Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1608 | 1609 | (Page 1610) | 1611 | 1612 | .... | 3283 | newer

  0 0

   Mkuu wa Mafunzo,  Uongozi na Usimamizi wa Talanta wa Benki ya Barclays Tanzania, Veronica Muumba (wa pili kushoto) na Mjumbe wa Bodi ya benki hiyo, Fatma Karume (wa pili kulia), wakikata keki kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani katika hafla waliyoiandaa jijini Dar es Salaam jana. Wanaongalia kutoka kushoto ni baadhi ya maofisa wa benki hiyo, Elizabeth Willilo, Faith Majiwa, Flavian Siweya na Mkurugenzi Mtendaji wa Barclays Tanzania, Abdi Mohamed.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Barclays Tanzania wakifurahia keki kuadhimisha siku ya wanawake jijini Dar es Salaam jana. 

   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Tanzania Abdi Mohamed akizungumza katika hafla hiyo.
   Baadhi ya wafanyakazi wanawake wa Benki ya Barclays Tanzania wakipozi kwa picha ya kumbukumbu katika hafla hiyo.

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  NA VICTOR MASANGU, KIBAHA 

  WAKINAMAMA wa kata ya Pangani wanaoishi katika mitaa minne ya Lumumba,Kidimu, Liwale pamoja ma mkombozi katika halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mji Mkoa wa Pwani wanakabiliwa na kero kubwa ya ukosefu wa maji safi na salama hivyo kuwalazimu wakati mwingine kuamka usiku wa manane kwa ajili ya kwenda kuchota maji visimani kitu ambacho kinahatarisha usalama wa maisha yao kutokana na mazingira yenyewe kuwepo katika mapori.

  Kilio hicho cha wakinamama hao wamekitoa baada ya Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka kufanya ziara yake ya kikazi katika mitaa mbali mbali iliyopo katika kata ya Pangani kwa lengo ya kuweza kufanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo na kuweza kuzungumza na wananchi ili kubaini changamoto ambazo zinawakabili.

  Wakinamama hao akiwemo Maria Benjamini ,Zawadi Ibrahimu,pamoja na Asimu Mendani walisema kuwa wanashindwa kufanya shuguli nyingine za kuleta maendeleo kutokana na kutumia muda mwingi wa kutafuta maji hivyo wameiomba serikali kupitia mamlaka zinazohusika kuliingilia kati suala hilo kwa lengo la kuweza kuwapatia huduma ya maji.

  Kilio cha wakinamama hao kinamgusa na kumwinua Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka na kuamua kumwagiza mbele ya mkutano wa adhara Injinia wa maji katika halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mji kuhakikisha wananchi wa mitaa minne ya Kidimu, Lumumba,miwale pamoja na mkombozi iliyopo kata ya Pnagani wanapata maji ya bomba haraka ili waweze waondokana na adha waliyokuwa wanakabiliana nayo kwa muda mrefu.
  Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akizungumza na wananchi wa kata ya Pangani baada ya kufanya ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kuweza kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili.
  Baadhi ya wananchi wa kata ya pangani katika halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mji wakimsikiliza Mbunge wakati akiwahutubia katika mkutano wa adhara uliofanyika katika viwanja vya mtaa wa kidimu.
  Diwani wa kata ya Pangani Agustino Mdachi akifafanua jambo kwa wananchi katika mkutano huo uliondaliwa na mbunge ikiwa ni moja ya ziara yake ya kikazi.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU).

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0

   Naibu katibu Mkuu CCM Bara,Ndugu Rodrick Mpogolo akimsikiliza Katibu Itikadi na Uenezi  Humphrey Polepole walipokuwa wakipanga mikakati kufanikisha mkutano mkuu wa CCM uatakaofanyika katika ukumbi wa mikutano, Dodoma leo
   Katibu Itikadi na Uenezi  Humphrey Polepole akiwa ameongozana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Jitegee,Bwa.Antony Machundewalipokuwa wakikagua maandalizi ya mkutanao Mkuu wa CCM,utakaofanyika mjini Dodoma  Msaidizi wa Mwenyeikiti wa CCM Suleiman Mwenda akimuelekeza jambo  Naibu katibu Mkuu CCM Bara,Ndugu Rodrick Mpogolo walipokwenda kujionea maendeleo ya maandalizi ya ukumbi kwa ajili ya Mkutano mkuu wa CCM,unaotarajiwa kufanyika mjini Dodoma

  0 0

   Mashirika na asasi zote ambazo hazikumbatii na kukubali mfumo wa kuendesha biashara kidigitali zinajiweka pabaya kutemwa na wateja wao.

  Kutokana na tishio hili, Telkom and Business Connexion inazindua rasmi BCX, mfumo mpya na wa kisasa kidigitali unaoongoza barani Afrika, unaotumika kurahisisha mawasiliano ya miamala ya biashara na mawasiliano.

  Toleo hili jipya la teknolojia, lililoandaliwa kwa ushirika kati ya Telkom Business na Business Connexion, ni la kipekee katika ufumbuzi wa kitekinolojia unaosambaa kwa kasi barani Afrika kuwezesha na kurahisisha mawasiliano na ufanisi wa kibiashara.

  “Uzinduzi wa BCX kwa kweli unafungua ukurasa mpya katika mwelekeo wa ufanisi wa kibiashara kwa tekinoljia pevu barani Afrika,” alisema Seronga Wangwe ambaye ni Mkurugenzi wa BCX Tanzania, katika hotuba yake ya ufunguzi aliyoitoa hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency, jijini Dar Es Salaam.

  “BCX imejengwa kutoka katika msingi imara wa Telkom Business yenye maarifa na elimu pevu ya miundombinu ya mawasiliano pamoja na taaluma ya muunganisho wa kibiashara inayojali kutoa huduma kwa ukaribu na unyenyekevu kwa wateja wake.

  “BCX sasa ni bidhaa mpya ya mawasiliano barani Afrika yenye ufanisi wa kutoa huduma kwa umakini mkubwa’, aliongeza Bwana Wangwe.

  Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya BCX Tanzania Bw. Seronga Wangwe (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam katika uzinduzi wa kampuni ya BCX ambayo imejumuisha kampuni za Business connexion na Telkom katika hafla fupi iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency, Kulia ni meneja mauzo wa kampuni hiyo Bw. Ebenezer Massawe.

  Kutoka kushoto ni Bwa. Seronga Wangwe, (mwakilishi) kutoka Mozambique High Commission, Bwa.Frans Van Aardt- Councelor kutoka ubalozi wa Afrika kusin,Bi.Monica Patricio Clemente- Balozi wa Msumbiji, pamoja na Bwa.Althon Beukes- mkuu wa BCX International wakiwa katika picha ya pamoja.

  . Mgeni rasmi Bw. Frans Van Aardt ambaye ni Councelor wa Ubalozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania. Akizungumza katika Uzinduzi wa kampuni ya BCX uliofanyika Hyatt hotel Dar es salaam
  Mkuu wa BCX International Bw. Althon Beukes akizungumza na wageni katika hafla fupi ya uzinduzi wa kampuni ya BCX, iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam
  Wageni mbalimbali waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa BCX Tanzania .


  0 0
 • 03/10/17--04:01: KUMBUKUMBU
 • Mpendwa Baba yetu Urban Peter Mbuya, leo umetimiza mwaka mmoja tangu mwenyezi Mungu akuite nyumbani kwake  juu mbinguni. Umetuachia majonzi makubwa lakini tuna imani uko mahala salama ukituombea. 

  Unakumbukwa  sana na mke wako Tertula Lyinna, watoto wako Rose, Flora, Juliet, Brenda na Gloria pamoja na wajukuu zako Joan, Michael, Christabell, Malaika, Noela, Cleopatra na Urban. Tunazidi kukuombea upate pumziko la milele. 

  "Raha ya milele umpe eeh "Bwana na mwanga wa milele umuangazie, upumzike kwa amani.." Amen !

  0 0

  Meneja Utawala na Utumishi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Amina Ally, akikabidhi baadhi ya vifaa kwa Muuguzi Kiongozi wa wodi ya wazazi ya hospitali ya Mwananyamala, Sista Eva Njalla, Dar es Salaam katika kuadhimisha Sikukuu ya Wanawake duniani.
  Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mwananyamala, Dk. Daniel Nkungu (kushoto), akiwashukuru wafanyakazi wa SSRA, mara baada ya kupokea misaada hiyo.
  Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mwananyamala, Dk. Daniel Nkungu (kulia), akiwatambulisha wafanyakazi wa SSRA kwa baadhi ya wafanyakazi wa hospitali hiyo.
  Meneja Utawala na Utumishi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Amina Ally, akikabidhi baadhi ya msaada kwa mmoja wa wazazi waliokuwepo kwenye wodi hiyo.
  Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) wakiwa na baadhi ya vifaa kwa ajili ya kukabidhi Hospitali ya Mwananyamala, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni katika kuadhimisha Sikukuu ya Wanawake duniani.

  0 0

  SHIRIKA LA Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (DAWASCO), limetangaza kuwapo kwa tatizo la upatikanaji wa huduma ya Majisafi kwa wakazi wa  jiji la Dar es salaam, pamoja na Miji ya Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani kutokana na kuzimwa kwa mitambo ya uzalishaji Maji ya Ruvu Juu na Ruvu Chini kwa wastani wa saa 8 siku ya Jumapili.

  Meneja uhusiano wa DAWASCO, Bi. Everlasting Lyaro, ameeleza sababu ya kuzimwa kwa mitambo hiyo ni kuruhusu Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kukamilisha kazi ya kuunganisha umeme kwenye mtambo mpya wa Ruvu Juu, ikiwa ni moja ya hatua za maandalizi ya uzalishaji wa maji mapya baada ya upanuzi wa mtambo huo.

  “Kutokana na Matengenezo hayo yatakayofanywa na Tanesco yatapelekea ukosefu wa huduma ya Maji kwa wakazi wa maeneo ya Mlandizi Mjini, Ruvu Darajani, Vikuruti, Disunyara, Kilangalanga, Janga, Mbagala, Visiga, Maili 35, Zogowale, Misugusugu, Tanita, Kibondeni, Kwa Mathias, Nyumbu, Msangani, Kwa Mbonde, Picha ya Ndege, Sofu, Lulanzi, Gogoni, Kibamba, Kibamba Njia Panda Shule Kibwegere, Mloganzira, Kwembe, Kibamba Hospitali, Kwa Mkinga, na Luguruni,”.

  “Mji Wa Bagamoyo, Vijiji Vya Mapinga, Kerege na Mapunga. Bunju, Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi Beach na Kawe” alisema Lyaro.

  Maeneo mengine yaliyotajwa ni Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Manzese, Mabibo, Kijitonyama, Kinondoni, Oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, City Centre, Ilala, Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, Hospitali Ya Rufaa Muhimbili, Buguruni, Changombe, Keko pamoja na Tabata. 

  “Tunaomba wananchi wahifadhi Maji kwa kipindi hiki ili wasipate shida wakati tutakapozima mitambo hiyo”. alisema Bi.Lyaro 

  0 0


  Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.


  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa upelelezi uliokuwa ukifanywa ndani ya nchi ya Tanzania katika kesi ya uhujumu uchumi dhidi ya Kamishna Mkuu Mstaafu wa TRA, Harry Kitilya na wenzake umekamilika.

  Hayo yameelezwa na wakili wa Jamuhuri Estazia Wilson mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

  Hata hivyo Wakili Wilson amedai kuwa huyo bado wanasubiri upepelelezi unaofanywa nje ya nchi ambao bado haujakamilika.

  Mbali na Kitilya washtakiwa wengine ni Miss Tanzania, 1996, Shose Sinare na Sioi Graham Solomon.Wanadaiwa kutenda makosa nane likiwemo la utakatishaji wa fedha wa kiasi cha USD milioni sita.

  Baada ya taarifa hiyo ya upelelezi, Wakili wa utetezi Majura Magafu aliiomba mahakama kuwaleza upande wa jamuhuri waeleze hali ya upelelezi ikoje na siyo kuleta liugha za ujanja ujanja.

  “Tunaomba upande Jamuhuri watupe majibu yenye muelekeo, waache lugha za ubabaishaji, kama upelelezi haujakamilika waseme basi siyo suala la kutueleza umekamilika ndaniya nchi lakini nje bado, haileti maana yoyote.”Amesema Magafu.

  Akijibu hoja hizo,Hakimu Mkeha amesema kitendo cha kesema upelelezi wa ndani umekamilina inaonyesha kesi imepiga hatua kwa kiasi Fulani hivyo ameugiza upande wa jamuhuri ukija tena ueleze hali ya upelelezi huko nje ikoje.

  Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 24,mwaka huu.

  Mbali na shtaka la utakatishaji wa fedha, watuhumiwa hao wanakabiliwa na tuhuma za kula njama, kutoa nyaraka za uongo na kughushi.

  Wanadaiwa kutenda makosa hayo katika tarehe tofauti kati ya Machi2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa Mkopo wa USD 550 wa Serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Standard ya Uingereza.

  Watuhumiwa wa kesi ya uhujumu uchumi Miss Tanzania wa Zamani Shose Sinare na kamishna mstaafu wa TRA ,Harry Kitilya n Sioi Sumari wakiwa katika kizimba cha mahakama ya kimu mkazi kisutu mara baada ya kusomewa mashtaka yanayowakabili 
  Kamishna mstaafu wa TRA ,Harry Kitilya na Sioi Sumari 


  aliyekuwa Miss Tanzania Shose Sinare akishuka katika ngazi za mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Kamanda Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari juu operesheni mbalimbali zilizofanyika na jeshi hilo kwa wiki moja leo jijini Dar es Salaam.

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linawashikilia watuhumiwa wawili  wanaodaiwa kujihusisha usambazaji wa dawa kulevya pamoja na utumiaji wa dawa hizo.

  Watuhumiwa hao ni mwanamziki Vanessa Mdee na Dumisha Heri ambao wamekamtwa na polisi hivi karibuni.

  Akizungumza  leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamanda Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Polisi (CP), Simon Sirro amesema wasanii hao walikamatwa hivi karibuni katika mazingira ambayo hakutaja kutokana na masuala ya kiupelelezi.
  Amesema kuwa baada ya kukamilika kwa  upelelezi watafikishwa mahakamani kujibu mashataka yanayowakabili.

  Wakati huo huo Jeshi la Polisi linawashikilia watu wanaojihusisha na utapeli kwa kutumia vicoba kuhusisha majina ya Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP , Dk. Reginald  Mengi ,Mke wa Rais Mstaafu na Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Salma Kikwete pamoja na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee.

  Amesema kuwa matapeli hao wametengeneza mtandao wa Focus Vicoba ambao watu wakiingia katika mtandao huo wanakuta taarifa mbalimbali zikiwemo za viongozi na watu wenye uwezo wa kifedha kuwa ndio wanaoendesha Vicoba hiyo kwa kutumia namba za simu za 0757 308381 na 0768 199359 ambazo sio namba za viongozi hao.

  Kamishina Sirro amesema kuwa mwaka jana walimkamata Boniface Samson Ojwando (27) kwa tuhuma za kuhusika katika matandao huo na kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu kwa mtandao wa kijamii.

  Kamanda Sirro amesema matapeli wengine walikuwa wanatumia gari  zenye namba usajili T 400 CNC aina ya Toyota  Mark II Grand  katika maeneo ya Sinza kwa madai kuwa linauzwa baada ya na baada kukubaliana maziano hufanya  uhalifu wa kupora fadha hiyo iliotaka kununulia gari hilo.

  Katika hatua nyingine jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limekusanya zaidi ya milioni 840 za makosa mbalimbali ya usalama Barabarani.
  Kamanda Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akionyesha dawa za kulevya zilizokamatwa katika operesheni leo jijini Dar es Salaam.
  Kamanda Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akinyesha gari lililokuwa linatumika kwa ajili ya utapeli na magari yaliyokamatwa kwa tuhuma mbalimbali leo jijini Dar es Salaam.
  Kamanda Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akionyesha pikipiki zinazopita katika barabara ya mabasi yaendayo haraka leo jijini Dar es Salaam.

  Kamanda Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akionyesha bunduki iliyoteleekezwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi leo jijini Dar es Salaan.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.


  0 0

   Msaidizi wa Rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Juma Matandika  akitoka mahakamani baada ya kukutwa hana kesi ya kujibu na kuachiwa huru.
  Na Karama Kenyunko

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru watumishi wawili wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Martin Chacha na Juma Matandiko baada ya kuwaona hawana kesi ya kujibu 

  Uamuzi huo umetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

  Akisoma uamuzi huo, Hakimu Shahidi amesema kuwa amewaachia huru washtakiwa baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi saba wa upande wa mashtaka na kuona upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa washtakiwa wametenda kosa.

  Washtakiwa Matandika na Mecky wanatuhumiwa kwa kuomba rushwa ya Shilingi milioni 25.

  Awali ilidaiwa kuwa Februari 4 mwaka jana, washtakiwa hao wakiwa wajajiriwa wa TFF walishawishi kuomba rushwa ya kiasi hicho cha pesa kutoka kwa Salum Kulunge na Constatine Morandi ambao ni maofisa kutoka Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Geita na Klabu ya Mpira wa Miguu Geita.

  Ilidaiwa kuwa watuhumiwa hao waliomba rushwa hiyo kama kishawishi kwa TFF na Idara ya Uhamiaji Tanzania kutoa uamuzi dhidi ya klabu ya Mpira wa Miguu Polisi Tabora ili kuisaidia klabu ya ya Geita kupanda katika ligi kuu ya Tanzania. 

  Akitoa uamuzi huo, Hakimu Shahidi alisema katika ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka unaonesha hakuna mtu aliyeenda Takukuru kulalamika juu ya washtakiwa kuomba rushwa zaidi ya sauti ya CD kusambaa katika mitandao.

  Amesema upande wa mashtaka haukuonesha kama kweli washtakiwa walitoka Geita kuja Dar Saalam.

  Kuhusu sauti zilizotambuliwa za Mecky na Matandiko kupitia CD, Hakimu Shaidi amesema watu wana sauti za kufanana na hata kuigizana hivyo hauwezi kujikita kwenye ushauli kuwa ni washtakiwa wenyewe ndio wanaosikika kwenye hiyo CD.

  Amesema, ni wajibu wa upande wa mashtaka kuthibitisha pasipo kuacha mashakama kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo.

  Hakimu Shahidi ameenda mbali na kueleza kuwa kwa mujibu wa ushahidi ulitolewa mahakamani hapo, imedaiwa kuwa kanuni za TFF zinaeleza wazi kuwa, mchezaji akibainika kudanganya ndiye anayepaswa kuadhibiwa lakini si timu kunyang'anywa pointi.

  "Hawa hawakuwa na mamlaka ya kunyang'anya pointi, hivyo wasingeshtakiwa kwa kuomba rushwa na hata kama walitenda kosa basi wangeshtakiwa na tuhuma zingine, labda utapeli", amesema.

  Kutokana na upungufu wa ushahidi, Hakimu Shaidi aliwaachia huru washtakiwa kwa sababu hawana kesi ya kujibu.

  Kesi hiyo ilikuwa inaendeshwa na Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru),Leonard Swai.
  Kaimu Mkurugenzi wa mashindano Martin Chacha Mecky akitoka mahakamani Mara baada ya kuachiwa huru kwa kukutwa hana kesi ya kujibu.

  0 0

  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Machi, 2017 ameongoza Kikao cha Usalama na Maadili cha chama kilichofanyika Chamwino Mkoani Dodoma.

  Kikao hicho kimehudhuriwa na wajumbe wake wakiwemo Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndg. Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Idd.
  Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongoza  Kikao cha Usalama na Maadili cha chama kilichofanyika Chamwino Mkoani Dodoma.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza jambo wakati wa kikao cha Usalama na Maadili kilichoongozwa na Rais Dkt Magufuli,Chamwino mkoani Dodoma.
   Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein mapema leo,Chamwino mkoani Dodoma,pichani kati ni Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan
    Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na  Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein mapema leo,Chamwino mkoani Dodoma.

  0 0

   Gwiji wa siasa ya uchumi kutoka nchini Misri Profesa Samir Amin (wa pili kutoka kulia) akitoa mhadhara kuhusu 'Uwezo wa Kujitawala, Ujenzi wa Demokrasia na Ustawi wa Kijamii Afrika' katika ukumbi wa Nkurumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mapema leo. Mhadhara huo uliandiliwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja, Mwenyekiti wa Mhadhara Profesa Martha Qorro na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo - Utafiti Profesa Cathbert Kimambo.

   Mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Issa Shivji akichangia katika mhadhara uliofanyika mapema leo.
   Mkusanyiko wa wanafunzi, wahadhiri na watu mbali mbali waliojitokeza kumsikiliza Profesa Samir Amin mapema leo katika ukumbi wa Nkurumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 
   Mchumi mbobezi nchini Tanzania Profesa Samwel Wangwe akichangia katika mjadala.
   Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja akizungumza katika mhadhara huo kwa kutoa salamu za shukrani kwa niaba ya waandaaji.

  Waziri Mkuu mstaafu Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba ambaye pia ni Rais wa Jumuiya ya Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Samir Amin pamoja na meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa DARUSO na UDASA kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


  0 0

  Na. Vero Ignatus, Arusha.
  WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene amewaagiza maafisa utumishi kuwa waadilifu na wakweli katika kutunza nyaraka zinazowahusu watumishi wenzao.

  Aidha serikali inatambua kuwa inadaiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii na inajitahidi kulipa madeni hayo inayodaiwa na mifuko ya Hifadhi za Jamii .

  Simbachawene amesema hayo wakati akifungua mkutano wa tisa wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

  Amesema baadhi ya maafisa utumishi wamekuwa kama miungu watu na kupoteza nyaraka za watumishi huku wanapobanwa na waajiriwa kuhusu taarifa za watumishi husema uongo  wakijua wenzao wanafamilia kama wao.

  Pia amekemea tabia ya watumishi wa masijala ambao wanapoteza kumbukumbu za watumishi kwa makusudi hali inayosababisha baadhi yao kupunjwa madai yao kutokana na baadhi ya kumbukumbu kupotezwa.

  "Nawaomba nyie maafisa utumishi muwe makini sana na maisha ya watumishi wenzenu oneni huruma kwao mnapoteza kumbukumbu au kutoa ruhusa kwa watumishi halafu mkibanwa mnasema hamna taarifa hii inawaumiza watumishi wenzenu maana wanafamilia zao kwanini muwafanyie mambo yasiyofaa mjirekebishe nyie pamoja na watu wa masijala ".

  Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Lapf, Profesa Faustine  amesema kuwa mfuko huo unajitahidi kutoa huduma kwa wakati ikiwemo kuongeza idadi ya wanachama na kubuni mbinu za kukuza uchumi katika sekta ya viwanda.

  Alisema mfuko huo utaendelea kutoa huduma kwa wakati akiwemo fao la kulipwa jana kwa wanachama wastaafu sanjari na kutoa mkopo wa maisha popote unaotolewa kwa waajiriwa wapya kwakushirikiana na Benki ya CRDB.

  Naye Mkurugenzi wa mfuko huo, Eliud Sanga alishukuru wanachama hao kwa kushiriki katika mkutano huo sanjari na kuuchagua mfuko huo ambao utatoa jana na hivi sasa wapo katika uchambuzi wa Kiwanda cha chai cha Mponde, kilichopo Tanga, Kiwanda cha Kuchataka nyama kilichopo Morogoro pamoja na kiwanda cha vifaa vya hospitali Mkoani Shinyanga ambapo miradi hiyo itaanza kutekelezwa mwishoni mwa mwaka huu.

   Waziri wa nchi ofisi ya Raisi Tamisemi mhe,George Boniface Simbachawene

  0 0

  Ernst & Young will be starting its Graduate Recruitment Programme for 2017 from 15th March to 26th April, 2017. All finalist students and those who recently graduated from different Universities are invited to make their application from 15th March to 26th April. Visit our web site www.ey.com /careers and upload your application.

  Ernst & Young is named as one of the Top three global employers in the Universum survey of business students and as one of the Top 25 Best Multinational Workplaces by Great Place to Work and #2 Top Employer in Africa!

  About EY:

  Ernst & Young Tanzania is a member of Ernst & Young Global Limited of the United Kingdom. Ernst & Young is a Global leader in Assurance, Advisory, Tax, and Transactional Advisory Services (TAS). Worldwide, our 230,000 people based in 728 offices in 150 countries, organized in 28 Regions and Four (4) Areas are united by our shared values and an unwavering commitment to quality. 

  At EY we are committed to doing our part in building a better working world. The insight and quality services we deliver help build trust and confidence in the capital markets and in the economies the world over. We develop outstanding leaders who team to deliver on our promises to all of our stakeholders. In so doing, we play a critical role in building a better working world for our people, for our client and for our communities.

  0 0
  0 0

    Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akijumuika na waumini wengine katika misa ya Njia ya Msalaba katika Kanisa Kuu la Katoliki la Mtakatifu Paulo wa Msalaba mjini Dodoma  Ijumaa Machi 10, 2017
    Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akijumuika na waumini wengine katika misa ya Njia ya Msalaba katika Kanisa Kuu la Katoliki la Mtakatifu Paulo wa Msalaba mjini Dodoma  Ijumaa Machi 10, 2017
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akitakiana amani na watawa wakati wa  misa ya Njia ya Msalaba katika Kanisa Kuu la Katoliki la Mtakatifu Paulo wa Msalaba mjini Dodoma leo Ijumaa Machi 10, 2017
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akijumuika na waumini wengine kupokea Ekaristi  Takatifu wakati wa misa ya Njia ya Msalaba katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo wa Msalaba mjini Dodoma  Ijumaa Machi 10, 2017
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na waumini baada ya misa ya Njia ya Msalaba katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo wa Msalaba mjini Dodoma  Ijumaa Machi 10, 2017 PICHA NA IKULU

  0 0


  Diwani wa Kata ya Kilungule Mh. Saidi Fella leo amepokea msaada wa vitabu vya kufundishia na  kujifunzia kwa wanafuzi wa shule za msingi pamoja na Sekondary kutoka kwa rafiki zake wa Oxford University Press Tanzania, Vitabu hivyo vimegawiwa katika shule ya msingi Charambe, Chemchem pamoja na Kingugi na kwa upande wa Sekondary ni Charambe na

  Diwani Saidi Fella amewashukuru Oxford na kuwasisitiza wanafunzi kusoma kwabidii kupitia vitabu lakini pia kuvitunza kwa maana ya wadogo zao kuju kuvitumia vitabu hivyo kwa baadae, hata hivyo amewata walimu kuhakikisha wanavipiga mihuri vitabu ili wanafunzi wanapo azima kwenda kusoma nyumbani wakumbuke kuvirejesha.

  Maria Mlay kutoka Oxford amewasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii kupitia vitabu hivyo ili kutimiza ndoto zao katika maisha lakini pia kuvitunza vitabu hivyo.

  Aidha Saidi Fella amewashukuru Oxford kwa mchango huo wa vitabu katika kata yake na ameendelea kusisitiza wadua kuendelea kumsapoti katika kata yake ya Kilungule kwani ni Kata mpya na bado inamaitaji mengi zaidi ya miundo mbinu, Afya pamoja na Elimu.

  Picha ya Pamoja wanafunzi na walimu baada ya kupokea vitabu

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0
  TAARIFA:


  SHIRIKA la Umeme Nchini (TANESCO) linakanusha Taarifa iliyotolewa na Shirika la Maji Safi na Maji taka jijini Dar es Salaam (DAWASCO), kuhusu kukosekana kwa Huduma ya maji kwa siku ya Jumapili  tarehe 12/03/2017 kwa wakaazi wa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani  ili kupisha TANESCO kufanya matengenezo ya ukamilishaji kazi ya  kuunganisha umeme kwenye mtambo mpya wa maji wa Ruvu Juu.

  Aidha, Taarifa hiyo ya DAWASCO iliainisha kuwa ukosefu huo wa Huduma ya maji unatokana na matengenezo yatakayofanywa na TANESCO kwa siku husika.(12/03/2017).
  TANESCO inapenda Umma ufahamu yafuatayo;
  Mosi,  TANESCO ilipokea ombi  la DAWASA kupitia Mkandarasi wao (M/s Mollel Electrical Engineering) wiki iliyopita la kuomba kuzimwa umeme ili wakamilishe kazi ya mradi wa kuongeza mashine za kusukuma maji kwenye kituo cha Ruvu juu kilichopo Mlandizi, kupitia mradi huo mashine nne zinazohitaji megawati 2 kila moja zimefungwa.
  Wataalam wa TANESCO waliishauri DAWASA wajenge laini ya kilovolti 33 kutoka Chalinze hadi Mlandizi ili kuzipatia umeme  mashine hizo mpya walizoongeza.
  Pili,  Baada ya wataalam wa TANESCO kutembelea eneo hilo na kufahamu uharaka wa mradi huo wa maji kwa Wananchi ilishauri DAWASCO kwa barua kuwa umeme uzimwe siku ya ijumaa tarehe 10/03/2017 ili Mkandarasi wa DAWASCO kufanya kazi hiyo, ushauri ambao DAWASCO iliupinga wakiomba umeme uzimwe siku ya Jumapili tarehe 12/03/2017 ili wapate muda wa kuwaarifu Wateja wao na TANESCO iliridhia.
  TANESCO imeshangazwa na Taarifa hiyo ya DAWASCO kuwa TANESCO inafanya matengenezo ambayo yatapelekea ukosefu wa huduma ya maji huku ikitambua TANESCO inatekeleza ombi lao walilolileta.
  Tunasisitiza kuwa,  taarifa za TANESCO kufanya matengenezo si za kweli na uzimaji umeme siku ya Jumapili tarehe 12/03/2017 ni kwa ajili ya kupisha Mkandarasi wa DAWASCO kufanya kazi kama walivyoomba na  si TANESCO.
  Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano TANESCO Makao Makuu.

  0 0


  Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili ukumbini kuendesha kikao cha Kamati Kuu ya CCM mjini Dodoma leo. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM-Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

  Mwenyekiti wa chama cha CCM, Rais Dkt Magufuli akiwakaribisha wajumbe kwenye kikao cha Kamati Kuu ya CCM na kufungua kikao hicho mapema leo asubuhi,kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar).Dkt Shein,wa tatu kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman .


  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza jambo wakati wa kikao cha Kamati Kuu kilichoongozwa na Rais Dkt Magufuli,leo mkoani ni Dodoma,Kulia Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar).Dkt Shein.
  Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi,Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongoza Kikao cha kamati kuu ya CCM, mapema leo Mkoani Dodoma.
  Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga akizungumza jambo na Katibu wa Itikadi na Uenezi Hamphrey Polepole mapema leo kabla ya kuanza kikao cha kamati kuu,mjini Dodoma
  Wajumbe wa Sekretarieti wakijadiliana jambo ukumbini kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya CCM leo mjini Dodoma
  Kikao cha kamati kuu ya CCM kikendelea.

  0 0

  Wananchi wa jamii ya wafugaji katika kijiji cha Mbukeni,Kata ya Harashi ,tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro jana wamezuia kwa muda msafara wa kamati ya kudumu ya Ardhi,Maliasili na Utalii wakishinikiza kusikilizwa kero zao.

  Katika Pori tengefu la Loliondo lililopo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha kumekuwa na mgogoro  uliodumu kwa zaidi ya miaka 25 sasa huku suluhu ya utatuzi wa kiini cha mgogoro huo kikitafutiwa ufumbuzi.


  Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii imetembelea maeneo mbalimbali ya Pori hilo kwa lengo la kujionea hali halisi kabla ya kutoa tamko juu ya mgogoro huo ambapo ikiwa njiani kuelekea Mamlaka ya Ngorongoro ikakutana na kundi la wafugaji wakiwa wamezuia barabara


  Hatua ya wafugaji hao kusimamisha msafara wa kamati inakuja muda mfupi baada ya kamati kufanya kikao na wawakilishi wa wafugaji hao,kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Domel.

  Wananchi wa jamii ya wafugaji katika kijiji cha Mbukkeni ,kata ya Harashi wakiwa wamezuia msafara wa kamai ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii iliyofanya ziara kutembelea Pori tengefu la Loliondo kupata hali halisi ya mgogoro uliopo .
  Wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii walilazimika kushuka na kuzungumza na wananchi hao.
  Wajumbe wa kamati hiyo wa kuzungumza na wananchi wa jamii ya wafugaji katika eneo hilo.
  Vijana wa jamii ya wafugaji wakiwa wamebeba silaha za jadi .
  Mbunge wa Jimbo la Siha ambaye pi ni jummbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii,Godwin Mollel akizungumza na wananchi wa jamii ya Wafugaji katika kijiji cha Mbukeni baada ya kuzia safara wa kamati hiyo.


older | 1 | .... | 1608 | 1609 | (Page 1610) | 1611 | 1612 | .... | 3283 | newer