Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

BOT GOVERNOR MEETS CEOs OF COMMERCIAL BANKS

0
0
NDULU
DISCOUNT RATE REDUCTION SHOULD MAKE BANKS THINK ABOUT LENDING RATES
The Bank of Tanzania Governor, Prof. Benno Ndulu, has urged banks and financial institutions to take note of the downward review of the discount rate from 16 per cent to 12 per cent in their operations.
“The Bank of Tanzania’s expectations are that the move will enhance credit growth and reduction in lending rates, he said.
Prof. Ndulu made the call during a meeting with chief executive officers (CEOs) of banks and financial institutions at the Bank of Tanzania headquarters in Dar es Salaam.
He, however, cautioned them, when disbursing loans, to ensure that only customers with good track record are being considered. This is due to the recent increase in non-performing loans (NPLs) among many banks.
The Bank of Tanzania reviewed the discount rate from 16 to 12 per cent effective from March 6, 2017. In its letter to banks, the Bank said the revised discount rate took into account the prevailing 91 and 182-day weighted average yields and the monetary policy stance geared towards sustaining price stability. It will also be used to discount Treasury securities.
On their part, CEOs of banks and financial institutions sought assurance from BoT as to the duration of being in force of the newly announced discount rate, lest they adjust their loan policies only for the discount rate to move upward without a warning.

More News Click here


TTB NA MAURTIUS KUUNGANISHA NGUVU KATIKA KUTANGAZA UTALII.

0
0
Na: Geofrey Tengeneza -Berlin

Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na Mamlaka ya Ukuzaji Utalii ya Mauritius zimetiliana saini mkataba wa ushirikiano baina yao katika kutangaza wa nchi hizo mbili kwa pamoja katika baadhi ya masoko ya masoko ya Marekani, China, Australia, India na masoko mengine barani la Ulaya. 

Mkataba huo uliosainiwa leo katika maonesho ya Utalii ya ITB na wakurugenzi wakuu wa taasisi hizo ambao ni Bi Devota Mdachi kwa upande wa Bodi ya Utalii Tanzania na Bw. Kelvin Ramkaloan kwa upande wa Mamlaka ya Ukuzaji Utalii ya Mauritius una lengo kuvutia watalii zaidi kutoka barani Ulaya, Amerika na Asia. 

Akizungumzia mkataba huo Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB Bi Devota Mdachi amesema kuwa katika mkataba huo wamekubaliana kushirikiana katika kutangaza vivutio vya utalii vya nchi hizo mbili sambasamba na kuhakikisha kuwa watalii wanaotembelea Mauritius ambayo ni maarufu kwa utalii wa fukwe wanatembela pia Tanzania kwa ajili ya utalii wa kutazama wa wanyama katika hifadhi zetu mbalimbail za Taifa , kupanda mlima Kilimanjaro na kutembelea maeneo mengine ya vivutio vya utalii. 

“Tutazitangaza nchi zetu kama maeneo pacha ya utalii lengo likiwa ni kutumia fursa ya watalii wanaotembelea Mauritus kwa ajili utalii wa fukwe kuunganisha safari zao na kujakutembela pia Tanzania kupitia shiika la ndege la Mauritus kwa ajili ya kujionea vivtio vyetu kama vile wanyama , mlima Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro, na vingine vingi ambavyo Mauritus hawana.” alisema Bi Devota Mdachi.

Mkurugenzi mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bibi Devota Mdachi (katikati) na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Ukuzaji Utalii ya Mauritius Bw. Kevin Ramkaloan (kushoto) wakisaini mkataba wa ushirikiano katika utangazaji wa utalii wakati wa maonesho ya Kimataifa ya utalii ya ITB Berlin Ujerumani. Anayeshuhudia kulia ni Mwenyekiti wa TTB Jaji mstaafu Thomas Mihayo.
Mkurugenzi mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bibi Devota Mdachi (katikati) na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Ukuzaji Utalii ya Mauritius Bw. Kevin Ramkaloan (kushoto) wakisaini mkataba wa ushirikiano katika utangazaji wa utalii wakati wa maonesho ya Kimataifa ya utalii ya ITB Berlin Ujerumani. Anayeshuhudia kulia ni Mwenyekiti wa TTB Jaji mstaafu Thomas Mihayo.
Mwenyekiti wa TTB Jaji mstaafu Thomas Mihayo akibadilishana mawazo na Mkuu wa Idara ya mauzo ya shirika la ndege la Condor Bw. Andre Horn muda mfupi baada ya TTB na Mamlaka ya Ukuzaji Utalii ya Mauritius kusaini makubaliano ya ushirikiano.

Benki ya CRDB tawi la Mlimani City yaadhisha siku ya wanawake na wateja wake

0
0
Baadhi ya wateja wa akaunti ya Malkia ya Benki ya CRDB tawi la Mlimani City wakiwa na zawadi zao walizopewa na benki hiyo wakati wa kusherehekea siku ya wanawake iliyoadhimishwa leo ofisini kwao jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wateja wa akaunti ya Malkia ya Benki ya CRDB tawi la Mlimani City pamoja na maofisa wa Benki hiyo, wakisherehekea siku ya wanawake iliyoadhimishwa leo ofisini kwao jijini Dar es Salaam.
wafanyakazi wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City wakiwa katika picha ya pamoja wakifurahia siku ya wanawake duniani.
Meneja Huduma kwa Wateja wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Lilian Lema akigawa biskuti kwa wateja wa benki hiyo Leo ikiwa ni sehemu ya kuazimisha siku ha wanawake duniani. Sherehe hizo zimefanyika katika benki hiyo tawi la Mlimani City Jijini.

COCA-COLA YAZINDUWA MUONEKANO MPYA WA AMSHA SHANGWE NA COCA-COLA MKOANI MBEYA LEO

0
0
Mkurugenzi Mkazi wa Kampuni ya CocaCola Tanzania, David Karamagi akionja Msisimko na muonekano mpya wa Coca-Cola kwanza uliobatizwa jina la Amsha Shangwe na Coca-Cola uliozinduliwa leo katika kiwanda cha Coca-Cola kwanza kilichopo Iyunga Jirani na Tazara mkoani Mbeya, timu nzima ya Coca-Cola kuzama Mtaani na kutambulisha muonekano Mpya wa Coca-Cola Amsha shangwe kwa wanambeya wote.
Mkurugenzi Mkazi wa Kampuni ya CocaCola Tanzania, David Karamagi akizungumza jambo wakati akiwapongeza wafanyakazi wa Coca-Cola kwanza kwa kufanya vizuri Katika mauzo na kuwataka wafanyankazi kuongeza bidii kwa kufanya kazi yakinifu katika masoko ili kuleta tija katika kampuni hiyo. 
 Meneja wa Coca-Cola Tanzania, Sialouire Shayo akizungumza jambo mbele ya wafanyakazi na wadau wa Coca-Cola kwanza (hawapo pichani) Katika hafra fupi ya kuzinduwa kampeni ya muonekano mpya wa Coca -Cola Mkoani Mbeya uendao kwa jina la Amsha Shangwe na Coca-Cola kwa wakazi wa Mkoa wa Mbeya.
Meneja Masoko wa Coca-Cola Tanzania, Peter Mpara Nae alipata Fursa ya kuelezea muonekano huo wa Amsha Shangwe na Coca-Cola kwa wakazi wa Mkoa wa Mbeya Katika hafra fupi ya kuzinduwa kampeni ya muonekano mpya wa Coca -Cola Mkoani Mbeya uendao kwa jina la Amsha Shangwe na Coca-Cola kwa wakazi wa Mkoa wa Mbeya..
Baadhi ya Wafanyakazi na wadau wa Coca-Cola kwanza wakipata burudani ya muziki sanjari na kupiga picha kwa pamoja kwa kuamsha shangwe na Coca-ColaKatika.

PICHA ZOTE NA MR.PENGO MMG MBEYA.

WAZIRI NAPE AONGOZA TULIA MARATHONI JIJINI MBEYA

0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye Akiwaongoza wakazi wa Jiji la Mbeya kwenye Mbio za Tulia Marathoni zilizofanyika jijini Mbeya akiwa ameambatana na aibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk Tulia Ackson Mwansasu Pamoja na Wadau Mbalimbali waliojitokeza kwenye Mbio hizo leo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye Leo ameongoza Wakazi wa Mkoa wa Mbeya kwenye Mbio za Tulia Marathoni zilizoandaliwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk Tulia Ackson Mwansasu Kupitia Taasisi yake ijulikanayo kama Tulia trust. Mbio hizo zilizohusisha KM 21 ,KM 5 na KM 2 kwa wazee zilifana baada ya Wakazi Wengi wa Mbeya Kujitokeza kwa Wingi Wakiwemo Viongozi Mbalimbali na Mabalozi wanaoziwakilisha Nchi zao Hapa Nchini,Lengo la Mashindano hayo ni kupata fedha kwa ajili ya uboreshaji wa huduma za afya na elimu hususani uboreshaji Majengo na vyoo katika sekta hizo.
  Rais wa Chama cha Riadha Nchini na Mkuu wa Mkoa wa Simuyu Mh Anthony MtakaAkimweleza Jambo Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk Tulia Ackson Mwansasu kabla ya Mbio za Tulia Marathoni zilizofanyika Jijini Mbeya leo wakiwa Pamoja na  Pamoja naAfisa Mtendaji wa Shear Illusions Tanzania Mama Shekha Nasser ( Kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa GS1 Tanzania Mama Fatma Kange
 Tulia Marathon lengo lake ni kukusanya fedha kwa ajili ya kuboresha huduma za afya na elimu, maeneo yanayolengwa kwenye afya ni Kituo cha Afya cha Ruanda kilichopo Mwanjelwa na Hospitali ya Wilaya ya Rungwe Makandana ambako utafanyika uboreshaji wa wodi ya wazazi,”

 Katika Elimu maeneo yanayokusudiwa kuboreshwa ni pamoja na Shule ya Wasichana ya Loleza ambayo itafanyiwa maboresho kwenye mabweni mawili na vyoo pamoja na shule tatu za msingi,” alisema Lwiza.Mshindi wa Mbio hizo Amejishindia kitita cha Sh. Milioni moja wa Pili Sh. 700,000 na wa tatu atapata Sh. 500,000.Katika Mbio fupi za kilomita mbili ambazo ziliwahusisha wabunge mbalimbali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwamo Naibu Spika Mwenyewe .
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye Katika Picha ya Pamoja na Afisa Mtendaji wa Shear Illusions Tanzania Mama Shekha Nasser ( Kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa GS1 Tanzania Mama Fatma Kange  Waliposhiriki Mbio Hizo leo Jijini Mbeya.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MWENYEKITI WA CCM DK. JOHN POMBE MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA MAGEUZI MAKUBWA MJINI DODOMA

0
0

 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana akizungumza mara baada ya kikao hicho kufunguliwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mkoani Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Dk. John Pombe Magufuli akielezwa jambo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kabla ya kuanza kwa kikao cha NEC mjini Dodoma leo. kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein. 
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akifungua kikao hicho leo kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma,Mh.Adam Kimbisa kabla ya kikao cha NEC kuanza mjini Dodoma eo.
Wajumbe wa NEC William Lukuvi akisalimiana na Mama Salma Kikwete kabla ya kikao kuanza mjini Dodoma,Pichani kati ni Mwigulu Nchemba.

Kikao cha NEC kikiendelea.


 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika foleni ya kuchukua chakula pamoja na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mkoani Dodoma.

YANGA YAVUTWA SHATI NA ZANACO TAIFA LEO, YATOKA SARE YA BAO 1-1

0
0
 Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

WAWAKILISHI wa Tanzania katika Michuano ya Kombe la Klabu Bingwa Afrika, "Dar Young Africans" wameshindwa kutamba kwenye kiwanja cha nyumbani katika mchezo wa kwanza dhidi ya Zanaco ya Zambia uliofanyika leo Jijini Dar es salaam.

Mchezo huo ulioanza saa 10 alasiri, ilikuwa ni Yanga iliyowachukua dakika 38 kuandika goli  la kwanza kupitia kwa Simon Msuva akiifungia goli la kuongoza akipokea pasi ya Justine Zulu.

Yanga walishindwa kutumia nafasi walizozipata na mpaka kufikia mapumziko Yanga wanaenda wakiwa kifua mbele.

Kipindi cha Pili kinaanza kwa kila upande kulishambulia goli la mwenzake, hali iliyompelekea Kocha George Lwandamina kufanya mabadiliko kwa kumtoa Donald Ngoma na Thaban Kamosoku na kumuingiza Juma Mahadhi na Emanuel Martin.

Katika Dakika ya 82, Atram Kwame anaisawazishai Zanaco wakitumia mwanya wa kutokuwa na maelewano baina ya mabeki wa Yanga.

Mpaka dakika tisa zinamalizika Yanga 1-1 Zanaco ambapo mechi ya marudiano inatarajiwa kuwa kati ya Machi 17-19.
 Nahodha wa Timu ya Zanaco, Ziyo Kola akiwania mpira wa juu na Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva katika mchezo wa Kombe la Klabu Bingwa Afrika, uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Timu hizo zimetoka sare ya kufungana bao 1-1.
 Beki wa Yanga, Hassan Kessy akikabiliana na Mshambuliaji wa Timu ya Zanaco ya nchini Zambia, Kennedy Musonda, katika mchezo wa Kombe la Klabu Bingwa Afrika, uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Timu hizo zimetoka sare ya kufungana bao 1-1.
 Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva akiruka 'Samasoti' mbele ya mashabiki wa Yanga, baada ya kuifungia timu yake goli, katika mchezo wa Kombe la Klabu Bingwa Afrika, uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Timu hizo zimetoka sare ya kufungana bao 1-1.
 Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma akiangalia wa kumpasia mpira, katika mchezo wa Kombe la Klabu Bingwa Afrika, uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Timu hizo zimetoka sare ya kufungana bao 1-1.
 Juma Mahadhi wa Yanga, akijarimu kupiga mpira wakati wa shambulizi katika lango la Timu ya Zanaco, wakati wa mchezo wa Kombe la Klabu Bingwa Afrika, uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Timu hizo zimetoka sare ya kufungana bao 1-1.

NEWZ ALERT:HAYA NDIO MAAMUZI YA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YALIYOTOLEWA LEO MJINI DODOMA


MASHINDANO YA MABALOZI WA MTOTO MFANYAKAZI WA NYUMBANI YAFANA JIJINI MWANZA.

0
0
Wanafunzi wa shule ya msingi Nyamagana wameibuka washindi kwenye mashindano elimishi kwa klabu za mabalozi wa mtoto mfanyakazi wa nyumbani dhidi ya wakubwa zao kutoka shule ya sekondari Nyakurunduma, zote za Jijini Mwanza.

Mashindano hayo yaliyoandaliwa na taasisi ya kutetea haki za mtoto mfanyakazi wa nyumbani (WoteSawa) ya Jijini Mwanza, yalijumuisha michezo mbalimbali ikiwemo maigizo, ngonjera pamoja na mashairi yenye jumbe za kuainisha aina za ukatili wanaokumbana nao watoto wafanyakazi wa majumbani ikiwemo vipigo, utumikishwaji na fursa ya kukosa elimu, na kuiasa jamii kuachana na vitendo hivyo.

"Ukiona mtoto anatendewa ukatili wa aina yoyote, paza sauti (toa taarifa) sehemu mbalimbali ikiwemo WoteSawa, polisi kupitia kitengo cha dawati la jinsia, kwa Mwenyekiti wa Mtaa ama Mtendaji wa Kata". Amesisitiza mgeni rasmi, Wambura.

Naye Mkurugenzi wa taasisi ya WoteSawa, Angel Benedicto, amebainisha kwamba bado watoto wafanyakazi wa majumbani wanakabiliwa na vitendo mbalimbali vya ukatili ikiwemo kutumikishwa kwa kuajiriwa ili kutembeza bidhaa mtaani kwa ujira mdogo, kunyimwa fursa ya kusoma pamoja na vipigo kutoka kwa baadhi ya waajiri hivyo taasisi hiyo inaendelea kutoa elimu katika jamii ili kuhakikisha vitendo hivyo vinatokomezwa.

"Lengo ni kupunguza ukatili wa watoto majumbani, kulinda haki za watoto, kuibua vipaji ikiwemo uchoraji na uigizaji ili kuvitumia katika kufikisha elimu ya kupambana na ukatili dhidi ya watoto". Imefafanua sehemu ya risala ya klabu za wanafunzi mabalozi wa mtoto mfanyakazi wa nyumbani kutoka shule ya msingi Nyamagana na Nyakurunduma sekondari, iliyosomwa na Neema Christopher. 
Shule ya msingi Nyamagana wakifurahia ushindi wao ambapo igizo wamepata asilimia 93 dhidi ya 92 za Nyamagana sekondari, Shairi Nyamagana wamepata asilimia 74 dhidi ya 85 za Nyakurunduma huku Ngonjera Nyamagana wakipata asilimia 91 dhidi ya 77 za Nyakurunduma. Ushindi wa jumla, shule ya Msingi Nyamagana wamepata asilimia 86 dhidi ya 85 za Nyakurunduma sekondari.
Mabalozi kutoka shule ya sekondari Nyakurunduma wakipokea kombe baada ya kushika nafasi ya pili kwenye mashindano hayo
Pia mabalozi wote wamepatiwa vyeti kwa kujitoa kuwa mabalozi wa mtoto mfanyakazi wa nyumbani.


VODACOM TANZANIA FOUNDATION YASHINDA TUZO MAALUM YA KUSAIDIA AFYA YA MAMA NA MTOTO

0
0
 Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC,Kanda ya Ziwa, Ayubu Kalufya(kushoto) akipokea tuzo kutoka kwa Mkurugenzi wa Asasi ya Nitetee Flora Lauo,Ikiwa ni tuzo maalum kwa  mchango wa kampuni hiyo kwa kusaidia afya ya mama na mtoto kupitia mfuko wa kusaidia jamii wa kampuni hiyo”Vodacom Tanzania Foundation”, kwenye hafla ya Nitetee Women's Awards iliyofanyika jijini Mwanza juzi. 
Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Kanda ya Ziwa,Ayubu Kalufya(katikati) Meneja Mauzo na Usambazaji wa kampuni hiyo Wilayani Magu,Gift Tesha(kushoto) na Meneja Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania PLC,Mwanza mjini, Victoria Chale wakifurahia tuzo maalum kwa  mchango wa kampuni yao walioshinda kwa kusaidia afya ya mama na mtoto kupitia mfuko wa kusaidia jamii wa kampuni hiyo”Vodacom Tanzania Foundation”, kwenye hafla ya Nitetee Women's Awards iliyofanyika jijini Mwanza juzi.

SHYROSE AWASILISHA MUSWADA BINAFSI KUSAIDIA WENYE ULEMAVU

0
0
Muswada binafsi wenye lengo la kutungwa kwa sheria ya kuwalinda albino umewasilishwa kwenye kikao kinachoendelea mjini Kigali, Rwanda. Muswada huo umewasilishwa bungeni na Mheshimiwa Shyrose Bhanji, mbunge wa Tanzania. Katika muswada huo, Bhanji ameelekeza haki za msingi zinazopaswa kutolewa kwa walemavu hao kutoka Serikalini, Taasisi binafsi na kwenye jamii zetu. Muswada huo kama utapitishwa na Bunge na hatimaye kukubalika na Marais wa Afrika Mashariki, utatumika kwa nchi zote za Afrika Mashariki na utakuwa umesaidia watu wenye Ualbino. Mheshimiwa Shyrose Bhanji[/caption] "Ninamshukuru Mungu kwa fursa hii, " anasema Bhanji huku akisema kwamba kwake yeye jana ilikuwa ni siku ya furaha kubwa kwani hatimaye aliweza kuwasilisha bungeni muswada huo binafsi ambao unaoitwa The EAC Protection Of People with Albinism Bill 2017. Mwanamuziki mahiri nchini Chege Chigunda aliandika katika page yake ya Instagram ambapo alimpongeza mbunge huyo kwa namna anavyofikiri na kutetea walemavu aliandika: “Hongera sana Mbunge wetu wa Afrika Mashariki Mhe. ShyRose Bhanji @shyrosebhanji kwa kupigania haki za ndugu zetu wenye ualbino. Hakika umeacha alama kubwa ya uwakilishi wako Tanzania na Afrika Mashariki. Tunajivunia.”
Kipande cha nakala ya muswada huo.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MARCH 12,2017

FATIKIA HOTUBA YA MWENYEKITI WA CCM, DKT. MAGUFULI KUPITIA HAPA

0
0
Kwa wale ambao mpo mbali na Luninga matangazo ya moja kwa moja 'Live' kutoka Mkutano Mkuu Maalum wa CCM ambao Mhe. Rais Magufuli anahutubia muda huu mnaweza kuyapata matangazo hayo kupitia tovuti rasmi ya Rais ambayo ni www.ikulu.go.tz 

Matangazo haya yanarushwa kupitia TBC1. Vituo vingine vya Televisheni vinavyorusha matangazo haya ni Azam Two, ITV, Star TV, Clouds TV, Chanel Ten, Vituo vya redio mbalimbali na vingine ambavyo sikuvitaja.
KARIBUNI

MWENYEKITI WA CCM,RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AONGOZA MKUTANO MKUU MAALUM MJINI DODOMA

0
0
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri wa Tanzania, Dk. Joseph Magufuli akiwahutubia wajumbe wapatao 2356,ambapo walipaswa kuwa wajumbe 2380 katika mkutano huo Mkuu Maalum wa CCM uliokuwa na lengo kuu la kufanya baadhi ya mabadiliko ndani ya Katiba ya chama hicho,ambapo mabadiliko hayo yamepitishwa kwa asilimia 100 na wajumbe hao waliohuhudria mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza mambo mbalimbali mbele ya wajumbe waliohudhuria katika Mkutano Mkuu Maalum mjini Dodoma.

Baadhi ya Wajumbe wa mkutano mkuu Maalum wa CCM wakishangilia kwa shangwe huku wakiwa na mabango yao yakionesha mikoa wanayoiwakilisha.

 Sehemu ya baadhi ya wajumbe wa mkutano huo pamoja na wageni waalikwa wakiwa tayari ukumbini.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri wa Tanzania, Dk. Joseph Magufuli akisalimiana na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho na Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete wakati akiwasili katika ukumbi wa mkutano mkuu wa CCM, Mjini Dodoma
 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri wa Tanzania, Dk. Joseph Magufuli akisalimiana na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM,Waziri Mkuu Mh. Kasim Majaliwa wakati akiwasili katika ukumbi wa mkutano huo.
  Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri wa Tanzania, Dk. Joseph Magufuli akiwa pamoja na viongozi wengine wastaafu wa Serikali na kichama walipowasili kwenye ukumbi wa mkutano na kukaribishwa na wajumbe.
 Mabalozi na wawakilishi kutoka sehemu mbalimbali  ndani na nje ya nchi wakiwa wamehudhuria Mkutano Mkuu Maalum wa CCM,mjini Dodoma.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Fighting for his life - please help

0
0
Haji Rajab is in a coma fighting for his life. He was found three days ago by a passerby unresponsive on the side of a road while on his usual exercise routine in the park. A CPR attempt to stabilize him, an ambulance ride to ER and eventually a medivac flight to the Houston medical center, Haji is still unconscious. The doctors at the medical center are still unclear as to what caused his heart to fail and are conducting numerous tests to determine what to do next. He is hooked to a machine helping his now weak heart pump.

Haji was supposed to meet his family for a celebration of their son's school achievements after his exercise. This humble father of two beautiful boys had his wife worried when he was uncharacteristically late and her phone calls to him went unanswered for a long time. Her last phone call was answered by the paramedics who were busy working to resuscitate him.

Haji is going to need long-term medical and emotional care. His family is overwhelmed by his condition, the potential piling up of the medical bills, and what to do about living expenses.

We need your help to ensure that his wife focuses on his recovery rather than the worsening financial situation. Please help by praying for him, donating to cover the expense, and forwarding this message to others who can do the same.

Haji is fighting for his life. Please help him so he gets to go home to celebrate his son's achievement. The boy is still waiting for him.

The family wants to thank all of the medical staffs who are working extra hard to help Haji recover. Thank you for your support and contribution.
Help spread the word!


NYAYO ZA ZAMADAMU ZATIKISA MAONESHO YA ITB UJERUMANI

0
0
Picha ya mchoro wa binadamu wa kale wakitembea katika eneo la Laetoli lililoko km 45 kusini mwa Olduvai gorge. 
Na Geofrey Tengeneza- Berlin.

Nyayo na picha za michoro ya binadamu wa kale (zamadamu) zinazooneshwa katika banda la Tanzania kwenye maonesho ya Kimataifa ya ITB yanayoendelea hapa Berlin Ujerumani sambamba na maelezo sawia ya historia yake inayotolewa na mhifadhi wa Paleontolojia (masalia ya kale) Dkt. Agnes Gidna kutoka Makumbusho ya Taifa Bi wakishirikiana na maafisa waandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania inawapagaisha maelfu ya wageni wanaotembela banda la Tanzania katika maonesho hayo.

Nyayo na michoro hiyo ya binadamu wa kale anayesadikiwa kuishi miaka takribani milioni 4 iliyopita katika eneo la Laetori kilometa 45 kusini mwa Oldvai gorge pamoja na vielelezo mbalimbali vya vivutio kadhaa muhimu vya Tanzania kama vile mlima Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro, wanyama wanaohama katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti n.k vimekuwa chachu ya kuvutia wageni wanaotembelea banda la Tanzania ambao pia wameonesha dhamira kubwa ya kuitembelea Tanzania.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bi Devota Mdachi pamoja na utangazaji mkubwa wa vivutio mbali mbali vya utalii vya Tanzania unaofanywa katika maonesho haya, TTB imeamua pia mwaka huu kuweka mkazo maalumu katika kuitangaza Tanzania kama chimbuko la binadamu wa kale.
Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania Bw. Geofrey Meena (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa wageni kuhusu vivutio mbalimbali vilivyopo Tanzania kwa wageni wanaotembelea banda la Tanzania katika maonesho ya ITB.
Mhifadhi wa Masalia ya kale (Palentolojia) wa makumbusho ya Taifa Dkt. Agnes Gidna akitoa maelezo kuhusu historia ya binadamu wa kale pamoja na nyazo zake zilizo umbuliwa Laetori Tanzania kwa wageni wanaotembelea banda la Tanzania .
Mtangazaji wa kituo cha Umma cha televisheni cha Ujerumani Bw. Hoeks akifanya mahojiano mubashara na Mhifadhi wa Palentolojia wa Makumbusho ya Taifa Dkt. Agnes Digna mbele picha ya mchoro na nyayo za zamadamu ndani ya banda la Tanzania lililopo katika maonesho ya ITB Berlin Ujerumani.

WATANGAZAJI WA MICHEZO WATAKIWA KUZINGATIA MAADILI

0
0
 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo, Yusuph Omari akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo na Warsha ya Wanahabari za michezo  juu ya maadili ya utangazaji kwenye radio na Televisheni na kuzingatia taaluma.
 Mkurugenzi mtendaji wa makampuni ya Superdoll, Jamal Baiser akizungumza wakati wa mafunzo hayo kwa watangazaji wa waandishi wa habari za michezo
 Mwalimu Alex Kashasha akitoa mada juu ya kuwaleta wasikilizaji na watazamaji kuwa sehemu ya watu waliopo uwanjani pasipo kusababisha mfarakano wa moyo na kulaumu marefa na wachezaji kutokana na aina ya utangazaji tulionao sasa
 Baadhi ya washiriki wa Semina hiyo wakifatilia kwa makini  masomo yalikuwa yakitolewa katika mafunzo hayo

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Waziri Mahiga ampokea Mjumbe Maalum kutoka Ujerumani

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akizungumza na Mjumbe Maalum, Balozi Harro Adt aliyewasilisha Ujumbe Maalum kutoka kwa Kansela wa Ujerumani, Mhe. Angela Merkel kwenda kwa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Pamoja na mambo mengine walizungumzia pia namna ya kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizi mbili.
Mazungumzo yakiendelea.
Waziri Mahiga akiagana na Balozi Adt mara baada ya kumaliza mazungumzo. 
Waziri Mahiga (wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mjumbe Maalum, Balozi Adt (wa nne kushoto) pamoja na Maafisa Waandamizi kutoka Wizarani pamoja na Ubalozi wa Ujerumani nchini. 

=================================================== 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga amesema kuwa Tanzania na Ujerumani zitaendelea kuimarisha ushirikiano katika masuala mbalimbali ikiwemo yale yanayohusu kudumisha amani na usalama duniani pamoja na kuheshimu misingi ya haki za binadamu kupitia Jumuiya za Kikanda na Kimataifa.

Mhe. Waziri Mahiga ameyesema hayo alipokutana kwa mazungumzo na Balozi Harro Adt, Mjumbe Maalum wa Kansela wa Ujerumani, Mhe. Angela Merkel kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli alipofika Wizarani kwa ajili ya kuwasilisha ujumbe huo.

Katika mazungumzo yao, Mhe. Waziri Mahiga alisema kuwa, Ujerumani na Tanzania zina mahusiano ya kihistoria tangu enzi za ukoloni hadi sasa. Katika masuala ambayo Tanzania inanufaika na ushirikiano huo ni pamoja na ujenzi wa miundombinu, maboresho katika sekta ya elimu na mchango katika uhifadhi wa wanayamapori.

“Uhusiano wa Tanzania na Ujerumani ni wa kihistoria tangu ukoloni. Hata hivyo Ujerumani wamejaribu kutafsiri ushirikiano wetu katika misingi bora sasa kuliko ile ya kikoloni. Ujerumani imekuwa ikiisaidia Tanzania moja kwa moja katika sekta mbalimbali kama elimu, wanyamapori na miundombinu na misaada mingine imekuwa ikipitia Umoja wa Ulaya” alisema Waziri Mahiga.

Akizungumzia ziara ya Balozi Adt nchini, Mhe. Waziri Mahiga alisema Mjumbe huyo Maalum wa Kansela wa Ujerumani ameleta ombi kwa Mhe. Rais na kwa Watanzania la kuiunga mkono Ujerumani kwenye nafasi ya Mjumbe asiye wa Kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakati wa uchaguzi utakaofanyika mwaka 2018. Aliongeza kusema kuwa, Ujerumani imedhamiria kugombea nafasi hiyo ikiwa na dhamira ya kuunga mkono mageuzi ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ikiwemo kuziunga mkono nchi za Afrika kwenye harakati za kupatiwa nafasi mbili za kudumu kwenye Baraza hilo.

Aidha, Mhe. Waziri Mahiga alifafanua kwamba, katika kufikia malengo hayo Ujerumani imejiwekea misingi mikuu minne ambayo ni:- Kusaidia jitihada za amani na usalama duniani; Kusimamia Haki ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa; Kuhamasisha mageuzi ya Teknolojia na Kuhimiza ushirikiano na Ubia wa Kimataifa.

Mhe. Mahiga alieleza kuwa kwa kuzingatia misingi hiyo, amemueleza Balozi Adt azma ya Tanzania kuiomba Ujerumani iisadie Afrika kujenga Jengo la Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu ambapo Tanzania ndio Makao yake Makuu huko Mjini Arusha.

Mhe. Mahiga pia alimhakikishia Balozi Adt kuwa ameupokea ujumbe wa Kansela wa Ujerumani na atauwasilisha kwa Mhe. Rais.

Kwa upande wake Balozi Adt, Mjumbe Maalum kutoka Ujerumani alisema kuwa amefurahishwa na mapokezi aliyoyapata baada ya kuwasili nchini. Pia ana imani kuwa Tanzania ambao ni rafiki wa kihistoria wa Ujerumani itawaunga mkono kwenye nafasi hiyo ili kuwawezesha kutekeleza malengo waliyojiwekea ikiwemo kuhakikisha Afrika inapata nafasi mbili za kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, 
Dar es Salaam, 12 Machi, 2017

WANANCHI MKURANGA WAPATA HUDUMA ZA VIPIMO VYA AFYA ZAO BURE

0
0
 Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii
Wananchi wa Mkuranga wametakiwa kujitokeza kupima magonjwa mbalimbali na pale wanapokutwa kuweza kutibu kwa wakati mwafaka.

Akizungumza katika upimaji wa Afya huo,Mkurugenzi wa Taasisi ya Ibun Jazar na Mwenyekiti wa Jumuiya kuhifadhisha  Qur-uan  Tanzania, Othman Kaporo amesema kuwa katika dunia ya sasa jamii inawajibu wa kupima afya kujua ana tatizo au hana ili kuweza kuchukua hatua pamoja na kujinga na magonjwa mbalimbali yanatokana na mfumo wa maisha.

Othman amesema kuwa huduma hiyo itatolewa  kwa wa wananchi wa Mkuranga, Vikindu, Mwanambaya, Mbagala na maeneo  mengine yaliyo karibu.

Amesema wamechagua Wilaya hiyo kutokana watu wengi wanashindwa kuifikia na kuona kwa taasisi hiyo inawajibu wa kupima afya za wananchi ha.

Aidha amesema kuwa watu wengine ambao wanauwezo wajitokeze katika kutoa huduma ya upimaji ili waweze kujikinga na magonjwa ambayo yanatokana na mfumo wa maisha.

Amesema tangu jana walipoanza kupima watu zaidi ya 500 wamwjitokeza kupima na mwitikio umekuwa  mkubwa wa kuweza kuvuka malengo ya upimaji huo.

Huduma ya vipimo walivyotoa ni Msukumo wa Damu (BP), Sukari , Unene na Urefu kuendana sawa na mwili (BMI) Ushauri Nasaha  na Upimaji wa VVU,Utafiti wa Saratani ya matiti pamoja na utafiti wa Saratani ya Kizazi.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Ibun Jazar na Mwenyekiti wa Jumuiya kuhifadhisha  Qur-uan Tanzania, Othman Kaporo akizungumza na waandishi habari (hawapo pichani) wakati wa upimaji wa afya kwa wananchi wa Wilaya ya Mkuranga leo.
  Muuguzi Mariam Adamu akipima kipimo cha Sukari na Msukumo wa Damu
 Wananchi wakisubiri huduma ya vipimo vinavyotolewa na Taasisi ya Ibun Jazar leo.

MBUNGE APONGEZA KUKAMILIKA KWA UJENZI WA BARABARA KWA KIWANGO CHA LAMI ,ASEMA WANAWAKE WAMEANZA KUNUFAIKA KWA BARABARA HIYO

0
0
MBUNGE wa Viti maalum Wanawake mkoani Ruvuma, Jackline Msongozi kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ameipongeza serikali ya awamu ya tano kupitia Wakala wake wa barabara Tanroads mkoani hapa, kwa kusimamia na kukamilisha ujenzi wa barabara kiwango cha lami inayounganisha upande wa Mangaka mkoani Mtwara hadi Namtumbo mkoani Ruvuma kwa madai kuwa baadhi ya wanawake wameanza kunufaika na mradi huo kiuchumi kutokana na kuuza bidhaa mbalimbali.

Msongozi alisema hayo katika maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani ambapo kiwilaya yalifanyika katika viwanja vya soko la Mjimwema lililopo mjini Songea.Alisema kuwa kukamilika kwa mradi huo kumechochea kasi ya maendeleo kwa akina mama wajasiriamali kujiinua kiuchumi kutokana na kuanzisha biashara ndogo ndogo pembezoni mwa barabara hiyo pamoja na kusafirisha mazao yao kwa urahisi.

Aidha amewataka wanawake hao kutumia fursa ya kukamilika kwa miradi ya ujenzi wa barabara, kujikita kwenye shughuli za uzalishaji mali ikwemo katika nyanja ya kilimo na ufugaji kwa lengo la kujipatia kipato badala ya kuwa tegemezi.

Mbali na mambo mengine Mbunge huyo ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo, amewapongeza pia wanawake hao kwa kuonesha moyo wa ujasiri katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi za kisiasa mkoani humo.

Awali akisoma risala kwa niaba ya wanawake wenzake mbele ya mgeni rasmi, Joyce Mwanja alisema kuwa kutokana na uhamasishaji wa wanawake wengi kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali kumesaidia kuongeza uelewa na ari ya utendaji kazi kiuchumi ambapo jumla ya vikundi 300 vya wanawake wazalishaji mali vimeundwa mjini hapa.

Mwanja alisema kuwa katika kipindi hicho chote shughuli mbalimbali za uzalishaji mali zimefanyika ikiwemo usindikaji, kilimo, uanzishwaji wa magenge ya kuuzia biashara, ufugaji, kilimo, ufumaji na uhifadhi wa mazingira ambapo katika kipindi cha mwaka 2014/2015 hadi mwaka 2016/2017 jumla ya vikundi 172 vya wanawake wajasiriamali vimepatiwa mikopo midogomidogo yenye masharti nafuu yenye thamani ya shilingi milioni 87.1.Habari na www.ruvumatv.com
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images