasisi hiyo itasaidia pia katika afya ya mama na mtoto, kukabiliana na ugonjwa wa malaria na kuboresha lishe ya wananchi.Katika elimu, itaboresha elimu katika kuwasaidia wajasiriamali kwa mafunzo na pia itasaidia katika utawala bora na utafutaji amani.

  Taasisi hiyo imesajiliwa na itakuwa chini ya uongozi wa bodi ya wadhamini wa kimataifa yenye wajumbe kutoka ndani na nje ya Tanzania ikiwemo Guinea Bissau na Marekani.

  Wajumbe kutoka Tanzania ni aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandara, Daktari Bingwa wa Upasuaji Profesa William Mahalu, Balozi Mwanaidi Maajar, Genevive Sangundi na Mkurugenzi Mtendaji wa kundi la makampuni ya SS Bakhresa, Abubakar Bakhresa.

  0 0

  Balozi,Sir George Kahama amefariki leo alasiri katika hospitali ya Taifa  Muhimbili,alikokuwa amelazwa kwa matibabu.Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema pepono-Amen.

  Taarifa zaidi za msiba huo tutazipata baadae kidoogo.


  0 0
  0 0
 • 03/12/17--22:03: TAARIFA KWA UMMA • 0 0


  Na Immaculate Makilika- MAELEZO

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga amefanya mazungumzo na mjumbe maalum wa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, Balozi Harro Adt, ambapo alipokea, niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, ujumbe maalum kutoka kwa Kansela Markel.

  Akizungumzia ziara ya Balozi Adt nchini, Balozi Dk. Mahiga alisema kuwa "Kansela Merkel amemtuma Balozi Adt, kuleta ujumbe maalum ambao ni ombi kwa Rais Magufuli la kuisaidia Ujerumani katika kugombea nafasi ya kuwa mjumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakati wa uchaguzi wa nafasi hiyo unaotarajiwa kufanyika mwaka 2018".

  Balozi Dk. Mahiga alieleza kuwa dhamira ya Ujerumani ya kugombea nafasi hiyo ni kusaidia mageuzi ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ikiwa ni pamoja na kuridhia nchi za Afrika katika mchakato wa kupokea nafasi mbili za kudumu katika baraza hilo. Nchi nyingine zinazogombea nafasi hizo ni Israel na Ubelgiji.

  Balozi Mahiga alisema kuwa, Ujerumani imeahidi masuala kadhaa kama vile kusimamia amani katika jumuiya ya kimataifa na katika ukanda wa Afrika, kusimamia haki za binadamu katika ngazi ya dunia na kuendelea kuimarisha uhusiano wake na nchi nyingine.

  Aidha, Ujerumani imesisitiza nia yake ya kuunga mkono mageuzi mapya katika bara la Afrika ambayo yataikomboa Afrika na kuleta maendeleo zaidi barani humu.

  Katika mazungumzo hayo, Balozi Dk. Mahiga alisema kuwa ameiomba Ujerumani isaidie ujenzi wa jengo mahususi la mahakama ya Afrika iliyopo mjini Arusha ikiwa ni pamoja na kuboresha mfumo mzima wa mahakama barani Afrika pamoja na kuisaidia Afrika katika kupambana na masuala ya mabadiliko ya tabianchi.

  Kwa upande wake, mjumbe maalum kutoka Ujerumani Balozi Adt, alisema kuwa amefurahishwa na mapokezi aliyoyapata alipowasili nchini.

  Aidha, Mjumbe huyo Maalum wa Kansela wa Ujenrumani alieleza matumaini yake kuwa Tanzania ambayo ni rafiki wa Ujerumani kihistoria itatoa msaada juu ya nafasi hiyo ili kusaidia kutekeleza malengo waliojiwekea kiufanisi kuhakikisha Afrika inapata nafasi mbili za kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

  Uhusiano kati Tanzania na Ujerumani ni wa kihistoria na wakati wote nchi mbili hizo zimekuwa zikifanya kila jitihada za kuuimarisha.

  Chini ya uhusiano huo, Ujerumani imekuwa ikiisaidia Tanzania katika sekta mbalimbali za maendeleo kama vile elimu, miundombinu na wanyamapori.

  0 0

  Kamati ya Utalii ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya ikiongozwa na Afisa Utalii wa Jiji Bi.Levina Modest na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.Geofrey Kajigili wanaofanya kampeni hii kabambe ya utambuzi wa Vivutio vyote vilivyopo Jijini Mbeya kwa kushirikiana na asasi zisizo za kiserikali za Uyole Cultural Tourism Enterprise pamoja na Elimisha .

  Pia wamemtembelea Mzee Mkongwe wa Siasa nchini, Mzee Rashid Ally Sinkala ambaye amewahi kuwa Diwani wa iliyokuwa ikiitwa Kata ya Soko Matola (sasa Kata ya Maendeleo) kwa miongo kadhaa,na amewahi kutumika kama Meya ya Halmashauri ya Mbeya Mjini.

  Mzee Sinkala ameiambia Kamati ya Utalii kuwa Miaka zaidi ya 50 iliyopita wakati wa Siasa za Ukombozi wa Tanganyika enzi za Chama cha Tanganyika African National Union (TANU)Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa akifikia kwenye nyumba ya mwanasiasa Mkongwe mwanamke aliyejulikana kwa majina ya Zaituni Binti Matola.Binti Matola alitenga chumba kimoja nyumbani kwake kama Maficho ya Mwalimu Nyerere.
  Mzee Sinkala akiwa mlangoni mwa Chumba maalum alipokuwa akifikia Mwalimu Nyerere ndani ya nyumba ya muasisi wa TANU na mwanamke mashuhuri Hayati Zaituni Binti Matola aliyesababisha maeneo hayo kuitwa "Soko Matola" Jijini Mbeya
  Wajumbe wa Kamati ya Utalii Jijini Mbeya wakimsikiliza kwa makini Meya mstaafu wa Halmashauri ya Mbeya Mjini Mzee Sinkala ndani ya nyumba ya kihistoria ya Binti Matola.

  0 0
 • 03/13/17--01:07: kumbukumbu
 • Marehemu Ibrahim Werrema John. 

  Ni miaka 4 sasa toka ndugu yetu kipenzi Ibrahim Werrema John ututoke, unakumbukwa sana na mke wako kipenzi, Bi. Agatha, wazazi wako Mr. & Mrs John Keraryo, dada na kaka zako, baba mkwe mzee Soka, ndugu jamaa na marafiki. Kimwili hauko nasi lakini busara na upendo uliokua nao kwetu bado vinaishi nasi. Mapenzi ya bwana na yatimie. 

  AMEN

  0 0

  Kampuni ya Maxcom Africa (Maxmalipo) inawakaribisha watanzania kushiriki manunuzi ya hisa za makampuni yaliyoorodheshwa kwenye Soko la hisa la Dar es salaam(DSE) kwa njia ya mtandao (simu za kiganjani) na kufanya malipo kupitia kwa mawakala wa Maxmalipo waliopo nchi nzima Tanzania.
  Mkuu wa kitengo cha Masoko na Ubunifu wa Kampuni hiyo, Deogratius Lazari Mosha, amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo kwamba Maxcom Africa (Maxmalipo) ikishirikiana na soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) kwa kutumia mfumo madhubuti wa simu za viganjani unamwezesha Mtanzania kuweza kushiriki kwenye Manunuzi ya hisa za makampuni yaliyoorodheshwa kwenye soko la awali la mitaji (primary markets ) kwa kupiga *150*36#, ameongeza kwamba baadhi ya makampuni hayo kwa sasa ni Vodacom na TCCIA.

  Akifafanua hili, Lazari amesema ili Mtanzania aweze kushiriki Manunuzi ya hisa kwa mfumo huu anatakiwa kubonyeza *150*36# kisha ataingia kwenye Menyu ya soko la hisa na Kuchagua IPO kisha atachagua kampuni anayotaka kununua hisa, baada ya kufanya hivyo mteja atalazimika kujisajili na kisha atapata nafasi ya kuainisha idadi ya hisa anazohitaji(zisizo pungua 100 katika awamu ya kwanza).

  Lazari ameongeza kwamba baada ya hatua ya uanishaji wa hisa, mteja atapokea ujumbe mfupi wa simu kutoka DSE wenye nambari ya kumbukumbu ya malipo, idadi ya hisa na kiasi anachotakiwa kulipia. Ili kukamilisha malipo haya mteja atatakiwa kufika kwa wakala yeyote wa Maxmalipo aliye karibu naye na kufanya malipo kama ilivyo ainishwa kwenye ujumbe aliopokea kwenye simu yake. Mteja anahimizwa kuhakikisha kwamba anapatiwa risiti pindi anapolipia hisa kwa mawakala wa Maxmalipo ili kutunza kumbu kumbu zake.

  Kwa kuongezea, Lazari ameeleza kwamba mfumo huu rafiki unamwezesha mteja kushiriki manunuzi ya hisa kadiri ya uwezo wake (Mfano, Mteja Anaweza kila siku akanunua hisa 100 kulingana na kipato chake au zaidi). Pamoja na mwakala wa Maxmalipo mteja anaweza kulipia kwa kutumia mitandao ya simu.

  Mfumo huu wa kununua hisa kwa simu za kiganjani ( *150*36#) umetengenezwa na kampuni ya kitanzania ya Maxcom Africa (Maxmalipo) ikishirikiana na Soko la hisa la Dar es Salaam(DSE) na ni mfumo rasmi wa kuuza na kununua hisa kwenye soko la hisa .

  Watanzania wamepewa wito wa kushiriki ununuzi wa hisa kwa njia ya simu ya kiganjani na kuhakikisha wanafanya malipo mapema kupitia kwa mawakala wa Maxmalipo walioko nchi nzima takribani Mawakala Elfu kumi na sita .

  0 0

  Na Geofrey Tengeneza - Berlin

  Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imeingia mkataba na kampuni tatu za Ulaya na Marekani ili kutayarisha mikakati maalumu ya utangazaji utalii mahsusi katika nchi za Ujerumani, Uingereza na Marekani ikiwa ni utekelezaji wa mkakati wa kuhakikisha inajipenyeza zaidi kaika masoko ya makuu ya utalii yalioanishwa katika mkakati wa Utangazaji utalii wa kimataifa wa miaka mitano katika masoko mbalimbali ya utalii duniani.

  Mkataba huo umesainiwa katika maonesho ya Kimataifa ya utalii ya ITB katika banda la Tanzania na Mkurugeni Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bi Devota Mdachi na Wakurugenzi wakuu wa kampuni hizo ambazo ni Africa Oracle Company kwa ajili ya soko la Uingereza, 7o7 Marketing GmbH Ltd kwa ajili ya soko la Ujerumani na Tourism Intelligence International kwa jili ya soko la Marekani.
  Bw. Recknagel Markus, Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya7o7 Marketing GmbH ya ujerumani na Mkurugenzi mwendeshaji wa TTB Bi Devota Mdachi wakionyesha jarida la TTB lililotayarishwa kwa lugha ya Kijerumani kwa lengo la kuutangaza utalii na vivutio vya utalii vya Tanzania katka soko la ujerumani na nchi zinazozungumza Kijerumani.

  Kwa Mujibu wa Meneja Masoko wa TTB Bw. Geofrey Meena pamoja na kuwa mkakati wa Kimataifa wa miaka mitano umeainisha masoko kumi na mbili ya utalii duniani, wameamua kuanza na masoko hayo matatu kwa kuwa ni miongoni mwa masoko muhimu kwa Tanzania hivi sasa. Masoko makubwa manne yanaoongoza kwa watalii wengi kutembelea Tanzania ni Marekani, Uingereza, Italia na Ujerumani.

  “Kwa kuanzia tumeanza na masoko haya na baadae tutakwenda pia katika masoko mengine. Wataalamu hawa kutoka masoko hayo matatu wakikamilisha kututayarishia mikakati hiyo maalumu kwa kila soko itatusaidia kujua mbinu gani sahihi za kujipenyeza na kulikamata kikamilifu kila soko” alisema Bw. Meena

  Kusainiwa kwa mikataba hii kumefanyika siku moja tu baada ya Bodi ya Utalii Tanzania kusaini mkataba wa ushirikiano na Mamlaka ya Ukuzaji Utalii ya Mauritius katika utangazaji wa pamoja wa utalii wa nchi hizo mbili.
  Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bi Devota Mdachi (kushoto) na Dr. Auliana Poon Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni Tourism Intelligence International wakisaini mkataba kwa ajili ya mkakati wa TTB kwa ssoko laMarekani huku Mwenyekiti wa TTB Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akishuhudia utiaji saini huo.
  Bi Devota Mdachi, Mkurugenzi Mwendeshaji w TTB akibadilishana mkataba na Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya 7o7 Marketing GmbH Limited Bw. Recknagel Markus mara tu baada ya kusaini mkataba huo kwa ajili ya soko la Ujerumani.
  Dr. Auliana Poon wa Kampuni ya Tourism Intelligence International ya Marekani akibadilishana mkataba na Bi Deota Mdachi, Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB mara baada ya kusaini.

  0 0

   Kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali hapa jijini Dar es salaam leo, soko la Sinza limelazimika kufungwa kwa muda kutoka na kujaa maji eneo lote la soko hilo.
   Barabara nyingi za Dar leo zimejaa maji, hali inayopelekea magari mengi 'kubuma' kama ionekanavyo pichani hapa.
  Afande akitafakari jambo kufuatia uwingi wa maji katika barabara ya Bagamoyo eneo la Goigi jijiji Dar es salaam leo.
  Wadau wakifanya mambo katika moja ya chemba iliyoziba kutoka na wingi wa uchafu uliokuwa umesombwa na maji hayo.
   Magari yote yamelazimika kupita upande mmoja wa barabara kutoka na wingi wa maji upande mwingine.


  0 0

  Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza(TPS SACCOS LTD) akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika afungue rasmi Mkutano Mkuu wa Nne wa TPS SACCOS Ltd leo Machi 13, 2016 uliofanyika kwa siku moja katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga – Dar es Salaam.
  Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Tusekile Mwaisabila ambaye ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Lindi akitoa hoja ya kuthibitisha Notisi ya Mkutano Mkuu mbele ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Nne uliofanyika kwa siku moja katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga – Dar es Salaam.
  Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika, Bw. Colin Nyakunga akitoa salaam ya Ushirika kabla ya kutoa Hotuba ya Ufunguzi wa  Mkutano Mkuu wa Nne wa TPS SACCOS Ltd leo Machi 13, 2016 uliofanyika kwa siku moja katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga – Dar es Salaam.
  Wajumbe wa Mkutano Mkuu ambao ni Maafisa, Askari na Watumishi raia wa Jeshi la Magereza wenye vyeo mbalimbali ambao ni Wanachama wa TPS SACCOS LTD kutoka Mikoa yote Tanzania Bara wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi katika Mkutano huo.


  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewataka wadau wa usafirishaji kuweka mikakati dhabiti ya kupunguza ajali za barabarani nchini ili kuokoa maisha ya watanzania wanaofariki dunia kila mwaka kutokana na ajali hizo.

  Waziri Mbarawa ametoa agizo hilo alipofungua mkutano maalumu wa kanda wa kujadili na kutathmini changamoto za usalama barabarani na jinsi ya kuzikabili unaofanyika jijini Dar es salaam.

  Profesa Mbarawa amesema kuwa ajali za barabarani zimekuwa zikikatisha maisha ya watanzania wengi kila mwaka ambao wengi wao ni vijana na nguvu kazi ya taifa hivyo ni jukumu la wadau kubadilisha hali ya usalama barabarani.

  “Kama tukijifunza vizuri na kuyafanyia kazi mafunzo haya tunaweza kubadili hali ya usalama barabarani kwani inaumiza kuona vifo vya watu wengi vinavyotokana na ajali za barabarani hivyo ni wakati wa Jeshi la Polisi, na Mamlaka ya Usafiri wa nchi Kavu na Majini SUMATRA kushirikiana kukomesha ajali hizi”. Amesisitiza Profesa Mbarawa.

  Ameongeza kuwa Serikali itatoa kipaumbele kwa yale yatakayojadiliwa na kuamuliwa katika mkutano huo ili kuongeza kasi ya udhibiti wa ajali za barabarani hapa nchini na kupunguza idadi ya ajali zinazoepukika.

  Naye Mwenyekiti wa Mfuko wa Barabara nchini (RFB), Bw. Joseph Haule amesema kuwa Bodi hiyo inashirikiana na taasisi nyingine katika kuhakikisha ubora wa miundombinu ya barabara inakuwa salama na kupitika wakati wote.

  Kwa upande wake Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani hapa nchini Mohamed Mpinga amesema kikosi cha usalama barabarani kitaendelea kuhakikisha kuwa ajali za barabara zinadhibitiwa.

  “Suala la ajali za barabarani ni jukumu letu sote kwa pamoja hivyo tukiungana kwa pamoja na kushirikiana tutaweza kupunguza ajali hizi kwa kiwango kikubwa”. Amesema Kamanda Mpinga.

  Mkutano huo wa siku mbili ulioanza leo jijini Dar es salaam umewakutanisha wadaau mbalimbali wa kimataifa wa masuala ya ujenzi na usimamizi wa usalama wa watu na mali wawapo barabarani .
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wadau waliohudhuria mkutano wa siku mbili wa Usalama barabarani katika ukumbi wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini (RFB) Bw. Joseph Haule akitoa taarifa ya udhibiti wa ajali za barabarani kwenye mkutano wa wadau wa usalama barabarani uliofanyika jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kulia) akiongea na Naibu Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano wa Namibia Mhe. Sankwasa James Sankwasa wakati wa mkutano wa siku mbili wa kutathmini usalama barabarani, Jijini Dar es Salaam.


  0 0


  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema jiji la Dar es Salaam linatakiwa kubadilika  katika kufikia viwango vya majiji ya kimataifa. Makonda ameyasema hayo leo wakati akikabidhiwa barabara ya kurasini iliyojengwa kwa zege yenye urefu wa Kilomita moja, amesema  barabara hiyo ndio kiungo kikubwa kwa upande wa bandari.

  Mkuu wa Mkoa ametoa onyo kwa kampuni za ukandarasi zinazofanya shughuli zao hapa jijini chini ya viwango ya kuwa  kuanzia sasa kampuni hizo pale zitakapotambuliwa zitatakiwa kurudia miradi hiyo kwa gharama zao binafsi na kupewa adhabu ya kufungiwa kandarasi yoyote hapa jijini  kwa miaka mitatu.

  "Wananchi wamechoka kutengeneza magari kila mara kutokana na ubovu wa barabara, wakina mama wamekuwa wakijifungulia barabarani hasa nyakati za mvua kama hizi kutokana na ubovu wa barabara zilizojengwa hata miezi sita haijapita" amesema Makonda .

  Amesema barabara hiyo imejengwa na kampuni ya kizalendo ya Grant Tech Company ya jijini Dar es Salaam na maombi ya barabara ni miezi miwili iliyopita lakini imekamilika kwa muda mwafaka .

  Makonda amesema miundombinu ya barabara ni moja ya nyenzo ya ukuaji wa kiuchumi kwa taifa lolote lile. Makonda ameelekeza manispaa zote zisimamie vyema fedha za barabara ili kupunguza adha za usafiri kwa  wananchi wa Dar es salaam ambao wamechoka kupita kwenye barabara zenye mashimo zinazoleta hitilafu hata kwa vyombo vyao vya usafiri.

  Makonda amemshukuru mkandarasi huyo kwa uzalendo wake na kujitoa kwake kuijenga Dar es salaam kwani kwa kufanya hivyo ni  ndoto ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ya kukuza uchumi na kufikia Tanzania ya viwanda  inaendelea kutimia.

  Mkandarasi huyo (Grant tech), Masito Mwasingo amesema kuwa wamefanya ujenzi kwa muda mwafaka kutokana umuhimu na kuunga kuunga mkono utendeji kazi wa serikali ya mkoa wa Dar es salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva na watendaji wakitembelea barabara Kusasini iliyojengwa kwa zege yenye urefu wa Kilomita moja leo jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza katika uzinduzi wa wa akikabidhiwa barabara ya kurasini iliyojengwa kwa zege yenye urefu wa Kilomita moja leo jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva akizungumza katika uzinduzi wa kukabidhiwa barabara ya kurasini iliyojengwa kwa zege yenye urefu wa Kilomita moja leo jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda pamoja na Mkuu Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva  wakikata utepe kuashilia kukabidhiwa barabara ya Kusasini iliyojengwa kwa zege yenye urefu wa Kilomita moja leo jijini Dar es Salaam.
  Muonekano wa Baarbara hiyo

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein walipokutana kwa mazungumzo Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Jumatatu Machi 13, 2017. Picha na IKULU
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahi jambo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein walipokutana kwa mazungumzo Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Jumatatu Machi 13, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein walipokutana kwa mazungumzo Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Jumatatu Machi 13, 2017.


  0 0  0 0


  Warembo wakiwa katika picha ya pamoja siku ya Jumamosi March 11, 2017 Fairfax, Virginia kwenye V.I.P. Reception Awards Gala iliyohudhuriwa na Balozi wa Kenya nchini Marekani Mhe. Robinson Njeru Githae
  Mwanamitindo nguli wa kimataifa Asya Idarous Khamsin akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Kenya nchini Marekani Mhe. Robinson Njeru Githae.

   Mrembo akiwa katika vazi la mwanamitindo nguli wa kimataifa Asya Idarous Khamsi.

   Vazi kutoka kwa mama mitindo wa kimataifa Asya Idarous Khamsin.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete amesema kuwa anapenda kuendelea kufanya shughuli zinazosaidia kuleta maendeleo kwa watu na jamii.

  Akizungumza na waandishi wa habari  leo Jijini Dar es salaam, wakati alipokuwa  akizindua Taasisi yake ya Jakaya Kikwete (Jakaya Mrisho Kikwete Foundation)  alisema kuwa kwa muda mrefu amekua akipenda na kujihusisha na shughuli mbalimbali za maendeleo ya watu na hivyo Taasisi yake itamsaidia katika kufikia malengo yake.
  “Nimetumia muda wangu kwa ajili ya maendeleo ya watu, baada ya shule, nilikitumikia Chama cha Mapinduzi(CCM), nilitumikia Jeshi na baadae Serikali, kwangu Taasisi hii imekuwa chombo kitakachonisaidia kuendeleza maono yangu na kutimiza ndoto zangu katika kuendelea kusaidia watu” alisema Dkt. Kikwete.

  Akiizungumzia taasisi hiyo Kikwete alisema kuwa, Taasisi yake ina wajumbe 9 kutoka sehemu mbalimbali duniani wenye nyadhifa na heshima kubwa katika nchi zao.

  Ameongeza kuwa Taasisi hiyo imejikita kusaidia jamii katika maeneo makubwa manne, maendeleo ya jamii  hasa katika kujikita kuondoa umaskini, mabadiliko ya hali ya nchi na kilimo  kwa wakulima wadogo.

  Pia Taasisi hiyo imejikita katika huduma za afya, kutokomeza malaria na afya ya mama na mtoto.

  Maeneo mengine ambayo Taasisi hiyo inajihusisha nayo ni  ni elimu kwa  vijana ili  kukuza vipaji vyao na kuwapa mafunzo kuhusu uongozi bora, usawa wa kijinsia na namna ambavyo Serikali inavyotoa huduma kwa wananchi.

  Aidha, alisisitiza kuwa Taasisi yake itaisaidia Serikali, mashirika na Taasisi mbalimbali ili kushirikiana kuwaletea maendeleo watanzania na watu mbalimbali duniani.

  Dkt. Kikwete amewataja Wajumbe wa Bodi ya Udhamini ya Taasisi yake kuwa ni Balozi Ombeni Sefue aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Profesa Rwekaza Mukandala Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Willium Mahalu Mhadhiri Mwandamizi  katika Chuo Kikuu cha Tabibu cha Bugando.

  Wengine ni Balozi Mwanaidi Maajar aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Abubakar Bakhresa, Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa, Genevieve Sangudi  Mtaalamu wa Masuala ya kibishara ya Kimataifa kutoka Marekani.

   Pia wapo Dato’ Sri  Idris Jala, Waziri asiyekuwa na Wizara Maalumu nchini Malyasia,  Balozi Charles R. Stith aliyekuwa Balozi wa zamani wa Marekani nchini Tanzania pamoja na Dkt. Carlos Lopes ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taaisi ya Mafunzo na Utafiti ya Umoja wa Mataifa (UNITAR).

  Taasisi ya Maendeleo ya Jakaya Kikwete ilisajiliwa tarehe 17, Februari 2017, na hii ni mara ya kwanza kwa wajumbe wa bodi ya wadhamini kukutana tangu kuanzishwa kwake. Imeandikwa na Immaculate Makilika- MAELEZO

  0 0


  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamiii

  Ikiwa imepita zaidi ya miezi minne tangu shindano la Miss Tanzania 2016  lifanyike huko jijini Mwanza na taji lake kuchukuliwa na mrembo Diana Edward, bado mrembo huyo hajakabidhiwa zawadi yake ya gari na kiasi cha pesa Shilingi milioni mbili.

  hata hivyo katika siku ya mwisho wa shindano hilo, mrembo Diana alionekana akikabidhiwa gari aina ya Toyota IST, Ukumbini hapo kumbe ilikuwa danganya toto kwa watu wote waliofika katika shindano hilo ili waweze kuamini kuwa mrembo huyo kuwa kapewa gari.
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura akionekana kumkabidhi gari mrembo huyo siku muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi.

  Diana ambaye alikaa kwenye gari hiyo akiwa na furaha kubwa sana akimini kuwa ndio mchuma wake wa kwenda nao nyumbani kwao lakini mpaka leo mrembo huyo bado ni mtu wa kupanda daladala , Bajaj na Bodaboda.

  Akizungumza na Ripota wetu, afisa habari wa Baraza la Sanaa nchini (BASATA), Agnes Kimwanga amesema kuwa waliwaita kamati ya Miss Tanzania katika kikao cha tahmini na wao kukiri kuwa hawajampatia zawadi zake zote mshindi huyo pamoja na washiriki wengine  wanne.

  “mara baada ya kujieleza katika kikao chetu cha Tathmini wakajitetea kuwa watatoa zawadi hizo tarehe 30 Aprili mwaka huu kwa kumpa Miss Tanzania 2016 zawadi yake ya gari na kiasi chake cha pesa Milioni mbili ambacho kimebaki” Amesema Agnes.
  Miss Tanzania 2016, Diana Edward akiwa na washiriki wenzake siku aliyotwaa taji hilo.

  Akithibitisha hilo, Afisa habari wa Miss Tanzania, Haiden Ricco alikiri kutomlipa mrembo huyo stahiki zake zote ikiwepo gari.

  "Ni kweli mrembo wetu hajawalipwa na sio yeye peke yake, hata wale warembo wengine wanne hawajalipwa pia" alisema Ricco.

  Amesema kuwa fedha zilizobakia wanazodaiwa na warembo hao ni kiasi cha jumla ya shilingi milioni nane hivyo zote watalipwa kuanzia mwezi huo wanne.

  Rico ametaja kuwa shindano lao kwa kutegmea wadhamini wamejipanga kuanzia mwezi ujao kuanza kuwalipa warembo hao kadri watakavyokuwa wanapata fedha kutoka kwa wadhamini na wadau wa shindano hilo.

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akifungua semina elekezi kuhusu mabadiliko ndani ya Chama, kwa Wenyeviti na Makatibu wa mikoa na wa wilaya na watendaji, leo katika Ukumbi wa Sekretarieti katika Jengo la Ofisi ya Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma 
   Washiriki wakiwa kwenye semina elekezi kuhusu mageuzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi, leo katikaUkumbi wa Sekretarieti Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
   Washiriki wakiwa kwenye semina elekezi kuhusu mageuzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi, leo katikaUkumbi wa Sekretarieti Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
  Baadhi ya viongozi wakiwa kwenye semina elekezi kuhusu mageuzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi, leo katikaUkumbi wa Sekretarieti Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM-Zanzibar Dk. Abdalla Juma Abdallah, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu- Zanzibar, Vuai Ali Vuai, Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, na kutoka kulia ni Katibu mpya wa NEC Oganaizesheni, Lela Ame Silima na Katibu wa NEC Oganaizesheni mstaafu Mohammed Seif Khatib. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO.


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan leo amezindua mpango wa Ugawaji wa Vishwambi"Tablets" 5000,laptops na projectors kwa Shule za Msingi 10 za Jimbo la Dodoma Mjini.

  Mama Samia  amesisitiza kuhusu utunzaji wa vifaa hivyo na matumizi sahihi ya vifaa hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa ili kusaidia kuinua kiwango cha Elimu katika Jimbo la Dodoma Mjini

  Aidha Makamu wa Rais amepongeza jitihada na ubunifu wa Mbunge wa Jimbo hilo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi,Vijana na Ajira Ndg Anthony  Mavunde na kuahidi kuendelea kumpa ushirikiano katika kuwahudumia wanadodoma Mjini.

  Pamoja na hilo Mama Samia ameahidi kuunganisha Jimbo la Dodoma Mjini na mpango wa Umoja wa Mataifa wa kusaidia watoto wa kike kupitia mfumo wa ufundishaji kidigitali wa Sillicon Valley.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mradi wa Pro Futuro Bi. Rosemary Terry (kushoto) juu ya Vishikwambi (Ipad) vitakavyotumika katika kufundishia shule 10 zilizopo ndani ya jimbo la Dodoma mjini, kulia ni Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Anthony Mavunde . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).


   Makamu wa Rais Mama Samia  Suluhu Hassan (wa pili kutoka kushoto) pamoja na wageni waalikwa wengie wa meza kuu wakionesha baadhi ya Vishwambi mara baada ya kuuzindua mpango huo wa Ugawaji wa Vishwambi"Tablets" 5000,laptops na projectors kwa Shule za Msingi 10 za Jimbo la Dodoma Mjini. 
    Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali kwenye hafla fupi uzinduzi wa mpango wa Ugawaji wa Vishwambi"Tablets" 5000,laptops na projectors kwa Shule za Msingi 10 za Jimbo la Dodoma Mjini.
   Baadhi ya Wageni waalikwa kwenye hafla hiyo wakifuatilia kwa umakini tukio hilo
   Baadhi ya wanafunzi wakishuhudia tukio hilo adhimu kwao


older | 1 | .... | 1610 | 1611 | (Page 1612) | 1613 | 1614 | .... | 3285 | newer